Shetani alimpelekaje Yesu kwenye mji Mtakatifu?

mathayo
Kisha ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu”  Mathayo 4:5

Swali; inawezekanaje Yesu mwana wa Mungu anaweza kuchukulia na shetani? ktk hali ipi? ya kimwili au kiroho au ‘akamchukua mpaka mji mtakatifu’  kwa namna ipi naomba ufafanuzi wenu wapendwa.

–Siaka   Nyanchiwa
Advertisements

8 thoughts on “Shetani alimpelekaje Yesu kwenye mji Mtakatifu?

  1. Bwana yesu asifiwe.

    Ibilisi alimchukua Yesu mpaka mji mtakatifu kwa dakika moja nilivyoelewa mimi ni kwamba shetani alimteka Yesu katika mwili na si roho akijua kuwa atashawishika. Yesu alivyokuja duniani alivaa mwili tu lakini yeye alibaki kuwa Mungu. Hili ni andiko ambalo liliandikwa ili utimilifu wa kazi yake ya ukombozi ikamike na pia kutufundisha kuwa tukimpenda MUNGU tusipende vya dunia.

  2. “Kisha ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu“ Neno ibilisi akamchukua ni dhahili kabisa kwani gari pamoja kuwa limetengenezwa na watu lakini bado linawabeba watu hao hao

  3. Yesu alipozaliwa na mariamu ili awe km binadamu wengine ila alikuwa roho wa wa mungu kwahiyo alipojaribiwa na shetani ilikuwa vigumu kwa kuwa mungu alikuwa pamoja naye tofauti na sisi tuliozaliwa ktk dhambi na laana za mababu zetu.

  4. Ni katika Roho, Shetani hawezi kumgusa Yesu kwa vyovyote vile. Jinsi tunavyojaribiwa kupitia mawazo ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu, Shetani alimjaribu kupitia mawazo tu. Barikiwa.

  5. Sorry Siaka Nyanchiwa kwa makosa ya uchapaji naomba isomeke akamchukua hadi mji mtakatifu na sio mwili mtakatifu. Ahsante.

  6. Ukisoma pia habari hiyo katika injili ya mtakatifu Luka uanaweza ukapata mwanga fulani. Safari ya Kuelekea jangwani alikuwa katika hali ya mwili akiongozwa na ROHO ili ajaribiwe na shetani kwani ilikuwa ni lazima katika kumkamilisha kiongozi wa wokovu wetu naye apitie mateso na majaribu yale yale ambayo sisi tunapitia. lakini katika kumjarbu, shetani hakuja katika mwili bali alikuja katika roho. akamchukua hadi katika mwili mtakatifu akampandisha katika kinara cha hekalu au akamchukua hadi mlima mrefu na kumwonyesha milki zote za dunia kwa dakika moja. Ni wazi kuwa katika mwili na kwa dakika moja isingewezekana kuonyeshana milk zote za dunia. Hivyo ndivyo mimi nifikiriavyo. kama kuna wapendwa wana mawazo tofauti basi wanaweza wakatuelimisha zaidi

  7. Yesu alisikia njaa kwa sababu alikuwa na mwili wa kibinadamu kabisa na alikuwa anasikia maumivu kabisa, na alikuwa na hisia za kibinadamu kabisa kwa sababu ya mwili aliokua nao. Hivyo anapoambiwa kuwa ageuze mawe yawe mkate maana yake aliumwa na njaa. Habari ya shetani kumchukua haipo ila yale yalikuwa ni mawazo yaliyoletwa na shetani kwa sababu jaribu lilifika mahali pagumu sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s