Unaweza kuzaa bila utungu! – Mtazamo

ujauzito

KWA mama aliyeokoka (au mwanamke aliyeokoka) hatakiwi kuzaa kwa uchungu …Kuzaa kwa uchungu ilikuwa ni laana kabla ya YESU kuja..lakini kwa wale waliokoka laana hiyo haitakiwi kufanya kazi kwao…..kwa hiyo chukua neno la Mungu linalosema kuwa Umekombolewa toka laana na mengine yanayohusiana nayo Uyaamini na kuyakiri kila wakati then Utazaa bila uchungu.  Wapo waliozaa bila uchungu wanaishi kwa kuwa waliami kuwa Wamekombolewa toka laana hiyo…AMEN

Moses Kwabhi

Advertisements

33 thoughts on “Unaweza kuzaa bila utungu! – Mtazamo

 1. I’m amazed, I have to admit. Rarely do I come across a blog that’s both equally
  educative and amusing, and without a doubt, you have hit the nail on the
  head. The issue is something which not enough men and women are speaking
  intelligently about. I am very happy I stumbled across this during my search
  for something concerning this.

 2. Thanks sister Dolly for helping me out ..
  No more pain .. Whatsoever … We have been redeemed from that by Jesus Christ..

 3. Duh! Mkandya ndg yangu, mbona umeamua kunipaka matope nisiyostahili!
  Tumejadili vizuri kabisa, sioni ni wapi nilipokuletea dhihaka kama unavyodai, au ni kwa vile sikulizungumzia jambo hili unaloniambia, “Mwishowe utasema kuwa na ule msukumo tulio nao wa haja ndogo nao ni laana”?

  Mambo mengine ni kama yalivyo, huu mfano wa dada Dolly unaosema mambo hayo unayajua kwa zaidi ya miaka kumi, huu ndio uliotufikisha katika kukubaliana kuwa kabla ya Anguko uchungu haukuwepo, vinginevyo huko kuzaa kwa dada huyu bila uchungu/utungu itakuwa ni jambo jipya kabisa tangu kuumbwa kwa mwanadamu, jambo ambalo sidhani ni sahihi, pia nawe silo unalolisema!! Au wewe ni nini unachosema, kwamba uchungu ulikuwepo kabla ya Anguko na baada ya hapo ukazidishwa, halafu Kristo alipokuja akauondoa kabisa, hata ule wa kabla ya Anguko? Kwamba sasa amemuumba upya mwanamke akiwa bora kuliko pale mwanzo, kwamba kulikuwa na makosa? Hebu kiseme straight unachotaka kusema halafu tunaweza kuendelea katika tofauti zetu, at least at this while!

  Kuhusu hizo koma zilizohamishwa, sijajua unachokilalamikia ni kipi. Wasabato wamehamisha hiyo koma ili kupotosha ujumbe wa Injili kutoka katika maana halisi ya yule mwivi kuingia paradiso siku ile pale Kalvari na kuisogeza mbele ili kuleta maana inayokubaliana na fundisho lao la kwamba mwivi yule ataingia huko mbele katika siku ya ufufuo! Tena kuhamisha huko hiyo koma kunaifanya ile 1Petro 3:18-20 “…mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, …” wao hukikataa kifungu hiki kumaanisha hivyo kinavyo maanisha nao hukirudisha huko nyuma ili kukidhi fundisho lao lisemalo ukifa unabaki kaburini, mpaka huko katika ufufuo!!! Kwahiyo mimi nina ulazima gani wa kuyakubali mambo ya jinsi hii? Au kuliweka kwangu wazi jambo hili ili nanyi muwaone hao wanaoyapindisha Maandiko, ili mjihadhari nao, unaniona ni kama mtu ninayejidai? Basi kuna haja gani ya kuandika humu kama tutakuwa tunaogopa kuyaweka wazi yaliyopotoshwa, au kujadiliana kwa maana ya kujifunza? Au kwa vile wewe ni msabato, ndio umechukia na kuamua kunipaka matope nisiyostahili?

  Kimsingi hata mimi sioni tutaendelea katika lipi kwenye mada hii maana mawazo yetu yalikuwa sawa, tulipishana katika tafakari tu ambayo sasa imeoana!

  Nami nakushukuru kwa mawazo na majadiliano kwa kadiri ya umbali tuliofika, ninaamini wengi wamefaidika!

  The Lord bless you, my brother in Christ!

 4. Lwembe mojawapo ya shida yako kubwa ni dharau na kejeli ambazo hazina faida yoyote. Ndio maana kuna watu unapovutana nao katika mijadala inafika mahali mnaanza kutukanana matusi ya rejareja, na hii si mara yangu ya kwanza kukwambia hivyo.

  Mimi huwa sipendi dhihaka za kipuuzi. Na kwa sababu sihitaji kufikia mahali pa kujikuta na mimi natoa matusi ya rejareja, tufanya kama moja ya kanuni ya majadiliano (negotiation) inavyosema kwamba tukubaliane kutokukubaliana.

  Kumbuka katika mjadala wa ‘ni mti upi Hawa alitwaa..’ ulijaribu kuonesha kuwa unajua ujuzi wa matumizi ya koma kwa kujaribu kuonesha mahali fulani kuwa ile koma inaonesha kuwa kinachofuata baada yake ni kitu kisichohusika na kilichosemwa kabla ya hiyo koma. Kwenye suala la baraka katika Mwa 2:28 inataka kung’ang’aniza mantiki nyingine.

  Kumbuka point kubwa katika mjadala huu nikuona kama inawezekana leo kwa mwamini kuzaa bila utungu uliozidishwa.
  Kuamini ni kuchagua, mtu akichagua kuamini,yote yawezekana kwake aaminiye.

  Kwa kifupi ni kwamba wewe amini unavyoamini, kama ni kuendelea kuzaa kwa utungu uliozidishwa amini hivyo.
  Na mimi naendelea kuamini kuwa leo katika neema hii ya kristo mtu akiamni anaweza kuzaa bila huo utungu. Na mfano mmojawapo ni dada Dolly katupa huo ushuhuda.

  Hakuna kitu cha maana sana ambacho tutaendelea kujadili hapa Lwembe. Zaidi ya kujaribu kuoneshana ufundi wa kujua. Jambo la msingi limeshafahamika,na kila mtu mwenye kujifunza ameshajifunza linalomfaa

  Nashukuru kwa mchango na mda wako.

  Mimi nimemaliza.

  Ubarikiwe.

 5. Mkandya, mimi huwa sipendelei kupresume katika mambo ambayo yako wazi. Sijajua umekwamia wapi katika understanding ili nikusaidie, maana jambo la uzazi liko wazi sana. Unapozungumzia uzazi ni lazima kuwepo na hicho kilichozaliwa ili ijulikane unachoongelea. Sijaona mtoto yeyote yule aliyezaliwa kabla ya anguko, kwahiyo huwezi ukalisemea jambo ambalo halipo!

  Pia sijaona mahali popote kulingana na kuumbwa kwa Adamu na mkewe, panapo elezwa kuhusu uchungu wala utungu, ninachokiona ni declaration ya Mungu kuhusu vyote alivyoviumba, “Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.” Mwa 1:31; hii ndio state of PERFECTION ninayoiona mimi kulingana na jinsi ninavyomuamini Mungu katika Neno lake, unless neno “chema” linajumuisha na “uchungu na utungu” jambo ambalo sidhani liko hivyo!

  Pia hali ya mtu aliyeanguka matopeni haifanani na ya yule aliye safi! Kwahiyo huku kuzaa na jinsi yake inayoendelea, ni jinsi ya matopeni, ndipo huwezi ukadraw conclusion from a perverted issue na ukalipata jibu katika usafi! Mimi nimezaliwa katika pervasion, lakini nafahamu kuwa jinsi hii si katika Mapenzi Makamilifu ya Mungu, ndio maana nimesema sijui wangezaaje katika perfection, iwapo wangesubiri tungelijua hilo, kwahiyo linabakia kuwa ni siri ya Mungu!

  Tunapozungumzia “kuzidisha”, ninaamini sote tuko katika maana moja, kwamba unakizidisha kilichopo. Tunatofautiana katika kukamata hicho kilichopo, wewe unasema kwamba Uchungu na Utungu wake ni sehemu ya Perfection ya Mungu, kwamba alipomuumba mtu na huo utungu na uchungu vilikuwa ni sehemu yake. Hilo ndilo linalonishangaza, kwamba uchungu anaoupata Eva katika uzazi ni furaha ya Mungu!!!

  Lakini ukweli ni kwamba kule kuanguka kwao kumekuja na mambo mengi sana, uchungu na utungu vikiwemo katika package hiyo. Hauwezi ukadondoka katika matope halafu ukawa safi! Nao uchafu wowote ule huashiria kifo, ndio maana mchafu huhitaji kusafishwa. Kumbuka sheria ya Mungu iliwatangazia kifo iwapo watayala matunda ya mti waliokatazwa, na sidhani kama kuna kati yao aliyewahi ku experience kifo kabla ya kuanguka. Uchungu/utungu ni sehemu ya hicho kifo, yaani ni hatua za kukiendea kifo kamili! Basi kutokea hapo ndipo Mungu anavizidisha hivyo vilivyomo ktk package hiyo ya kifo!!

  Kwa kadiri ninavyokufuatilia katika haya unayoyasema, naona umelielewa vizuri sana jambo hili, kuwa katika mpango wa Mungu kwa wanae, ktk huko kuzaa na kuongezeka’, mambo ya uchungu na utungu hayakuwemo! Labda unashindwa ku connect mwili na roho ili roho ipate kuuongoza mwili! Maana naiona roho yako ikikubaliana kabisa na Perfection ya Mungu kwamba hakuna jambo la uchungu, lakini unarudi mwilini tena unaanza kuutilia shaka ufahamu huo, ndipo unauona uchungu kuwepo kabla ya Anguko!!!

  Hebu itazame kauli yako hii, “Na mimi nakubaliana na wewe kuwa huko ni kuionja ile hali ya kabla ya anguko, maana alihisi kama vile tumbo linapapaswa tu.” Hapa unakubaliana nami kuwa kabla ya Anguko kulikuwa hakuna Uchungu wala Utungu, tena unaendelea kunisisitizia, “Lwembe mimi hili suala nimelifahamu zaidi ya miaka kumi iliyopita, si tu kutokana na ushuhuda wa dada Dolly”!! Basi bakia ktk ufahamu huu, huu ndio ufahamu correct wa Maandiko!!!

  Kuhusu Neema katika kuyapitia machungu ya maisha, hiyo ndiyo nguvu inayotupitisha katika hayo tukimshukuru na kumtukuza Mungu kinyume na walio nje! Maana neema haiji mbinguni wala katika mileniamu, hiyo yaja kikombe kinapojaa, nawe utaijua kwa kadiri inavyokuokoa! Kuhusu adhabu kuwepo kwa Adamu, hilo bado linaendelea, ndio maana ninamuhitaji Bwana anitangulie katika nyendo zangu zote ili anishindie katika yanayonikabili katika hiyo adhabu. Kwahiyo Mkandya sasa hivi unakula laiiiniii…! Duh uko wapi ndugu yangu nami nikufuate huko uliko?

  Mwa 1:28, unasema kila fungu la maneno linajitegemea! Well, sijajua inakusaidia nini kuvitenganisha vifungu hivyo, labda niyasubiri maelezo yako! bali baraka zilizomo katika sentensi hiyo, zinalifunika mpaka jambo la uzazi, au wewe hujawahi kusikia watu wakisema nimebarikiwa mtoto wa kiume/wa kike? Labda kwa vile unaishi katika dimension nyingine, huko usikotoka jasho!

  Kuhusu kuzaa bila uchungu leo hii, kwamba sasa unaelewa kuwa kuzaa kwa uchungu si jambo la asili, basi unapoamini kuwa unaweza kuzaa bila utungu, sidhani kwamba kuna jambo ambalo Mungu hulifurahia kwa watoto wake kuzidi Imani iliyo ndani yao! Ukifikia kuliamini Neno la Mungu, basi yote tunayo ahidiwa ni mali yetu, kama unaweza kumchallenge Mungu katika hilo, basi utakula bila jasho!! Hebu isome 1Tim 2 yote, uzione conditions zinazopasa kabla huja mwambia mkeo!

  Asante sana!!!

 6. Ndugu Mabinza umejitahidi kujibu, japo swali la mwisho hujalijibu kwa maana hakuna kifungu kwenye biblia. Lakini pia swali la Eva alianza lini kuwa mke wa Adamu, kabla au baada ya anguko, jibu lako si sahihi maana mstari uliotoa wa Mwa 2;6 hausemi hivyo.

  Lakini ningekushauri jambo moja kuwa fikiria sana kama Eva alikuwa mke wa Adamu kabla ya anguko halafu uone kama kama walikuwa mume na mke bila tendo la ndoa.

  Pengine ungesoma mistari hii Mwa 2:24. Therefore shall a man leave his father and his mother, and shall cleave unto his wife: and they shall be one flesh.

  Unaweza sasa mwenyewe kusema kama kuliwezekana kuwa na dhana ya mwili mmoja bila ya tendo la ndoa. Maana hayo maneno yalisemwa kabla ya anguko. Sasa sijui kama yalisemwa kwa kutabiri kuwa mwanadamu atakuja kuanguka na ndipo suala la kuwa mwili mmoja lianze kuwepo.

  Halafu unaonaje wewe bwana Mbinza, ivi tunapotoa haja ndogo yaani kukojoa, na yenyewe huwa ni aina moja wapo ya utungu.
  , ambao yawezekana Adamu na Eva walikuwa wanakojoa kwa namna ya starehe zaidi kabla ya anguko?

  Ubarikiwe sana.

 7. Lwembe unasema hujui kama wangezaaje lakini unasema wasingezee kwa njia hii ya sasa; unaposema kwa njia hii ya sasa unamaanisha nini; je unamaanisha kwa njia ya kukutana kimwili na mwanamke kubeba mimba kisha kuzaa mtoto?

  Lakini pia kama unakiri kuwa hujui wangezaaje mbona hii njia ya sas unaikataa kuwa isingekuwa yenyewe? huko kutokujua kwako ni kupi hasa?

  Halafu Lwembe mataumizi ya neno kuzidisha nafikiri hatuelewani. Kuzidisha ni neno la mlinganyo, kuwa unazadisha kitu kwa kulinganisha na kitu kilichokuwepo. Haiwezi kuwa kweli kwamba Mungu aliamua Eva azae kwa utungu uliozidishwa,lazima ujiulize aliuzidisha kutoka wapi. Kama ingekuwa tu ni utungu mkali basi angesema utazaa kwa utungu mkali. Huwezi kutoa kitu ukasema kimezidishwa bila kuwepo kwa kitu cha awali ambacho kilichozidishwa kilizidishwa katika hicho.

  Halafu Lwembe usiniwekee maneno kinywani kwa ujanja, mimi sijakiri laana, wewe ndio unafikiri kuwa nimekiri laana kulingana na mtazamo na ufahamu wako. Najua unasema nimekiri laana kwa kusema kulikuwa na kuzaa kwa utungu usiozidishwa. Mwishowe utasema kuwa na ule msukumo tulio nao wa haja ndogo nao ni laana.

  Unasema tumeletewa ya kutusaidia kupita katika mambo hayo; mambo yapi hayo na tunapitaje? hebu fafanua
  Maana kama neema ipo kutusaidia kwa nini hutaki kukubali suala la kuzaa pasipo utungu uliozidishwa? Maana neema kwa kifupi ni kupata ambacho ulikuwa hustahili na inaenda sambamba na rehema ambayo ni kutopata adhabu uliostahili.

  Ni vema sasa ukaelewa kuwa kwa ujio wa Yesu kristo tunapata baraka ambazo haikuwa haki kwa sisi wenyewe kuzipata, na tunaondolewa/hatupati adhabu ambayo tulistahili kupata.

  ” Kama Eva ameondolewa kuzaa kwa uchungu katika ujio wa Kristo, sioni kwa nini naye Adamu asiondolewe adhabu yake!” Hivyo ndivyo umesema Lwembe. Adhabu ipi ambayo Adamu hajaondolewa Lwembe, je ya kula kwa jasho na kuchomwa michongoma? Vipi wewe unakula kwa jasho bado?

  ”Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, …” (MWA. 1:28 SUV)
  Lwembe kuna koma za kutosha tu kutoka kwenye neno “Mungu akawabarikia” mpaka kwenye maneno ”zaeni mkaongezeke”.
  Kwa nini huoni kuwa maneno ”Mungu akawabarikia”, na maneno ”zaeni mkaongezeke kila fungu la maneno linajitegemea?

  Lwembe, narudia kusema nilichosema kuwa suala hili si lazima wewe au mtu mwingine aamini kama mimi na dada tnavyoamini. Wewe kama unaona ni sawa leo kuza kwa utungu uliozidishwa mfundishe na kumwaminisha hivyo hata mke wako pia.
  Lakini mimi naamini unaweza kuzaa bila huo utungu na nitamwambia hivyo pia mke wangu.
  Ubarikiwe

 8. Mkandya,
  Kuna jambo moja ambalo ni la msingi sana, kuutafuta Moyo wa Mungu! Unapofika katika kujiaminisha mawazo yako, kuwa katika Baraka za Mungu ndani yake kuna uchungu, hilo laonesha kuna shida mahali fulani katika kumjua kwako Mungu. Aidha unamjua intellectually, au humjui kabisa! 

  Huko kuzaa bila utungu na uchungu wake kabla ya anguko ninakokuzungumzia mimi, ni kulingana na Neno alilolitamka Mungu. Kwamba nafahamu Mungu akisema, inakuwa hivyo; lini? Hapo ndipo panapohitaji subira iliyojikita katika Imani! Ibrahim aliisubiri Ahadi ya mwana kwa miaka 25, ninaamini kama ungepita hapo nyumbani kwake unauza vinguo vya watoto, akiona ni kizuri basi angemwita mkewe, halafu akakinunua, nawe ungemuuliza, yuko wapi mtoto mwenyewe? Mwishoni ungewasimulia chinga wenzako kuhusu yule mzee ‘chizi maarifa’ anayenunua vinguo vya mtoto asiyekuwa naye!

  Lakini, Mungu aliwabariki, wangezaaje? Mimi sijui, kama wangesubiri, wangeelekezwa, ila jambo moja ninalolijua ni kwamba wasingezaa kwa jinsi hii ya sasa.

  Pia fahamu kwamba dhambi haiji na asali, inakuja na kifo. Nao uchungu wa aina yoyote ile ni sehemu ya kifo. Kwahiyo ni dhahiri kwamba uchungu ni matokeo ya kuanguka, kama walivyojiona wako uchi, wakatengenezewa mavazi, basi jua kuwa kuongezewa matatizo kwa Eva, ni juu ya hayo aliyojiletea mwenyewe, naye Mungu akayazidisha!

  Kuhusu laana, tafsiri za kikamusi ni nzuri kilugha, lakini maana kamili ya Laana kiBiblia ni kama nilivyokuambia, ni kuwa cut off from the Main Stream of Life which is God! Ni kama mtoto aliyefukuzwa nyumbani, akiwa amelaaniwa, si lazima apate shida moja kwa moja, anaweza akashamiri, lakini ni kwa kitambo tu! Au uangalie ule mti alioulaani Kristo, kwani ulikauka wakati ule ule? Uliendelea kupendeza na kama ungepita hapo, ungeweza kuununua, ila ungekukaukia!!

  Pia waangalie hao waliolaaniwa, jaribu kukagua iwapo Mungu aliwafanyia lolote lile la kuwasitiri au jema lolote lile, HAKUNA! Ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa wakristo kufundishwa sawa sawa kuhusu Laana. Si wewe tu Mkandya unayeikiri laana kirahisi, bali nimewaona wakristo wengi sana wakiikiri laana, licha ya kukiri kwao kuokoka, hawaijui hatari hiyo, maana kama unavyoukiri wokovu na kuupata, basi pia laana!!!

  Pia ni vizuri ukafahamu kwamba, kuyatanguliza mawazo yetu katika mambo ya Mungu kunaweza kutuletea hasara, lakini kumsubiri yeye kuna faida kubwa. Sijaona popote pale katika Maandiko panapozungumzia Mungu kuiondoa adhabu yake juu yetu, ninachokijua ni kwamba tumeletewa Neema inayotuwezesha kupita katika mambo hayo. Kama Eva ameondolewa kuzaa kwa uchungu katika ujio wa Kristo, sioni kwa nini naye Adamu asiondolewe adhabu yake! Unaona! Usipokuwa makini unaweza kujikuta umezama katika fundisho lililokinyume na Biblia, ambalo mitume hawajafundisha, na ukaishia kulaaniwa kwa kufundisha Injili mpya, “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.” (GAL. 1:8 SUV) haya ndio tunapaswa kuyakwepa kwa bidii!!

  Hapa unaniambia, “”Umewewezaje kusema kwamba kuwa ”fruitful” (kuzaa)ni baraka wakati hakuna neno ‘baraka’ lililotamkwa hapo,”” Ninaamini utakuwa hujaisoma vizuri Biblia yako, lakini Maandiko kuhusu jambo hilo la ‘Baraka’ yanasema hivi: 
  “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi,  …” (MWA. 1:28 SUV)

  Ninaamini jambo hili litayabadili mawazo yako, ukiyatupilia mbali na kuyabadili na kifungu hicho cha Neno la Mungu.

  Ubarikiwe!

 9. Mpendwa Mkandya,
  Nimeuona msisitizo wako kuwa, nawachanganya asomaji kwa wingi wa maneno na hata mimi eti nikirudia komenti hizo sitazielewa! Sina hakika sana na hilo, ila tuliache tuje kwenye mada.Umeuliza,

  1).‘Viungo vya uzazi mwanadamu aliwekewa kabla au baada ya anguko?

  – Jibu: Kabla ya anguko.Mw.1:27’ tunatambuana tofauti za kimaumbile tokana na jinsi zetu.

  2).Eva alinza lini kuwa Mke wa Adamu, baada au kabla ya anguko?

  – Jibu: kabla ya anguko, Mw. 2:6,

  2). Adamu na Eva walishiriki tendo la ndoa kabla ya anguko?

  – Jibu: Sina jibu, sioni mahali popote kama Adamu na mkewe Eva walitenda tendo la Ndoa kabla ya anguko ama la.

  Uendelee kubarikiwa na Bwana.

 10. Bwana Lwembe, nataka kwanza nikukumbushe kitu kimoja kitokanacho na hoja zetu za awali kuhusu suala la kuzaa kwamba lilikuwepo kabla ya anguko, japo wewe ulisema lilikuja baada ya anguko.

  Nashukuru hapa umekiri mwenyewe kuwa huko kabla ya anguko kulikuweko na kuzaa bila uchungu uliozidishwa. Nanukuu: ” Nao ushuhuda wa dada Dolly ulipaswa ukufungue macho Mkandya, uone kuwa kwa kuzaa kwake bila uchungu na utungu wake, hilo litakuwa ni kuionja ile hali ya kabla ya anguko!”
  Lwembe mimi hili suala nimelifahamu zaidi ya miaka kumi iliyopita, si tu kutokana na ushuhuda wa dada Dolly

  Na mimi nakubaliana na wewe kuwa huko ni kuionja ile hali ya kabla ya anguko, maana alihisi kama vile tumbo linapapaswa tu.

  Kuna kitu nakunukuu tena hapa; ” Hivi haufahamu kwamba kabla ya anguko walikuwa wanatembea uchi na miili yao haikujaa manyoya wala haikuwa na ngozi ngumu kama ya kiboko ili kuwa kinga, bali ilikuwa ni ile ngozi laini”

  Kitu ulichokisema hapo sidhani kama unaweza kukithibitisha, mimi naona ni cha kusadikika zaidi.

  Lwembe pengine ngoja tusilitumie neno laana katika suala la kuzaa, maana tunachokijadili hasa hapa hasa siyo laana bali ni ule utungu wa kuzaa uliozidishwa ambao wewe umeuita adhabu, mimi nasema kwamba chini ya neema huo utungu uliozidishwa (adhabu) wa kuzaa kwa mtu anayeamini hatakuwa nao katika kuzaa kwake, kama ilivyokuwa kwa Dolly.

  Katika kamusi ya Collins wamefafanua laana kama ifuatavyo; if u say that there is a curse on someone, you mean that there seems to be a supernatural power causing unpleasant things to happen to them”

  Bwana Lwembe mimi naamini kuwa hiyo unayosema ni adhabu ambayo Adamu alipewa, kuja kwa Yesu kumeikomesha na kutoa nafasi ya atakayeamini kutokuwa chini ya hiyo adhabu.
  Ni kama ambavyo magonjwa na umasikini Yesu alivimaliza msalabani lakini leo waweza kuona jamii kubwa ya waamini bado wameshiliwa na vitu hivyo, kwa sababu ya kukosa ufahamu unaopeleka kuvunja kanuni za kuvipata hivyo vitu

  Umesema baraka ni pamoja na huko kuzaa na kuongezeka, lakini ambako mimi nimetafsiri kuwa ni pamoja na kuzaa kwa utungu.

  Umewewezaje kusema kwamba kuwa ”fruitful” (kuzaa)ni baraka wakati hakuna neno ‘baraka’ lililotamkwa hapo, lakini ukasema kuzidishwa kwa utungu wa kuzaa sio laana,je ni kwa sababu tu hakuna neno laana lililotamkwa hapo? Matokeo ya kitu yaweza kutosha kukujulisha kuwa kuna laana au baraka nyuma ya hicho kitu, bila neno baraka au laana kuwa yametamkwa.
  Tutaendelea na suala la kifo.
  Ubarikiwe.

 11. Mabinza sioni kama uko makini vya kutosha kutoa uchambuzi wenye kueleweka katika mada hii.

  Una maneno mengi mno ambayo badala ya kumsaidia msomaji kujua ukweli yenyewe ndio yanamchanganya zaidi.

  Hebu mwenyewe rudia makala yako uone kama utaielewa.

  Ila unisaidie kujibu swali hili: viungo vya uzazi mwanadamu aliwekewa baada au kabla ya anguko?

  Pia uniambie, Eva alianza lini kuwa mke wa Adamu,baada au kabla ya anguko?

  Ujuavyo wewe , je Adamu na Eva walishiriki tendo la ndoa kabla ya anguko?

 12. Mkandya, Dolly na wengine,
  ‘Kuzaa kwa utungu kupo vilevile, ikitokea mtu akazaa bila utungu, kunategemea anachoamini mtu huyo, maana jambo lolote likifanyika kinyume na Neno la Mungu, ni dhahili linatoka kwa Yule mwovu, maana hata kwa shetani ni imani ndiyo inayofanikisha ibaada yake! Mungu tamko lake husimama wima siku zote! Maelezo kuwa Yesu alikuja kuondoa laana, ni lazima ujue mambo mawili laana uisemayo kama kweli ni laana! Na pili ujue hiyo laana inatoka kwa nani!. Yesu alikuwemo Bustanini, nayeye ndiye aliye gawa adhabu kwa kila Mhusika humo katika bustani ya huko Edeni. Kamwe asingeweza kuiruka kauli yake!’

  Baada ya utangulizi huo niseme;
  Nimeshawishika kuingia hapa baada ya kuona mambo makuu mawili yaliyosimamia mjadala huu, kuhusu swala la kuzaa kwa utungu kulikozidishwa na Mungu kwa Eva, na kuaminika kuwa ni sehemu ya Laana aliyolaaniwa Eva! Mambo hayo mawili niliyoyaona ni; moja, wapo wanaolitazama jambo hilo na kuamini kuwa ndivyo lilivyo, kwamba ni Laana, kumbe wanalijua na kujiaminisha hivyo kupitia imani za kidini, na hawa ndiyo wengi na ndiyo bahati mbaya kuliko bahati mbaya zote! Bahati mbaya? Ndiyo, “wala Neno lake hamnalo likikaa ndani yenu……mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mnauzima wa milele… ” (Yn.5:38-40). Mtu akifundisha bila kuwa na msingi juu ya Neno amekwisha kufa, Mtu asipokuwa na Neno, biblia inasema mtu huyo ni mfu! Sasa jihoji, unasimama juu ya andiko gani unaposema kuwa, aliongezewa Eva utungu kwa sababu alilaniwa? Ukipata bahati ya kumuona mtu anatembea, anaimba pambio, anahubiri na au anatoa mapembo kwa jina la Yesu, kisha Mungu akakwambia kuwa, umuonaye Alisha kufa zamani, na kwamba hayupo tena Duniani, utaenda kumsikliza mtu huyo na mahubiri yake? Kumbe bahati mbaya kuliko hii ni ipi?

  Lakini la pili ni kwamba, wapo wanaolitazama jambo hili na kulipatia ukweli kupita Imani inayojengwa juu ya Neno la Mungu, na hawa kwa bahati nzuri ni wachahe sana! Bahati nzuri? Ndiyo, ni bahati nzuri kwa sababu, “tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yn. 8:32).Haipo bahati nzuri kama mtu kukaa na Neno kwa wingi ndani yake, maana Mungu ndiye Neno lenyewe!

  Kwanza nikubaliane na Lwembe CK. kwamba, Mungu hakumlaani Adamu wala Eva. Pili nakubaliana naye pia kwamba, Utungu ulianza kuwepo mara tu baada ya anguko, kwa sababu utungu ulitajwa na Mungu juu ya namna atakavyozaa Eva kwa mara ya kwanza, ni pale tu walipokwisha anguka. Na Mungu akauzidisha (Mw.3:16). Lakini mimi kama mimi nakubali kwamba, zidisho la utungu lililofanywa na Mungu kwa Eva kama sehemu ya Uzazi kwake, ni Mungu alikuwa akilihuhisha Neno lake (hilo nasema mimi) Kwa nini? Kwa sababu, Mungu ni Neno “…naye neno alikuwa Mungu” (Yn.1:1), na kwa Neno kila kitu kilifanyika. “…..pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika” (Yn.1:3). Kumbe yapo yanayoonekana kuwa yapo kumbe hayapo! Kwanini hayapo japo kwa macho au kwa akili tunatambua yapo? Kwa mjibu wa hiyo Yn. 1:3, tunajifunza kwamba, yote yaliyopo au yanayokubalika kuwa yapo, kama yapo pasipo tamko la Mungu, mambo hayo hayapo! Ni sawa na kusema kuwa mtu anayeishi bila kuwa na Neno la Mungu, mtu huyo hayupo alishakufa zamani kabla ya hata kuzaliwa kwake! Kwa maana hiyo, na kwa mjibu wa ile Yh. 1:3, mimi najifunza kwamba, utungu ulikuwepo kwa Eva, lakini usinge kuwa Utungu bila tamko (Neno) la Mungu! Hakuna kilichofanyika bila Neno la Mungu! Sentesi katika Mw. 3:16, “….hakika nitakuzidishia utungu wako….” Inaonyesha kuwa utungu Eva alikuwa nao mara tu baada ya anguko, kwa nini? Kwasababu, Biblia inaeleza kuwa, Utungu wa kama mwanamke azaaye,ni adhabu kwa wavunja sheria na huwapata wenye madhara (waovu)! Ukitazama ile Hosea 13:13 inasema, “utungu wa mwanamke mwenyemimba utampata; yeye ni mwana asiye na akili…..” ukiitazama ile Isaya 26:16-18 inaeleza, Isaya akimkumbusha Mungu jinsi, watu walivyomlilia Mungu walipopatwa na taabu zao, nakuomba maombi mengi walipopatwa na adhabu ya Mungu, na kuifananisha na utungu kama wa mwanamke anayekaribia kuzaa….!

  Mungu ni pendo na upendo ndiyo sheria yake, hivyo, yeye (Mungu) hawezi kuweka sheria kisha yeye akaivunja, na pia halipo andiko linalosema kuwa, mtu apate adhabu bila hatia. Ile Rum. 13:10, inasema “Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria” kwa hayo niliyonukuu hapo juu na kwakuwa hakuna andiko linalosema Mungu alimuumba Eva na utungu, lakini lile neno kuwa “nitakuzidishia” linathibitisha kuwa Eva kabla ya tamko hilo alikuwa na utungu! Utungu ambao ulikujakudhilishwa na lile Neno la Mungu kwamba, “Hakika nitakuzidishia”.

  Kwa mjibu wa Neno (Yn.1:3b), jambo linakuwa jambo, iwapo limetamkwa na Mungu. Pasipo tamko hilo la Mungu, hakuna mtu leo angetoa madai kuwa, hali inayompata mwanamke katika kuzaa ni laana ama la! Bila kuwepo na tamko au Neno Mungu angepoteza sifa yake kama Mungu, maana yeye ni NENO! Isingekuwa rahisi kukuta liko jambo linaloitwa Utungu bila kuwepo uumbaji wa utungu huo, maana Neno ndilo huumba!
  Je, Eva aliumbwa akiwa na utungu? Hasha, Mungu alimuumba Mtu kwa mfano wake (Mw.1:27), Mungu hazai mtoto kwa utungu, Mungu huzaa kwa Imani, kwa sababu, watoto wake si waovu! Na tunajua kupitia Neno lake hilohilo kuwa yeye ni Mwema, ana huruma ni mpole na anapenda watu, hivyo isingeingia vema akilini kuwa mwenye kuwapenda watu kwa kiwango cha juu kiasi kile na hata akaupenda ulimwengu kwa upendo mkuu ule aliousema katika ile Yn. 3:16, kumbe tena bila kukosewa chochote anaweza kukupa maumivu! Ni wazi jambo kama hilo, lingepokelewa kwa hisia mbaya sana na lingepoteza maana halisi ya Mungu kwa wanaosikizishwa injili, maana Neno linasema, “Pendo halimfanyii jirani neno baya” Rum. 13:10!

  Kwa hiyo ileweke kwamba, kila mimba achukuayo mwanamke, ni mimba ya wakati wa “Uovu” ndiyo maana mwanamke hupata utungu katika kujifungua kwake, utungu ambao aliupata mara tu baada ya anguko kama tulivyokwishaona hapo juu n nyongeza ilifanywa na Mungu kwa sababu za Mungu mwenyewe. Wanadamu wote walianza kuzaliwa baada ya anguko la pale Bustanini, na hivyo mama yao kuendelea kuupata utungu hadi leo. Eva aliupokea utungu tangu hapo, ukisoma Zab. 7:14 inasema “Tazama huyu anautungu wa uovu, amechukua mimba ya madhara…” kumbe tunaona kuwa ni mathara ndiyo yaletayo utungu. Mika 4:10 inasema, “Uwe na utungu, utaabike ili uzae….kama mwanamke mwenye utungu….utakaa mashambani…utafika mpaka babeli ndiko utakakookolewa, huko ndiko Bwana atakakokukomboa katika mikono ya adui zako”. Kwa hiyo utungu ni adhabu itokanayo na hatia.
  Utungu ni Laana?
  Hapana utungu ni hukumu, ni adhabu. Hukumu ama adhabu hudumu muda wote wa kipindi chake kama ilivyopangwa. Laana nayo ni adhabu itokanayo na hukumu vilevile, lakini kama ilivyo hukumu hupishana kulingana na kima cha hatia ama kosa.Adhabu ya laana ipo kwa ajili ya shetani na uzao wake tu na si vinginevyo, Japo shetani naye huwalaani wana wa Mungu, lakini laana kwa watoto wa Mungu, huondolewa na Mungu, mwanzo kwa sadaka za kuchinjwa lakini sasa kwa Damu ya Yesu kristo. Mungu halaani watoto wake, Mungu hakumlaani Eva. Lakini pia ikumbukwe Eva ndiye mama wa kila mwanadamu. Ndiye mama wa Uzao wa Mungu na ndiye mama wa uzao wa Nyoka! Mungu humlaani shetani na uzao wa nyoka tu! Laana ya kwanza kwa wanadamu tunakuja kuiona kwa Kaini katika ile Mw.4:11-15, na pia kwa mmoja wa wana wa Nuhu. Mbalikiwe zaidi na Bwana.

 13. Mkandya, acha ujanja!

  Hivi ni kweli Mkandya kwamba unaamini uchungu wa kuzaa kwa mwanamke ni sehemu ya mapenzi makamilifu ya Mungu? Hivi haufahamu kwamba kabla ya anguko walikuwa wanatembea uchi na miili yao haikujaa manyoya wala haikuwa na ngozi ngumu kama ya kiboko ili kuwa kinga, bali ilikuwa ni ile ngozi laini, kushinda hii wanayohangaika nayo dada zetu kwa cosmetics, na hawakuchomwa na miiba wala kukwaruzwa! Walipoanguka ndugu yangu, mambo yote yalibadilika, dhambi haiingii na keki bali kifo, nao uchungu ni sehemu ya kifo. Ulikuwa kwa kiwango gani huo uchungu unaoandamana na dhambi, mimi sijui ila najua kuwa Mungu aliuzidisha!

  Kuhusu laana:
  CURSE: damn, condemn a person to suffer eternal punishment in hell: be forever damned with Lucifer.

  Halafu mcheki nyoka; “BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni;”
  Na Kaini naye, “Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;”
  Eva na Adamu ni sehemu ya Mungu, kwa hiyo Mungu hawezi kujilaani, hao aliwapa adhabu tu, ambayo wanaitumikia mpaka leo. Hata hivyo kwa kuwahurumia katika adhabu hiyo amewaletea Neema. Nao ushuhuda wa dada Dolly ulipaswa ukufungue macho Mkandya, uone kuwa kwa kuzaa kwake bila uchungu na utungu wake, hilo litakuwa ni kuionja ile hali ya kabla ya anguko!

  Mkandya, kwani kuwa fruitful lazima iwe ni kwa jinsi hii iliyopo? Hauoni kuwa huo uchungu unaoambatana na kuzaa unaashiria kuwa hayo hayakuwa mapenzi ya Mungu? Jaribu kuyatafakari zaidi mambo haya, maana hakuna kati yetu anayeijua mipango ya Mungu kwa uhakika ya huko nyuma kabla ya anguko!

  Baraka Mkandya si tumeziona hapo walipoambiwa wawe fruitful, ambavyo wewe umetafsiri kuwa ndiko huko pamoja na kuzaa kwa uchungu, si ndio umeziita baraka! Hii multplication ya uchungu ni adhabu tu na si laana. Ukilaaniwa Mkandya, unakuwa cut off from the Main Stream of Life which is God! Unaitafuta Nod yako nawe, yaani mnaishiana na Mungu na kuambatana na Lucifer, unakuwa chombo chake! Ila akina Adamu walipewa adhabu tu ndio maana Mungu aliwatengenezea mavazi ili aweze kuwatazama na kuwaangalia maana ni wanae!

  Hiyo John 11:25/26 kaka, hii ndiyo wanaambiwa akina Adamu na mkewe na vizazi vyao, hao walioletewa Injili iwakomboe, waliolaaniwa haiwahusu hii! Hata hivyo ningependa kulisikia wazo lako kuhusu habari hii ya kufa na kuishi, unajua changamoto za Injili na nyingi na zinatujenga!

  Ubarikiwe

 14. Ha ha haa, bwana Lwembe!

  Nakuelewa sana unataka tujibuje unaposema hakuna mahali popote ambapo Eva au Adamu alilaaniwa, na baada ya sisi kuwa tumejibu hivyo nahua utasema nini.

  Sina uhakika kama unaelewa vizuri na kwa mapana maana ya laana. Na kwa sababu hili suala la kuzaa bila utungu hatuwezi tukalazimisha kila mwanamke aliyeokoka liwe sehemu yake kama ambavyo kuamua kutokuwa mgonjwa ni suala binafsi na linawezekana kwa anayetaka,ningeomba kila mtu aendelee kuamini anavyotaka kwake iwe. Kwa nakubaliana na wewe kuwa hatuwezi kulifanya kuwa ”standard” au fundisho la msingi (doctrine)

  Kwa mwanamke anayetaka kujifungua bila uchungu nasisitiza kuwa inawezekana akiamua kumwamini Mungu. Na ambaye anaona kujifungua kwa uchungu au hata kwa kuchanwa tumbo basi kwake itakuwa hivyo.

  Kabla hujatoa kibanzi kwa mweenzio toa kwanza boriti katika jicho lako Lwembe. Unatuambia tusisome biblia tukiwa tumevaa mawani, je wewe umetoa mawani yako?

  Ona ulivyosema hapa:”hata jambo la kuongezeka, wangeongezekaje hakuna anayejua mungu aliwapangia jinsi ipi. Kama ni kuzaa, tunakuona baada ya anguko”

  Kwa nini unataka kutudanganya kwa kitu ambacho kiko wazi kabisa? Mungu alipomaliza kuwaumba aliwaambia zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi, halafu ndugu Lwembe unasema suala la kuzaa limekuja baada ya anguko.(Mwa 2:28. And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the earth, and subdue it)

  Ndio maana baada ya anguko kwa Eva kuna habari za kuzidishwa kwa utungu wa kuzaa. Neno kuzidishwa hapo kama wewe ni msomaji mzuri linakuonesha kuwa hicho kinachozidishwa kilikuwepo. Kama hapakuwepo na huo utungu basi biblia ingesema tu kuwa ‘utazaa kwa utungu’. Lakini sasahivi imesema ”nitauzidisha utungu wa kuzaa kwako”( Mwa3:16. Unto the woman he said, I will greatly multiply thy sorrow and thy conception; in sorrow thou shalt bring forth children;.
  Utaniambiaje kuwa hayo maneno kwa Eva yalikuwa ni baraka, au ulitaka iseme ”umelaaniwa utazaa kwa utungu” ndipo ujue kuwa hayo maneno hayakuwa baraka bali laana? Ndio maana nimekuuliza kama unajua vizuri maana ya laana.

  Lwembe pale mwishoni umesema kuhusu mkristo kuumwa na kufa. Ndiyo, mimi naweza kutamatisha kuwa mkristo hatakiwi kuumwa. Na kwa habari ya kufa kama utataka tuijadili tutafanya hivyo ili kujua kwa nini tunapaswa kuondoka katika hii dunia kwa njia ya kulala (ambako wengi wetu tunakuita kufa) kabla ya unyakuo kufika.
  Yatafakari haya maneno ya Yesu ”John 11:25b,he that believeth in me, though he were dead, yet shall he live:
  26a. And whosoever liveth and believeth in me shall never die.

  Kazi njema.

 15. Mkandya,

  Ni kweli kabisa mateso mengi tunayoyapata wanadamu si mapenzi ya Mungu. Kwa sisi tuliompokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu tunatakiwa tuzijue ahadi za Mungu zilizo kwenye neno lake na kuzifanyia kazi, hakika tutamwona Mungu katika maisha yetu.

  Kuna mambo mawili ninapenda kuwashirikisha wapendwa na hasa wamama wenzangu:

  1. Kujifungua kwa operesheni
  2. Kushindwa kumnyonyesha mtoto kwa maziwa yako kwa kuwa maziwa ni machache mtoto hashibi au wewe mwenyewe hutaki tu kunyonyesha.

  Mambo hayo si mpango wa Mungu kabisa. Mungu alipomuumba mwanamke alimtengenezea na njia ya mtoto kuzaliwa. Na pia alimuumba mwanamke akiwa na kiwanda cha kutengeneza chakula cha mtoto anapokuwa amezaliwa (maziwa). Mambo hayo mawili Mungu alipoyaweka ndani ya mwanamke lengo kuu ilikuwa ni kujenga uhusiano wa karibu kati ya mtoto na mama yake tangu anapozaliwa hadi anapokuwa mkubwa. Mahusiano haya ni muhimu katika maisha ya mtoto huyo na pia ni muhimu kwa mama mwenyewe (Kiroho na Kimwili).

  Inapotokea mtoto anazaliwa kwa operesheni, jambo linalotokea ni kukosekana kwa mahusiano ya karibu ambayo Mungu aliyakusudia kati ya mama na mtoto kwakuwa mama hakuhusika katika kumleta mtoto huyo duniani, kazi hiyo aliifanya daktari na mama huyo alipoamka kutoka kwenye usingizi wa operesheni hiyo alikabidhiwa tu mtoto wake. Wakati mwingine pia mama anaweza akawa na tatizo la kupata maziwa kidogo hata akashindwa kumnyonyesha maziwa mtoto wake au wamama wengine hawataki tu kunyonyesha watoto wao ili maziwa yao yabaki katika hali ya usichana.

  Unaweza kushangaa ni kwa nini siku hizi wamama wengi hawana upendo kwa watoto wao, mama anaweza kumwacha mtoto mchanga na mtu mwingine na akatoka na kukaa masaa mengi bila kujisikia vibaya wakati zamani mama zetu ilikuwa ni vigumu kufanya hivyo hasa anapokuwa na mtoto mchanga. Pia watoto wengi siku hizi hawana upendo au heshima kwa wamama zao.

  Ewe mama uliyeokoka Mungu anapokujalia kupata ujauzito fanya maombi ya kukataa operesheni ya uzazi, kataa pia kupata tatizo lolote wewe au mtoto wako wakati wote wa ujauzito wako hadi wakati unajifungua. Si mapenzi ya Mungu tuzae kwa kukatwa matumbo yetu !! Mungu alituumba tuwazae watoto kwa njia ya asili na tuwanyonyeshe watoto wetu maziwa yetu.

  Neno la Mungu linasema yeye ndiye aliyemweka huyo mtoto tumboni mwako, je atashindwaje kuzalisha?? Mungu ndiye aliyekuumba wewe mwanamke ukiwa na kiwanda cha kutengeneza chakula cha mtoto wako, atashindwaje kuyatoa hayo maziwa ili mtoto wako ayanyonye?? Hizo ni hila za shetani !! Zikatae katika jina la Yesu mwana wa Mungu aliye hai. Mwombe Mungu wakati wa ujauzito wako kwamba mtoto anapokaribia kuzaliwa ageuke kwa kuelekea katika njia ya asili na azaliwe kwa njia ya asili na si kwa operesheni. Mwombe Mungu aifungue mirija ya maziwa yako tangu ukiwa mjamzito ili mtoto atakapozaliwa asikose maziwa hayo na anyonye hadi aache katika umri unaostahili.

  Usisahau pia kuiombea Hospitali utakayokwenda kujifungulia pamoja na siku yenyewe ambayo Bwana amepanga wewe ujifungue, Bwana Yesu ndiye akuzalishe yeye mwenyewe na malaika ndio wakuhudumie siku hiyo, kataa kuhudumiwa na madaktari na manesi ambao ni wakala wa shetani. Takasa ile hospitali, chumba, kitanda, na kila kifaa kitakachotumika siku hiyo kwa damu ya Yesu, na ombea mikono itakayompokea mtoto wako siku ya kwanza atakapozaliwa iwe ni mikono sahihi na si ya adui katika Jina la Yesu, ikiwezekana iwe ni ya mtumishi ambaye atamwombea mtoto huyo kabla hajakamatwa na mtu mwingine yeyote jambo hili ni muhimu sana katika ulimwengu wa roho. Na baada ya kujifungua kumbuka kumshukuru Mungu na kumpeleka mtoto wako madhabahuni kwa Bwana ili awekwe wakfu ili Bwana awe ndiye awe mlinzi wa mtoto wako maana neno la Mungu linasema “Bwana asipoulinda mji waulindao wakesha bure.”

  Kwa kuwa tumepewa maarifa ya kuzijua hila za adui tuwakumbuke pia kuwaombea wale wamama ambao bado hawajampokea Bwana Yesu na ni wajawazito kwa wakati huo ili Mungu awaguse pia na wao na watoto wao kwani ni mapenzi ya Mungu kuwa watu wote waokolewe na waifikie toba, kwa majira na siku aliyoikusudia nao waokoke na uzao wao.

  Mimi ni shahidi pia wa tatizo la kukosa maziwa baada ya kujifungua watoto wangu maziwa yalikuwa yanatoka kidogo mwisho mtoto akiwa na miezi 2 mwenyewe aliamua kuacha kwa kuwa alikuwa ananyonya anaona hayatoki, ilikuwa ikiniuma sana kama mzazi kwani nilikuwa natamani kunyonyesha lakini maziwa hayatoki. Lakini nilipogundua kuwa hakuna jambo linalomshinda Mungu wetu, nilifanya maombi ya kuyafungua maziwa yangu ili mtoto atakapozaliwa anyonye hadi mimi mwenyewe nimwachishe akiwa na miaka miwili na ndivyo ilivyokuwa.

  Shetani siku zote halali anafanya kila linalowezekana kuwaletea uharibifu wana wa Mungu kwa kuwa yeye ni adui wa uzao wa mwanamke.

  Nawasihi wamama ambao hawajaokoka wampokee Bwana Yesu awe Bwana na Mwokozi wa Maisha yao, Shetani anamchukia sana mwanamke na uzao wake, lakini ukiwa ndani ya Yesu unapokea ulinzi wa damu yake na hata unapokwenda mbele zake kwa maombi Mungu atataonekana katika maisha yako.

  Asante sana Mtoa Mada Moses Kwabhi kwa mada nzuri ambayo imetubariki sana na pia kwa wachangiaji wote wa mada hii, Mungu awabariki sana. Tuendelee kuelimishana katika Kristo Yesu.

  Dolly

 16. Kwanza ninakubaliana na Mr. Milinga kwamba ndg Moses amelifafanua jambo hili nje ya muktadha wa Maandiko. Amewapachika watu laana ambayo Mungu hahusiki! Nasi kwa uvivu wa kuwa wasikivu tunapoyasoma Maandiko, tunayakubali mambo ambayo hayapo, na mwishowe tunapoteza muda mwingi kupambana na jambo ambalo halipo!

  HAKUNA mahali popote pale ambapo Eva wala Adamu walilaaniwa. Kwa hiyo kujenga hoja zetu juu ya msingi wa laana ya kufikirika, hatutaifikia ile Kweli iliyokusdiwa kutuweka huru, na hivyo kubaki kuwa watumwa wa fikra zetu duni.

  Suala la mwanamke aliyeokoka kuzaa bila utungu na uchungu halipo! Na wala wazo la kwamba kuzaa kwa uchungu kulikuwepo kabla ya anguko, pia halina mashiko kiBiblia. Unawezaje kupata utungu wa kuzaa kabla ya kupata mimba? hata jambo la kuongezeka, wangeongezekaje hakuna anayejua mungu aliwapangia jinsi ipi. Kama ni kuzaa, tunakuona baada ya anguko. Na pia Mungu hawezi akawa alimpangia mwanawe uchungu kuwa sehemu ya maisha yake, huyo ambaye hana kosa lolote, hivi inawaingia hiyo akilini kweli? Yaani huyo ambaye Mungu amemuumba kwa mfano wake awekewe uchungu wa kudumu, sasa hilo lingemfanya Mungu kuwa pia anao uchungu wa kudumu! Upendo wa Mungu uchanganyike na uchungu wa uzazi, uchungu kwa kosa gani? Kwani Adamu au Hawa ndio waliomuomba Mungu kwamba wanataka kuzaa?

  Kama walivyotafuta nguo za kujihifadhi, hiyo ilikuwa ishara tosha kuwa mambo yashakuwa si shwari, si salama kwao, na uchungu ulizaliwa hapo walipoanguka, naye Mungu aliuzidisha huo kutokea hapo. Maana kabla ya hapo Mungu alikwisha kusema kuwa “kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana” Mwa 1:31; basi uchungu na utungu wake vyaweza kuwa ni sehemu ya huko kuwa “ni chema sana”? Haiwezekani, au lugha imepoteza maana!

  Kuhusu mwanamke kuzaa bila uchungu au utungu baada ya maombi, hauwezi kulifanya jambo hilo kuwa ndiyo standard kwa waliookoka, utakuwa umejichanganya, na kujiingiza katika cults kifikra. Mungu amesema kwa kupigwa kwake sisi tumeponywa, hakusema maradhi yameondolewa, kwamba sasa hayapo tena! Adhabu na laana ni vitu viwili tofauti. Hivi unapomtandika fimbo mwanao kwa kosa alilofanya, huwa ndio unamlaani au unamnyoosha akae sawa! Msijipachike malaana tu wapendwa yatakuja kuwang’ang’ania mshindwe hata pa kutokea. Mungu ametuletea Neema yake ili ituwezeshe kupita katika adhabu zake alizozitamka. Kwa hiyo kama huyo dada amepata Neema hiyo ya kufurika, hilo haliondoi adhabu. Kwani Lazaro aliyefufuliwa, yuko wapi leo hii? Basi unaweza kutamatisha kuwa mkristo aliyeokoka haumwi wala kufa?

  Mwisho ninawaasa, someni Maandiko bila kuvaa miwani ya dini!

 17. Dolly nimesoma huu ushuhuda wako nikahisi machozi kunitoka. Umesema kitu ambacho nilitamani kila mtu hasa mwanamke aliyeokoka akijue, maana mimi ninakiamini hivyo jwa asilimia mia moja.

  Ushuhuda huu kutoka kwa mtu ambaye amekiexperience kitu hicho utusaidie kuujua ukweli wa neno la Mungu na kuuamini, mateso mengi ambayo tunadhani ni mapemzi ya Mungu yataisha.

  Niliposimuliwa na shemeji yangu yalivyo yale maumivu ya kuongezwa njia nikasema kuwa hayo hayawezi kuwa mapenzi ya Mungu kwa mwanamke hasa mwamini.

  Asante sana Dolly!

 18. Shalom wapendwa,

  Ninakubaliana na maelezo ya Mkandya na Mathew. Hakika yote yanawezekana kwake yeye aaminiye. Ninao ushuhuda kuwa inawezekana ukazaa bila utungu ule uliozidishwa baada ya anguko la Adamu na Eva nami ni shuhuda wa hilo. Mimi ni mwanamke niliyeolewa na ninao watoto watatu walio hai na mmoja alifariki akiwa na miezi sita. Nilikuwa sijaokoka wakati nilipokuwa ninawazaa watoto wawili wa mwanzo.

  Mwaka 2006 nilikuwa mjamzito wa mtoto wangu wa 4 baada ya kupita katika mapito ya kufiwa na mtoto wangu wa 3 akiwa na miezi 6 aliyefariki mwaka 2005. Mara zote tatu nilipokuwa nikijifungua watoto wangu hao nilikuwa ninapata utungu mkubwa ikiwemo kuwekewa maji ya uchungu, vidonge vya kuzidisha uchungu pamoja na kuongezwa njia – yalikuwa ni mateso makali yasiyoelezeka. Nilipopata ujauzito wa mtoto wangu wa 4 nilifanyiwa maombezi na mtumishi ambaye alinifundisha somo kuwa inawezekana kumwomba Bwana Yesu apunguze ule utungu wa laana aliongezewa Eva ili ubaki ule utungu ambao Mungu aliuumba kwa mwanamke. Niliamini somo hilo na kulitendea kazi, nilifanya maombi hayo na siku ilipofika ya kujifungua, ilibidi Roho Mtakatifu amtumie mume wangu kunisisitiza anipeleke hospitali kwani mimi nilikuwa ninaona ni dalili tu lakini muda wenyewe bado haujafika kwakuwa sikusikia utungu niliouzoea, kwani nilichokisikia ni kama mtu ananipapasa taratibu ndani ya tumbo langu, sikujua kumbe ndio ulikuwa utungu wenyewe. Daktari na manesi walionizalisha walishangaa mno kwani wakati wao wanadhani muda bado mtoto alizaliwa tena bila kikwazo chochote nami sikusikia uchungu wala maumivu yoyote hata baada ya kujifungua, jambo hilo halikuwa la kawaida kwangu. Hakika nilimwona Bwana Yesu akinitendea mambo makubwa wakati wa kuzaliwa mtoto huyo. Nilikwenda Kanisani na kutoa ushuhuda kwamba kumbe inawezekana kwa mwanamke aliyeokoka akiamini na kuomba kwa jina la Yesu anaweza kupunguziwa laana ya kuzaa kwa utungu ule ulioongezwa baada ya Eva kumwasi Mungu.

  Nilichojifunza ni hiki: Mwanamke anaweza kuzaa kwa utungu ule wa mwanzo ambao Mungu aliuumba kwa kila mwanamke baada ya kumwomba Mungu aondoe ule utungu uliozidishwa baada ya anguko la Adamu na Eva.

  Mbarikiwe sana,

  Dolly

 19. Asante Methew, mchango wako ulikuwa haujaingia wakati naandika wa kwangu, lakini nimeona jinsi ambavyo tumejikuta tunaongea kitu kimoja nimefurahi.

  Na huo ndio ukweli labda kama mtu hataki kuukubali tu.

  Naomba wapendwa tuongeze bidii ya kuchunguza maandiko.

  Ubarikiwe!

 20. Naomba tuliangalie vizuri hili suala kwa kurejea kwenye maandiko.

  Kwanza napenda tujue kuwa tangu mwanzo mwanamke alikuwa anazaa kwa utungu, kama ambavyo Adam alikuwa anatakiwa kulima.

  Walipokosa Eva aliambiwa utungu wake wa kuzaa utaongezwa( na hiyo ilikuwa ni adhabu au laana) Mwanzo 3:16a. ”Unto the woman he said, I will greatly multiply thy sorrow and thy conception; in sorrow thou shalt bring forth children; ”

  Mimi naamini kuwa kifo cha Yesu kilirudisha mambo katika hali ya kwanza, kwamba lile zidisho lililoongezwa katika huo utungu halipo kama mtu atataka kuamini.

  Kuhusu Yesu kutotangua torati bali kutimiliza wengi pia huwa hatuelewi maana ya neno kutimiliza. Neno hili maana yake ni kukamilisha. Kwamba Yesu alikuja kuikamilisha torati na hiyo kazi aliifanya akaimaliza. Maana yake ni kwamba Yesu ndo mtu pekee aliye- ”meet demands” za torati, maana wengine wote walishindwa.

  Kwa hiyo laana ya makosa ya Adamu haipo!

 21. Ukisoma vizuri, Mwanzo 3:16 utaona kuwa kuzaa kwa uchungu haikuwa laana ambayo Mungu alimwambia Mwanamke. Hebu tuyasome maneno haya “Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto;…….” (SUV). Tafsiri za kiingilishi zinasema “I will greatly multiply your sorrow and conception………..” (NKJV). Kwenye RSV it reads; “I will greatly multiply your pain in childbearing …..” Hivyo kwa maneno haya kuzaa kwa uchungu kulikuwepo kabla ya anguko, baada ya anguko Mungu anasema atazidisha. Hata wana mahesabu wanajuwa kuwa sifuri (0) zidisha (X) namba yoyote (hata ikiwa ni bilioni) jawabu lake ni sifuri. Ili tendo la kuzidisha lilete tofauti ni lazima namba zote zite zaidi ya sifuri. Hivyo Mungu anaposema atazidisha ina maana uchungu ulipangwa uwepo wakati wa kuzaa hata kabla ya dhambi . Zidisho la uchungu ndiyo laana.

 22. mimi ni swali . mwanamke aliambiwa atazaa kwa uchungu na mwanaume aliambia atakula mwa jasho. Sasa je kwa mwanaume aliyeokoka hapaswi kula kwa jasho,?

 23. Nakubaliana sana na ndugu Milinga kwamba utungu wa kuzaa utaendelea kuwepo licha ya Mwokozi wetu kusulubiwa msalabani. Ijapokuwa kuna uzazi unoitwa kwa kitaalam “precipitated labour” mama akazaa kwa haraka sana kuliko muda unotarajiwa kwa wastani na akapata utungu kwa kiasi kidogo. Na pia ipo teknologia ya mama kutumia dawa za kuondoa maumivu asisikie utungu wakati wa kuzaa.

 24. Mungu wa agano la kale hajabadilika ni yuleyule, Yesu alipokuja hakubadilisha amri alizoweka Baba yake ila alizitimiliza. Hivyo kuzaa kwa utungu kuko palepale ni lazima neno la Mungu litimie. Mwanamke kama atazaa bila utungu ina maana mtoto anaweza akatoka tumboni bila mama kujua jambo ambalo ni hatari hasa ikitokea kuwa mtoto anataka kutoka wakati mama amelala usingizi.

 25. according to the bible, every woman is punished by Eve’s sin, with pain , sorrow , toil, trouble during childbirth. the childbearing itself is not a curse, but the pain with it is.
  kupata chochote kizuri lazima ukifanyie kazi. Christo Yesu aliumia msalabani ili tupate makombozi. bila kuumia makombozi yasingekuwepo. angeweza kupewa uwezo wa kutoumia na baba yake, lakini aliumia kwelikweli akajuta kwa nini amekikubali kikombe hicho. hivyohivyo wakina mama wakiwa na uchungu hujilaumu sana kwa nini walikubali kubeba hiyo mimba. lakini baada ya mtoto kuzaliwa wanasahau yote.

 26. Kama kuchomwa na michongoma na kula kwa jasho alikoambiwa Adamu kulikuwa ni laana, basi hata kuongezwa kwa uchungu wa kuzaa alikoambiwa Eva kulikuwa ni laana.

  Kuna mama namfahamu alikpofahamu huu ukweli wa kuzaa bila uchungu ilimtokea akzaa bila uchungu na manesi walishangaa.

 27. Mpendwa Moses,

  Nadhani unafafanua andiko hilo nje ya mkutadha wake. Laana ambazo hazijaondolewa na kifo cha Yesu Msalabani kati ya zile zilizotajwa baada ya Adam na Eva kutenda dhambi ni laana mbili ambazo ni KIFO na UTUNGU.

  Inabidi utofautishe UTUNGU na UCHUNGU. Nadhani wewe umechanganya mambo mawili yenye maana tofauti. Na hili ndilo tatizo la wainjilisti wetu wengi na watanzania walio wengi, Kiswahili chetu bado kinatupiga chenga na kukuta pia tunayafafanua maandiko nje ya maana iliyokusudiwa.

  UCHUNGU ni maumivu ayapatayo mtu kutokana na maumivu fulani sehemu yoyote ya mwili wake kutokana na sababu yoyote ile kama vile kukatwa na kitu chenye ncha kali, kuchomwa na kitu mwilini, kuchomwa moto au kuunguzwa na maji ya moto, nk. Kwa hiyo wakati wa kuzaa mtoto mwanamke hubakia na uchungu sehemu za siri kutokana na maumivu aliyoyapata wakati anazaa mtoto. Wapo wanawake wengine njia ya kupita mtoto hulazimika kuongozwa na madakitari ili mtoto aweze kupita kwani anakuwa ni mkubwa sana kupita njia yenyewe.

  Wanawake Wengine hawapati uchungu wowote baada ya kuzaa mtoto kutokana na kwamba mtoto aliyezaliwa ni mwembamba sana na njia (uke) ni kubwa sana kuliko mtoto mwenyewe. Hawa huwa hawapati UCHUNGU wowote wakati wa kuzaa na baada ya kuzaa pia.

  Kwa hiyo, unaposema wapo waliozaa bila UCHUNGU kwa sababu eti wameishinda roho ya laana unakuwa hujalielewa vyema somo la kuzaa kwa UTUNGU au kwa UCHUNGU.

  Kwa upande wa neno UTUNGU, Maandiko yanaposema (Yer 4:31) Nanukuu, “Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa UTUNGU wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji” Mwisho wa nukuu.

  Maandiko hapo yanaonesha kwamba UTUNGU ni tofauti na UCHUNGU. Utungu ni ile hali wanayokuwa nayo wamama kwanza inayoashiria kwamba mtoto anakaribia au anataka kuzaliwa. Ni ule mchakato wote ambao mwanamke anaupitia mpaka mtoto anapozaliwa ikiwemo kuanza kuona maji maji mengi yakimtoka baada ya chupa la mtoto kupasuka, mtoto kuanza kujisukumiza ili atoke tumboni, ikiwemo tumbo la mama kujisukuma (compelling the child to go out of the womb), nk. Huu ndio UTUNGU.

  Mfano mzuri wa UTUNGU ni ile hali anayokuwa nayo mtu awapo katika kutekeleza haja kubwa. Kama haharishi choo basi lazima afanye zoezi la kujikamua au kujikakamua ili haja kubwa imtoke. Hali kadhalika mama mjamzito asikiapo utungu (siyo uchungu) hufanya bidii ya kusukuma ili mtoto aweze kutoka. Kule kujikakamua au kujiakamua mpaka mtoto anapotoka huletwa “automatically” na mfumo wa ubongo na viungo vyote vinavyohusika na huu ndio UTUNGU wa uzazi.

  Bila UTUNGU mwanamke hawezi kuzaa mtoto kwani hatajua kama mtoto amekuwa tumboni na kama anahitaji kuzaliwa. UTUNGU ndio unaomwambia kwamba saa ya kuzaa imewadiaa. UTUNGU hauwezi kuuleta kwa makusudi bali unajileta wenyewe baada ya saa ya kuzaliwa mtoto kuwadia.

  Uchungu kama nilivyoanza kueleza, ni maumivu ayapatayo mwanamke baada ya kuzaa mtoto ikiwa tu alikumbana na UZAZI PINGAMIZI. Uzazi pingamizi unaweza kutokea kwa mwanamke endapo tu njia ya uke ni ndogo sana kuliko mtoto mwenyewe na hapo ndipo hoja ya UPASUAJI inapoanzia. Au uchungu waweza kumpata mama aliyejifungua kama alichukua muda mrefu sana kukaa na UTUNGU labda alikosa msaada wa wakunga au madaktari, nk, Au uchungu waweza kusababishwa na michubuko mikubwa iliyojitokeza wakati mtoto anazaliwa, nk.

  Kwa hiyo, Mungu alipomleta Yesu Kristo na akafa msalabani hakuondoa utaratibu wa kupatwa na UTUNGU kabla ya kuzaa mtoto. Hata swala la UCHUNGU pia halikuondoka kwani bado kuna wanawake wenye kubeba mimba zenye watoto wanene sana swala linalosababisha UCHUNGU au MAUMIVU mengi sana wakati wa kuzaaa mtoto.

  Bila shaka mpendwa Mosea tumeelewana, kama bado unaweza kusema ni wapi hatujaelewana.

 28. Bwana asifiwe
  Kweli iyi changamoto ni rahisi kuli jibu. kwa nini ninapofikiria ivo.Juu ya Bwana wetu YESU mwenyewe alisema yeye hakuja kutoa TORATI ama kufuta TORATI ao nisema kwa swahili zingine kutoa SHERIA. LA Bwana YESU alikuja kukamilisha SHERIA ama kutujulisha ile SHERIA ipo tangiya kuhumba Ulimwengu . Juu yeye pia YESU mwenyewe alipokuwepo.kwa kiroho UTATU WA MUNGU..Sasa juu ya ile neno linasema juu ya sisi KUKOMBOLEWA toka LAANA ya maBABU yetu ni juu ya kwabudu miungu mengine ndio Mungu iko na wivu sana hataki kumujanga ama kumufananisha na kitu yoyote kwa iyo ndio tulikombolewa na DAMU ya YESU.kutoka laana ya mababu yetu. lakini neno kama ilivyo andikwa UTAZAA KWA UCHUNGU itabaki apo apo juu iko kitu ya damani sana ndio njia YESU alikuja kupitia mimba na kuzaliwa.ulimwenguni.

  Ndugu kama nimekosea munisaidiye

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s