Naomba mapenzi ya Mungu kwenye uchumba wangu!

maombi

Bwana asifiwe wapendwa, Wapendwa naomba mniombee sana,nina jaribu zito kwa kweli linanitesa sana. Mimi ni binti naitwa Rachel.Nina mchumba ambae nimekuwa nae kwa mda wa miaka 3, na kwa sasa tuko katika hatua za kutaka kufunga ndoa, yeye ni Mkatoliki mwenye hofu ya Mungu,na mimi ni AIC, kutokana na kutofautiana madhehebu tumekubaliana kufunga ndoa mseto na tukakubaliana kumwomba Mungu atuongoze ili kwa pamoja tupate sehemu ambayo tutamwabudu Mungu kwa pamoja sawasawa na Neno lake na tunaendelea na maombi hayo mpaka sasa, haya yamekuwa ni maombi yetu ya kila siku. Amekwisha kuja nyumbani kwa utambulisho wa awali na January wazazi wake watakuja nyumbani kwa ajili ya kuzungumzia swala la mahari pamoja na kutoa.

Katika kipindi chote hiki tumekuwa tukimwomba Mungu kwa pamoja kuhusu kuutimiza mpango wake kwetu na kwamba kama ni kusudi lake atuunganishe na kama sio basi jambo hili lisiendelee na kila mmoja ashike njia yake. Naomba maombi yenu sana wapendwa, nimesoma shuhuda za watu wengi kwenye blog hii na jinsi ambavyo wametoa shuhuda zao,NIMEOGOPA SANA,Namwomba sana Mungu anipe utulivu na usikivu ninapoendelea kumwomba ili atakaposema nami nimsikie na nimwelewe na kufata kile anachotaka nikifanye katika hili,Nawaomba sana mniombee wapendwa wangu,nina wakati mgumu sana. Mungu awabariki.

Rachel

Advertisements

13 thoughts on “Naomba mapenzi ya Mungu kwenye uchumba wangu!

 1. Mimi siji kwa mtizamo wa kidini sana ila nataka nichangie kwa kutumia akili ya kawaida tu(common sense)

  Wewe dada mimi ninachokiona hapo ni kwamba wewe umeingiwa na roho ya kusitasita, ama baada ya kusikia mambo fulani yaliyowapata watu fulani. sasa mimi nakushauri sikiliza ya watu ama msikilize Mungu huyo unayesema unamwamini. Kwa sababu hapa inaonekana kabisa kuwa huyu bwana(mchumba wako) unamjua vizuri mko kwenye uchumba kwa miaka mitatu, dini yake unaijua! sasa tatizo hapa ni nini? tena wewe mwenyewe umesema mlikubaliana muwe na mseto. sijaona mahali uliposema yeye amekataa kuwa na huo mseto sasa shida iko wapi? Angalia usijekuea umepata mtu mwingine ndo unaanza kujua hata kuna tofauti za kidini kati yako na yeye.

  Majuto ni mjukuu!

 2. dini si tatzo kilichofungwa dunian hata mbingun pia na istoshe din ni iman ya mtu na wote na wakristo msiwaze Mungu yupo..

 3. Bwana Yesu asifiwe wapendwa!!! Tatizo nililo liona kwa watu wengi wanafikiri mtu anaye omba ushauri anataka faraja tu ili aendelee mbele.

  Naomba kama huelewi bora ukae kimya kuliko kuipoteza roho changa inayo hitaji maziwa yasiyo ghoshiwa. Katika fani yangu ya Udaktari nimewahi kukutana na mtu mwenye JIPU mguuni linamuuma sana na hana raha nalo japo hakunieleza kalipataje. Sikutaka kujua zaidi juu ya hayo zaidi ya KUMKAMUA.

  Narudi kwako dada Rachel, fikiri jinsi ulivyo mpata huyo kaka, je hamkuanzia mazoea ya urafiki? Je ameokoka na je hata wewe umeokoka? ubatizo?

  Bahati nzuri Katoliki naifahamu fika na AIC ndo usiseme, dada hizi iman zimepishana kitu ambacho hata Mtumishi Herbert Eliya amekisema!!

  Ndoa takatifu ni Mungu mmoja , Imani moja na Ubatizo mmoja wa Yohana mbatizaji. Kwa wale wanao kwambia amani ya Kristo iamue kwako wanakupajibu kuwa mtu uliye naye si sahii maana ni miaka mitatu saizi bado moyo wako hauoni mapenzi ya Mungu badala yake unaona ni JARIBU ZITO…. Saizi ni uchumba tu ni zito… Ukiolewa je? Tambua kuwa moyoni mwako hakuna amani kwanini ulazimishe?

  Ushauri wangu.

  Waambie wazazi hali uliyo nayo moyoni
  Mwambie Mchungaji wako hali halisi
  Mjulishe huyo kijana unavyo jisikia moyoni
  Lefusha muda wa kufunga ndoa
  Kata mawasiliano na huyo kijana kwa mwezi mmoja
  Ingia kwenye maombi ya kufunga ya uthibitisho na baadhi ya watumishi wa Mungu
  Uwe tayari kuachana naye kwa gharama yoyote ile
  Soma neno la Mungu likuongoze

  Mungu akupe hekima na utulivu.
  Aombae mkate hatapewa JIWE na samaki, NYOKA.

 4. Hongera dada Rachel kwa kupata mchumba, mimi nakushauri upitie mafundisho ya mtumishi wa Mungu mwalimu Mwakasege kuna somo la vijana, linasema mambo ya kutafakari kabla ya kuoa au kuolewa, litakusaidia, pitia kwenye mtandao, http://www.mwakasege.org, pia endelea kumuomba Mungu na amani ya kristo itaamua moyoni mwako na kama ni kusudi la Mungu mfunge ndoa na huyo kaka mtafunga kwa sababu kusudi la Mungu always litasimama. mbarikiwe.

 5. YESU atakaporudi atakuja kunyakua mtu mmoja mmoja sio kikundi cha watu au kundi la watu tuelewe Yesu anaangalia moyo na uthamin wako kwa huyo unayemwamin na kama ndan yako dada kuna AMANI YA YESU pangen taratibu zote za ndoa zifanyike muoane. kukashifu dini au thehebu sio suluhisho kwako. je dada unayo aman ndani ya moyo wako? naamin hata wapo ambao wameoana na ni wa sehemu moja {iman) lkn wamekosana. soma Zaburi 37:5

 6. Kaka Emanueli binafsi sijakuelewa unaposema wakubaliane sehemu watakayolelewa kiroho wote kwa pamoja kabla ya kufunga ndoa,huoni kuwa hapo watafanya kwa ajili ya wao kufurahishana na si kumpendeza Mungu?na hata dada recho kufikia hatua ya kuomba msaada wa mawazo juu ya suala hili elewa kuwa tayari kuna shida hapo,kwani kila mtu anaona hapo alipo ni sehemu sahihi,ushauri wangu kwa kuwa kuna tatizo hapo waachane na mpango wa kufunga ndoa.

 7. Nionavyo mimi; kitu cha kwanza ilikuwa ni kukubaliana wapi mtaabudu na mipango mingine ifuate mimi sina tatizo na ukatoliki au AIC kama mnaamini kitu cha kufanana na tofauti zenu zikawa ni dhehebu REKEBISHENI HIYO KASORO KABLA YA KUFUNGA NDOA ILI MTAKAPOAMUA KUFUNGIA NDOA YENU BASI MKULIE NA KULELEWA HAPO. UBARIKIWE

 8. Dada kwa bahati mbaya mimi huwa sina injili ya kumpaka mtu mafuta,maoni ya wachangiaji hapo juu si mabaya lkn mimi niko tofauti nao kidogo ktk hili,wanakuambia omba Mungu atakusaidia lakin hawakuambii madhara yake,unamkumbuka mfalme Sulemani pamoja na hekima yake,utajiri aliokua nao,unajua yaliyomkuta hebu soma 1wafalme 11:1-13,alipopenda wanawake ambao hawakuwa waisraeli(imani)yake hapo ndipo tatizo kati yake na Mungu lilipoanzia,Dada wewe unaamini kuwa yesu ndie anayekuombea WARUMI 8:26,yeye kwa imani yao wanaamini mwombezi wao ni bikira maria,Biblia yako inasema ulevi ni dhambi,wao wanasema kunywa usilewe,tafakari kwa umakini uamzi wako huo dada recho,kama uko tayari kuikosa mbingu kwa ajili ya kujifurahisha kwa kitambo kazi ni kwako,mauti na uzima vi ktk uwezo wako,tumia akili yako vizuri.

 9. Dada yangu mpendwa katika Kristo,
  Shalom!
  Unajua, Mungu huiangalia na kuisikia mioyo yetu kabla hata hatujaanza kuomba! Ninaamin kwa kuishinda kwako aibu, hiyo gravitation, hata ukalileta suala hili hapa, ni ushuhuda mkubwa sana wa Imani yako kwake Bwana wetu mwenye Mapenzi makuu sana kwetu. Kama yule mwanamke aliyekuwa akivuja damu, ninaamini nawe katika uchanga wako, umeligusa pindo la vazi lake! Basi kwa kadiri ya imani yako, amini kwamba Bwana atakuongozeni nyote, ili mumfikie Yeye aliye tumaini la wokovu na maisha yetu yote!

  Basi muyaendeapo hayo, katika hatua zenu changa, jifunzeni kuibadili hofu ya Mungu katika ujumla wa mafundisho ya kidhebu, kuwa hofu ya Mungu katika kulipenda na kulitii Neno lake. Kwani kwa kulipitia hilo Neno kwa pamoja, mtapata fursa ya kuongea na Mungu kwa pamoja, ndipo atazidi kuwajenga, nanyi kuwa waraka kwa jamii yote inayowazunguka!!!

  Bwana na aizidishe furaha yake kwenu!

 10. rachel u might b confused i was once in a situation like yours but mruhusu Roho Mtakatifu aseme na wewe katika uhusiano wenu ruhusu kila pando ambalo hajalipanda yeye ling’olewe…siku zote ukitaka cha Bwana jifunze kusikiliza sauti yake..kusudi lake lazma lisimame..

 11. Bwana Mungu na atimize haja ya hitaji lako katika jina la Yesu kristo wa Nazareti aliye hai!.

 12. DADA RACHEL,
  Kwanza nakupongeza kwa kupata Mchumba. Mungu anasema hana haja na wasitasitao! Ili ufanikiwe fanya mambo 2, 1.-Amini Neno la Mungu. 2.- Usifanye jambo la kiroho kwa mtindo ws kibinadamu, Mungu hasikilizi wala hawi pamoja na mipango “Mseto” fanyeni mambo yenu, mipango na maombi yenu kwa Imani moja. Mungu haangalii Dini, anataka wachaji wanaomwabudu ktk Roho na kweli. Ujue Mungu hushughurika na watoto wake tu! Je wewe na mwena wako mmeitimiza kweli na kuitekeleza? ile Mdo 2:38? Simameni ktk Neno!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s