Mapigano yameibuka kati ya Wakristo na Waislamu Geita, chanzo uchinjaji wa mifugo

mifugo

Mapigano yameibuka na yanaendelea kati ya Wakristo na Waislamu katika mji Mdogo wa Buselesele wilayani Chato Mkoani Geita wakigombania kuchinja. Mapigano yametokea baada ya Wachungaji wa AIC kutenga eneo la Buselesele kwa ajili ya machinjio ya Wakristo, hali hii imesababisha maeneo ya Katoro na jirani kutokea vurugu.

Zaidi ya watu 15 na mchungaji wa kanisa la PAGT Mathayo Kachira(45) inadaiwa ameuawa kutokana na mapigano hayo,Mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Endelea kuomba kwa ajili ya watu hawa.

Advertisements

24 thoughts on “Mapigano yameibuka kati ya Wakristo na Waislamu Geita, chanzo uchinjaji wa mifugo

 1. Labda Milinga ili upate jibu la waislamu wanatoa sadaka kwa sanamu ipi, tuambie kwanza kama waislamu wanamwabudu Mungu huyu Jehova tunayemwabudu. Ukishajua wanamwabudu Jehova au la tayari utakuwa umepata jibu la swali lako.

  Halafu hakuna mkristo ambaye amekuwa akiuliza kama mnyama amechinjwa na mwislamu au la .Ispokuwa binafsi nimesema sana kuwa ishu katika swala hili ni wakristo kulazimishwa kuchinjiwa na waislamu,kana kwamba wao wakichinja ni dhambi kwa Mungu.

  Wewe si mwislamu wa kuwasemea mambo yao ndg. Milinga. Wao wanasema kuwa kwao kuchinja ni ibada halafu wewe unasema kuwa siyo kweli bali ni manaeno tu. Ni vema tu ukajipambanua kuwa ungependa waislamu waendelee kuwanyanyasa wakristo kwa kuwachinjia wanyama kwa jina la kulinda kinachosemwa kuwa ni amani ya nchi.

  Lakini kaa ukijua kuwa ”motive” ya waislamu iko zaidi ya kuchinja wanayama. Elewa wamaechakachua mpaka biblia,wakaamua kuingiza biblia ambazo zimebadilishwa baadhi ya maneno. Hayo yote ni kwa ajili ya kutekeleza kampeni iliyopo ya kufanya nchi hii kuwa ya kiislamu.

  Halafu unaposema mtu akikutonya kuwa nyama hii iko hivi na vile ndipo uache kula, utakuwa unamiss maana. Kinachomaanishwa hapo ni kupata taarifa. Ni kupata taarifa inaweza kuwa kwa kuambiwa au kwa kuona mwenyewe. The issue ni ukishajua bila kujali umejuaje,tayari kitu hicho kinakuwa na shida kwenye nafsi.

  Ni vema kuchambua haya mambo katika namna ya kuwafanya watu wajua zaidi ya kinachoonekana nje. Napenda wakristo wajue kuwa kinachoendelea chini ya kapeti katika mikakati ya waislamu si cha kusubiri kuona matokeo yake, itakuwa too late!

  Pamoja na kwamba si sawa sisi kulazimishwa kuchinjiwa na waislamu, lna hata wao wanajua hivyo, na hata kitabu chao kinawaambia hivyo, lakini wana lazimisha hili suala kama hatua mojawapo ya kuelekea mahala fulani ambako si vema tukawaruhusu waende maadam katiba ya nchi hii inaturuhusu kutowaruhusu waende huko.

  Ndg. Milinga sihitaji kuzozana na wewe katika hili suala kwa kuoneshana ujuzi wa kujua maandiko na kujenga hoja,nafikiri kila mkristo mwenye Roho mt. ndani yake sasa anaweza kuelewa nia ya waislamu ni nini.

  Wewe kama unaona ni vema wakristo kulazimishwa kuchinjiwa na waislamu basi endelea kuwatetea waislamu. Jambo kwenye mchango wako fulani ulisema huwatetei, ila kwa maandishi yako iko wazi kabisa unawalaumu wakristo wanaopinga hili pasipo hata wewe mwenyewe kusema nini sasa kifanyike.

  Nakushauri ufanye utafiti na ufuatiliaji wa kilicho nyuma ya pazia la mikakati ya waislamu.

  Nimetosha, ubarikiwa!

 2. Bwana apewe sifa, Amani iwe nanyi. Mimi ningependa kujua au kupata maoni yenu juu ya swala hili la KUCHINJA. Maana huku kanda ya ziwa limekua gumzo mapaka limefikia hatua kutoa uhai wa mtumishi wa Mungu(mchungaji), na serikali haioneshi kujishughulisha na jambo hii, wakati ni NIHAKIYETU wakristo.

 3. Mpendwa Mkandya, Huyo Mungu wa waislam ni yupi? Jina lake unalijua? Ni nani basi?
  Kama waislam wanachinja nyama kwa ajili ya kutoa kafara kwa sanamu alizokuwa anazungumzia Paulo naomba uniambie waislam wanatoa sadaka kwa sanamu ipi?

  Mimi nadhani hapa maandiko hata wewe hujayaelewa kama unavyosema kwamba mimi sikuyaelewa. Inaonesha wote hatujayaelewa yanamaana gani.

  Hata hivyo, Nami tena naomba turudie huo mstari wa 28 wa barua ya Paulo kwa Wakorintho kama ulivyonukuu kwa kimombo, “28. But if any man say unto you, This is offered in sacrifice unto idols, eat not for his sake that shewed it, and for conscience sake……”

  Hivi wewe Mkandya ukiyasoma maandiko hayo unaelewaje? Je, unaelewa kwamba wakristo wanaashwa kutokula nyama iliyochinjwa na mwislam kwa kuwa yeye kuchinja ni Ibada? Bila shaka wewe umewahi kuwasikia waganga wa jadi wanaotibu mtu baada ya mtu huyo kutoa sadaka ya kuku mweusi au mweupe au baada ya kutoa sadaka ya mbuzi au ngombe mwenye rangi moja tu.

  Kumbuka anayechinja hatoi sadaka bali aliyetoa mnyama achinjwe ndiye anayekuwa ametoa kafara. Hapa tunazungumzia mtu mmoja kutoa sadaka ya kafara na mwingine kuchinja kwa niaba yake kutoa kafara hiyo.

  Waislam wanapochinja kabla ya kumkata shingo mnyama hutamka neno kama hili, “Bisumillah” huku wakimtazamisha mnyama anayechinjwa kuelekea makka au kibra. Neno hilo linapotamkwa lina maana ya ” Kwa jina la mwenyezi Mungu” basi wanaanza kukata.

  Waislam wasemapo kuchinja ni ibada siyo kweli bali ni maneno tu wayatumiayo kama ghiliba fulani ili waendelee kuchinja na wasinyimwe tenda hiyo. Kumbuka wanapochinja wanapewa pesa, filigisi, maini, utumbo, nk. kwao siyo ibada bali ni uchumi tu wasije wakakudanganya. Uliwahi kuona Ibada inayofanyikia machinjioni tena bila kuvua viatu? Ibada gani ya mwislam inayofanyika bila kusujidu, kuvua viatu, kutawadha, nk?

  Kwa hiyo kama wewe unakataa kula nyama iliyochinjwa (siyo kutolewa sadaka) na mwislam kwa sababu ametamka kwamba yeye kuchinja ni ibada, wewe bado ni mchanga sana wa Imani hii.

  Ukiona mkristo anayekataa kula vyakula fulani kwa hoja yoyote ya imani yake katika ukristo, huyo ni mchanga wa Imani sana. Bado anahitaji kulishwa au kunyweshwa maziwa kwani hajakua bado.

  Wapendwa wote wanaokomaa na mada hiyo ya kutokula ngombe aliyechinjwa na waislam mimi nawahesabu kama wakristo ambao hawajakua. Na hapa siyo mimi tu, hata Paulo Mt. aliwahesabu hivyo.

  Wakristo tunapaswa kutofautisha kati ya kuchinja mnyama kwa ajili ya kitoweo na kuchinja mnyama kwa ajili ya sadaka kwa sanamu au miungu. Paulo anaposema (1 Kor 10;28), ‘kama mtu akikutonya wakati mnataka kula akasema kwamba hii nyama ambayo iko mbele yetu tunayotaka kula imetolewa sadaka kwa ajili ya miungu, basi wewe usiile kwa sababu ya kulinda dhamira ya mtoa habari lakini siyo kwa sababu Mungu hapendi akimaanisha kwamba kama angekaa kimywa kabisa ukala chakula hicho mpaka mwisho hakuna dhambi yoyote ambayo ungekuwa umetenda”.

  Uhalisia ulivyo Tanzania ni kwamba, ukienda kwa mama Lishe au Baba Lishe ukaagiza Wali wa nyama au Ugali nyama kuku hakuna mpendwa yeyote anayeuliza uliza kuhusu nani amechinja nyama hiyo. Mara nyingi tunaagiza chakula hicho na kuanza kula baada ya sala ya kutakasa chakula hicho. Kama utakutana na Mpendwa anayehoji mwenye Hotel au Mgahawa akitaka ajue aliyechinja ninani kabla hajala nyama hiyo, huyo mpendwa siyo wa kawaida.

  KAMA LEO HII WAPENDWA TUTAANZA KUULIZA WENYE HOTELI NA MIGAHAWA WATUTAJIE ALIYECHINJA KABLA HATUJALA CHAKULA HICHO NDIPO TUENDELEE KULA, BASI UKRISTO WETU NI SIFURI KABISA.

 4. Ndugu Milinga ambaye mara nyingi hukuona mchambuzi mzuri wa mambo, nashangaa sana kuona unachukua mstari mmoja kwenye badala ya kuangalia maudhui yote yaliyo katika sura husika.

  Hapa unataka kudanganya wana wa Mungu. Nami nasisitiza kuwa si sawa kula kilichotolewa kafara huku ukifahamu kuwa kimetolewa kafara. Laki haitakiwi kuuliza uliza kama kimetolewa kafara.Na kumbuka mitume wote walipokaa walisema tuwakataze(mataifa waliookoka) kula nyama zilizosongolewa na damu

  Baada ya kusema hivyo naomba usome hii mistari sasa ili upate maudhui kamili ya nini Paul alikuwa anasema: Ingawa imeikopi,alakini au hukuisoma yote au uliisoma halafu hukuielewa, na nisingetegemea Milinga usiielewi hii mistari kiasi hicho

  ”I Cor 10: 25. Whatsoever is sold in the shambles, that eat, asking no question for conscience sake:
  26. For the earth is the Lord’s, and the fulness thereof.
  27. If any of them that believe not bid you to a feast, and ye be disposed to go; whatsoever is set before you, eat, asking no question for conscience sake.
  28. But if any man say unto you, This is offered in sacrifice unto idols, eat not for his sake that shewed it, and for conscience sake: for the earth is the Lord’s, and the fulness thereof:

  Kwenye mstari wa 28 anapodema mtu akikwambia kuwa kimetolewa kafara,ina maana ileleile kwammba hata ikijua bila kuambiwa kuwa kimetolewa kafara hautakiwi kukishiriki.

  Bila shaka haya maandiko yako wazi kuwa hautakiwi kula ukishajua kuwa kimetolewa kafara, halafu Milinga unasema nisome maandiko kwanza kabla sijaanza mjadala. Nafikiri tatizo si kuyasoma , bali ni kuyaelewa yanasema nini!

  Waislamu wao wenyewe wanasema kuwa kwao kuchinja ni sehemu ya ibada, na unajua ibada huwa ni kwa Mungu, na Mungu ni mmoja Jehova. Ambapo wao hawamwabudu huyo. Sasa hiyo ibada yao ya kuchinja ni kwa Mungu yupi?

 5. WAPENDWA

  Tuachane na Ushabiki.

  Naomba wapendwa mnieleze ni maandiko gani Viongozi wa makanisa ya Kikristo Mwanza wametumia kuzuia waumini wasile nyama iliyochinjwa na waislam?

  Kama kuna mtu anayajua maandiko hayo yaliyotumiwa kama kigezo cha kuweka mgomo wa kula nyama ya ng’ombe iliyochinjwa na waislam naomba anipe orodha ya maandiko hayo.

  Ieleweke kwamba siko hapa kuitetea dini ya kiislam hata mimi siungi mkono serikali kuwapa kifua waislam wachinje nyama peke yao eti ndipo nyama hiyo iwe halali kwa watu wote.

  Hoja yangu hapa ni kwamba siungi mkono maaskofu waliokataza waumini wao kwamba wasile nyama iliyochinjwa na waislam kwa hoja kwamba inakuwa siyo nyama halali kwa mkristo kuila.

  Maandiko yako wapi yanayowapa msimamo huo au ni ushabiki wa kidini na wivu wa kidini? Kama siyo WIVU kwa waislam kwamba serikali inawapendelea ni hoja gani ya maandiko?

  Naomba majibu kwa wasomaji.

 6. Mtumishi wa Bwana, Mkandya,

  Ni matumaini yangu kwamba maelezo uliyoyatoa ukirejea maelezo ya CK Lwembe nami sina budi kukusaidia angalau kidogo kwani naona kama mada hujailewa vyema.

  Kwenye maelezo yako ya mwisho umejaribu kummuliza Lwembe hivi, nanukuu, “Lakin pia Lwembe ni wapi biblia imeturuhusu kula vitu vilivyotolewa kafara huku tukijua kuwa vimetolewa kafara? Kwa hiyo basi hata kibudu kula ni sawa kama nitaamua tu kukiona kuwa si najisi!”

  Inaonesha wewe maandiko yote yahusuyo vyakula hujayasoma. Na kama umeyasoma hukuyaelewa sawa sawa. LWEMBE amejaribu kufafanua vyema kabisa. Hebu rejea maandiko yote aliyoyanukuu ikiwezekana chukua Biblia uyasome kwa kutafari kwa undani.

  Ufafanuzi wa Lwembe ameutoa aliponukuu Maandiko ya Mt. Paulo kwa Warumi. Naomba nimunukuu tena, “Rum 14:14 “Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.” Mnaiona hii hatari ya kunajisisha vitu? Msilivuke Neno la Mungu, nawasihi!” mwisho wa nukuu.

  Lakini kwa kukazia zaidi chukua Biblia usome 1Kor 10:23-30. Maandiko yanasema kwamba hata kama chakula kimetolewa kafara wewe kula kwani chakula hakiwezi kukutia wewe unajisi labda ujinasi wewe mwenyewe kwa mawazo na fikra chafu.

  Mkandya soma maandiko kwanza kabla ya kuanza mjadala huu.

 7. finally people have justifications…nakubali kuwa tumezoea kuchinjiwa na waislam.na hii ni kutokana tu na kutokufahamu maandiko.kumbe sio lazima wala si dhambi kwa mkristo kuchinja…hakuna najisi

  asante CK na wachangiaji wengine

  waislamu wanaabudu wasichojua

 8. Mr. Lwembe wewe unapokuwa na mambo yamekusonga huwa unawatafuta manabii wa kanisanai kwenu ili wamuulize Mungu kwa habari ya hayo yanayokusonga?

  Tofauti ya huduma ya nabii kwa agano la kale na la sasa ni nini? maana agano la kale Roho mt. alikuwa anakaa kwa manabii na makuhani tu, ndio maana mtu yeyote hata mfalme akitaka jambo alitakiwa kumtafuta nabii. Lakini katika agano jipya Roho mt. yuko juu ya kila mwamini, kwa hiyo ulazima wa kumtafuta nabii ili aje aniulizie kwa Mungu linakuwa si la lazima, maana yeye atauliza kwa huyo huyo ambaye mimi pia naweza kumwuliza.

  Hata wewe naona katika kulitolea majibu swala hili unatumia tu logic za kawaida kuliko hekima ya Roho mt. kama unavyotaka wengine wafanye.

  Ulitakiwa kujua tu kuwa waislamu wanachotaka hasa si kuchinja wanyama, na wala wakristo hawajakiuka wala kuvunja sheria yoyote ya nchi wala ya dini ya waislamu,na wala hawana ugonvi na waislamu katika suala hilo. Mwenye mamlka na hilo ni serikali na imeshakiri kuwa katiba haijamwasaini mtu yoyote kuchinja, ispokuwa ni mazoea. Na una uhakika gani kuwa hatua waliyochukua wakriso si hatua ambayo imeongozwa na Roho mt. au kwa kuwa imesababisha mauaji ya mchungaji?

  Si kweli kwamba wakristo kazi yetu ni kumwomba tu Mungu kila tunapofanyiwa jambo fulani. Yako mambo ambayo ni ya kuomba, lakini mengine ni ya kushugulikia kwa mujibu wa sheria za nchi zilizopo. Paul kuna wakati alikwepa mapigo kwa kucheza tu na sheria,kuna mahali alisema yeye ni myahudi na kuna mahali tena alisema yeye ni mrumi akiwa anajua kuwa akiwaambia kuwa ni mrumi kuna sheria katika sheria za nchi inawabana wasimwadhibu kwa kuwa ni mrumi.

  Kama haujui ajenda ya waislamu nyuma ya pazia unaweza kuona hili swala kama vile wakristo wamekosa hekima ya kulikabili. Lakini tukae tukijua kuwa leo wanang’ang’aniza kuchinja kesho watang’ang’aniza wanawake wote wavae hijabu au ndoa zote zifungwe kiislamu. Kwani Zanzibar kuna haki gani wamenyimwa mpaka wawaue wakristo?

  Hata hivyo wewe pia ni sehemu ya kanisa na una Roho mt. kwa nini usichukue hatua ya kutafuta suluhisho ya hili suala badala ya kuendelea kulalamika na kuwalaumu watumishi wa Mungu wanaolishughulikia, ambao unasema au hawana Roho mt. ama wanatumia hekima ya dunia hii? Maana Mungu hahitaji watu wengi ili kufanya kitu.

  Lakin pia Lwembe ni wapi biblia imeturuhusu kula vitu vilivyotolewa kafara huku tukijua kuwa vimetolewa kafara? Kwa hiyo basi hata kibudu kula ni sawa kama nitaamua tu kukiona kuwa si najisi!

 9. Zab 91:11 “Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.”

  Amani aliyopewa mkristo, ni Roho Mtakatifu! Mkristo awapo chini ya uongozi wa RM huzishinda hali zote. Hata ikiwa ni mikasa kama hiyo anayoisimulia ndg Mkandya, mwisho wake huwa ni salama iliyojaa Utukufu kwa Mungu, maana ndiye mwenye kutuongoza katika njia zetu katika kukabiliana na changamoto zote!

  LOGIC ni akili au hekima ya kidunia ambayo huingoza dunia katika maamuzi yake katika jinsi ya kukabiliana na changamoto iliyo mbele yao. Pia RM anapokosekana, LOGIC huijaza nafasi hiyo kwa kuichanganya hekima ya dunia na Neno la Mungu, hata huonekana ni Hekima itokayo kwa Mungu, hii ndiyo hatari zaidi!

  Basi katika kanisa, Mungu ameweka Huduma Tano humo, in any local church, ili kuliongoza kusanyiko na kuwakamilisha watakatifu wake. Humo kuna Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu. Hizo ndizo sifa zinazoambatana na kusanyiko la Mungu. Hiyo ndiyo kazi ya RM katika kuliongoza kanisa.

  Hata yanapokuja maswala kama haya ya kuchinja, kanisa lilipaswa kuwaita manabii wake katika hayo makusanyiko yao ili wamuulize Mungu kuhusu jambo hilo. Halafu wasubiri mwongozo.

  Lakini naona wamejipenyeza watu wasiostahili huduma nao wanayaongoza makusanyiko yetu hata ningewaza kwamba hao viongozi wamemtaarifu tu Mungu kwa uwazi kabisa, kwamba, “””Bwana sisi twafahamu fika kuwa umeagiza ktk Law 17:13 “Mtu ye yote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga.” Jambo hili la msingi tunajua kuwa linatimizwa na jirani zetu Waisilamu; na pia tunafahamu kuwa umetupa uhuru wa kula chochote hata kikiwa kimetolewa kafara, kwa Neno lako kafara hizo hutakasika katika Mamlaka uliyotukabidhi, kama mtumishi wako Paulo uliyemtuma kwetu watu wa Mataifa alivyotufundisha. Bali juu ya uelewa huu, tunautia NAJISI uchinjaji wa jirani zetu Waisilamu, tukijtenga nao, na kuanzia leo hii, mnyama au ndege yeyote aliyechinjwa na hao, nyama yake itaambatana na mapepo, na uchawi wa alubadili na majini na vibwengo na nuksi za kupata mali na laana zoote! Hayo yote na yawe juu yetu tutakaoshiriki chakula hicho”””
  Rum 14:14 “Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.” Mnaiona hii hatari ya kunajisisha vitu? Msilivuke Neno la Mungu, nawasihi!

  Ni wakati wa kuyachunguza makusanyiko yetu ili kuona yamejengwa juu ya msingi gani. Maana kanisa limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Sasa iweje tukio kama hili liwapate watoto wa Mungu bila tahadhari yoyote? Hawa manabii wanaotuitia utajiri, wakitusisitizia kuongea na Mungu na kupewa neno la unabii juu yetu, wako wapi? Au unabii wao ni wa posho tu? Kusanyiko lolote ambalo halina vipawa hivyo vitano vya msingi halifai kuitwa kanisa!!!

  Milinga nimekuona! Orbi uko wapi, unawaona manabii wako!!!

 10. Bwana Milinga asante kwa wako mchango. Je ni halali mkristo kulazimishwa kumtafuta mwislamu ili aje amchijie?

  Unasemaje, kwamba waislamu wanaabudu mungu wasiyemjua, je ni Mungu gani huyo, Jehova?

 11. Wapendwa,

  Mimi nimekuwa nikishangaa sana watumishi wa Mungu wanaokomaa kuhusu uchinjaji wa ng’ombe na mbuzi.

  Migogoro yote imejikita kwenye ng’ombe na mbuzi ila kwenye kitimoto na kuku au bata hakuna mgogoro.

  Kwanza ieleweke kwamba hakuna Sheria yoyote Tanzania inayohalalisha kundi moja la kidini kuwa na uhalali wa kisiasa, kijamii au kiimani kuchinja ng’ombe na mbuzi. Si waislam wala wakristo.

  Hata waislam wanaojifanya kuwa na uhalali huo usiolindwa na sheria za nchi wala Quraan yao tukufu hawana uhalali wowote wa kudai kuwa kuchinja ni haki yao na hivyo wakristo wasiipokonye haki hiyo. Huu nao ni ujinga wa maandiko na sheria.

  Ajitokeze Mwislam hadharan atuleteee maandiko ya Quran yanayosema kwamba Mwenyezi Mungu amewahalalishia kuchinja ng’ombe na mbuzi tu na hivyo makundi au watu wengine wao ndipo waweze kula na kwamba mtu yeyote alaye nyama ya ng’ombe isiyochinjwa na Mwislam kwamba amelaaniwa. Hakuna maandiko hayo hata kidogo kwenye Quran.

  Tukirudi kwa Wakrsito na Maaskofu wao, watuambie maandiko kwenye Biblia yanayokataza wakristo kula nyama iliyochinjwa na waislam au watu wa Imaani nyingine.

  Nimesoma Maandiko sijaona ni wapi Yesu au mitume wake walipowakataza wafuasi wao kutokula nyama iliyochinjwa na watu wasiokuwa wakristo. HAKUNA ANDIKO HATA MOJA.

  Ukisoma maandiko mengi yanasema kwamba tule chochote kilichopo sokoni au kwa mtu yeyote tunayemtembelea bila kuuliza-uliza. Sisi wakrsito hatujazuiliwa kula nyama yoyote hata kama imetolewa sadaka kwa sanamu, ila kama unaona kwamba ukiila nyama hiyo utamkwaza mwenyeji wako aliyekualika nyumbani kwake na akakwambia kwamba chakula hicho anachokupa mezani kilitolewa sadaka kwa sanamu ndipo uache kula kwa sababu ya dhamiri yake aliyekualika na wala siyo kwa sababu ya dhamiri yako. Mtume Paulo anasema kuleni vitu vyote viwekwavyo mbele yenu bila kuuliza-uliza kwa maana dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo (1 Kor 10:23-30). Ni Askofu gani leo anayemzidi Mtume Paulo aliyesema hayo na akawaruhusu watu kula kila kitu lakini leo Askofu anawazuia waumini? Wewe umepata wapi mamlaka hayo?

  Ukitaka kuelewa kwamba walikosea sana Maaskofu waliotoa tamko la kuzuia waumini wao wasile nyama iliyochinjwa na Waislam; soma maandiko yote yahusuyo kuchinja au kula nyama. Hakuna hata andiko moja limekataza watu wasile nyama au wasiruhusu watu wa imani nyingine hata kama Imani zao hazikubaliani na misingi ya Ukristo. Hakuna maandiko yanayowapa kiburi zaidi ya ushabiki wa kidini na labda kisiasa au kiuchumi.

  Ukisoma Rumi 14:1-23, na 1Kor.1-8. ndo utaona kwamba Mt. Paulo hajakataza waumini wasile nyama iliyochinjwa kwa kutamka maneno ya kiarabu au kijerumani au kifaransa. Waislam wanapochinja hawatambikii mizimu wala sanamu. Na hataka kama wangekuwa wanafanya hivyo, bado maandiko hayajazuia wakristo kwamba wasile nyama hiyo kwani ikumbuke kwamba Waislam hawaabudu sanam bali wanaabudu Mungu wasiyemjua tu na hilo bado halituzuii kuishi nao kwa amani hata kula nao, kusoma nao, kuishi nao, kuwapenda na kula nyama ya ng’ombe waliyochinja wao.

  Nahitimisha kwa kusema kwamba:

  KULA NYAMA YA NG’OMBE ILIYOCHINJWA NA MUISLAM SIYO DHAMBI BALI KUTOKULA NYAMA KWA VISINGIZIO VYA IMANI YAKO HIYO NDIYO DHAMBI.

 12. Kama kulivyo na hejima ya Mungu na hejima ya dunia, ndivyo kulivyo na mantiki ya ki-Mungu na matiki ya kidunia.

  Mungu aliposikiliza hekima ya Musa kuhusu kuwaangamiza waisrael wote jangwani na kumfanya Musa kuwa taifa kubwa aliona kuna mantiki ndani yake akaamua kukubaliana naye (Musa).

  Tunkuh kuna logic ya msingi sana umeionesha katika mchango wako, na mimi nakubaliana na wewe kabisaa. Na umenifurahisha kuwa kama wanaona wakristo kuchinja ni kuwadhulumu haki yao basi waanze kutuchinjia na nguruwe.

  Ni amani ipi hasa ambayo mnadhani kuwa tuko nayo katika nchi hii? Amani tunayosema inapelekwa sokoni ni ipi, na tuliachiwa na Bwana yupi?

  Yesu hakutuachia amani ya dunia hii ambayo tafsiri yake ni ile hali ya kutokuwepo vita na vurugu. Haujasoma alivyonena juu ya amani aliyotuachia ; Amani yangu nawapa, niwapavyo mimi si kama ulimwengu utoavyo. Paul alipochapwa viboko na kutupwa gerezani moyoni mwake alikuwa amejaa hiyo amani ya kristo ndio maana aliimba nyimbo

  Maana ya amani si kutokuwepo vita au machafuko. Maana ya ukristo si kuwa wanyonge kwamba mtu anakuja anavunja mahali penu pa kusalia halafu nyinyi mnamwambia ubarikiwe kisha mnaanza kuchangishana ili kujenga tena.

  Ni haki gani hasa ambayo waislamu tumewanyang’anya wanayotaka tuwape?

  In fact kula nyama ambayo amechinja mwislamu kwa makusudi kabisa kwamba yeye ndiye mwenye haki ya kuchinja huyo mnyama ni kula nyama haramu. Ni haramu kwa sababu amefanyiwa ibada kwa miungu. Mungu wa waislamu si Jehova aliye hai, na wao kuchinja ni ibada.

  Katika mambo ya imani kitu kikishawekewa masharti kwamba lazima kifanyike kwa namna fulni tu ndipo kiwe halali, unatakiwa uwe makini sana. Uchinjaji wa islamu ni ibada ya sanamu.

  Hatuwezi kulazimishwa kufanya mambo kwa mfumo wa imani ambayo ki msingi ni imani ya kishetani.

 13. Ukiingiza LOGIC katika maswala ya imani, mwisho wake huwa kama huu! inasikitisha saaana, lakini masikitiko hayasaidii, wala ukiwa! Tuliachiwa AMANI ya BWANA, iko wapi???

  Ni kiongozi gani aliyeipeleka AMANI yetu sokoni ikajaribiwe kwa minofu ya ng’ombe? Hebu tuisafisheni kambi yetu kwanza, HEKIMA tumemuacha ameondoka!

  Hao viongozi wa madhehebu waliokutana Mwanza, na kutoa tamko lililoyufikisha hapa, WAJIUZURU!!!

 14. Shalom. Mt. Paulo alifundisha tusikwazwe na vyakula ni sawa kabisa, lakini ni ktk mazingira gani? sio kwamba hicho chakula kimepatikana ktk mazingira yasiyokuhusu? (yaani ktk eneo geni na mazingira yako) Sivyo ilivyo kwa hawa, aliyechinjwa ni ng’ombe mali ya Mkristo, wachinjaji Wakristo, Butcher iliyotumika kuuzia mnyama huyu ni la Mkristo, walengwa (walaji) ni wakristo sasa nini tatizo ? Madai yao wanataka haki, utawezaje kudai haki juu ya mali isiyokuhusu? kilichochinjwa na mimi wewe kinakuhusu nini? maana mlaji ni mimi na watu wangu. Basi kama wanataka haki watuchinjie na nguruwe.

 15. Ndugu zangu, kwanza nawapa pole sana kwa hayo matatizo pili naomba sana MUNGU atupe hekima itokayo juu. Kwa maana upande wa pili huwa wanashabikia sana mapambano ya jinsi hiyo kwa vile ni sehemu ya utekekelezaji wa dini yao. Amani imekuwepo katika nchi hii ni kwa vile sisi tumekuwa ni sehemu ya hiyo amani. Upande wa pili wanachohitaji ni kupata fursa tu ya kuleta mapambano. ikitokea hawaiachi. Sisi basi kwa vile tupo tofauti na wao tusiwape hiyo fursa ya kufanya mauaji yasiyo na sababu.

 16. Mtume paulo ametufundisha wazi wazi kwamba tusikwazwe na vyakula , pale ambapo tunakuwa na mashaka basi tuvitakase kwa Jina la Yesu then tule, hii habari kuchinja mbona ni jambo dogo tu ,haya ni matokeo ya wakristo kutolijua neno vizuri,
  Tuombe hekima ya R/Mtakatifu itawale

 17. Jamani poleni sana wapendwa wa Chato. Ninaamini kama Serikali haitafanya maamuzi ya haki juu ya hilo huenda vurugu kubwa zikatawala nchi nzima. Ushauri wangu ni kwamba ili kuwepo na usawa kwa pande zote mbili kuwaruhusu wataalamu wa mifugo tu kuchinja kuliko kuchagua dini fulani. Tumuombe Mungu ili azidi kutupa upendo na amani. Mbarikiwe sana kwa kutupa habari na kujengana kiroho kupitia blog hii!!

 18. AMANI YA INCHI YETU INAELEKEA WAPI. Km vyanzo vya AMANI vina anzisha Vurugu Wapi tunako elekea! MUNGU NYOOSHA MKONO WAKO.
  Aymen

 19. wakati machafuko yanafikia hatua hii,serikali ya upande mmoja wa dini ilikuwa wapi?Eee MUNGU TUEPUSHE NA HILI JANGA

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s