Nashukuru Mungu nimepata kazi!!

asante

WAPENDWA BWANA YESU ASIFIWE!  Namshukuru MUNGU kupitia maombi yenu nimepata kazi. Jina la YESU lihimidiwe

–Win

————————————————————-

Hapo Kabla Win alituma maombi yake hapa  tarehe 18/10/2012

Shalom wapendwa, mimi nimeokoka, nahitaji maombi yenu nipo kwenye mapito ya kiuchumi na kimahusiano. Natafuta kazi sipati, namuomba Mungu anipe mume mwema lakini hata mchumba tu sijapata. nampenda sana Yesu na nimekuwa mwaminifu kwake.  Naamini kwa maombi yenu atasikia.

————————————————————-

Dada Win, asante sana kwa kurudi na kutoa ushuhuda wako, hii inatupa nguvu ya kuendelea kuomba zaidi. Mungu amefungua mlango wa kazi, atafungua na milango mingine katika jina la Yesu.

Mungu awabariki wana maombi wote mnaoombea maombi mbali mbali kutoka kwenye blog hii.

Utukufu kwa Mungu!

 

Advertisements

6 thoughts on “Nashukuru Mungu nimepata kazi!!

 1. asanteni sana wapendwa mbarikiwe ntazingatia mafundisho yenu maana naamini mmeongozwa na Roho Mtakatifu.. naimani na maombi mengine yote Mungu atafanya kama alivofanya hili
  ….. dada vicky nakutia moyo kuwa na imani Mungu atakutendea kama alivonitendea mimi tuzidi kumuomba na kumwaminia……mbarikiwe sana
  SG mbarikiwe sana

 2. kwako VICKY ULIYEPATA KAZI:

  kUTOKA 16:4

  “Ndipo BWANA akamwambia Musa,Tazama,mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mikate kutoka mbinguni;na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku;ili nipate kuwajaribu ,kwamba watakwenda katika sheria yangu,ama siyo.”

  Wengi wanatendewa muujiza wa kupata kazi lakini wanashindwa kusimama kwenye kazi

  wengi wanajisahau wanazani kumtumikia Mungu ni kanisani tu wamesahau kuwa Mungu anatafuta watu kama Yusufu ili serikali na watendaji wake wamtangulize Mungu katika kila kitu wanaenda hadi kumtumikia ushirikina na uchawi

  Dada VICKY umebeba makusudi ya Mungu kwenye hiyo kazi,hapo alipokuweka alikuwa anamtafuta mtu kama wewe usimamae katika zamu yako kwenye hilo eneo

  alipomlokole iwe ofisini au kwenye biashara nk. ni marufuku ushirikina kusimama

  Tulipomlilia Mungu wenzio atupe kazi akatupa,nikamlilia tena kuwa hapa uliponiweka umekusudia nini nifanye akanionyesha cha kufanya ndilo kusudi ninalolisimamia

  KAMA BADO HAKIKISHA UNAMLILIA MUNGU AKUFUNDISHE MASOMO YAFUATAYO YATAKUSAIDIA KWENYE UTUMISHI WAKO HAPO KAZINI

  1. JICHO LA ROHONI(POSITIVE THINKING& SEEING)
  1. KUTAKASWA ROHO,NAFSI NA MWILI
  2.ULIMWENGU WA ROHO NA MWILI UNAVYOFANYA KAZI
  3.USHIRIKA/URAFIKI NA ROHO MTAKATIFU
  4. NGUVU YA SADAKA NA AINA ZA SADAKA
  5.USHINDI KATIKA DAMU YA YESU
  6.VIFUNGO NA MITEGO VYA SHETANI KWA WALIOOKOKA
  7.LAANA NA MAAGANO

  AMEEEEEEEEEEEEEEEN!

 3. Win,
  Mara zote ushindi upo kwa washindi tu. Na Mungu hujua sikitiko, kwa maana hiyo yeye hujua namna ya kuwafariji Watu wake! Umenitia moyo sana. Basi utukufu na shukrani tumrudishie Mungu wetu ambaye hujishughulisha nasi sana.

 4. Wapendwa bwana apewe sifa naomba maombi yenu mwenzi wangu amebadilika mno, mwenendo wake umekuwa taofauti, majibu yake hata katika mambo ya ushauri yamekuwa yakuumiza sina amani hata kidogo. Naumia wapendwa. Naitwa viky

 5. Amen Dada Win jina la Bwana Yesu lihimidiwe.

  Ila kumbuka kumtolea Mungu wako Malimbuko pia uwe mwaminifu kumrudishia 10% yake Mungu bila kuchakachua.

  Kwenye Malaki 3:10 amesema leteni zaka KAMILI ghalani,umeona enhe!! Amesisitiza zaka kamili yaani ukitoa hapo hata buku ukasema ngoja niweke vocha nimpigie Pastor nimwambie nina sadaka ya fungu la kumi ujue hapo umeshaharibu kabisaaaa.

  Mungu akubariki

  Flano
  Download the latest BlackBerry® applications from Zantel on http://www.zantel.com/zantelapps

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s