“MINYOOO’” INANIGA/KABA KANISA NA UTUMISHI WAKE MBELE ZA MUNGU

tafakari

Daktari mmoja alinipa abc ya baadhi ya parasites mfano minyoo wanavyofanya vitu vyao, waingiapo kwa mwanadamu. Mwanadamu ana mfuko wa chakula,utumbo mpana na mwembamba. Unapopakia vyakula vitamu na bora sana Mungu alivyotupa duniani hapa tuburudike navyo mfano mahindi choma, mihogo, samaki aina ya sato, mumi, kamongo, na wanyama kama sungura,nguruwe,pia matunda, mayai, chips,wali,ugali,ndizi nk, vyote ivyo huenda mdomoni na kushambuliwa na meno(tayari usagaji wa chakula umeanza hapo)kisha husukumizwa kwenda tumboni-stomach-hapo kemikali-acid kuachiliwa kutapakaa/kushughulikia icho chakula ulichojibariki nacho na acid iyo hugeuza menyu iyo ndani kua vibonge-vibonge( yaani umeng’enyuaji wa  meal ndio unaendelea ivyo. Kisha chakula huenda kwa utumbo mwembamba humo enzymes za kusaga chakula tikitiki huachiliwa, ndiposa unashangaa ulitumbukiza ‘’pieces of sweet blessed pork meat’’, yet unapokwenda ‘’main office’’ hutoi pieces kama zilivyo, ni vitu vingine kabisaa, kweli shughuli ni pevu iliyofanywa na vimeng’enyuaji ivyo, lo! asante Mungu…yaani unaingiza muhindi choma kwa tumbo lakini kule mahala, hautoi mhindi kama ulivyo, hii nayo ni muujiza! si tu muujiza uwe kupata visa to USA, gari, mchumba,mtu kukupa pesa nk maana ni ajabu tumboni na utumboni mwembemba, hakuna mashine zilizojengwa humo kwa chuma wala generator ya umeme yet vitu vinasagwa tikitiki! Alleluyah! Usagaji wa mwanzo mdomoni, then ktk tumbo na huu wa nguvu sana ktk utumbo mwembamba unamalizika, kunatokea virutubisho vya mwisho tayari kuchukuliwa na damu zilizo nyingi sana ndani ya vijamaa vinaitwa ‘’Villi’’-kama tuvidole tufupi vilivyo katika surface ya utumbo huo huo mwembamba-ndivyo vinavyofyonza kusambaza nutrients izo kwa mwili ili huweze kukimbia, kulala, kusoma, kuendesha, kutembea, kuandika, kuona,kulima,kuhubiri, kuimba nk.

Sasa Minyoo hao nilioambiwa ushuuda wao, maana nimeambiwa wako wa aina nyingi, sijui nani aliwapa akili ya ajabu kweli na sijui walijifunza wapi tabia hii! wenyewe hawakai mdomoni na katikati ya meno kwenye shughuli kali ya kupasua-pasua miamba,wala hawakai kwa mfuko wa chakula ambako kuna shughuli pevu ya ndugu acid na wala mwanzoni kwa utumbo mwembamba kuliko na shughuli pevu zaidi ya rafiki enzymes, wala hawakai mwisho wa utumbo mpana kwakua wanajua wataishia kwa toilet tena haraka BALI wanakaa maeneo ya ufyonzaji na ndugu mpolee anaitwae villi, wakidaka/kula vile vitamu vya mwisho vilivyoshughulikiwa na ndugu meno,mdomo,ulimi,mate, mfuko wa chakula, acid, enzyme kabla ya kupelekwa kwa ubongo mpaka dole gumba na kucha yake.

Kanisani/usharikani/fellowship wako watu wa aina iyo, hawahusiki kwa lolote, iwe kuwahi kabla kuombea ibada,kuimba kwaya,praise and worship, kutoa sadaka,vitu, kwenda kushuudia mtaani, hospitalini, kufagia kanisa,kuosha vyoo vya kanisa,kuhudumia wageni,kudaka wanaookoka uwanjani ktk crusade, kuja ktk mkesha na maombi,kufunga na kuomba,kusoma Biblia,kutia moyo,hata kuimba na kufurahi na wenzake, hawana mpango, hawashiriki usagaji kwa namna yoyote, yaani yeye ni kuja kusikiliza-kufyonza na kuondoka kulala, tena kuja kufyonza na kuondoka. Umeng’enyuaji ukitangazwa kanisani eg uchangiaji wa harusi ya mpendwa hasiyejiweza, mkutano wa injili,kujenga jengo jipya la kanisa,kukesha na kuomba, kuacha chips na ice cream ili kufunga na kuomba kuombea nchi,kanisa na mchungaji wako, hayupo ila vinavyopatikana baada ya wenzake kushiriki usagaji wa chakula kama seminar-mgeni aliyeletwa kwa changizo kubwa,jengo jipya kuisha na kuzindulilwa, Mchungaji kuhubiri ujumbe moto moto wa mbinguni, hapo ‘’mnyoo wapendwa’’ utawakuta sharp wakiramba tu baraka na kucheeeeeekaaa kwa raha ya rohoni..shindwa kabisa! Jamani, mnatukaba bwanaa kanisani na utumishi mwema wa mchungaji wako,  hamna huruma ndugu? Kha!

Katika 1Wakorinto.12:14-26, Viungo ni mbalimbali ktk mwili mmoja, kila kiungo kiwe kikubwa,kidogo,kinaheshimika au la, vyote vinahitajiana na kila kimoja chapaswa kufanya kazi kwa faida ya mwili wote.Kimoja kikijidai hakihitaji kingine chenzake au kikaa tu bila kufanya kazi yake mahususi ambayo ni chenyewe tu kiliumbwa/pewa/chaguliwa kufanya iyo kazi, au kikajidhania chenyewe tu kwa ujinga wake au kujikataa tu kua hakifai kuwepo ktk mwili, basi kitakua kinatesa sana viuongo vingine, kinakwamisha maono,ndoto na mtembeo wa viungo vingine na kwakweli kikiendelea ivyo, bora kufanya operation na kuking’oa-BABA YANGU NI MKULIMA,KILA TAWI LISILOZAA, HULIONDOSHA ILA LINALOZAA,LINASAFISHWA ILI LIZAE SANA-Yoh.15:1-2. 

Wapendwa, plz tusitesane makanisani bwanaa, tusiwahumize wachungaji jamani, kila mtu achakarike/asage chakula, we huwezi kaa tu pale kwa ‘’villi’’ na upako wako wa ‘’ki-parasites’’-kufyonza vitamu vya mwisho, we vipi! wenzako wakesha, wafunge, waombe na mambo yatiki kanisani, nchini, Mungu aje lively,wewe unakula tu bila kushiriki, STOP IT. ALL ‘’MINYOO INAYO-SUFFOCATE WATU NA MAONO YA KANISA NA MTUMISHI WA MAHALI HUSIKA, SHALL BE TAKEN AWAY.

—Edwin Seleli
Advertisements

3 thoughts on ““MINYOOO’” INANIGA/KABA KANISA NA UTUMISHI WAKE MBELE ZA MUNGU

 1. Lenda
  Kwa haraka-haraka mtu akisoma uliyoandika, anaweza dhani ni kweli tupu lakini tukitafakari kwa kina cha Neno la Mungu, yako baadhi -sio yote, kati ya uliyo share hakuna nguvu ya kweli ya NENO bali ni mtazomo tu wa kibinadamu ambao unaweza kua kweli kwa macho ya mtu lakini yakawa si hoja ya msingi kwa mtu mwingine, kwa nini? kwa sababu ni mtazamo tu. Labda nipitie macheche ya uliyosema na kukuuliza baadhi ya maswali uweze PATA PICHA YA KWA NINI NASEMA, POINTS ZAKO NYINGINE NI CONCEPTS TU SI NENO LA MUNGU!

  Umesema zile tabia 22 ni watu wa makanisa ya siku za mwisho….una uhakika tabia izo hazijawahi kuwako kuanzia kanisa la kwanza mpaka sasa? mpaka umenukuu baadhi ya maandiko yanayoonyesha watumishi walisemaje, maana yake mambo hayo tulionayo leo, yalikuwepo ndio maana yakasemwa ktk maandiko mbalimbali, sasa huo u-mwisho wa tabia za maknisa ya leo unatoka wapi, mwisho upi ni mwisho na tabia zipi ni special ambazo hazijawahi kuwako kanisa la kwanza?

  Pia umetia moyo wavivu kanisanai na ktk huduma ukisema sisi kama wanadamu si kazi yetu kuwakataliwa mbali watu! umeshindwa kuelewa ni Mungu ktk Yohana.15:1-2 kasema kila tawi lisilo zaaa huondolewa na lizaalo, husafishwa lizae sana, nani alikuambia Mungu yuko na hamu ya wavivi, wasio tenda jambo, watu wenye talanta na wanazizika chini, wanakaa tu? wewe hu nani kwenda akinyume na Mungu aliyesema hasiye zaa anaondolewa, aaminiwe nani, NENO AU HISIA./HURMA ZAKO? je umesahau yule mtumwa alipewa talanta na hakufanya kazi, alipokuja Bwana wake, aliadhibiwa na kutupwa nje? je si Mungu aliyesema na aalaaniwe afanyaye kazi yake kwa ulegevu? nadhani ni hatari kuchanganya NENO na hisia zetu za kibinadamu, Luka 13:9 ni Mungu anasema pia kua watakatwa! KWA IYO MTU AKISEMA WATAKATWA UA WAONDOSHWE KAMA LINANENOVYO NENO, HASEMI KWA MAMLAKA YAKE BALI KAMA NENO.

  Na je unapohimiza kuwaombea wavivu, wasio fanya kitu kanisani, hawasimami na mchungaji wao ili iweje? nani kakuambia kwa maombi ya aina iyo mbingu itasikia? huoni kua unapoteza muda na kufunga bure wavivu walioamua kua mavivu kabisa kwa maana watu hao hao ukiwa kuta katika mambo yao ya maisha na shekeli, wana nguvu a ajabu ya kufanya kazi na kusaka shekeli, watu hawa ndio unasema tumenyeke tuwaombea? utakua huna ya kuombea inawekezkana.

  Umesema kua makanisa yaliyo na tabu ya wakristo ”minyoo” hayafundishi watu kujua talanta zao! nionyeshe kanisa lolote ambalo unadhani linafundisha na kuzingatia yote uliyosema na mimi hapo hapo kama sitakuthibiitishia ”wapendwa minyonyo wapo hapo hapo? je unajua kanisa lolote ambalo hakuna ”minyoo’ kabisa kwa kua wanafundisha sana watu wao kujitambua na talanta walizo nazo?

  Na je mtu ukishaookoka , unatakiwa seminar ya nini kumwambia/ kumshuudia mtu kuhusu mabadiliko dhahiri Yesu aliyoyafanya ? je umesahamu kipofu ambaye aliweza kuwaambia watu wabishi wale kirahisi kabisa kuhusu uponyaji wa Bwana?Yohana.9:1-34 hunahitaji seminar kumwambia mtu habari ya YESU ALIVYOBADILISHA MAISHA YAKO KWELI? SI NDIO UVIVU NA U-MINYOO HUO? AMBAO UMEUTETEA?

  Umesema pia…”Kujionyesha kwa matoleo makubwa na minada yenye kuleta heshima kwa matajiri na kupuuza kidogo cha maskini ni sehemu ya mtindo wa kanisa”’ Nani alisema kua maskini atoe kidogo nani? je hujui kua hata kama ni maskini bado ktk umaskini wake ,utoaji wake mbele za MUNGU UKAWA WA OVYO?

  Umesema…”’Hukosa kuombea karama na vipawa (2 Timotheo 1:6)”” ilo andiko halisemi tuombee bali tuchochee..si maombi, kufanya maombi uko ndiko kulea uvivu, na si tija kwa kanisa na ufalme wa Mungu

  Pia umesema“MTU AKIHUDUMU, NA AHUDUMU KWA NGUVU ANAZOJALIWA NA MUNGU” 1 Petro 4:11, 1 Kor.4:10-13, maandiko hayo yanahusika na mkristo mtu wa kazi na si mvivu, huwezi mwambia mpendwa minyoo kua..na ahuduma kwa kwa nguvu alizojaliwa..ahudumu vipi wakati haudumu kabisaaaa, ni mvivu tu wala hayupo kazini? na Paul naposema hapo tu dhaifu, haimaniishi hata chemmbe kua ni mvivu, yatupasa kusoma Biblia vema kwa mantiki nzima ya mahali husika siyo kuchuka tu andiko na kulibandika

  Lakini pia ktk tabia za wakristo wa makanisa ya siku za mwisho kama ulivyosema, kati ya izo, ni tabia za mvivu..kwa iyo tabia izo pia unazifahamu na bado tena umetetea tuwaombeaye tu, wapi na wapi ndugu?

  NADHANI NI VEMA KABLA YA KUINGIZA HISIA/MITAZAMO NA UZOEFU, MAMBO AMBAYO NI VITU VYEMA, NI BORA KUANZA NENO, ANGALIA UVIVU UNAVYOMKERA PAUL MPAKA ANAAMUA KUMWACHA MARK ALIYE WAACHA WENZIWE NA KURUDI KUPUMZIKA KUACHA KAZI NA KURUDU NYUMBANI…MVIVU SI WA KUOMBEA HATA KIDOGO labda kama una muda wa kuchezea.Mdo.15:36-40

 2. Duh!mtumishi hapa umegusa ukweli mtupu!kwani kuna baadhi ya matendo hata Mimi nahusika,nitaacha Mara moja!

 3. Napenda kuwatia moyo wote wanaokohudumu katika kweli ya Injili na wahudumu bila kuchukia wala kutenga wasiohudumu, tumia talanta yako kila moja atadaiwa iwapo wanawali wangetaka kuwapunguzia mafuta wale waiolala ingekuwa shida kwao wasiohudumu hawatengwi ila wanaombewa na kufundishwa kuvumbua na kutumia talanta na aliye na talanta aitumie kwa nguvu zote “MTU AKIHUDUMU, NA AHUDUMU KWA NGUVU ANAZOJALIWA NA MUNGU” 1 Petro 4:11, 1 Kor.4:10-13. Na si kazi ya mwanadamu kuwakatilia mbali bali ni BWANA soma Luka 13:9
  TATIZO HILI LIPO KATIKA MAKANISA MBALIMBALI HASA YALE AMBAYO
  1. Hukosa kuombea karama na vipawa (2 Timotheo 1:6)
  2. Kiwango gani roho anagusa waumini kujitoa kwa ajili ya Yesu.
  3. Hayana madarasa ya malezi kwa watoto na vijana na masomo ya malezi . makundi wanandoa ,wazee na wajibu wa kila kundi kwa kanisa ( 1 Timotheo 5:5,4:12,5:17)
  4. Umilikishwaji binafsi wa kanisa kama vile mwanzilishi kujionesha mmiliki badala ya kuilweka kanisa chini ya Yesu. (1Timotheo 3:2) (Tito1:7)
  5. Makanisa yanayopokea waumini kiwango kikubwa bila kuwatambulisha na kujua wanamjuaje Kristo na wanashirikije na kutotembelea waumini (Matendo20:20)
  6. Yana Waumini wasio na makazi maalum wanaohamahama na hayatunzi kumbukumbu za wageni na kukarimu wageni Waraka wa tatu wa Yohana 1:5-8.
  7. Yana Waumini wanaodai hawana dini ila watahudhuria popote injili inapohubiriwa
  8. Yana Waumini wengi wanaojifunza na kutaka kujua undani kwanza wa kanisa kama lina sifa ya ushuhuda kwa Kristu kabla ya kuhudumu. (Matendo 17:11)
  9. Kuwapo kwa makundi katika kanisa yanayokwezwa na kuonekana juu zaidi kwa mali.n.k hivyo wengine huwa wanyonge na kujiona si sehemu ya kanisa. (Yakobo 2:2)
  10. Waumini kujiona mioyo yao ni michafu sana na kutojiona wanafaa kwa huduma yeyote wanapojiona bado wanatumikia dhambi zilizowatesa siku zote.
  11. Yanayoombea zaidi mibaraka ya pesa,uponyaji magonjwa na kutojali mafundisho ya utume na taarifa za kazi za waumini
  TABIA ZA WATU NA MAKANISA YA SIKU ZA MWISHO
  1. Kupenda vitu vya msisimko wa kimwili katika Ibada.
  2. Kupenda vitu vipya,bila vitu vipya waumini hupotewa na mvuto wa kuabudu.
  3. Kama huduma ya kanisa haina kitu cha kusisimua haina mvuto
  4. Maonyo ya Mungu kuhusu ujio wake mara ya pili na hukumu hayavuti hisia. (Ufunuo 1:3)
  5. Huduma zaidi ni juu ya miujiza na kubarikiwa kipato.
  6. Ngoma,dansi na makelele na usengenyaji.
  7. Mitindo ya mavazi, ulimbwende na kujipenda nafsi,miili.
  8. Mibaraka ya kimwili,mali ndio huvuta hisia.
  9. Upuuzi wa kiroho (kudharau wengine)
  10. Waumini hawako tayari kuzikana nafsi zao na kujitwika msalaba.
  11. Hukili kuwa “nimeokoka” lakini moyoni hubaki na maswali “nifanyeje ili niokoke”?
  12. Waumini wake hawafanywi wapya katika mioyo na kubadili matendo ya kale.
  13. Makanisa hujaa watu wanaopenda Jina la Mungu huku wakikana kanuni zake.
  14. Hawako tayari kuikana dunia na mambo yake bali huikumbatia.
  15. Sherehe,tafrija,hafra huchukua sehemu kubwa.
  16. Sifa kwa mtoa huduma huwa juu ya Sifa ya Mungu,kusifia mwimbaji,mhubiri.
  17. Wapenda starehe na wenye majina makubwa huwa na nafasi kubwa katika makanisa huku hawana mahusiano thabiti na Yesu msulubiwa.
  18. Kujionyesha kwa matoleo makubwa na minada yenye kuleta heshima kwa matajiri na kupuuza kidogo cha maskini ni sehemu ya mtindo wa kanisa.
  19. Mahusiano ya wenye mali na wasio na mali huwatofautisha mbele ya Kanisa.
  20. Kuwapa heshima wenye mali ndani ya kanisa. (Yuda1:16)
  21. Kumiliki ardhi, magari,nyumba ni vipimo vyao vya kukubalika na Mungu huku mambo ya kimbingu yakikanwa.
  22. Majigambo,na Kujisifu ya karama uponyaji,na mitindo ya pekee ya utoaji huduma na vionjo ndio heshima kwa wahudumu.
  SIFA HIZO KWA PAMOJA NDIZO ZINAZOFANYA WAUMINI WASIJIEA KATIKA KAZI YA BWANA.
  Wapendwa zingatieni Upendo bila kubagua waumini kwa kipato,ukaribu,undugu, Ombeeni vipawa, kushirikisha hata pale tunapoona pana maslahi binafsi. (1 Wakorintho 13:1-8) (Yuda 1:16).Basi tuonyeshe mvuto wa Kristo na kushirikisha kazi na kuwafanya waumini wajisikie kufanya kazi ya Kristo kwa nguvu zote soma Isaya 40:31. Na vijana wafundishwe Biblia si namna gani watacheza muziki wa Injili tu na Kutoa CD huku Biblia ikiwa ni kama handbag ya akinamama mkonononi Watashuhudiaje? “Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio Roho ya Unabii” Ufunuo 19:10, Isaya 8:20

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s