Tusipende Injili za kutia moyo!

mhubiri

Shalom wapendwa!!.
Ninayo furaha kubwa sana kwa kazi njema ya Mungu inayosonga mbele kupitia blog yenu. Mungu azidi kuwabariki sana na kuwazidishia maono zaidi ya kuwafikia wengi zaidi katika kufundisha kweli yote ya Neno la Mungu. Ni muhimu kufahamu kuwa siku hizi za mwisho mafundisho mengi ya walimu wengi yametoka nje ya lengo la kuwapeleka watu mbinguni. Wengi wanafundisha mafundisho ya uongo kutokana na roho zidanganyazo zitendazo kazi siku hizi za mwisho ( 1 TIMOTHEO 4:1; 2TIMOTHEO 3:1,13 ). kwa sababu watu wengi siku hizi wanapenda mafundisho laini na kuwafurahia walimu wanaochuja Neno la Mungu, Mungu mwenyewe sasa anawaletea roho ya upotevu watu hao ili wauamini uongo kwa sababu hawataki iliyo kweli (2 WATHESALONIKE 2: 10-12; 2 TIMOTHEO 4:3-4 ). Kuna watu ambao hawapendi kuambiwa kweli au nkuhubiriwa kweli kama wale wa nyakati za Nabii Isaya ( ISAYA 30:9-10 ). Nyakati za Isaya walikuwepo watu waliowaambia walimu wao wawafundishe mafundisho laini yadanganyayo.

Kutokana na watu kutopenda kweli, Mungu anaachilia pepo wanaoitwa pepo wa uongo kuingia katika vinywa vya watumishi na kufundisha mafundisho laini yadanganyayo ( 2 WAFALME 22:20-22 ). Tunaona nyakati hizi za mwisho unabii ukitimia mbele za macho yetu. Yesu Kristo alisema kuwa siku za mwisho maasi yataongezeka na kufanya upendo wa wengi kupoa ( MATHAYO 24:12 ). Ni upendo upi unazungumziwa hapa? Upendo unaozungumziwa ni upendo wa kumpenda Mungu yaani kuzitii sheria zake na amri zake ( YOHANA 14:19:21,23 ). Watu wengi siku hizi hawataki kuongozwa na sheria ya Mungu, hawataki kuishi sawasawa na maagizo ya Mungu. Ni watu wanaochagua baadhi ya maneno ya kutendea kazi katika Biblia na hawataki kuishi sawasawa na kweli yote ( 2 WAKORINTHO 13:8 ).”Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli bali kwa ajili ya kweli”. Daudi anasema ( ZABURI 119:6 ) “Ndipo mimi sitaaibika nikiyaangalia maagizo yako yote”.

Watu wameuacha upendo wa kwanza ( UFUNUO 24) wahubiri wengi wanakwepa kufundisha baadhi ya maandiko katika BIblia kwa mfano ( 1 TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:3-6; KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5; ISAYA 29:16, WARUMI 9:19-21; MWANZO 35:1-5; KUTOKA 33:4-6; EZEKIELI 23:26-30,40,42 ). Waumini wengi wamekuwa vuguvugu wala si moto au baridi na shetani anajua kuwa vuguvugu wote watatupwa motoni. Vuguvugu ni watu wote wanaoyapenda mambo ya dunia wakati huohuo wakitafuta kuingia mbinguni. Mungu anasema tusiipende dunia wala mambo yake ( 1YOHANA 2:15-17 ). aipendaye dunia hujifanya adui wa MUngu ( YAKOBO 4:4 ). Utakuta makanisani leo wanawake wamevaa suruali tena wengine wakihudumu madhabahuni. Suruali siyo vazi la wanawake kabisa na Biblia inawataja wanaume kadhaa wakiwa wamevaa suruali. Kuna mipaka katika mavazi na Mungu analijua hilo na yeye ndiye mwanzilishi wa mavazi ( KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5 ). Nyakati zilizopopita miaka michache hapo nyuma makanisa mengi yalikuwa yakichukizwa na kuchukia kuona wanawake wakisuka nywele na kuvalia mapambo kinyume na Neno la Mungu (1 TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:3-5 ). lakini leo hii upendo wa kwanza hata kwa watu wanaoitwa watumishi wa Mungu (viongozi wa makanisa ) umepoa. Maasi yanafananishwa na baridi. Kadri baridi inavyozidi kuongezeka makali yake ndivyo kitu kilichokuwa na moto ( joto ) kinazidi kupoa vivyo hivyo na maasi yanavyozidi siku hizi za mwisho kabla ya palapanda ndivyo na upendo wa wengi unapoa na hatimaye makanisani wanajaa watu vuguvugu ambao hawawezi kuingia mbinguni ( UFUNUO 3:15-16; MATHAYO 24:12 ). Dunia hii hatutaweza kuitikisa na kuupindua ulimwengu kama mitume wa kanisa la kwanza ( MATENDO 17:6 ) kama hatutakaa katika msingi wa mitume na manabii ( WAEFESO 2:20 ) na kuziepuka injili za kutia moyo watu kuendelea kufanya uchafu na machukizo mengi kwa Bwana. Nguvu ya Mungu haiko leo makanisani kama nyakati za mitume kwa sababu ya kuingiza machukizo ndani ya maskani mwa Mungu ( 2 NYAKATI 36:14-16 ). Hata ile inayoitwa miujiza katika majumba ya ibada ambako kweli yote haihubiriwi na utakatifu wa kweli ( WAEBRANIA 1:9 ) tunapata kujua kuwa ni roho zidanganyazo na ishara za uongo za siku za mwisho. Mungu wa walimu wa uongo wasiofundisha Kweli ya Neno la Mungu ni Tumbo na maandiko yanasema ( WARUMI 16:17-19 ).

Namshukuru Mungu kwa blog hii yenye mafanikio makubwa sana kwa kuwa na watu wengi wanaoingia na kutoka kila siku. Nawaombea mafanikio zaidi katika kuujenga mwili wa Kristo. Nawaomba sana ujumbe huu msiufanyie Editing ya aina yoyote kwa lengo la kuupunguzia makali yake. Kumbuka kuwa kuna chakula cha watoto wachanga kiroho na chakula cha watu wazima (waliokomaa ) kiroho.

Asante sana na Mungu awabariki sana kwa usomaji wenu mzuri,

–David Carol

9 thoughts on “Tusipende Injili za kutia moyo!

 1. Cha kushangaza na kuhuzunisha,unapo simama mbele ya waumini ukiwaambia ukweli wa matakwa ya Mungu,kuna wenye wanaghadhabika na kuanza kujenga mawazo ya kukuchukia wakiwemo wenye wanaonekana kama/ kuwa ni watumishi wa Mungu.MUNGU MUUMBA WETU atusamehe na atusaidie kwa hii kazi yake.

 2. Asante sana mtu wa Mungu David Carol kwa KWELI hii ya neno.
  Kwako Ndugu Geromy unaposema kwamba Ndugu David amwombe Mungu Asikwazwe na vitu vya nje kama mavazi unakuwa umeingia ktk mtego ule ule wa uongo ambao David ameuongelea. Watu wasiomjua wanapoangalia watu waliokoka hawaangalii roho zao wanaangalia miili yao ambayo juu yake kuna mavazi. Kama ni mavazi yasiyo na heshima lazima tu yatakwaza watu. Wagalatia 5;19 inaongelea matendo ya mwili kuwa ni dhambi nabyote yanafanyika kwa nje. Acha kujifariji na uongo ndugu yangu fuata KWELI upone

 3. Asante sana ndg. David kwa sms yako nzuri na yenye mafundisho mazuri. Nimeipenda sana. Mungu akubariki sana.

 4. Asante sana mtumishi, injili kama hizi siku hizi kuzipata ngumu na hata zikitolewa waumini tunajihami maana hatutaki kuonywa,wala kukosolewa endelea kutufundisha ili tupone

 5. Aksante ndugu David kwa ujumbe nimeuelewa na ndo maisha ya sasa na kabisa tunakoelekea ni upotevuni ni kwaninini tunapotoshana kwa maneno ya ufariji ili hali kabisa ni kinyume cha mafundisho ya Mungu. Neno la Mungu hufundisha , huonya na hata kukosoa, basi tuzidi kumwomba Mungu awainue wale wanaolihubiri jina lake wahubiri kweli watu tuishi kweli ya Mungu. Mungu anatamani sana wote tuende mbinguni na tumshinde shetani na tamaa zake.
  Yesu anasema anaenda mbinguni kuandaa MAKAO JAMANI KWELI TUNAACHA NAFASI HII IPOTEE BURE SABABU YA DUNIA “Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo”. YOHANE 14:3
  MBARIKIWE

 6. Nimefarijiwa sana na maelezo yako David na ni kweli watu siku hizi wanataka sana mambo ya kidunia kama pesa,majumba,magari,mavazi n.k ukiwapa neno kwamba Mungu anatutaka kutaka sana mambo ya rohoni wana mistari yao ndani ya biblia watakutajia kwamba wokovu ni kutajirika kupendeza n.k wao wanawake kuvaa suruali sawa,kiburi kwao sawa,majivuno kwao sawa.Neno la Mungu linatumiwa vibaya unaweza kumkuta mvulana anamwambia msichana tupendane na tusinyimane kwani biblia inaruhusu huku akiwa ma lengo baya kwa huyo msichana kisa katumia neno la Mungu kumlaghai msichana.Si ajabu kuona watu wamekaa baa wengine wakristo wakinywa bia siku hizi huku wanasikiliza gospel Music wapo waliokoka unaweza kuwaona nao wakipita eneo hilo huku wakicheka.Kwa ujumla siku hizi KUNA WOKOVU FEKI NA MAHUBIRI FEKI NA NDIO MAANA NENO LINASEMA NJIA YA KWENDA UZIMANI NI NYEMBAMBA NA WATAKAO ENDA NI WACHACHE WENGI WATAENDA NJIA PANA YA MOTONI .Amen…

 7. David zipo suruali za kike, ambazo wewe huwezi kuzifaa kulingana na tamaduni yetu… Suala la mavazi si suala la kumtia mtu unajisi,,ila kama wewe unaona si sawa basi ni kwako, na mimi nionaye sawa basi ni kwangu..imeandikwa katika Biblia ufanyapo jambo pasipo imani ni dhambi..pia soma 1 Wakorintho 8.

  Ushauri wangu ni kwamba jitahidi na pia umuombe Roho Mtakatifu usipate kukwazika kwa vitu vya nje (visivyomtia mtu unajisi), kwa sababu inakupelekea kufanya hukumu kitu ambacho kama muamini na mfuasi wa Kristo hutakiwi fanya.,

  mbarikiwe nyote

 8. Shalom ndugu David Carol
  Kweli mambo zote unasema ndio inasimama makanisani ya leo. Ile upendo ya kujuwa NENO la Mungu ndio iko naenda na kupoa juu ya tamaa ya Cheo na Pesa ndani ya makanisa . kitu ya kufanya ni kutuniya Ngabo ya IMANI kumukono ya kushoto na Upanga waroho kumukono ya kuliya pamoja na maombi ya kweli. Mungu awatembelee .Kuna maneno mengi unaposema lakini nikuanza somo ya Neno moja kwa moja .unajuwa mafalio utembea pamoja na tamaa nyuma yake inatafuta Cheo na Kiburi inajitokeza . Kuna mengi ya kusema ile ndio wazo langu kama nimekosea munisamehe
  Mubarikiwe

 9. Binafsi, nimeipenda sana text yako hii mtumishi. Bwana akubariki sana David. Umeisema ile kweli kabisa. Nimefurahi sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s