Ushauri wa bure kwa waimbaji

bish

Kuna watu wamejiingiza kuimba muziki wa Injili, sio kufanya huduma. Bali kwa sababu eti “Rose Muhando anaendesha Prado, Bahati Bukuku kajenga ghorofa”. Kwa hiyo wanaimba kwa sababu muziki ndio biashara inayolipa fasta. Wanachafua kanisa kwa kuimba vituko na wameteka vituo vya redio kwa kuhonga watangazaji ili nyimbo zao zipigwe kwa fujo na wapate mialiko makanisani. Saa ya anguko la watu kama hao imekaribia. Mtazunguka na CD bila kupata ndululu. 2013 Mungu anakumbuka watumishi wake kweli kweli kwa jina la Yesu”

Bishop Nickodemus Shaboka Jr.
Advertisements

8 thoughts on “Ushauri wa bure kwa waimbaji

 1. Maandiko yanasema kwamba msingi wa imani yetu in Yesu mwenyewe.Waefeso 2:20-22 na sisi tunapaswa tujengwe juu ya misingi ya mitume na manabii waliotutangulia,kwa lugha nyepesi ni kwamba tunapaswa tuige na kufuata mafundisho ya mitume na manabii walio tutangulia ambao na wao walimfuata Bwana Yesu 1 kor 4:16;Filipi3:17;1 kor 11:1,sasa kutokana na mafundisho haya ya mitume na manabii,hakuna sehemu yoyote wanayofundisha kwamba uimbaji ni hiduma maalum.Lazima tuwe wasomaji wa Neno maana Neno ni Yesu mwenyewe.Yohana 1:1-5;10-14;Ufunuo 19:13.

 2. KAZI YA MUNGU HAIWEZI KUWA BIASHARA HATA KAMA NI KIPAWA CHAKO MAANA HICHO KIPAWA UMEPEWA NA MUNGU KWA AJILI YA NENO LAKE LIENEE KWA NINI IWE SEHEMU YA KIPATO CHAKO? MAANA KAMA INGEKUWA INAWEZEKANA MUNGU KUWA BUNIA MRADI BASI HATA WAHUBIRI INABIDI

 3. Aksante ndugu kwa ushauri tuzidi kumwomba Mungu talanta hii aliyotupa ya Uimbaji tuitumie katika Roho na kweli na sio kutafuta faida katika ulimwengu huu maana hapa tuko safarin. Mali hazitupeleki mbinguni wala kujulikana na wanadamu wenzetu.
  UIMBAJI iwe ni OFISI YA KUTUPELEKA MBINGUNI NA SIO KUTAFUTA FAIDA ZA DUNIA..

 4. Ndugu Miranda, umenishtua sana na hiyo aina ya ushabiki ”Bishop waambie hao”.

  Siyo sawa kuwa na ushabiki wa namna hiyo kama kweli wewe ni mkristo, huo ni ufarisayo na kujihesabia haki!

  Ni vema ukachangia mawazo kwenye hoja ya msingi.

 5. Hoja hii ni nzito, nashauri kuwa isiwalenge waimbaji tu, ilenge mtu yeyote analiye na tegemeo la kuingia Mbinguni. Maana Mtume Paul aliwaandikia Wakoritho KAZI YA KILA MTU ITAKUWA DHAHIRI,MAANA ITAPIMWA KWA MOTO, IKITEKETEA MTU HUYO ATAPATA HASARA, IKIKAA ATAPATA DHAWABU. 1 kor 3.10…15. Nimeshauri ushauri huu ulenge kila anayefanya kazi ya Mungu, awe Mtume, Nabii, Mwinjilsti, Mch. Na Mwalimu, pamoja na huduma Zingine zote. Wafilip waliambiwa hivi, wengine Mungu wao ni TUMBO. Filp 3..19 kusudi lao ni Tumbo, wengine ni FITINA, HUSUDA, ni vizuri huu wa bure utufanye tujihoji kila mmoja wetu, je hili ninalolifanya kusudi langu hasa ni nini?. Naweza nikasema ktk mdomo, lakini ktk moyo ndipo kusudi linapokaa, na Mungu anauangalia moyo. Asante kwa ushauri wa bure.

 6. Jamani huduma ni nini katika kipaji cha mtu kuimba?

  Au je kila aliyeokoka mwenye kipaji cha kuimba lazima aimbe kama huduma?

  Mleta hoja naomba unisaidie ili niendelee kuchangia mawazo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s