Enenda kwa Roho, Ushinde Majaribu

neno

Mtu ajaribiwapo, asiseme, ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. – Yakobo 1: 13 – 16 SUV

Ibilisi anatuletea majaribu akiwa na lengo la kutusababisha tutende dhambi na hilo litufanye tukose ujasiri mbele za Mungu, na hivyo polepole aidhoofishe na hatimaye kuiua imani yetu na ikiwezekana na sisi wenyewe pia. Mungu hamjaribu mtu kwa uovu badala yake hutuwekea mlango wa kutokea ili tuweze kustahimili na kushinda. Chanzo cha majaribu yetu mengi ni tamaa zetu wenyewe na njia pekee ya kuyashinda ni kutokuruhusu tamaa zetu za mwili zitutawale. Lakini kuzishinda tamaa za mwili kwa nguvu zetu sisi wenyewe hatuwezi, ndio maana Neno linasema: Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. – Wagalatia 5: 16 SUV

Unaye Roho Mtakatifu ndani yako, yeye ni mwalimu wako, msaidizi wako, mtetezi wako, mwombezi wako, ndiye anayetuwezesha kutembea katika ushindi ambao tunao ndani ya Yesu. Ikiwa umeanguka katika dhambi usikubali shetani akujaze shutuma na hukumu, upendo wa Mungu na neema yake kwako havijabadilika, mgeukie Bwana Yesu bila kusita, alishateswa kwa ajili ya dhambi zako zote, usinyong’onyee wala usimruhusu ibilisi akutese nazo tena. Inuka endelea mbele kwa ujasiri ukiitikia wito wa Mungu juu ya maisha yako.

Sisi tuliomwamini Bwana Yesu tumehesabiwa kuwa wenye haki mbele za Mungu, tunashinda na zaidi ya kushinda kwake yeye aliyetupenda. Roho Mtakatifu na atukumbushe kweli hii tunapokabiliana na majaribu mbalimbali.

Mungu azidi kuwabariki

Patrick
Advertisements

10 thoughts on “Enenda kwa Roho, Ushinde Majaribu

  1. Ubarikiwe sana mpendwa, Ni kweli kuwa baada ya kumjua Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo hatutakiwi kuishi katika dhambi tena. Itokeapo mkristo ameanguka ktk dhambi basi shetani huja na mahubiri ya ” wewe basi hufai tena kwa ufalme wa MUNGU. wokovu haupo kwa ajili yako” hivyo ni kweli kabisa kama ulivyo sema mtu akisha pokea mahubiri hayo hainuki tena. Ahsante sana kwa ujumbe mzuri.

  2. asante kaka kwa ujumbe wenye kutia moyo kwa wale waliokufa moyo.Mungu akubariki sana!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s