Tumetoa wapi hii? wakati wa kuombewa ili kunena kwa Lugha

Pentecost

Hi! Plz lets us chew  this out….

Wengi wetu ktk huduma na mimi nikiwemo…tunapowaombea watu kujazwa Roho Mt tunawaambiaga waseme ”asante Yesu”.. mara nyingi and kila mara huku tunachochea maombi na at last kunatokea ishara nyingi zinazoonyesha  wapo waliojazwa mfano kunena kwa lugha.
Hiyo kitu tumeitoa wapi? ni rhema? tukibanwa na wana maandiko bila Roho  tunatokaje ngoma iyo? kwa kua ktk Bible actions zilizo WAAAAZI  zilizotumika Roho Mtakatifu akajaa watu ni ..kupulizia hewa..Yesu akawavuvia pokeeni Roho Mtakatifu, kuombea-wakajazwa, Kuweka mikono na kuombea wakajazwa, mahubiri yanaendelea-Roho bila kuombwa akawajaza watu…Kwa Neno na kutii maagizo/Neno ..Yesu..wasitoke Yerusalem wangoje ahadi..then Mdo 2: 1-4 walikua pamoja wamekusanyika..wakajazwa..where did we get the ”asante Yesu..asante Yesu thing? any lovely catastrophic justification(by logos,rhema,revelations,any other source) to cement any querry of madini-dini humans?…how and where can we draw some tips/clues from the Bible ili ku-back up the ”many -many asante asante Yesu” mchakato to bring or rather to gear creatures to receive or make HSpirit come and fill them?
Besides, Tunapotakaga kuombea ujazo or mambo mengine..tunatumia pia sometime..kuwambia watu ”watafutisha kuhesabu   mara 7 basi ikifika mara 7 mtu furu kujiachia kwa Bwana kama ni kuomba au kulia sawa tu..so mhubiri anahesabu moooa..wote moooja..then wote tnafuta moooja… mbili..wote mbili…mpaka 7 na kweli kunapasuka vibaya sana.. furu uwepo na nguvu za Mungu za kutisha na kuzama-zama kimaombi,  wingu liko clear paaaa…safiiiiii  tunasambaa huku mawinguni from bongo hanu- hanu but unapotea kwanza……Tumeitoa wapi iyo kitu?..Yeriko mara saba? fine but that was used for kubomoa ngome and a word specific came to instruct them so..sisi je who specifically instruct such applications? and why tumeshift application ya kule na kuingizia mambo ya kwetu ya kupata Roho or baraka wakati ilitumika kufyatua kuta pepo zile bila magereda yenu ya city hapa duniani kwenu huku na Magufuri wetu the no nonsence man i like most in the govrt?
Amani ya Bwana iwe nanyi nyote,
Edwin Seleli
Advertisements

22 thoughts on “Tumetoa wapi hii? wakati wa kuombewa ili kunena kwa Lugha

 1. Siyi,

  Anthony alichojibu, ni very clear and Biblical, nadhani umeelewa!
  Sasa kama unadhani una very serious swali au hoja na unataka sana kuelewa na kwa kweli unauhitaji huo na si mambo ya dini mfu na kuchezesha maneno, uliza yote na yatanyukwa kwa nguvu sana yote . Karibu

  Press on

 2. Bwana Michael John N, Siyi,
  Kwa kifupi sitaweza kukupa majibu kama unavyotarajia kwa akili ya Binadam wa kawaida. Nirejee na nikwambie kabisa ROHO MTAKATIFU hasubiriwi kana anayesubiri embe lidondoke hivyo basi hutaweza kusikilizia ati jirani yako ananena nini, Labda uwe agent wa Shetani.
  Nimesema hivyo kwa sababu tunajua tafsiri moja kuu inayosema kwamba, maombi ni namna ya mtu kuwasiliana na Mungu au Maombi ni mawasiliano kati ya mtu na Mungu wake. Sasa Kama wawasiliana na Mungu Je, wawezaje kupata nafasi ya kusikiliza huyu na yule kama wananena nini??
  Kwanza documentary nyingi za watu hapo juu ukiwa na wewe Michael mnapinga kusema kwa lugha mpya, sasa Utashi huu wa kutaka kulielewa suala hili kwanza kwa akili umeweka kitu kama ukuta ndani ya moyo. Suala la kunena kwa lugha ni suala ambalo hata Yesu mwenyewe alisema kwamba ni moja ya ishara zitakazofuatana nao wanaomwamini. Kwa hiyo ni jambo ambalo ni halisi kwa wale waaminio.

  Kunena kwa lugha ni mawasiliano katika ulimwengu wa roho. Rejea coments yangu hapo juu ‘’ Kunena Kwa faa sana akipatikana mfasiri lakini kama wanena hakuna mfasiri na uende ukajiburudishe kwa LUGHA HIYO YA MBINGUNI CHUMBANI KWAKO. Biblia imesema wazi (1cor14:1—-25) hapa nilimaanisha kunena kwa lugha kwenye kusanyiko. Soma 1corint14:1—-20, kwa maana mtu ye yote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu, Kwa kuwa hakuna mtu ye yote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa Roho. anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa, Kwa kuwa yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, isipokuwa kama kuna mtu wa kutafsiri, ili kanisa zima lipate kujengwa.mfano; kama tarumbeta haitoi sauti inayoeleweka, ni nani atakayejiandaa kwa ajili ya vita? Au Mziki unapiga ala isiyoeleweka hata mpangilio nani ataweza kuimba.

  Katika swali lako la pili kuna tofauti yoyote kati ya lugha ya Baba, Mwana RM? Sijui elimu ya sabato inasemaje juu ya Baba, Mwana, Roho mt. maana umeuliza kama hawa ni miungu watatu wanasema kila mmoja kivyake. Mmmhuu kazi kweli kweli.

  Sipendi kuandika sana maana najua wengi wameandika sana humu. ila tu la msingi kujua ni kwamba KUNENA KWA LUGHA NI MOJA YA ISHARA YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU. ZIPO ISHARA NYINGINE NYINGI TU KUJUA KAMA UMEJAZWA ROHO MTAKATIFU.

  NAWASLISHA
  ANTHONY

 3. Anthony,
  Umekuja na mambo mazuri. Hoja nzuri. Zenye mashiko kabisa.
  Mimi naomba unisaidie hili;
  Kwanza, Je, tutatambuaje kuwa Siyi ananena lugha za kipepo ilhali ni muumini tofauti na anavyonena Anthony ambaye ni muumini mwenzake? Au tofauti iko kwa waganga wa kienyeji na waumini peke yake?
  Pili, kuna tofauti yoyote kati ya lugha ya Baba, Mwana RM?
  Nitashukuru kukuona kwa mwitiko wako (na yeyote atakayewiwa kujibu)
  Kwa upendo wote

 4. Shalom,
  Nimepitia mjadala kwa kadri nilivyojaliwa, ninaomba nitoe tu yale ninayoyajua japo naweza nisiwe na supporting verses,
  1. Kujazwa na ROHO MTAKATIFU ni kitu kisichopingika kwa kila aliyeamini, japo kujazwa huko kutatofautiana namna na wakati mtu anajazwa.
  2. Ili Kujazwa na ROHO MTAKATIFU kuna maandalizi ya moyo wa mtu husika.
  3. Si kila atakaposema mchg. useme asante Yesu ndipo utajazwa ROHO MTAKATIFU hapana, ile ni Supporting ya wewe ili uweze kunena kwa Lugha.
  4. Kunena kwa Lugha sio pekee ndio Kujazwa na ROHO MTAKATIFU, hapana wapo wasionena kwa lugha lakini wamejazwa ROHO MTAKATIFU, na WAPO WANENAO LAKINI YUMKINI wanena Lugha ya kipepo, hapa nina maana kwamba hata waganga wa kienyeji Hunena lugha za kipepo nina Ushahidi.
  5. Kunena Kwa faa sana akipatikana mfasiri lakini kama wanena hakuna mfasiri na uende ukajiburudishe kwa LUGHA HIYO YA MBINGUNI CHUMBANI KWAKO. Biblia imesema wazi ktk (wakorintho).
  Pia Tujiulizi, Kwanini Kuwa na LUGHA MPYA (YA ROHO MT) na wapi itumike, na nani aitumie, je ukiwa umeshindwa kunena hujaokoka???

  Barikiwa sana
  Anthony, A M

 5. Robert,
  MAwazo mazuri kaka.
  Ulichosema ni kweli kabisa. Lakini kuna kitu hapa na mimi nataka utafakari. Enzi za Musa, walikuwepo wenye uwezo karibia na ule aliokuwa amepewa Musa na Mungu. Enzi za akina Eliya mtishibi, kulikuwa na manabii wa Baali vilevile. hata na agano jipya, kulikuwa nawalimu wazushi, Yuda 1:4 anawataja kwa tahadhari sana anasema, ” Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo”.
  Nachelea kusema kuwa makanisa yoooote yako sahihi na yanapeleka watu mbinguni. Kuna akina Musa, Eliya, Mitume nk lakini pia kuna akina Kora, wachawi, manabii wa Baali na wazushi. Sasa tutawatambuaje??
  Biblia iko wazi sana. Mimi nakutia moyo ufuatilie mambo yote ya ibada mnayoyafanya kanisani kwenu, na ukijiridhisha kuwa yako sawasawa na Biblia, endelea kusali huko. Ukiona kuna shida, chomoka huko rafiki yangu, utaishia kubaya tu.

 6. “Hii ni mijadala kama waliyoanzisha akina kola kuhoji uhalali wa Musa kutumiwa na Mungu kadhalika miriam na Haroun na matokeo yake kila anae soma biblia anajua hatima yao ilivyokuwa.Watu wengine kazi yao ni kukaa na kuangalia vitu wanavyo fanya wengine na kuvianzishia mijadala lakini hawana muda wakumuuliza Mungu ukweli wa mambo, hii ni hatari sana kwa sababu kuna wengine watamkufuru Roho matakatifu na hawatasamehewa kabisa na kupata hasara kubwa ambayo haijawahi tokea kwenye biashara yeyote chini ya jua yaani kuikosa mbingu.Na kila neno atakalo nena mwanadamu chini ya jua lazima atalitolea hesabu nyie mnataka experience mnazojua,Mungu haendi hivyo.Watumishi ambao mmpewa ufunuo kwa jambo hili msikate tamaa kwa maneno yao,bali endeleeni mbele huku mkilitumia kwa uhalali neno la Mungu na bila shaka mmewekewa taji mbinguni,maadamu hayo maneno si matusi tunayaamini kama chombo tu kitumiwacho kwa imani kumleta Roho mtakatifu, Mungu irehemu Tanzania, Mungu rehemu kizazi changu, Roho usiondoke.Amen!!”

  Ubarikiwe sana kaka Mligo kwa mchango wako nimeupenda sana.Katika mijadala mingine watu wanafanya mizaha bora kutoshiriki kabisa! ndo maana watumishi wa Mungu hawashiriki kwa kuogopa hilo.(Zaburi 1) Pia hii blog imenifumbua macho nimefahamu pia katika imani ya kipentecoste kuna makundi mengi sana yanayoamini tofauti tofauti.Pia kuna kundi la watu wachangiaji sana na maarufu sana humu ndani ambao wao wanaamini kuwa wao ndo wako sahihi sana kuliko wengine na wanajua zaidi, hawapendi hata kujifunza kutoka kwa wengine! Kile wanachokijua wao ndo hicho hicho wanakishikiria huku wakiwaona wangine kuwa wamepotea.Lakini neno la Mungu linasema ajidhaniae amesimama na aangalie asije akaanguka. Kwani ukikaa mbele za Mungu na kumuuliza kuhusu jambo hilo linalokusumbua au kuumiza kichwa chako hatajibu?Au Mungu siku hizi hajibu maombi ya mtu binafsi?Tafakari

 7. Lenda,
  Hawa watu kuna siku niliwauliza swali, walikimbia hadi leo. Hakuna hata mmoja aliyejibu. Niliuwauliza kuwa;
  Mungu katika historia zote tangu agano la kale hadi jipya, pindi alipotaka kunena na watu wake, alinena kwa lugha zinazoeleweka. Je, sisi wanadamu wa leo, imekuwaje, tunapotaka kunena na Mungu tunanena kwa lugha ambazo hata sisi wenyewe hatuzijui? Kama tumefikia hatua ya kumpiku/kuwa above kimatendo, ina maana sisi tuna akili sana kumzidi Mungu?
  Mpaka leo swali hili hakuna aliyelijibu, na sidhani kama litapata jibu… Wenzetu kaka wanatia huruma sana. Tuzidi kuwaombea sana pia.

 8. PIMA KWA MAANDIKO HAYA KAMA LUGHA UNAYONENA NI MAAGIZO YA BIBLIA AU MAPOKEO

  1 WAKORINTHO 14:21
  “IMEANDIKWA KATIKA TORATI, NITASEMA NA WATU HAWA KWA WATU WA LUGHA
  NYINGINE”

  ISAYA 28:11
  “LA, BALI KWA MIDOMO YA WATU WAGENI, NA KWA LUGHA NYINGINE ATASEMA NA WATU HAWA”

  MATENDO 2:8
  “IMEKUWAJE BASI SISI KUSIKIA KILA MTU KWA KILA MTU LUGHA YETU
  TULIYOZALIWA NAYO?”

  MATENDO 2:4
  “WOTE WAKAJAZWA ROHO MTAKATIFU, WAKAANZA KUSEMA KWA
  LUGHA NYINGINE, KAMA ROHO ALIVOWAKALIA KUTAMKA”

  1 WAKORINTHO 14:13
  “KWA SABABU HIYO YEYE ANENAYE KWA LUGHA NA AOMBE APEWE KUFASIRI”

  1 WAKORINTHO 14:28
  “LAKINI ASIPOKUWAPO MWENYE KUFASIRI NA ANYAMAZE KATIKA KANISA”

  1 WAKORINTHO 14:27
  KAMA MTU AKINENA KWA LUGHA, WANENE WAWILI AU WATATU, SI ZAIDI, TENA
  ZAMU KWA ZAMU, NA MMOJA NA AFASIRI.”

  1 WAKORINTHO 14:29
  “NA MANABII WANENE WAWILI, AU WATATU, NA WENGINE WAPAMBANUE.”

  MATENDO 2:8-11
  “IMEKUAJE BASI SISI KUSIKIA KILA MTU LUGHA YETU TULIYOZALIWA NAYO?. WARPATHI NA WAMEDI NA WAELAMI, NAO WAKAAO MESOPOTAMIA, UYAHUDI NA KAPADOKIA, PONTO NA ASIA. FRIGIA NA PAMFILIA, MISRI NA PANDE ZA LIBIA KARIBU KIRENE, NA WAGENI WATOKAO RUMI, WAYAHUDI NA WAONGOFU, WAKRETE NA WAARABU; TUNAWASIKIA WAKISEMA KWA LUGHA ZETU MATENDO MAKUU YA MUNGU”

  HIYO YA KUSEMA MARA SABA HALAFU LUGHA HAINA MTAFSIRI NI MACHAFUKO.

  1 WAKORINTHO 14:33
  “kWA MAANA MUNGU SI MUNGU WA MACHAFUKO, BALI WA AMANI; VILEVILE KAMA ILIVYO KATIKA MAKANISA YOTE YA WATAKATIFU”

 9. Mligo,
  Maandiko yanatuambia sisi ni askari na sehemu nyingine yanasema sisi ni jeshi, basi jeshi hilo likiwa ni la askari waoga, sijui litapiganaje na adui; haswa adui huyo akiwa ni Mapokeo!!

  Ukimbize huo uoga wa kuyakagua Maandiko, vinginevyo utakwama kuingia mbinguni kwa vifurushi vya Mapokeo unavyovibeba!

 10. Evangelist Seleli,

  Kwanza nikushukuru kwa kulirejea tena swali uliloniuliza zaidi ya mara mbili. Kulingana na moyo wa kujifunza, nilijaribu kulipanua wazo lako ili tufike mahali ambapo tutakuwa tunaongelea jambo moja, ndipo maswali yanaweza kujibika kirahisi. Lakini naona umetatizika, sijajua ni kwa nini!

  Katika maelezo yako na swali uliloniuliza, nimeona kwamba umenitengenezea mazingira ya kukufuata katika njia yako katika namna ya kwamba hizo “Asante Yesu” zinaporudiwa rudiwa huwafikisha watu katika kujazwa Roho Mtakatifu; ila unauliza tumetoa wapi jambo hili, ukijaribu kutafuta sehemu ambayo unaweza kujiegemeza katika Biblia! Kwamba ninaposema hilo si la kiBiblia na pia halina uhusiano wowote na Mungu, ndipo unaniuliza nilijazwaje??

  Niliuliza hivi, Vipawa vya Roho Mtakatifu ndiye Roho Mtakatifu? Swali langu lililenga kuliweka wazi zaidi jambo hili ili tuondoke katika kawaida tuliyoizoea ambayo iko makosani, na tuyatafute yaliyo halisi.

  Hizo “Asante Yesu” na milipuko inayoambatana nazo, ambayo wewe unadhani ndiko kujazwa Roho Mtakatifu, si jambo la kweli. Nafahamu kwamba katika mfululizo wa hizo “Asante Yesu” mwishoni hugeuka kuwa ni “Kunena kwa Lugha” ambako wewe hukutambua kuwa ndiko kujazwa Roho Mtakatifu, jambo ambalo ni kinyume na Maandiko. HAKUNA Andiko lolote linalofundisha jambo hilo kama hivyo, hayo ni mafundisho ya kibinadamu yasiyo na tija kwa yeyote anayeyashiriki maana humdumaza asiendelee mbele kuufikia ukamilifu! Kwa hiyo hilo ni Fundisho la Udanganyifu ambalo wengi wameuziwa na wanaendelea kulitunza jambo hilo FEKI wakiamini kuwa ni LULU!!

  Kwa kifupi, kuwa na kipawa cha Roho Mtakatifu si kuwa na Roho Mtakatifu! nako Kunena kwa Lugha ni kipawa tu cha Roho Mtakatifu na si Roho Mtakatifu!!! Vipawa vya Roho Mtakatifu hujitokeza sana katika hatua ya pili tuuendeapo Ukamilifu, ile “roho mpya” ambayo Mungu hukupa, hiyo ndiyo inayoleta shamra shamra hizo. Furaha inayoambatana na roho mpya uliyopewa ndio hukuleta katika kiwango hicho. Yaani ukiisha kutolewa ule moyo wa jiwe na kupewa moyo mpya wa nyama, kule kumpokea kwako Kristo kwa imani, ndipo Mungu hukupa roho mpya, hapo ndipo makosa yanapofanyika, walimu wasio na Hekima wakawafundisha watu kuwa wamejazwa RM, jambo ambalo si kweli!!!

  Basi ndugu yangu sikukujibu swali lako kama ulivyonitaka kwa sababu nilitaka kwanza ufike katika uelewa huu ya kwamba ushuhuda wako ulioutoa na mada hii uliyoileta, vyote vyashuhudia kuwa una “roho mpya”, na kwaye, ndio hii furaha ninayoiona kwako katika kiwango kikubwa na kitamu saaana, basi endelea mbele, wafuate nyuma mitume, watakufikisha kwa uhakika!!!

  Basi ukifika hapo, kazi ya kwanza ya Roho Mtakatifu ni kukuaminisha Maandiko, utaitikia “Aminaaaa…” kwa kila Andiko, maana yeye hulifunua hilo ili kukupa ufahamu kamili, Biblia huwa “MPYAAA!!!

  Ubarikiwe!

 11. Ndugu yangu Seleli,

  Nilifikili nitachelewa kurudi hadi usiku, nashukuru nimepata wasaa sasa hivi, twende kazi;

  Mimi Binafsi sidhani kama tunaweza hasa kuijua hali halisi ya Mtu akijazwa Roho mtakatifu anakuwaje, bila ya kuangalia wale wanafunzi ndani ya Nyumba walipojazwa na Roho mtakatifu siku ile ya Pentekosite (Mdo.2:1-4) na kuyarejea yale mazungumzo ya Yesu na Mwalimu Nikodemo katika ile Yh.3. Ndipo tutajua hasa kinachomtokea Mtu anapojazwa, Kuzaliwa ama kubatizwa kwa Roho mtakatifu. Na hiyo ni Ahadi ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa Wanafunzi wake na inapaswa kuendelea hadi leo; Iwapo watafuata kanuni kwa mjibu wa Biblia!

  Seleli, Yesu alipokuwa akizungumza na yule Mwalimu wa Uyahudi-Nikodemo katika ile Yh.3, alizungumza mambo makuu mawili, moja ni lile la Mtu asipozaliwa kwa mara ya Pili, hawezi KUUONA Ufalme wa Mungu (Yh.3:3), lakini lile la pili ni kwamba, Mtu asipozaliwa kwa Maji na kwa Roho HATAINGIA katika ufalme wa Mungu(Yh. 3:5)!
  Hiyo ndiyo hali impatayo Mtu akijazwa Roho mtakatifu. Lakini, Je, Ufalme huo wa Mungu ni nini anaouingia au Kuuona Mtu aliyejazwa, au kubatizwa au kuzaliwa kwa Roho mtakatifu? Katika ile Rum 14:17 inasema, ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho mtakatifu. Kumbe Mtu, asipojazwa Roho mtakatifu hawezi kamwe kuona Amani, hawezi kutenda haki na hawezi kabisa kuwa na furaha ya kweli, japokuwa ameokoka!

  Kwa hiyo nukuu fupi iliyopo hapo juu, unaweza kuona kwanini Yesu aliona kuwa ni mhimu Wanafunzi ‘wasiivagae’ kazi ya Uhubiri bila ya Kujazwa Roho Mtakatifu kwanza! Lakini hebu angalia na ujipeleleze wewe mwenyewe kwanza uone, je, ulipojazwa Roho mtakatifu unayemkubali:

  1.Roho huyo ni Yule wakweli?
  2.Ulibatizwa ubatizo wa nani?

  “… wa kwa Jina la Baba na la mwana na Roho mtakatifu au ni ule wa Yohana au ni upi hasa?” Nimeamua kukuuliza haya kwakuwa, bado hukubali maelezo yangu kuhusu nilichokiona wakati ule, nilipo jazwa Roho mtakatifu. Sasa nataka kujua ni kwa nini hasa? Maana kweli huamini, hujisingizii, wala huzalishi udadisi tu, ni kweli hujui! Kwanini hujui? Ahaaaa!….ndiyo, hujui kweli,….Inawezekana tumetofautiana katika kitu kimoja!…. Ni nini hicho?….Ooo ni Neno, Neno la nani? Neno la Mungu!

  Seleli, huwezi kukipata au kukielewa, nilichokipata mimi nilipobatizwa kwa maji na kujazwa Roho mtakatifu iwapo, hukubatizwa sawa na ile Mdo 2:38! Kama mimi! Maana hutapata kile Yesu alichomwambia Nikodemo na ile hali waliyoipata Mitume kiutendaji katika Injili! Kwasababu, unabatizwa ubatizo sahihi na unajazwa Roho mtakatifu ipasavyo ndipo unapata matokeo hayo Bora!
  Kuwachochea watu kwa Asante Yesu…asante Yesu!….asante Yesu!….asante Yesu nyiiiiiiingi! Ili

  “Kumgeinisha momentamu” Roho mtakatifu hiyo ni uigizaji, na uigizaji huwa sawa na tendo halisi, na wengi huamini maigizo zaidi kuliko ile kweli. Imani ni imani lakini tofauti huwa ni yale MATOKEO wayapatayo hawa wawili yaani, yule Mwigizaji na yule Mhalisia! Kwa hiyo, ndiyo maana hata wewe unajikuta una pandisha Roho unaposikia ile Asante, asante nyiiiingi, sisemi hiyo type ni Feki, Maana sijui iko ua haiko katika maandiko! Wewe uliniuliza nikakujibu, hukuamini, nisawa, lakini sababu ya kutokubaliana mimi na wewe katika hili hali sisi ni ndugu, nitaka kujua leo, wewe mwenzangu umepitia njia gani ya ubatizo uliopelekea Roho wa kweli akujae na kisha aje akae kwako, na kukufanya kila unapoisikia ile Asante Yesu nyiiiiiingi inakuwa kama “Katarisiti” hadi Roho mtakatifu akawa “Iginetedi”?! Mimi nilipojazwa Roho mtakatifu matokeo yalikuwa yale niliyokuambia. Sasa Ishu nikuwa, wewe ulibatizwaje?!

 12. Hii ni mijadala kama waliyoanzisha akina kola kuhoji uhalali wa Musa kutumiwa na Mungu kadhalika miriam na Haroun na matokeo yake kila anae soma biblia anajua hatima yao ilivyokuwa.Watu wengine kazi yao ni kukaa na kuangalia vitu wanavyo fanya wengine na kuvianzishia mijadala lakini hawana muda wakumuuliza Mungu ukweli wa mambo, hii ni hatari sana kwa sababu kuna wengine watamkufuru Roho matakatifu na hawatasamehewa kabisa na kupata hasara kubwa ambayo haijawahi tokea kwenye biashara yeyote chini ya jua yaani kuikosa mbingu.Na kila neno atakalo nena mwanadamu chini ya jua lazima atalitolea hesabu nyie mnataka experience mnazojua,Mungu haendi hivyo.Watumishi ambao mmpewa ufunuo kwa jambo hili msikate tamaa kwa maneno yao,bali endeleeni mbele huku mkilitumia kwa uhalali neno la Mungu na bila shaka mmewekewa taji mbinguni,maadamu hayo maneno si matusi tunayaamini kama chombo tu kitumiwacho kwa imani kumleta Roho mtakatifu, Mungu irehemu Tanzania, Mungu rehemu kizazi changu, Roho usiondoke.Amen!!

 13. SELELI,
  Nikushukuru kwa kujari hitaji langu. Kimsingi umeufurahisha sana Moyo wangu!
  ILA,utaratibu, namna na mda wa R/Mtakatifu kumjaa mtu ni mpango wa Mungu ili kukamilisha wokovu kwa mwamini. Jambo hili ni hatua ya pili kati ya tatu ili mwamini awe kamili,Watu wengi wakijazwa nguvu za RM hudhani tayari RM amekwishahamia ndani yao! Hawaelewi kuwa tukio hilo ni maandalizi tu ya RM ili aje akae ndani ya Mwamini hatua ya kukaa RM ni ya tatu na ya mwisho!
  Nitakuletea ufafanuzi baadaye leo usiku.

 14. Lazaro Mabinza,

  WANAFUNZI(mitume pia walikuwemo ambao ndio hao tunafunzwa kufuata msingi wao) ktt mdo 2:1-12 walipojazwa, mstari wa kwanza unasema…..ilipotimia siku ya PENTEKOSTE walikua WOTE MAHALI PAMOJA….fuatilia ktk tamaduni/historia zao za mambo ya sheria na dini/imani..walikua wanafanyaga nini siku ya mavuno(pentekoste)-religious/in our/their case then… spiritual practices including kumshukuru Bwana, mambo ya Ibada nk…ktk hali hiyo ya kuka pamoja(si kwa ajili ya kucheza bao or draft au kuongelea movement for change ya miaka yao) hahiitaji special God’s mind au Human good thinking au ufunuo kujua kua wao being watu wa Mungu, wanafunzi wa Yesu tena wako pale kwa instruction ya YESU….Mdo 1:4, ni wazi kua ktk kukaa kwao pamoja na kufanya ibada…maneno ya kumshukur u Yesu…eg asante Yesu or kumshkuru Yehova..eg asante Yehova na mengoine yafananayo na hayo…yalikua part of their utterance wakati wanaabudu, wanasifu, wanamshukuru Mungu then in that atmosphere suddenly..mistari ya :2:2-4 kitu ndani ya nyumba. So today tukiwaongoza watu kua ktk atmosphere ya kiuwepo-uwepo, kiroho-roho, kii-ibada-ibada, kimaneno-maneno ya kumuadhimisha, kumsifu pia kumshukuru Mungu wakati tunataka kuwaombea ujazo ofcoz au jambo lingine lolote toka kwa Bwana, no sweat at all, ni baraka tu, ni Biblica tu, ni kimsingi wa kimitume na kimanabii still..wewe hulioni ilo/ili?

 15. SELELI,
  Tafadhali ukijibu au kupost jambo ktk SG-group unikopi kwa littraders3@gmail.com (LAZARUS S MABINZA) nitakushukuru!
  Kuhusu tofauti ya jibu (Naijibu post yako ya tr. 27/12/012. 12 mp) uliyoiona
  inatokana na uelewa. “ASANTE” ni njema na ipo
  kimaandiko, lakini “ASANTE”
  hiyohiyo haipo kimaandiko
  kama “TOOL” ya kumfanya
  mtu ajazwe R/Mtakatifu!
  Tumefunzwa kufuata Msingi wa mafundisho uliojengwa JUU ya Mitume.
  Endelea kubarikiwa na BW. YESU KRISTO-Usiache kufanyia kazi ombi langu tafadhali

 16. Herbert,

  Kiswahili,Kiingereza, Kiarabu si lugha za pepo, ni za wanadamu, nani baraka sana kuzijua na kuzitumia, umeshawahi kufikiri ajabu iliyoje kkt Mdo. 2:1-12, Walipojazwa na Roho Mt, moja wapo ya lugha wapendwa wale walitiririka ni kiarabu? lugha ya jamaa zetu wale ambayo wakati mwingine kwa mpendwa ambaye haelewi, ukisikia mtu anaitumia au anaongea unakemea na kudhani/kujisikia eti kama lugha ya majini-majini vile… Yako maneno utayaeleza vema sana kwa Kiingereza na yako mengine yanapenya zaidi kwa Kiswahili na pia nadhani hapa wana-visit watu wa aina mbalimbali si wa Tz tu lakini pia hata wa Tz wenye experience tofauti..wengine wako so exposed ktk lugha na matumizi ya lugha ya Kiingereza kiasi kwamba ktk kujieeleza atajikikuta tu kirahisi anflow kiingereza na mwingine pia ni Kiswahili…ndio maana pia mtu unaweza kutumia zote ili mradi tu kufkisha ujumbe…tunapojifunza Biblia kuna wakati tunalazimika kutumia maneno ya lugha za Biblia za kwanza hebrews and Greek.. so karibu uchangie where did we get..asante..asante method tunapowaombea watu ujazo? nadhani na wewe umejazwa au huamini ktk Holy Spirit filling? …ulijazwaje?..

 17. Mabinza/Lwembe,

  Naomba msome vema post…sijakataaa kua ni mbaya..mimi pia mara ya kwanza nimejazwa Roho Mt. nikiwa naomba mwenyewe chumbani lakin nimekua pia ktk seminar na ibada mbalimbali, kukiitishwa wale wanaotaka kujazwa mara ya kwanza na wale wanotaka kujazwa tena, kufurikishwa zaidi, kujichaji zaidi watoke mbele..nimekua natoka na kwa kutumia one of the ways ya kuwa-gears watu ya ..asante..asante Yesu..nimekua nafurika tena…. Swali langu nilitaka tupate Biblical grounds hata kama hakuna plain/straight sciptures inayosema mkitaka kuwaombea watu waambieni waseme ..asante..asante….Ni kama tunavyokemea uvutaji sigara– je wapi imeandikwa wazi wazi ..””eeeeeeenyi wanadamu msivute bange na sigara”’ wapi? but mbona tuna grounds nyingi tu Biblically za ku-rule out kua iyo kitu kuiingiza ktk hekalu la Roho Mt-our bodies ni batili? Afterall Mr. Mabinza kule ktk SG group..wewe ni kati ya watu walijibu vema hoja yangu…ulileta gorunds kua…”’tunaanza kusema ..Asante kwa kua tunaamini kua yale tuyaombayo yamekua yetu”’..sio wewe au nimekuchanganya na Patrick Kamera ?

  By the way, Lwembe and Mabinza..Kindly tushuhudieni kama nilivyowashuudia wazi wazi, nini experience yenu ya kujazwa Roho Mtakatifu? ilikuaje? naomba ushuuda then we can continue from there…niliomba ushuda huu toka kwako Lwembe kule ktk group..hukunijibu…i real wonder kama mtu unaweza ulizwa jambo tamu na zuri kweli kukuhusu wewe kua ..je lwembe wewe ni mwanaume? wewe ni Mtz? wewe umeoa na unampenda mpenzi wako? kama kweli wewe ni super mwanaume kiroho, kimwil,kinafsi tena ni proud Mtz na umeoa and you are in pure deep love with her..will you answer be like ….IF YOU ARE AT KINONDONI, THEN U GO TO KARIAKOO VIA TAGETA? OR YOU WILL JUST, IN A ROCKET SPEED, EASILY AND HAPPILY CRISS-CROSS VIA MAGOMENI, JAGWANI THEN TAAP U R THERE?

  Press on,

  Blessings

 18. Mnapokuwa na hoja za msingi tafadhalini tumieni lugha yenye kueleweka,kuliko kuchanganya lugha,maana sio wote wanaojua kiingereza na wanapenda kujifunza kupitia hapa,mbarikiwe.

 19. Sasa hao waliojazwa kwa njia ya asante Yesu tunawaweka kundi gani jamani, walijazwa nini?

 20. Seleli,
  Kule kwenye Grupu niliiona hiyo hoja, nimeikuta tena hapa, hali hii imenifanya “nikonsetreti” upya kwa sana! Ktk Biblia hakuna popote panaposema tuwatie “Spidi” kwa Asante Yesu nyiiiingi,ili Watu wampokee RM, mipango hiyo ni ya Shetani, Waganga hutumia maneno kama hayo kupandisha Majini! Asanteni sana wana SG,Seleli na Flano mmenigundulisha mambo mazuri sana, Lwembe CK, kweli ninyi ni “Sojaz” wa Yesu!

 21. “Asante Yesu, Asante Yesu, Asante Yesu, Asante Yesu, x 666!!”

  Katika jambo hili hakuna cha ‘Rhema’ wala ‘Logos’; hakuna ufunuo unaoweza kuyazidi Maandiko, hizo “Asante Yesu” labda mzifanye kuwa ndizo zile kazi kubwa mlizoambiwa mtazifanya!! Vinginevyo, katika urahisi wa uelewa, Logos ni Neno, hayo Maandiko, yakiwako hapo katika Biblia yako kwa siku ya leo, na kadiri unavyoibeba kwenda kanisani au popote pale, basi jua huyo uliyembeba ndiye Logos. Rhema ni kule kunena, utterance. Yaani unapoisoma Biblia yako, iwapo utaisikia sauti ikiyaongea hayo unayoyasoma, ikayafunua kwako, nawe ukayaelewa hayo, basi hicho kinachokutokea, huyo uliyemsikia sauti yake, ndiye Rhema. Kwa kifupi ni kwamba Logos ni Kristo akiwa amesimama hapo, na Rhema ni Kristo huyo huyo akiongea nawe!!!

  Basi hizo “Asante Yesu” kama mnavyoona, hazina uhusiano wowote na Maandiko wala Rhema, chimbuko lake ni nje ya Maandiko ambayo ndiye Roho Mtakatifu! Kwahiyo kwa kifupi tuelewe tu kuwa hizo “Asante Yesu” ni invocations zinazoyaleta maroho ya dini na kuwalipua watu into kushandarize na maishara na mawingu ya upako yakiwaingiza into “full kujiachia” yakilileta kusanyiko zima kinyume, sawasawa na kile mtume Paulo alichosema msikifanye!!! 1Kor 14:23
  “Basi, kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanza kusema kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaida au wasioamini, je, hawatasema kwamba nyinyi mna wazimu?”

  Lakini jambo kubwa lilopelekea kujipenyeza kanisani kwa urahisi kwa haya maroho ya dini, ni wale viongozi kama akina Seleli walipokataa kuisikiliza Rhema, wakati Mungu anaongea nao wanaongea, wakaishia kuondoka na jambo ambalo sio! VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU na ROHO MTAKATIFU ni vitu viwili tofauti ambavyo wao viongozi wamekifanya ni kimoja!!!

  Basi jaribuni kuyatenganisha kwanza hayo mambo mawili, Vipawa na mwenye vipawa vyake, yanayofuata hayana tabu, yote yanajipanga sawasawa, sasa ndio utayapata yaliyo halisi, yakijiendesha ndani ya UTARATIBU, kila kitu halisi, kuanzia vipawa mpaka Roho Mtakatifu wa Kweli! Vinginevyo tutaendelea na ‘mahepe’!!

  Bless u all

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s