Unawaza nini kuhusu suala la kuchinja nyama machinjioni!!

wachungaji

Wapendwa, kuna suala limeibuka la akina nani wanastahili kuchinja nyama mpaka maaskofu kutoa tamko? Hivi karibuni Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jijini Mwanza, umetoa tamko kali kwa kuwataka waumini wa dini hiyo kutokula nyama yoyote iliyochinjwa wa Waislamu.

Tamko hili limetolewa mwisho wa mwezi uliopita na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu, mbele ya viongozi wa madhehebu mengine, katika kikao cha pamoja kilichoketi kwenye moja ya majengo ya Kanisa la Kwa Neema Jijini Mwanza.

Kauli hiyo ya viongozi wa kiroho imekuja siku chache baada ya kuibuka mgogoro mkubwa baina Waislam na Wakristo juu ya nani mwenye halali ya kuchinja nyama hasa maeneo ya Machinjioni.

Mbali na Umoja huo wa madhebu ya Kikristo jijini Mwanza, unaojumuisha Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), umetangaza pia kusudio la kuufikisha mgogoro huo Mahakamani, ikiwa ni pamoja na kuitaka Serikali itafsiri kisheria ni nani hasa kati ya Waislamu na Wakristo mwenye mamlaka ya kuchinja nyama.

Vyombo mbali mbali vya habari Tanzania

Advertisements

27 thoughts on “Unawaza nini kuhusu suala la kuchinja nyama machinjioni!!

 1. Kama huyu ng’ombe tunayeulizana kachinja nani, mbona hatuulizi kafuga nani na alikuwa anamfanyia ibada nani ili amfanikishe kwenye ufugaji wake? Tunanunua vitu sokoni, hivi tunajua ni mungu yupi na madhabahu zipi zinayoendesha hizi biashara au wale waliotengeneza hizo bidhaa. Hivi ukienda hospitali ukaambiwa unahitajiwa kuwekewa damu, utawaambia unataka damu iliyotoka kwa Mkristo tu? Ukiletewa damu na ukaambiwa ilitolewa kwa mganga fulani hivi au shekhe, utakataa kuwekewa hiyo damu? Too much doubting to everything reduce our level of faith.

 2. wale wanasiasa walipotoka tu walipotamka yale matamko ambayo ndio yanasababisha vurugu sasa,ni bora wangesema wote wanahaki ya kuchinja na watu tunakula tu bila shida na si kweli kwamba ni haki ya mwislamu tu…..naamini Jehova yu mwenye rehema na atatupitisha katika hili kwa kukaa chini na kuchukuliana ila kuchinja nyama ni haki ya wote na mkristo hatakiwi kulazimishwa kuchinjiwa njama na asiyetaka kula na asile kama kitimoto tu.
  barikiwe

 3. Linaweza kuwa haramu kwao, lakini swali langu mimi inakuwaje haramu kwao pale ninapochinja nyumbani kwangu? Na kama wanavyo dai kwamba kwao suala la kuchinja ni ibada, inakuwaje wanalipwa ili watimize hiyo wanayo iiita ibada?

 4. Richard bila shaka unajua hata sisi wakristo huwa tunakula tu siku zote bila hata kuuliza nani kachinja, na hata sasa tunaendelea kula bila kuuliza nani kachinja. Leo nimekula nyama hata sijui nani kachinja, maana sihitaji kujua.

  Shida inakuja pale mtu anaposema ili nyama iwe halali kuuzwa buchani lazima awe amechinja muislamu, akichinja mkristo hiyo ni haramu. Na pale ninapofanya sherehe kijijini kwetu na kuamua kuchinja ng’ombe ati lazima nikamtafute muislamu aje anichinjie.

  Neno haramu na halali yana maana katika misingi ya kiroho, waislam wanaposema kitu ni haramu au halali ujue hicho kinahusika na suala la ibada au kibali mbele za Mungu. Ndio maana wao wanapochinja kuna masharti fulani ya imani yao lazima wayatimize.

  Mimi nakataa kuchinjiwa na muislamu kama lazima si kwa sababu akichinja kitanidhuru, bali ni kwa sababu anataka kujaribu kunionesha kuwa ati mungu wake yeye ni mkubwa kuliko Mungu wangu.

  Kumbuka nia ya waislamu ni kutaka watu wote wafuate imani ya kiislamu ikiwezekana, leo tukiona ni poa tu wao pekee ndo wawe na haki ya kuchinja kesho watataka wanawake wote wavae baibui, kesho kutwa watataka mtu asibebe biblia hadharani, mwisho watataka nchi iwe ya kiislamu.

  Kumbuka wameanz na mahakama ya kadhi, jiulize kwa nini wanataka mahakama hiyo iwekwe kwenye katiba ya nchi. Yaani katiba iseme ” kutakuwa na mahakama ya kadhi……..

  Wakristo wenzangu mambo mengine ni ya kushugulikia kwa kutumia sheria za nchi ambazo pia zinatuhusu hata sisi tukiwa kama raia wa hii nchi.

  Tukisubiri yapitishwe tuanze kuomba Mungu, tutakuwa hatujawa werevu wa kutosha

 5. pengine ingetupasa kuwauliza mashehe kuwa inakuwaje wakinunua nyama katika mabucha ya wakristo wanakwenda kula pasipo kuuliza KACHINJA NANI MKRISTO AU MUISLAMU?…Pia tukiwakalibisha majumbani kwetu kula kuku na pilau,wanakula bila ya kuuliza kuwa akiyechinja ni dini gani…iko mifano mingi sana kama kwenye mahoteli ya kikristo nk.,huwa hawaulizi kabisa zaidi ya kula.sasa hoja yangu hapa kwa ndugu zetu hawa wangetusaidia kwa kutujibu kuwa inakuwaje mnyama aliechinjwa na mkristo ni haramu kwao hafai kuliwa wakati huo huo mazingira fulanifulani WANAFAKAMIA NYAMA HIZO PASIPO KUCHUNGUZA ALIECHINJA NI DINI GANI?….kwa kuwa hata wakijitetea kuwa hawawezi kuchunguza na kujua kirahisi aliechinja..je,sababu hiyo ndiyo inatosha kuifanya nyama ile isiwe haramu kwake kwa mujibu wa dini yake?,…tusidanganyane bwana kama ni vitu haramu tunavila sana kwa mazingira mbalimbali tusiyoweza kuyatambua lakini mungu pekee ndiye atulindaye….swala la kachina huyu au yule kwa hiyo mimi sili ni misingi ya imani potofu za waziwazi na itikadi hizi za kidini kamwe haziwezi kujenga upendo na usawa wa mwanadamu kwa mwanadamu haya ni MAPOKEO TU YA KUTENGANISHA WATU NA WALA HAYAWEZI KULETA UPENDO WA KWELI WA MUNGU ALIETUUMBA….pia kwa upandewa hao wakristo kuweka mikakati ya kutonunua nyama katika mabucha ya waisilamu ni makosa makubwa sana ya kiroho!!…sielewi kwa nini maana hakuna sheria iliyopitishwa inayowakataza wakristo kuchinja hivyo inatupasa tuendelee kuchinja kuuza na kula pasipo visasi na uhasama…atakae nunua anunue atakae kataa na akatae hilo halituhusu bora maisha yanaendelea lakini UKISHINDANA NA MWENDAWAZIMU BASI HAKIKA NA WEWE NI MWENDAWAZIMU!!..Na zaidi ya hapo kwa mkristo annaefanya hivyo huyo hajajitambua na ni mwana wa ibilisi kwa kuwa amenaswa na mtego wa ibilisi na kupoteza sifa za kiroho…yeye bado anashindania mambo ya kimwili na damu na nyama kama lile andiko la bwana mmoja hapojuu anavyosema katika mchango wake.Tuwe macho hizi ni nyakati za mwisho yanakuja mengi magumu kuyafanyia uamuzi lakini biblia neno la kweli la mungu pekee ndilo lenye majibu yote ya mambo hayo yanayokuja…asie na neno atashindwa na mitego ya shetani na kutumbukia upotevuni.siasa na visasi sio jibu bali BIBLIA NENO LA MVNGU NDILO JIBU LA YOTE.mbarikiwe

 6. Wapendwa kwa mimi binafsi sijui kama kuchinja kunahusiana na ibada kwa Mungu wetu, aidha sifahamu pia kama Bwana wetu Yesu Kristo aliposema kuwa MUNGU ni ROHO na wao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli alimaanisha mambo ya kuchinja yanaingia kwenye ibada hiyo. Pengine nitahitaji ufafanuzi zaidi juu ya andiko lisemalo vyakula havituhudhurishi mbele ya MUNGU.

 7. Mimi nafikiri kimsingi tumeshaelewana katika hili jambo!

  Ki uhalisia wakristo wa Mwanza waliamua kutonunua nyama iliyochinjwa na waislamu kwa kutaka kufikisha ujumbe kuwa si sawa wao (wakristo) kuzuiliwa kuchinja.

  Kama hili jambo litafikia muafaka kuwamba wakristo nao wachinje na nyama hiyo iizwe buchani, najua kitatokea kitu kifuatacho: waislamu walio wengi watataka kununua nyama kwenye bucha za waislamu wenzao, lakini wakristo watanunu nyama popote,si lazima kwenye bucha ya mkristo. Naupenda sana ustarabu ulio katika ukristo.

  Sebastian nimeguswa sana na hii kauli yako, ”Wakristo tunapaswa tuseme ukweli ili waislamu pamoja na serekali watumbue kuwa tupo,tusifarijiane kwa maandiko bila kusemea kuwa tuna haki pia katika hayo wanayopinga, kuwa hatuna haki ya kuyatenda”.

  Asante ndg Chiwango kwa kukubali kuujua ukweli wa mgogoro huu. Ni kweli hata mimi nakubaliana na wewe kuwa baada ya huu mgogoro kuisha, wakristo wasianze kuwa wanauliza ” nani kachinja hii” bali wanunue tu, maana hakuna cha kuwazuru.

  Mungu azidi kuribariki kanisa!

 8. wakristo tuamke sasa, waislamu kuchinja kwao ni ibada hivyo wanatulazimisha ibada tusiyopashwa kuifuata,halafu tujiulize kabla ya uislam wakristo tulikuwa tunachinjiwa na nani? haiwezekani mkristo afuge mnyama halafu muislam afuge kisu kwa ajili ya kumchinjia mkristo, mungu wa waislam siyo mungu wa wakristo kwahiyo haiwezekani ktk kuchinja atajwe mungu wao halafu sisi tukipokee chakula hicho,halafu mbona wao hawakubali wakristo wachinje, wakristo kuweni makini ni mnyama(666) aliyetajwa kwenye kitabu cha ufunuo, mungu wetu awape macho ya kuona vitu vya kiroho,amina

 9. Mkandya ndg yangu, jamii haijazaliwa leo, wala Ukristo na Uisilamu havijaingia hapa kwetu leo, bali tumekuwa pamoja na katika kuvumiliana kwa kipindi kirefu sana. Tena yawezekana kuwa hujui anayemvumilia mwenzie ni nani, Mkristo ndiye mwenye uvumilivu kutokana na Amani inayomtawala!

  Zamani, nikiwa katika uelewa mdogo nilidhani kwamba mtu mgomvi ni yule mwenye nguvu, na nikawa nashangazwa sana na watoto wadogo wasio na nguvu lakini ni wagomvi, nao hupigwa pigwa sana katika ugomvi wao. Lakini baadaye ndipo nilipofahamu asili ya hao kuwa wagomvi, kumbe ni INFERIORITY COMPLEX waliyonayo! Pia nilidhani watu wenye complex hii watakuwa ni wenye aibu na wapole, loh, kumbe they are very violent! Ukija katika mambo ya dini, hii dini ya Kiisilamu, kulingana na mafundisho yake, na maudhui yake yote, inazalisha waumini walio katika Complex hiyo, haijalishi ni msomi kiasi gani!!! Yaani kwa complex hiyo waliyonayo, na mafundisho yao, yamewajengea explosive nature, yaani nature yao ni cantankerous, (yearning to explode, yaani wanangojea direction tu)! Kinachowatuliza ni utulivu na busara inayotawala katika maisha ya jirani zao Wakristo, ile sophistication ya Ukristo, kule kuwa juu ya principalities nk!!!

  Kwahiyo wakristo, mkiona nanyi mnaweza kuwa na akili kama zao, yaani kutoka huko rohoni mlikoanzia, na sasa mnataka kuishia mwilini, hiyo ni hasara kubwa sana! Sasa tusemeje, Hekima akiondoka kunabaki nini? Mtaipasua jamii katika mambo mengi sana, maana bila Hekima huwezi kumtawala hata mbwa uliyemfuga! Hao maaskofu wanaotuongoza katika mafarakano, ni maaskofu wa kola nyeupe. Unajua kola nyeupe inaashiria nini? Kola nyeupe ni badala ya RM, Hekima alipoondoka walimbadili na kola nyeupe ili kuyamiliki makusanyiko!!!

  Muwe macho wapendwa, hatujifariji kwa Maandiko, bali tumeziuza roho zetu kwa hayo Maandiko! Mkijichanganya kwa ushindani mnaouingia na kunajisisha vilivyochinjwa na Waisilamu, ilihali mnajua fika kuwa mnyama huyo amechinjwa kulingana na matakwa ya kuchinja, damu imwagike chini, basi mtakuwa mmenajisisha kwa msingi gani, maana Maandiko yanasema, Law 17:13 “Mtu ye yote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga.” Kama ibada zao zinawagusa kwa matakwa yenu wenyewe, basi msiishie kwenye nyama tu, mabasi yao yoote ya abiria huwekwa wakfu, maduka yao yote pia. Hamjaviona vikaratasi vyenye maandishi mekundu vikining’inia milangoni kwa ndani? Hamjaingia katika ofisi za Wabudha na kukuta mishumaa ikichomwa katika vinyago na sadaka zikiwekwa hapo? Msururu ni mrefu saana, dunia yoote iko polluted na hayo madude.

  Basi iwapo mtajiingiza katika mashindano hayo, Mungu atawadai Hukumu ziendanazo na hayo mnayoyanajisisha ambayo aliwapa uhuru juu yake, nayi mmeamua kurudia nyuma!

  “Mbona washangaa njiani, mbona warejea nyuma, warudi tena gizani, alimokutoa Bwana, …”!!!

 10. Mkandya nakubaliana na wewe japo wengi wanaonekana kukupinga lakini ukweli unabaki pale,mfano mwingine mdogo ni pale wakristo wadai haki ya kula nguruwe katika maeneo ya mikusanyiko kama kwenye shule za boding au viuoni maana hiyo ni haki yao pia.
  Tunajaribu kuchukuliana nao lakini inaonekana sasa mambo yote ni haki yao na serekali inaona hivyo na ndo maana haya yanatokea na serekali isipoangalia kwa makini tunaweza kufika mbali.
  Wakristo tunapaswa tuseme ukweli ili waislamu pamoja na serekali watumbue kuwa tupo,tusifarijiane kwa maandiko bila kusemea kuwa tuna haki pia katika hayo wanayopinga, kuwa hatuna haki ya kuyatenda.

  Mpende Adui yako!!

  Mungu Ibariki Tanzania!

 11. Ndugu Mkandya, nashukuru kwa maelezo yako ya ziada kuhusiana na namna mgogoro ulivyoibuka, Hapo umenifungua macho, Kama kweli hivyo ndivyo ilivyokuwa sioni uhalali wa kuwapeleka hao ndugu mahakamani kwani hata katiba ya nchi haijampa mwisilam haki ya kuchinja. Binafsi nimekuwa na amani siku zote kwenda kununua kitoweo bila kuuliza kachinja nani. Ni kitu ambacho sikujaribu hata kufikiria. Wasi wasi wangu ni kuwa asije shetani akataka kutuingiza kwenye angle ambayo sio target yetu, mwisho wa siku tukajikuta katika mapambano ya kimwili ambayo sio maelekezo ya Mungu wetu. Si unamjua Mungu wetu alivyo hodari na asiye ishiwa maarifa wala mipango. Lakini bado andiko lisemalo kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni bila kuuliza uliza kwa ajili ya dhamiri linanibariki sana. Lakini pia sikubaliani na mtu anayesema kuwa yeye peke yake ndiye mwenye haki ya kuchinja.

 12. Bwana Lwembe nadhani sijayaelea maelezo yako!

  Kwa ndugu yangu Chiwango, naweza kuona jinsi ambavyo hili suala hata hujui lliivyoanza huko Mwanza. Hakuna mkristo ambaye ameenda serikalini kutaka haki ya kuchinja, ispokuwa ni pale mkristo alipoandaa sherehe fulani akachinja mwenyewe na waislamu wakakasirishwa. Ndipo mkuu wa mkoa akaenda huko kwenye tukio akatangaza kuwa wakristo wasichinje na baadhi ya wakristo wakapelekwa mahakamani kwa kuchinja.

  Nimekwambia kuwa suala la kuchinja ni la kiibada, na kama wewe utataka kuwakaribisha waislamu kwenye sherehe yako kama ulivyosema, ukaamua uwape wao wachinje ili usichinje wewe wakashindwa kula kwa vile nyama hiyo kwao itakuwa haramu, ati ukiwa na maana ya kuwaonesha upendo wa kristo, basi hujui unachokifanya.

  Amini nakwambia bwana Chiwango utakuwa umeshiriki ibada ya sanamu, maana umefanya hivyo kwa makusudi.

  Ni kweli hata mimi nikienda kwa mwislamu akachinja nakula, na huwa nafanya hivyo. Lakini kitendo cha mimi kumtafuta yeye aje anichinjie ati kwa vile mimi nikichinja ni najisi, hilo halipo.
  Anasema ni haramu kwa sababu mimi simwabudu Mungu ambaye yeye humwabudu, simwamini mtume Mohamad, kwa hiyo maana yake ni kwamba Mungu wangu( Yehova) na mwokozi wangu (Yesu kristo) si lolote mbele ya mungu na mtume wa waislamu.

  Halafu hakuna mahali nimewashauri wakristo wasile nyama iliyochinjwa na mwislamu, soma vizuri maudhui yaliyo katika maelezo yangu.

  Chiwango nani kasema kuwa tunawachukia waislamu? na je ni sawa kumwionesha upendo mtu(adui) kwa kumdharilisha Mungu wetu?

  Kama unaweza kuchukua fimbo ukamfukuza kibaka ajae nyumbani kwako, basi nataka ujue kuwa si kila kitu ni cha kupambana kwa maombi au kiroho. Kuna mengine ni ya kupambana kisheria, mengine ki mwili tu kama hilo la kibaka.

  Unauliza kama Yesu angelikuwepo duniani! ivi unadhani kuwa Yesu kazi yake ilikuwa kuamka asubuhi na kuingia mitaani kuwahubiria watu au kwenda mlimani kuomba? Kubuka kafanya kazi ya huduma full time kwa miaka mitau na nusu tu, sasa fikiria hiyo miaka mingine alikuwa anafanya nini.

  Inawezekana angekuwepo angeitaka serikali isiwazuie wakristo kuchinja. Mbona alichapa watu hekaluni? hakuwachapa kiroho bali kimwili kabisa

  Wakristo hawadai haki ya kuchinja, bali wanadai haki ya kutokuzuiwa kuchinja.

 13. mimi siwezi kushiriki ibada ya mwingine mtu mmoja ameshasema hapo juu kwa nini wa kichinja kichwa lazima kielekezwe kule wao wanaita maka sijui kibra? wanajua wao.baada ya kujua hili kuwa wao ni ibada sasa nitakuwa nachinja mwenyewe.

  ninachojiuliza nchi zilizoendelea kama ulaya nani huwa anachinja? mbona ni mashine tu mbona kule na waislamu wanakula? au mnafikiri huwa wanaitwa kwenda kuchinja? tujilindeni na chachu ya mafarisayo.

 14. Swala la kuchinja ni la KIROHO ndio maana hata Mungu akaagiza lazima mnyama achinjwe na damu imwagike ardhini.Na kama Neno linasema chakula kikipokewa kwa shukrani na kikiombewa kinatakaswa,je sala za waislamu wakati wa kuchinja haziwezi kuwa na madhara kwa wasioombea chakula au nyama iliyochinjwa na waislamu ? kwa ushauri wangu mi naona ni sawa swala hili liangaliwe ki undani kama tumezinduka katika hili la kuchinjiwa na dua tusizozifahamumaana mi ninachoamini,hata mungu asiye Mungu,huwa nae ana utendaji wakekwa waumini wake. Kwa hiyo endapo waislamu wanaamini mungu asiye Mungu wa kweli,anaweza kuwa na madhara kwa wakristo wasio na ulinzi wa Mungu.

 15. Ndugu Mkandya kaa nipo nyumbani mimi na familia yangu nachinja wala sihitaji mtu anihukumu juu ya hilo. Ninachozungumzia mimi ni ile hali ya sisi wakristo kwenda serikalini na kuanzisha mapambano juu ya haki ya kuchinja. nyumbani kwangu hata binti yangu huchinja bila ya kujali kichwa kimeelekezwa wapi. Akija mtu wa dini namkaribisha wala siileti mezana hoja ya kachinja nani labda yeye aniulize. Na akiniiuliza majibu yangu ni injili ya Kristo. Lakini kama nimeandaa karamu nyumbani kwangu na wao ni walengwa wangu katika kuwaonyesha upendo wa Mungu wangu nitamtafuta moja wao aje achinje.

 16. Ndugu Mkandya, unadhani Yesu kristo angekuwepo katika mwili duniani leo angekwenda serikalini na kudai haki ya kuchinja na kuwashauri akina Petro wasile nyama ya kuchinjwa na kundi fulani la watu ambalo linashindana naye, au angekuwa mitaani akiwahuburi watu watubu kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia. Mamlaka tunayopambana nayo hapa ni ya ibilisi katika ulimwengu wa roho uwanja wa mapambano ni katika mioyo, akili na fahamu zetu. sio masoko ya kuuzia nyama, Hatushindani na Uzinzi kwa kuwapiga mawe wazinzi hadi kufa bali kwa kutumia Roho wa kristo tunaondoa roho ya uzinzi katika mioyo, akili na fahamu zetu ili mamlaka inayotawala katika fahamu zetu iwe ni Roho wa Kristo na sio pepo la uzinzi. Unaamini kwa kuwashauri wakristo wasile nyama iliyochinjwa na mwisilamu itawafanya warithi uzima wa milele. Tuwapende adui zetu na kuwaonyesha upendo wa Mungu wetu. Ili waone tofauti kati ya Mungu wetu na mungu wao. Tukiendekeza mambo kama hayo, shetani atatufikisha mahali tukaanza kushindana juu ya viongozi wa serikali lazima wawe wa dini fulani na hatutaishia hapo mwishowe tutasema lazima wawe wa madhehebu fulani. lakini jambazi akija nyumbani kuiba nitapambana naye. Akija kuomba maji ya kunywa nitampa tena yale ya baridi na kisha nitamuhubiri habari njema za Yesu Kristo mwokozi ili aokoke na kuacha ujambazi.

 17. Hahahaha! Mkandya, unauliza, “Juu ya falme zipi na mamlaka yapi?” Je, ni kweli kuwa hujui??? Acha usanii!!!

  Haya, kwa mfano, tukiunga katika mawazo yako, tukakukubalia kuwa suala la uchinjaji, ambalo kwa Waisilamu ni la kiroho, basi kwa hilo kuwa la kiroho, nayo roho hiyo ikiwa ni ya mpinga Kristo, kushiriki kula hicho kilichotayarishwa katika ukiroho huo ni najisi! Kwa kadiri ya UNAJISI, haswa kiibada, kwa hilo Mungu huhitaji damu ya mshiriki huyo imwagike; basi ni wangapi watahitajika kumwaga damu zao leo hii, haswa tangia waliposhiriki vitoweo hivyo?! Simuoni hata wa kupona mijini!!!

  Halafu, wewe ukisema kitu fulani ni najisi, basi Mungu hukukubalia katika hilo na atakutaka ujiepushe nalo kikamilifu. Ukishindwa, kwa vile Mungu ni mwenye Haki, itamlazimu akuadhibu sawa sawa na hitaji la adhaabu ya kosa hilo, hata ikiwa ni damu yako kumwagika!!!

  Ushabiki wetu ni vizuri tuupime kwanza, Mungu hachezewi!!!

 18. Juu ya falme zipi na mamlaka yapi?

  Nini maudhui ya hilo andiko la kushindana kwetu sisi…. bwana Chiwango? kuna nini kilikuwa kinaendelea kwa waefeso mpaka wakaambiwa hivyo.

  Halaf kwani kuna mkristo kachukua bunduki au mshale kwenda kushindana na mwislam?

  Anyway, wewe kama unaona suala hili halina maana usipate shida, ukitaka kufanya sherehe nyumbani au kanisani kwako kamtafute mwislamu aje akuchinjie.

  N kwa kuwa kushindana kwetu si juu ya damu na nyama kama unavyotafsiri wewe basi akija kibaka nyumbani kwako usichukue hata fimbo kumfukuza, bali kemea tu!

 19. Iweni macho, Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. lakini kila kiuzwacho sokoni kuleni bila kuuliza uliza kachinja nani? nk, nk. Shetani asije akawatoa kwenye shbabaha na malengo aliyotuelekeza AMIRI JESHI MKUU.

 20. Mimi nikikuta mwislamu kachinja nakula bila shida wala siwezi sema ni haramu. Lakini kwa nini yeye akikuta nimechinja aseme ni haramu?

  Uharamu na uhalali unaosemwa hapa ni suala la kiroho, ni ibada hiyo.

  Kwa nini mimi nikitaka kuchinja kwa jina la Mungu wangu niambiwe kuwa nilichokichinja kimekuwa haramu, halafu yeye akichinja kwa jina la mungu wake hicho ni halali?

  Kwa nini nikitaka kuchinja mnyama wa kwangu mpaka niende nikamtafute jirani yangu mwislamu aje achinje kwa jina la mungu wake? Kama kuchinja mnyama kunahusu imani kwa Mungu,je Mungu wa mkristo ni mnyonge na wa mwislamu ndiye mwenye nguvu? Hii ni dharau.

  Ukweli siyo sawa kumwita mwislamu aje anichinjie mnyama asemeseme yale maneno yao, bisimilah…nini huko…! Halafu ili kukuonesha kuwa hiyo ni ibada, lazima mnyama atazamishwe mwelekeo fulani ndipo achinjwe.

  Kwa habari ya kuchinja buchani ni vema serikali inayosema kuwa haina dini isitake watu wa dini fulani ndio wachinje, ispokuwa kuwepo na watu ambao ni wataalamu wa mambo ya uchinjaji hao ndio wachinje, bila kuhusisha dini zao. Ili kila mtu abaki na nini dini yake inamwambia kufanya akikuta nyama ya mnyama ambye hajui kachinjwaje. Yaani dini/imani ya mtu isiwe kigezo cha uhalali wa mtu kuchinja.

  Kwa nini serikali inahusisha dini katika kuchinja wakati yenyewe ilishasema haina dini? Ati mpaka watu (wakristo) kule Mwanza wakashitakiwa kwa kuchinja mnyama kwa ajili ya matumizi ya sherehe yao wenyewe!

  Sikubali kulazimishwa kuchinjiwa na mwislamu, hiyo ni dharau!!

 21. Mimi nadhani, wakristo tumetekwa na mihadhara ya kidini, ambayo kimsingi ni akili zetu, na sasa tuko katika kuiendeleza hiyo badala ya kutuliza vichwa vyetu na kurudi katika Biblia ili tukae katika nafasi zetu! Hakuna mahali Biblia inaagiza tufanye mashindano ya kidini, tumeambiwa tukaihubiri Injili, hiyo inayoambatana na ishara na miujiza, sio kukebehiana!

  Suala la kuchinja, katika jamii yetu mchanganyiko, nafikiri ni moja ya mambo ambayo hushuhudia ukomavu wetu na uhuru tulionao katika Kristo. Tumeishi na ndugu zetu Waisilamu miaka yote, na tukiwa na mbuzi au kuku au chochote kile cha kuchinja, ili mradi tunaye jirani muisilamu, basi Upendo tuliokuwa nao siku hizo, ule wa kiUngu, ulituongoza kuwatafuta hao ili watuchinjie ili watoto wao, hao wanaocheza na wanetu wakija majumbani mwetu tushiriki nao na hata watu wazima! 1Kor 10:28-29
  “Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri. Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?”

  Kwa hiyo, Busara na Hekima ya Mungu vyapaswa kufuatwa badala ya hekima za kibinadamu ambazo ndizo zimechukua hatamu kuyaongoza makundi yetu na kuyaingiza katika mafarakano ya kijamii pasipo umuhimu huo.

  Mpende Adui yako!!!

 22. Aliye na nafasi ya kuchinja na achinje tu mm nikila kwanza nataja JINA LA YESU WAPENDWA MAANA HATA UKILA KITU CHA KUFISHA KAMA IMANI YAKI I HAI HAIDHURU

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s