Maombi ya dharura kuhusu Tanzania

makubaliano
Wapenzi wa Strictly Gospel (SG), marafiki na watumishi wote wa Mungu popote mlipo,
Tutakuwa na maombi ya kufunga na kuomba kuanzia tarehe 20 hadi 22 mwezi February 2013.
Masaa 72 ya kufunga unaruhusiwa kunywa maji pekee. Kwa wale wasioweza kwenda masaa 72 unaweza kufunga kwa masaa 12 kwa siku.
Tutakuwa tukiweka update kuanzia siku ya kwanza hadi ya tatu katika ukurasa huu, Hivyo watu na makundi mbali mbali mnaweza kufuata ratiba hii ili twende sawa.
Kwa wale walioko Dar es salaam Tanzania, Siku ya tatu Ijumaa tarehe 22 February 2013 tutakutana kwenye ukumbi wa kanisa la JESUS CELEBRATION CENTRE (JCC) URAFIKI. Kuanzia saa nne usiku hadi asubuhi. Kutakua na Ibada ya Sifa, Kuabudu, Maombi kwa ajili ya Tanzania.
Ikiwa utashiriki nasi kwenye mkesha wa maombi tafadhali tujulishe kwa email strictlygospel@yahoo.co.uk
Pia kwa wale mlio mbali wasiliana nasi kwa email hapo juu
Tutaomba kwa ajili ya Rehema za Mungu na Ulinzi wa Mungu ukawe juu ya nchi, pia tutaomba kwa ajili ya watumishi wa Mungu Tanzania.
BWANA asipoijenga nyumba, Waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji, Yeye aulindaye akesha bure” Zaburi 127:1
Advertisements

4 thoughts on “Maombi ya dharura kuhusu Tanzania

 1. Bwana Yesu asifiwe!

  Leo tunaanza maombi yetu,

  SIku ya kwanza, tutaomba Mungu airehemu Tanzania na watanzania kwa ujumla. Mungu atusamehe maovu yetu na kusikia maombi yetu…
  —————————————————————

  MAOMBI SIKU YA PILI: Kwa kuwa Bwana ametusamehe na kuiponya nchi yetu 2 Chro 7:14….Leo Tarehe 21 February tunasimama kinyume na kila lililo kinyume na mwili wa Kristo Tanzania, kinyume na ustawi wa watanzania, lililo kinyume na ulinzi na usalama wa Tanzania, lililo kinyume na amani ya Tanzania na lililo kinyume na uhuru wa kuabudu Tanzania. Tunatamka hukumu dhidi ya kila roho itendayo kinyume na kusudi la Mungu katika Tanzania.

  Tunaomba uweza na mamlaka ya Mungu kutawala kila mfumo wa haki, sheria na utawala, elimu, rasilimali na shughuli zote za uchumi.

  —————————————————

  MAOMBI SIKU YA TATU NA MKESHA:

  Tunaomba Neema, Utakatifu wa kiMungu, Upendo, Umoja, Hekima, Maarifa na Nguvu yake Jehova vilitawale kanisa; Tunatangaza Mapenzi ya Mungu kulitawala kanisa na huduma zote. Tunatangaza na kuamuru Neema na nguvu ya upendo katika; kuinuana, kuonyana, kujengana, kutiana moyo na kufanya kazi ya Mungu kwa pamoja. Tunatangaza kanisa kusimama kwenye nafasi yake katika ulimwengu wa roho na wa mwili katika jina la Yesu.

  Tunatangaza haki ya kila Mtanzania kujulikana wazi na kutimizwa pasipo mapungufu; tunatangaza haki ya uhai, ulinzi, usalama, huduma bora pamoja na uhuru wa kuabudu. Tunatangaza Amani na Usalama utokao kwa Kristo Yesu kuanzia Ikulu ya Magogoni hata kitongoji, kijiji, mtaa mpaka kaya. Tunaendelea kutangaza kwa mamlaka ya Kristo Yesu; Mtu yeyote, kikundi ama taasisi iwe ya binafsi ama ya uma, ya kidini ama kijamii ama kisiasa, inayokusudia ama iliyokusudia chochote kinyume na amani, maendeleo na ustawi wa Tanzania na watanzania VIHARIBIKE NA KUPOTEZWA KWA MKONO WA MUNGU ALIYE HAI. Kila mtandao na usambaratike, kila fikra na elimu vimtii Krito. Tunaviweka vyombo vyote vya ulinzi na usalama mikononi mwako Jehova, vikafanye na kusimamia lile lililo mapenzi yako kwa utukufu wako na kwa amani na furaha ya Watanzania. Asante Mungu wetu, uliyewapigania wanao Israel dhidi ya maadui zao wengi sana kwakuwa uliwasamehe walipokukumbuka na kukulilia wewe uliye msaada. Baba tunashukuru kwa kukubali sala zetu na maombi yetu. Asante kwa kutuwezesha kuomba. Baba usituache kuwa na muunganiko nawe na uwepo wako usiiache Tazania.

  Omba kwa jinsi Roho Mtakatifu atakavyokuongoza. Pia kwa tunasisitiza wale mtakaokuja kwenye mkesha ijumaa hii tujulishe kwa email strictlygospel@yahoo.co.uk au simu no. 0659 953 240

  Ili iwe rahisi kuandaa chai na vitafunwa kwa Idadi ya watakaohudhuria.

  Mungu atutie nguvu siku ya leo tena.

  “Basi ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mwajua kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana” 1 Wakorintho 15:58

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s