Kuna Chuo cha kigaidi Tanzania?

Al Qaeda

Hofu ya Al Qaeda

– Wananchi wakihusisha chuo na ugaidi
– Mbunge ataharuki, aandaa hoja. binafsi
– Mkuu wa’Mkoa, DCwakwepa kunena

HOFU ya kuwapo kwa magaidi wa mtandao wa Al- Qaeda, imetanda katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza baada ya kuvuja kwa taarifa za kuanzishwa kwa chuo kimoja cha kidini kinachohofiwa kutoa mafunzo yenye mwelekeo wa kigaidi visiwani humo.

Taarifa     hizo zimeeleza kuwa chuo hicho kinajulikana kwa jina la Markaz, Aljazeera na kimeanzishwa kwa ufadhili wa raia wa kigeni ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu.

Makundi yanayotajwa kufadhili uendeshaji wa chuo hicho ni AI-Qaeda na AI shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani. Uchunguzi uliofanywa na Mtanzania Jumatano wilayani Ukerewe, umebaini kuwa chuo cha Markaz kinatoa rriafunzo kwa watu wa rika mbalimbali yenye mwelekeo wa kujihami na kushambulia kama Karate na Kung-fu.

Aidha, taarifa nyingine za kiuchunguzi ambazo gazeti hili lilidokezwa na wakazi wa kisiwani humo walioonyesha wasiwasi wa kuwepo kwa chuo hicho, zilidai’ kuwa, aina nyingine ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho na kushambuliana kwa silaha aina ya jambia. Uchunguzi ulibaini zaidi kuwa, wanafunzi katika chuo hicho ni watoto wenye umri wa kati ya miaka sabahadi 10 na pia kuna wanafunzi vijana na watu wazima. Baadhi ya wakazi wa wilayani humo waliopata kufanya kazi katika chuo hicho, waliliambia gazeti hili kuwa chuo hicho kimekuwa kikipokea mizigo ya aina mbalimbali, ikiwa imefungwa kwenye maboksi ambayo katika udadisi wao walibaini kuwa, baadhi ya bidhaa zinazokuwa kwenye shehena hizo ni kanzu, seti za televisheni, vitabu na silaha za aina mbalimbali.

Walidai kuwa, walianza kukitilia mashaka chuo hicho baada ya kubaini kinapokea silaha katika baadhi ya mizigo yake. Mbali ya hilo, wakazi hao walilieleza gazeti hili kwamba aina ya wageni ‘ wanaoingia na kutoka visiwani humo kwa minajili ya kukitembelea chuo hicho, ni jambo jingine ambalo limekuwa ‘likiwafanya wazidi kukitilia shaka chuo hicho.

Kwa mujibu wa wakazi hao, wageni hao wamekuwa wakiingia kisiwani kwa njia ya mitumbwi wakipita katika njia za panya nyakati za usiku. Wageni hao kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la Nansio ni wale wanaodaiwa na kuaminika kutoka katika nchi jirani za Kenya na Uganda ambazo mipaka ya Ziwa Victoria inapita.

Wa f a n y a b i a s h a r a wanaojihusisha na usafirishaji abiria waliozungumza na gazeti la Mtanzania Jumatano walieleza kuwa, wageni wanaowapakia kuwapeleka chuo cha Markaz au maeneo mengine ya kisiwa hicho huwalazimisha kuondoa misalaba waliyoivaa shingoni au waliyotundika katika magari na pia huwataka wazime redio katika magari yao.

Hofu hiyo ya wakazi wa Nansio ilisababisha gazeti hili kumtafuta Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli (Chadema) ambaye naye alikiri kulifahamu jambo hilo. Akizungumza kupitia simu yake ya kiganjani, Machemli alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ambayo wakazi wake wanayahusisha na matendo ya kigaidi.

Mbunge huyo alisema hofu zaidi kuhusu chuo hicho ni kuwapo kwa taarifa zinazodai kwamba, baadhi ya wanachuo ambao wamewahi kupata mafunzo chuoni wanatajwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi ya AI Qaeda na AI-Shabab. Kwa mujibu wa mbunge huyo, miongoni mwa hatua ambazo amepata kuzichukua ili kutafuta majibu ya wasiwasi wa wananchi wa Ukerewe ni pamoja na kumsaka mmoja wa watu anayekijua chuo hicho. “Ni kweli tuna wasiwasi na hatuoni kazi ya umma kinachojihusisha nacho. Niliwahi kumuuliza Diwani wa Kata ya Nansio, Sheikh Ramadhani Mazige (CCM) kuhusu uhalali wa kuwapo kwa chuo hicho kwa sababu alikuwa akisimamia ujenzi wake na nikashauri juu ya umuhimu wa kubadili aina ya mafunzo yanayofundishwa chuoni hapo na jibu lake lilikuwa wenye chuo hawataki.

Alipoulizwa     iwapo     anawafahamu wamiliki wa chuo hicho, alikana kuwatambua kwa kueleza kuwa, jitihada zake za kuwafahamu hazikufanikiwa baada ya Diwani Mazege kukataa kuwataja. Machemli alisema kuwa, amepanga kulifikisha suala hilo kama hoja binafsi kwenye Baraza la Madiwani ili kuomba kibali cha kutembelea chuo hicho kuona shughuli zinazofanyika na kwamba iwapo atakwamishwa, atalifikisha suala hila katika ngazi za juu.

Akizungumza kuhusu raia wa kigeni wanaopitia njia za panya kwa usafiri wa mitumbwi nyakati za usiku kufika chuoni hapo, Machemli alisema hilo hawezi kulipinga. Kwa mujibu wa Machemli, jiografia ya visiwa vya Ukerewe inavifanya viwe wazi kuhusu mipaka yake na kwamba jambo hila alipata kulizungumza bungeni ingawa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alimpuuza. “Nilizungumza katika mkutano uliopita wa Bunge kuhusu mipaka ya Ukerewe kuwa wazi sana, nililalamika kwamba, wanajeshi wa Kenya na Uganda wanakuja hadi katika kisiwa hicho kufanya mazoezi yake na kuondoka, lakini nashangaa waziri akanipuuza,” alilalamika Machemli.

Alipotafutwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Ernest .Mangu kwa ajili ya kuzungumzia juu ya hofu hiyo, alisema anaomba apewe muda kwa sababu yeye ni mgeni mkoani humo na huu mwezi wa pili akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, hivyo yapo mengi ambayo hayafahamu. Hata hivyo, Mangu aliliahidi gazeti hili kufuatiliajuu ya suala hila na kulitolea ufafanuzi baadaye. Kwa up an de wake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mary Tesha alikana kufahamu chochote na badala yake akahoji sababu za mwandishi kumtafuta wakati tayari suala hila lilisharipotiwa katika gazeti hili hivi karibuni.

Kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa vikundi vinavyojihusisha na utoaji mafunzo ya . kigaidi hapa nchini, vikiwa vimejificha katika mwamvuli huku lengo halisi likiwa kuhatarisha amani ya kitaifa. Tayari Rais Jakaya Kikwete amekwishaagiza kusakwa kwa makundi yenye mwelekeo huo yanayohisiwa kuhusika na machufuko na mauaji hapa nchini, wakati akitoa salamu za pole baada ya tukio la kuuawa kinyama kwa Padre wa Kanisa Katoliki Evaritus Mushi huko visiwani Zanzibar.

Mwisho.
Kwa     habari     zaidi     fuatilia mfululizo wa makala kuhusu hofu hiyo ya ugaidi kisiwani Ukerewe katika ukurasa wa 15 wa gazeti hili.

–Mtanzania

20/Februari/2013

Advertisements

10 thoughts on “Kuna Chuo cha kigaidi Tanzania?

 1. Kama uliwahi kusoma kitabu cha Esta ktk biblia utajua kuwa Mungu ni mwenye nguvu , mti aliouchonga Amani hili umtundike Modekai ulimtundika yeye mwenyewe, maana yake ni kwamba mti wa kumtundika Modekai ulikuwa tayari lakini na farasi wa kumpadisha Modekai Mungu alishamuweka tayari, kama wewe umeokoka endelea kumuomba Mungu soma kitabu cha Esta kwa habari hii utajua kuwa ninayosema ni kweli, hayo mafunzo wanayojifunza ya ugaidi wataanza kuchinjana wenyewe , Mungu wetu ni moto ulao, mimi ni mtanzania nimeokoka ninaishi nchini Marekani, kila kukicha naombea nchi yangu maana ukweli ni kwamba vitendo vichafu vimeingilia taifa langu, kama aluvyosema mfalme Yeoshafati ktkt 2 nyakati 20;12, Ee Mungu je hutawahukumu?maana sisi hatuna huwezo juu ya jamii kubwa hii wanaotujia juu yetu wala hatujui tufanyeje lakini macho yetu yatazama kwako, Ndugu zangu huu siyo wakati wa kulala , na siyo wakati wa kuangalia na kuongelea hari hizi kinyume, ni wakati wa kuomba na kumtazama Mungu, imeandikwa kila amwaminiye hatatahayarika, Warumi 10:11. Malaika wa Mungu aliyeshuka akampiga mfalme Herode kwa chango akafa mdo 12:22-23.kama umeokoka na hujawahi kusikiliza kanda alizofundisha mtumishi wa Mungu mwalimu Mwakasege nakushauri usitafute na uanze kusikiliza mafundisho ya somo la MILIKI NA UTAWALE KWA NJIA YA MAOMBI. Nakuhakikishia ukisikiliza somo lile utakuwa nje na hofu na utaanza kutembea kifua mbele ukijua kuwa utakapoanza kusimama ktk nafasi yako ya ufalme na ukuhani Mungu atasikia na kujibu. maana sisi tuliokoka tukisimama ktk nafasi zetu mbingu zitatekeleza tunalosema . waache wachimbe mashimo lakini nasema watadumbukia ndani yake ktk jina la Yesu. na pia ktk kuomba tusiombe maombi ya ubinafsi tuombee nchi nzima na dunia nzima , usiombee ukelewe tu kwa kuwa una ndugu yako anayekaa ktk kisiwa kile, usiombee Dar peke yake kwa kuwa mjomba wako anakaa kule, usiombee kisiwa cha zanzibar kwa kuwa aunt yako Nancy anafanya kazi kule , umbea taifa zima hata wale ndugu wasiomjua Bwana waokolewe , na siyo taifa tu bali dunia nzima maana kila coner kuna jambo baya sasa hivi. TIME IS UP SATAN GOD IS TAKING OVER.

 2. Huyu mpendwa anayejiita “By Mtumishi” mbona anatoa mambo ya ajabu sana. Kama hapo kwenu Dar maeneo ya Vingunguti vijana wa kiislam wanafanya mazoezi ya vita na wewe umeshuhudia umechukua hatua gani za kulipoti kwenye vyombo vya serikali ya mtaa au mamlaka kuu zaidi ili uone ni hatua gani serikali itachukua?

  Hivi kweli, wakristo tunatumia akili kweli? Wewe unawezaje kuona watu wanafanya mazoezi ya vita msikitini au kambini kisha wewe ukakaa kimya? Are you serious” Hivi unaipenda kweli nchi yako Tanzania? Ulipeleka lini taarifa hiyo kwa IGP, au Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa?

  Tunataka wakishatoka kambini wakaanza kuchoma makanisa na kuua watumishi wa Mungu ndipo tuanze kutoa mayowe kwamba serikali imeshindwa kuwadhibiti kumbe ni sisi wenyewe tulishindwa kutoa taarifa mapema? Nani amekwambia kwamba serikali ya nchi hii ni ya kiislam mpaka uogope kutoa ripoti polisi au kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar? Uliogopa kwamba ukitoa taarifa utauwa? Acha woga Mtumishi nenda ukawaripoti?

  Tafuta taarifa za uhakika ikiwezekana jipenyeze mpaka ndani ya kambi kwa siri ukiweza uchukue na picha za mnato au video wakiwa wako kambini au wakiwa wanafanya mazoezi hayo kisha picha hizo ukizipata uzimwage mtandaoni na kwenye magazeti tuone kama serikali haitachukua hatua yoyote ndipo tuihukumu kwamba inawalea hao wanaoitwa magaidi.

  FANYA HIMA TAFADHALI.

 3. shalom huu si wakati wa kunyamaza ni kuomba kwa bidii, mfalme herode alipoinuka kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa tukisoma matendo 12:1- ndo haya yameanza tanzania yetu, hapa dar es salaam maeneo ya vingunguti vijana wa kiislamu wapo kambini wanasoma dua na kufanya mazoezi ya kivita , tuombeni jaman mauti imeamriwa kwa kanisa, kanisa lilipoomba kwa bidii petro aliokoka na mauti. hakuna acheni magugu na ngano viote pamoja ni mda wa kuomba sasa.

 4. Ni kweli kuwa magugu yalipandwa wakati watu wamelala, lakini watumishi(malaika) walipotaka kuyang’oa Bwana alisema msiyang’oe acheni vyote vikue. Hivi sisi kama ngano hatuna biashara yoyote na magugu.Biashara ya magugu anayo BWANA mwenyewe. Shabaha ya ibilisi kupanda magugu ilkuwa ni kuisonga ngano, kuinyima chakula na kuhakikisha haistawi. Ili badala ya kuzaa masuke yenye ngano iliyokomaa aidha izae makapi au ife kabisa. Ndugu zangu hebu na tuifuate hekima ya bwana wetu YESU KRISTO ambaye alisema viacheni vyote vikue. Kwa maana gugu haliwezi kuizuia ngano isipate chakula ambalo ni neno la MUNGU. Neno hilo limelindwa kwa nguvu za MUNGU hadi limetufikia sisi leo. Pia Bwana wetu YESU KRISTO anaimwagilia na kuinywesha ngano kinywaji cha maji ya uzima. gugu haliwezi kuzuia ngano isipate chakula, gugu haliwezi kuizuia ngano kupata kinywaji cha roho(maji ya uzima). Tusipoteze muda kuyaangalia magugu yanafanya nini, wala tusipoteze muda kujaribu kuyang’oa hatutaweza maana ni bwana ameamuru yaache yakue. Geuzeni macho yenu na fikra zenu muangalieni KRISTO aliye nguvu yetu, hekima yetu, ushindi wetu na tumaini letu. Nyamazeni kimya mtauona wokovu wa MUNGU wetu. Hapa inasisitizwa kuwa kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anaenenda kama inavyoipasa injili ya KRISTO. kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anaye ROHO WA KRISTO ndani yake. Kila mmoja ahakikishe kuwa ametubu dhambi zake na anishi katika utakaso kwa msaada wa ROHO wa MUNGU. Wakati wao wanafanya maandalizi ya mapambano ya kimwili hebu sisi tujiandae kunyakuliwa. BWANA YESU yuaja asitukute tumelala. Achaneni na hayo magugu.

 5. Jana kanisa lingine lilichomwa moto, Habari kutoka kwa Millard Ayo

  Baada ya hili kanisa la Pool of Siloam Kianga Zanzibar kuchomwa moto saa 9 usiku wa kuamkia february 19 2013, Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo Penuel Elisha amesema sio rahisi kujua kwa haraka aliyehusika na hilo tukio japokua kumekuwepo na historia ya mgogoro kati ya kanisa hilo na msikiti uliopo karibu na eneo hilo.

  Namkariri Elisha akisema “tukio lilivyokua, majira ya saa kumi na dakika 34 nilipigiwa simu na mchungaji mwenzangu aitwae Israel akaniambia kanisani kwetu kumeshavamiwa na mlinzi anapigwa mawe, nikachukua hatua ya haraka kuna mchungaji wetu mgeni ambae ni mkuu wa kanda nikamuamsha nikamwambia tumeshavamiwa, nilikua na namba ya polisi mmoja wa Mwera ambae alietusaidia kwenye tukio lililopita la mwaka 2011, nikampigia akapokea na kuchukua hatua za haraka sana”

  Kwenye sentensi nyingine naendelea kumkariri mchungaji huyu akisema “nakumbuka mwaka 2011 walikuja watu zaidi ya 80 wakiwa na nyundo na sururu wakalibomoa hili kanisa lakini jana yake uongozi wa Msikiti wa Kianga ulituita kwenye nyumba ya Sheha wakawa wanadai kwamba tunadai hatimiliki, uhalali wa kujenga kanisa hapa”

  Mlinzi wa kanisa hilo ambae alikuepo wakati wa tukio amesema “mi nilikua nimekaa nyumba ya kisima cha kanisa, walivyopita nikatoka kule nikaingia humu ndani badae wakarudi wakanurishia mawe nikatoka nikakimbia kuwaamsha jamaa kwamba nimevamiwa, nikampigia mchungaji simu”

  Mpaka sasa Jeshi la Polisi Zanzibar limesema linachunguza chanzo cha huo moto uliounguza sehemu ya kanisa hilo la POOL OF SILOAM lililopo Kianga nje kidogo ya mji wa Zanzibar, naibu Mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar Yusuf Ilembo amesema hilo tukio linahitaji uchunguzi wa kina ili kufahamu waliohusika ambapo mpaka sasa hakuna aliekamatwa.

 6. Ni kweli kama kuna manabii halafu mambo haya yanatokea wala hatuwasikii wakisema chochote kuna tatizo katika utumishi wa watumishi hawa wa Mungu.

  N ninachokiona ni kuwa kuna maandalizi fulani waislamu wamefanya na wanaendelea kufanya ya kujiandaa na mapigano dhidi ya wakristo.

  Hizi chokochoko wanazofanya wanafanya ili wakristo wakasirike yawe mapambano,na wao wakiamini kuwa watawashinda wakristo kutokana na hayo mafunzo wanayoendelea kufanya.

  Wziri wa ulinzi mwenyewe ni mwislamu na nilimwona alivyomjibu mh. Machemli kwa kejeli siku ameuliza hilo suala la wanajeshi wa Kenya na Uganda kuingia visiwani ukerewe.

  Siwaamini waislamu hata kidogo,lazima kutakuwa na kitu kinaendelea na ndio maana wanataka
  sana rais ajaye aendelee kuwa mwislamu.

  Ugonvi wowote unaoweza kutokea kutokana na watu wanafunzwa mafunzo ya kigaidi ni hatari kuliko tunavyoweza kudhani. Huu wa mtaani tu unaotokana na hasira hufika sehemu mtu akaona ninaopambana nao wengine ni ndugu zanagu kwa kuwa unaweza kuta familia baba mwislamu mama mkristo. Lakini huu wa mafunzo waliofunzwa wanakuwa wameondolewa hiyo hali ya kukumbuka ndugu, wanaua hata mzazi wao.

  Tudhanipo kuwa kuna amani ndipo uharibifu utujiapo kwa gafla.

 7. Hivi waziri wa mambo ya ndani yuko wapi mpaka chuo cha kigaidi kinajengwa nchini? Mimi nafikiri tumrudishe mheshimiwa Augustine L. Mrema awe waziri wa mambo ya ndani wa milele, maana wengine hawajui wajibu wao na hiyo dini ya mama mdogo kwa kweli imezidi kudekezwa washughulikiwe mara moja washike adabu.Au wanipe mimi niwe waziri wa mambo ya ndani.
  Mbarikiwe sana.

 8. Lazima ukristo wetu unatatizo, maana twajinadi zaidi kuwa na manabii wa kizazi cha nne???

  Wanaume tupo wapi sasa, nchi inavamiwa, watu wanauawa, watoto wanatupwa, Je tupo salama ktk Yesu.??

  Akina mama Mpo?? ni Changamoto ya ukristo sasa. imetupasa kuwa macho maana tulipolala ibilisi alianza kupanda magugu. yamkini siku ya kung’oa magugu itatoa na mbegu njema. maana twajifanya hatuoni machipuko ya mbegu magugu.
  Barikiwa
  Anthony

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s