Heri ya mwaka mpya 2013……..Ushindi zaidi kiroho na kimwili

heri-ya-mwakampya
Wapendwa nawatakia 2013 iliyojaa matumaini ya ushindi kimwili na kiroho.

-Mungu alinde yote mazuri aliyotujalia 2012 na akatuzidishe kwa utukufu wa jina lake.
-Atusamehe tulipokosea na akatutie nguvu ya kushinda yale tuliyoshindwa 2012.
-Akafanye mapya&mazuri zaidi yatakayotusahaulisha yaliyotuumiza au tuliyopoteza.
-Atuongezee unyenyekevu, upendo na haki ili wengine wafurahie uwepo wetu duniani.
-Tukaishi kwa usafi na utakatifu zaidi kwa kuwa siku zetu kuishi duniani zinapungua..

Isaya 43;18-19
Msiyakumbuke mambo yaliyopita, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitafanya jambo jipya! Sasa litachipuka, je, hamtalitambua? Nitafanya njia jangwani & vijito vya maji katika nchi kame.

Isaya 60;18 & 20
Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako,wala maangamizi au uharibifu…Nazo siku zako za huzuni zitakoma.

1Wakorintho
“Lile jambo ambalo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia, wala halikuingia moyoni Mungu alilowaandalia wale wampendao.

–Imani Kapinga

Advertisements

9 thoughts on “Heri ya mwaka mpya 2013……..Ushindi zaidi kiroho na kimwili

 1. cha msingi kuishi maisha ndani tukiwa na yesu kristo, utakatifu ili tuishi naYesu milele zote,asante kwa salam za mwaka mpya ubarikiwe sana

 2. Rafiki yangu Siyi,
  Hahahahah…! umenifurahisha sana kwa ujanja wako!
  Hebu ondoka katika wishful thinking, njoo katika uhalisi wa mambo. Hapa tunazungumzia salamu za “mwaka mpya” kulingana na kalenda ya Gregory, hatuzungumzii hesabu za utofauti wa miaka ya kiBiblia na ya hii kalenda inayotumika. Hatuzungumzii elimu ya mambo hayo, ingawa ni jambo zuri kwa wapendwa kulijua hilo, bali tunazungumzia jambo tulilonalo, ndipo nikasema, “Labda tukusikilize nawe Nzala, Kalenda yenu ikoje?” Yaani uitazame kalenda yenu mnayotumia halafu utupatie hiyo tarehe! Au kama nanyi hamna hiyo kalenda, bali wepesi wa kulaumu na kulalamika tu, ili mradi kupanda mbegu za hitilafu na kuwavuruga watu, ndiyo tungependa yajulikane hayo!

  Basi kama nanyi mnayo kalenda yenu tupe tuikague kulingana na Maandiko ikiwa iko sawa sawa, tutajumuika pamoja kuipigia debe!!!

  Ubarikiwe, Siyi na woote!

 3. Nimeituma post yangu miaka imeparanganyika. Ukiangalia hapo, utachukua hizo siku 8993.25 ugawe kwa 360 ili upate hesabu sahihi

 4. Mwaka Una Siku Ngapi??
  Ukisoma historia ya mambo ya kale kabisa(kipindi cha miaka 3000’s BC,), kumbukumbu nyingi za mambo hayo, zinaonesha kuwa, dunia hadi leo ina miaka zaidi ya 6,000 tangu kuumbwa kwake. Na tangu mwanzo, miaka ilikuwa ikihesabiwa kutoka juu kushuka chini hadi kipindi cha Kristo. Mabadiliko mengi ya wakati na majira katika ulimwengu huu, yalianza kuonekana kushika kasi kuanzia karne ya nne japo mipango ilikuwepo hata kipindi cha kuzaliwa kwa Kristo. Mpaka leo, mabadiliko makubwa yamefanyika, kiasi kwamba wanadamu wasiomjua Mungu wamebaki njia panda . Na wengine, wamebaki kuunga mkono sera ya ibilisi, jambo ambalo ni hatari sana.
  Biblia Mwongozo Wetu
  Kama wafuasi wa Kristo, Biblia itakuwa ndiyo msingi wetu mkuu kwa mafunuo ya mambo haya ili tuyajue. Tangu uumbaji, nyakati(mida) zilikuwa zikipimwa kwa kutumia mianga ya nuru (mwz 1:14-19) na vizazi vya Adamu. Kibiblia, miezi tunaambiwa ilikuwa na siku 30(mwz 7,8 na ufu 11). Na hakuna msatari ndani ya Biblia unaosema kuwa mwezi una wiki nne tu (yaani siku 28). Biblia iko wazi kwa saa za siku nzima kuwa ni 24(Yohana 11:9), Juma siku 7 na mwezi siku 30 tu na siyo idadi ya wiki ndani ya mwezi bali siku tu.
  Swali la kujiuliza, kwa nini leo kuna tofauti??
  Ukitumia kalenda ya Biblia, utagundua ulaghai wa Ibilisi. Shetani kupitia mawakala wake(wanadamu waovu) alibadilisha mpango mzima wa Mungu wa majira na sheria ili litimie neno lililotabiriwa na nabii Daniel 7:25( “….naye ataazimu kubadili majira na sheria…..”) . Ndani ya Biblia, mwaka mzima una miezi kumi na mbili tu. Mimi sijaona sehemu ambayo tunaarifiwa kuwa miaka ilikuwa na na miezi zaidi ya hiyo. Mungu aliwafundisha watu kuhuesabu miezi kuanzia mwanzo mpya wa mwezi(mwonekano wa mwezi mpya) hadi mwanzo mwingine. Mungu aliita miezi wa kwanza, pili, tatu nk. Majina ya miezi hii, waliita wanadamu kwa sababu walizoziona wao. Angalia miezi ndani ya Biblia…

  Mwezi wa Kwanza – Nisani au Abibu (Esta 3:7, Nehemia 2:1, kutoka 12:2, torati 16:1)
  Mwezi wa Pili – Zivu au Iyari (1 Falme 6:1, 37)
  Mwezi wa Tatu – Siwani au Sivani (Esta 8:9)
  Mwezi wa Nne – Tamuzi (2 Falme 25:3, Jeremia 52:6, Ezekiel 8:14)

  Mwezi wa Tano – Abi au Av (2Falme 25:8, Hesabu 33:38, Ezra 7:8-9)

  Mwezi wa Sita – Eluli au (Nehemia 6:15, Hagai 1:1, 15)

  Mwezi wa Saba – Ethanimu (1Falme 8:2)

  Mwezi wa Nane – Buli au Cheshvani (1falme 6:38, 12:33)

  Mwezi wa Tisa – Kisleu (Zekaria 7:1, Nehemia 1:1)

  Mwezi wa Kumi – Tebethi (Esta 2:16)

  Mwezi wa Kumi na Moja – Shebati (Zekaria 1:7)

  Mwezi wa Kumi na Mbili – Adari (Esta 3:7, Ezra 6:15)
  Hii ndiyo miezi ya Biblia ambayo hata watakatifu wa zamani waliifahamu vizuri. Shetani aliibadilisha tu na kuichanganya sana ili wanadamu wachanganyikiwe na kufuata mawazo yake ya kuudanganya ulimwengu. Tunamshukuru Mungu ametupatia NURU, nuru ambayo ni neno lake. Nasi tunaotembea katika hiyo NURU, sharti tuuone udanganyifu wake(ibilisi) huo na kisha tuukatae kabisa. Angalia alivyochanganya mianzo na miisho ya miezi. Mwezi wa shetani ulianzia katikati ya mwezi wa kibiblia na kuishia katikati ya mwezi mwingine wa kibiblia. Angalia…

  Mwezi wa Kibiblia Urefu wake Kalenda ya Kirumi
  1. Nisani Siku 30 March-April
  2. Zivu/ Iyar Siku 30 April-May
  3. Siwani/ Sivan Siku 30 May-June
  4. Tammuzi Siku 30 June-July
  5. Abi/ Av Siku 30 July-August
  6. Eluli Siku 30 August-September
  7. Ethanimu/ Tishri Siku 30 September-October
  8. Buli/ Cheshvan Siku 30 October-November
  9. Kisleu Siku 30 November-December
  10.Tebethi/ Tevet Siku 30 December-January
  11. Shebati/ Shevat Siku 30 January-February
  12. Adari Siku 30 February-March

  Hadi kufikia kipindi cha kuzaliwa kwa Kristo, vuguvugu la kubadilisha miezi hii lilikuwepo japo lilikuwa halijashika kasi. Baada ya Yesu na mitume wake (thenashara) kupita, mabadiliko rasmi ya miezi hii yalifanyika miaka ya 300’s AD(karne ya 4). Kipindi hiki ndipo tunawaona akina Julias Caesaria na wengine wengi waliofuata (utawala wa Rumi), wakibadilisha taratibu nyingi sana(majira na sheria na sheria za Mungu) ndani ya Neno la Mungu. Ukisoma Katheksimu ya Waumini kipengele cha sheria za Mungu, utaelewa ninachokisema hapa. Hawakubadilisha miezi tu. Walibadilisha Saa(ndiyo maana leo ukiambiwa ni saa 1:oo aubuhi, itasomeka 7:oo asubh), Mianzo ya siku (Badala ya siku kuanza jua linapochwea, wao wakaamua siku ianze usiku wa manane), Siku za juma(ya kwanza ikawekwa ya mwisho na ya mwisho ya kwanza), Siku za miezi(badala ya mwezi kuwa na siku 30, wakaamua miezi mingine iwe na siku 28, 29, 30 na 31).
  Shetani amefanya haya yooote kwa makusudi kabisa. Ameiba miaka mingi ya Mungu ili tusifikiri kuwa muda umekwisha sana na Yesu yu karibu kuja kulichuka kanisa lake. Kwa mf. Ukichukua ile miaka 5 (kwenye idadi yake ya siku kwa mwaka ambayo ni 365¼) na ukazidisha na mwaka wa leo kuanzia karne ya nne, utapata miaka mingi sana aliyoiba shetani. Sasa tufanye kidogo..
  2013-300= 1713
  Chukua 1713 x 5 = 8565
  1713 x ¼ = 428.24
  Jumla utapata siku 8993.25
  360

  Miaka iliyopotea ni 24.9 au 25
  Sasa chukua miaka 25 uijumulishe na 2013 = 2038. Hiki ni kipindi cha rehema. Ukiangalia historia ya wenzetu wa Gharika, ilikuja miaka 2000 tangu kuumbwa kwa dunia. (Sodoma, Gomora na ile miji mingine mitatu), waliangamizwa miaka 2000 baada ya gharika. Na miaka 2000 ilipita hadi kipindi cha Yesu kuzaliwa. Tangu hapo hadi leo, ni miaka 2000 tena na zaidi…
  Sherehe ya Mwaka Mpya
  Je, tunaweza kusema sasa kwa miaka hii kuwa leo ni mwisho wa mwaka au mwanzo wa mwaka? Kwa misingi ipi? Je, tunaweza kuikokotoa ile miaka yoote aliyoiba shetani, halafu tukafahamu miisho na mianzo ya miaka mipya kwa leo?? Inawezekana kweli? Tukiweza, na tufanye hivyo kama Wakristo. Tukishindwa kuipata vizuri na kwa usahihi wake, NI HERI TUKAKAA KIMYA KULIKO KUENDELEA KUDANGANYA WATU kuwa leo ni mwisho au mwanzo wa mwaka mpya. Mungu anatushangaa sana wengine tunapotangaza hadi makanisani, eti sabato/ibada ya mwanzo wa mwaka au mwisho wa mwaka. Ni lazima tuwe tofauti na wengine(wasiomjua Mungu). Na wakituuliza sababu, tuwaambie tu!! Hakuna haja ya kuwapigia watu filimbi ya shetani ya kuwapeleka watu jehanamu. Heri tuendelee kung’ang’ana na Bwana wetu. Tuko kwenye kipindi cha mwisho sana. Ni muda wa kumtafuta Mungu tu. Si muda wa kuchezacheza na kutaka kufanana na dunia. Moto anaouzungumzia Mtupe Petro(2 Petro 3:7) u karibu kuichoma dunia na dhambi zake. Utakuwa wapi wewe. Mtafute Mungu!! Tafuta kweli ya Neno lake ukaokolewe!!
  Bwana awabariki nyote
  Nduguyenu ktk Bwana
  nzala

 5. Nzala,
  Hebu yakamilishe maelezo uliyoyatoa kuhusu siku katika mwaka. Unasema mwaka wa Biblia una siku 360 tu, na unawakataza watu wasisherehekee mwaka mpya huu wa siku 3651/4, ingependeza sana kama ungetuonesha mwaka huo wa Biblia ambao ninyi mnautumia, unaanza lini na kuishia lini, kama ambavyo Waisilamu wameweka wazi miezi yao, wakiiegemeza katika miandamo ya mwezi, ambao huwa una aidha siku 29 au 30 .

  Na wengine nao, wale wa kundi la “nabii Eliya”, hawa mwezi wao una siku 28, na hivyo mwaka wao utakuwa na siku 336. Kundi hili husherehekea Krismasi katika mwezi wa Februari tarehe 28, au kiBiblia mwezi wa Adari, ukiwa ndio mwezi wa 12, kwa hiyo mwaka mpya wao utakuwa mwezi March.

  Lakini kwa kadiri utakavyo watazama ndugu hawa, (wa kundi la “nabii Eliya”) utagundua kuwa ni kundi lililochanganyikiwa! Hebu tazama jambo hili: mwezi wao una siku 28, kwa hiyo mwaka ni siku 336, kwahiyo iwapo mwezi wa Adari ndio February wa kalenda inayotumika, hiyo Gregorian, basi kwa tofauti ya jumla za siku kati ya kalenda hizi mbili, mwezi wa Adari hauwezi kubakia kuwa huo Februari katika miaka yote, unapaswa kuwa unahama hama kulingana na tofauti hiyo ya siku hizo 291/4; lakini kwao hiyo miezi iko fixed, unabii wa Uongo!!!

  Labda tukusikilize nawe Nzala, Kalenda yenu ikoje? Isije ikawa mlipewa ujumbe nusu na nabii wenu, nanyi mmetoka nao hivyo hivyo, na sasa mnaleta confusion kwa kukaririshwa mambo msiyoyaelewa. Nangojea hiyo kalenda yenu inisahihishe kauli hii niliyoitoa!

 6. Wapendwa Strictly Gospel,

  Namshukuru Mungu kwa ajiri yenu na kuwatakia Baraka tele za Mwaka 2013.

  Uwe wa mafanikio mengi katika kulisha kondoo wa Mungu.

  Barikiwa

    Josephat Kyaruzi, Managing Director, InfoBridge Consultants Ltd. GIS,Remote Sensing, Surveying, MIS, EMIS Consultant, GeoSpatial Training

  2nd Floor, Room 6B, Blue Pearl Hotel, UBUNGO PLAZA, Morogoro Rd, P.O. Box 32108, Dar es Salaam, Tanzania Mob: +255-71-3453213 or +255-75-5219322, Tel/Fax: +255-22-2461212, http://www.infobridge.co.tz

  ________________________________

 7. Asante ksks imani,ni vyema tukamtukuza mungu kwa kila jambo,hili nalo la kuumaliza mwaka ni la kumtukuza amina.

 8. Asante sana mtoto wa Baba. Lakini kama Mkristo, jaribu kufikiri kama tunasherehekea 2013 kihali. Mwaka ndani ya Biblia una siku 360 tu. Na mwishoni mwa siku hizo, sisi (Wakristo), ndiyo tulipaswa kuusherehekea mwaka mpya. Je, tunapoungana na ulimwengu kuusherehekea 3651/4 kama mwisho wa mwaka, Mungu atatuweka kwenye kundi gani ikiwa sisi ni kundi alilotuchagua na kutupa elimu kubwa kuliko walimwengu???
  Bwana awabariki sana.
  nzala

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s