John Lisu azindua album yake kwa mafanikio!!

Mwimbaji wa gospel nchini kijana John Lisu na kundi lake hapo jana alifanikiwa kuzindua album yake ya sauti iitwayo ”UKO HAPA” kwa mafanikio makubwa na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viunga vyake katika uzinduzi ambao umefanyika ukumbi wa kanisa la kisasa la City Christian Centre (CCC) lililopo maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ulioanza majira ya saa tisa ulisindikizwa na waimbaji kama Glorious Celebration, Cosmas Chidumule, The Voice, Pastor Paul Safari, Next level na wengineo, ambapo kama yalivyokuwa maombi yake Joh Lisu kwamba Mungu apate kujaza uwepo wake mahali pale ndivyo ilivyotokea na kwamba watu waliofika wamebarikiwa na kile ambacho mwimbaji huyo na timu yake walijiandaa zaidi ni kuona akipata sapoti kubwa kutoka kwa mkewe ambaye alipiga gitaa la bass huku pia akiwa ni mmoja wa watunzi katika album mpya ya mumewe.
Mwite Tumaini Ona Machang’u katika pozi, ni back vocalist wa John Lisu.
Pam akiwa na mke wa John Lisu, Ney Lisu(kuume) kabla ya kupanda stejini.
John Lisu akiwa na mpapasa kinanda wake Fred Masanja, a.k.a Rick Jeph van Rickbell.
 
Samuel Yonah akiongoza jahazi kabla ya Lisu.
Baadhi ya umati wa watu, waliofika mapema kuwahi sehemu ya kuketi wakifuatilia jambo stejini.
The Great John Lisu on stage akimsifu Mungu.
 
Mambo yalikuwa mazuri hakika. picha by Samuel Sasali.
Nelly Lisu mke wa John Lisu akicharaza gitaa la bass. hakika Mungu atakupa wakufanana nawe mwe mwe! picha Samuel Sasali.
Fred Msungu na Fred Masanja au mwite Rick wakipapasa vinanda.
 
Mpiga gitaa la bass kijana Danny Silandah akiwajibika kwa furaha bila kushurutishwa.
Samuel Yonah akikung’uta gitaa la solo. Picha kwa hisani ya John Lisu na Rickbell.

–Gospel Kitaa

Advertisements

One thought on “John Lisu azindua album yake kwa mafanikio!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s