Naomba kujua tofauti Sala, Dua na Maombi!

sala

Shaloom wapendwa,naomba mnisaidie tofauti ya maneno haya ,sala,dua,na kuomba,pia je wafu wanahifadhiwa wapi kabla ya hukumu

–Samuel Elisante

Advertisements

10 thoughts on “Naomba kujua tofauti Sala, Dua na Maombi!

 1. helleluyaa! mbarikiwe sana wapendwa katika bwana. hakika nimejifunza kitu hapa. ahsanteni sana.

 2. Shalom wapendwa ktk bwana nafurahi sn kwa mitazamo mbalimbali inayotokana na maada tajwa sijui km nimechelewa ila namshukuru sn Mung kwa hili bac nami naweza kusema kuwa sala na maombi ni maneno tofauti na na utumikaji wake pia upo tofauti ijapokuwa zote ni njia za mawasiliano kati yetu na Mungu maombi kwanz ijulikane ni hitaji,rai lakini sala ni mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mwanadam na Mung wakati mwngn huweza kubeba maombi ndani yake lkn sala ni njia kuu ya kuwasiliana na Mung pia inaweza kuwa ni kuusifu utukufu wa Mungu au wakati mwng inawezekana ni kusema na baba labda kwa nia au kusudi maalum ndo maana katholic Wanasala zao na pia wanamaombi yanaweza yakawa ya mmoja mmoja au ya ujumla hivyo maneno haya hutofautiana kwa namna hiyo.
  Zaid ya yote nashukuruni kwakuwa nilitaka kujua na kwa kupitia hili bac pia Nina neno lakusema
  Amen

 3. SHALOM WAPENDWA!
  Kuhusu DUA SALA NA MAOMBI sina cha kuongeza kwani rev.Lee Cosmas ameshamaliza na ubarikiwe sana mr.Lee.
  kuhusu wafu wanahifadhiwa wapi wala usipate tabu wala hakuna anayezungukazunguka duniani bali biblia imesema mwanadamu amewekewa kufa mara moja na akishakufa ni hukumu kwa kujiridhisha soma LUKA 16:19-31

  BARIKIWA!!

  HARRISON

 4. Wapendwa wachangiaji wamesema vizuri nami napenda kuongeze tu machache kuhusu sala, dua na maombi. Kwa Kiswahili chetu maneno haya yanaingiliana sana na si rahisi kuyatofautisha.
  Katika Injili ya Mathayo Sura ya 6 ukianzia ule mstari wa 7 utalikuta neno “kusali” na ule mstari wa 8 lipo neno …….”hamjamwomba”. Mstari wa 9 unasema “Basi ninyi salini hivi” Ndipo Bwana Yesu anawafundisha marafiki wanafunzi wake namna ya kusali. Kwa mtazamo huu basi, mtu anaposali anatamka maneno ya sala. Hebu nijaribu kuchanganua “SALA YA BWANA” nina haki ya kwamba hii ina majibu ya kutosha kuhusu swala hili:
  Inaanza hivi:
  “Baba yetu uliye mbinguni
  Jina lako litukuzwe,
  ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe,
  hapa duniani kama huko mbinguni.
  Kipande hiki ni “dua” kumsihi Mungu – “supplication” na kumpa Mungu utukufu wake.
  Kisha baada ya hapo maombi yanafuata:
  Utupe leo riziki zetu (hapa ni maneno ya kuomba kupatiwa mahitaji yetu-yawezekana ugali, chapati, mavazi, mke au mme, watoto, Mark II au IV nk.)
  Utusamehe makosa yetu……………ni kama vile mtuhumiwa mahakamani anavyoomba msamaha kwa hakimu kutokana na kaso lake alilokiri mwenyewe.
  Usitutie majaribuni lakini utuokoe na yule mwovu………..hayo ni maombi. T
  Mpendwa, kuomba mtu anaweza kujiombea mahitaji yake mwenyewe na pia kuwaombea wengine.
  Kwa kuwa wako ni ufalme…………..
  sala hii inamaliza kwa kumrudishia Mungu utukufu wake yaani kwa dua. SUPPLICATION
  Mbarikiwe
  Rev. Lee cosmas Ndeiy

 5. Tofauti kati ya sala na maombi ni hii Sala ni yale madai ambayo mtu anayapeleka kwa Mungu ambayo hata asipoomba anapewa mf. anaomba chakula nguo hayo hata usipoomba utapata ndiyo maana kila mtu anapata hata wasiomuabudu (angalieni ndege wa angani hawalimi…..).
  Kuomba au maombi ni yale madai ambayo usipoomba hutapata na ukiomba kisha akapata yatamrudishia Mungu utukufu.
  Wafu waliokufa katika Bwana wanakwenda katika mangojeo hadi siku ya mwisho ndiyo maana Yesu akamwambia yule mwizi msalabani Amini nakuambia leo hii utakuwa nami paradiso au peponi sio mbinguni maana hawaendi mbinguni. Waliokufa katika uharibifu hatujui ila logic yetu tu inasema wapo wanazungukazunguka tu katika dunia katika ulimwengu wa roho ndiyo maana tunawaona katika ndoto.

 6. sala ni kile kitendo cha kumwabudu Mungu. Dua, ni yale maneno unayowasiliana na Mungu. na Maombi ni mjumuiko wa sala, dua, nyimbo pamoja na kusoma neno la Mungu.
  Nafikiri umenipata rafiki
  nzala

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s