Nisaidieni Niondokane na Upweke

upweke.

Shalom watumishi.
Nahitaji maombi yenu wapendwa. Jinsia yangu ni kike umri miaka 36, nina mtoto mmoja wa kiume miaka 3. Nahitaji mume yule atokaye kwa BWANA. Sikuwahi kufikiri km nitazaa nje ya ndoa, lakini imeshatokea na naumia sana kwa hili, nikiangalia ktk familia ni mimi pekee sijaolewa na hata ktk ofisi yangu ktk wanawake 20 wadogo kwa wakubwa ni mimi tu ambaye sina ndoa. Hii hali inaniumiza sana maana kuna watu wananinenea maneno ya uchungu juu ya hili.

Awali nilishapata mchumba nilikaa nae miaka 7 ktk mahusiano, baadae alioa kwa siri kisa eti kazi niliyokuwa naifanya wakati ule (askari jeshi) hakuiridhia. Nilimshukuru MUNGU nikaendelea na maisha. Muda kidogo nilipata kazi Taasisi mojawapo ya serikali, yule bwana alinitafuta na kuniomba msamaha, alichoniambia anajuta. Binafsi ni mwingi wa msamaha lakini nina misimamo isiyoyumbishwa, nilimsamehe lakini sikuhitaji uhusiano wowote nae zaidi ya salaam.

Miaka miwili (2009) mbele nilipata mchumba alinitambulisha kwao na kwetu pia walimjua, bahati ilikuwa kwangu maana mama na ndugu zake walinikubali saana mpaka hivi leo. Mwaka 2011 wakati huo nina mtoto tayari nikagundua mwenzangu sio mwaminifu, tulijadili hilo swala na ndugu zake wakambana sana, lakini hakubadilika na huyo mke aliyenae ni mtu wa vituko na mpenda starehe sana ni mdogo sana kiumri 22yrs lakini huyu mwenzangu asikii wala haambiwi. Nilichoamua ni kusitisha uhusiano, nikapima afya yangu ashukuriwe Mungu niko vzr, nikaamua kumpa Yesu maisha yangu, nimeokoka tangu 2011 nov.

Wapendwa ktk Yesu binafsi ninaomba na kufunga juu ya hili maana ninapenda nami niwe na familia yangu. Kwani wakati mwingine nashikwa na upweke wa ajabu, ukizingatia sina wazazi ndugu wametawanyika na mwanangu bado mdogo siwezi kubadilishana nae mawazo. Nimeona niwashilikishe hili maana umoja ni nguvu km ulivyoonekana ktk Mnara wa Babeli.

Jina la BWANA libarikiwe….

–TUKUH

Advertisements

25 thoughts on “Nisaidieni Niondokane na Upweke

 1. Dada Tumaini, uliye “Mrembo katika Kristo”,
  Shalom!
  Tazama dada yangu, hakuna lisilowezekana kwa Mungu, haswa kwa hao wamwaminio. Basi tuseme nini, kwamba tulimwamini Mungu naye hakututimizia? La hasha, Bwana ni mwaminifu juu ya Ahadi zake zote, shida iko kwetu, hatujiachilii kwake kikamilifu, tunabaki na mashaka mashaka juu yake!

  Lakini Mungu ni mwingi wa Rehema, juu ya mapungufu yetu mengi, yeye bado ametunyooshea mkono wake atushike na kutuinua hapo tunapopungukiwa na imani. Mgeukie yeye kikamilifu, mtazame yeye ili akuponye katika yote yanayokukabili, usiyakabili peke yako kwa akili zako, kama hivi ulivyofanya kuibandika simu yako hapa. Hii ni njia isiyo salama, Mungu anaijua mpaka siku uliyotungwa mimba huko tumboni mwa mama yako. Lielewe jambo hili hivyo kwamba anakujua, tena anaijua shida yako kabla hata haujaitamka kwa yeyote yule; basi mtamkie yeye, jinyenyekeze kwake, umpokee Kristo moyoni mwako ili umpe nafasi ya kuyaongoza maisha yako na ya mwanao katika namna itakayomrudishia yeye Utukufu, kwa kukupa mume wa haja yako tena aliye bora kuliko hayo mawazo yako ili iwe ushuhuda wa mapenzi yake makamilifu kwako!

  Jaribu kuusoma ushuhuda wa mrembo mwenzako hapo juu, huyo anayeitwa Mama K, wakati mwingine Mungu katika kuyajua yanayokusibu kabla hata hujalia yeye hukutangulizia jinsi ili ikuongoze kumfikia apate kukutatulia shida yako. Yasome hayo kisha ujipime hapo, ishike hiyo njia uitembee, jipe moyo, Msaada wako u karibu nawe sana dada yangu maana Bwana huifurahia kazi hiyo ya kuwarejesha wanae katika furaha Yake!

  Hiyo simu yako uliyoiweka hapa, iondoe, toa hicho kichip, vinginevyo itakuletea “matumbusi” wa mapenzi wengi na mwisho hali yako yaweza kuishia kuwa mbaya kuliko sasa, mwamini Bwana na umsubiri Sirini!

  Bwana na akushike kwa Mkono wa Upendo

 2. Mimi ni msichana naitwa Tumainieli, nina miaka 33 nina mtot mmoja wa kike, natafuta mume wa kuishi naye maisha ya ndoa ambae yuko tayari kwa uvumilivu wa maisha ya ndoa, na ambae yuko tayari kwa shid ana raha. Awe mcha Mungu, asiwe mtumia vilevi, atakayenipenda kwa dhati mimi na mwanangu, nimetendwa vya kutosha sihitaji kuumizwa tena. no yangu ni. 0655417441.

 3. Pole kwa kuwa mpweke ila Mungu u pamoja nawe,nitafute kupitia namba hii 0762050325 ili tuongee zaidi.

 4. Mimi ni mama nilioyeolewa nikiwa na miaka 31, ni baada ya kuachana na mambo ya duniani nikampokea BWANA YESU, nikatulia na kuangalia neno linasemaje kuusu mimi kuwa na mume, nilishikiria neno la Isaya 7:7 nikawa natamka na kuhamini kuwa neno la mimi kuwa peke yangu halitasimama wala halitakuwa ktk maisha yangu , pia nilishikiria Mithali 21:1 kuwa moyo wa mfalme huwa ktk mikono ya Mungu ni kama mfereji wa maji huugeuzia apendapo, nilikuwa nikitamka kuwa baba ktk jina la Yesu moyo wa yule mtu ambaye anatakiwa awe mume wangu umo mikononi mwako naomba ukaugeuzie kwangu, Pia nilikiri na kutamka ile mwanzo 2:18 si vema mtu uyu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye, nilikuwa nikitamka na kukiri kuwa baba asante ktk jina la Yesu utanikutanisha na mtu ambaye nitakuwa msaidizi wake, yupo na unamjua wewe naomba umvute uuelekezee moyo wake kwangu, nilianza kutamka maneno hayo kila nilipokuwa nikijiwa na wazo la kuolewa , hata usiku wa manane, njiani ,na bafuni na chooni , sehemu yoyote hile nilikiri na kutamka nilichokuwa ninahamini na nilichotaka kitokee ktk maisha yangu , ( you can have what you say Marko 11:22-24), nilipokuwa ninamaliza kutamka nilikuwa ninamsifu Mungu na kuabudu, nilihamini kabisa kuwa tayari yameishatokea , kumbuka Mungu utangaza mwisho tangu mwanzo,baada ya kutamka kila wakati , matokeo yake shauri la Bwana lilisimama nilipata safari ya kuja Marekani kufanya kazi kwa mda wa miezi mitatu, baadae boss alinitaka niendelee kukaa nikaongezewa VISA, ktk kuendelea kukaa nilizidi kutamka na kumshukru Mungu, kumbuka Mungu hawezi kusema uongo Hesabu 23:19. , nilikuja USA 21:12:2003, tah 18:9:2004 nilikutana na kijana mzuri mwenye akili kazi nzuri na kila sifa niliyokuwa ninamuomba Mungu mume wangu awe nayo, tah 12:2:2005 tulifunga ndoa , kesho yake tulisafiri tukaja Tanzania tulienda nyumbani akalipa mahali na leo hii mimi ni mama wa mtoto mmoja, na mume mwema na pia nina Green Card ya miaka 10 . siyo tu kuwa Mungu alinipa mume ambaye ni baraka ktk maisha yangu, bali alinifanyia makuu zaidi ya yale niliyokuwa ninayawaza na kuyaomba sawa na Effeso 3:20 nina mume , nina green card ninaenda Tanzania kutembelea ndugu na kurudi pasipo shida ya kuomba VISA, nina kazi , mushaara mzuri, nina mtoto ambaye ananibariki kila sekunde , ninapokwambia ushuuda huu siyo kujisifia au kutangaza habari zangu , bali uone Uhaminifu wa Mungu , unaposhikilia neno lake na yeye analiangalia neno lile analitimiza Yeremia 1:12.pia ni kutaka uone kuwa kwa Mungu hakuna lisilowezekana, yote yawezekana kwake aaminiye, usiangalie mazingira yaliyokuzunguka , umuangalie Mungu kupitia neno lake, yeye anasema kuwa majani yanyauka maua yakauka neno la Bwana Mungu wetu lasimama milele, usiangalie hari bali endelea kulitamka neno na kumshukru , Mungu atakupa haja ya moyo wako. nasema haya kwa ujasiri maana ninajua nilikopitia na Mungu alichonifanyia , nakwambia dawa ambayo niliwahi kuitumia na nikapona kabisa. haya siyaandiki kwako wewe tu bali na kwa kila atakayesoma ujumbe huu ambaye ana haja kama yako , kama ulimpokea Yesu awe Bwana na mwokozi wewe ni mwenye haki , umo ndani ya Kristo ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya. . ONYO . unapoanza kutamka na kuhamini neno la Mungu itakubidi utulie usitamke neno huku ukijaribu kufanya mambo yatokee mwenyewe, yahani usiende kujirusha au kuwa na maboyfriends , hapo utajichanganya , na utakuwa hupati unachoomba maana inabidi utulie huku ukimuomba Mungu , kusudi mume yule akitokea ujue kabisa kuwa ametoka kwa Mungu si kwa nguvu zako, na kwa mtaji huo utamrudishia Mungu utukufu wake ,mtazame Bwana Yesu mwanzilishi na mkamilishi wa imani yetu.. ubarikiwe na Zaburi ya 20. mama K.

 5. Dada Tukuh pole.
  Ninachopenda kukusaidia usipende sana maneno ya faraja hayatakusaidia sana na utapoteza muda mwingi sana ukisumbuka na mwisho utamlaumu Mungu kuwa wewe hajakusikia ukawa umefanya dhambi nyingine.
  Yuko mume unayeweza kumpata wewe mwenyewe kwa kwenda kupatana na mwanaume (a man of your choice) bila kumshirikisha Mungu. Lakini yuko mume unayeweza kumpata kwa kumuomba Mungu na akakupa kweli na wengi wamepata.
  Mume wa kutoka kwa Mungu ana masharti kumpata, maana ni kweli “mke/mme mwema mtu hupata kutoka kwa Mungu.) Kubwa zaidi Mungu huwa hatoi vitu vya dezo hata mke/mme kwa dezo. Iko gharama ya kumpata huyo mume. hapa sitaki kuzungumza juu ya gharama hizo maana zinahitaji kuzama sana katika Mungu. Ushauri wangu ni huu hapa:
  i) Usibadilishane mawazo na watu wengi au kushauriwa na watu maana watakupa habari za matatizo yao zaidi na hivyo watakutoa katika mstari mwisho utakata tamaa.
  ii) Ujue kabisa kuwa wewe huna Mungu wa kwako vinginevyo angekuwa amekusaidia. Ila naomba uelewe kuwa wako ambao wana Mungu na sisi tunajibariki kwao tu. Km Mfalme Nebukadrezza akasema watu wote na waabudu kwa Mungu wa Danieli Je? unaonaje mambo aliyofanya Danieli? Kwahiyo yuko Mungu wa Samweli, na Yuko Mungu wa Mitume na Manabii. Nenda kwa hao kamtafute Mungu wao atakusaidia na sio kila mtu. Maana Mungu kuna mahali ameweka jina lake ukienda hapo hilo jina litakutoa katika shida zako. Mungu akusaidie.

 6. Sharom watumishi nazidi kusema nashukuru kwa michango yenu mizuri na Mungu wangu awabariki sana.

 7. Dada Mpendwa,

  ……………………………..

  wafuatao ndio watu muhimu kwako wa kubadilishana nao mawazo badala ya mume unayemtafuta:

  1. Badilishana mawazo na Yesu Kristo katika maombi na dua naye Yesu atakupa mawazo mazuri ya maisha haya na yale ya milele.

  2. Tafuta wanawake wacha Mungu hasa wale wenye umri unaokuzidi ubadilishane nao mawazo ya kiroho na kiuchumi na kimaisha.

  ………………..

 8. Kwa sehemu kubwa jumbe ambazo watu wametoa hapa ni za kukutia moyo pamoja na kukufariji. Lakini mimi ngoja nikupe ujumbe wa tofauti kidogo!

  We dada unadeka na ungependa watu wakufariji kwa kukuonesha huruma. Ivi kama siyo kudeka tangu lini upweke wa kuoa au kuolewa unageuka na kuwa ugonjwa?
  Hata watu wanaofiwa na wenzi wao ambao ndio wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kukumbwa na upweke huwa hawadeki kiasi hiki jamani.

  Ungekuwa na tatizo la kukosa chakula, au kukosa mtoto angalau ningesema kweli unahitaji maombi ya dharula. Ni vema ukajua kuwa Mungu hatakutendea kitu kwa sababu ya huzuni unayoonesha, bali atakutendea kwa sababu ya ujasiri wa imani unaoonesha mbele zake.

  Usijaribu kujihuzunisha mbele za Mungu kwa ajili ya kupata mume, bali endelea na shughuli zako huku moyoni mwako ukimwamini Mungu. Kuwa bize na mambo yako na wala usijaribu saaana kumwonesha mwanaume yeyote kuwa una uhitaji saana wa kuolewa, utapata galasa.

  Wanaume pia huwa wanaangalia mtu ambaye yuko bize na mambo yake, kuliko mtu ambaye ameinua macho na masikio yake kwenye kuolewa tu.

  Si lazima kuwa dawa ya kuondokana na upweke ni kuwa na mwenzi, unaweza ukawa unaongeza msiba.

  Unahitaji mwanaume wa kuondoa upweke upi?;

  Je ni mtu wa kubadilishana naye mawazo? Kabla hajaja badilishana mawazo na marafiki zako

  Au je ni mtu wa kukuondolea hisia za mahaba? Kabla hajaja utiishe mwili kwa kutosikiliza sana unatakaje, pamoja na mazoezi ( wewe ni askari bana)

  Haya mambo yote kwa watu walio bize huwa siyo ishu kabisa. Huwa yanajitatua yenyewe tu bila hata ya ku-struggle. Usisikilize sana wasemavyo watu fulani au ile hali inayokwambia kuwa utapitiliza muda.

  Sikia dada,usiruhusu shetani akunyanyase na vijihisia vya keupweke, komaa na shughuli zako za maisha na kumtumikia Mungu utashangaa mtu makini atakufuata kwa wakati usioutegemea.

  Tena wewe ni soja, just uambie mwili unyamaze na hisia zake kwa jina la Yesu, na utaona mambo yanajipa.

  Sikiliza wimbo wa Ambwene Mwasongwe – Misuli ya imani!!

 9. Nimeguswa na jambo lako dadangu, wapendwa wametoa mchango mzuri me nakuongezea LUKA 1:37

 10. Pole sana dadangu.ila mungu mwenyewe ywajua kwanini upitie hayo.atakusaia kwa wakati wake.

 11. *Upendo Wenye matokeo; tafuta watu ambao unawajua au unadhani wanaHITAJI KAMA LAKO wale unaowafahamu waandike majina yao,
  *Weka mkakati wa kuwaombea ili wapate kile ambacho unafikili wewe ungehitaji kwanza (MUME). Kila wakati waombee hao wala usijiombee kibinafsi kuhusu hilo,
  *Pata muda katika huo wa maombi watabirie NDOA zenye mafanikio na ujitabirie nawe pia; kinywa chako kimepewa uwezo wa kuumba.

 12. dah! ni mtihani tu wa maisha, shinda mtihani dada yangu, wako yupo Mungu amekuandalia, jiandae kumpokea na uendelee kumshika sana YESU nakusihi sana Usimwache!!!

 13. Mimi nitakuombea dada yangu, ila tu jitahidi usitoke nje ya mapenzi ya Mungu ili maombi yetu
  yasiwe kelele na kupata pingamizi,Bwana hawahi wala hachelewi jipe moyo,itatusaidia nini
  tukipata vyote duniani(i.e mume/mke) kisha tukaikosa mbingu so katika hili mtegemee Yesu
  mpaka mwisho!

 14. Mpendwa Tun Bwana Yesu asifiwe,
  Nakushauri usubiri wakati wa Bwana kwani Mungu huw hawai wala hachelewi na mipango ya Mungu sio kama ya wanadamu.Kumbuka kuwa Mungu alishaahidi kukupa wa kufanana naye hivyo mume wako yupo ila wakati wa Bwana haujafika. Hao wanaokukebehi wasikutishe kumbuka hata Yesu mwenyewe pale msalabani kuna baadhi ya watu walimdhihaki. Sisi tuliookoka hatuishi kama wanadamu wanavyotaka ila kwa neno la Mungu. Hata mimi ninashida kama yako na nimeanza kumwomba Mungu anipe Mume toka 2007 na Mungu alinijibu ila bado wakati wa hayo majibu kudhihirika katika mwili. Ni kweli kuwa makanisani kuna vijana wengi lakini kumbuka kuwa kila mtu ana mume/mke wake kutoka kwa Bwana na yeye ndiye pekee anaejua mume wako yuko wapi. Cha msingi ni kudumu katika maombi na kulishika neno. Toka nimeanza kusoma Biblia sijaona sehemu inayoonesha ukomo wa kuolewa au kuzaa. hivyo yasiyowezekana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana. Hakuna mtu aliyemtegemea Mungu akachwa aadhirike. Bwana akubariki na akupe haja za moyo wako.

 15. UWE NA AMANI itokayo juu dada. kwa BWANA kila mmoja ana wakati wake, tena ambao hakuna ajutaye ukifika. BWANA ANAMTENGENEZA ALIYE WAKO. kumbuka wewe umetwaliwa katika ubavu wa MWANAMME (MUME WAKO). Mshukuru na Kumshangilia MUNGU MPAJI WAKO. kumbuka, Mathayo 7;7. angalia usije ukawa unachanganya nyakati na majira. wakati wa kuomba, omba; kutafuta, tafuta; kubisha, bisha. wewe je unajua uko wakati gani? nenda SAMBAMBA na MUNGU. WKO YUPO TAYARI. JE, UMEJIANDAA KUMPOKEA? VAA utu wako wa ndani. MWOMBE MUNGU AKUUMBE UPYA VILE MUMEO ATAKAVYOKUKUBALI KUWA UMETOKA KWA BWANA. BARIKIWA NA ZABURI 16:1-2.

 16. Sharom watumishi.
  Asanteni kwa ushauri mzuri wenye kutia moyo. na Mungu wangu azidi kuwatumia ktk hili.
  Mungu wangu awabaliki.

 17. hili suala la kuoa na kuolewa naona limekuwa tete sana kwa wapendwa wa TZ…hebu tujaribu kwa kina kulichambua hii ishu ndugu zangu…yaani vijana wote waliookoka wanashindwa nini kuwaoa dada zao wapendwa?.maana hivi vilio vimekuwa vingi sana..tatizo hasa lipo wapi jamani?..tena siku hizi idadi ya wasichana wanaompenda Bwana imeongezeka sana kuliko zamani maana zamani ilikuwa ni wamama tu lakini siku hz wadada ambao hawajaolewa ni wengi tu wanaompenda Mungu…Je tatizo ni wakaka waliookoka kushindwa kuchukua maamuzi ya kuwaoa dada zao?.au ni nini hasa kwa kweli?au wadada waliookoka wanachagua sana?.

  Felix

 18. Mpendwa TUN,
  Usife moyo hauko peke yako. Tupo wengi tulio na kilio kama chako…lakini tunasonga mbele kwa moto. Upweke utatupisha wala co cc kuupisha.
  C kama Baba haoni ama hajui haja zetu (anayajua yote hata kabla hatujamwomba) narudia UCFE moyo.

  Ili uwe mke na mtumishi bora wa Mungu lazima kuna gharama za kulipa ikiwa ni pamoja na hili la kukubali mapenzi ya Mungu yatimizwe maishani mwako. Co rahic but km kweli unataka kuwa salama ktk wokovu wako sharti umngoje BWANA sbb wakati wake ni sahihi zaidi zaidi. masimango ya watu yackutoe kwenye mstari. watasema wala hutanyofoka hata ngozi mwilini mwako. Shinda kila jaribu b4 you.

  Binafc mm ni mkubwa kuliko ww na cjaolewa japo nimetamani sana tangu nikiwa binti mdogo. Japo utu wetu wa nje unachakaa but wangu my dear, laaaa unalipa. Ninarejeshewa ujana wangu km tai kila uchao. Hutaki sasa, c neno la Mungu lasema hivyo. Nimelishika ninamdai aliyeniumba mwanamke maana anajua ni lazima niwe na mume tena wangu mwenyewe. na anajua fika tabia za ndg zetu hawa, sura mbele kiroho baadaye, Wachungaji mpo? Tusaidieni maana msipotia bidii ktk hili nalo kwa mabinti na vijana kuna watu kufika mbinguni wakiwa chokest.

  Mara ya mwisho Mungu kunambia anashughulikia mambo yangu (baada ya kumbana sana kwa habari ya ndoa) ni miaka 3 ago. Tena hapa Mungu alisema kwa sauti.
  Ckuchoka kuendelea kumuuliza na kumkumbusha. Huwezi amini Mungu amenipa Mchumba HAJAOKOKA. Kila nilipohoji inakuwaje BWANA alikaa kimya. Cku nimeamua kughair uchumba ule alikuja mtumishi mmoja home nikampa picha ya mchumba wangu nikamwambia aombee picha ile tuwe na hakika km kweli ni Mungu ameruhusu. Palepale RM alijibu kuwa sihitajiki kuendelea kuomba bali NIMSHUKURU MUNGU.(kwangu ni mtihani mwingine, Kwake Imekwisha) Neno hili limethibitishwa na watumishi wa2 tofauti. Wewe ungefanyaje? naendelea kumngoja BWN amtengeneze, mpk lini? mi sijui.

  Nataka tu kukuonesha kuwa UPWEKE co wako peke yako, kuuendekeza na kutafuta suluhu ya fasta fasta co SOLUTION ya kudumu.
  1.Zingatia ushauri wa ndg zetu waliokupa na ungojee wakati wa BWANA ambao ni sahihi zaidi tena hauna majuto.
  2.Ikatae roho ya upweke maana ikikutawala utaanza kuzini kwa kutamani vya wengine na mwishowe utafanya masterbation. ucruhusu ht kidogo upweke ukutawale kwani utajikuta pabaya kuliko ulivyotarajia.
  3. Jipe muda wa kutosha ktk kuomba, kusoma na kutafakari Neno la Mungu. Mtafakari Yesu na ukuu wake, utajaza hazina kubwa ya mbinguni moyoni mwako na upweke utaondoka bila hata kukemewa. (mume utapewa kwa ziada ukiupata ufalme wa mbinguni)
  4.Mruhusu Yesu Kristo akuondolee magamba yote ili ufae kulika kwake na kwa mumeo. (asomaye na afahamu)

  Yote kwa Baba wa mbinguni yanawezekana kaa tu kwenye mstari. Ameolewa dada wa rafiki yangu akiwa na 67 yrs na hakuwahi kuolewa, cc ni nani Baba atusahau?

  Tiwa moyo, Mungu hajatuacha tukubali tu kutolewa magamba.
  Mumeo anakuja, subiri.

  Gladys

 19. Pole na hongera kwa msimamo wako wa rohoni Mungu atakujibu kwa wakati wake.
  Naomba nikupe ushauri mdogo tu.
  1. Kwakuwa sasa umeokoka ni vema na slama ukapata Mume kutoka nyumbani mwa bwana ingawa pia nilazima umchunguze maana wapo waliovaa ngozi ya kondo lakini ndani ni chui.
  2. Kwa maelezo yako huko nyuma kabla hujaokoka ulifanya kosa kwa kudhani kuwa ukimpa mume mtarajali mapenzi ndio nafasi ya kukuoa kumbe sivyo wakati mwingine ndio unaharibu kabisa

  3.Ni vema kabla hujaanza mahusiano na mtu uone kuwa mnavigezo vinavyoambatana (common interest), wote mnapenda vitu vinavyo fanana
  4. Wanaume wengi huoa kwa msukumo kutoka upande wa binti, unapompata unayemkubali nafsini usimpe nafasi mbane kwa upendo, adabu, upole, na msimamo akuoe.
  5. Muda wa uchumba au urafiki usiwe mrefu sana utaleta mazoea na kudharauliana kwa kujuana udhaifu hivyo kulegeza nia ya ndoa.
  6. Mwili unachakaa na kupoteza uzuri wake jinsi siku zinavyokwenda ni vema kujipanga mapema kabla ya muda kupotea punguza msimamao mkali na kuwa flexible lakini makini maana wanaoume huwaogopa wanawake wenye misimamo mikali
  7. Mungu nimuaminifu atakupatia haja ya moyo wako tunaendelea kukuombea
  sallu

 20. pole sana kwa uchungu Mungu atakutuoa huo uchungu sali sana hiyo roho ya uchungu iondoke na ujazwe nguvu za Roho mtakatifu.samehe na sahau yote yaliyokukwaza hapo nyuma,nmekuelewa uliposema hauhitaji chochote zaidi ya salam ni kweli maana kuna vijana wengine mkianzisha mazoea anarudi kukutakla tena kimapenzi wakati tayari alishaoa bora uepuke vishawishi kw akukaa naye mbali.Mungu ni mwaminifu atakupatia mume mwema kw awakati muafkaa usijali kuona wengine wameolewa wewe bado muangalie Mungu na kila siku umkumbushe haki yako atakupatia.Kila la heri mpendwa!

 21. “”Kwani wakati mwingine nashikwa na upweke wa ajabu, ukizingatia sina wazazi ndugu wametawanyika na mwanangu bado mdogo siwezi kubadilishana nae mawazo.
  ni mimi tu ambaye sina ndoa. Hii hali inaniumiza sana maana kuna watu wananinenea maneno ya uchungu juu ya hili””

  MANENO HAYO YAMENIGUSA :
  Mdada huyo amempokea Bwana?

  “”Binafsi ni mwingi wa msamaha lakini nina misimamo isiyoyumbishwa, nilimsamehe lakini sikuhitaji uhusiano wowote nae zaidi ya salaam.””

  1.Basi Dada huyu ampokee Yesu kama Mwamba katika Maisha yake. Ili Yesu aweze kuwa dira ya Maisha yake.
  2. Kusamehe na kuachilia kila jambo moyoni, ili Mungu apate nafasi tena ndani ya Moyo wake aanze kutenda kazi za “kuifanya mioyo ya Baba iwaelekee watoto, na ya watoto iwaelekee Baba zao””
  3.Kuacha kabisa kukwazika na kulalamika.ili MUNGU asighairi baraka zake kwako.
  4.Kumjua MUNGU sana kutamletea amani, UPWEKE UTAONDOKA, na MEMA (yaani Mume ambaye yeye ni mke wa Ujana wake) atamfuata…
  5.Kisha anza kumletea Hoja zako za nguvu Bwana wa Majeshi, maana yeye ni MUME wa wajane, na Baba wa watoto yatima..hapa utaanza kuwa TUNU na Baraka kwa Ndugu zako na watakutafuta WEWE uwape majibu.
  6. Usiumizwe MOYO na hali hiyo, bali UUTUNZE moyo wako UULINDE kuliko kitu chochote ili maji ya uzima yaanze kutiririka kwenda kuiponya miti pembeni ya mto na kuyaponya maji ya Chumvi.uwe na LUGHA nzuri yenye zaburi inayobariki wengine.

 22. Mungu akutie nguvu kumngoja Bwana sio kupoteza muda as longer unaye Yesu jua umepata kila kitu tena Yesu anaposema ndiyo hapana awezaye kubatilisha nitakuombea kwa Mungu wetu naye atakujulisha nani ni mwenza wako wa ndoa ubarikiwe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s