Ndani Ya Kristo Baraka Zote ni Zako!!

baraka

Wapendwa, napenda kushirikiana nanyi andiko hili ili tuweze kutiana moyo tunapouanza mwaka huu mpya.

“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Krist” – Waefeso 1:3 SUV

Mungu atujalie kila mmoja wetu mwaka huu mpya wa 2013, kuwa na imani na ujasiri wa kuendelea kutembea katika baraka zake ambazo tayari ameshatubariki nazo katika Kristo. Kumbuka kuwa wewe unayemwamini Bwana Yesu umeshabarikiwa kwa baraka zote na pia Neno linatuambia ya kuwa ahadi zote za Mungu kwetu sisi ni NDIYO nasi tunasema AMINA na kuzipokea katika Kristo.

Tuuanze mwaka huu tukiliamini Neno la Mungu, tukiziamini ahadi zake kwetu, tukifahamu ya kuwa tumeshabarikiwa tayari. Tegemea kuona udhihirisho wa baraka za Mungu katika maisha yako leo kwa maana katika Kristo Yesu tayari umeshabarikiwa!

Mzidi kubarikiwa na Bwana Yesu!
Patrick
Advertisements

4 thoughts on “Ndani Ya Kristo Baraka Zote ni Zako!!

  1. AMINA ndugu nmebarikiwa na neno lako la kututia nguvu kwamba tuendelee kushikiria imani hata kama muda mwingine tunapitia hali ngumu kiafya na kiuchumi huku tukifahamu kwamba Mungu wetu anaweza.
    Leo Ipo shida kubwa kwa wapendwa wengi pale wanapo ona mtu asiye haki amefanikiwa na yeye bado anapitia hali ngumu. Mtu huyo hufikia hatua ya kufanya mambo hatarishi katika imani yake mfano, kupokea rushwa, kujihusisha na mapenzi n.k imuladi tu na yeye amefanana na jirani yake asiye haki. Biblia inasemaje ktk ile Mithali 1:32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.

  2. Bwana apewe sifa zake mara dufu atupe nguvu ya kirho pia kimwili na mukono wandani ishike upanga ndio NENO lake AMINA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s