Mamlaka Yetu Katika Kristo!

neno,

Sisi tunaomwamini Bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wetu, Neno la Mungu linatuambia ya kwamba Yeye yuko ndani yetu na sisi tumo ndani yake, pia linatuambia tumeketishwa pamoja naye katika ulimwengu wa roho juu sana kupita falme na mamlaka zote (Waefeso 1:20-23, 2:6). Neno la Mungu pia linasema aliyeko ndani yetu ni mkuu kuliko aliyeko katika dunia, yaani ibilisi (1 Yohana 4:4).

Kama vile hiyo haitoshi Bwana Yesu alituambia hivi:

Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na ng’e na nguvu zote za yule adui na wala hakuna kitakachowadhuru – Luka 10:19 SUV

Hivyo hatuna sababu yoyote ya kumwogopa ibilisi shetani, mapepo na makuadi wao, maana tayari wameshawekwa chini ya miguu yetu. Tunao ushindi, naam zaidi ya ushindi kwake yeye aliyetupenda hata akajitoa kwa ajili yetu, yaani Bwana Yesu mwokozi wetu! Kama watenda kazi pamoja  na Kristo, tusisite kuyatumia mamlaka tuliyonayo ndani yake kuwafungua wote wanaoteswa na iblisi kila hitaji linapojitokeza.

Mpendwa, tembea katika mamlaka uliyopewa na Bwana Yesu, wewe ni mwakilishi wake hapa duniani, wewe ni balozi wake popote pale ulipo, na kama balozi, mamlaka ya mbinguni yako pamoja nawe. Hivyo basi tuyatumie mamlaka tuliyopewa kuuharibu ufalme wa iblisi na kazi zake ili kuueneza na kuujenga ufalme wa Mungu!

Mbarikiwe na Bwana Yesu!

–Patrick

Advertisements

4 thoughts on “Mamlaka Yetu Katika Kristo!

 1. Shalom,nimebarikiwa na neno nami nazidi sana katika kuomba na nimeanza mazoezi ya maombi ya hatari na nishaanza kujifungua mwenyewe kwa maombi na vita na falme na nguvu za giza zinaendelea tuungane kwa mamlaka tuliyopewa ya kuhesabiwa wana kuvunja ngome zote za ibilisi.Amen

 2. Mpendwa Pratrick,
  Nimeyakubari mafundisho yako, Neno la Mungu ndilo njia, ni kweli, ni Roho tena ni uzima! Ulichokiandika hapo hakihitaji ujuzi wowote wa ziada kuelewa kuwa TULISHAKWISHA KUKABIDHIWA MAMLAKA YOTE! Ni ukweli usiopingika kwamba, hatupaswi kumuogopa ama kumhofu Shetani na Malaika zake. Yesu aliyajua hayo yote ndiyo maana akatukabidhi “Uwezo” huo ambao ni wa ki Mungu, kwani hutokeza majibu yake kupitia kutamka tu kwa kinywa na kuamini tu kwa Moyo.

  Nikifikia hapo ndipo ninapomwelewe vizuri Mungu anaposema kuwa, UKIKILI kwa kinywa ya kuwa Yesu ni Bwana na UKIAMINI ya kuwa alikufa na kufufuka wewe tayari umeokoka. Kumbe nguvu tunayo katika KINYWA na katika MOYO (Inasemwa, Mtu hukili kwa kinywa na huamini kwa moyo, maana mawazo ya Mtu yamo moyoni mwake!).

  Ama kweli kinywani mna nguvu na katika Moyo mna uwezo. Nikweli, kwa ulimi tunaweza, kulaani ama kubariki – au niseme kwamba kwa ulimi twaweza, kuangamiza chochote kile cha Muovu na kwa ulimi twaeza kuokoa chochote kitoke mikononi mwa Yule mwovu, lo, ni ajabu kweli, kuna wakati hujiuliza, hivi upendo wa Baba yetu huyu MUNGU mbona hauwezi kufikilika ama kuchambulika na kujua kiwango cha upendo anaotupenda, hata kuwekeza kiasi kikubwa cha uweza wake kwetu kwa namna hii ya kutisha ki rahisi rahisi tu hivi bila gharama sisi kuingia!

  Wapendwa, ni vizuri kufarijika na uweza huu wa kuwatimua mapepo, kukanyaga nge na nyoka, na hata kufanya miujiza mikubwa mikubwa, lakini kutoelewa kama kweli uweza na mamlaka uyatumiayo hayatokani na Mwovu si busara hata kidogo! Yafaa nini kutoa kiasi kikukbwa cha mali zako kununua HEKIMA wakati huna UFAHAMU? Unaweza kukataa hilo, lakini huo ndiyo ukweli, maana wapo waendeshao magari bila ufahamu juu ya sheria za Barabara. Kwa kifupi, WENYE UWEZO WA KULITUMIA JINA LA YESU, NA KUFUKUZA MAPEPO NA KUKEMEA MAGONJWA, KUKANYAGA NGE NA NYOKA, KULA VITU VYA KUFISHA NA WASIFE ni watoto wa Mungu tu, wengine wote ni waendeshao Magari bila kujua kanuni na sheria za Barabarani. Neno linasema, kunawatu watakao sema kuwa, waliponya na kukemea mapepo nk, lakini Bwana atawatimua mbele zake na kusema hawatambui. Watu wengi hujidanganya kwa upako na karama na kujiaminisha kuwa ni watoto wa Mungu, bila kujari sifa zinazomfanya na kujipatia haki ya kuwa Mtoto wa Mungu. Inasikitisha sana kuona kwamba hata wale wajiitao watumishi, kumbe hawana sifa za ‘u-wana’ wa Mungu. Neno la Mungu linasema, ili uweze kuwa na vipawa vya Roho mtakatifu na kusamehewa Dhambi ni lazima UBATIZWE! Jiulize unakemea pepo, unaombea wagonjwa na ama kufanya miujiza mikbwa vile, UMEBATIZWA? Kama unafanya hayo yote bila kubatizwa, jua kuwa wewe haujafutiwa Dhambi zako, na maandiko yanasema, aliye ndani ya dhambi ni washetani. Pengine utasema, mbona ninaupako nafukuza mapepo, naombea wagonjwa na nimebatizwa, ninashida gani tena? Nakushauri uuchunguze aina ya ubatizo wako, bila hivyo utadumu kuwa dhambini na mwisho utakataliwa na Mungu mwenyezi, jambo ambalo ni baya na ni bahati mbaya sana! Kuwa na vipawa hiyo si hoja, Neno linasema, vipawa havinamajuto, na Mungu hulichunguza Neno lake apate kulitimiza, maadamu unafanya hayo sawa sawa na Neno la Mungu na kama ipo imani kwa anayepokea, basi, muujiza utatimia, lakini wewe mwisho wa yote utakataliwa.

  Ili ufanye kazi ya Mungu kwakukubarika na uwe na uwezo wa kweli wa kukemea nguvu za shetani, uondokane na hofu za shetani na uwe mshindi pamoja na Kristo. Labda unajiuliza, “ili niweze kuyafanya haya yote nikiwa ndani ya Kristo ni lazima nifanye nini?” jibu lako liko ni hili, “Petro akawaambia, tubuni mkabatatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, mdo. 2:38”

  Unapaswa kubatizwa kwa jina la Yesu na si Kwa jina la baba na la mwana na la Roho Mtakatifu maana hayo si majina ila ni sifa za utendaji wa Mungu, ambaye ni mmoja tu – Yesu Kristo, Jina ambalo huondoa dhambi na ndilo pekee tulilopewa ili katika hilo tuokolewe.

  Muendelee kubarikiwa na Bwana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s