Swali kuhusu Valentine

valentine

Shalom!
Naomba kuuliza ni vibaya kwa vijana wa kikristo kukusanyika siku ya wapendanao (Valentine day), mfano kupata chakula usiku na kuwa na burudani, ikiambatana na mafundisho ya mahusiano. Pia nikosa siku hiyo kuwa na mchumba wako? (NAWAPONGEZA KWA KAZI NZURI YA MUNGU MNAYOIFANYA AMEN!)

–Samwel Sheggah

12 thoughts on “Swali kuhusu Valentine

 1. JINA VALENTINE LINATOKANA NA VALENS=MIGHTY MEN=NIMROD MWANZO 10:8,9

  496 .A.D PAPA GELASIUS ALIBADILISHA LUPERCALIA IFANYIKE 14TH FEBRUARY NA KUIITA VALENTINES DAY.

  VALENTINE ALIUAWA 270 A.D NA KUITWA MTAKATIFU, NDIO HUSHEREHEKEWA FEBRUARY 14

  VALENTINO ALIPELEKA UA JEKUNDU KABURINI KILA TAREHE 14,KWA MWANAMKE ALIYEMPENDA.

  JINA FEBRUARY=FEBRUTA: MUNGU WA KIPAGANI WA RUMI

  FEBRIS=FEVER OF LOVE= “JUNO FEBRUTA+LUPERCALIA”=MIUNGU WAPENZI,
  LUPERCALIA= HUNTER GOD (NIMROD MWANZO 10:8,9)
  FEBRUA “PURIFICATION”

  FEBRUARY 14=HUKO RUMI WASICHANA 14 WA MIAKA KUMI NA KITU WALIANDIKWA MAJINA NA WAVULANA HUCHAGUA MAJINAYALIFICHWA BILA KUJUA UNAYEMCHAGUA KISHA=UNACHEZA NAE DANSI KISHA UNAENDA KULALA NA UILIYEMCHAGUA.

  HAPO NYUMA TAREHE 14 SHEREHE HII ILIWEKWA NA KUTAKASWA BIKIRA MARIA KAMA ILIVYOKUWA SHEREHE ZA “FEBRUA” = UTAKASO NA BAADAE PAPA ALIIRUDISHA SHEREHE YA MARIAM KUWA TAREHE 2 FEBRUARY.

  SIKU AMBAYO WASICHANA HUPOTEZA USICHANA WAO,WENGI KUINGIA KATIKA NGONO WAKISHEREHEA MIUNGU HII MIWILI YA MAPENZI YAANI JUNO FEBRUTA NA LUPERCALIA

  PIMA MIZANI KAMA MKRISTO INAKUFAA

  1 YOHANA 4:8 “…KWA MAANA MUNGU NI PENDO”

 2. Mkandya, kwanza nikushukuru kwa kuniweka sawa katika jambo hili la, “Dunia ni kitu kimoja na Ulimwengu ni kitu kingine.”! Katika mambo ambayo huwa yananichanganya, ni hilo la utofauti wa “Dunia na Ulimwengu”; na jingine ni la “Watu na Wanadamu” haswa kiMaandiko. Ila sasa hukuniwekea maana zake ili nami nichangamshe akili. Ila hata katika kamusi, bado inazingua, hebu angalia tafsiri ya maneno hayo:
  earth n 1 the ~ dunia; ulimwengu
  world n 1 the ~ n dunia, nchi zake na watu wake. a citizen of the ~ raia wa dunia. 2 (as 1 above; used attrib) -a dunia, -a ulimwengu a ~ language lugha ya ulimwengu.

  Kuhusu hiyo Yoh 14:30 ni kweli inasema Shetani ni mtawala wa ulimwengu, mimi niliunga tu nikijua yote ni moja!

  Asante!

 3. Ndugu Lwembe hili si jambo ambalo ningependa linichukulie muda sana kulijadili. Lakini napenda tu kusema kuwa maelezo ya Mgreth ni moja tu ya ”assumptions” nyingi zilizopo juu ya suala zima na sikukuu ya wapendanao. Hata wana historia na waandishi wanakiri kuwa hakuna chanzo kwenye ”archives” kinachotupa uhakika wa moja kwa moja wa suala hili. Hiyo sikukuu ya “LUPERCALIA” yenyewe haikuwa inasherekewa Febuary 14, ila ni Feb. 15.

  Katika kufutilia mbali sherehe za kipagani Pope Gelasius I aliamua kuibatilisha hiyo sikukuu ya kipagani na kuamuru iwepo sikukuu ya kumbukumbu ya mt. Valentine na isifanyike Feb.15 kama ilivyokuwa inafanyika ile ya kipagani, ila ifanyike Feb 14.

  Tangu mwanzo maudhui ya upendo wa siku hii hayakuwa ya mahaba (Eros-passionate love)ila ya upendo wa ki Mungu (Agape Love)

  Historia inaonesha kuwa aliyekuja kubadilisha maudhui ya siku hiyo ni mtu mmoja anaitwa Chaucer katika karne ya 14. Alianza kubadili aina ya upendo unaotakiwa kuonesha siku hiyo kutoka upendo wa Agape kwenda upendo wa mahaba(Eros) kwa hiyo akaingiza mambo ya “romance”

  Ndio maana nikasema kimaudhui siku hiyo ilitakiwa kuwa ya kuwakumbuka watu walio katika hali ngumu za namna yoyote, kama wagonjwa, wafungwa,yatima. Kwa sababu ilikuwa siku ya kuonesha upendo wa Agape.

  Magreth yeye amechukua zaidi mkanganyiko hasi zaidi uliogubika siku hii. Sasa kwa mtu asiependa kufuatilia vitabu anaweza kudhani kuwa huo ndio ukweli wote juu ya siku hiyo.

  By the way, kama mtu anakosa maana madhubuti ya kuonesha upendo wa Agape katika siku hii, basi asijilazimishe kufanya chochote, maana wala sio siku ambayo tunalazimika kuikumbuka.

  Lwembe kwa habari ya umiliki wa dunia hii kuna vitu viwili ambavyo umevichanganya, na si wewe tu bali watu wengi huvichanganya wakidhani ni kitu kimoja.
  Dunia ni kitu kimoja na Ulimwengu ni kitu kingine. Shetani siyo mungu wala mtawala wa dunia hii, bali ni mungu na mtawala wa ulimwengu huu.

  Na hata andiko la Yoh 14:30 ulilonukuu halisemi kuwa shetani ni mtawala wa dunia hii ila ni mtawala wa ulimwengu huu.

  Huwa sioneshi upendo wa mahaba katika siku hiyo ninapokuwa nimeamua kuonesha upendo.

 4. Iwapo tunapenda sana kushawishika kwa urembo na starehe na mambo laini laini, basi hiyo Siku ya Wapendanao au maarufu kama Valentine au katika ujumla wake, yaani uifukuapo mizizi yake ili kuibaini kisawa sawa, hiyo Sikukuu, kiroho inaitwa, “LUPERCALIA”, ‘Sikukuu ya Lupercus’ yule mungu wa Kirumi aliyewalinda wasishambuliwe na mbweha. Katika sikuu hiyo huyo ndiye anayeshukuriwa, basi nasi kujiunga katika sikukuu hiyo, iliyopachikwa jina la mtakatifu wa Kikatoliki, kwamba haina madhara, kama ndg Mkandya anavyoshauri, si kweli!! Hiyo ndiyo hatari inayomkabili mkristo anaye elea elea bila kufungiwa nanga katika Neno, wanaishia kupeperushwa na kila upepo wa miungu, wanajiabudia tu!!!

  Dada Margreth kachukua wasaa wake kutafuta ukweli wa jambo hilo, na kauleta; tena uko wazi kabisa kwamba sikukuu hiyo ni ya kipagani, haina uhusiano wowote ule na Neno la Mungu. Lakini mwalimu Mkandya anatuambia eti,
  “Mpaka hapo sioni ubaya wowote wa siku hiyo. Tena kwa mtazamo wangu haikupasa kuitwa siku ya wapendanao, bali ingeitwa ”siku ya kuonesha upendo”. Maana kwa maelezo ya hapo juu sioni kama kuna uhusika wowote wa mambo ya mahaba. Ulikuwa ni upendo wa dhati kabisa wa kwenda kuwaona wafungwa ikiwezekana na wagonjwa pia.”!!!

  Hivi jamani kuna mahali katika hayo maelezo paliposema kuwa hao Warumi walikuwa wanakwenda kuwatazama wagonjwa au wafungwa? Hili jambo si kweli, kuibandika ma make-up ya wema hiyo sikukuu, isiyo na mizizi katika Kristo, Mkandya, hakuwezi kuigeuza kuwa ya kikiristo, itabakia kuwa ni ibada ya kipagani wanayoshiriki wakristo wanao elea elea tu. Upendo tunaoujua uko mmoja tu, na huo ndio unaotuongoza tusishiriki ibada za miungu, Yn 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

  Kwamba hii dunia si mali ya Shetani, hilo ni kweli. Lakini mmiliki wa hii dunia ndiye aliyetuambia kuwa Shetani huyo huyo ndiye mtawala wa dunia hii, Yn 14:30 “Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.” Kwa hiyo kuvibeba vitu vyake na kuvileta kanisani kwa kisingizio kuwa aliwaibieni, ni mambo ya kitoto, twapaswa kumpinga na mambo yake yote. Vitupilieni mbali vinyago vyake ili muwe salama!!!

 5. Helen wala usipate shida, inaonekana ni Roman kwa sababu ndio dini ya kwanza. Huwezi kuisema historia ya ukristo bila kuutaja uroma/urumi.

  Na wewe si mroma bali ni mtanzania mkristo, romani kwako ni jina la dini tu!

  Barikiwa.

 6. Tusitishane sana wapendwa!
  Ukiangalia kama Magreth alivyoonesha asili ya Valintine siyo mbaya ila hapo katikati iliharibiwa.

  ”Established as a religious holiday, the Feast of St. Valentine honored the Roman priest who lost his life during the reign of Roman Emperor Claudius II. According to various historical accounts, Valentine, a priest in Rome, was persecuted for his beliefs and executed on Feb. 14. Approximately 270 A.D. Valentine became a symbol of love and compassion. Several hundreds of years later when the Roman Catholic Church gained a stronger foothold in Europe and set about substituting pagan rituals with more “Christian” sounding names, Valentine was officially recognized”

  Mpaka hapo sioni ubaya wowote wa siku hiyo. Tena kwa mtazamo wangu haikupasa kuitwa siku ya wapendanao, bali ingeitwa ”siku ya kuonesha upendo”. Maana kwa maelezo ya hapo juu sioni kama kuna uhusika wowote wa mambo ya mahaba. Ulikuwa ni upendo wa dhati kabisa wa kwenda kuwaona wafungwa ikiwezekana na wagonjwa pia.

  Ni kawaida kwa watu wa dunia hii katika kizazi cha leo kubadilisha kila kitu ili na kuingiza mambo ya mapenzi. Hata pasaka wasiomwamini Yesu kwao ni siku ya kufanya ufuska tu, hawana kitu kingine.

  Siku zote ni za Mungu, na ni vizuri kufanya jambo lolote jema katika siku yoyote maana huko ndo kudhihirisha kuwa tumebadilishwa nia zetu tofauti na wasioamni ambao wao huenenda katika ubatili wa nia zao. Hapo kinachoazimishwa sio siku ispokuwa ni kusudi la moyo la yeye mwenye kuazimisha.

  Hii dunia si mali ya shetani jamani, ni mali ya Baba yetu. Kama ni mali ya shetani kwamba tumwachie kila kitu basi tulipaswa tukiokaka tu tunaenda mbinguni.

  Tusifanye dhinaa wala ubaya wowote siku ya wapendanao!

  Halafu si kila tunachofanya lazima kiwe kimeagizwa na Bwana kwenye biblia, ila ni lazima kufanya kile ambacho Bwana ameagiza kama alivyokiagiza.

 7. hivi ni Romans tu wanasheherekea valentines?tuangalie pande zote jamani sio kila siku Romans Romans……wengi tu tunawaona wanasheherekea na wala si Romans.Kila ushetani wa wakristo ni Roman ila wengine?

 8. velentine’s day mwiba wa shetani msiukanyage epuka! kimbia ni upagani na umizimu siri nzito.
  utamu kwenye ndoano ya shetani mwenyewe na ibada za mizimu. mafundisho ya wanadamu yanaangamiza dunia hii wana wa Mungu. Tutajificha wapi siku ile kuu.

 9. Valentine’s Day
  In this Teen Bible Study Guide, we’ll discuss the origins of Valentine’s Day and examine what God says about it.
  Introduction
  Hearts and flowers, cupids and candy—today’s symbols of Valentine’s Day are well removed from the circumstances which instituted this yearly display of affection.
  In this installment of Teen Bible Study Guide, we’ll discuss the origins of Valentine’s Day and examine what God says about it.
  History
  Established as a religious holiday, the Feast of St. Valentine honored the Roman priest who lost his life during the reign of Roman Emperor Claudius II. According to various historical accounts, Valentine, a priest in Rome, was persecuted for his beliefs and executed on Feb. 14. Approximately 270 A.D. Valentine became a symbol of love and compassion. Several hundreds of years later when the Roman Catholic Church gained a stronger foothold in Europe and set about substituting pagan rituals with more “Christian” sounding names, Valentine was officially recognized.
  “Lupercalia”
  In ancient Rome this pagan feast day was known as Lupercalia, the “feast of Lupercus.” Mid February was traditionally the time of the festival, an ode to the God of fertility and a celebration of sensual pleasure, a time to meet and court a prospective mate.
  Lupercus was the Roman god that protected them from wolves, which were a great danger in that area. So, each year in the middle of February the Romans honored the god Lupercus, giving him thanks for protecting them. The people feasted, danced and played games. When the young men wanted partners for the dancing and games, they drew names of girls from a bowl. Sometimes they became sweethearts, too. This went on for hundreds of years.
  Modernization
  As more and more people throughout the Western Roman Empire converted to an increasingly popular “Christianity,” they brought many of their favorite customs with them, including this “feast of Lupercus”. In AD 496, Pope Gelasius outlawed the pagan festival. But he wanted to replace it with a similar celebration. He needed a “lovers” saint to replace the pagan deity Lupercus. The martyred bishop Valentine was chosen as the patron saint of the new festival.
  Thus, “the church endeavored to amalgamate (mix), as it were, the old and new religions, and sought, by transferring the heathen ceremonies to the solemnities (observances) of the Christian festivals, to make them subservient (subordinate) to the cause of religion and piety… The result has been the strange medley (mingling) of Christian and pagan rites…” (Chambers’ Book of Days, Vol. 2).
  And that’s how the feast of Lupercalia was replaced with the feast of St. Valentine.
  Still others claim that sending greetings to loved ones on Feb. 14 dates to the middle ages when it was believed that this day marked the beginning of the mating season for birds.
  1. What was the motivation to rename Lupercalia? How successful (on a scale of 1 to 10) do you think the strategy was?
  2. But, despite it’s obvious pagan roots, is it still all right to keep it?
  What does God say?
  DEUTERONOMY 12:29-32 ” When the LORD your God cuts off from before you the nations which you go to dispossess, and you displace them and dwell in their land, take heed to yourself that you are not ensnared to follow them, after they are destroyed from before you, and that you do not inquire after their gods, saying, ‘How did these nations serve their gods? I also will do likewise.’ You shall not worship the LORD your God in that way; for every abomination to the LORD which He hates they have done to their gods; for they burn even their sons and daughters in the fire to their gods. Whatever I command you, be careful to observe it; you shall not add to it nor take away from it.”
  1. Why does God not want us to look at other nations and other ways of worship and adopt those for our worship of Him?
  2. Why do you think we should be careful in our worship of God?
  3. What did Christ say about it?
  Mark 7:6-7

  He answered and said to them, “Well did Isaiah prophesy of you hypocrites, as it is written: ‘This people honors Me with their lips, But their heart is far from Me. And in vain they worship Me, Teaching as doctrines the commandments of men.’ ”
  4. How do these words of Jesus apply to the celebration of Valentine’s Day?
  5. Did Christ uphold God’s commandments? Read John 15:10
  and 14:15 and then answer.
  COMMENT: Jesus is our example so we should follow His conduct (I Cor. 11:1).
  Summary
  1. With what is Valentine’s Day associated today? Do any religious ideas come to mind? If so, which ones?
  2. What are the origins of Valentines’ Day? Why is it important to know the origin of Valentine’s Day?
  3. What does God say about how we worship Him?
  4. Why is it important to keep God’s commandments?
  5. What other days are celebrated in today’s culture that don’t come from the Bible?

 10. Bwana Yesu asifiwe wapendwa, mi nadhani jambo zuri kujua nini kiini cha Valentine day na aliyeanzisha hii siku alikuwa ana leno gani? Nadhani ifike kipindi wakristo tusikurupukie na kuiga vitu ambavyo havina utukufu katika kujenga mwili wa Kristo mi nadhani kuna semina nyingi tu makanisani ambazo zinatusaidia katika kukuza haya mahusiano yetu na si siku hii ya valentine day.;

 11. Siku ya Valentina ni Msumari ambao shetani ameuchimbia chini , ukilogwa tu ukapita hiyo njia iitwayo valentina day basi lazima utakuchomwa tu kwa sababu aliouweka sio Mungu bali ni shetani na mpango wowote ambao shetani ndio ameutunga hata kama kwa nje unaoneka mzuri kama LuLu na nia yake sio nzuri hata kidogo.
  Mimi nashauri vijana wakikristo tusipeperushwe na upepo wa dunia ,hii siku ya tar 14 Feb. tuendelee na kazi zetu kama kawaida

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s