Babu wa Loliondo atangaza watu kumiminika upya, Apata maono mengine.

millard

Millard Ayo wa Clouds FM Alipokua akifanya mahojiano na Mchungaji Ambilikile Masapila maarufu kama Babu wa Loliondo

Hivi karibuni mtangazaji maarufu Millard Ayo katika kipindi chake cha Ampifaya alifanya mahojiano na Mchungaji Ambilikile Masapila na kuelezea kwa urefu mwanzo wa huduma yake ya kikombe, changamoto, walioiga kutoa vikombe, vipingamizi pamoja na waliokufa, ambao hawakupona hawakufuata masharti ya dawa.

Mwishoni mwa mahojiano Babu wa Loliando akasema kuhusu mafuriko mapya yatakayotokea hivi karibuni huko Samunge, alizungumza hivi

Siwezi kusema moja kwa moja kwamba ni mwezi wa tatu, ingekuwa pengine mpaka sasa tungeanza kupata watu wengi, na inawezekana ikawa mwezi huo wa tatu, au kabla au baada, mimi siwezi kusema moja kwa moja kwasababu kuna vipingamizi vingi tu, ambavyo Mungu anasubiri vitimie ndipo kazi hiyo ianze, Kuna miujiza mingi imeandikwa ndani ya biblia kitabu cha Mwanzo, Zaburi, Ezekiel, Ufunuo yapo maajabu mengi ambayo Mungu ameyaandika hayakutimia katika nchi ya Israel yatatimia hapa, Samunge, kwahiyo mafuriko ya watu watakaokuja si kwa ajili ya kunywa dawa tu lakini ni kwa ajili ya mambo mbali mbali kuja kuona miujiza ya Mungu itakayofanyika

Alipoulizwa ni maajabu gani yatakayofanyika akasema

“Si vizuri, sijamwambia mtu yeyote ba hata hapa kwako sitasema, isipokuwa mimi nimeyaona mengi tu nimeyaona tayari lakini Mungu hajaniambia tangaza napewa (Maono) kila wakati linakuja hili, linakuja hili napewa kila wakati lakini si zaidi ya labda nusu mwaka sasa

Ili kulinganisha habari ndipo mtangazaji Millard Ayo alipomuuliza Mchungaji Onesmo Ndegi ni maajabu gani hayo ya kwenye biblia

Mchungaji akasema “Hakuna muujiza ambao haujatendeka zaidi ya ule muujiza wa unyakuo, miujiza mingine yote iliyotabiliwa ilishatendeka kwa mfano ukisoma muujiza mkubwa sana ambao Mungu aliuzungumza kutoka Mwanzo 3:15 biblia inasema hivi nami nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake huo utakuponda kichwa na wewe utauponda kisigino, sasa hapa alikuwa anazungumzia juu ya ujio wa Kristo na ushindi wa Kristo dhidi ya nguvu za giza au shetani na ilishatokea na tunaishi katika kipindi hicho, Yesu Kristo alishakuja akazaliwa, na uwezo wake ukadhibitika ushindi dhidi ya shetani ulionekana pale msalabani, kwa hiyo hakuna muujiza mwingine ambao utasema kuanzia mwanzo haujatimia sasa kuna mtu anataka kuutimiliza, hakuna muujiza wa namna hiyo

Babu wa Loliondo alipoulizwa tena ana ushauri gani kwa Serikali juu ya maajabu  hayo makubwa yatakayotokea hivi karibuni akajibu

Nilitaka kusema kwa upande wa Serikali, nitasema ya kwamba Serikali iwe makini kupokea watu watakaokuja maana ni wengi, ni mafuriko kwa hiyo wawe makini”

Hata hivyo babu amewasamehe watu wote waliomsema vibaya “Kisasi ni kwa Bwana” alisema

–Millard Ayo

Advertisements

16 thoughts on “Babu wa Loliondo atangaza watu kumiminika upya, Apata maono mengine.

 1. MAONO YA BABU SIO MAONO YA MUNGU WA KWELI! KAMA NI YA MUNGU WA KWELI NA AYASEME BASI TUYAJUE. NA KWAKUWA SIYO MAONO YA MUNGU WA KWELI HAYAWEZI YAKAFANIKIWA TENA NDANI YA TAIFA HILI KWAKUWA SASAHIVI TAIFA HILI LIMECHAGULIWA NA MUNGU MWENYEWE KWA AJILI YA KUTIMIZA MAONO YA MUNGU WA ELIYA. KWAKUWA NABII WA KWELI AMEINULIWA NDANI YA TAIFA HILI ILI KUSIMAMISHA MAKUSUDI YA MUNGU WA KWELI, HIVYO BASI HAKUTAKUWA NA maono yoyote ya nabii wa uongo yatakayosimamandani ya Taifa hili. Babu mwenyewe amesema HAJUI itakuwa lini. Mungu akikupa MAONO LAZIMA AKUPE RAMANI INAYOKUONYESHA MAHALI ULIPOTOKA, ULIPO NA UNAKOKWENDA. AACHE FIX BWANA! ALETE NENO sio MANENO! Kutokana na mambo ya kikombe tulipata kujua kuwa Dini yake ya KKKT kumbe maana yake ni KUNYWA KIKOMBE KIMOJA TU! ASIKIAYE NA AFAHAMU! SHIKA NENO!

 2. Bwana yesu apewe sifa!
  Sina hamu na huyu babu loh!! mwogopeni tena usitekwe na maono yake!! Jamani wakristo tuombe sana tusipeperushwe,watu walishatubu kwa kwenda Loliondo,
  sasa anarudi tena!!! wewe babu inabidi uombe karama ya kufasiri roho utajua hiyo roho imetoka wapi!!Eti waliokufa walikosea masharti!!! Masharti ya mungu ukitenda dhambi unakufa,walikufa kwa vile walitenda dhambi ya kuacha kuamini neno na kukimbilia kikombe ,Jamani watanzania msiende mtakufa na kwenda jehenamu

  mbarikiwe sana!!

 3. ukitaka kujua ukwel halisia wa jambo uwe tayar kuchukua gharama ya kufanya utafiti juu ya jambo hilo kulikoni kuwa mwepesi kusema.

 4. sasa jamani huo maono mbona hayapo katika msingi la neno la uzima, tangu ki ni kikombe cha dawa kuwa inaleta matibabu kumbukeni neno ,la MUNGU la sma hivi” BWANA asema hivi, amelaaniwa mt yule amtgmeaye mwanadamu , Amfanyae mwanadamu bkuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. YEREMIA 17:5

 5. Shusha cup nyingine baaabu watu waje kugonga na wengine wanufaike na usafirishaji.

 6. jamani wapendwa tuwe macho, tusipende sana mambo ya mkato mkato, twende wenyewe magotini mana Mungu huwasikia wote wamuitao, sasa haya mambo ya vikombe sijui nini mmmh kwa kweli Mungu aingilie kati na aonyeshe ukweli uko wapi

 7. Bwana Yesu apewe sifa!
  Ndg. Alferd ninakuunga mkono kwa sababu siku hizi watu wanatumia neno la Mungu kuwaibia watu. Ukweli hakuna aliyesikika anatoa ushuhuda wa kupona kwa kikombe cha babu. Hata Serikali nayo kupitia Wizara ya Afya waliahidi kufanya utafitit ili kubaini ukweli wa dawa ya babu lakini mpaka leo hakuna majibu sahihi yaliyotolewa. Wapendwa tusome na kuyashika maneno ya Mungu maana mwisho umekaribia (Ufu.1:3). Pia tumuombe Mungu ili atupe macho na akili za rohoni.

 8. Hao watu wawili wameniacha hoi. anayehojiwa ana sura ya kukasirika na anayehoji anatabasamu lenye matumaini. kila la heri.

 9. niliwahi kuutofautiana na wakristo wenzangu kipindi babu alipotangaza uponyaji wa kikombe na wengi waliniona kama adui lakini mwisho wa siku walikubaliana na mimi! binafsi siamini ufunuo wa babu na nilitofautiana hata na uhamasishaji uliokuwa unafanywa na Askofu ambaye sasa ni marehemu askofu dk Laizer(rip). ni nani hapa ktk sg anayeweza kutuletea ushuhuda wa mtu aliyekunywa kukombe cha babu akapona ukimwi au kansa n.k? (uponyaji au muujiza wa Mungu unadumu na si wa muda).binafsi nimeshuhudia watu waliokwenda kunywa kikombe hasa wagonjwa wa kisukari baada ya kuacha kutumia dawa kwa imani kuwa wamepona walikufa na wale walioathirika na ukimwi walipoacha kutumia dawa za kurefusha maisha afya zao zilitetereka na mwisho wa siku walirudia dawa zao! lakini wamemuacha babu na utajiri mkubwa mno ambao hata wakati mirladi anamuhoji thamani ya gari tatu anazomiliki ni kiasi gani hakutaka kutaja na mtu mmoja anehusika na biashara ya magari alipoulizwa thamani ya haraka ya magari anayomiliki babu alisema ni 120milioni! kitu gani ambacho ninataka kusema hapa? ni kwamba ,kwa sababu watu wanataka kusikia yale amabayo wanataka kusikia na kwa sababu watu wanataka kufanyiwa yale ambayo wnataka wafanyiwe, kumeibuka watumishi wajanja sana (werevu) amabao wanajua kucheza na akili za watu kama wanasiasa wanavyojua kucheza na akili za watu. angalia lengo la watu hawa ni nini? pesa!!! na kwa sasa ni matajiri wakubwa sana sana wanamiliki magari na majumba ya kifahari huku waumini wao wakiwa masikini wa kutupwa! watu wanataka kuishi kimiujiza-ujiza,watu wameacha msingi wa neno la MUNGU kujenga imani zao kwenye miujiza! watu wanataka maisha rahisi ambayo kwa kutumia shida walizonazo wajanja wachache kwa kutumia akili wametokea hapo! yesu alisema mkikaa katika NENO LANGU mtaifahamu KWELI na hiyo KWELI itawaweka HURU!! NJOO NA MAONO YAKO YOOTE HATA UKIAGIZA MOTO USHUKE KUTOKA JUU HATA UKIIFANYA SANAMU IWE NA UHAI TUTAYAPIMA MAONO HAYO NA KAMA HAYAENDANI NA NENO LA MUNGU NA KAMA YAMEFICHA SIRI NYUMA YAKE TUTASEMA! WAJINGA NDIO WALIWAO ENDELEA KUMUWEKA YESU PEMBENI NA UFUATE MAONO HALAFU UTAONA MWISHO WAKE!!

 10. Afadhali asiyaseme maono yake watamuibia. Kama walivyoiga wengine wakati akitoa kikombe, alipopotea babu na wao wakapotea. Tunasubiri mafuriko tukamiminike Loliondo

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s