Askofu Thomas Laizer Wa Dayosisi Ya Kaskazini (KKKT) Afariki Dunia

Askofu aliyedumu kwenye nafasi ya Uaskofu zaidi ya Miongo Mitatu, Askofu Thomas Laizer amefariki jioni ya leo Katika Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa wa Arusha. Askofu Thomas Laizer amefikwa na mauti hiyo baada ya kuugua na kukaa Hospitalini hapo zaidi ya mwezi Mmoja.

Askofu Laizer amefariki huku Dayosisi Ya Kaskazini ya Kanisa la KKKT ikiwa inamuhitaji pamoja na busara zake kuweza kutatua mgogoro unaolikabili Kanisa hilo kwa sasa kufuatia deni la mabilioni kadhaa.

Askofu Laizer alianza kuugua mapema mara baada ya mgogoro kuanza kushika hatamu, haijafahamika moja kwa moja kama ugonjwa wa Baba Askofu una uhusiano wa moja kwa moja na mauti iliyomfika.

Baba Askofu Laizer atakumbukwa kwa ujasiri wake  wa kuikosoa Serikali pasipo woga, lakini puia atakumbukwa sana Kipindi cha Babu Wa Loliondo na Kikombe chake Cha Tiba.

–Sam Sasali blog

Advertisements

8 thoughts on “Askofu Thomas Laizer Wa Dayosisi Ya Kaskazini (KKKT) Afariki Dunia

  1. Poleni sana wapendwa, waumini na wanandugu kwa ujumla kwa kupata msiba huo mzito. Msife moyo maana hakuna atakayebaki, sote ndio njia yetu. Tumombee ili Mungu ampokee na ampumzishe katika mkono wake wa kuume.Amen!

  2. mungu aitie nguvu familia askofu thomas laizer na ampokee mpendwa wetu,ampuzishe kwa amani sisi tulimpenda,mungu amempenda zaidi.bwana ametoa na bwana ametwaa.jina la bwana lihimidiwe.ameen

  3. Poleni sana kanisa la kkkt kwakumpoteza mtumishi mungu askofu thomas laiza, mungu awatie nguvu. AMETOA NA AMETWAA. Amina.

  4. poleni familia ya baba askofu laizer mungu awatie nguvu katika kipindi hiki.apumzike kwa amani

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s