Ajinyonga na kufa akidai anakwenda kwa Yesu!

dunia

MWANAUME mmoja mkazi wa mitaa ya Vumilia mjini Kahama, Bw.Mayala Mwagala 58 amejinyonga hadi kufa chumbani kwake kwa madai kuwa anakwenda kwa Yesu.

Marehemu huyo anadaiwa kujinyonga kwa kutumia kama ya katani juzi usiku baada ya kukutwa akiwa mening’inia kwenye kenchi chumbani kwake alikokuwa amepanga.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo lilisema kuwa Dada wa marehemu, Bi. Josephina Mwagala alisema kaka yake alikuwa naye siku moja kabla ya kujinyonga kazini kwake kwenye grosale ya Sadala katika mazungumzo ya kidugu na aliachana saa nne usiku.

Bi. Mwagala alisema wakati akiwa nae marehemu kaka yake alikuwa akimtamkia kuwa saa sita usiku itakuwa mwisho wa maisha yake duniani atakwenda kwa Yesu. Alisema wakati anaongea maneno hayo hakuwa anamjali na wala hakuweza kumuuliza kwa nini anasema hivyo kuwa usiku huo itakuwa mwisho wa maisha yake na anakwenda kwa Yesu.

Bi.Mwagala alisema kuwa kaka yake huyo hakumueleza kama kuna tatizo lolote linalomkabili na familia yake. Alisema baada ya kuachana naye yeye alikwenda kwake na mke wake alikuwa amemwacha shamba katika kijiji cha Burungwa wilayani hapa na kwamba anashanga muda wa saa tano mchana alifuatwa na wapangaji wenzake na kumueleza kuwa kaka yake amekufa kwa kujinyonga.


Patrick Mabula, Majira, Kahama.

Source: wavuti

 

Advertisements

4 thoughts on “Ajinyonga na kufa akidai anakwenda kwa Yesu!

  1. Oh jamani, ndio maana Yesu alisema Math 24.4 Angalieni mtu asiwadanganye. Na ili asitudanganye tunahitaji kufahamu Biblia inavyosema, na ndio maana pia akasema, Nanyi mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. Biblia ni Neno la Mungu, na ina jumla ya mistari 31,173. Lakini mistari ile tu mtu anayoijua ndiyo itamweka huru, kwa hiyo huyu jamaa aliyejiua, kwanza ALIDANGANYWA, pili HAKUIFAHAMU KWELI. Maana pia imeandikwa WAUAJI HAWATAURITHI UZIMA WA MILELE. Hata angejua kuwa angejaribu kujiua, akakamatwa angeshtakiwa, na angeweza kufungwa. Ushauri wangu ni huu. 1.wachungaji wafundishe washirika wao Neno kwa usahihi. 2. Wakristo wawe tayari kufundishwa, wasiwe wavivu. Mbarikiwe.

  2. Naona mwenyematatizo ni mchungaji wake,sidhani kama alikuwa amefundisha kuhusu safari ya kwenda kwa yesu mmojammoja kabla ya unyakuo,Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

  3. hakuwa na ujuzi sahihi juu ya biblia na kifo na tatizo wachungaji na wainjilisti sote tumekaaa ofisini tunasubili sadaka badala ya kwenda kuwafundisha watu kama hawa neno la MUNGU mtu kama huyu angejua biblia vizuri asinge jinyonga nina uhakika huyu kwa sasa yuko jehanam anaungua ila wachungaji msibani utasikia awekwe pema peponi.kweli wachungaji na wote wenye uwezo wa kuhubiri tutahukumiwa kwa kutotangaza ukweli tunaoujua

  4. Hakuna mbingu ya watu kama hao. Kwa tendo hilo amekwenda JEHANUM moja kwa moja maana hukumu haingoji ( WAEBRANIA 9:27 ). Jehanamu ni sehemu ya mangojeo ya wenye dhambi. Kuna mateso makali lakini hayalinganishwi na ukali wa moto wa Ziwa la Moto ambako watakaa milele watenda dhambi mara baada ya hukumu ile iliyo kuu.

    Pia kuna tofauti kati ya mbingu ya sasa na mji wa Yerusalemu anaouandaa Yesu Kristo ( YOHANA 14:1-6 ). Watu wote waliokufa katika Bwana wako katika mbingu ya tatu ( mbingu ya sasa ). Mbingu ya kwanza ni hii tunayoiona juu na ya pili ni huko kuliko na sayari mbalimbali lakini ya tatu ni kule kusikoonekana. Watakatifu wataishi na Bwana milele katika mji anaouandaa. Ikumbukwe kuwa kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya ( UFUNUO 21:)

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s