Kijana Soma Ujumbe wa Leo!!

vijana

Salaam,Peleka ujumbe huu kwa kila Kijana unayempenda, Utabarikiwa sana kwa kuwasaidia wengine. Neno la Leo:  Mhubiri 11:9-10 “Wewe, Kijana, uufurahie ujana wako, na Moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za Moyo wako, na katika Maono ya macho yako; Lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta Hukumuni. Kwa hiyo ondoa MAJONZI Moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; Kwa maana Ujana ni Ubatili …..” TAFAKARI:

Kila kunapokucha tunashuhudia asilimia kubwa ya Vijana wakipoteza mwelekeo wa Maisha, wale waliokuwa wanategemewa na wazazi na hata jamii unashangaa ghafla maisha yao yanakuwa ya Majuto daima, wimbi la vijana Machangudoa, mateja, walevi wa madawa na pombe, wanaofeli mitihani, wanaoacha shule, wanaopata mimba nje ya ndoa, Vichaa na mazezeta, wanaojiua kwa kukosa Amani, n.k. yanazidi kuwa tatizo sugu yanayoongezeka katika kizazi chetu kila siku Wewe Kijana! bila kujali uwezo wa akili ulio nao, kiwango cha elimu yako, uzuri wako, vipaji ulivyo navyo, uwezo wa mali yako, kazi nzuri uliyonayo, bila kujali una wapenzi wangapi wanaokupa raha; kama hutasikia sauti ya Mungu inayosema nawe leo, katika muda usioutarajia utaomba Dunia ikufunike usiendelee kuishi. Hayo yote unayoyaona yana SUZA moyo wako na kujisikia unakula BATA ni MABOMU ambayo Adui shetani ameyatega, yakifyatuka hakuna wa kuyazuia mpaka yatimize kusudi la kuua.

Wewe mwenyewe ni shahidi, fikiri juu ya huyo unayemwita “sweet” na mapigo ya moyo kwenda mbio mnapokuwa naye faragha au kupagawa unapopata sms ya mapenzi kwa njia ya simu au mtandao, na hatimaye kujituliza kwa kuvunja Amri ya Mungu inayosema USIZINI – Hilo ni Bomu, tarajia kuvuna upepo wa Kimbunga. Kumbuka kila anasa unayoifanya, inakufanya kuwa Adui wa Mungu aliye Muumba wako: somaYakobo 4:4 “Enyi wazinzi hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa Dunia ni kuwa ADUI wa Mungu?…..”  Sio salama kuweka UADUI na Mungu ambaye ndiye mwenye hatma ya maisha yako.Utakuta kijana anatembea bega moja chini na jingine juu huku kavaa suruali makalio nje utafikiri anakwenda haja, akina dada nao matumbo wazi huku maziwa yakichomoza kama embe dodo zikingoja wa kudungua, hata kwenye majumba ya Ibada imekuwa sehemu za Biashara za Viungo vya akina dada. Uchaji Mungu umepotea kwa Vijana, ndio maana utakuta nyimbo za kizazi kipya zinaimbwa Makanisani mfano. Hi pop, RNB, Rege, Ndomboloo n.k. Vijana wana RAP kama hawana akili nzuri. Hayo yote yanaonyesha ni kwa kiasi gani ADUI shetani ameteka mioyo ya Vijana.Wito:Vijana bado rehema za Mungu zingaliko, amueni kusimama upande wa Mungu atawashindia, Yule aliyebadili maisha ya Makahaba, majambazi, wauaji, wavuvi n.k wakawa wahubiri wa Injili, yuko tayari pia leo hii kuwaumbia mioyo mipya kwa njia ya Roho mtakatifu. Yakobo 4:7 “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia” Ni wakati wa Kusema Shetani “NO”.
MUNGU AWAPATIE USHINDI NA BARAKA TELE KATIKA SIKU ZA MAISHA YENU.

–Ev:  Eliezer Mwangosi

Advertisements

3 thoughts on “Kijana Soma Ujumbe wa Leo!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s