Ruhusu amani yake, Kataa mahangaiko

amani

Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. – Yohana 14: 27

Bwana Yesu ni Mfalme wa Amani, yuko ndani mwetu kwa njia ya Roho wake, hivyo basi tunayo amani yake ndani mwetu! Tusimruhusu ibilisi atuibie amani hiyo, tusiyaruhusu masumbufu ya maisha haya yatupore amani tuliyonayo ndani ya Yesu.

Labda unajiuliza, ninafanyaje kuzuia amani ya Mungu isiondoke ndani mwangu? Jibu ni kuliamini Neno la Mungu linavyosema na kulishika. Mfano, Baba yako wa Mbinguni anasema, “sitakuacha wala sitakupungukia”, unalishika Neno hilo unalitafakari, yakikujia mawazo (toka kwa yule adui) kama “Mungu amekuacha au Mungu hana mpango na wewe” badala ya kuyapokea unayakataa na kuendelea kukiri ahadi ya Mungu kwamba hatakuacha wala kukupungukia. Amani yake itaendelea kutawala moyoni mwako.

Usifadhaike moyoni mwako wala usiwe na woga kwani amani yake imo ndani mwako, na tayari unao uwezo wa kukataa hofu na mahangaiko yoyote yatakayojaribu kukuibia amani hiyo.

Iruhusu amani yake itawale katika kila eneo la maisha yako leo! Mbarikiwe sana!

Blessings,

Patrick

Advertisements

6 thoughts on “Ruhusu amani yake, Kataa mahangaiko

  1. Kweli kaka amani ikiamua huwezi kuona ugumu wowote ule hata ukiwa kwenye majaribu,hawa wafuatao waliiruhusu amani ya Kristo ndani yao wakiwa kwenye shida:-MTUME PAULO,STEPHANO,AYUBU,DANIELI,YEREMIA,SHEDRAKA,MESHAKI NA ABEDNEGO,MTUME PETRO,BATROMAYO,NA WENGINE WENGI.

  2. PATRICK!
    UENDELEE KUBARIKIWA NA BWANA WETU YESU KRISTO, NDG YANGU.

    Lazarus SM.

  3. UBARIKIWE AMAN YA YESU NI YA KUITUNZA DAIMA. HAKIKA AMAN YAKE INAPITA FAHAMU NA AKIL ZA KIBINADAMU

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s