Ubatizo kwa watoto wadogo

ubatizo

Unadhani ni sawa kumbatiza mtoto mdogo? kwa nini? maandiko yapi?

–Emmanuel mchamungu

Advertisements

42 thoughts on “Ubatizo kwa watoto wadogo

 1. Ki ukweli swala la unatizo ni fumbo coz kama wakati YESU KRISTO alipozaliwa Yohana mbatizaji alikuwepo na kwa hakika huduma yake ya ubatizo ilikuwepo. Swali langu ni hili. Kwa nini baba yake na mama yake hawakumpeleka YESU KRISTO akabatizwe?. Ki ukweli nadhani ubatizo ulikuwa wa watu wazima na kibinaadamu nadhani hata Yusufu na Maria walibatizwa kwa ubatizo wa maji mengi ndo maana hawakumpeleka mtoto wao YESU KRISTO WA NAZARETI akabatizwe.

 2. BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA.HONGERA NA KAZI YA BWANA.KAZI YENU NI NZURI SANA.NIMEBARIKIWA NA KAZI YENU

 3. MTU MMOJA ALIOKOKA NA HAKUWA RADHI KUBATIZWA MAJI MENGI KWA HOJA YA KUSEMA ALIBATIWA MAJI MACHACHE. SIKU MOJA AMELALA AKATOKEWA NA YESU USIKU NA KUMWAMBIA, “LEO NATAKA ROHO YAKO ILA HUWEZI KWENDA MBINGUNI UTAENDA JEHANAMU” AKAMUULIZA KWA NINI NAMI NIMEOKOKA NA NIMEKUAMINI YESU? YESU AKAJIBU, “NI KWASABABU HAUKUTIMIZA HAKI YOTE YA KUBATIZWA MAJI MENGI” AKASEMA NISAMEHE NAOMBA USINICHUKUE NAENDA KUMWAMBIA MCH, ANIBATIZE. ALIPOAMKA ASUBUHI AKAENDA KWA MCH KUMWELEZA YOTE NA KUOMBA MSAMAHA NA KUBATIZWA. KULIFANYA NENO LA MUNGU KAMA LA KWAKO NA UNALITOLEA MAAMUZI WEWE NI KUPOTOKA AKILI. KUBALI KUBATIZWA MAJI MENGI BAADA YA KUAMINI UBATIZO WA KICHWANI NI NI BATILI.

 4. SHALOM.
  Ubatizo wa watoto wadogo ni Fundisho la kipagani liloanzishwa na dhehebu la Katoliki Baada ya kuanza kuwaua WAKRISTO WALIOAMINI INJILI YA MITUME.
  MARKO 10:13-16-YESU ALIWABARIKI WATOTO SI KUWABATIZA.
  Pia, kama BWANA YESU, mwanzilishi WA IMANI YA KIKRISTO ALIBATIZWA AKIWA MTU MZIMA WEWE NDIO AKUKUBALI KWA UBATIZO WA WATOTO
  Mbona unaongelea mambo mengi kutoroka Wajibu?MFANO, HABARI YA NYUMBA YA KORNELIO,MWIZI MSALABANI.HUJUI HATA UKITAFUTA LA KUTENDEA UOVU UTALIPATA?
  YESU ALISEMA NI MTU ANAYEAMINI (MARKO 16: 15-16) SI ANAYEAMINISHWA NA MDHAMINI AU NA DHEHEBU FULANI.
  UBATIZO ULIOPO KWENYE BIBLIA NI WA WATU WAZIMA TENA “KWA JINA LA YESU KRISTO”
  SI KWA VYEO,BABA, MWANA, ROHO MTAKATIFU BALI NI KWA “JINA”
  Hakuna mtu aitwaye Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu Duniani.Hilo lilikuwa fumbo (MATHAYO 13:34-35) Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni Bwana Yesu Kristo.Soma-MATENDO 2;36, 4;10-12,YOHANA MT,17;6,11-12WAFILIPI 2;10-11.Mitume ndio walioachiwa Maagizo na wengine wote wanaotaka kwenda Mbinguni hujenga kwenye Msingi huo,soma-1KOR 3;10-15, LUKA 10;16,WAEFESO 2;20.Mitume Waliokuwa na Ufunuo Walibatiza KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO.Soma BIblia Yako vizuri-MATENDO 2;38, 8;12,16, 10;47-48, 19;4-5,WAKOLOSAI 3;17.Sasa kama HUJABTIZWA Kwa Jina La BWANA YESU KRISTO, UMELAANIWA ( SOMA KWA MAKINI-WAGALATIA 1:8-9).
  Ni ukweli usiopingika wanaowapinga Mitume wa Bwana Yesu ni wapinga Kristo.Kuwa Mpinga Kristo ni kuwa Mpinga Neno,na kuwa mpinga Neno ni kuwa mpinga YESU (Luka Mtakatifu 10:16)
  KAMA UNA ROHO MTAKATIFU HUTAPINGA NENO LA MUNGU KAMWE.
  KAMA MTU YEYOTE ANAYEDAI KUWA NI MKRISTO NA HAJABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO (MATENDO 2:38-39, 8:14-16, 10:48, 19:1-5) BADO NI MPAGANI.
  ****NA WATU WOTE WASEME AMINA****

 5. Towashi katika Matendo 8: 27-38 alikuwa mwanafunzi wa Filipo kwa muda, baada ya kujifunza akahitaji kubatizwa. Kabla ya kubatizwa akataka kujua kama kuna jambo linaweza kumzuia asibatizwe, mwalimu Filipo akamwambia “UKIAMINI INAWEZEKANA”

 6. Ezekil Umaso, Umeona marko 16:15 tu au hata mstari wa 16 upo kwenye biblia yako? Hubiri kwa kila kiumbe ila aaminiye ndiye atabatizwa. Pia kumfanya mtu kuwa mwanafunzi ni kumfundisha sio kumbatiza, ila mwanafunzi huyu akiamini anabatizwa. Tena kuna mmoja hajafahamu tofauti ya ubatizo wa Roho na ule wa maji. Lakini huyo Yesu unayedhani kuwa hatambui huo ubatizo si kwamba alibatizwa tu bali alisimamia ubatizovwa maji tele huko Ainoni. Ushauri wangu TUSILAZIMISHE BIBLIA KUPIGIA MISTARI MAWAZO YETU ILI YAKUBARIKE BALI TUSOME TULIYOPEWA NA KUYAFUATA HAYO. NA KILA ANAYETOA FUNDISHO ASIKWEPE UKWELI HATA KAMA UKO KINYUME NA MAWAZO YAKE. ILA KAMAVUNATOA MAWAZO YAKO BASI SEMA WAZI.

 7. Mhina,

  Maelezo ya kiongozi wako wa dini kwa sehemu kubwa, ama yote katika ukamilifu wake ni “sahihi” kulingana na dini hiyo anayoiongoza!

  Bali kama utayaleta katika kipimo cha Maandiko, yaani Neno la Mungu, NI BATILI na hivyo hayastahili kwa chochote kile zaidi ya jalala la moto ili yasiharibu watu wanyofu kama wewe!

  Mungu anapenda watu jasiri, wenye maamuzi, na si wenye kuyumbishwa; Yos 1:7 “Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.”

  Sasa iwapo ndg yangu Mhina, nawe umesimama ktk nafasi ya Joshua wa leo, ukiwa na lile Neno alilokuamuru Kristo, ambalo wewe mwenyewe umelikiri: “Kibiblia ubatizo unaotambulika wazi ni ule wa watu wazima kuzamishwa mwili mzima”; inakuaje tena unayumbishwa na tungo za dini zisizoweza kukufanikisha ktk lolote?

  Sikufahamu ktk mwili zaidi ya kukutana kwetu hapa, lakini bado ninaamini kwamba unawajua watoto wadogo. Labda nikuulize, unaonaje iwapo Mungu atakurejesha katika utoto na kukuacha katika hali hiyo kwa miaka yako yote utakayoishi hapa duniani ili ufahamu wako kiroho uongezeke na uwe imara zaidi katika Imani kulingana na mafundisho ya huyo kiongozi wako?

  Yaani katika huo utoto utakaorudishwa licha ya kwamba hauwezi kuelewa kinachofanyika kimwili lakini kiroho, utaelewa kabisa kwa sababu, Mungu amekuwekea misingi ya nguvu kinywani mwako, yaani ’MWANGA WA IMANI YA YESU KRISTO’! Mimi nadhani mafundisho ya huyo kiongozi wako yamekurudisha katika utoto, na hiyo ” misingi ya nguvu kinywani mwako, huo ’MWANGA WA IMANI YA YESU KRISTO’” ni sehemu ya ufahamu wako wa kiroho ambao sisi watu wazima hatuuelewi!!

  Wale watu waliokwenda kubatizwa, walikuwa ni watu wenye ufahamu kamili kwahiyo suala la kuvipeleka vichanga vyao vikabatizwe halipo, hata hawa wanao wadanganya kwamba wanawabatiza hao watoto ni waongo tu kama huyo kiongozi wako; kubatiza ni lazima uzamishwe ndani ya maji usionekane hapa juu, ndipo wanapaswa wawazamishe hao watoto!!!!

  Halafu unasema alikuambia ukasome Mdo 2:38-39 ili uione ahadi ya watoto kubatizwa; nawe unatusisitiza kwamba hilo ni kweli!!!! Labda nikuulize, kwanini usirudi rohoni kule ulikowekewa misingi ya nguvu kinywani mwako, mwanga wa imani ya Yesu Kristo; ukalipambanue jambo hili huko rohoni, likuongoze uyajue na haya Maandiko aliyokubambikia tafsiri potofu kiongozi wako baada ya kukurudisha utotoni huko ambako amekudanganya kwamba umewekewa nguvu kinywani mwako, hicho kinywa kisichoweza kunena, nawe ukaamini!!!??

  Vifungu alivyokunukulisha hivi hapa:
  “38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

  Kwa taarifa yako, Hakuna mtoto mchanga anayerithi chochote kile zaidi ya kuhesabiwa kuwa ni mrithi, nako kuhesabiwa kuwa hao watoto ni warithi wa Ufalme wa Mungu, ndiko huko kuwekewa mikono alikokufanya Kristo! Urithi wanauchukua hapo wanapofikia kuwa watu wazima wenye kuwajibika kama hao unaowaona hapo katika hivyo vifungu alivyokunukulisha kiongozi wako bila ufahamu! Hao walipoelezwa makosa yao yanayowaondoa katika hesabu ya warithi, wakiiona ile kweli ya jambo hilo, ndipo wanauliza wafanyeje ili wapate kuurithi Uzima wa milele?

  Jibu unalolisoma katika hicho kifungu cha 38, ndilo unalopaswa nawe kujipima iwapo utakuwemo katika orodha ya warithi pamoja na hao? Tena umuulize na kiongozi wako iwapo anajua chochote kuhusu jambo hilo la KUONDOLEWA dhambi zake kwa kubatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo au anajiimbia tu ngonjera za wokovu zisizo na “wokovu’? HAKUNA wokovu pasi kuondolewa dhambi!!!!!

  Kujifunza ni kuzuri lakini ni lazima kuambatane na moyo mnyofu!

 8. Martine Kayinga
  umesema anayestahili kubatizwa ni yule mwenye uwezo wa kupambaua mambo tu. naomba kukuuliza, Je! mtu mwenye mtindio wa ubongo/mgonjwa wa akili hastahili kubatizwa?

 9. Nafurahi sana kwamba watu wamepanua na nimekaa kimya sana. Maswali kadhaa hayajapata majibu ya kibiblia. Majibu yaliyotolewa ni mitazamo ya watu tu au madhehebu na mwisho wa siku tunaishia pale niliposema kwamba ni suala la kimadhehebu zaidi hivyo liachwe tu maana hakuna mwisho hapa:
  (i) Nani kathibitisha hapa kuwa ubatizo wa Mt 28 na Mk 16 ni ubatizo wa maji?
  (ii) Watoto wachanga wanaweza kuamini, au hawawezi? Kuamini ni kupi?
  (iii) Kuzaliwa kwa maji ina maana ya kubatizwa? Je hii ni kuzamishwa, au kuibuka majini?
  (iv) Neno ‘batiza’ lina maana ya kuzamisha pekee? Sio kuosha pia au kutia rangi kama asili ya neno lilivyo?
  (v) Nini faida ya kubatizwa basi? Mbona tunaona waliobatizwa kwa kuzamishwa na wengine kwa kunyunyiziwa maji wakiwa watenda dhambi wakubwa na hatia haziondoki?
  (vi) Kuna uhusiano gani wa kubatizwa, kwenda mbinguni, kuuona ufalme wa Mungu, kuuona ufalme wa mbinguni au kuokoka?
  (vii) Ukifa ukiwa hujabatizwa lakini umempokea Yesu na kumkiri na kumwamini utapata madhara au hasara gani?
  (viii) Waacheni watoto wadogo waje kwangu, Yesu alimaanisha waende kubatizwa, au waende kumwamini au wapelekwe tu?
  (ix) Ubatizo wa Yohana upo, au haupo siku hizi? Maana alisema kuwa yeye alikuwa anabatiza kwa maji
  (x) Hivi Yohana Mbatizaji, yeye alibatizwa au alijibatiza mwenyewe kwanza kabla ya kubatiza wengine au Yesu alimbatiza au ilikuwaje? Na kama hakubatizwa anasimama wapi kwenye thamani ya ubatizo kwa mwanadamu kama yeye?
  Mbarikiwe sana mnapoendelea kutoa ufafanuzi.
  Emmanuel Lyatuu

 10. Ndg Asaeli John andiko hilo ktk Yohana 3:5 neno maji halina maana hiyo uliyoisema hapo juu si maji kimiminika bali neno maji linamaanisha Neno.(Neno la Mungu). Ubarikiwe

 11. SHALOOOM!!!!!!!!!!!! ubatizo wa maji ni lazima, hii inathibitishwa na maneno ya yesu mwenyewe katika yohana 3:5, lakin katika ubatizo wa watoto mi naona ni sahihi tu kwa kuwa kitu chochote kati ya ubatizo na kuokoka kinaweza kukitangulia kingine! unaweza kumopkea yesu kwanza halafu ukabatizwa,kwa sababu Biblia imesema kuwa “Aaminiye na kubatizwa ataokoka” , pia unaweza kubatizwa kabla ya kuokoka na baadaye ukaokoka,(“Yesu akamjibu, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.” [Yohana 3:5] -ameanza kwa maji, yaani kubatizwa na kisha kwa Roho(kuokoka)) kwa hiyo mtoto anaweza kubatizwa na kuja kuokoka akikua

 12. Mhina hongera kwa kufuatilia maandiko ya ubatizo. Unadai umekubaliana na ndgu Mkandya kwamba ubatizo wa watoto ni sawa, lakini kama ungeendelea kusoma mstari wa 40 na 41 ungeshangaa kuona kwamba kumbe wapaswao kubatizwa ni wale tu wenye kuupokea ujumbe kwa furaha ndiyo wanaopaswa kubatizwa. Mbona hapo hasemi walibatizwa walioupokea na watoto wao? Kimantiki ni mtu yule mwenye kuweza kupambambanua mema na mabaya ndiye anapaswa kubatizwa. Martin.

 13. Bwana Yesu asifiwe wapendwa…….Ubatizo ni ishara ya nje inayoonyesha mabadiliko ya ndani.Hii maana yake ni kwamba, zile tabia zetu mbaya na ule utu wetu wa kale unakufa,kwa hiyo, watu wanategemea kuona utu mpya ndani ya huyo aliebatizwa.Pia tunaweza kusema “UBATIZO NI KUZALIWA UPYA NA KUFANYWA MWANAFUNZI WA BWANA YESU”,Soma(mathayo 28:19-20). kibiblia ubatizo unaotambulika wazi ni ule wa watu wazima kuzamishwa mwili mzima, nafikiri wanawake na watoto wadogo hawajaonekana kutokana na utaratibu wa torati wa kuwahesabu wanaume pekee kuwa ndiyo waliokuwa wawakilishi wakubwa.Kwa mitazamo ya watu wengi huamini kwamba ubatizo wa mtu mzima ndiyo sahihi kwa kuwa mtoto hana uwezo wa kuamini wala kubadili chochote katika maisha yake kwa kuwa wao huwa kwa asili hawana dhambi.Hili ni kweli tena ni sahihi lakini nilipomuuliza kiongozi mmoja wa dini, aliniambia kuwa tusijaribu kumuwekea Mungu mipaka katika kazi yake mbele za watoto.Nilipomuuliza kivipi? alinipa maelezo yafuatayo: Alisema kuwa biblia inatufundisha kwamba mwenyezi Mungu ni mwalimu wa kwanza wa kila mwanadamu.Akasema “nikweli kabisa kwamba watoto wadogo hawawezi kuelewa kinachofanyika kimwili lakini kiroho, wanaelewa kabisa kwa sababu, Mungu ameweka misingi ya nguvu vinywani mwao, yaani’MWANGA WA IMANI YA YESU KRISTO’,Soma(zaburi 8:2).Akaendelea kuniambia, ‘Bwana yesu alisema hivi: BASI,YEYOTE AJINYENYEKESHAYE MWENYEWE KAMA MTOTO HUYU, HUYO NDIYE ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI,Soma(mathayo 18:4), Kumbe kimwili tunavyofahamu ni sawa lakini kiroho, watoto wadogo ndiyo wakubwa wenye ufahamu na unyenyekevu mkubwa wa kiroho mbele za Mungu kuliko hata watu wazima!!.Kwa hiyo akasema, watoto ndiyo wanafunzi wa kwanza wa bwana yesu kiroho hata kabla ya watu wazima, halafu mafundisho yale ya awali rohoni mwao, ndiyo yanakujawahekimisha mpaka kufikia imani ya wokovu “IMANI MPAKA IMANI”.Kuhusu jambo hili biblia inasema”NA YA KUWA, TANGU UTOTO UMEYAJUA MAANDIKO MATAKATIFU, AMBAYO YAWEZA KUKUHEKIMISHA HATA UPATE WOKOVU KWA IMANI ILIYO KATIKA KRISTO YESU.Soma(2Timotheo3:15).Kwa hiyo akasema, hapo utaona kuwa mtoto mdogo tayari anayo imani ya asili ya yesu kristo na kwa hali hiyo katika utu wa nje anaweza kupokea ubatizo kwa njia ya imani, ili baadaye kupitia hekima ya mafundisho ya neno la Mungu…anakuja kuokoka(kusamehewa dhambi) anapokuwa mtu mzima.”AAMINIYE NA KUBATIZWA= ATAOKOKA.Hivyo watoto wanayo tayari imani ya asili> hivyo wanabatizwa ili waje kuokoka.Akasema: mtume petro aliweka wazi swala hili la ubatizo kuwa Mungu aliahidi liwe si kwa watu wazima pekee bali pia kwa watoto na watu wote waliombali watakaoitwa na bwana Mungu wetu wamjie!!.Nilipomuuliza liko mahali gani hilo andiko katika biblia?…akaniambia kasome (matendo 2:38-39).NIKAKUTA NIKWELI!!.Akamalizia kwa kuniambia “nikweli kuwa bwana yesu alibatizwa ili kutimiza haki yote, lakini sio kwamba alitimiza kwa ajili yake pekee bali ni kwa ajili ya watu wote waliodhaifu ili wamuendee kwa imani na kuwapa haki yake.Akasema “hatufuati vielelezo vya bwana yesu kwa ajili ya haki ya kwenda mbinguni bali tunafuata kwa ajili ya utiifu wetu mbele za bwana kama msingi wa imani yetu…kwa hiyo ni makosa sisi kujiona bora kuliko wengine wakati wote tumeokolewa kwa imani na si matendo yetu mazuri ya makanisani…”MMEOKOLEWA KWA IMANI, MTU AWAYE YOYOTE ASIJISIFU KWA MATENDO MAANA NI KIPAWA CHA MUNGU KILETACHO WOKOVU’.Mzee huyu akahitimisha kwa kusema”hata sisi watu wazima hatuelewi vyema maana ya ubatizo kwa hakika kwa kuwa yote haya ni mafumbo ya Mungu yaliyozidi maarifa ya akili zetu za kibinaadamu, hivyo, tumuachie Mungu atufanyie kazi anayoijua yeye mwenyewe.Akasema kuwa tunajifunza pale bwana yesu wakati anatimiza haki yote kwa ajili yetu, alimuweka Petro kwenye kundi la watu wasiojua chochote lakini akubali kwanza halafu baadaye ataelewa na kuamini,”NIFANYALO WEWE HUJUI SASA LAKINI UTAFAHAMU BAADAYE”,Soma(yohana 13:6-7).Baada ya hapo, mimi mhina niliona mawazo ya mwalimu yule yanamantiki ya kiimani na kimaandiko kwa kiasi kikubwa sana….sasa naomba mwalimu au mkristo yeyote anisaidie kukosoa hoja hizi za huyu mwalimu ili na mimi nijifunze zaidi.Asanteni

 14. Imanuel Lyatuu,lete maandiko usiongee hewani.ktk efeso 4;4-6 imeongelea mambo ambayo yatupasa tuyafanye kwa umoja, mfano Roho mmoja,mwili mmoja,tumaini moja,Bwana mmoja,imani moja,ubatizo mmoja,Mungu mmoja nk.Ninaogopa sana jinsi watu wanavyogawanyika kiimani na bado wanasema kilamtu na imani yake,wakati NENO linasema imani moja.Ktk kubatizwa tunasoma ni ubatzo mmoja je kama ubatizo tunatofautiana je Mungu atatuhesabu vipi ?

 15. Ndg Mkandya, nadhani katika Biblia yuko Kornelio, huyo ndiye aliyepokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu kabla ya Ubatizo wa maji, Mdo 10:44-48
  “Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo.”

  Sababu za jambo hilo kuwa hivyo linaeleweka, na pia kama wapo wengine, basi mazingira ya wao kupewa yatakuwa wazi kulingana na mapenzi ya Mungu, lakini laid down standard ndio hiyo, unabatizwa maji mengi halafu unaketishwa kufundishwa na kisha unajazwa Roho Mtakatifu.

  Pia unaniuliza, “Lakini pia Lwembe suala la kubatizwa kwa jina la Yesu pekee lilitoka wapi wakati Yesu alisema mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho mt?(Mathayo 28:19)”

  Kwanza niseme hivi, hili jambo la “kubatizwa kwa jina la Yesu pekee” si la kiBiblia hakuna mahali popote lilipoagizwa, kwa hiyo hilo ni fundisho la kidhehebu linalokuingiza katika dhehebu hilo, na si katika ukristo halisi. Ubatizo ulio wa kiBiblia ni huo unaoonekana katika kitabu chote cha Matendo ya Mitume, kuanzia hapo 2:38.

  Ni kweli kuwa Yesu aliagiza wabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu kama ilivyo katika Mt 28:19. Je, tuseme kuwa mitume walikengeuka? La hasha, wamebatiza sawa sawa na hiyo Mt 28:19, waliochemka ni wanatheolojia, walishindwa kukamata maana rahisi ya kifungu hicho cha maneno, wao wakazigeuza hizo titles kuwa majina! Vinginevyo basi sentensi ingesema mkawabatize kwa “majina” na si “jina” au tuseme basi, “Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” ndilo jina lenyewe, yaani iwe hivi, “mkawabatize kwa jina la “BabanalaMwananalaRohoMtakatifu”!!! Haileti maana, tunapaswa kufunuliwa jina hilo ni lipi, nao ufunuo wa jina hilo ndio huo hapo peupe katika kitabu cha Matendo! Na hata ukirudi katika Biblia huwezi kumkuta yeyote yule aliyewahi kubatizwa kwa jina la Baba na Mwana na RM, HAKUNA!! Basi kama ndani ya kiongozi hakuna mfano wa jambo hilo, sisi tunaliiga kutoka wapi?

 16. Lenda hoja yako inaweza ikawa ya msingi, lakini lazima tutumie misingi ya haki kuihalalisha hoja. Unawezaje kuthibitishaje kjuwa mtoto mdogo hawezi kuamini? kwani hawezi kusikia ambako ndiko kunaleta imani? Tukumbuke sana kuwa Yesu hakusema watoto wadogo wana tiketi ya bure ya kwenda mbinguni. Huo nao ni uongo kama wa wasemao Mungu amesema jisaidie nami nitakusaidia.

  Ila pia kwa ndugu Lwembe, si lazima mtua aanze kwanza kupokea ubatizo wa maji ndipo ufuatie wa Roho mt. Uhalisia unatuonesha kuwa kuna watu wengi tu walipompokea Kristo walijazwa Roho mt. hata kabla ya kubatizwa kwa maji.

  Lakini pia Lwembe suala la kubatizwa kwa jina la Yesu pekee lilitoka wapi wakati Yesu alisema mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho mt?(Mathayo 28:19)

 17. Rev. Lee Cosmas Ndeliy,

  Umenishangaza kwa kauli yako kuwa, “kwanza katika kusoma Biblia kwangu hakuna mahali ambapo nimekuta wazi wazi ya kwamba hairuhusiwi kuwabatiza watoto. Hii ina maana kwangu ya kwamba wanaastahili kupokea ubatizo kama NEEMA ambayo ni zawadi.”

  Ubatizo unahusisha suala la kuzamishwa majini, hivi Rev, unategemea mtu mwenye akili timamu anaweza kumpeleka kichanga wake akazamishwe? Yaani ulitegemea Mungu aanze kuwaonya watu kuhusu jambo hilo? Usitegemee kuliona jambo ambalo halipo! Kama kila mtu ataanza kuzisikiliza sentiments zake, unadhani rev. utabaki na kusanyiko? Haya mambo ya kujitungia Mungu hawajibiki nayo, yeye amesema waleteni watoto kwake, akawawekea mikono, nawe fanya hivyo maana hatuna tunalolijua la Mungu, isipokuwa hilo tulilooneshwa!

 18. Unadhani ni sawa kumbatiza mtoto mdogo? kwa nini? maandiko yapi?
  Nimepitia kwa makini sana maelezo na hata malumbano kuhusu swali hili. Napenda tu niongezee kwa unyenyekevu na ule ufahamu wangu mdogo katika maswala ya kiroho na hasa yale yagusayo wokovu wetu.
  UBATIZO: Neno lenyewe “ubatizo” linatokana na neno la Kiyunani “baptisma” neno hili lina maana pana sana. Ukilichunguza sana maana yake ni kuzama, kuzamisha, kuchovya lakini pia kusafisha hata kuosha. Wayunani waliweza kulitumia neno hili hata wakati wakitia rangi nguo zao ili kupata rangi moja na hata kama mtumbi ulizama walisema umebatizwa. Hivyo basi kwa maana hii ubatizo una maana ya kuzamisha, kuosha, kuingia ndani ya, kuunganishwa na, kuwa na umoja na, kupata kuwa sehemu ya.
  Kweli kuna maswali mengi kutoka kwa waamini wa makanisa na madhehebu mbalimbali kuhusu swala la ubatizo wa watoto (wachanga/wadogo). Kuna mafundisho na mafafanuzi kutoka makanisa na madhehebu yanayokubali ubatizo wa watoto-Wachanga/wadogo na hata kuwapinga wanaokataa ubatizo huu.
  Je nina basi kati ya makundi haya kwamba yu sahihi?
  Je ni kwa namna gani wabatizwe?
  Je ni sababu gani zaweza kutolewa ili wabatizwe au wasibatizwe?
  Mchango wangu mdogo ni huu tu; kwanza katika kusoma Biblia kwangu hakuna mahali ambapo nimekuta wazi wazi ya kwamba hairuhusiwi kuwabatiza watoto. Hii ina maana kwangu ya kwamba wanaastahili kupokea ubatizo kama NEEMA ambayo ni zawadi.
  Jambo jingine ambalo naliona watu wengi wanalizungumzia ni ubatizo wa imani kisha toba …………na watu hujenga hoja ya kwamba watoto wadogo hawana dhambi.
  Yoh. 3:6 Kilichozaliwa na mwili ni mwili…..hii kwangu ina maana ya kwamba mtoto azaliwapo anayo dhambi ya asili. Dhambi- mshahara wake ni mauti Rum 6:23 Watoto wachanga wadogo wanaweza kufa mara tu wazaliwapo au baada ya masaa, siku wiki mwezi mwaka……..Kutokana na hali hii basi kama wasingekuwa na dhambi ya asili adhabu hii isingelikuwa juu yao. Na kama Mungu anaruhusu kifo kwa watoto wachanga wasio na dhambi basi atakuwa hawatendei haki.
  Kama Mungu anaweza kuwaadhibu watot wachanga bila wao kujua sababu, basi Mungu huyo huyo anaweza kuwapa neema ya ubatizo bila ya wao kujua.
  Kama ilivyo kwa mtoto kuona njaa na kiu bila yakujua maji na maziwa ni nini basi ni vivyo hivyo
  aweza kuwa na kiu na njaa ya neema na wokovu kiroho ili aipate.
  Ili kuupokekuamini na kuupokea ufalme wa Mungu watu wazima ni lazima wabadilike wawe kama watoto na wala si watoto wawe kama watu wazima.
  Kuhusu kuamini “imani” napo sioni kama ni sharti kwani tukumbuke ya kwamba wazazi wa mtoto huyu wanapompelekwa mtoto wao kubatizwa wana imani – wanafanya kama vile ile habari ya mtu aliyepooza, aliyebebwa na kupelekwa kwa Yesu. Imeandikwa hivi “Yesu alipoiona imani yao alimwambia yule mwenye kupooza, jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako”. Mathayo 9. Rafiki wa yule mtu hakuweza kumsaidia ila walimbeba na kumpeleka wakiwa na imani ya kwamba Yesu anaweza kutenda muujiza wa uponyaji. Hata kabla ya kutubu, Yesu akatenda..
  Iwapo ubatizo ni zawadi ya bure ambao hutokana na neema ya Mungu basi sioni sababu ya kuwazuia watoto wasibatizwe.
  Shalom na Mbarikiwe

 19. Ubatizo Kwa watoto
  A) Imani hizi za Mapokeo zimejegwa katika misingi ya Mapokeo ubatizo wa watoto kugombea waumini katika makanisa katika miaka ya giza ili kuwafanya watu wasifuate wanamatengenezo waliokuwa wakifuata misingi ya biblia na rumi iliyokataza usomaji biblia kwa waumini wake.

  B) Kuendeleza tamaduni ile iliyoanzashwa na mfalme aliyekuwa akiumwa na wakahofia kumtumbukiza kisimani kwa ubatizo eti walikuwa wanamheshimu sana lakini pia kuogopa angekufa iwapo wangemzamisha majini. Hivyo kanisa la Rumi likaruhusu kumnyunyizia maji kichwani hivyo ikaendelea mpaka sasa. Shida yetu wakristu ni washabiki wa dini sio washabiki wa Kristo ambaye ni neno, nae neno ni nuru, nayo nuru ni neno la Mungu ambalo liko katika Biblia ambalo watu hwalitii bali hutii watu na Mapokeo yao.
  OLE MAANA WAKATI U KARIBU FANYA MATENGENEZO
  Yesu ambaye ni neno Yohana 1:1, ambaye ni nuru anasema “WATU HAWA HUNIHESHIMU KWA MIDOMO, ILA MIOYO YAO IKO MBALI NAMI; NAO WANIABUDU BURE WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO YALIYO YA WANADAMU” Marko 7:6,7

  Agizo la Yesu juu ya ubatizo limeelezwa sehemu tofauti tofauti katika biblia.
  Mathayo 28:19
  19 Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la baba, na mwana, na roho mtakatifu;20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari.
  Marko 16:16
  Aaaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa.
  Basi inatulazimu vipi kubatiza watoto wadogo wasio weza kuamini. Hata Yesu aliwawekea watoto wadogo mikono kuwabariki,lakini tumegezaje mambo haya watu wazima tunawabariki na watoto ndio tunawabatiza.
  Kwa nini tubatizwe?
  Warumi 6:3 3
  Hamfahamu ya kuwa sisi sote tulibatizwa katika kristu Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Basi tulizikwa nae kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristu alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. (Warumi 6:3)
  Unapozamishwa ndani ya maji ni ishara ya kukubali kufa unapoinuliwa kutoka maji ni ishara ya kufufuka na kristo hivyo kujikabidhi kwa imani kwa ufufuo na kuvikwa mwili mpya.
  Wakolosai 2:12
  “mkazikwa pamoja nae katika ubatizo;na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
  Yohana 3:5
  Yesu akajibu akawaambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
  Ni ubatizo gani tunapaswa kubatizwa?
  Waefeso 4:5 tunaambiwa
  5Bwana mmoja, imani mmoja,ubatizo mmoja
  Yohana 3:23
  “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele;
  Basi kama tumeambiwa Bwana ni mmoja lakini pia imani ni mmoja basi imani hiyo ndio ya Yesu kristu ambaye alibatizwa kwa maji mengi Yordani basi kwa kuwa mbio zetu ni kuiga matendo yake basi imetupasa kufuata ubatizo huu.
  Ukisoma Maandiko Katika Mathayo 3, Marko1 Na Yohana 3 utatambua kuwa Yohana mbatizaji alifanya ubatizaji ndani ya mto Yordani kwa maji mengi isingefaa basi kushuka hata Yordani kwa matone machache ya maji.
  WAKRISTU TUACHE MAPOKEO HATA BIBLIA INATUAMBIA HIVI
  “watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wathesalonike; kwa kuwa walipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kwamba hayo ndivyo yalivyo” Matendo 17:11
  YESU ANASEMA HIVI
  “watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami; nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo ya wanadamu” Marko 7:6,7

 20. Unajua ndg Mkandya, hakuna tafsiri ya jambo inayolizidi jambo lenyewe! Basi unapoongelea Ubatizo wa Yohana, huo ulifanyika mtoni, watu walizamishwa huko, hebu jaribu kuchunguza iwapo kuna yeyote aliyempleka kichanga wake akazamishwe! Hakuna, wao walifahamu maana kamili ya jambo hilo!

  Pia Ubatizo wa wa roho na moto, unaousema, huo ni ubatizo wa Roho Mtakatifu ambao hufanyiwa huyo aliyeupitia Ubatizo wa Maji, maana imeandikwa, Yohana 3:5 “Yesu akajibu Amin Amin nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Kwa hiyo ni muhimu kupita kwanza katika Ubatizo huo wa Maji, ndipo huyo aliyeyaagiza hayo huja kulitimiza hilo aliloliahidi.

  Kuhusu Ubatizo wa Yohana, huo kazi yake ilikuwa kuwaongoza watu wampokee Kristo, Mdo 19:1-5, lakini kwa siku ya leo, huo sasa umebadilika kidogo, kwani sasa unafanywa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo, ili dhambi ziondolewe ndipo Roho Mt aweze kuja kukaa kwako, na yote yamhusuyo, Mdo 2:38.

  Kuhusu hilo alilolitangaza mtume Paulo, hilo liko sawa, halipingani na agizo la ubatizo. Kimsingi, kumkiri Kristo, ni kukubali kuongozwa katika yote yamhusuyo, hauwezi ukamkiri Kristo halafu ukaupuuzia ubatizo! Mwangalie Kornelio, Roho Mt alipowashukia, hawakuishia hapo, bali aliwaongoza majini kuikamilisha Haki yote. Pia tangazo hilo la mt. Paulo liliwaingiza katika wokovu wale wote ambao hawakuwa na fursa ya kutimiza ubatizo, labda kutokana na kukabiliwa na kifo, aidha kwa ugonjwa au wakati ule wa kuteswa na kuuliwa kwa Wakristo, labda leo usiku ndipo umehubiriwa Injili, ahadi ya kubatizwa ni kesho, lakini alfajiri askari wa kirumi wamekufikia, nao wanakuuliza, “Mkandya! Tunasikia ya kwamba nawe ni Mkristo, ukiikana imani hiyo ya wazushi tunakuacha tunaondoka, lakini ukiikiri tunakupeleka kule uwanjani kwenye wale simba wenye njaa, unasemaje?” Basi hao walioikiri imani hiyo katika namna hiyo anayoifundisha Paulo, Mungu aliwahesabia Haki kwa kukiri kwao, huo ndio ulikuwa Mlango wao wa Wokovu!

  Kuhusu kuhubiria viumbe, hilo ni sawa, Mungu ndiye azijuaye siri zote. Kwahiyo sisi yatutosha kuyatimiza yale yaliyofunuliwa kwetu. Iwapo unaweza kuwakusanya simba au chui au mbuzi, kisha ukawahubiria Injili, na baada ya hapo wakakuthibitishia kuwa wameamini, basi sioni ni kwa kigezo gani hao vichanga wetu pia walioipokea Injili wasibatizwe, ilimradi simba na chui na nyati umewabatiza! Ila unapokwenda huko porini, jitahidi uongozane na askari wa wanyama pori!

  Ni kweli, “Tufikirieni vizuri ndugu zangu,tusiseme kwa mazoea tu” maana watu watakuta Biblia tu, Mkandya kaliwa na simba, imebaki Biblia yake tu!!!

 21. Sawa kabisa ndg Lwembe, aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini aaminiye na kubatizwa kwa ubatizo upi, wa Yohana au wa yeye ajaye anayebatiza kwa roho na kwa moto?

  Kama wokovu unakamilishwa na ubatizo wa maji ilikuwa Paul yeye akasema ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni bwana na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka? Mbona hapa huyu mtu anaokoka bila kubatizwa?

  Halaf nani kasema kuwa mtoto mdogo hawezi kuhubiriwa injili? kwani yeye siyo kiumbe?
  Yesu kaagiza kuenenda katika ulimwengu na kuihubiri injili kwa kila kiumbe wala hakusema kwa watu wazima tu, bali kwa kila kiumbe. Na mtoto mdogo naye ni kiumbe.

  Tufikirieni vizuri ndugu zangu,tusiseme kwa mazoea tu.

 22. Mkandya, usitembee katika nchi usiyoijua kwa kutumia akili zako, utapata hasara!
  Unajua kauli yako kwamba, “…ubatizo wa maji hauna nafasi yoyote unayoongeza katika maisha ya ya wokovo ya mtu. Yaani wokovu bila ubatizo wa maji bado ni wokovu kamili.” Kwa kauli hii nakuona unaungana na hao wanaobatiza watoto, ambavyo mwisho wa siku nyote hamtapata lolote!!! Hakuna Wokovu bila ubatizo!

  Injili iko wazi, Marko 16:15-16 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Sasa Mkandya ni lipi lisilo eleweka hapo? Injili inayookoa ndio hiyo ndugu yangu, na hatua zake ndizo hizo, kuna mtoto anayeweza kuhubiriwa Injili?!

  Tena, ubatizo sio wa kunyunyiziana maji, huo si ubatizo, ni mchezo wa kuigiza tu. Ubatizo ni lazima uambatane na toba, kisha uzamishwe katika maji, kwa jina la Bwana Yesu Kristo, ili upate kuondolewa dhambi zako, ndiposa unaweza kukiri kuokoka, maana Dhambi zako si kwamba umesamehewa, hapana, bali ZIMEONDOLEWA, hazipo tena, zimetupwa katika bwawa la usahaulifu!!!
  HAYO NDIYO STANDARD YA WOKOVU!!

  Basi nanyi mnaowabatiza vichanga vyenu, vileteni tuvizamishe!!

 23. Elly ni nini kinatangulia, ubatizo kwanza ndipo umkiri Yesu na kumkataa shetani au kumkiri Yesu kwanza ndipo ubatizwe?

  Na kama ni kubatizwa kwanza ndipo umkiri Yesu kama wewe ulivyofanya, basi nini hasa nafasi ya ubatizo wa maji katika wokovu wa mtu?

  Halaf ipi bora kati ya kubatizwa kwa hiari yako huku ukijua kinachoendelea na kubatizwa ukiwa hujijui halafu unasubiri kuja kusimuliwa, je wakikudanganya kuwa ulibatizwa kumbe hukubatizwa utajuaje sasa?

  Ivi mtindo wa kubatiza watoto wadogo tena kwa maji ya kuwamwagia ulitoka wapi? kwa nini wakati wa Yohana mbatizaji watoto hawakubatizwa kama ambavyo wa kiume walikuwa wanatahiriwa siku ya nane?

  Halaf mtoto akibatizwa na baada ya kukua akakataa kuwa mkristo tutasemaje, kuwa amemwasi Bwana?

  Msimamo wangu ni kwamba ubatizo wa maji hauna nafasi yoyote unayoongeza katika maisha ya ya wokovo ya mtu. Yaani wokovu bila ubatizo wa maji bado ni wokovu kamili. Huu ni utamaduni tu ambao tu wa kikristo (christian ritual) ambao sio mbaya ni mzuri maana ndio unaojaribu kuionesha dunia kuwa mtu fulani kweli kawa mkristo. Lakini kigezo kabisa cha mtu kuwa mkristo ni kumkiri Yesu na kumwamini siyo kubatizwa.

  Naamini ubatizo wa Yesu kristo siyo wa maji, bali ni wa Roho mtakatifu kama Yohana mbatizaji alivyosema alipokuwa akisema habari za kuja kwa Yesu baada yake.

  Amina.

 24. Naam,kila mtazamo wa suala nyeti kama ubatizo ulio hapa ni wa kimadhehebui japo nafahamu niukisema hivyo nitapigwa kucha za mashambulizi.
  Binafsi sina shaka na ubatizo niliobatiziwa nikiwa MLUTHERI yaani mtoto mdogo.Sijafikiria eti wazazi wangu walikosea,eti mchungaji hakuielewa biblia vizuri na mambo kama hayo.
  Mimi niko pamoja na wale wanaoamini kuwa BIBLIA ni NENO LA MUNGU siyo LITERALLY bali contextually.Tena watunzi/AUTHORS wa Injili za Marko,Mathayo,Luka na Yohana,wote waliandikia makundi tofauti ya waumini kwa hiyop tafsiri yoyote literal haina faida kubwa.
  Kwa mfano:Kwa kuwa mto Yordani upo na Yesu alibatiziwa hapo kwa nini tusifunge safari tukachote upako kule?
  Suala lililoko mbele yangu na la muhimu ni kwamba je ni kweli basi ninaishi katika misingi ya ubatizo wangu? hasa baada ya kuw a mtu mzima nikathibitisha kwa kusema NAMKATAA SHETANI NA MAMBO YAKE YOTE NA KAZI ZAKE ZOTE.NIAJITOA KWAKO EE MUNGU ILI NIKUTUMIKIE KWA UAMINIFU HATA NITAKAPOKUFA.

 25. Jambo la kusema watoto wadogo ufalme wa mbinguni ni wao Yesu alilisema akimaanisha nin hasa?
  _ Kwamba tujue sifa alizo nazo mtoto mdogo ni Mnyenyekevu, Mpole,Husamehe na kusahau, Hupenda kujifunza, ni mkweli, ni mtii nk (mathayo 18:4), hivyo wapendwa tusipokuwa kama mfano wa watoto wadogo hatuwezi kuuona ufalme wa Mungu. yatupasa kujishusha. mathayo 18:1-3.
  KUHUSU UBATIZO
  Hebu tusome MARKO 2:3-5 9 (IMANI ZA WALE WATU WANNE WALIZOKUWA NAZO MGONJWA ALIPONYWA AU HAKUPONA. Sasa mnaposema tusiwabatize watoto mpaka wawe wakubwa?

 26. David unaposema ” sisi” unamaanisha ninyi akina nani?

  Na huo mtazamo mmeutoa wapi wa kufanya hivyo?

  Kwanza nani alikwambia kuwa ubatizo wa maji unampeleka mtu mbinguni?

  Unaposema wakifa waende mbinguni, ni nani kasema mtu akifa anaenda mbinguni, kwenda kufanya nini huko mbinguni?

  Tafakari kibiblia siyo kidhehebu!!

 27. Endapo utasubiri mpaka uwe mkubwa ili uamini na kubatizwa halafu ukafa je utakwenda motoni au utakwenda mbinguni? ndio maana sisi tunabatiza watoto wadogo ili hata kama watakufa waende mbinguni

 28. BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA;
  Mimi ninaamini ubatizo wa watoto unakubalika kwa MUNGU.
  KWANINI;
  Moja, Ukisoma katika kitabu cha Mark16:15 Biblia inatoa witu wa kuwahubiria VIUMBE VYOTE habari njema tukiwabatiza kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.
  Kwa mantiki hii kila kiumbe kinapaswa kuhubiriwa NENO la MUNGU regardless of its nature.Kama kila kiumbe kinapaswa kuhubiriwa NENO ,je mtoto si kiumbe.

  Mbili, ukisoma Mathayo 28:19 Biblia inatoa wito wa kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wa YESU.
  Swali kwamba,Je watoto wao hawapaswi kuwa wa YESU?Kama inawafaa ,basi hakuna njia nyingine zaidi ya njia ya UBATIZO.
  Tukumbuke kuwa wale wanafunzi wa YESU walipotaka kuwazuia wale watoto kwenda kwa YESU ,YESU aliwakemea akasema “Waacheni watoto wadogo waje kwangu……”
  Biblia inazungumza kwamba hakuna namna nyingine ya kuwa wa YESU zaidi ya kupitia ubatizo hivyo ili watoto waje kwa YESU inawabidi wabatizwe.

  SISI TUSIWAZUIE WATOTO KUJA KWA YESU BALI TUWASAIDIE KUJA KWA YESU KUPITIA MLANGO PEKEE AMBAO NI WA UBATIZO.
  AHSANTENI SANA WAPENDWA.
  AMINA

 29. Kuna mapungufu katika michngo mingi ya waliochangia kukataa ubatizo kwa watoto,kiasi kwamba hawajalenga kumfundisha anayeamini katika ubatizo huo.

  -Tulitakiwa tuambiwe mtoto ni yupi kwa muktadha wa ubatizo
  -Tujue ubatizo unaoongelewa hapa ni upi, wa Yohana(maji) au wa Yesu/ Roho mtakatifu (moto)
  Sijawahi kusoma mahali ambapo Yesu alibatiza watu kwa maji, wala mahali ambapo alisema tuwabatize watu kwa maji, maji mengi au kidogo.

  Alipotoa kinachoitwa agizo kuu alisema tuwabatize kwa jina la Baba,mwana na Roho mt., hakusema tuwabatize kwa maji. Kwa hiyo neno muwabatize si lazima iwe kwa maji.

  Siamini kama Yesu naye alikuja kuendeleza ubatizo wa Yohana(wa maji) ambao unaitwa ubatizo wa toba. Yeye alibatizwa kwa maji na Yohana kwa sababu ilimpasa kuitimiza kwanza torti na manabii( kuitimiza haki yote)

  Yohana mwenyewe alisema “mimi nawabatiza kwa maji lakini ajaye nyuma yangu yeye atawabatiza kwa moto. Ni rahisi kuaminui kuwa moto anaousema Yohana mbatizaji ni Roho mtakatifu kuliko kudhani ni maji yalayale ambayo yeye alibatizia

  Kusema kweli pia siioni sana nafasi ya ubatizo wa maji katika kuukamilisha wokovu.
  Petro alibatiza watu kwa maji ikiwa ni pamoja na yule towashi, lakini huwa nina hisia kuwa hata akina Petro hawakuwa wameelewa sana ubatizo Yesu aliouagiza, maana sioni popote walipobatiza watu wakati wangali na Yesu mwenyewe ( Hapa haya ni mawazo yangu mimi)

  Halafu suala la kusema mtoto mdogo ufalme wa mbinguni ni wake sio kweli, hakuna mahali biblia imesema hivyo.

  Sikubaliani pia na hoja kuwa watoto wadogo hawawezi kumwamini Yesu,hayo ni mawazo yetu tu. Yesu mwenyewe ametaka tuupokee ufalme wa Mungu kama watoto wadogo, halafu wewe unasema ati watoto hawawezi kumwamini Yesu! ajabu.

  Wapendwa nimesema hayo yote ili tufikiri kwa umakini zaidi juu ya suala hili,na kuyachambua maandiko kwa umakini zaidi.

  Samahanini sikuweka vifungu vya maandiko, biblia yangu ya soft copy imepata shida kidogo!

  Mbarikiwe!!

 30. anayebatizwa ni mtu mzima na si mtoto mdogo kama wachangiaji wengine walivyosema, na neno la Mungu huwa halipingwi.

 31. Wapendwa, hebu tuyarahisshe mambo, Ubatizo halali wa kiBiblia ni wa kuzamishwa katika maji mengi, yaani unatumbukizwa unapotelea huko chini ya maji ikiwa ni ishara ya kuzikwa na Kristo; basi ndugu zangu vileteni vichanga vyenu tuvibatize, na asiwepo wa kutulilia!!!!

 32. shalom, Kujadili maandiko, wengi wamefunguka na kujua ukweli, Hata kule kuomba tu kuwa tupewe maandiko yanaonyesha ubatizo wa watoto, pia ni kujifunza maana itambidi anetaka kujenga hoja aingie ndani ya Biblia na kutafuta, hatimaye asipoona ndipo ataamini kuwa agizo ni kubatiza WAKUBWA NA SI WATOTO.

  mbarikiwe.

 33. KWA HIYO TUUACHE UONGO WA SHETANI UENDELEE BILA PINGAMIZI KISA NI TARATIBU ZA DINI? @ Emmanuel Lyatuu.

 34. Samuel na Edwini, Bwana awabariki sana kwa kusema black Black and white. Na hiyo ndiyo sera ya Mungu. Wengi hufikiri kuwa, ukweli wa Biblia ni wa dhehebu fulani…. Mtoto mdogo HABATIZWI HATA DAKIKA MOJA. Edwini na Samuel wametoa hints makini sana. . Mtu anayepinga, ajue kuwa anampinga Mungu, maana neno limesema.

 35. Neno la Mungu linasema waacheni watoto wadogo waje kwangu maana ufalme wa mbingu ni wao hivyo hata hawahitaji kubatizwa kwani tayari ufalme wa mbingu niwa kwao. Vilevile Neno linasema mkiamini na kubatizwa mtaokoka hivyo mtu anatakiwa kuamini kwanza kisha ndio abatizwe hivyo huwezi kusema mtoto mdogo ameamini hivyo abatizwe na hapa yanatakiwa maamuzi binafsi na sio maamuzi ya wazazi/walezi. Mungu awabariki.

 36. Namshukuru Mungu kwa ajili ya Blog hii, Mungu ameiweka kwa makusudi yake, ninavyojua sio ya dini fulani, kama ingekuwa ya dini fulani ingesema mambo ya dini hiyo. Lakini inatufundisha Neno la Mungu, na ukisema Neno la Mungu, unasema Yesu, na kama ni Yesu, basi alichokifundisha mwenyewe, na kukifanya ndicho tunatakiwa tukifundishe, na tukifundishe, tunatakiwa tufuate nyayo zake ona 1Pt 2.21 kwa sababu ndio mlioitiwa, maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo mfuate nyayo zake. Yeye alibatizwa akiwa mtu mzima, akamwambia Yohana ambatize, ili watimize haki yote kama alivyochangia ndugu Edwin. Yule mbatiza mtoto mdogo ndiye anaweza akasema aliupata wapi, lakini Biblia inasema ubatizo ni Mazishi, Rum 6.4 Tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, viivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Biblia inatuagiza kuwabatiza watu, inaitwa Agizo kuu. Math 28.19. Soma utaona hilo Agizo kuu. Huo ndio mchango wangu. Ameni.

 37. Marko 16:16-“Aaminiye na kubatizwa ataokoka.asiyeamini ataukumiwa”-Hivyo ubatizo ni muhimu.Hata Yesu alibatizwa ili kutimiza haki yote.Math 3:15.

  Mark 16-inasema aaminiye na kubatizwa-Maana yake kabla ya mtu kubatizwa ni sharti aamini yeye mwenyewe kwanza halafu kubatizwa kunafuatia.Tukiwa wadogo tunakuwa hatujaamini sisi wenyewe ni wazazi tu ndiyo wanaotuongoza au walezi.Hivyo anayetakiwa kubatizwa ni yule aliyemuamini yesu kwanza kwa kuikubali injili hakafu anabatizwa.

 38. Kwa mtazamo wangu suala la kubatiza mtoto mdogo, mtu mzima, kubatiza kwa maji mengi haifai kuijadili hapa maana hizo ni taratibu za Mathehebu Na hazileti afya. Tujadili mambo yanayojenga na yapo mengi

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s