Mchungaji Antony Lusekelo alitabiri Uchaguzi wa Kenya!

KENYA/

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama “Mzee wa Upako” Alitabiri mnamo tarehe 31 January 2013 kwamba Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga angeshinda uchaguzi dhidi ya Uhuru Kenyatta.

Akiongea ndani ya kanisa lake, “Mzee wa Upako” alisema “Raila Odinga atashinda uchaguzi wa Kenya na Uhuru Kenyatta hatashinda labda asubiri miaka ijayo na si kwenye uchaguzi huu”

Utabiri wake unatofautiana na Nabii Thomas Manton wa Kenya aliyetoa unabii Jioni ya Jumamosi 23 February 2013 kwamba “Bwana asema: Uhuru Kenyatta ni chaguo langu kuwa Rais wa Kenya awamu ya nne”  Kusoma zaidi unabii wake fuata link hii 

Utabiri wa Mchungaji Anthony Lusekelo haukutofautiana na utabiri wa Maalim Hassan Yahaya Hussein ambaye naye tarehe 13 January 2013 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam alisema Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga angeshinda uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.

Hata hivyo, Uhuru Kenyatta ndiye aliyepata kura nyingi na kupelekea kuteuliwa kuwa Rais wa awamu ya nne nchini Kenya, vyombo mbali vya dola vimewashukuru wakenya kwa utulivu na amani katika kipindi chote cha uchaguzi.

Uteuzi wake utaleta changamoto nchini Kenya kwa Uhuru Kenyata na mwenzake William Ruto kufuatia kesi waliyonayo Mahakama ya kimataifa kutokana na machafuko yaliyotokea mwaka 2007 kupelekea vifo vya zaidi ya watu 1,200 na mamia ya wakazi kukosa makazi ya kuishi.

Advertisements

21 thoughts on “Mchungaji Antony Lusekelo alitabiri Uchaguzi wa Kenya!

 1. Wapendwa tusiwe watu wa kusimamia maneno ya kusikia, je tunaushahidi kuwa kweli Odinga alishinda au ni maneno ya kusikia tu. Tutafanya dhambi kwa ushabiki tu.
  Pili kusema mtumishi kadanganya kwani kumsema mtumishi vibaya. Biblia inatuagiza kuambia ukweli kila mmoja na mwenzake nje ya hapo tunaleta siasa makanisani.

  Watumishi wengi wameingiwa na tamaa ya kutaka kuonekana wao ni wa kiroho zaidi kuliko walivyo na hilo ndilo limekuwa jaribu linalowafanya waingize manipulation na uongo ilihali wakijuwa kuwa sio Mungu anayetenda kazi nao bali ni udanganyifu ilikujiongezea kondoo wasiotaka kujitaabisha kwa kuyachunguza maandiko. Kama tukiwa wakweli tunawajibu wa kuwaonya.

  Hiki ndicho ninachoamini Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote aliyetayari kubeba gharama kuliponya kanisa. Sasa tukiingiza hekima za kibinadamu (SIASA) tumekwisha.

 2. unabii unaotoka kwa Mungu lazima utimie,haijalishi mazingira au hila za wanadamu.chamsingi wewe kama mtumishi wa Mungu,si lazima utabiri,yawezekana wewe si NABII bali unaforce.
  pia imeandikwa ni nani asemaye neno nalo likafanyika ikiwa BWANA hakuliagiza

 3. Kwa uelewa wangu wa siasa kutoka pale udsm, siasa zote za Africa zina matatizo makubwa. Kwa uelewa wangu juu ya Mungu na jinsi anavyowapaka mafuta viongozi kwa ajili ya nchi, nashawishika asilimia zote kupingana na wale wanaoamini eti siasa za Africa Mungu anahusika. Nikupe tu mifano kadhaa; viongozi wa Mungu ni wabinafsi?, viongozi waliochaguliwa na Mungu hawasikii vilio vya wananchi na hata kumwaga damu?, viongozi waliopakwa mafuta wanatumiwa kama vibaraka? etc. Niwaombe watu wa Mungu kukumbika sisi ni nuru ya ulimwengu hebu tuangaze vyema ili mataifa yamgeukie Yesu kristo mwana wa Mungu. Tukidumu ktka ushirika na roho mtakatifu na neno la Mungu hakika unabii usiotoka kwa Mungu hautapata nafasi ya kuchelewesha juhudi zetu za kuipigania imani na kujenga mwili wa kristo. Ebrania 2 tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii? Mbarikiwe kwa michango yenu mizuri.

 4. Kwa kawaida MUNGU akisema lazima kitu hicho kitokee.Nabii atabirie jambo anathibitika kama jambo lile linatimia.kwa hiyo kama jambo halikutimia hakutumwa na BWANA.ila ni msisimuko wake tu akatamka.N ni vizuri kubaki na NENO kuliko kutegemea unabii.Sasa huoni Mzee wa upako ametoka droo na Sheikh maalim mtoto wa Yahya Hussein-aliekuwa akifundisha uchawi/majini channel TEN?mimi sasa nina hofu kubwa ya manabii/mitume wa leo kama kweli wamejiweka au wamewekwa na MUNGU.Mtu alikuwa mchawi akiibuka anakuwa mtume-si ana uwezo wa utambuzi kama alivokuwa zamani?kuna shida gani watu wanajaa ukumbi -wanaita huduma inayokuwa kwa kasi=kwenda wapi?Tusikimbie maombi shetani kwa taarifa anatafuta kuwaondoa watumishi wote halali wa MUNGU ili abaki na wa kwake.Mtwatambua kwa matunda yao.Mungu awabariki-Mr Lwembe na wengine

 5. Huduma ya Kinabii inahitaji mtu kuwa makini nayo, maana ukikosea kidogo, inakuwa imekula kwako, hata ile heshima ya kinabii au uchungaji inakuwa ya mashaka, ndiyo hapo watu wanapoanza kusema nabii wa uongo.
  Ni bora kubaki kama mtume, mwalimu au mchungaji na ukaheshimiwa kama mtumishi wa Mungu kuliko kujiita kuwa nabii au kutoa unabii usiyotimia na ukapoteza imani za watu kwako.

 6. Raila Odinga Oginga alishinda uchaguzi Kenya. Wataalam wa electronics waliuchakachua. Raila ni chaguo la Wakenya wengi. Si kweli kwamba Wakenya walimchagua mtu wa kuendelea kuwanyima ardhi na makao wao wakadumu kuwa maskwota.

 7. Bwana yesu asifiwe watu wa Mungu… Mimi binafsi naona Lusekelo anajizalilisha. achana na nabii zisizo timilika anazo zitoa lakini pia maneno anayo ongeaga kanisani kwenye kituo chake cha maombezi (coz sio kanisa) ni ya matusi some times uzalilisha Ukiristo ambayo industry aliyoitiwa kutumikia bila kujali hao anao wasema ni watumishi wenzie. One day nimemsikia akitoa maneno mazito kama Nyie wajinga, wapuuzi, waswahili n.k . achilia mbali juu ya huduma na kanuni anazotakiwa kuenenda, ila pia maadili katika jamii hayamruhusu kufanya vile. kwani kanisani hapo kwake hamna watu wanao mzidi umri? naamini wapo hata wanao weza kumzaa. Mimi binafsi nachukua mzigo wa kumuombea coz hiyo roho si ya kawaida inayo msingizia Mungu kasema kwa kivuli cha unabii na isitimilike. Kama ni neno la Mungu kaliweka kinywani mwake hata siku moja lisingepita bule, lazima ingekuwa. By ht way kwenye swala la uchinjani hakufanya fare kuongea vile tena kwa zarau na matusi kwa wenzake. Mimi nipo zanzibar siku hiyo nilikuwa na wenzetu wa imani tofauti (waislam) walikuwa wakicheka sana na kutuona hatuna umoja na hata kujithibitishia kuwa walikuwa sahihi kwa hilo. Niliona aibu sana ila Mungu alinitia nguvu.very shame

 8. Samahani, hao watumishi wa Mungu mnaodai wasinenewe mabaya ni akina nani?!!!-Urira

 9. Miaka michache iliyopita alikuja Arusha. ilikuwa ni kipindi cha mvua. akaikemea kwa mamlaka ya kinabii! akajisemea na maneno yake! mwishowe yeye ndiye aliikimbia mvua. samahani wapendwa kwangu mimi lusekelo ni opportunist!!

 10. Unabii ninaopendelea mimi ni ule ambao umetolewa kabla ya kampeni kuanza kwa kuwa unakuwa hauja athiriwa (influenced) na yanaoyendelea (the senses).

  Nilimsikia mtu anasema hata kule Marekani kuna nabii (Kim Clement) ambaye kutokana na wakristo wa Republican wenye ushawishi wa kipesa na ambao mara nyingi ni wabaguzi wa rangi alilazimika kupindisha unabii wake na kudai kuwa Romney angeshinda. Sasa Romney kashindwa sasa sijui inakuwaje?

 11. Mungu anaweza kumtumia uhuru kuijenga kenya, mipango ya Mungu ni ya ajab sana.

 12. Hivi kumnenea mabaya mtumishi inajumuisha utii kwa hisia zetu au kwa Neno la Mungu? Kauli kama “Usimnenee vibaya mtumishi wa Mungu” zinaficha upumbavu au ni ujinga wa Maandiko?

  Punguzeni siasa, Neno liko wazi nendeni mkalitafute katika Biblia zenu, nabii yeyote akisimama akasema, “Bwana asema, …” lisipotimia jambo hilo basi jueni kuwa huyo ni nabii wa Uongo na adhabu yake ni kifo! Licha ya kwamba hakuna kati yetu aliye na mikono safi ya kuitimiza adhabu hiyo, lakini, spiritually nabii huyo amekufa, na kusanyiko analoliongoza nalo ni la wafu, maana wafu hawajui lolote, Mhu 9:5 “lakini wafu hawajui neno lo lote”!

  Ndio maana utawakuta watu wametulia tu, licha ya unabii wanaopewa kutokutimia, lakini wapo tu, wengine waliwahi kuambiwa Kristo angerudi tarehe 22 Oct, 1844, wakajitayarisha lakini hayakutokea, wakapigwa fix kuwa eti hajaja kwa sababu kanisa limeshindwa kuitunza Sabato, wapo wanaoishi katika uongo huo hadi leo hii, wafu wa Agano jipya wanatembea barabarani, wanapanda daladala, wanakopa pesa, wanaimba sana kwaya, lakini ni wafu!!!

  Nabii Yeremia kwa Neno la Bwana aliwaambia Israeli watachukuliwa utumwani kwa miaka sabini. Akasimama nabii wa dhehebu akaivunja ile yoke aliyokuwa amevaa Yeremia, akasema Bwana amemwambia ni miaka miwili tu! Mungu alimuua!!!

  Lakini kabla hamjamuua kwa kauli zenu, kagueni kwanza iwapo alisema “Bwana asema” au alikuwa anabashiri tu kwa nyota, msije mkamwaga damu isiyo na hatia!

 13. Neno la Mungu linasema, mtu akijazwa Roho mtakaifu ndiye anaweza kutabiri Lk. 1:67.

  Lakini, Nabii ambaye unabii wake usipotimia, Biblia inasema adhabu yake ni nini?

  Lusekelo naye ni mtumishi wa Bwana, watu wasimnenee mabaya, yumo katika shamba la ngano. Naye kaajiriwa na Bwana, akusanyaye Ngano na kuipeleka Ghalani na Yule afungaye Mgugu Matita matita katika shamba la ngano ili yakatiwe moto, naye ni mtubishi, wote ni watumishi wa Bwana kila mmoja atalipwa ujira wake toka kwa Bwana yuleyule kwa kazi aliyoifanya. Kwakuwa wote hao ni watumishi wa Bwana, tusiwanenee mabaya, asante Tunu umesema kweli!

 14. Tunu kusema kwamba Mch. Lusekelo alitoa unabii ambao haukutimia si kuwasema vibaya watumishi wa Mungu kama unavyodhani.

  Nakubaliana na Chiwango kuwa unabii wa Mungu haukwamishwi na kitu chochote kutimia, maana si unabii ndio wenye kutimiza hicho kitu ispokuwa unabii ni taarifa ya kitu mbacho kinasemwa leo kwa ajili ya kesho kikiwa kimetimia.

  Yaani kusema kwa Lusekelo siko ambako kungemfanya Odinga awe rais, lakini kusema kwake kulitakiwa kuwe ni taarifa kutoka kwa Mungu mwenye kuyanena yajayo kana kwamba yamekwisha kuwako, kwamba mambo yote yatafanyika lakini mwisho wa yote Odinga ndo atakuwa rais.
  Lakini kama alitoa taarifa ambayo alisema imetoka kwa Mungu halafu matokeo yakawa tofauti na hiyo taarifa, basi taarifa hiyo haikutoka kwa Mungu.

  Kwa maana hiyo kuiba kura, kufanya uhuni, na mambo yote hakukutakiwa kuzuia Odinga kuwa rais kama kweli ni Mungu alikuwa ametoa taarifa kwetu kupitia kwa Mch. Lusekelo kuwa Odinga ndo atakuwa rais

  Lakini mchakato wa uchaguzi haujamalizika, pengine Odinga anaweza kuibuka mshindi (suala liko mahakamani)

  Tuendelee kungojea!

 15. Sawa nimekuelewa Tunu kwa upande wa kuwaombea Kenya machafuko yasitokea

 16. Msiseme vibaya watumishi wa Mungu, Odinga angekua rais wa wakenya ila watu wamefanya uhuni kuiba kura. @George kwani hujawahi kuona manabii wa uongo?. Tuwaombee Kenya machafuko yasirudi tena

 17. Mtu anayetoa maoni yake aseme haya ni maoni yangu, au mtu anayetoa ubashiri wake aseme huu ni ubashiri wangu. Unabii wa MUNGU hauwezi kudanganya hata siku moja. ukiesema rais wa kenya atakuwa huyu basi ni huyo huyo bila kujali amechaguliwa na wakenya au wakikuyu.

 18. Hayo ya mzee wa upako sishangai. Natafakari tu kama haku kopi na kupaste utabiri wa Hassan Yahya!

 19. Wapendwa,

  Swala la kutabiri nani atakuwa nani katika uchaguzi wa viongozi wa nchi ni swala ambalo limekuwa likisumbua vichwa vya wengi.

  Mwaka 2000 wakati wa Uchaguzi Mkuu Tanzania, Askofu Kakobe alitoa unabii wake kuwa Mh. A.L. Mrema angeibuka kidedea kwenye uchaguzi wa Rais wa mwaka huo. Kilichotokea wote tunakikumbuka. Aidha, Mchungaji Mtikila alitabiri kwamba Prof. I. Lipumba angeshinda uchaguzi huo wa mwaka 2000. Naye unabii wake uliishia hewani na Lipumba hakushinda. Shekhe Yahya (marehemu kwa sasa) naye akaibuka mwaka huo na kutabiri kwamba Mzee Ben Mkapa angeshinda uchaguzi huo wa Urais mwaka 2000.

  Baada ya Ben Mkapa kushinda uraisi watu wakajiuliza, hivi hawa manabii wa Kikristo hutoa unabii fake na uongo au wanatafuta umaarufu?

  Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania tena mwaka 2005 watu wote walikaa kimya isipokuwa shirika la Utafiti la Synovate liloibuka na utabiri wa kiutafiti kwamba Mzee JK angeshinda uchaguzi huo. Uchaguzi ulipokwisha Maaskofu wote wakasema JK ni chaguo la Mungu.

  Ilipofikaa mwaka 2010 Maaskofu wote walikaa kimya. Hakuna aliyeibuka kutabiri labda kama mimi sikumsikia. Shirika la Synovate kama kawaida yake likaibuka na utabiri wa kiutafiti kuwa JK angeshinda uchaguzi. Kisha baada ya Muda kukajitokeza taasisi nyingine (siikumbuki jina) iliyoibuka na matokeo ya utafiti wake kwamba Mzee wa Karatu Dr. W. Slaa angeshinda uchaguzi huo mkuu wa Urais na baadhi ya maaskofu walikuwa wakimuunga mkono Dr. Slaa ama kwa uwazi au kwa nyuma ya pazia hadi taarifa zikamfikia Dr. Jakaya Kikwete na CCM yake wakaanza kutafuta mbinu za kuwarudisha maaskofu waiunge mkono CCM.

  Baada ya uchaguzi wa 2010 hadi sasa sijasikia watu hasa Maaskofu wala Mashekhe wakitoa tamko kwamba Dr. Jakaya Kikwete ni chaguo la Mungu. Sijui wamepotelea wapi manabii wetu.

  Juzi juzi kuna mtumishi aliibuka na kusema kwamba Mungu amemwambia kuwa Rais ajaye wa tano Tanzania atakuwa Mzee Edward Ngoyayi Lowasa. Watu wamemuunga mkono na wapo walioshindwa hadi leo kuunga mkono unabii huo. Hata mimi sijaukubali mpaka pale utakapotimia.

  Mzee wa Upako (Anthony Lusekelo) naye amejitia aibu ya mwaka kwa kutaka umaarufu ambao huwezi kupatikana kwa kutoa unabii rahisi rahisi tu. Tatizo la Manabii wa uongo wanapotabiri vitu vikashindikana kutokea wanaanza kujitetea kwamba aaah oooooh unajuaaaa bwanaaa, haijatokea kwa sababu kura ziliibwa, walichakachua, mara hayo matokeo yamepikwa, na visingizio kibao. Huu ndio udhaifu wa manabii wanaojiita mabii wakati siyo manabii bali wainjilisti tu.

  Mzee Anthony Lusekelo nimekuwa nikifuatilia mahubiri yake kupitia TV, yapo mambo ambayo anapoyasema anaweza kuwa yuko sahihi lakini siyo siku zote kila anachokisema au kukitabiri lazima kiwe sahihi.

 20. Ni kweli Odinga ni chaguo la wakenya na Uhuru ni chaguo la wakikuyu. Mchungaji yu sahihi.

 21. huu ulikuwa ni unabii wa kutafuta umaarufu kama kawaida yake! kama mtumishi wa Mungu ambaye unaonyeshwa mambo yajayo mbona hakuonyeshwa mambo yaliyotokea ktk nchi yetu kuhusu habari ya uchinjaji ambazo zilisababisha maafa? kwa nini hakuonyeshwa maafa yaliyotokea z,bar kabla ili awaonye watu juu ya hayo? matokeo yake mzee wa upako anajitokeza kwenye tv wakati maafa yameshatokea na kuanza kusema viongozi wenzake wa dini eti wanajipendekeza,wanataka kupiga picha na waziri mkuu. kwa mtumishi kama yeye hakupaswa kuongea maneno kama yale ya kuwasema wenzake tena mbele ya wasioamini! aliongea maneno mengine ambayo hayakunipa shida ila yalikuwa yamepitwa na wakati na kama angeyaongea kwa wakati kiukweli yangesaidia madhara yaliyotokea ktk habari ya kuchinja.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s