Je UMEJIANDAA kukutana na Mungu????

swali

Watu wengi wanapenda kumwona Mungu, lakini wanashindwa kumwona Mungu kwa kutofahamu vizuizi viwafanyao wasimwone Mungu maishani mwao. Je, umewahi kujiuliza “kwanini watu wengi hukata tamaa na kuhisi kama Mungu hayupo, au Mungu amewaacha?” ebu tuangalie kwa Pamoja,

Maandiko matakatifu yanasema “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana yamambo yasiyoonekana,” (Waebrania 11:1).  “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza, kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao,”  (Waebrania 11:6)

Mungu  ametukaribia sana kwa kumtuma mwanae Yesu kuutoa uhai wake kwa ajili Yetu sote na siku zote anazidi kukaribia watu wote. Maana yeye ni Yehova, Mungu wetu,  na hushika mkono  wetu  wa  kuume  na  kutuambia, usiogope, nitakusaidia. lakini wanadamu wanaangamia,wanapotea na wachache sana wanaoingia ufalme wa Mungu.”kama ilivyoandikwa (Mat.7:14:Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyo ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.’’)

Tunaweza kusema kuamini   ni   KUJISALIMISHA    KWA   MUNGU .     Mtu   unapojisalimisha,  huwa   hakuna unachobakiza.   Unajitoa kabisa kwa yule unayejisalimisha  kwake ili akutendee apendavyo. Ni hakika tunahitaji  kujisalimisha  kwa Mungu ili atutendee  kama apendavyo.   Na tunafanya hivyo kwa kujua wazi kile anachotaka kutufanyia kwa kuwa yeyeni mwaminifu, tofauti na ambavyo unaweza  kufanya  kwa  mwanadamu anayebadilika-badilika.     Imani  kwa  Mungu  ni jambo  la hakika  (soma Waebrania11:1).

Lakini Jeshi la mapepo wanakimbia kimbia huko na huku kwasababu wanajua muda wao karibu kwisha, kwasababu muda wa kuwaharibu/kuwapoteza  wanadamu unakaribia kufungwa.  Wamebeba silaha za kuharibu watu na kuwapeleka kuzimu. 

Hivyo imetupasa kupokea imani yote kama tulivyohubiriwa na kufundishwa na KWA KADRI YA ROHO MTAKATIFU maana Neno lasema Yoh12:48.Yuko amhukumuye yeye anikataaye Mimi na kutokuyapokea maneno Yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. Hivyo kuzimu ni halisi na Mbingu ipo. “lakini kuzimu haikuwekwa na Mungu kwaajiliya wanadamu bali kwajili ya shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat. 25:41) lakini,kwasababu ya dhambi na kukosekana kwa toba, wanadamu wataishia huko kuzimu, na ni wengiwataangamia kuliko watakaofika katika utukufu wa MUNGU yamkini wengine ni ndugu wa damu, Yesu kristo alitoa maisha kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie [Kuzimu]bali ni kwa upendo na huruma, ili wanadamu waendee toba na kuingia katika ufalme waMbinguni.” Yesu anaiangalia dunia kwa huzuni na huugua kiasi cha kushindwa kustahimili maumivu, kadri aonavyo watu wanaendelea kuasi. 

Yapo mambo mengi yatakayowazuia wanadamu leo kuingia ufalme wa Mbinguni.lakini nitazungumzia baadhi tu. 

1. Kusamehe na unyenyekevu 

Kusamehe nilazima  kwasababu Yeye alitusamehe makosa yetu yote, na ndiyo maana wengi tupona amani ya Kristo ndani yetu, lakini ukishindwa kusamehena na ukiwa na chuki miongoni mwa watakatifu wa Bwana, tuache malaumu, mafundisho ya mabaya, masengenyo, kwa kuwa ni muda wa kusamehe! Bila kusamehe ujue utakwenda kuzimu, kwakuwa hakuna awezaye  kununua  maisha. Hakuna aliyejilipia gharama mwenyewe isipokuwa YESU KRISTO pale kalvari na ameagiza kwenye maelezo ya the said sala ya Bwana pale kwenye Mathayo kwa kuwa yeye alikuwa wa kwanza kusamehe kalvary. Kuna nafasi kwa hao walioko duniani, ambao hawajafa, walio hai, wanaomuda wa kutubu! 

Unyenyekevu ndio uliomfanya Musa amwone Mungu ktk maisha yake ebu ona hapa Exodus 33:11BWANA akazungumza na Mose uso kwa uso, kama vile mtu azungumzavyo na rafiki yake. Kisha Mose akarudi kambini, lakini msaidizi wake kijana Yoshua mwana wa Nuni hakuondoka mle hemani. Na kuonyesha kwamba kakutana na Mungu alinga’aa sehemu za paji la uso wake na watu walishindwa kuvumilia uwepo wa BWANA kwa kumwangalia kwa Muda mrefu. Deuteronomy 34:10 na ktk Israel hajatokea  mtu aliyepata kuzungumza uso kwa uso na Mungu. Na zipo sifa zile ambazo Mungu amezisema mwenyewe kwamba alifanya hivyo kwa Musa kwa sababu alikuwa mtiifu,mnyenyekevu asiye na kiburi n.k. Alitii neno akafanya kama lilivyo. Lakini siku izi Mungu akikuinua mtumishi kidogo tu unakuwa hushikiki na hata unaanza kuuza hata kipawa cha Mungu kwa pesa. Ati kwamba una pesa ngapi uombewe? 

2. Bize na dunia.

Watu wengi maarufu(waigizaji wanamuziki, wachungaji, maaskofu, mapadri, mapapa, maraisi nk)wataenda kuzimu kwa sababu wanatumia mda mwingi sana kuwa duniani kwa kumsaidia ibilisi. Tunakuta wanamuziki maarufu sana duniani wakifanya miziki isiyo na tija kwa wanadamu na kuwafanya watu dunia nzima kufuata mambo yayoimbwa humo.neno linasema Zaburi 11:6 Juu ya waovu atawanyeshea makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao.. Ujira wa asiye tubu. Maana kazi wanazozifanya hazina ujira kwa Mungu wetu. Hivyo kama ilivyo andikwa 1yohana2:15Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu ye yote akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Wapo watu wengi maarufu na wanaijua kweli na tena wengi ni Maaskofu wachungaji kwa makusudi wanaipotosha kweli ili waendelee kuwa na washirika wasio watakatifu na wala hawakusema kweli kama ilivyo japo kweli waliijua ila wanapenda fedha zaidi ya kuhubirihabari za kweli ya wokovu. Hawatoi uhalisi wa injili bali wamepindisha wanavyotaka wao si kama Mungu atakavyo.

Tukumbuke kwamba haipo nafasi ya kurudi duniani,  ili ututubu ukifa ni basi.

Wapo watu wengi wanaongoza makanisa makubwa sana kwa umati mkubwa na huku wakiabudu sanamu. Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa bali ni YESU pekee awezaye kuokoa, na nje yake hakuna mwingine aokoaye. anawapenda wenye dhambi, lakini anachukia dhambi.

Anthony 

Advertisements

7 thoughts on “Je UMEJIANDAA kukutana na Mungu????

 1. “Tunzeni nafasi zenu ambazo Mungu amewapatia… wingi wenu huu katika usiku wa leo hauna maana kama hatutakuwa na uhusiano mwema na Mungu kwani hata shetani ana watu wake na huwa anawapatia mahitaji yote… kila mmoja wenu aanze upya na Mungu”, alisema.

 2. s mtoa soma ila kwa maswali yaliyo ulizwa hapo ju kidogo naomba niekeze kuwa buzy na dunia maana yake nn maana yake tulid ktk kifungu hicho kinacho1yohana 2;15-17 dunian kuna maas ukiyapenda maas yaliyo dunia kumpenda mungu hakumo ndan yako.mambo meng yaliyo chin ya dunia n ubatr.m2 ambaye pendo la kristo lko ndan yake huwa akimbilii mabmbo ya dunia anakuwa mwangalifu ktk kristo ili asje akamkosa mungu. njia ya mbingun imesonga kwa sababu weng wanaipenda dunia na starehe zake kulko kumpenda Mungu.unaweza ukazsema kuwa npo dunin swez kuish kitakatifu me nasema inawezekana kupitia kristo yesu. kumbuka skila m2 amwitaye bwana bwana ataingia mbingun hapana usje ukajifarj kwa sababu me naimba sana naomba sana na hubiri sana nimefanya miujiza ming ndo ikwa n tket ya kuingia mbingun hapana.

 3. Shalom,

  Samahani kwa watoa maoni, ndugu milinga na wengine. nimechelewa kujibu kwa sababu sikujua kama ni mada maana, ipo kwenye title ya injili ebu angalia vizuri na wala haiko kwenye maswali na majibu.

  lakini Kuhusu maswali ya Millinga ni kwamba dunia = dunia kama ilivyoandikwa kwenye biblia na tafsiri yake inabaki hivyo. na kuhusu watumishi wapo pia wanafanya kazi nzuri hata Mungu anaijua ila wapotoshaji wapo na pia wapotoshaji wa makusudi wapo pia. Mengine ni alert ndugu msomaji kama yamekuumiza sorry maana hata mimi yalinigusa kwa sehemu. MAANA NENO NI KAMA UPANGA UKATAO KUWILI.

  BARIKIWA SANA
  ANTHONY

 4. Mi nionaovyo mtoa Mada yupo sahihi kabisa tunaweza kuwa tunakazi jtt had I ijumaa kama hujishughulish NA mambo ya mungu ni bure tu, hata alivyotaja ma pastor, ndio ma pastor wengi siku hizi wanahubiri panda mbegu, sio udunia huo ndivyo yesu anavyotaka tufundishane pandambegu utavuna mume, gari, nk.

  Tusishambulie kila Mada kama umeona haikufai usiwaamlie wengine.tuelimishane, turekebishane twende mbinguni.

  Shalom.

 5. Hii mada inataka nini hasa jamani?

  Ndugu mtoa mada unaweza kuniambia kwa kutumia mifano jinsi tunavyokuwa buzy na mambo ya dunia?Au je ninapokuwa muda mwingi niko kazini J3 hadi J’mosi ndio huko kuwa buzy na dunia?

  Pia unaposema wanamuziki wataenda kuzimu kwa vile wanatumia muda mwingi kuwa duniani ni wanamuziki wapi hao,waliookoka au wasiookoka?

  Na kama ni wasiookoka, mada hii kuwekwa hapa imelenga kuwasaidia watu gani hasa, waliokoka( kanisa) au wasiookoka?

  Maana wanamuziki wasiookoka tungetegemeaje wasiwe busy na mambo yasiyokuwa ya Mungu? Vinginevyo huo ungekuwa ni muujiza.

 6. Mtumishi,

  Naomba kuelewa maana ya kuipenda dunia? Unaposema kuwa bize na dunia una maana gani? Unapowataja watumishi wa Mungu (kama ulivyowaorodhesha) kwamba wanatumia muda mwingi duniani kwa kumsaidia Ibilisi, una maana gani?

  Maswali hayo kama hujayajibu au kuyafafanua mada yako haitakuwa na mwelekeo wala msaada kwa wasomaji.

  Asante.

 7. ameen, kuzimu ilikuwa si ya mwanadamu ni shetani pamoja na malaika zake zake,ila kwa mwendo huu wa sisi wanadamu wengi wataingia kwa kuipenda dunia,tumekuwa bize na vitu na vya duniani hatushughuliki na mambo ya Mungu,kweli baba yetu aliye juu atashughulika na ya kwetu?hata km tunashughulika na mambo yake ni kwa muda mchache sana,tumejaza vinyago ndani ya mioyo yetu,oh ! Mungu tusamehe kwa hilo,mji ule hautaingia kinyonge sisi ni miji hivyo mioyo yetu yuijaze kicho cha Bwana,yer 31:31,…. anasema ataweka kicho chake nani ya kila mmoja wetu mkubwa kwa mdogo,hakuna kufundishana,Roho Mtakatifu atakufundisha kuacha dhambi.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s