Je huwa anakuwepo/anakuja/anakaa na kutoweka au wanakaa/wapo siku zote?

kusanyiko

Wandugu,

Nadhani ni vema na haki kua watu wa Kiroho sana lakini hiyo sidhani kwamba inatuzuilia kutumia uwezo wa kibinadamu Mungu aliotupa vilevile yaani akili, uelewa, kuwaza,kufikiri kwa kina na kupima mambo kwa fikra za kawaida au pevu.Nadhani tukilalia upande mmoja tu  kwamba kila kitu ni kwa roho tu na  na kwamba upande wa pili hauna kazi, kuna mambo tutashindwa kuyapeleka au  kuyafanya kwa uzuri

Kwa msingi huo basi, naomba nikuchagize tufikiri kidogo pamoja na kwamba tuko rohoni. Neno la Mungu linasema ..”walipo wawili watatu Mimi nipo kati yao” na pia ”Bwana huketi ktk sifa za watu wake”… in effect, tunakua tunaamini na kwakweli kwa hakika tunajua ni ndivyo ilivyo. Sasa tufikiri maswali yafutayo:

Tunakua ndani ya ibada..zaidi ya watu 2,3…na tena tunasifu na kuabudu ivyo tunakua na some of the basic qualifications at least ya Mungu/Yesu/RM kua katikati yetu, NEVERTHELESS, mpendwa akiambiwa aombee sadaka au safari, au wakati wa Neno,anasema ”Baba ktk Jina la Yesu, ninamfunga shetani na kutimua mapepo yote” hao majaaa wamekujaje /walikaa wapi wakati MZE WA SIKU,MASTER na GIANT HOLY SPIRIT wote walikuwepo/wapo?

AU tunapoomba tunakua na concept  ile ya Ayubu 1:7 ambayo nayo ni Neno la Mungu kua shetani alimjibu Mungu anatoka zunguka huku na kule duniani ndio maana tunajua/dhani kua hata kama tumeimba/abudu na  MZE WA SIKU,MASTER na GIANT H.SPIRIT wamejaa tele yet devo anaweza zuka katikati yetu?

Kwani ktk uwepo wa hosts of heaven’s head quarter mahala fulani,devo atakaaje hapo au anakaa but nje ya zone ya mwisho wa uwepo wa delegation ya mbinguni yaani kama uwepo umefika mabwepande-mbagala-gongolamboto to kigamboni then rishetani litakua kuanzia miisho iyo kuendelea mbali na si kuulekea uweponi mwa Mungu wetu?

Kama jibu ni ndiyo, Je uwepo wa Mungu una mwisho? si dunia  hii yote ni sehemu ya kuweka miguu? Yule jamaa  na madogo yake wanakuaga wapi?

AU hawa majamaa dont exist kama invissible creatures bali ni kimawazo tu na ivyo tunao benet-benet kwakua mawazo tunayo tu as long as tumebeba vichwa-(wana heri wasio na vichwa bali roho tu) na ivyo ni sahihi kila mara kupambana naye/nao hata wakati wa kuombea sadaka, safari,Neno hata kama tumo ndani ya uwepo wa Mungu?

Lakini Je hatuooni ni wakati wa kuangalia upya (revist) mambo ambayo tumekua tunayafanya miaka na kuya-adjust mfano..wakati wa kuombea NENO,safari,sadaka, tukasema….”Baba nakushukuru kwa kua huko hapa/pale na siku zote unanisikia ivyo kwakua uko hapa/pale/naye basi Neno lako litapokelewa kwa uzuri/ watu watasikia raha na kutaka kutoa sadaka na safari itakua njema?

Je kila mara tukiwa tunamkemea jamaa ingawa hatumpendi siyo kwamba tunampa credit ambayo hana kwakua wakati tupo Dar tunakemea, kule Moro,Arusha,Singida,  mida iyoiyo ya Neno, sadaka wanakemea nako, je amekua na sifa/ ame-acquire hi quality ya kua na nguvu ZOTE,kuwepo mahali KOTE, maarifa YOTE  lini?

Je tunaweza balansi/connect vipi  maandiko/Neno kama  ilo la Ayubu la devo/wadogo zake kuonekana kama wako karibu-karibu na Mungu vile wanapiga story, au la mfalme kupigiwa music ili devo apoe au la saul/mganga kumpandisha mzimu kama vile samweli na sauli kuongea naye, au la roho mbaya akatoka kwa Bwana, Yesu kumfyatua devo alo-sijui mwingia au mtumia Petro, kwa upande mmoja na yale maandiko mengine matamu ya walipo 2,3 nipo,or Bwana kukaa ktk sifa, nitakua nanyi siku zote-yaani benet-benet nasi, makuhani wakashindwa kuperform kwa uwepo uliojaa hekaluni,mimi na Baba tunafanya home ndani yake nk?

Press on befriending the powerful book, The Bible

Amani iwe nanyi enyi nyote,

Edwin Seleli

Advertisements

8 thoughts on “Je huwa anakuwepo/anakuja/anakaa na kutoweka au wanakaa/wapo siku zote?

 1. Ndugu yangu Seleli Edwin,
  Unatusisitiza tu ’Press on befriending the powerful book, The Bible’; hili ni jambo jema saana. Basi utakuwa umenisaidia saana na kunijengea huo urafiki na Biblia, ukinionesha ni Maandiko yapi yanayosema “mganga alimpandishia Sauli mzimu uliojifanya kuwa ndiye Samweli” kama kauli yako hii: “au la saul/mganga kumpandisha mzimu kama vile samweli na sauli kuongea naye” inavyoonesha!

 2. Bwana akubariki Eunice, after all, life is just a song, a song of praise, we will praise the Lord Jesus Christ, all the way up!!!!

 3. Bwana uu sehemu yangu, rafiki yangu wewee
  Katika safari yangu, tatembea na wewe
  Pamoja na wewe

 4. SHETANI HAJAZUILIWA KWENDA AU KUWA KULIPO NA MAHUDHURIO YA KI-MUNGU! NA HUWA HAPO KIKAZI TU, KUKEMEA AU KUVUNJA KAZI ZAKE, KUTAFANIKIWA TU IKIWA SHETANI YUPO HAPO KWA KIBALI CHAKE MWENYE, MAANA NAYE NI MTUMISHI! WAAMINI WENGI HAWANA, NA HAWATAKI KUWA NA ELIMU YA KUMJUA SHETANI NA KAZI ZAKE, MATOKEO WANABAKI KUONGOPEWA TU “NAULI YA WOKOVU NI MAARIFA!”HUWEZI KUJIFANYA ATI UNAMJUA YESU NA JINA LAKE WAKATI UPO “ZERO” KTK MAFUNDISHO YA R/MTAKATIFU NA MAAELEKEZO YA MITUME, MTU “ZERO”HUJIKUTA ANAMKEMEA HATA MUNGU!

 5. MILINGA,

  SIJUI ASHUKURIWE MUNGU MAANA TUNAO HUMU WANATUMIA KISWAH NA KINGEREZA,SIKU WAKIINGIA WACHINA,ITABID TUANDIKE..hihuhaa.chinchonchii na Kiswahili ili wote wafikiwe/wabarikiwe/wachangie…heri sasa Kiswange kwakua wote wanapata, wanaojua Kiswahili tu na wanajua Kiingereza tu……Haya sasa niambie Kwanini ukiambiwa kuombea Neno, unamshughurikiwa jamaa,katoka wapi wakati ulikua tu ktk uwepo na sifa na kuabudu kulishamleta Bwana kati yenu na tena navyokuhisi uko kiunjilist zaidi, nadhani ukipewa kuombea sadaka wewe,unafyatuaga pepo zote duniani, why this…wametoka wapi hawa majamaaa, kwani tulipokua tunasifu na kuabudu maana ndipo Bwana hushuka na kukaa ktk sifa, so was this devo among the delegation in the midst of us, wanakaje pamoja, ivi MILINGA seriously una kemeaga nini hapo

 6. Kumbuka shetani hakuogopa kumfuata Yesu ili amshawishi pamoja na kwamba alijua ndiye mwana wa Mungu na tena alikuwa amefunga siku za kutosha.
  Shetani yupo wakati wote, akipata tu nafasi anaitumia.
  Neno lisema wawili watatu wakikusanyika suala huwa si kukusanyika lakini tafsiri halisi ni wawili watatu wakikubaliana jambo kwa ajili yangu mimi nipo katikati yao kulitenda.
  Ikisema kuwa shetani hutushitaki leo haina maana huenda kwa Mungu bali hutushitaki katika nafsi zetu wenyewe ili tukose ujasiri.

 7. Nakubaliana nawe kuwa tuna namna fulani ya kuomba ambayo siyo sahihi. Hasa lifikapo suala la kumkemea shetani, utasikia hata amba walikuwa kimya watasema kwa Jina la Yesu.
  Mimi husema huko ni kuwa na uoga fulani juu ya shetani.
  Lakini suala la shetani kuwepo tulipokusanyika hilo mimi nakubali kuwa huwa yupo. huwa tu hawezi kuwa na tija kwa sababu ya kuzidiwa na utendaji wa uweza wa Mungu kati ya hao walokusanyika. Lakini kukiwa na upungufu wa nguvu anaweza kutenda kazi yake.

 8. Mpendwa,

  Ubarikiwe sana. Maoni yako yamejaa philosophical thinking. Hata hivyo natamani ungetumia lugha rasmi ya Kiswahili maana hapa umetumia sana kiswakinge mno.

  Unaonaje kama ukitumia Kiswahili rasmi au kiingereza tu ili kuwafanya wasomaji wako waelewe vyema ujumbe wako. Hiki kiswakinge cha Dar wengi wetu kinatushinda hasa tulioko mikoa kama Kagera, Kigoma au Rukwa. Au unaonaje wewe?

  Asante.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s