Iweje Ushindwe na shetani?

kifungo

Kwa nini watu wengi huwa wanashindwa na dhambi na kuanguka? wakianguka wanasema eti binadamu ni dhaifu hawez kuwa mkamilifu wakati biblia inasema sisi (tuliookoka) ni washindi na zaidi ya kushinda sasa iweje ushindwe na shetani? ninachojua mimi kuwa shetani hana nguvu hata chembe za kumshinda mwana wa Mungu sasa iweje watu wengi wanakiri udhaifu wakati Yesu wetu ni muweza wa yote?

Unaposema shetani ana nguvu hivyo unamtukuza kuwa yeye ni mweza kuliko Yesu anayeweza yote. Watu wengi wanasingizia udhaifu wa dhambi.

Ukijikana mwenyewa na kuubeba msalaba utaona ushindi wa ajabu juu yako ukitenda kazi.  Hivyo kikubwa ni kuchukua iman na kuona Yesu ana uwezo mkubwa kuliko shetan na shetan ni takataka.

Usimpe nafasi ya kukutawala ndani ya moyo wako ushindi uko kwako endapo ukiijua kwel na mamlaka yako acha kukiri udhaifu kiri ushindi kiri mafanikio katika maisha yako kiri kubarkiwa hata kama unaona maisha n magumu we kiri ushindi daima, fikiri kushinda na si kushindwa. AMINA

MTUMISHI WA KRISTO

–Baraka

Advertisements

25 thoughts on “Iweje Ushindwe na shetani?

 1. Mkandya unamafundisho ya ukweli bahati mbaya unaojibizana nao walishafundishwa kujua wakaamin kwamba wanajua! ni unafiki kudhani kwa kuwa umeokoka hutendi dhambi kamwe. Yesu aliwaita watu kuwa wanafunzi wake na mwanafunzi anasifa yakukosea japo kuwa anawajibu wa kuhakikisha hakosei. nimeyapenda mahojiano yenu sana nataman kama ningehusika pia! tunahesabiwa haki kwasababu tunamwamini Yesu atupae neema{upendeleo} ya kuwa na haki na wala si kwa bidii zetu za kukwepa dhambi. Ahsante.

 2. Nimevutiwa sana na michango yenu hakika ni mizur…. ila lazma tusimame ktk kwel ya Mungu.
  kumbuka utakaso is “a continuous process” huwez kujiita mtakatifu et kwa sabab umebatizwaa la hasha! ni hakika hata km umebatizwa unaweza ukatenda dhambi.. na kuna njia nying za kutenda dhamb “hata kwa kuckia tu na kufikir” ukijua haki then u fail to do it it’s sin…mfano mzur umetolewa hapo juu abt moses wakat shetan anakuja kudai mwil wake….

 3. Bwana Yesu asifiwe
  mimi kijana wa umri wa miaka 22 nimekua nikiangua kwenye dhambi ambayo siipendi ila najikuta imetokea nimeifanya …kwa sasa hata nimekata tamaa ya kutubu sababu naona hasira ya Mungu i juu yangu ..naomba msaada

 4. Mabinza uko makini vya kutosha au unasoma tu makala zangu juujuu na kuanza kujibu?

  Ukirudia tena kusoma swali nililokuuliza utagundua siyo hilo ulilonijibu. Sijakuuliza kama ulitubu dhambi zako ndipo ukaokoka.
  Bali nimekuuliza baada ya kuwa umeokoka, je ilishawahi kutokea siku ukaomba msamaha mbele za Mungu?( yaani ukiwa umeokoka tayari ulishawahi kumkosea Mungu ikabidi utubu?)
  That’s the question I have asked you Mabinza.

  Kwa habari ya Theolojia naweza nikaamua tu kukuacha kama ulivyo kwa sababu unaonyesha kuwa hujui kitu kabisa kuhusu theolojia ni nini.
  Lakini pasipo kujua kuwa hata wewe unaitumia sana katika kusema kila kitu unachoema kuhusu Mungu.

  Hauna tofauti na mwanakwaya anayelikataa darasa la sauti na muziki,lakini ukimuuliza kuwa anaimba sauti ya ngapi anakwambia ya kwanza au ya pili. Maana yake ni kwamba kujua kwake kuwa kuna sauti ya kwanza na ya pili ndilo darasa lenyewe la sauti na muziki japo yeye hajawahi kulihudhuria kama mwanafunzi rasmi.

  Soma hiki ulichosema hapa Mabinza: … na hivyo, kama alivyo Mtu hai akikosea kwa Baba yake ama kwakuwakosea wengine hivyo kumkosea Mungu kwa namna moja ama nyingine yeye kwakuwa yu hai na ana matunda yapasayo Toba, HUOMBA KUSAMEHEWA ‘MAKOSA AMA KUKOSEA KWAKE HUKO’, huwa Siyo dhambi kwakuwa analiamini Neno la Mungu na ndilo hilo linampa kuomba Msamaha, kwakuwa dhambi yake ilishafutwa kwa Damu ya Yesu alipo iamini Injili ambayo ilimletea Toba ya kweli hata kuondolewa kwa dhambi moyoni mwake, ambayo kwakweli ni kutoliamini Neno la Mungu!

  Mabinza ulichokisema hapo ni HERESY (Ni uongo kabisa). Kama unabisha, basi thibitisha hayo maneno yako kwa maandiko hata mawili tu.

  Kila kosa unalomkosea Mungu au kila kosa linalipelekea ukatubu kwa Mung ni dhambi. Lakini si kila kosa unalomfanyia mtu na kulzimika kuomba msamaha ni dhambi. (sijui kama hiyo lugha utaielewa)

  Haiwezi kuwa toba kwa Mungu kama kinachotubiwa siyo dhambi!!

 5. Mkandya Mwana wa Mungu,

  Naona kuwa, unadhani nakuzungusha zungusha tu, sitaki kukubaliana nawe kwakuwa ati unapatia!. La, niseme kwamba mpendwa THEOLOJIA si mimi tu nisiyeikubali, bali hata NENO lenyewe la Mungu haitaji THeolojia kuwa ni Neno au ni Njia au ni Mbinu ya kufundishia NENO la Mungu, kama sivyo, nipe Mstari unao ku ‘sapoti!

  Nimekupata kwa mambo mhimu mawili, la kwanza, unataka kujua kama nilishawahi kutubu Dhambi zangu kwa Mungu; na la pili ni kwamba, usemi wangu kuwa “Kwa hiyo aliyeokoka hatendi tena dhambi, ukitenda hupati Msamaha wa dhambi hiyo maana haipo tena Damu ya kumwagika mara ya pili!” unakuchanganya!,

  Naanza na la kwanza, NILISHATUBU KWA KUWA NILIIAMINI INJILI, NA NI KABATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO! Si kwamba nilisimama pahala na kusema kuwa nilikosa hiki na kile, hadi makosa yangu yote yakaisha kisha nikasamehewa! Biblia inasema katika Marko 1:4 kuwa, 4Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Baada ya kuisikia Injili nilijisikia Mkosa, nikahuzunika na kujiona kuwa nahitaji msamaha Kujuta kwangu huko, ndiko nakuita KUTUBU kwangu kwa Mungu na kweli NIKASAMEHEWA DHAMBI ZOTE! Naona nipo sawa kwa maana ya mstari huu wa tano wa hiyo Marko 1, ambao unasema “5Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea, naye akawabatiza katika mto Yordani, wakitubu dhambi zao.” Kwa kifupi Mtu hawezi kutubu kwa akili na maarifa au kwa nguvu zake, toba ni MAJALIWA toka kwa ROHO MTAKATIFU ambaye ni Mungu mwenyewe; Mdo. 11:18, inasema “ 18Waliposikia haya hawakuwa na la kupinga zaidi. Nao wakamwadhimisha Mungu wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu Mataifa toba iletayo uzima wa milele.” Nafikiri swali kama hilo huwezi kuniuliza tena! Maana, mtu hatubu mwenyewe tu, bali Mungu humjalia mtu toba ya kweli. Na kujua kuwa Mtu huyu kweli Alisha tubu, utayaona MATENDO yake, Math. 3:8 inasema, ‘‘ 8Basi zaeni matunda yastahiliyo toba.”

  Kuhusu lile la pili ni Kwamba, kwanza nikujulishe maana ya Dhambi, kwa tafasri nyepesi na yakweli, kuwa; Dhambi ni KUTOKULIAMINI NENO LA MUNGU! Mtu aliyeokoka ni Yule ALIYEAMINI NENO la Mungu, Neno la Mungu linasema “Mtu hupata haki kwa kuamini” na linazidi kusema kuwa “mwenye HAKI wangu ataishi kwa Imani.” Utaona kuwa kinyume cha kuishi ni MAUTI, maana dhambi ikichukua mimba huzaa Mauti! Ni katika Kijiji ama Nchi gani ulishaona MAITI inatubu?! Je, ikitokea mpo mazishini mnamzika jamaa aliye kuulia Mtoto wako wa Pekee, akanyanyuka katika Jeneza wakati unapita pale kwa heshima za mwisho, Maiti ile ika sema kwa sauti ya unyenyekevu na inatoa machozi kwa sauti ikisema “…MKANDYA MY BROTHER NISAMEHE!” kisha ikarudi tena jenezani na kulala kama mwanzo, hutavuruka mstari wa watoa heshima wenzio kwa kukimbia?! Hebu kuwa realistic Mkandya!!!

  Ndiyo maana nakuambia kwamba ukiokoka hufanyi tena dhambi, kwakuwa Dhambi ni MAUTI; Biblia inasema “kwa Mtu mmoja MAUTI (Dhambi) iliingia Duniani na kwa Mtu mmoja UZIMA (Wokovu) nao uliingia Duniani” Mwamini au mtu aliyeokoka, ni Kiumbe hai katika Roho na hivyo, kama alivyo Mtu hai akikosea kwa Baba yake ama kwakuwakosea wengine hivyo kumkosea Mungu kwa namna moja ama nyingine yeye kwakuwa yu hai na ana matunda yapasayo Toba, HUOMBA KUSAMEHEWA ‘MAKOSA AMA KUKOSEA KWAKE HUKO’, huwa Siyo dhambi kwakuwa analiamini Neno la Mungu na ndilo hilo linampa kuomba Msamaha, kwakuwa dhambi yake ilishafutwa kwa Damu ya Yesu alipo iamini Injili ambayo ilimletea Toba ya kweli hata kuondolewa kwa dhambi moyoni mwake, ambayo kwakweli ni kutoliamini Neno la Mungu! Kwakuwa mtu ana Matunda “yapasayo Toba” moyoni mwake mda wote, huyo anaambiwa na MUNGU hivi; Sasa mkisali salini hivi “…..UTUSAMEHE MAKOSA YETU, KAMA TUNAVYOWASAMEHE NA SISI WALIOTUKOSEA….” Karibu wakati wote Mkandya,

  Usiwe na hofu kuwa Upotoshaji wowote juu ya ile kweli ya Mungu utafanikiwa, maana “…..na milango ya kuzimu haitaliangusha…” Hofu za namna hiyo huwa kwa watu wasiyo LIAMINI NENO LA MUNGU LOTE! Bali huamini sehemu na sehemu huikataa, kama walivyofanya wale Sabini mbele ya Yesu!

 6. Mabinza nimejaribu kupitia mchango wako fulani wa nyuma nikakuta kitu fulani kwamba mtu aliyeokoka ikitokea ametenda dhambi hawezi kusamehewa. Na nakuu “Kwa hiyo aliyeokoka hatendi tena dhambi, ukitenda hupati Msamaha wa dhambi hiyo maana haipo tena Damu ya kumwagika mara ya pili!”

  Mabinza nakushauri ukae chini tena na mwalimu wako akufundishe vizuri juu ya hili swala, au muulize mchungaji wako au yeyote anayeijua biblia atakwambia ukweli.

  Kwa namna fulani unaikataa theology, lakini kwa kufanya kwako hivyo utajikuta unapotosha mambo mengi sana. Na mengi ya makosa unayofanya yako kwenye matumizi ya maneno zaidi, ambayo ung’amzi wake uko kwenye theology. Kumbuka hii biblia ya kiswahili imeandikwa kwa kutafsiriwa kutoka katika lugha mbalimbali.

  Lakini nakusisitiza ujibu swali langu hili:
  Je wewe tangu umeokoka hujawahi kutubu mbele za Mungu?

  Hebu kuwa realistic Mabinza!!!

 7. Mabinza pamoja na kupotea kwa miezi bila kunijibu maswali yangu, nashukuru leo umerudi kwenye hii hoja. Lakini nasikitika sana kuwa hujajibu maswali yangu na ukaniongeza maswali mengine.

  Ni vema ukanijibu maswali yangu pia Mabinza.

  Lakini kuna kitu nimekiona kwenye swali lako la 1a, kuhusu damu ya Yesu kumwagika mara moja. Kabla ya kwenda mbali niseme kitu hapa kwamba Paul anaposema kuhusu damu ya Yesu kumwagika mara moja hakuwa anamaanisha kuwa kuna mmwago mmoja wa damu ya Yesu kwa kila mwenye kutubu, kwamba akitshatubu na kutenda dhambi tena hapati mmwago mwingine.

  Alichomaanisha ni kwamba ule mmwagiko wa damu ya Yesu uliofanyika pale Kalvari unatosha kusafisha dhambi zangu/zako za jana na mwaka ujao kama itatokea nimetenda dhambi. Tofauti ni ile ya wanyama amabayo yenyewe ilikuwa lazima imwagwe kila mtu anapotenda dhambi.

  Yes,mwamini baada ya kuonja vipawa akitenda dhambi akitubu atasamehewa dhambi zake. Lakini kuna anagalizo hapo limetolewa, nalo ni lile suala la kutenda dhambi makusudi baada ya mtu kuufahamu ujuzi wa ile kweli. Kwa huyo mtu haibaki dhabihu kwa hizo dhambi zake. Dhambi ya kusudi nalo ni somo jingine,wala si kitu chepesi kukitenda kama watu wanavyodhani.

  Kwa Lugha nyingine ni kwamba, hata wanaotubu dhambi zao kwa mara ya kwanza huwa wanasafishwa na huo mmwagiko wa damu ya Yesu wa mara ya kwanza na ya mwisho uliofanyika miaka 2000 iliyopita, wala si kwamba leo ati mtu akitaka kuokoka kuna damu ya Yesu inamwagika tena.

  Nafikiri hayo maelezo yamejibu swali lote la kwanza.

  Swali la 2a:
  – damu ya wanyama ilikuwa haiondoi dhambi ila ilikuwa inazifunika tu
  – damu ya wanyama ilikuwa inatakiwa kila mwaka mnyama auawe,lakini ya Yesu pale ilipomwagika miaka 2000 iliyopita inatosha kuondoa dhambi za milele yote.
  -damu ya Yesu inafanya kazi kwa imani, lakini ya wanyama ilikuwa inashikika na walitakiwa kuinyunyiza. Ya Yesu hakuna mtu aliwahi kuichota au kuikinga na kuinyunyiza.
  – damu ya Yesu haitolewi au haigawiwi mahali popote ati kwamba mtu akitaka kutubu anapewa, hamna kitu kama hicho.

  Swali la 2b na c:
  Haya ni ya kitheolojia zaidi naomba niyajibu next time kwa ufasaha

  Ubarikiwe.

 8. Mungu atupe ushindi maana tunayaweza mabo yote katika yeye atutiaye nguvu si kwa uwezo wetu kristo alikufa ili tuwe nahaki kwa njia ya imani na kwa matendo ya sheria

 9. Mkandya mpendwa,
  Si mimi ila ni maandiko, hebu soma hii nukuu kutoka kwenye Mathayo 12:33-35
  33‘‘Ufanye mti kuwa mzuri nayo matunda yake yatakuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya, kwa maana mti hutambulikana kwa matunda yake. 34Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake. 35Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka katika hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake……..” Mwisho wa kunukuu.

  Mpendwa nahitaji kujua yafuatayo:-
  1).(a) Iwapo dhambi huondolewa kwa Damu ya Yesu, nayo ilimwagika mara moja kwa kila atakayetubu na kuokolewa. Mwamini aliyekwisha okolewa na kuonja vipawa vya Mungu, ‘akianguka dhambini tena’ Neno la Mungu linasemaje, Mwamini huyo atasafishwa tena dhambi zake kwa Damu ya Yesu akitubu?

  (b) Iwapo si Damu ya Yesu, ni nini kitaondoa dhambi hiyo ‘Mpya’ ya mwamini aliyeitenda?

  (c) Maandiko yanasemaje, Damu ya Yesu inaweza kumwagika mara kwa mara kwa ondoleo la dhambi kwa Mwamini anayefanya Mchezo wa kuanguka anguka na kisha kwenda kutubu kanisani mara nyingi kadri aangukavyo?

  2).(a) Tofauti ni nini kiutendaji na kinamna ilivyokuwa ikitolewa Damu ya wanyama kama Sadaka ya ondoleo la dhambi katika Agano la Kale, ukilinganisha na damu ya Yesu kiutendaji na kwa utolewaji wake kwa mjibu wa Agano jipya au Biblia kwa ujumla?

  (b) Ni nini tofauti ya Dhambi na Kosa, na nikipi kati ya hivyo huondolewa Kwa damu ya Yesu pekee?

  (c) Wanadamu hutendeana makosa au Dhambi ukilinganisha na, Yesu katika ile sala aliyo ifundisha kwa wanafunzi, aliposema “…utusamehe makosa yetu…..”

  Nakoma hapa nikikungojea nikitegemea mengi toka kwako ili nijifunze tafadhali.

 10. Bwana Mabinza rafiki yangu, neno atendaye dhambi ni ibilisi kwenye tafsiri za asili lina maana hii kwamba; mtu ambaye kutenda dhambi ni sehemu ya maisha yake ya kila leo, au mtu mwenye kuzoelea kutenda dhambi huyo ni wa ibilisi/shetani.

  lakini halina maana kwamba mtu aliyeokoka ambaye dhambi si mazoea yake, ikitokea ameanguka dhambini ati anakuwa mali ya shetani/ibilisi.

  La sivyo Musa alitakiwa awe mali ya shetani,na hata shenitani alidhani hivyo,lakini ilibidi apambane na malaika wa Bwana

 11. theolojia n nzuri tena sana. inasaidia kutambua mengi lakini kumbuka kuwa mambo ya kufunuliwa na roho ni mazur zaid kuliko mapokea ya kibinadamu pia kumbuka kuwa mambo ya rohoni. kazi kubwa ya roho ni kutufundisha na kutukumbusha na kutupasha mambo yajayo YAHONA16:13-15, Lakini si kwamba tunapinga theolojia hapana.nakumbuka neno linasema ktk 1WAKORITHO 2:10-16 mtu aliye rohoni hawezi kutambulika na mtu kwa sababu yeye yupo ktk ulimwengu mwingine ameamishwa ktk roho ameket pamoja na Mungu aliko ISAYA 57:15. ukitaka ujua mafumbo ya roho ni lazima kukaa ktk darasa la Roho mtakatifu ili akufundishe siri za Mungu.
  KWA HABARI ZA DHAMBI
  Yesu alikuja kwa kazi ya uwaweka huru wanadamu ambao hapo mwanzo walikuwa ni watumwa wa dhambi. na kuwa ktk vifungo vya aina mbalimbali,na neno linasema ktk YAHONA 8:32 hiyo kweli ni neno la Mungu na huo uhuru unao zungumziwa ni kwa habari ya kutokuja haki zako ktk kristo usipo zijua haki zako ktk kristo ni lazima shetani atakusumbua na kukutesa kwa maana hujaijua kweli ya kristo ktk hosea 4:6 huko kuangamizwa kkwa kukosa maarifa ambolo ni neno la Mungu. ukijua kazi ya msalaba utajua hata jinsi inavyo kupasa kumuhubiria mwenye dhami utajua kuhurumia kama yesu anavyo taka paulo ktk nyaraka zake amesema wagaratia 5:16a. ukienenda kwa roho huta zitii tamaa za mwili mwili huwa hauokolewi ila Roho ndiyo inayo okolewa mwili ni wadunia utarudi mavumbini.ukisikiliza mwili ni lazima utashindwa tu.ktk mambo yote hatuwe kwa akili zetu hata kushinda dhambi hatushindi kwa akili zetu bali ktk yeye hatutia nguvu,iweje sasa ushindewe na shetan somo nlilo lileta .Kristo akingia ndani ya mtu huwa anaondoa kila uchafu wa dhambi na huyo mtu anakuwa safi amahesabiwa haki bure pasipo matendo yake lakini haiishii hapo inampasa huyo mtu kujifunza zaidi neno la Mungu ili aweze kutambua fikra za mwovu 2 kOR usipo zijua fikra za shatani nim lazma utaingia ktk dhambi tu. 1yahana 5:18 ili usingie ktk dhambi ni lazma ukilinda uyakataa mambo ya ulimwengu na kuto endelea kutenda dhambi na inawezekana kama kweli neno umelipata vizur. Hata binadamu afya ya mwili wake unajengwa kwa chakula bora.Na kuishi kitakatifu inawezekana bila kutenda dhambi kwa maana Mungu hawezi kutuambia usifanye hivi wakati anjua huwezim kufanya Mungu anasema tusitende dhambi kwa sababu anajua kuwa huo uwezo wa kushinda endapo utajikabidh kwake na roho mtakatifu wa kukuongoza sehemu za hatar kama umejaa atakuongaza. hata kama mtu kakuletea dhambi roho atakijulisha hilo nmerishuhidia jins roho anavyo tenda kazi ukikataa kuongozwa naye na laziama utaingia ktk makosa maana umelataa wewe mwenyewe kupngozwa naye.
  MUNGU AWABARKI
  MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI AYUBU 22:21

 12. Mabinza umemaliza kusemezana na Baraka. Basi rudi sasa tuuangalie ukweli kuhusu mtu aliyeokoka kutenda dhambi.

  Halafu ni vema tukakuwa pia kimtazamo na ufahamu kupitia maarifa juu ya Mungu. Naona Mabinza na Baraka mnaponda Theolojia, lakini ni kwa sababu tu hamfahamu kwa undani maana yake ni jinsi inavyohusika kuwafanya hata ninyi muwe angalao na ufahamu wa Mungu.

  Usipojua theolojia utajikuta unang’ang’aniza kuitafsiri biblia kwa mtazamo wa kisukuma na kihaya wakati yaliyoandikwa hayakuwa yanaandikwa kwa wasukuma au wahaya moja kwa moja.

  Ndio maana mnapotosha vity vingi sana katika kuyafafanua kwenu maandiko.

 13. Mpendwa Baraka,
  Kama jina lako lilivyo nimebarikiwa sana na hoja ulioileta hapa, ni kweli kama mtu akija na ujuzi wa ki-thiolojia, atakuwa off-side katika somo na fundisho lako. Lakini kiukweli, ipo haja kubwa sana ya watoto wa Mungu wajiulize kama ipo sababu ya msingi ya kudai kuwa wao kweli ni watoto wa Mungu huku, wakishindwa nashetani na kujilisha kwa dhambini zao, wakati tayari walishafutiwa hatia hiyo. Si jambo dogo kuuacha udini na kuitazama ile kweli, Neno linasema kuwa, ‘watu wanapenda giza kulikoni nuru!’ kwa maana nyingine ukisema ile kweli, tegemea kukosa sapoti ya watu wa Dini. Mkandya nimempenda sana kwa sababu, anaonyesha waziwazi aina ya watu katika tabia zao Nne kuu. Mkandya anajua mambo mengi na makubwa makubwa ya Neno la Mungu, hivyo anategemea pia kuona kila fundisho lijalo ni lazima liwe la kiwango chake, lakini sana zaidi anategemea kuona hoja inayoikiri ile kweli aijuayo! Hali kama hiyo si ya Mkandya pekeyake, watu wengi hufanyia kazi zaidi “Postive pole” na kuiacha “Negative pole” ikielea hewani bila jawabu, jambo ambalo haliwezi kumfikisha mhusika katika kisima cha ile kweli yote. Thioloji na elimu zingine za dini, zimewapa watu kiburi na kujihakikishia kibali cha kuwa wamekubalika na Mungu mwenyezi kuwa wao ni watenda kazi wasio nasababu ya kutahayari, kumbe ni vipofu na masikini sana! Wanazubaishwa na wao kuwazubaisha wenzi wao kwa vipawa na miujiza, huku wakiliacha Neno la Mungu ambalo ndiyo kweli yote, wanadhani kwamba, ati kwakuwa wana vipawa vya Roho mtakatifu basi, wanaye na Roho mtakatifu, aaawapi, hiyo ni kamali, Karama za Mungu hazina majuto Rum. 11:29, unaweza kushusha hata moto toka mbinguni uje ulimwenguni kumbe wewe, tayari ni mfu wa miaka mingi!

  Baraka, usishangae kuona watu wakionekana kwa macho kuwa wameshindwa kuacha Dhambi, usifikiri hivyo, hao hawajashindwa na shetani hata kidogo ila, Shetani ndiye baba yao. Biblia inasema ‘Mwana hafanyi kazi, isipokuwa kamuona baba yake akifanya kazi ile,’ na Katika 1Yn. 3:8 inasema, “atendaye dhambi ni wa shetani” full stop. Shetani hafanyi tena Dhambi, yeye yumo humohumo dhambini, huwezi kusema samaki kuwa majini anaoga, hasha, humo ndimo mwake! Kama habari yenyewe ndiyo hiyo, wewe utashangazwa na nini kusikia ama kuona kuna watu wanashindwa na shetani? Baraka, pengine ndiyo maana Mkandya kasema, umejaribu kuleta hoja usiyoijua, lakini kwa upande wangu labda niseme tu kwamba, si kwamba hauijui, ila hivyo ndiyo unavyojua! Unashangazwa kuona na kusikia Mtu asemaye ameokoka bado yumo zambini. Mpendwa, Waamini wapo wa aina tatu Kanisani, sikia;

  Kundi la kwanza ni wale wasioamni hata kidogo Neno la Mungu, lakini wamo kanisani kama kawaida, japo Neno wanalisikia likisema, dhambi ni kutokuliamini Neno la Mungu, wao wamo tu, na habari huingilia upande mmoja wa sikio na kutokea upande wa pili, hawaelewi chochote hata uwachune ngozi ‘Kusikia kwa kenge mpaka damu itoke masikioni! – wasukuma husema’ Biblia inawasema watu wasioamini ni wa ibilisi Luka 8:13 inasema, wanasikizishwa Neno lakini mawazo yao huwa mbali na Neno, hufikilia mali, vitu nk. Watu wa aina hii hawaguswi kabisa na Ujumbe wa Mungu katika mioyo yao lakini kanisani nao wamo, na hawa huongoza katika kuanguka lakini hawatubu kama lile kundi la pili!

  Kundi la pili; Wamo wanaojifanya waamini, hawa Biblia inasema katika Luka 3:8 kuwa, “Wanajifanya ni wana wa Ibrahimu, lakini bila Matunda yapasayo toba!” kwa hiyo wanaojifanya watoto wa Ibrahimu (hujifanya wameokoka, watoto wa Mungu) huko makanisani lakini hawataki kutubu ili waokolewe. Mchezo wao huwa ni kutubu kisha kuanguka,….. ni tubu anguka, tubu anguka,.…ngoma huwa hiyohiyo tu, mpaka basi! Na kwa vile thiolojia inafundisha kuwa, hata kama umeokoka ni lazima utatenda dhambi tu basi, lazima kila ukizini, ukiiba, ukiongopa, ukichonganisha watu, ukienda kwenye matambiko nk, njoo utubu tu, Mungu atakusafisha tena kwa Damu ya mwanaye Yesu kristo. Wanadhani Yesu ni kama mwigizaji, hufa na kufufuka, kisha hufa tena na kufufuka, na wakati mwingine hufa na kufufuka, mara chungu nzima kilasiku ili kusafisha dhambi za walokole chungu mzima, wenye eti kuangukaanguka dhambini na kutubu kila siku ulimwenguni mote! hao si wana wa Ibrahimu kikweli, wanajifanya tu, imani yao ni yakitambo kidogo tu kisha husongwa na Dunia na hivyo kurudi Duniani tena Lk. 8:14 inathibitisha hivyo!

  Na kundi la tatu; wamo waamini halisi, hawa huliamini Neno la Mungu lote, tena hawana mashaka hata kidogo, imani yao ni kama ya mtoto mdogo, Neno hulipokea na kuliishi kama llivyo Lk. 8:15, hawa hzaliwa na mung hivyo hawatendi dhabi hawana dhambi ya kutubu tena 1Yn. 319.

  Kwanini Shetani naye yomo kanisani, zipo sababu nyingi, lakini iliyokubwa ni Imani, imani ndiyo ibaada, shetani naye anaamini juu ya Mungu kuwa ni mmoja kama ambavyo Waamini wote wanavyoamini, vulugu huja katika kuliamini Neno la Mungu, maana kuamini kuwa Mungu ni mmoja si hoja , hoja ni Kuliamini Neno, Maana Dhambi si kutoamini Mungu ni mmoja tu peke yake, bali ni pale mtu asipoliamini Neno la mungu lote. Kama ni kuamini juu ya uwepo wa Mungu, shetani amefanikiwa sana katika hilo, kwani yeye huamini kuwa Mungu ni Mmoja tena anaamini hivyo kwa kutetemeka Yak. 2:19; Ndiyo maana naye kanisani yumo na bila Roho mtakatifu kumugundua ni kazi kwelikweli, kujua na kugundua makanisani, tujiulize Je, tunaamini Mungu zaidi ya shetani? (Mtu asijibu haraka swali hilo, ajihakiki kwanza!)

  Baraka za Bwana zitawale, tupate amani ya Kweli itokayo kwake, ili tuwe na tuishi kitajiri.

 14. Mabinza katiak mchango wako kuna mambo makubwa yafuatayo:
  1. Maana ya wokovu
  2. Suala la aliyeokoka kutenda dhambi tena
  3.Tofauti kati ya dhambi na kosa
  4.Kusamehewa/kutokusamehea kwa aliyeokoka akitenda dhambi
  5. Tofauti ya kuokoka na kuongoka
  6. Maana ya toba

  Kwa leo nitajaribu kusemea machache ya hayo mambo hasa yanayohusu hoja ya msingi.

  Mabinza toba au kutubu ni kukubali makosa au kujuta moyoni kw a ajili ya makosa uliyofanya. Makosa hayo kama yatakuwa kinyume na amri au neno la Mungu huitwa dhambi au uasi.

  Baada ya mtu kutubu huja kitu kinaitwa uongofu au kuongoka, ambako ni kuamua kugeuka na kuelekea njia sahihi au ya haki kinyume na njia ya ukosaji ambayo ulikuwa unaishi kwayo hapo kwanza.

  Mtu akishaongoka kinachofuata kwake ni wokovu au kuokoka ambako neno lake la kibiblia huitwa ‘sozo’ lenye maana ya kusamehewa dhambi, kuondolewa laana, kuponywa magonjwa, kujazwa amani ya Mungu, nk. Neno wokovu lina vitu vingi sana ndani yake ambavyo ndiyo hasa yanapaswa kuwa maisha ya mkristo/mwamini.

  Kwa hoyo si kweli ulivyosema, ati kwamba uongofu (wongofu kama ulivyoandika mwenuewe) ndio hatua ya ukamilifu wa wokovu wa mtu. Mabinza sijui haya umeyatoa kwenye biblia gani na ni nani aliyekufundisha. Haya wala si mambo ya ufunuo ni elimu kabisa ya kawaida tu ambayo iko kwenye vitabu.

  Kuhusu dhambi, bila shaka unajua kuwa kila kisicho haki ni dhambi, na kila kinachofanyika nje ya imani ni dhambi pia. Sasa ningetaka bwana Mabinza uniambie ni makosa gani ambayo si dhambi lakini unatakiwa kuyatubia kwa Mungu. Na ufikirie kuwa ni mangapi umewahi kufanya without faith.

  Pia uniambie maneno kama “mwenye haki hunguka mara saba….(nimekosa muda wa kutafuta huo mstari),na uniambia mistari hii alikuwa anaambiwa mpagani au mwamini (1Yoh 2:1b My little children, these things write I unto you, that ye sin not. And if any man sin, we have an advocate with the Father, Jesus Christ the righteous:)

  Pia mfikirie Daudi ( a man after God’s heart) mtu aliyeufurahisha moyo wa Mungu, uone alianguka mara ngapi.
  ( Wala usidhani natetea mwamini kuanguka ,la hasha)

  Kuna ukweli ambao waliookoka huwa hawataki kuusikia wala kuukubali nao ni huu kwamba aliyeokoka anaweza akatenda dhambi.

  Wengi hawautaki kabisa huu ukweli,lakini ikifika mahali ambapo wahaya husema ‘where rubber meets the dust’ mambo huwa tofauti. Mahali hapo kwa ufafanuzi panaitwa kwenye uhalisia wa mambo.

  Cha kuzingatia ni kujua aliyeokoka akitenda dhambi nini hutokea au nini kinatakiwa kufanyika. Na hapo ndipo litakapokuja suala uliliosema bwana Mabinza, la kusamehewa au kutosamehewa aliyeokoka akitenda dhambi.

  Nikomee hapa kwa leo

 15. Mkandya mtumishi,
  Kwanza naomba ladhi kwa kuchelewa kukujibu. Rafiki, wewe nivumilie tu kama sijasema kwa ufipi uupendao. Sasa ni hivi:-
  Umeniuliza kuwa, “….je wewe tangu umeokoka hujawahi hata siku moja kutubu mbele za Mungu? Hebu kuwa mkweli na muwazi katika hili…..” – jibu: NIMEWAHI!
  Mkandya kutubu ni neno la jumla sana, sitalielezea hapa kwa sasa, lakini kwakifupi, “Toba” huambatana na “Ungamo”. Lakini cha msingi hapa ni kuelewa wewe kwa sasa ni nani; Ukijijua wewe unanafasi gani kwa Mungu ndipo utaielewa haki yako unayopaswa kuidai kwa Mungu. Mwamini akishaokolewa tayari, katika maisha yake ya wokovu hutubu “Makosa” na si “Dhambi” – soma, , 2Nyak. 33:19, lakini yote mawili ni hatia, zenye kiwango tofauti. Dhambi ni Kifo, Rum. 6:23. Na mwenyekusame Dhambi ni Mungu tu peke yake Mk. 2:7, dhambi husamehewa au huondolewa mara moja tu, kama ambavyo iliigia kupitia Mtu mmoja (Adamu) vivyo hivyo mwenye kuiondoa alikuwa Mtu mmoja (Yesu) Rum. 5:12. Dhambi huondolewa kwa sadaka ya Damu, dhambi ikiondolewa tunapatanishwa na Mungu Rum. 5:9-11.

  Mkandya, ukishafikia uongofu yaani wokovu kamili, unakuwa huna Hati tena ya mashitaka kwa Mungu, hati ya Mashitaka hayo inakuwa imekwishafutwa na Yesu ka njia ya Msalaba Kol.2:14. Ukiwa ndani ya maisha hayo hutendi tena Dhambi maana unakuwa umetiwa Mhuri wa Roho mtakatifu ili kuthibitishwa kuwa sasa wewe ni Mwana wa Mungu, Neno la Mungu linasema, Kilichozaliwa na Mungu hakitendi dhambi 1Yh. 3:9. Na ukitenda dhambi unakuwa ni mali ya Shetani 1Yn. 3:8, naamini unajua matokeo ya kuwa mali ya Shetani! Kwa hiyo aliyeokoka hatendi tena dhambi, ukitenda hupati Msamaha wa dhambi hiyo maana haipo tena Damu ya kumwagika mara ya pili! Waweza kujirithisha katika hili kupitia pia 2Pet. 2:22 kwakweli hutapata tena msamaha, unakuwa na dhambi ya milele Mk 3:29, hutasamehewa kamwe, mkubwa! Mt. 12:31-32.

  Tatizo la waamini wengi, linalosababisha Mungu asikamilishe wokovu wao na kupelekea waangukeanguke dhambini na kisha kutubu kila mara ni kwamba, WANAAMI, sawa, LAKINI HAWABATIZWI IPASAVYO! Waamini wengi hawajabatizwa kwa JINA LA YESU sawa na ile Mdo. 2:38 ili, waondolewe dhambi zao na kupata vipawa vya RM, ndiyo maana wamebaki kulialia na kuchezacheza na dhambi, na ijulikane kwamba, hata ukijifariji vipi Neno la Mungu lipo palepale kwamba, NI JINA LA YESU PEKEE NDILO TULILOPEWA TULITUMIE. Wagonjwa, wenyemapepo, vipofu nk, wanaponywa kwa jina la Yesu iweje, dhambi ziondoke kwa jina la baba na la mwana na la Roho mtakatifu, ambapo hapo tunaona wazi kuwa, hayo si majina au jina ila ni sifa tu? Sifa zaweza kuokoa na kuondoa dhambi? Neno litabaki kuwa Neno kuwa, “Hakuna jingine ambalo wanadamu wamepewa chini ya jua…isipokuwa ni jina la Yesu….” Mkandya, kama ulivyoniuliza mimi, nakuuliza nawe hivi; “Uwe mkweli tafadhali unadai kuwa wewe ni Mtoto wa Mungu, ulishaondolewa dhambi zako?” Kumbuka bila kuitekeleza ile Mdo 2:38, utakuwa Bado mpagani, maana dhambi ni kutoliamini Neno la Mungu, na wapagani hawaliamini Neno la Mungu!

  Labda kabla sijamaliza, nieleze kwa kifupi kuwa Mwamini licha ya kuwa ameokolewa hufanya makosa (ambayo yasiyo dhambi!) Najua inaweza kuwa vigumu kueleweka lakini maandiko yameeleza wazi kuwa Kabla ya Sheria dhambi ilikuwepo, na hivyo Torati ilikuja kutokana na Dhambi, kwa maana nyingine Torati ndicho kipimo cha Dhambi! Na tunajua pia kupitia Neno la Mungu kuwa, Haiwezekani kumpendeza Mungu kwa njia ya Sheri. Moja ya dhambi iliyo mbaya sana ni KIBURI, tunajua hivyo tokana na kile kilichompata Lusfa! Hebu tuseme kuwa, Kiburi kiwakilishe dhambi yoyote inayoitwa dhambi. Je, Mtu akiondolewa Kiburi, tuseme huwa hana kosa lolote ambalo linahitaji msamaha wa Mungu? Jibu siyo; Kwa nini siyo, wakati amesafishwa Dhambi zake? Biblia inasema,kwasababu ya Midomo tunakosea na humo ndimo hutokeza`mitego kwa mtu mbaya Mith.12:13. Kwa hiyo kukosea ni kutenda Dhambi? Hasha, Makosa ni kuvunja sheria ya Upendo, Yesu alisema, “Amri mpya nawapeni, mpendane” Yh. 13:34. Kwa hiyo utaona kwamba, Kosa ni kuvunjiana Sheria ya Sisi ka Sisi. Yesu wakati, anawafundisha wanafunzi wake kusali pamoja na mambo mengine alisema, “….utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tunavyowasamehe waliotukosea…..” Lakini pia katika sehemu nyingine sala hiyo inasomeka, “…..utusamehe DHAMBI zetu….,” lakini inamalizia kwa kusema kama sisi nasi tunavyowasamehe waliotuosea!
  Kwa nini? Kwasababu mwenyekusamehe dhambi ni Mungu tu Mk. 2:7, lakini kumbuka kuwa hatusamehewi au hatuondolewai Dhambi kwa vile tuliwaondolea wengine Dhambi zao! Wala hatukusamehewa dhambi kwa kumtimizia Mungu sharti Fulani. Akini hebu ona ili wewe usamehewe makosa yako, ni sharti umsamehe mwenzako makosa aliyokukosea wewe kwanza! Na sehemu ingine inasema, “nenda ukapatane na mdaawa wako kisha uje utoe sadaka” Kwa maana hiyo hapo, dhambi imesimama badala ya Neno kosa. Sheria ya Upendo inasimamia Uadilifu Zab. 19:8. Lakini kama nilivyotangulia kusema, mtu akiondoshewa kiburi chake, anakuwa ‘Safi’ lakini anakuwa yungali katika wigo wa kutenda makosa, Zab. 19:12. Makosa ni kuvunja maelekeza ya Sheria ya upendo angalia Mith. 16:20-23. Bali machukizo ni thambi Zab. 6:16-19.

  Kwakuwa ulisema nisiseme saaaana, natinga shughuli zako za Ofisi, basi hebu nimalizie na nukuu hii uliyosema, “Mabinza,kabla sijauchambua mchango wako ambao kwa sehemu unaukweli Fulani, lakini kwa sehemu kubwa pia mchango wako unapotosha kwa kuongea mambo makubwa ambayo wewe mwenyewe inaonekanahujayajifunza vyakutosha kiasi cha kuyaelewa na kuwafundisha wengine”

  Aaaa, katika hilo, sitalijibu, kwasababu sijajua umetumia kipimio gani na hata kufikia hukumu hiyo. Mimi kama mimi Neno hili tunalolijadili hapa siyo Neno langu, mwenye nalo ni Mungu, na analifunua kama apendavyo yeye na kwa makusudi yake, kupitia Roho wake mtakatifu. Inawezekana usielewe na kuona kama nababaisha hoja, lakini Roho anajua kiwango gani nipo kwa kazi hii, si shida yangu kujua saaaana, ama kupatia sana hoja, ninalolisema ndilo nililojaliwa! Upo wakati Neno likaeleweka tu kwa wanaokusudiwa lakini wasiokusudiwa likasikika kama Ngurumo tu, utanielewa vizuri ninachomaanisha ukisoma habari ya Sauli aitwaye Paulo katika kitabu cha matendo ya mitume, alipokuwa anaongea na Yesu. Kwakuwa Paulo ndiye aliyekuwa amekusudiwa yeye aliskia na kuelewa kile Yesu alichokuwa akikisema na kumaanisha, lakini kwa wale waliokuwa na Paulo, ujumbe ule haukuwahusu ndiyo maana waliishia kusikia Ngurumo tu! Hata hivyo, nashukuru kwakuwa kunakitu umekielewa na kuamua kukifanyia kazi kubwa kama hii uliyoifanya, Bwana aendelee kukubariki ndugu yangu.

 16. Bwana Baraka nimeshajua kuwa hoja uliyoileta hapa huijiu mapana yake,ispokuwa unaelewa kitu fulani tu ndani ya hiyo hoja ndio maana huwezi kabisa kujibu swali fupi nililokuuliza.

  Kwa hiyo naona siwezi kuendelea kujibu hoja zako maana ni kupoteza wakati, kwa sababu sidhani kama tunaweza kufikia mahali pa kuelewana.

  Vile unavyopangilia tu hoja zako kwa mtu mwenye kutaka kujua uwezo wa ufahamu wa aliyeandika hizo hoja atagundua kuwa uwezo wako ni mdogo au mtazamo wako uko ”biased”.

  Baraka nasema hivyo kwa sababu maudhui yaliyo katika hoja zako ni dhaifu sana ukilinganisa na hoja yenyewe uliyoileta. Mabinza akijibu, tutakuwa na kitu cha kujadili bila shaka, maana namfahamu anavyojenga hoja zake

  Uwe na amani tu Baraka wala usipate shida,nimeshakuelewa!

 17. naomba Mungu atie roho ya ufunuo apate kujua uweza wake na nguvu zake napenda kufunuliwa jambo na kia k2 ambacho mtu atakiongea haijalishi ni mtume na nabii au vyovyote vile kama halipo kimandiko hata akisema amefunuliwa uwo ufunuo uwambatane na neno s na hisia. 1kor 2:12 nmeyajua kwa sehemu niliyo kirimiwa na kristo shida kutoyajua mamlaka ya mwamin ktk \kristo ukiyajua utakuwa saf.MKANDYA je wewe unaishi maisha ya kushindwa kama hapo mwanzo ambapo hukuijua kwel?. na kama huajijua kwel na mamlaka yako juu ya shetan n yakupasa kuyatafuta. hivyo mimi Baraka ntazd kueleze nguvu ya iman maana nimeshuhudia ushind ktk iman s kwa kusikia kwa m2 fulan la!.Mkandya na ndugu wengne. hatupo kwa ajili ya kubishana aua kuoneshana ujuzi bali 2jenga ili kila mmoja we2 aishi amaisha ya ushindi ndani ya Kristo Yesu

 18. Baraka unajua unachokisema lakini au umekariri tu mapokeo?

  Swali langu hujajibu zaidi ya kuongea maneno mengiii yasiyo kwenye hoja.

  Umerukia hii mada kwa hisia tu ndugu yangu.

  Ngoja nione Mabinza atasemaje.

 19. kabla sjauijua kwel na kuatambua uwezo na nguvu zilizopo ktk iman (uchanga wa kiroho).chakula unacho kula kiroho unapo kuwa mchanga kinawezaa kukufanya uwe mshindi au dhaifu (chakula cha kiroho)nikawa na jiuliza nikapata majibu kuwa kristo n mweza . kwa kukosa kumjua na kuyajua maarifa twaanagamia hosea 4:6. kwa kumtii roho na kuongozwa nimeona maajabu na ushind mkubwa. 1yahona 5:18, sio hulindwa bali hijilinda yeye kama yeye. kwa kuwa yu ndan ya kristo na kristo yu ndan yake hivyo huwezeshwa. ustegemee. kuwa wewe ukae tu alafu yesu aje kukusaidia hapana kwa kumtafuta mithali 8:17. mtu anapo okoka anakuwa na haki kwa mungu haki inayo patikana kwanjia ya imani. kwa kadri unavyo zidi kutafuta mungu unazid kuupata utakatifu(utukufu wa kimungu) siwez kuendelea kukiri udhaifu wakati yesu ni mweza na mungu hajui kuwa kama mimi nimewahi kutenda dhambi maana nilipo tubu dhambi mungu alisahau uwa me ni mwovu bali anajua kuwa mimi ni wake nami ni wangu.wapendwa yatupa kumjua mungu kuliko shetan watu wengne wako tayari kunua vtabu vya shuhuda za kishetan na kusilizamafundusho ya mashetani lakin kijifunza neno 2wa wanalala 2tim 3:6-7na mstar12-15, 2tim 4:3-5.namuomba mungu wa bwana wangu yesu kristo awatie roho ya hekima na ufunuo macho ya mioyo yenu yatiwe nuru. si kwamba nimekwisha kufika,au mkwisha kuwa mkamilifu. la! bali nakanza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na kristo yesu.ndugu sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika ila natenda neno moja tu. nkiyasahau yaliyo nyuma kiyachuchumilia yaliyo mbele.nakaza mwendo niifikie mede ya ya thawabu ya mwito mkuu wa mungu ktk kristo yesu.BASI SISI TULIO WAKAMILIFU(TUMEKAMILISHWA KTK KRISTO)NATUWAZE HAYO NA MKIWAZA MENGINE KTK JAMBO LOLOTE MUNGU ATAWAFUNULIA HILO HILO LAKINI HAPO TULIPO FIKA NA TUENENDA KTK HILO. ukisha tubu dhambi hupaswi kujiona kuwa una dhambi damu ya yesu si kam ya mbuzi na kondoo yenyewe inaosha kabisa haibakisi kitu.kiri kushinda na si kushindwa utakula matunda ya midomo yako.OMBA ,SOMA NENO NA KURTAFAKARI,FANYA IBADA, HUBIRI KWELI YA KRISTO. JITAMBUE WEWE NI NANI KTK KRISTO s HUDUMA YAKO JE KTK WEWE NI NANI.JIFUNZE KWELI S KWA KUONYESHA KUWA UNAJUA ILA ILI WATU WAIJUE KWELI YA KRISTO IPATE KUWAWEKA HURU NA DHAMBI.MWOMBE MUNGU AJIFUNUE KWAKO. KUNA VITU KADHAA VINAVYO WAFANYA WAKRISTO WENG KISHINDWA KWA LEO NIISHIE HAPO SKU NYINGINE MUNGU AKINIPA KIBALI NITAVSEMA.AMANI IWE NYANI WATU WOTE.

 20. Bwana Mabinza, kabla sijauchambua mchango wako ambao kwa sehemu una ukweli fulani, lakini kwa sehemu kubwa pia mchango wako unapotosha kwa kuongea mambo makubwa ambayo wewe mwenyewe inaonekana hujayajifunza vya kutosha kiasi cha kuyaelewa na kuwafundisha wengine.

  Nataka kwanza nikuulize kama nilivyomwuliza Baraka hapo juu, kwamba je wewe tangu umeokoka hujawahi hata siku moja kutubu mbele za Mungu? Hebu kuwa mkweli na muwazi katika hili.

  Baada ya hapo sasa tutaendelea kujadili swala la mtu kushindwa na shetani.

  NB: Mabinza uwe unaandika kifupi fupi ili iwe rahisi kusoma mchango wako kwa ukamilifu maana mara nyingi wengi tunakuwa ofisini tunafanya kazi.
  Asante.

 21. Mtumishi Baraka,
  Nimefurahishwa sana na Fundisho lako juu ya “Iweje ushindwe na Shetani” Mimi pia kama wewe, siamini kuwa mtu aliye kamili katika wokovu anashindwa na Shetani! Maandiko yanatueleza wazi kwamba Tukiwa ndani ya Kristo na yeye atakuwa ndani yetu. Vile vile Neno hilohilo la Mungu linasema kwamba, “wote waliompokea aliwapa uwezo wakufanyika wana wa Mungu, wale waliaminio jina lake Yesu kristo”. Mpaka hapo tu, japo yapo maandishi mengi yanayoonyesha kuwa waliokoka ni washindi, inashangaza kuonekana tena kuwa hao wasemao kuwa wameokoka na haohao wakilio kuwa, Yesu ni Bwana wao, eti tena ni wenyekushindwa na shetani, si wenye kushindwa tu bali pia eti tena huanguka dhambini na kutubu tena!

  Pengine, kabla ya kufikia mwisho wa fudisho lako hili zuri tuyaangalie maandiko ili tujue Biblia inasemaje juu ya Dhambi na kama kweli kupo kuanguka na kutubu tena ikiwa mtu amekwisha okolewa na kufikia kiwango kamili cha wokovu. Katika Yohana 15:5 inasema, “maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote” kwa mstari huo, inaonyesha kwamba, watu hushindwa na shetani kwa sababu hawanaye Yesu kristo ndani yao, licha ya kujiaminisha na hata kukili kuwa wanaye na kwamba wanamtegemea Yesu! Katika Rumi 10:9 inasema, “kwa sababu, ukikiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.” Watu wote wakolewao, hukiri na kuamini juu ya Yesu kristo, lakini wanakuwa hawamtegemei katika safari yao ya wokovu. Utakuta watu wa jinsi hiyo huwa wanafanya bidii yao wenyewe kwa, akili zao, kwa maarifa yao, kwa ujuzi wao, kwa nguvu zao, kwa mafundisho na maelekezo ya Dini zao jinsi ya kushinda Dhambi. Wanajitahidi sana na kwa bidii sana kuacha dhmbi, mfano mtu akishaokoka tu, ikiwa alikuwa mlevi kwa mfano utamsikia, mimi bwana nimeokoka siwezi tena kunywa pombe, na kweli kwa akili zake na bidii yake hujizuia kunywa pombe, kwa kipindi Fulani huweza kufanikiwa kuacha pombe ile, lakini kwa kuwa kuacha kwake kulitegemea akili na bidii yake, mtu wa jinsi hii lazima ataanguka tena katika ulevi! Neno la Mungu lazima liwe vile vile kama lilivyotamkwa “pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote” (Yh.15:5).

  Kumbe, tunapaswa kuwa, tunapomwendea Yesu ili atuokoe yatupasa kwenda kama tulivyo, twende na uchafu wetu wote bila kujaribu kutumia akili zetu wenyewe kuacha uchafu huo ili kumpendeza Mungu, si kazi yetu wa kwa kwa mafundisho na tafsri za Dini, ili kujisafisha dhambi ama kujitahidi kwa bidii zetu bila kuhitaji msaada wa Mungu katika kuacha Dhambi zetu! Ukisoma ile Isaya 43:27 inasema, “baba yako wa kwanza alifanya dhambi na makalimani wako wameniasi” Tunapaswa kwenda kwake kama tulivyo huku tukijitambua kuwa sisi ni wenye Dhambi na hatuwezi kujisafisha kwa bidii zetu wenyewe. Tukisha kukiri na kuamini hivyo, ndipo Yesu huja kamili kwetu achukue jukumla la kutuosha tutokane na uchafu wetu wote, hayo ameyasema mwenyewe katika Mt. 11:28, “njoni kwangu ninyi nyote wenyekulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Kwa hiyo, ile kujikataza kufanya machafu yako kwa sababu umeokoka, huwezi, maana huna nguvu hiyo, na ukilazimisha kuigiza hilo ni lazima utarudia tu kufanya dhambi, maana Neno linasema mtu hawezi kujiondoa katika dhambi mwenyewe, soma methali 20:9. Upotoshaji mkubwa wa watu wenye kujifanya kuitafsri au kuifafanua biblia huwakosesha watu, na kuwalazimisha kubeba mzigo watu wasio uweza kwa mafundisho yao yakidini yaliyojaa hekima za kibinadamu, ambao ni kinyume na Neno la Mungu, kama Isaya 43:27 anavyosema.
  Wokovu hukamilika kwa hatua tatu, kwanza, Mtu akisha kuamini na kukiri kwa kinywa chake juu ya Kristo hatua ya kwanza hubatizwa kwa jina la Yesu kristo, na katika hatua hii ya kwanza, hupokea ondole la Dhambi na vipawa vya Roho mtakatifu na kuwa mwamini (Mdo. 2:38). Baada ya Mwamini huyo kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo, kama Neno linavyoagiza katika hiyo matendo 2 mstari wa 38, huingia hatua ya pili, hapo hutakaswa kwa Neno, hupewa moyo wa nyama na kuondolewa ule moyo wa jiwe usio wa utii na kupewa huo moyo mpya wa nyama ili atamani mambo mapya, hapo Mungu hutia sheria yake ndani ya Mwamini ili kumuwezesha mwamini aanze kuzishika hatua kwa hatua na kuzitenda Eze. 36:26, Zab. 51:10. Kwa kipindi hicho yani kutoka hatua ya kwanza na ile ya pili, Mungu huandaa ule moyo wa Mwamini kuwa makaazi ya Roho mtakatifu. Kaika hatua hii ya pili ambapo pana, utakaso na vipawa vya Roho mtakatifu kama vile, kunena kwa lugha, uponyaji nk, waamini wengi hubaki hapo kwa kujiaminisha kuwa tayari wanaye Roho mtakatifu na tayari wamekwisha ongoka. Lakini kiukweli mwamini katika hatua hiyo huwa bado hajakamilika katika kuufikia wokokvu kamili yaani Wongofu. Kutoka katika hatu hii ambayo hata Yuda naye aliifikia, mwamini huwa si kamili na Roho mtakatifu anakuwa hajahamia kwa mwamini wa kiwango hiki, japo mwamini huyu anavipawa vya Roho mtakatifu na pia amekwisha takaswa kwa lile Neno la Mungu, bado huwa dhaifu na kutokuwa nje sana na mambo yake ya kale, 1Pet. 4:2 inaizungumzia hali hii ya mwokovu awapo katika hatua ya awali; Mwamini akiwa yungali katika hatua hizi hafai hata kupewa uongozi katika Kusanyiko (Kanisa) maana kuna uwezekano akafutwa katika kitabu cha uzima akiasi Neno la mungu na kufanya dhambi. tunaweza kusema kuwa katika hatua hizi mbili za awali mwamini bado hajaokoka kikamili – yaani hajaongoka hivyo hafai kuwa Kiongozi, Kiongozi katika kusanyiko (Kanisa) lazima awe aliyefikia wokovu wa kiwango cha uongofu, 1Timo 3:6 inasema hivyo!

  Hatua ya tatu katika wokovu ni Kuongoka, kuongoka ni ukamilifu katika hatua ya mwisho ya wokovu, ni kuwa kamili katika Neno, kuliamini lote pasipo na shaka hata kidogo, kama aminivyo mtoto mdogo (Mat. 18:3). Ktika hatua hii Mwamini hutiwa mhuri na Roho mtakatifu Efe. 4:30, kuwa uthibitisho wa utakatifu na kufanyika makaazi ya Roho mtakatifu, na kuwa mwana wa Mungu kwa sababu anaongozwa na Roho mtakatifu (Rum. 8:14) na hapo ndipo mwamini huweza kuwaimarisha waokovu (Lk. 22:32) hapa mwamini huweza kuwa kiongozi katika kusanyiko maana tayari huwa amekwisha vionja vipawa vya Roho mtakatifu kwa ukamili, na Roho mtakatifu mwenyewe huwa tayari anakaa ndani ya mwamini. Katika hatua hii mwamini akifanya Dhambi husabiwa kama mbwa ayarudiaye matapishi yake au nguruwe ajivurugaye katika uchafu mara tu bada ya kuogeshwa, na hali hiyo yu mkini mtu huyu asingesikizishwa injili mwanzoni, maana hali yake itakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza 2Pet. 2:22 hapati tena msamaha, anakuwa na dhambi ya milele Mk 3:29, hatasamehewa kamwe! Mt. 12:31-32. Labda nimalize kwa kusema hivi; MTU ALIYEUFIKIA WOKOVU KAMILI HATENDI DHAMBI, maandiko matakatifu katika Yohana 3:9 yanasema, kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi Dhambi! Sasa linganisha na ile matendo 1728-29 inasema sisi ni watoto wa Mungu. Zamani ilikuwa ni Enzi za ujinga, Mungu akawa kama dhambi hazioni, lakini sasa Mungu anaagiza wote watibu Mdo 17:30.

  Wote muendelee kubaikiwa na Bwana.

 22. Amina mtumishi, Asante sana kwa hilo fundisho mana ni wengi tulikuwa gizani. Binafsi umenifundisha na kunifurahisha! Ubarikiwe.

 23. Mtumishi wa Mungu Baraka tangu uokoke ulishawahi kutenda dhambi hata mara moja?
  Ubarikiwe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s