Paula White azua gumzo!!

Paula-White-Trumpet-Awards

Mchungaji maarufu Paula White hivi karibuni amezua maswali mengi kuhusu mavazi yake jinsi yanavyobadilika tofauti na alivyoanza huduma .

Mtandao wa Praise Radio wameandika “Mavazi ya Pastor Paula White yanaleta gumzo jinsi gani mwanamke wa Kikristo anapaswa kuvaa…”

Vyombo mbali mbali vya kikristo vimekuwa vikiandika kwamba kwa sasa Mchungaji Paula White amezidisha kuvaa mavazi yanayoonesha mwili wake.

Advertisements

19 thoughts on “Paula White azua gumzo!!

 1. “Ole wake akwazae na ole wake akwazikae,” !!! aliposema tuvae mavazi ya kujisitiri alijua kwamba hapa kuna kukwazana!!! vilevile kama mwamini lazima neno likusafishe hata ukiona mtu kavaa mavazi yasiyoyakusitiri wewe hutamani, tataizo linakuja masaa yote mwamini yuko mwilini,anakuwa rohoni siku ya j pili au akiamua kufunga ndipo atakuwa rohoni, biblia inasema kesheni mkiomba msije mkaingia majaribuni!! si kukesha kwa kutolala ,ni kuwa hai ndani ya roho, uwe umelala usingizi uwe macho wewe unamtukuza mungu tu!!

  wakristo jehanamu ipo na ina watu wengi kwa kutokwenda sawa na maandiko!!! huyu roho mtakatifu ni mwaminifu sana, hutufunulia ila wanadamu tunafata mawazo yetu au tunaona kama hatujaenda na wakati !oh God tusamehe !!!

  Wengine wakasema suruari si vazi la heshima haya mtumishi wa mungu kavaa suruari?? jamani mavazi ya kujisitiri ndio mpango mzima mkiristo mwenzangu, roho mtakatifu ndi hutunulia mambo yote hata mafumbo ya mungu roho hutufunulia,

  asanteni ,na mungu awabariki!!

 2. Asante Lwembe kwa matusi ya chinichini.

  Lakini nataka ujue kuwa Yesu aliposema kuhusu kumtazama mwanamke kwa kumtamani hakusema kumtazamamwanamke aliyevaa nguo ambazo zinaonesha maungo ambayo hayatakiwi kuonekana hadharani. Bali kumtazama mwanamke akiwa katika form yoyote.

  Kwamba kama amevaa joho halafu ukmtazama kwa kumtamani ni uzinzi kama vile ambavyo atakuwa amevaa sketi fupi ukamtazama kwa kumtamani ni uzinzi vilevile. Ndio maana nikakupa mfano Zanzibar, wanajifunika kiasi kwamba hata macho huoni lakini gesti unakuta zimejaa watu wa short time.

  Hapo tatizo si la mwanamke, bali la mtazamaji anayetamani.

  Kuhusu kwamba hakusema amtazamaye mwanaume kwa kumtamani, Lwembe usiwe asiyejua kiasi hicho. Biblia imeandikwa kutoka katika utamaduni wa kiyahudi ambapo mwanamke alikuwa hahesabiwi. Bila shaka hapa unajaribu kusema kuwa suala la kutamani liko kwa mwanaume na si kwa mwanamke. Je hujasoma Mungu alipomwambia Eva kuwa na tamaa yako itakuwa kwa mumeo…? Kumbe mwanamke nae hutamani.

  Halafu kaangalie maana ya neno theolojia. Kama unadhani theolojia ni upuuzi , basi sishangai kukuona una-ague kwa hoja za juujuu. Unasema theolojia ziko nyingi, sawa, kumbuka hata tafsiri za biblia ziko nyingi lakini neno la Mungu ni moja

  Kwa hiyo unaposema matajiri wanaenjoy kuwatazama mabinti wameva vibikini, unataka kuniambia na wewe kama mkristo ikitokea uko mahali akaja binti amevaa bikini utaenjoy kuangalia sawasawa na hao matajiri?

  Lwembe ivi una picha gani kichwani mwako ya jinsi Yesu alivyo? Unadhani Yesu asingeenda uwanjani kuangalia riadha, wanawake kwa wanaume wamevaa vinguo ambavyo almost vinaonesha hata maumbile yao nyeti? Unadhani asingeenda kwa sababu ya kuogopa atatamani akiona mapaja ya wanawake, na matiti yao?
  Nakwambia hata bichi angeenda kupumzika bila shida yoyote. Au unadhani watu kuvaa vichupi beach wameanza leo,? hata wakati anahubiri akiwa kwenye pantoni kuna waliokuwa wamevaa hivyo.

  Lwembe kama wewe kweli uko na kristo moyoni mwako, suala la kutamani ni kuamua, maana nguvu hiyo imo ndani yako. Kama wewe utaamua kuwa huwezi kuacha kutamani wakiwa wamevaa ambavyo unadhani inatamanisha, basi uko kwenye hatari kubwa maana kila kukicha ndio wanazidi kuelekea kwenye hata kutembea bila nguo.

  Ni vema watu wote si wanawake tu, katika kanisa wavae nguo zinazokubalika na utamaduni wa jamii wanamoishi. Hakuna mahali biblia imesema watu wavae nguo fupi au ndefu za kubana au pana, zinazoonesha kwapa au zisizoonesha nk. Mashart hayo twayweka kwa sababu ya udhaifu wetu.
  Kuvaa nguo si kwa ajili ya Bwana bali kwa ajili yetu. Uchi wako haumtishi Bwana wala kujifunika kwako hakumtishi

  Lwembe wewe ni mwanafasihi mzuri sana!

 3. Mkandya, unajua ndg yangu, utakuwa a bit selfish! Sheria ya Mungu haimkamati mkristo peke yake, bali watu wote watakao pungukiwa katika hiyo. Kwahiyo iwapo wewe huwa huwatamani wanawake, basi ni towashi mzuri, lakini si kila mtu! Hata wakristo, kwani kuwa mkristo kunakufanya kuwa immune wa kuwatamani wanawake? Ni mabinti wangapi wanaojazwa mimba kwenye kwaya? hujasikia kuhusu yule mchungaji aliyekamatwa na nyumba ndogo? Au nawe mambo haya yanakuumbua?

  Sheria mpya ya Uzinzi inasema hivi, Mt 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Jaribu kuisoma bila papara, inasema “ATAZAMAYE MWANAMKE KWA KUMTAMANI” haisemi atazamaye mwanaume! Sasa kama kwa utashi wako hutaki kuyaelewa Maandiko yanachokuelekeza, ni kwa jinsi gani utakielewa ninachokisema? Theme ya mwanamke kuvaa nguo zinazositiri mwili wake inatokana na sheria hiyo. Kama huyo aliyemuumba anakwambia m,wanamke hutamaniwa, wewe ni nani hata umuone ni aliyepitiliza? Kwa hiyo wazo la kwamba mimi namuona mwanamke kama chombo cha starehe, litakuwa ni finyu kiuhalisia, bali ni msaidizi, na nguvu yake ya ushawishi ni kubwa sana, huwalainisha mpaka wafalme!

  Kuhusu wanawake kuhudumu, sijui unaongelea kutoka katika base gani, theologia au Biblia? Theologia ziko nyingi sana na katika kutofautiana, kwahiyo hatuwezi tukadraw a standard kutoka hizo. Wakatoliki hawaruhusu makasisi wanawake, lakini Wapentekoste wanaruhusu, sasa hivi wanajadili au wanabishana juu ya kuwasimika wanawake kuwa Maaskofu, kwa hiyo huwezi ukasema kwa uhakika ni yupi aliye sahihi kwa kuzitegemea hizo theologia.

  Lakini iwapo unaongea kutoka katika base ya Biblia, mbona liko katika urahisi. Hiyo 1Tim 2:12 iko hivyo hivyo kwa zaidi ya miaka 2000! Hivi unahitaji kumpata mwanazuoni wa Theolojia ambaye amebobea, ndio akuambie maana ya “Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali…”! Au Mkandya hauelewi tunachokizungumza? Kama umefika mahali ukajua kuwa mfreji wa matiti ya mwanamke hautamanishi, unashindwa nini kuelewa kifungu kama hicho? Au unajitoa uelewa kwa makusudi? Tena Maandiko hayakuliacha jambo hilo la kumkataza mwanamke lining’inie tu bila sababu, RM anamrudisha Paulo mpaka huko Edeni na anakuambia, “Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” Sasa iwapo mwenye kazi yake kasema mwanamke asiifanye, unadhani wewe kwa kulazimisha kwako itafaa kitu?

  Unamzungumzia dada yake Lazaro; hebu mcheki kwanza yule mwanamke aliyemuosha miguu kwa machozi na kumfuta kwa nywele zake, na kummiminia yale Mafuta ya bei mbaya, halafu ndio urudi kwenye huo utamaduni wenu, kwa huo ambao sasa nakuona uzalendo unakushinda, na umeanza kuelewa wanawake wanatamanika vipi!

  Hivi Mkandya, umewahi kuyatazama mashindano ya warembo? Unawajua wanaoyagharamia? Kwa taarifa yako ni matajiri, wanao enjoy kuwatazama mabinti katika hali zao hizo mpaka za vibikini! Wewe utakuwa unaziona zawadi na matangazo tu, au ni kati ya wale wanao starehe kimya kimya, lakini nyuma ya mambo hayo ziko roho, lusting spirits! Kwahiyo hiyo michezo ya tenis unayoipenda sana, jaribu kumuona Kristo mmekaa naye hapo, mkiwatazama hao mabinti, ukiona mko naye, hilo ni jema pia maana nwe umestarehe, ukiwa na shaka, isikilize hiyo shaka, inaweza kukuponya!

  Kuna vifaranga vya mbuni vilichukuliwa vikatunzwa shambani, vilipokuwa mbuni wakubwa, wakarudishwa porini; masikini, walikuwa hawajui chochote kuhusu fisi, wakaliwa woote! Ninakuona huna ujuzi wowote kuhusu wanawake kama wale wachungaji wanaoandaa mashindano ya “miss gospel”, AU haswa, utakuwa mtaalamu sana wa mambo hayo, kama ulivyouona mkao wa Mariam dada yake Lazaro, ambao wengi wetu hatujawahi hata kuuwazia!!

 4. Chiwango ni vema ukamwagiza binti yako avae kama utamaduni wenu unavyotaka.

  Kwa mfano wanavyovaa wanawake wa kimasai ni tofauti sana na kawaida ya wanawake wa jamii zingine. Kumbuka wanawake wakristo wa Tanzania wanavaa kama wanawake wa Tanzania wasio wakristo, maana suala la kuvaa ni la kiutamaduni wa jamii fulani wala si utamaduni wa biblia. Hata wanawake wakristo wa India hawavai kma wanawake wakristo wa Tanzania, bali wanavaa kama wanawake wa India wanavyovaa kwa utamaduni wao.

  Nakwambia hivi, wanawake wa kabila la watindiga (ambao bado wanakaa maporini zaidi) wakiokoka, kuficha sehemu ya mbele tu labda na chuchu halitakuwa tatizo kwa wanaume wa kitindiga waliookoka na wasiokoka, maana huo ndo utamaduni wao unaokubalika. Lakini najua kabisa kwa wenzangu na mimi ambao huo si utamaduni wetu tutapata shida na hayo mavazi.

  Kwa hiyo hapo tatizo si wao, bali ni sisi ambao huo si utamaduni wetu..

  Tusitake kuingiza utamaduni wetu fulani tukasema huo ndo utamaduni wa biblia, biblia haina utamaduni, bali wenye tamaduni ni watu wanaoiamini biblia. Suala la kuvaa halimshusu Mungu bali wanadamu, maana kama Mungu hujikwaa dada akivaa nguo fupi, basi huwa inabidi akina dada/mama wakiingia kuoga bafuni Mungu aondoke waoge kwanza na kuvaa wakimaliza arudi tena awe ndani yao.

  Ndio maana Paul akasema kwa watu fulani alikuwa mtu fulani( yaani aliamua kufanana nao ili awapate)

  Chiwango mambo haya yanahitaji ufahamu wa kutosha ili kuyafafanua sawasawa.

  Haiwezekani jamii nzima ya wakristo ikawa na utamaduni wa aina moja, ispokuwa maadili ya aina moja. Wakristo wanatakiwa kuwa ‘standard’ sawa ya maadili lakini si kuwa na utamaduni unaofanana.

  Haya barikiwa.

 5. Lwembe nimeshtuka mpaka nikaogopa. Kwamba huo mstari wa kifuani wa huyo mama hapo juu unaweza kukufanya uwakwe tamaa! Unatakiwa kumwona mwanasaikolojia haraka sana, maana una matatizo ya mwili na kiroho.

  Kama kuna idadi kubwa ya wakristo wako hivyo kama ulivyosema, basi wakristo wengi hutenda dhambi ya kutamani kila baada ya dakika tano.

  Shida yangu nyingine kwako Lwembe ni kwamba huwa nakuona mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kupembua mambo, lakini nahisi nimekosea sana. Bila shaka una upeo mkubwa tu katika mambo fulani ya Literature (Fasihi)

  Muktadha ulio katika chapisho lako ni kwamba wanawake hawaruhusiwi kabisa kusimama madhabahuni na kusema neno la Mungu. Kwamba wachungaji wanawake, manabii wanawake, walimu wanawake nk wako kinyume na neno la Mungu.

  Lwembe nenda kamuulize mwanazuoni yeyote wa Theolojia unayemfahamu ambaye amebobea akuambie maana na ‘application ya hilo andiko la 1Tim 2;12

  Ninavyojaribu kukuelewa hapa ni kwamba humwamini mtumishi yeyote wa leo ambae hafanyi kama vile ambavyo wewe ungetaka afanye, kwako inaonekana mtumishi wa kweli ni yule aliyeandikwa kwenye biblia. Labda nikuulize swali na wewe ; kwa nini biblia ilikoma kuandikwa, na kama ingekuwa inaendelea kuandikwa ni nani na nani waliopo leo wangeandikwa kwenye biblia kwa habari ya utumishi wao?

  Ulishawahi kufikiri kwa nini zinaa katika nchi za kiislamu iko kiwango cha juu kama tu ilivyo katika nchi zisizo za kiislamu? Nenda Zanzibar ukachunguze jinsi gesti zinavyojaa, lakini wanawake muda wote wamevaa baibui.

  Kwako naona mwanamke ni chombo cha starehe,kwamba mwili wake upo tu kwa ajili ya ngono, yaani ukimwona tu mwanamke wazo la kwanza linakuja ngono, ukiona tu mfereji wa maziwa yake unakumbuka ngono, ukiona tu kwapa yake ni tamaa kwa kwenda mbele. Mtu wa namna hii unahitaji tiba ya haraka sana.

  Hebu fuatilia habari ya Mariam dada yake Lazaro aliyefufuliwa na Yesu pale biblia inaposema alikuwa amekaa miguu pa Yesu wakati Martha anahangaika na mambo ya jikoni. Fuatilia neno ”miguuni pa Yesu” kwa tafsiri ya asili uone alikwa amekaa sehemu gani hasa. Halafu ukifikirie hicho kitendo kwa utamaduni wa kitanzania uone kama kinaleta picha nzuri.

  Frank usijikakamue sna mtumishi, maana ya neno mavazi yanayositiri kwa tafsiri ya asili ya maandiko ni mavazi yanayokubalika na jamii yanamovaliwa wala si mavazi yanayoficha sehemu fulani ya mwili kama unavyodhani.

  Kwa mfano: Mavazi yanayovaliwa kwenye mchezo wa tenis na wanawake ni mavazi yanayostiri katika huo mchezo japo kuwa ni kama vichupi tu fulani na kitop. Kwa maana nyingine ni kwamba ukivaa joho kwenye tenis utakuwa umevaa vazi lisilositiri

  Watu wenye akili nzuri wasiohitaji kwenda kumwona dokta wanapomwangalia Serena Williams anacheza tenis hawaangalii maungo yake bali wanaangalia anavyocheza tenis.

  Anyway, ngoja nimalize hivi; ni udhaidu mkubwa sana kwa mkristo kuwakwa tamaa ya mwili kwa kuona tu kwapa za mwanamke, wenzako tunaona ni kwapa tu wewe mwenzetu unaona nini?

 6. shaloom wapendwa
  Nakubaliana na hoja na ukweli wa kile mpendwa Lwembe anachosema.
  Mimi nilipookoka chini ya mch.Nkone wa VCC nikiwa udsm nasoma nakumbuka sana Roho Mtakatifu alivyonipa msukumo wa kubadilisha mavazi yangu kutoka katika jinsi ya kidunia(namaanisha kama wasanii wa bongo fleva) na kuwa na mavazi ya heshima.
  Hii ilifanya watu wengi wakubali na kuamini kweli nimeokoka na Mungu kanibadilisha.Hii ilimpa Mungu utukufu sana(elewa katika kila jambo unalofanya,linatakiwa limpe Mungu utukufu)
  Ushuhuda;dada mmoja anaitwa cecy nilijuana nae kitambo ktk mambo ya kidunia zaidi,nikiwa naenda kanisani victoria pale nikabahatika kukaa nae siti moja ktk daladala.Mara akaniuliza,kaka naona siku hizi unapendeza,unavaa nguo za heshima sana ,umeokoka nini,nikamwambia ndiyo nimeokoka,akasema Hakika Mungu anaweza,natamani na mimi niokoke nibadilike kama wewe!
  Hapa wapendwa tunajifunza kuwa katika mambo yote tunayofanya na kumiliki,tunapaswa tumpe Mungu utukufu(hapa ndipo kuwa barua ya kusomwa na watu) pia Kristo alisema”wayaonapo matendo yenu mema wamtukuze BABA wa Mbinguni”
  Wachungaji wengi hawaongelei mavazi,hii ni kuwapotosha kondoo na kuwapalia makaa ya mawe,kweli mavazi yako yakiwasasbabishia wengine kuingia dhambini hakika na wewe umetenda dhambi ni sawa na kumsaidia mtu kuiba hapo na wewe umekua umeiba tu!Tusidanganyike
  Hebu soma Hapa.Mwanzo mwanzo 3:7 Adamu na Eva baada ya kutenda dhambi wakajikuta uchi na aibu ikawashika wakajitengenezea nguo za majani wakajifunika.
  Lakini Mungu alipokuja na kuwaona aligundua mavazi yao yana kasoro na hayampi utukufu ndo maaana yeye MUNGU akawatengenezea mavazi ya kusitiri miili yao soma katika Mwanzo 3:21 Mungu akatengeneza mavazi ya ngozi akawavika.
  Sasa kama Mungu anachukua jukumu la kuwavika adamu na eva swala la mavazi Mungu analiangalia sana pia ,kwa mtumishi kama huyu ni aibu tena hafai kuigwa,tusidanganyike eti ni mzungu,mila za kwao nooooo,hapaaaan Neno la MUNGU haliangalii mazingira,heshima haiangalii ,mazingira.
  Usiumize kichwa etu mbona ni pastor,aaaa mtu aanaweza kuwa pastor au mtumishi kwa ujuzi tu aliosomea chuo na si moyoni mwake ndugu na kama n swala la kujaza watu kanisani kwake,inawezekana wanajaa kwa sababu sehemu hiyo ina mafundisho manyonge na mchungaji n kipofu haoni na hivyo watu wengi watapenda kwenda hapo watafanya mambo yao maovu bila mtu yeyote kugundua.Elewa ukiona kanisa kubwa watu wanajaa ni mambo mawili tu labda kanisa hilo lina nguvu kubwa sana ya Mungu au kuna mafundisho hafifu na manyonge tu yanayovutia watu yaani kanisa limepoa haliko na nguvu za Mungu.
  Mungu anaagiza watu wavae mavaz ya kusitiri miili yao,katika Biblia ,msitari nimeusahahu ila unasema na wanawake yawapasa kuvaa mavazi ya kusitiri miili yao.(KUSITIRI-Tafuta tafasiri yake uelewe zaidi) mimi nasema ni kuficha au kuhifadhi.Soma hapa 1petro2:12,3yohana1:11,1korinto 10:23,31-33
  1korinto 3:16 Miili yetu ni hekalu la Mungu,sasa inakuwaje hekalu la Mungu halipewi heshima?
  Bishop Kakobe lishafundisha somo linaitwa”MAVAZI YA KIKAHABA” hebu tafuta hii DVD upanue uelewa maana watu wanaaangamia kwa kukosa maarifa;
  Mbona wazungu wengi tu wanavaa nguo za heshima?
  Mungu awabariki sana wapendwa,
  Nawapenda katika Bwana.
  Amen.

 7. Mkandya! Unasema niache kupotosha!

  Nashindwa nianzie wapi ndg yangu! Hivi unajua lolote kuhusu kupatwa na “MFADHAIKO”? Basi kwa taarifa yako, watu wengi sana hupatwa na mifadhaiko, maofisini, ndani ya madala dala nk, ukiwauliza, ni nini kilikuvuta mpaka akili ikakutoka? Majibu utakayopewa utashangaa! Pia, unajua kuwa umbile la mwanamke ni la kupendeza na kutamanika? Hivi unajua chochote kuhusu kuusitiri mwili? Hivi Maandiko yanapotuambia “tuwe barua za kusomwa”, unavyofikiri wewe, msomaji wa barua hiyo ni nani, waliookoka au jamii nzima? Hivi Mkandya, huuoni huo mfereji wa matiti ya huyo dada hapo kwenye hiyo picha? Waliozibuni hizo nguo za jinsi hiyo, wanao uzoefu mkubwa sana wa mambo hayo. Wanazijua sehemu zoote za mwili wa mwanamke zinazoweza kuamsha hisia au attention ya wanaume na hata wanawake, na hivyo kuwa capture into a following, kama ambavyo nakuona nawe tayari umedakwa na una sympathize na jambo lililo kinyume na maadili ya Kikristo. Dunia nzima iko katika mahangaiko kwa sababu ya mwanamke mmoja tu, Adamu kwa kumpenda kwake mkewe aliamua aachane na Neno la Mungu na akaambatana na mkewe! Ndugu yangu, usicheze na wanawake!!!!

  Mkandya, jitahidi kuyaheshimu maumbile, mwili wa mwanamke uko annointed kumuangusha mwanamume! Hivi unajua kuwa makasisi wa Kikatoliki wengi wao wana watoto huko mitaani? Basi kukijua kilichowadaka hata kuwaangusha, utakuta, mwingine miguu, mwingine hiki mwingine kile, mpaka hizo kwapa, kama hujui! Haya ni ya mwilini.

  Kuhusu ya rohoni, unaniambia,
  “Lwembe unachotaka kutuambia hapa ni kwamba wanawake hawapaswi kuhutubu (kufundisha neno la Mungu). Huku ni kupotosha kwa hali ya juu sana”
  Maelezo unayoendelea nayo yamenishangaza sana. Umerudi mwilini saana! Kama tutafika mahali tukasema jambo hili liliwahusu Waefeso, hili liliwahusu Wagalatia au ah Paulo alikuwa anawachukia wanawake, tutakuwa tumeikosa maana nzima ya Injili, au akina Ben Hinn wan Injili mpya?! Agano Jipya si Agano la mwilini, bali ni la rohoni. Unaposoma, “kwa kanisa lililopo Efeso, andika,” yaangalie vizuri maelezo hayo, kisha rudi katika historia ya Kanisa, utaukuta wakati ambapo Kanisa lilikuwa katika hali hiyo kiroho! Hebu jaribu kuyatazama maelezo yanayolihusu kanisa lililoko Laodekia, utaiona hali yake ni sawa na hii tuliyomo, kanisa tajiri, limejitosheleza kwa vyote, lakini kiroho ni kipofu tena liko uchi nalo halijui! Maandiko yanasema simpi ruhusa mwanamke, wao wanasema hao walikuwa ni Waefeso, hivi, hamjui kuwa mt. Paulo aliziona hizo roho zikiwapandisha wanawake mimbarani hadi wakati huu wa leo yaani Waefeso wa leo?!

  Hivi Ben Hinn anapatikana katika kitabu gani humo kwenye Biblia? Ninawafahamu wanawake wengi sana ambao wametembea na wanatembea na Mungu, kwa kule kutembea kwao na Mungu huwa HAWALIVUKI Neno lake, wamejazwa Roho Mtakatifu, huyo aliyeiandika Biblia, kwa hiyo Roho huyo hawezi kujipinga. Kama huyo Ben Hinn aliwekewa mikono na mwanamke, hilo ni jambo la kusikitisha sana, maana hilo lingeonesha kuwa Roho aliyekuwa ndani ya Paulo, si huyo aliyemo ndani ya huyo mwanamke aliyemuwekea mikono, wala Ben Hinn mwenyewe aliyeipokea mikono hiyo!!

  Njia ya Mungu iko MOJA tu, Yesu Kristo, ambaye ndiye Neno, yaani hiyo Biblia yako yoooote, “Mtu hataishi kwa mkate pekee, BALI KWA KILA NENO litokalo katika kinywa cha Mungu.” Kinywa cha Mungu ni manabii na mitume, sina uhakika kama na Ben Hinn naye ni kinywa cha Mungu! Jaribu kuiamini Biblia yako zaidi kuliko watumishi ambao wanapaswa kuyarudia hayo Mungu aliyoyanena, ukiona wanakuambia mwanamke rukhusa kufundisha, kabla hujayameza hayo nawe kuyafundisha, hebu icheki kwanza ile Gal 1:8 inasemaje, ukiona uko sawa, basi ndugu yangu jitayarishe kwa yanayofuata, vinginevyo, TIMUA MBIO!!!

 8. Ipo kazi, kama tunasema ukweli ya kuwa mavazi hayo hayana shida basi naomba Mungu anisamehe maana mimi nakwazika na sio mtumishi tu hata mtu wa kawaida anapovaa kama hivyo. na siwezi kumruhusu binti yangu avae namna hiyo

 9. Jamani mafundisho yake mazuriiiiii, anafundisha namna ya kumjua, kumtumikia na kumuamini Mungu. Watu siku hizi tuna kiu ya neno la Mungu lakini mara nyingi unasikia watumishi wetu wanahubiri mafanikio tu ya kiuchumi which is good lakini tunataka uhalisia wa rohoni pia, Utamaduni wetu na wao tofauti, si bora hata yeye amevaa vizuri ukilinganisha na wengine niliowaona makanisani? Sikilizeni anayonena msifuate anachotenda

 10. Lwembe acha kupotosha!

  Nafikiri suala la mavazi na kutamani nafikiri tulishalijadili. Si sawa kumhukumu huyu mama kwa ushahidi wa hilo vazi lake. Kina dada wangapi katika matukio ya harusi zao wanavaa nguo hata kuzidi hiyo ya White? ina maana huwa mnatamani sana mkienda kwenye sherehe za harusi!

  Nini cha kutamani katika vazi hilo hapo juu? Kama kuona kwapa ya mwanamke inakufanya kutamani unahitaji kumwona dokta. Kila siku kwenye madaladala na kwenye mitaa tunaona kwapa za wanawake ziko inje, ki utamaduni wetu hiyo ni kawaida sana. Jamani kwapa ina matatizo gani mpaka uitamani kama si ugonjwa huo ni nini!

  Lwembe unachotaka kutuambia hapa ni kwamba wanawake hawapaswi kuhutubu( kufundisha neno la Mungu). Huku ni kupotosha jamii kwa hali ya juu sana. Andiko fulani linapoandikiwa jamii fulani ya kanisa,si lazima linawahusu na jamii nyingine ambayo haina tatizo kama la jamii iliyoandikiwa. Kwa nin ujumbe wa kanisa la Efeso haukuwa sawa na ujumbe wa kanisa la Laodekia katika Ufunuo 3? Ni kwa sababu matatizo yao hayakuwa yanafana.

  Kanisa la Efeso alilokuwa anachunga Timothy lilikuwa na matatizo ya wanawake kutaka kuwa na mamlaka juu ya wanaume, ndipo Paul akatoa huo mwongozo. Halafu leo wewe unataka kutuambia kuwa ati wanawake kote duniani hawapaswi kufundisha! Unalipotosha hilo andiko.
  Kama hawapaswi kufundisha kwa nini anasema watatabiri? au watakuwa wanatabiri wakiwa wamekaa jikoni wanapika? Yoel 2:28

  Unamjua aliyempaka mafuta Ben Hinn? Ichunguze historia Lwembe uwaone wanawake ambao walitembea na Mungu!

  Labda kama huyu dada kuna jambo jingine ambalo amekosea, lakini kama ni hilo vazi alilovaa, hatuna mamlaka wala haki yoyote ya kumhukumu kuwa hayuko katika njia ya Mungu.

 11. Dada Cathy ni kweli kwamba yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine ila kuna mambo sisi kama watumishi wa Mungu hatufanyi kwasababu ni dhambi ila kwasababu ya nafasi tulizonazo, hivyo tusijaribu kuiga namna ya dunia hii kwa namna yeyote ila mwenendo wetu umpendeze kristo na watu wake.

 12. Hii ni roho ya upotevu ambayo huwashika watumishi maarufu huyu mama anameshikwa na pepo la ukahaba hivyo alivyo hana tofauti na makahaba wengine,
  pepo la upotevu linakuja kwa njia nyingi, linaweza kuja kwa njia ya uzinzi unashangaa tu ghafla kusikia mtumishi fulani maarufu sana anatembea na wake za waumini wake bila aibu hatakidogo, au kwa njia ya kupenda sana fedha au kwa njia ya majivuno.
  Jukumu letu sisi kama wakristo ni kuwaombea watumishi wetu ili damu ya Yesu izidi kuwafunika na hekima ya R/M ikae juu yao

 13. Mkandya, mbegu ya mbuyu kwa udogo wake hailingani kabisa na mti wenyewe! Kwa hiyo, kama huko mwanzo ulitoka nje ya Neno hata kwa milimita moja, ukaiacha njia, basi kwa kadiri unavyoendelea katika safari yako, katika mwendo mfupi usingeiona tofauti, lakini ukisafiri km 10000, tayari utakuwa uko mbali sana na ile njia ya kweli, safari ya kurudi kule mwanzo ni ngumu sana, lakini inawezekana; bali wengi hushindwa kurudi, nayo makundi yanayoshabikia hukuongeza nguvu ya kuendelea na safari yako kuelekea huko unakokwenda! Basi, kumtenga mwanamke na sifa si jambo rahisi, lahitaji discipline ya kiungu. Huyo hapo mtumishi wako Mkandya, kifua nje, ni wanaume wangapi ambao kwapa za dada huyo zimewaingiza katika kumtamani? Au ni wasagaji wangapi wanahangaika jinsi ya kumpata? Huenda ni makundi hayo hayo yanayompa hizo tuzo!

  Biblia inasema, Mt 5:27-28 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Natumai Mkandya unajua kuwa ile adhabu ya kifo kwa mzinzi haijawahi kuondolewa, basi hebu niambie, ni wangapi watakaingia kifoni kwa huyo mwanamke?

  Vile vile Mkandya, utumishi wa Mungu, si kwamba unajicock mwenyewe na kujiingiza humo, wengi wa waliofanya hivyo wanaishia katika aibu. Mungu huwachagua watumishi yeye mwenyewe, na kuwasimamia. Tena Mungu si kigeugeu hata leo aseme hampi mwanamke ruhusa ya kufundisha, halafu kesho yake amsimike mwanamke huyo huyo kufundisha!

  Kuhusu kumuombea huyo “mtumishi”, mimi nadhani ungemuomba Mungu aibadili kauli yake kwanza, hiyo katika 1Tim 2:12, ukifanikiwa katika hilo, basi huna haja ya kumuombea huyo dada!!!

 14. Mh ndugu Lwembe naona kama umehukumu sana!

  Yawezekana kweli kuna tatizo kwa huyu mama, lakini bado ni mtumishi wa Mungu. Mimi naona hilo ni tatizo la kiutamaduni zaidi.

  Halafu sijkuelewa pia kwa nini umetumia hilo andiko hapo juu!

  Ni vema tukamwombea huyu mama kama tunaona unaekea kubaya, kuliko kumsema vibaya.

 15. Neno la Mungu halipitwi na wakati. Iwapo utajidanganya kuwa Mungu ni old fashioned, basi kwa huyu muhubiri na ujifunze jambo. Amepanda kuhubiri kinyume na mapenzi ya Mungu, “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.” (1 TIM. 2:12 SUV). Waliomsifia, definitely walikuwa ni sehemu ya yale mapepo yaliyokuwa yakimsukumia upotevuni, na sasa kulingana na hiyo “Glamorous Gospel”, msishangae hayo mavazi, nayo ni sehemu ya hiyo Injili! Having a form of Godliness…!!!!

 16. Nampenda pastor Paula White. Mavazi si kitu cha kupiga kelele, ni mwanadamu kama wengine

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s