Ustawi wa nchi, Maombi yanafaa sana!

A supporter of opposition leader Kizza B

2015 wapendwa Tafadhali, Tuingie/tusijihusishe katika siasa, tuanze sasa, mambo ya kizamani eti siasa ni pepo ilikua hakuna ufahamu tu wa Neno, adhari ya baadhi ya mapokeo/mahubiri tuliyopewa kwanza au viongozi wetu walikua na misistizo kwa mambo mingine mazuri  zaidi na hili la siasa likaachwa. Lakini ktk Biblia,kuhusika kwa watu wa Mungu ktk mambo ya serikali, siasa na utawala ni wazi kabisa wala hamna ugumu kuelewa.Mfano,yupo waziri Mkuu wa enzi hizo, Yusufu tena alikuwa mkimbizi, pia Shadrack, Daniel, Meshack, Abednego walikua magavana-wakuu wa majimbo, leo ni kama RC/DC  na pia Wafalme leo ma-Rais akina Hezekia, Saul, Daudi, Yeshoshafati. Kwanini tujihusishe? ni kwa kua tumefanya jambo moja tu..KUOMBA lakini tumeacha kabisa KUTENDA/KUCHUKUA HATUA..imani bila matendo haina matunda…kama tumewaombea miaka yote hii, hawabadiliki na tunaumia na kuchukia yatendekeyo, kwa nini tusihusike sisi wenyewe?

Mimi napenda na naweza sana na Bwana, kufanya uhamasishaji Nchi nzima katikati ya Wapendwa..AM SERIOUS! je mnaweza kuniunga mkono? tukatengeneza Team?  au nyie wenzangu mna mpango gani kuelekea 2015 kuhusu uhai wetu kikanisa na umiliki wa nguvu ya maamuzi ? Mtaendelea  kuomba tu kua watabadilika  siku moja? bila kutenda kitu cha sisi wenye nuru kukaba nafasi ya Ubunge, kujiunga na vayama vya siasa, kuchkua nafasi ndani ya vyama na hata nafasi nyingine za kufanya maamuzi ktk sekta za Kisiasa mpaka Kiuchumi na Kijamii?

Press on,

Seleli

Advertisements
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

3 thoughts on “Ustawi wa nchi, Maombi yanafaa sana!

 1. Yatosha hao wazee kutufikishia habari ya wokovu, japo kulikuwa na makosa mengi lakini wametusaidia tukamjua Mungu. Sasa ni wajibu wetu kuisema injili ya Yesu kristo kwa usahihi zaidi, hasa sisi vijana ambao tumesoma na kuelimika tunawajibika kuusema huu ukweli kwa nguvu zote,huku tukiwa tayari kupambana na upinzani (Resistance to change) wowote utakaojitokeza

  Tuyakatae mapokeo ya Usichanganye siasa na dini,maana kiukweli hakuna namna unaweza kuitenganisha siasa na imani ambayo mtu anaamini kwayo,maana siasa ndio inayohusu maamuzi ya kijamii yenye kuleta matokeo ya jinsi tunavyoishi kama jamii.

  Mfumo wetu na uhuru wa kuabudu ni matokeo ya maamuzi ya kisiasa, ndio maana sasa wakati umefika wa hao watoa maamuzi (wanasiasa) kuwa watu wanaomcha Mungu aliye hai.

  Kwa kufanya hivyo litatimia andiko lisemalo mwenye haki akitawala watu wote hufurahi, au lisemalo haki huinua taifa.

  Haiwezekani leo kanisa linakuwa limegawanyika, wengine wanapigia kura watu wenye haki na wengine wanapigia mafisadi, na matokeo yake wasio haki wanashinda na ndio wanaotoa maamuzi yenye matokeo tunayoyaona, umasikini kila kona, bila kubagua wacha Mungu (wapendwa) na wasio wacha Mungu

  Nimesema safari hii mimi nafunguka zaidi mbele za Mungu kwa kumwomba ampe mtu fulani ushindi au chama fulani. Siwezi kuendelea kufanya maombi ya kumung’unya maneno wakati wanaogombea tunakuwa tunawajua tabia zao na tabia za vyama vyao,halafu unakuta maombini tunaambiwa mwombe Mungu ajipatie mtu anayetaka mwenyewe, utadhani yeye ndiye anayeshuka kupiga kura

  Seleli andaa huo mpango vizuri,nitakuunga mkono!

 2. Mpendwa Seleli,

  Goodmorning to you. Nimefurahishwa sana na maono yako. Leo nimepokea SMS za wakristo wengi zikisambazwa kueleza kwamba Kanisa la Tanzania limepata pigo kwamba watanzania wengi karibu mikoa yote ukiacha Mbeya na Mwanza wametoa maoni mbele ya Tume ya Maoni ya Katiba wakitaka nchi iwe na Katiba inayoruhusu uwepo wa Mahakama ya Kadhi.

  Swala la kumiliki nguvu ya maamuzi sisi kama wakrissto wapendwa haliwezekani kwa mtazamo wangu kwani ukitazama kanisani wapendwa wengi wameishia darasa la VII. Yaweza kuwa zaidi ya 80% wote wana level ya darasa hilo. Wenye shahada ya Kwanza huenda wako 7%, wenye Masters Degree huenda waka 3% na 10% iliyobaki waweza kuwaweka kundi lolote ama la wasiomaliza hata drs la 7 au wasio na elimu kabisa.

  Ukitaka kuelewa hilo fanya survey ndogo tu uniambie hapa Tanzania ni makanisa mangapi ambayo maaskofu wao wameshatunukiwa shahada za Uzamili na za Uzamivu (Masters or PhDs) katika makanisa ya kilokole kama ni wengi wenye PhD za ukweli hawafiki 15 nchi nzima. Maaskofu au wachungaji wenye Masters Degree kama ni wengi hazidi 30 nchi nzima.

  Hii itakupa picha kwamba kanisa la Tanzania bado linaongozwa na watu wenye elimu ndogo sana. Yaani bado kabisa. Ikiwa hata kanisa halina wasomi kwa kiwango ambacho kinaridhisha je, unataka kanisa hilo hilo liende hadi kwenye kumiliki ngazi za maamuzi ya kisiasa?

  Kwanza tuhamasishe viongozi wa makanisa yetu wasome sana. Wenye Diploma ya Theolojia waende wakapate Degree ya Uchumi, Jamii, Siasa, Fedha,nk. Kisha waendelee wapate Degree za PhD. Yaani tunapaswa kuwa na wachungaji kibao wenye PhD kwa wingi.

  Yaani kama tuna wachungaji wa kilokole Tanzania wapatao 10,000 (mfano) basi kati yao wenye PhD wazidi 80%. Hapo Kanisa la Tz litakuwa na nguvu hata ya kukaripia watwala nao wakawasikiliza. Yes, watawala watakuwa hawana pa kuanzia wala kukwepea.

  Lakini leo hii, ni mchungaji yupi au Askofu wa kilokole mwenye uwezo wa kutoa taarifa za kiutafiti (Professional analysed and researched information) ambaye anaweza kuwakemea mawaziri hawa wenye Elimu kiwango cha Masters na PhD nao wakamsikiliza na kufuata ushauri wake? Hakuna. Hii yote ni kwa sababu kanisa lina wachungaji wengi wasio na elimu ya kiwango cha Juu kama ilivyo Amerika au Ujerumani au UK.

  Wachungaji wetu wengi hata kutoa “Press Conference” hawawezi. Hata kwenda kwenye TV au Redio wakahojiwe na watangazaji tu wanaogopa. Sembuse kwenda kwenye mikiki mikiki ya siasa uchwara za nchi hii? Weeeee, tulia kwanza.

  Seleli mimi nitakuunga mkono kama tu utaanzisha Team ya kuhamasisha Viongozi wa makanisa NA WAPENDWA wajiendeleleze kielimu hadi ngazi ya PhD. Baada ya miaka 10 tuwe na madokta makanisani wengi zaidi ya 60% ikiwezekana. Badala ya viongozi wengi siku hizi kukimblia Nigeria kutafuta maupako uchwara, wakimbilie vyuo vikuu vya Tanzania au nje ya Tz kupata mashahada kibao.

  Kumbuka siku hizi “Mungu hatumii watu waliosoma bali anatumia wanaosoma”

  Wachungaji wetu wengi zaidi ya 95% hawasomi wala kuandika vitabu. Mwakasege tu ndiye naona anaajitahidi. Wengine wanajidai kuwa wanaongozwa na Roho so hawana haja ya kusoma vitabu sembuse kuandika vitabu.

  Jiulize leo, “HUYO MCHUNGAJI WA KANISA LAKO AMESHAANDIKA VITABU VINGAPI? JE, ANA KIWANGO GANI CHA ELIMU?

  Hapo kanisani unaposali watu wenye PhD ni wangapi? Ukipata majibu Chukua Hatua.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s