Waislamu na Wakristo wapatana Geita

Picha na Global Publishers

Shehe Ismail Ibrahim na Mchungaji Isaya Ikiri

Baadhi ya viongozi wa Dini kutoka Geita walikaa pamoja na kuondoa tofauti. Kati ya makubaliano waliyofikia ni nyama yoyote inayochinjwa kwa ajili ya biashara wachinje waislamu lakini kwenye sherehe zinazowahusu waislam wachinje waislamu na sherehe zinazowahusu wakristo wachinje wakristo wenyewe. Hivyo sherehe zozote za kidini wasiingilizne kwenye taratibu za Dini mwingine.

Mhamasishaji alikuwa ni Erick Shigongo pamoja na Mhariri wa gazeti la Championi, wakristo na waislamu walikumbatiana kuonesha wamemaliza tofauti zao. Baada ya hapo, kwa pamoja wakaungana na kwenda kwenye mechi ya fainali kati ya Buseresere na Katoro, ambapo Katoro walitwaa kombe.

Kabla ya kukabidhi kombe, masheikh na wachungaji walizungumza na kusisitiza sana suala la amani pia wakazungumzia mapatano yao baada ya kikao na mashabiki waliokuwa uwanjani hapo wakashangilia.

Mmoja wa viongozi wa serikali aliyehudhuria ni mbunge, Gaudencia Bukwimba CCM

———————–

Ikumbukwe hivi karibuni kulikuwa na machafuko huko Geita na kusababisha kifo cha mchungaji wa PAGT Mathayo Kachira. Waziri Stephen Wasira na Waziri mkuu Mizengo Pinda walijaribu kusuluhisha bila ya mafanikio

Hali hii ilipelekea Mbunge wa Chadema Godbless Lema kutoa tamko lifuatalo “Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani

Picha na Global Publishers

Advertisements

25 thoughts on “Waislamu na Wakristo wapatana Geita

 1. De una bahati kwamba umejirekebisha sana kwemye huu mchango wako wa mwisho. Nilikuwa nataka nilikulipue vibaya sana kwa kuamdika maneno mengi ambayo msingi wowote ndani yake.

  Nawataka hata wale waliokupongeza wajirudi baada ya kusoma alichokisema ndg. Mathew kama wewe ambavyo umejirudi.
  Michango yako huko juu ilikuwa imejaa pumba na ushabiki, na waliokushangilia wakazidi kukuharibu kabisa na ukawa unaandika mikeka ambayo haina mantiki yoyote ya maana kwa mujibu wa hoja hii.

  Ni vema kila mtu ajifunze madhara ya kuchangia mawazo bila kufahamu chanzo cha suala linalojadiliwa
  Pia kwako Seleli hata na Deo na watu wengine, ni kwa sababu tu labda hamjui, lakini mnaonesha utoto wa hali ya juu kuchanganya Kiswahili na Kiingereza pasipo sababu za msingi, hiyo ilishapitwa na wakati.

  Kama kweli kuna mkristo anayetaka kuelewa nini cha kuchangia katika hoja hii, basi asome kwa makini sana kitu ambacho Mathayo ameandika. Maana huo ndio ukweli wenyewe. Kama mnadhani kuwa waislamu wana ajenda tu nyepesi ya kuchinja basi endeleeni kufanya huu utani wa kishabiki.
  Lakini mkae mkikumbuka kuwa siku mambo ambayo maandalizi yake ni hayo mnayofanyia utani na ushabiki leo yatakapojidhirisha na kushika hatamu na kuwatesa watoto wetu kesho, basi muwe tayari kuyapokea machozi yao kwa mateso watakayopata.

  Waislamu wako kwenye mkakati wa dhai dhidi ya ukristo, halafu ninyi mnasema tukae nao vizuri tuwahubiri injili. Sasa hivi mmewahubiri wangapi na kuwafanya wampokee kristo, kama sio ujuaji tu wa kuongea ili kuonesha kuwa mnajua na kumbe hamjui.

  Jifunzeni kujua yaliyo nyuma ya pazia, ili mpate cha kuongea kuliko kuongea tu wapendwa. Kanisa liko hatarini halafu wapendwa mnaleta mzaha! Maaskofu si wajinga kuungana na kutoa msimamo kwa serikali, na kutangaza maombi ya kufunga.

  Tufungukeni sasa tuyaone mambo katika uhalisia wake ili
  tusimame kwa ajili ya kristo.

  NB: Asante sana ndg Mathayo kwa kuuweka msingi wa tatizo wazi.

  Mbarikiwe.

 2. sidhani limefikia muafaka,hili suala kwa wakristo ni dhambi kushiriki ibada ya sanamu “kwani kwa waislam ni ibada kuchinja” kwaiyo ninaona bado kwa wakristo halijakaa sawa labda kama tumeamua kutofata muongozo wa Biblia na kushikiria mapokeo ya imani zingine “ber-zebuli”

  kuchinja nyama na wakristo wachinje wenyewe whether za biashara au za sherehe.

  basi na mahakama ya kadhi iingizwe katika katiba ya Tanzania kwani ni ibada ya waislamu kukamilisha nguzo 5 za ibada.

 3. Mathew,

  Kwanza nianze kwa kushukuru sana kwa jinsi ambavyo sasa umeliweka wazi tatizo na chanzo, yaani chimbuko huu mgogoro wote tunaoujadili.

  Kwa hiyo hii inatuonyesha kabisa kuwa lipo jambo kubwa la kujadili zaidi ya kuegemea pekee kwenye uhalali au uharamu wa nani achinje na nani asichinje. Hii ndiyo sababu ilinifanya nirudie mara kwa mara katika michango yangu, kwamba suala la kuchinja limeanzia Mwanza ikiwa zaidi ni reaction ya wapendwa wenzetu kupinga, mimi nilidhani ni mafundisho, kumbe si tu mafundisho bali manyanyaso ya Waislamu kutaka kuingilia hata uhuru na haki ya kuchinja wanyama wao binafsi.

  Kwa kweli nashukuru sana. Nilifanya juhudi ya kuelewa chanzo halisi lakini sikupata mtu aliyeweza kunifahamisha kwa undani kuhusu chanzo kama wewe ulivyofanya kwetu wana SG.

  Kwa nini Mwanza? Nadhani ni kwa sababu radical muslims, ambao kiongozi wao katika mahubiri niliyoyaona kwenye Youtube anasema wazi na kuhamasisha waumini wake kuwaua na kuwadhuru Maaskofu na Mapadre, tena akimsapoti Sheikh mmoja wa Mombasa aliyeauwa, ambaye hakuwa anasita kuwaita waziwazi wapiganaji wa Somalia kuwa ni ndugu zao, ndipo yeye pamoja na timu yake walipoweka kambi.

  Hebu tazama hii video kwenye Youtube, ndipo utajua kuna tatizo kubwa zaidi ya hilo la kuchinja wanyama.

  Kwa hivyo hili ndilo tatizo. Yaani suala la kuchinja ni sehemu tu ya picha kubwa zaidi ya kupenyeza radical faith ile ambayo hata mataifa ya kiislamu yenyewe yanapigana nayo. Wanaleta kila aina ya mambo ambayo yatafanya watu wa dini hizi mbili wapigane, ili watumie nafasi hiyo kuwa-radicalize waumini wao ambao wengi wao hapa Tanzania ni watu wa imani ya kawaida.

  Mimi naunga mkono kwamba kuweko na very strong dialogue kati ya viongozi wetu, Maaskofu, Serikali pamoja na Waislamu. Hii si tu kwa ajili ya suala moja la haki ya kuchinja, bali na mambo mengine. Kwa mfano, kwa nini Serikali inakaa kimya wakati watu wanatoa mafundisho ya kuhamasisha fujo na mauaji na wanaweka kwenye CD, hadi wanapost kwenye Youtube?

  Tatizo la Waislamu wenye msimamo mkali linaziumiza zaidi nchi za kiislamu kuliko nyingine zozote. Hapa Tanzania sehemu kubwa ya Waislamu ni wenye msimamo wa kawaida, ambao huko Somalia ndiyo wanaopigwa na kuuwawa kwa msimamo wao wa kati. Kipo kikundi ndicho kinafanya juhudi kubwa kuwa-radicalize ili wengi wawe na huo msimamo mkali, ambapo kwa Zanzibar wamefika hatua ya juu sana na ndiyo matokeo ya hayo tuliyoyasikia ya Padre kuuwawa.

  Hawa wamefanya Mwanza kuwa makao yao makuu, na ndiyo hasa mafundisho yao yamepenya sana kwa sababu wameachiwa kwa muda mrefu kuifanya kazi yao hii. Gazeti la Mtanzania liliandika habari na makala katika matoleo ya wiki tatu mfululizo kuhusu chuo kinachohisiwa kuwa kinafundisha ugaidi uko Ukerewe. Watu wa Ukerewe wanaona, viongozi wa Mwanza wanajua, lakini wanaogopa hata kuongelea juu yake. Tunajuaje kuwa pengine hata pengine Mhariri wa Mtanzania ndugu Kibanda kakutwa na yaliyomkuta kwa sababu ya ujasiri wake wa kaundika kuhusu habari hii?

  Kwa hivi kwa maoni yangu tunapaswa kushughulikia a much bigger problem, tusiishie kushughulikia vita ya kuchinja pekee bali tuupanue mjadala tunapokuwa tunatafuta kwa dhati suluhisho la tatizo hili. Kuna kitu kinaitwa mfumo Kristo. Kwamba wengi hawafiki vyuo vikuu kwa sababu ya mfumo huu, hawawi viongozi wa mashirika kwa sababu hii na mengi mengi mengi. Nilitamani Maaskofu waing’ang’anie Serikali kujibu hizi tuhuma ili watoto wao wasipandiwe chuki na uadui.

  Hili suala la mafundisho ya kwamba kuchinja ni ibada kwa waislamu pia limetokea kwa hawa hawa jamaa. Sasa sisi wakati tunatafuta suluhu kwamba watu wetu na sisi pia waruhusiwe kuchinja na kuajiriwa kama wachinjaji, kwa sababu jambo litachukua muda kidogo mpaka likae sawa na kufanikiwa, inatupasa kuwaondolea hukumu za dhamiri watu wetu wasijione wana hatia au wana dhambi wakiendelea kununua nyama mabuchani.

  Hapa ndipo nasisitiza tena, hawana ibada katika kuchinja ng’ombe au mnyama yeyote wa biashara. Ibada (sacrifice) inayoambatana na kuchinja au hata kutoa vitu inahitaji mnyama anayetolewa awe mali ya anayemtoa.

  1 Mambo ya Nyakati 21: 23-24
  Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng’ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa. Mfalme Daudi akamwambia Arauna, La, sivyo, lakini kweli nitazinunua kwa thamani yake kamili; kwani sitamtwalia Bwana kilicho chako, wala kutoa sadaka ya kuteketezwa isiyo na gharama. Basi Daudi akampimia Arauna thamani ya mahali pale shekeli mia sita za dhahabu kwa uzani

  Ili unachotoa kiwe sadaka ni lazima moyo wako uambatane nacho, na mahali hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wa mtu ulipo.

  Mathayo 6:21
  kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

  Kwa hivyo ushindi wetu wa kwanza kwenye vita hii uwe ni sisi kujivua hatia za dhamiri ili tusijione eti tunashiriki ibada zao, hapana. Itakuwa ni kuishusha sana kazi kubwa ya Bwana Yesu aliyoifanya kutupatia neno na mafundisho yake tangu Agano la Kale hadi Agano Jipya, ikiwa tutaongozwa na mafundisho yao.

  Tusiongozwe na “wao wanasema ni ibada”, yaani wao wamegeuka kuwa ndiyo walimu wetu? Wakati tunaendelea kujadiliana na ku ‘press-on’ ili na sisi Serikali itangaze haki ya Wakristo kuchinja, sisi dhamiri zetu ziko huru kwamba hata wakichinja, kwa mujibu wa Biblia hawana ibada yoyote, angalau kwa tafsiri ya maandiko haya.

  Kuna siku mfalme Sulemani alimtolea BWANA ng’ombe 22,000 na mbuzi 120,000. Kulikuwa na wachinjaji, lakini sadaka na ibada ilikuwa ya Sulemani, ndiye ambaye moyo wake uliambatana na hazina aliyoweka juu ya ng’ombe wale.

  1 Wafalme 8:63
  Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea Bwana, ng’ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Bwana.

  Kwamba wanatoa sadaka misikitini, kwa kweli Mentor nashukuru sana umetufumbua wengi, na pengine hili lina nguvu katika kudai kwao haki hii zaidi hata ya hayo mengine yote. Hili pia lisituzuie vijana wetu kuajiriwa kuchinja wakati ukifika wa kufanya hivyo, lakini kwa majadiliano si kwa kupigana.

  Nahitimisha kwa kushukuru tena. Poleni sana wana SG kwa kuandika ‘bonge’ la mkeka. Nami naomba katika hili pia nisikie kutoka kwa wengine pia, niwe mtazamaji nijifunze.

  DM

 4. Safi sana mtumishi.
  Mimi maswali yangu ni haya:
  1. Kwani ibada inafanywa kwenye nyama machinjioni tu? Maduka ya nguo ya wahindi, watu weusi na wengine hufanya biashara za majini
  2. Hata kama ni kutakasa, utatakasa nyama tu? Mbona maisha ya shuku ni magumu sana
  Mimi nadhani ukisimamia neno la Waebrania 4:12-13 juu ya uwezo wa neno la Mungu lililoko ndani ya mtu kwamba linamaliza kila kitu
  Ubarikiwe mtumishi

  Emmanuel Lyatuu

 5. Shalom Alistidia,

  Naomba niongezee vitu vichache katika ujumbe wangu wa mwanzo.

  Wengi kati yetu wapendwa tumekuwa tukiombea amani ya nchi yetu. Amani ambayo inaitambulisha Tanzania dunia nzima.

  Kinachoishangaza dunia ni jinsi ambavyo Tanzania ina makabila mengi lakini hakuna ukabila, na watu wake majority wapo katika dini mbili kubwa, Wakristo na Waislamu, lakini hakuna udini (nasema hakuna ingawa wengine wanasema tayari umeingia, mimi nasema bado maana udini usiombe kuuusikia, picha nzuri ni Nigeria ndipo upo hasa.)

  Asili ya jambo hili ni nini? Ni kuvumiliana, kutokuwepo kwa extremism, bali kila mmoja anaheshimu imani ya mwenzake bila ku-compromise imani yake. Yaani navumulia adhana za asubuhi misikitini, hata kama zinaniingilia usingizi wangu, ili nao Waislamu wavumilie mapambio yangu ambayo nayaimba kwa sauti ya juu hata kama nitakesha nikiimba tena huku natumia kipaza sauti na hali nikiwa nimezungukwa na nyumba za familia sita hadi kumi za Kiislamu.

  Huku ndiko kuvumiliana kulikoifikisha Tanzania hapa ilipo leo. Tanzania yenye watu wenye majina mchanyiko wa dini hizi mbili mengi sana, mfano Happiness Juma, Joseph Ramadhan, Kassim Clement n.k. yaani inamaanisha mtu alikuwa Muisilamu, akakutana na mhubiri mzuri akamuhubiria habari za Yesu akaamua kumpokea, akaokoka. Anarudi nyumbani anawajulisha amempokea Yesu hivyo sasa ni Mkristo.

  Pointi yangu ni nini?
  Amani tuliyonayo yatokana na Mungu, haitokani na vikao wa usuluhishi wa watu, kwa kuwa asili ya amani ni Mungu pekee.

  Yehova Shalomu maana yake ni, BWANA ni amani.

  Waamuzi 6:24
  Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu.

  Yaani jinsi Tanzania Wakristo walivyochangamana na Waislamu ndivyo alivyoweka Mungu, na ni ajabu sana, katikati ya hali hii amani imekuwepo. Ni kwa sababu YEHOVA Shalomu yupo na amekuwepo siku zote.

  Tunapaswa kufanya nini? Ikiwa tukiwaona Waislamu kuwa ni watu ambao hatupaswi kuchangamana nao kabisa, waende wapi? Ikiwa wao hawatatutaka kabisa, tuende wapi? Kuna nchi moja inaitwa Serbia waliamua kuwafuta kabisa Waislamu katika nchi yao, ikaishia kuwa ni mauaji ya kimbari, hadi leo hii aliyekuwa rais na aliyekuwa mkuu wa majeshi wapo mahakama ya dunia ya makosa ya jinai, na bado dini waliyotaka kuifuta nchini kwao bado ipo!

  Kilichotokea Zanzibar ni matokeo ya watu kufikiri kwa mlengo huu, wa “kwa nini hawa wahubiri habari za dini yao huku ambako sisi tuko 98%?” Sasa naona pia kuna Wakristo wameanza kufikiria, “hivi tutapatanaje na watui hawa ambao sisi ni nuru na wao ni giza?”

  Yesu alitufundisha jambo tofauti kabisa na kauli za namna hiyo, alitufundisha kuwa hawa tunaowaona na kuwaita giza ndio hasa tunapaswa kukaa nao ili tuwafanye kuwa nuru, watu hawa ni wagonjwa ndio hasa wanahitaji tabibu. Sasa iwapo tutakaa tulio nuru tupu wote tuemeokolewa, ni nani atawahubiria hao wanaohitaji kumjua Yesu ili nao wawe nuru?

  Mathayo 9:10-13
  Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake. Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

  Nayaunganishaje maelezo haya na suala la kuchinja nyama, na mapatano aliyofanikisha Shigongo?
  Ni hivi, ili tuweze kuendelea na amani Tanzania ni lazima tuweze kuendelea kuishi kwa amani baina ya Wakristo na Waislamu. Kauli za kutaka kuthibitishiana na kukumbushana jinsi tulivyo tofauti kwa kweli hazitusaidii sana, bali kadri wanavyozisikia ndiyo zinajenga “extremists” ambao hawakuwahi kuwepo Tanzania. Kumbukumbu zangu, ni kuwa Waislamu wengi sana wameokoka na wanaokoka kila siku. Huwa inafikia mahali naona ni rahisi kumhubiria Muislamu akaokolewa kirahisi kuliko kumhubiria Mkristo wa madhehebu yaq wasioamini katika wokovu. Tunayo mifano humu SG, yaani kila unapohubiri yeye anaona kana kwamba ndiyo anajua mara dufu yako, kwa sababu naye anasoma hiyo hiyo Biblia unayoitumia.

  Sasa tunafanyaje? Ni rahisi kwetu Wakristo kuongoza mapatano haya. Dawa kubwa ni kayafanyia kazi maeneo ambayo yanawezesha mapatano, kukumbatia yanayopatanisha kuliko yanayogombanisha. Hebu na tuifanyie kazi tofauti hii kubwa kati ya dini mbili, kwamba Waislamu wanashika sheria za mwili, zenye kufanana sana na namna watu wa Agano la Kale walivyopaswa, yaani kushika sheria zenye kuutiisha mwili. Mfano, ukisali elekea upande fulani, maandalizi ya kabla ya sala unawe hivi mara kadhaa n.k.

  Wakristo je? Sheria zetu ni za roho, hatupimwi kwa matendo ya mwili, mfano umekula nini, umeangalia wapi wakati wa kusali, uliinamaje, n.k.

  Ndio maana naona Wakristo wote tusiingie katika mpambano wa kung’ang’ania kuchinja, labda ikiwa ni kwa lengo la kuwafanya Waislamu waliozungumza vibaya kuhusu kuchinja wanyama kwa Wakristo wafute kauli zao. Kuwafanya wakiri kuwa hata Wakristo wana haki ya kuchinja wanyama.

  Lakini iwapo watakuja kwa mapatano watumishi wakubali. Yesu alisema kimtiacho mtu najisi si kile kimwingiacho, bali kimtokacho. Na bado hapa hakumaanisha kinyesi na mkojo (du, samahanini, ni haja ndogo) pekee, bali wivu, maneno ya uchonganishi, fitina n.k, yaani vile vitakavyo katika moyo wa mtu.

  Anayeng’ang’ania kuchinja huyo kwangu namwona ni mtumishi wangu, na hana kitu atakachokifanya katika nyama ile kitakachokuwa na nguvu kwangu, iwapo mimi nia yangu ni nyama, alimradi sishirikiani naye kwa namna yeyote katika ibada au mambo yake hayo.

  Kwa kumalizia, tukumbuke kauli ya baba wa Taifa, Hayati Mwl Nyerere ya kuwa dhambi ya ubaguzi ikianza huwa haina mwisho. Tukianza leo kutofautisha mabucha, tutaingia kutofautisha mabasi, tutakuja kutofautisha barabara, shule, masoko, mitaa n.k., mambo ambayo hayatawezekana na hayatatokea. Nayafuta yote kwa jina la Yesu Kristo yasitokee kamwe. Amina.

  Wao watekeleze sheria zao za mwili, sisi tutekeleze ibada zetu za kiroho, kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Wao wanatoa majini na mapepo kwa kusoma kitabu kwa masaa sita wakibembeleza na kutoa sadaka, tena yanakwenda kupumzika kwa muda tu, bali sisi tunayatoa yote kwa jina la Yesu Kristo, kwa amri moja hakuna kubembeleza, na yakitoka tunayaamuru tusiyaone wala kuyasikia tena kwa mtu yule, na yanatii kwa kilio na kusaga meno.

  Mwisho, watumishi wa Mungu wa Mwanza mmefanya kazi nzuri sana. Ilihitajika kufanya mlivyofanya na imesaidia sana Serikali kuamka kuweka kuheshimiana. Lakini sasa tukubali iwapo watakuja kwa ajili ya mapatano msifunge milango.

  Warumi 12:
  Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

  DM

 6. Kaka Deo shalom,
  Asante kwa ujumbe wako mzuri sana na unabariki,Ubarikiwe sana,Swala la ibada siyo nyama tu hata na mabasi tuyapandayo kila siku mengine yalifanyiwa ibada,baadhi ya maduka ,sokoni,mama ntilie hata nyumba tunazozipanga,Mungu wetu ni mwaninifu hawezi kutuacha tukaangamizwa kwa kukosa maarifa,
  Ubarikiwe sana mtumishi.

 7. Mtumishi DM,
  Nakupongeza kwa mchango wako muhimu sana kwa ustawi na uponyaji wa roho yangu. BWANA Yesu akubariki sana.

  Hata usipozikubali pongezi zangu BWANA Yesu ajua kuwa zimetoka moyoni na sio ushabiki.

  Nimefurahi kusoma insights zako.
  Sikuwahi kulifikiria jambo la wachinjaji kwa namna ulivyolinena. Barikiwa sana maana nimeongeza idadi ya watumishi na nyama nitaanza tena kula maana niliacha.
  Nafikiri CHUKI NA WOGA viliniingia bila kujua kuwa nimemfungulia devo mlango na kumpa nafasi ya kunichafua na kunicheka.

  Asante kaka umeiokoa roho yangu na maangamizi ya siri ya adui.
  Ama kwa hakika AMANI INATAFUTWA KWA BIDII lakini zaidi HUO UTAKATIFU ambao pasipo huo, hakuna yeyote ATAKAYEMWONA MUNGU Ebrania 12:14.
  Hili wapendwa wote tuliomo humu church na wasiomo twapaswa kulijua na kulitenda. Deo ameongea vema sana, kuwa waislamu wanapaswa kumjua Yesu, so nani atamjulisha Yesu kwao ikiwa tunapambana ktk mwili na hatuna amani nao? Hivi kweli ni nani alituroga hata kubeba bango la kuchinja?

  Oooh wana wa Mungu, tuweni macho kwani nyakati tulizomo ni za hatari. Hebu fikiria km Mwanaume Yesu angerudi jana kulitwaa kanisa lake kabla cjasoma msg ya Deo na kughairi mabaya hayo ya kuwachukia moslems moyoni mwangu ingekuwaje?

  Hebu kila mmoja wetu awe mwangalifu ili asije akayapoteza yote aliyoyatenda ktk Mungu maana Baba yetu haangalii ulivyoanza bali ulivyomaliza.

  Deo umenifungua ktk ufahamu zaidi nami nina kila sbb ya kumshukuru Mungu for using u in such a special way to me, cjui kwa wengine. Asante kaka ht kwa kukubali na kumtii RM kwa kile alichokupa kushare nasi. Mimi nimepokea and I promise to work on every powerful msg I have taken from your main msg. Nitabariki, na kula provided kwamba uwezo wa neno la Mungu wangu unabomoa na kuharibu ibada zao. Nilisahau kuwa niliyenaye ni Mkuu sana kuliko waliyenaye (wa dunia hii)
  Asante kwa kunikumbusha na zidi kutusaidia kila upatapo nafasi,

  Barikiweni nyote,

  Gladys

 8. Wapendwa Seleli na OGUDA,

  Sacrifice inayotolewa na wachimbaji, wajenzi wa madaraja, vifaa vya dhahabu, viwanda nakadharika ni sadaka za kwao hazituhusu sisi wafanyakazi. Nachojua ni sehemu za ibada zao wanafanya ivyo na wanagawa nyama zile kwa wafanyakazi wanaotaka kula. Ila sijawahi kupata ufunuo kwamba wakinigawia nipokee halafu niikomboe nile hahahaaaaa. Nimewaona wakifanya hivyo na sio wachina tu hata makampuni ya kizawa. Boss aliwahi sema hivi, kwa sababu tumefanikiwa sana mwaka huu na tufanye ibada (RC)kwa kumwita padre, halafu tutafanya na Sacrifice ambayo itaambatatna na sherehe. Hiyo sacrifice walichinja mbuzi na damu yake wakanyunyiza kuzunguka office. Lakini nilipoona hivyo nikashuhudiwa ibada ya kipepo hiyo sikuhudhuria na hakuna aliye niuliza.

  Nadhani utata mkubwa ambao wengi unasumbua kwa sasa ni kwamba, waislam wanasema kwamba kuchinja ni sehemu ya ibada yao. Shida ipo hapa tujadili kuanzia hapa na si vinginevyo. Je waweza kula nyama iliyotolewa kwa tambiko la kiukoo???

  Nadhani tunahitaji Neeema ya Mungu Kujua yote haya.

  Barikiwa Sana kwa michango yenu mizuri.

  Anthony

 9. Pastor Deo,

  Hakika nimebarikiwa sana, ONLY THREE points nitakua nimemaliza shauku ya moyo wangu

  First,.ninakutia tena moyo(ninapenda ku-appreciate sana kwakua ni KiMungu kabisa, bahati mbaya watu hu-take it simple/hupuuza au kutojali such sweet quality ya character na wengine ukiwa-appreciate..hawa-accept-hii nayo ni problem pia kama wale wasio-appreciate au kusema asante na ubarikiwe, Najua sadaka kubwa sana inayoingia mpaka mtu uje na pieces izi..ya kwanza na hII ulIyomwa-address Alistidia pekee! so bless you for your time, searchingin the Bible, typing, proof reading, other references..your sadaka will never go in vain, each deed/word ya Mtu is recorded.Rev. 20:11-12

  Second, Kuhusu mambo ya kuchinja na kua wanafanyia sala/ ibada zao na kua tuwe na zetu…Nimebarikiwa na argurments za Emmanuel na Alistidia pia kua ibada na matambiko yako pia ktk maduka ya nguo, mabasi tuyapandayo kila siku-bila shaka ya kwenda mikoani, bidhaa za sokoni,misosi ya mama ntilie, nyumba tunazozipanga naongeza hata madalala ya bongo, yapo yaliyopatikana kimizimu-zimu na yanapugwa mizimu originali kila baada ya kusanya ela kwa mwezi,, pia baadhi ya majina ya magari madongo-dogo ya saloon ya Japan ni majina ya miungu ya wajapani, baadhi ya majina hupewa magari hayo kama sadaka kwa heshima kwakwe na kila aliandeshaye duniani uko, autangaza utukufu wa mungu huyo aliyowawezesha kua na creativity na kupenya soko kali la kimataifa–imagine gari yako mpendwa inaitwa ……ya Japani kumbe ni mungu, so hunaendesha Dar hapa kumbe unafanya bonge ya ”’gospel” ukiutangaza utukufu wa bwana wa majeshi stupid yule wa Japan! pia baadhi ya products za electronic namely radio, Tv, laptops,saa ni miungu-imagine kumbe we buy gods za Japan and enjoy with them at our homes, hata baadhi ya vyombo vya ndani vya kichina na products nyingine, majina yale ni miungu na vimetolewa kwa minajili ile ile ya ibada na sadaka kwa heshima kwa miungu iyo, huwezi amni hata baadhi ya majina kwenye vyombo vya muziki, praise and worship, ni mapepo names given kwa miungu iyo kama ibada na sadaka, hata baadhi ya raba/viatu vya kichina ni madude hayo hayo nk…

  Kila kitu humu duniani ukikichambua sana kwa mlengo wa kipendwa, kikwetu, hakifai in this context!. la sivyo yatupasa kuhama duniani tena haraka baada ya kuookoka, tukapelekwa sayari ya Mars or jupiteri or else..wapendwa tuwe na maduka, viwanda, nyumba zetu na kupangishana sisi kwa sisi tu na viwanda kutengeneza magari na products zetu tu…unfortunately hili halipo na nadhani halitakuwepo til He comes back!!!!!!! no question wafilisti na wayebusi wataendelea kumiliki baadhi ya vitu na mambo tunayotaka sana on our daily life..NO WONDER TO MAKE THINGS EASY FOR US…YESU ALINYOOSHA SENTENCE MBELE YA BABA YAKE KWA KUSEMA KUA HASEMI/HAMWAMBII BABA YAKE KUA TUONDOLEWE DUNIANI BALI TUNADUNDA HAPA HAPA TUKINGWA DHIDI YA MWOVU NA PIA YESU MWENYEWE ALISEMA…WAKIWAWEKEA MISOSI MBELE YENU, NI KUPIGA KWA KWENDA MBELE-iNTERVIEWS SIJUI MEAL NI TAKATIFU OR ILINENEWA KWA NDIMI WAKATI INAANDALIWA CANCELLED!!!!!!!.Paul naye ali-make life simple with no pressure kwa kuclear the way…akasema…mkienda sokoni…msiulize ulize…nikununua meat na kuambaa nayo to home and make it disapper from its existence …no p.,, I am afraid kua sometimes in the zeal to please God-kitu ambacho ni chema sana, tunajikuta tena tuna complicate life na kuji-creatia artificial mapito na majaribu..the man-made..neither God nor devil is responsible to bring them into its existence to suffocate us.

  Third, Kuhusu Shigongo kuhusika pia ktk kuleta ”one table talk” ”one event chat”, in the first place, kwa wanaomfahamu Shigongo, ni mtu aliye na hofu ya Mungu na niliwahi kua informed kua alikua ni mpendwa though later baada ya mpenyo kupatikana na mafanikio, taratibu akataa net works za ndani..todate hata kama hatumuoni akiwa kama sisi but nakuhakikishieni has hofu ya MUNGU-ULE BASIC UCHAJI… ninashawishika may be atamrudia Bwana fully kama zamani before kutajirika..so walimponda kiaina, he is not that much bad or devilish brother..he is and has been doing good job kuhusu kunyanyua watu wa kipato cha chini na kusaidia vipaji na break thr za wengi sana ktk seminars, workshops zake na ile movement/vision yake STREET UNIVISERSITY. Lakini hata kama angekua off ya Mungu ie hajaookoka na hana hata chembe ya hofu/basic uchaji wa Mungu, awe mpagani kabisaaa, yet akafanya jambo jema,,WHY DONT WE APPRECIATE HIM? tatizo lile lile!!! gonjwa baya la kutosema asante/kua appreciate.

  Tatizo letu kwakua tu tunamjua Mungu sana, we want to make everybody and everything useless!Niliwahi kuuliza uko nyuma kua je just because watu hawawajaokoka na wako ktk ndoa, they COMPLETELY GOT NOTHING I CAN ADMIE AND LEARN AS A BORG AGAIN? ofcoz plenty-plent i can learn-Moses. Si mnakumbuka Nyerere alivyofanya kazi njema kuwapatanisha wahutu na watusi later Mandela akapick task? si mnakumbuka Mandela alivyofanya maajabu kwa kuwasamehe wazungu wabaya wale waliomfanyiwa unyama kwa miaka robo tatu ya miaka yangiu so far..akiwa ndani ya segerea ya kule- just because Nyerere alikua mtu both rozari, bikira Mary na mizimu-si mnakumbuka baadhi ya hotuba zake na kulitokea nini mwili wake ulipokua unanakaribia home kwakwe Butiama na just because Mandela todate hajaokoka na ni full traditions and customs za kimilia..then tusiwakubali kazi zao na kuwa-admire? kwamba eti tuwaponde… ooh nini bwanaaa…wana fungu gani sijui na nk…ajabu kabisa…Kama mnadauti au waga watu hawana apprecitions, Yesu alicomment jambo..alisema..wana wa ulimwengu wana hekima zaidi kuliko wana wa nuru na pia alkisema…mafarisayo mnaweza kuwasikiliza kwa kua wanasimama ktk kiti cha Musa..yaani its fine to get their lectures, they have got some stuff-ndicho Yesu alimanisaha ila tu kwa matendo yao ndio msi-cut na kupaste–if Jesus appreciated/accepted that wana wa ulimwengu can be smarter and pia Mafarisayo got nondo too, so be it with Shigongo, tusiponde ponde kila kitu ovyo..we need to change the atitude zetu..tupongeza mtu na kusema…good job bro..keep it up..si kunyuka na kusambatisha tuuuu kila kitu just because kafanya mnywa tusker laga na ikamlagai.

  Press on learning and practising good atitude ya appreciations by telling somebody.. asante, hongera, umefanya vema, endelea mbele nk

  Edwin Seleli

 10. Ooh, Seleli, ubarikiwe kwa combination ya hojaa karibu zoote za wapendwa.. DM, nawe ninakupongeza kwa maswali na uchangiaji mzuri. Bila kuwasahau wengine. Naam, sihitimishi, bali nina clarify baadhi ya mambo kkidogo. Binafsi, niseme ya kwamba,, sijamponda msuluhishi nimempongeza kwa jitihada zake, ila ukinisoma vyema toka huko nyuma juu ya mada hii y kuchinja na uletaji amani Geita, utagundua kuwa, i hv bn discussing 2 things, One, Kuchinja kwa Muslims ni ibada, hili ndg zangu si suala dogo km mnavyotaka kuliweka lionekane, it is irresponsible, or, does not come up, (i’m so sorry to say so), kufanya comparisson ya mifano mbali2 ya vitu zalishwa viwandani km nguo, magari, n.k., na kiumbe hai km mnyama ambaye kabla ya kuingizwa kwake matumizini, hutolewa uhai wake kwa kuchinjwa ili damu imwagike, naam, nanyi si Wakristo wadogo, mwaijua vyema nguvu ya agano la damu, na nyama, zinazosongolewa kama kwenye sadaka. Ibada za hawa jamaa, ni sadaka kwa mungu wao maelekezo y qibla. Ninyi mwaleta viwango vyenu vya imani, ni vyema, twajifunza kitu pia, asemapo, “chochote mkikutacho sokoni, kuleni pasipo kuuliza uliza”, maana, mkihoji, mtakuwa najisi, mtakwazika, ss, here comes a situation, where by the Muslims themselves wanayasema hayo na ktk mafundisho yao kupitia media wanayachambua wazi. Nambie, je, woote tuna imani sawa ndg zangu?? Maandiko yanasema, mwengine hana imani,yaani, ni dhaifu, anakula mboga tu, ww mwenye nayo, kula nyama, na endelea.Lkn pia, twaambiwa ya kuwa ktk Marko, “hata mkila sumu, haitawafisha”, nauliza, na km umekwisshakuitambua ya kuwa, ndiyo hii sumu yenyewe, waweza kuendelea kuibugia tu?? Hapa ndg zangu, limekaa kiroho sana, pata ufunuo wa kina, do not bring mazoea ya history, ati kwakuwa, wamekuwa wakichinja wao 4 so long, you see nothing wrong, hv talked to some good prayers may be, hili lina madhara mengi sana kiroho ndani y kanisa.

  Pili, katiba ya Tz haijabagua watu juu ya ajira, naam, kuchinja ni ajira na zimewekwa chini ya halmashauri, lkn, ati, waajiriwa ni Muslims pekee. Ww mwenyewe Seleli ume mention humu andiko kuwa, Kriisto alimwomba Babaye kuwa, asituhamishe ulimwengu huu, yaan, tubanane hmhumu. Dhana hii, ina ukaburu, and thats not good, na hapohapo, kumbuka, these guys/ Muslims, wanahangaika both kiroho na kimwili hii nchi wapewe wao waimiliki, makafara kibao ya ngami, na ss wanatingisha kiberiti kwa kututoa sisi Wakristo sadaka, wakidhani wamtolea mungu wao, sawa na Yohana Mtakatifu sehemu fulani mule ndani.Unashangaa juu y haya mambo ati kn kwamba niaje leo ndo Wakristo twayashtukia?? Lkn, nami ntawauliza pia, hv zamani ungeliweza wapi kusikia habari za misukule??? Au, wengine wetu sssi wkt tukiokoka, uokovu ulikuwa haukubaliki mno, je, siku hz je??Umehoji ya kuwa, je hayo mambo ya kuchinja kwa nini yawe Geita tu?? i just assume kuwa mnataka kuwa dhani hao ndg ztu hko ni wakorofi tu, hapana, kila kitu kina mwanzo wake, hata historia inaonyesha Wokovu Tz ulianzia pale kijiji cha Igale Mby, hivyo, hayo, yatafika tu na kwa maombi yako pia, na si kwa kupishanapishana ambako kumekwishakuonekana km ndo fungu la Walokole Tz. Mwisho, niseme ya kuwa, hata huko Geita ndg zangu wako watu wa Kiroho sn, tuwaelewe tu, na kiiiisha tushiriki kwa kuwaombea na si picha hii ya kuwakandamiza mnayoionyesha humu. Nina declare interest., i know and relate to no body there, but, the Christ body and brotherly love we ought 2 share with them. God blez you servants of God.

  Oguda J.E.

 11. Oguda Edmund,

  ..umesema very powerful point

  Maswali kidogo na fafanuzi kwa ajili ya majadiliano na kupanuana both spiritual and bodily thinking

  ….Ingawa ni ukweli mzito agano la damu lina nguvu kweli nonetheless, kwani wanapochinja wakiwa wamesema sala zao waga wana fanya agano in strict sense au wanafanya tu shukrani kwa mungu wao basi na kuombea kile kiumbe ili kukihalalisha/kukislimu? kwa sababu nina vyofahamu maana ya kuweka agano may not necessarily be in any na kila simple ibada au sala! what is your clear concept about KUWEKA AGANO? to me ITS IS CRITICALLY BIG THING, it is clear cut intended and rarely performed part of ibada for a certain partticular purpose! correct me if am wrong brother ili nipate nondo hapo

  ….buying from above..ie kua wayafanyayo siyo kufanya agano la damu in a real sence but rather normal religious practices ie ibada na sala zao then don’t you think kua hata vitu(maduka, nyumba tunazopanga,plots upon which tulijenga nyumba zetu,magari,misosi ya mama ntilie,mabus kwenda mkoa, hotels/guests house tulalazo, baadhi ya vifaaa vya electronics, kwa kutolewa kwavyo sadaka na hata vingine kupewa majina ya miungu wao au kufanyiwa sala hakuna agano la damu but ni religious practices tu,so no harm to us?

  ….. lakini tuchukulie kwa kiroho cha juu na ukali mkubwa kua kila kifanyikacho-iwe mnyama kauliwa au normal religious practices eg izo sala za kuchinjwa, YOTE YAWE NI MAAGANO, halafu ninachukua/nunua na kabla ya kutumia, nikamwaga maombi eg yale tunayoombaga mfano kuweka gari wakfu ukinunua au nyumba mpya au msosi wowote tunaomba kubariki na kutakasa kabla ya kula/kutumia, je kama mtu mwenye RM akiachilia maombi hayo kama alivyosema Deo, pia wewe…si tunakua tumefuta kila kitu, pressure iko wapi? why panic? si mambo fresh tu hapo? power,mamlaka tunayo, kuclear kila kitu mbele zetu au? kama ni kweli iyo nguvu tunayo, hata kama agano ni la adamu, kwani inatutisha sasa?

  ….Tukichukulia guidance ya Mdo 15:28-29, was it for zile zilitolewa kwa mashetani kwa maana iyo kali sasa ya agano la damu au hata kama hakukuweko damu but as long as zilifanyika religious practices kwa nyama zile kama sala za kuchinja vyote walipaswa kujiepusha? kujibu ilo linganisha na guidance hii pia I Wakorinto.10:23-33-angalia mstari 25 meat market Kiingereza inasema..eat whatever is sold in the, asking no questions for. conscience’ sake.Zingatia mpaka Paul azungumze kipekee kuhusu nyama sokoni, unaweza kua na uhakika walikua na tatizo kama la leo ie nyama nyingine zilikua zinafanyiwa sala na hata maagano so to speak but akatoa guidance, ipi?….hii… eat whatever is sold in the meat market, asking no questions for conscience na pia kwa mbaali kwa kua context ni nyingine but just a thought worth it to consider ni Luka 10:7-8 Yesu anasema…Stay in that house, eating and drinking what they give you; for the laborer is worthy of his wages. Do not keep moving from house to house. “Whatever city you enter and they receive you, eat what is set before you; A such serious spiritual Jesus more than Oguda and Edwin,Deo, Alistidia,Emmanel, Kombe, Mwikwabe,Cathy, i wonder why hakuweka conditions kua wanafunzi wawe makini sana kuhusu maagano, sala na religious practices kwakua possible kabisa Jesus alijua wanadamu wale walikua hawajaooka ivyo misosi yao ambayo wangewapa wanafunzi/wapiga injikli, in one way or the other lazima ilikua na madude or imefanyiwa madude yet Yesu akato guidance ipi?eat what is set before you na eating and drinking what they give you. Didnt Jesus know effects ya madude hayo…sala,religious practices zozote na maagano ya damu na vitu? bila shaka anajua kua we have power over all these.

  ….Kama iyo ya juu haikuungii, embu sema sasa tukaishi wapi na tukale wapi na tununue wapi kwa kua kila kitu kuanzia vitu mpaka nyama..kuna sala, matendo ya kiibada na maagano ya kidevo na damu? ivi unajua pia hata vito vya thamani kama bangili na eleni, mikufu, chain nk, vingine kama siyo vyote wanaochimba wengi ni wasiookoka na kuna ibada na maagano hata ya kulipua watu kumi au 5 kwa baruti wakiwa chini wanapasuka na kufa-damu nyingi iyo na kweli kabisaa dhahabu ndio inatoka na leo hii twawavisha mabinti sayuni ktk harusi na vigelegele vingi olololollolo kririririkrirkririririri….mtu unaondoka na mdada wa nguvu to honey moon but ringed by agano la damu thing kwa kidole kizuri kile? je wajua wachina wanapojenga barabara zetu huwezi amini ibada zinazofanyika? check na mpendwa mjenzi/mhandisi ktk kampuni izo akupe story, ni kafara zinatolewa mlimani uko wanaposua miamba na mabonde kisha mimi na Oguda haoooooo Musoma kwa bus la agano pia tena juu ya barabara ya agano tukienda kuubiri injili tumetumwa na SG? you know ma meen Oguda and all SG..i see Jesus alikua na akili sana…very smart kuomba iki..Yohana. 17:1- 26..it is so sweet maombi..YESU ANAONGEA NA BABA YAKE…SOMA YOTE TAMU SANA KISHA ZINGATIA MSTARI..6-20 halafu angalia kwa macho yote mistari hii 9,11,12,14,15

  ..mbarikiwe enyi wote

  Edwin Seleli

 12. Nalikuwa nasemaje mtumishi, kuwa, kuna wakti naliwahi kmuhoji mmoja wa watumishi walio frontline kuwa evangelize Moslems, alinifundisha siri nyingi saana za hawa jamaa, ndiposa, nikasema kuwa, hii ni Neema tu, mimi nawe, yawezekana tumeitwa kuliimarisha kns kwa mafundisho, lkn, wengine ndani ya kns wana kazi mahsusi. Mfano, wale wa Biblia ni jibu, sk moja nalikutana na mmoja wao, ndipo, nilipokuja kujua kuwa, hakuna limshindalo Bwn, alimgeuza mtu ambaye hakuwahi kuwa ht kuujua uislamu, ni RM mwenyewe alimpa interest na kumfundisha uislamu, kiasi kwamba wakimuona humkimbia. Mungu atusaidie. Oguda J.E.

 13. Shalom Wapendwa wote SG,
  Nimefuatilia michango yenu watumishi wa Mungu, nimejifunza mambo mengi sana. Ninakubaliana na wote wanaompongeza Shigongo kwa kazi nzuri (but temporal) yaliyoifanya. LAKINI TUJE KWENYE KIINI CHA TATIZO HILI, NI VEMA TUKILIELEWA SAWA SAWA.

  TATIZO SIO KULA/KUNUNUA
  Wapendwa TATIZO SIO KULA NYAMA ILIYOCHINJWA NA MWISLAMU kwa sababu kafanya ibada fulani wakati anachinja. Hilo ndilo ambalo wapendwa wengi wameaminishwa na ndiyo ambavyo hata watumishi wengi wa Mungu (nje ya Group hii walijua hivyo). Lakini baada ya kuelewa tatizo liko wapi nao wameungana kuhakikisha kuwa MPAKA KIELEWEKE MKRISTO NAYE ACHINJE. NA KAMA WAISLAMU HAWAKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WAKRISTO BASI KUWE NA MACHINJIO YA WAKRISTO NA WAISLAMU NA MABUCHA SAWIA.

  Inawezekana hata humu kwenye group tuna taarifa iliyoacha chanzo cha tatizo na kubakia na matokeo ya tatizo. Ndiyo maana tunashangaa ni nini hasa kinachoendelea. Tunajiuliza Je, mababa zetu wa kiroho hawakuliona hili huko nyuma? Why now? Lakini ambacho tulitakiwa tujiulize kama tatizo ni matambiko yanayofanywa na mchinjaji, mbona jambo hili linapigiwa kelele na Maaskofu wa dini zote za kikristo ambao ndani yake wamo ambao hufanya ibada za namna hiyo? Au ina maana kweli Maaskofu wetu hawajui kuwa wanaofanya biashara hizo hufanya matambiko mbali mbali awe mwislamu au mkristo? Kwanini matambiko yashikiwe bango kwenye kuchinja tu?

  TATIZO LENYEWE
  Kwa wale wanaofuatilia, tatizo hili lilianzia kijijini ambapo Mchungaji mmoja aliyekuwa na msiba alipochinja ng’ombe kwa ajili ya waombolezaji. In short (ili nisiandike mkeka) – Waislamu walifanikisha Mchungaji huyu alitengwa na Wananzengo kwa kosa la kuchinja. Hapo ndipo kwenye chanzo. Na nilishawaeleza kipindi cha nyuma kuwa tatizo hili LILIKUZWA na jinsi Serikali yetu ilivyoli-handle swala hili. Hebu fikiria kidogo; una msiba, umetoa ng’ombe umemchinja, waisalamu wamekuja na kutambua kuwa ng’ombe yule (sio wao, ni wako) hakuchijwa kwa taratibu zao na hivyo linakuwa ni kosa na kumtenga Mtumishi. Kumbuka Mchungaji ana kundi analolisimamia, asifanye kazi ya Mungu kwa sababu kachinja??? Na Serikali (ya kijiji/kata) inabariki jambo hilo n.k. Halafu baada ya hapo kunaambatana na matukio mengi sana ambayo yanatishia uhai na ustawi wa wakristo. Laiti tungekuwa well informed yaliyoendelea, na yawezekana watu wengine hatujakaa vijijini mkaona unyanyasaji ulipo huko. Swali lililopo hapa ni kuwa; Je, Maaskofu wetu wakae kimya kwa ajili ya haya – HAPANA HATA KIDOGO.

  Pastor Deo unasema ukiwa na kuku wako ruksa kuchinja mwenyewe ukiwa wapi? DSM au kijiji ambacho viongozi wake ni waislamu? Tena kijijini watu huwa wanachinja hata mbuzi, kondoo, ng’ombe n.k. Mambo haya sio rahisi kiasi hicho wapendwa, na tunapojaribu kuyawaza kwa mtazamo wa mjini tukumbuke kuwa kuna wapendwa vijijini ambao hawawezi kuwa na fedha ya kwenda buchani lakini ana mbuzi wake. Wapendwa JAMBO HILI LIMEFIKIA PABAYA NI VEMA LIKIWEKWA VIZURI na kutolewa msimamo na Serikali!!!!

  CHANZO CHA WAKRISTO KUDAI KUCHINJA
  Itakumbukwa kuwa jambo la kuchinja limeachiwa kwa muda mrefu kwa waislamu, hivyo ikazoeleka na kuchukuliwa ni sheria kwa waislamu kuchinja. Hivyo kama mazoea hayo yanawafikisha kuona wao ndio wenye uhalali huo kiasi cha kutengwa Mtumishi anapochinja mwenyewe (ingekuwa wamemtenga Edwin angalau ningeelewa nga kidogo) lakini Mchungaji – hapana wapendwa. HIVYO HEKIMA inaelekeza nini hapa??? FANYA NA WEWE. Yaani ili mambo haya yasiendelee kuwaathiri wakristo ni VEMA wakristo nao wakaonekana wakichinja ili kufuta mtazamo ambao umejengeka na kujenga uhalali wa kumpa mtu adhabu kwamba aliyechinja HASTAHILI KUFANYA HIVYO. Kwani kuna dini inayostahili zaidi!!!! Kumbuka Serikali yetu imekuwa na kigugumizi kwenye jambo hilo na kitu kibaya zaidi (ambacho yawezekana hamkifahamu) ni wakristo waliowekwa ndani kwa kosa la kuchinja halafu kesi zao zimegeuzwa ki-aina yake.

  IBADA WAKATI WA KUCHINJA
  Jambo mwislamu kufanya ibada wakati wa kuchija limeongelewa sana lakini tumesahau jambo jingine lililopo hapo. Je, twajuwa kuwa kila wanapochinja kuna gharama ya kuchinja ambayo sehemu ya mapato hayo huenda moja kwa moja misikitini? Hapo ndipo unapoweza hafamu kwanini hawataki kabisa wakristo wachinje. Nisiendelee zaidi hapa.

  MWISHO
  Kama kwa sasa imefikia hapa, Je, watoto wetu watafikishwa wapi kama jambo hili lisipoweka VEMA mapema? Tukumbuke kuna mahakama ya kadhi nayo inajengewa uhalali. Japokuwa mimi sio msemaji wa Maaskofu wetu imenilazimu kuyaeleza haya wapendwa ili muuone na upande wa KWANZA wa shilingi yenyewe.

  Be informed,

  Mathew.

 14. Bwana Yesu wasifiwe mtumishi wa Mungu Rev. Mkenda,

  Naomba nami nitoe maoni yangu juu ya upanatanishi huu kati ya Waislamu na Wakristo. Naomba nianze kwa kujiuliza maswali na kujijibu, kama nitaweza.

  Yaani haya niyaandikayo si majibu ya mchango wako baba Pastor, bali ni majumuisho yangu ya jumla ya michango mbalimbali juu ya jambo hili, bali tu imependeza niingilie hapa ikiwa ni kama sehemu ya kupanuana mawazo juu ya jambo hili.

  Swali la kwanza: je! ni jambo baya au zuri kwa Waislamu na Wakristo wa Geita kupatana na kuishi kwa kushirikiana tena kama zamani?

  Jibu langu: Ni jambo jema sana, na tena ni zuri si tu kwa watu wa Geita bali kwa nchi yote ya Tanzania. Ikumbukwe kuwa mbunge wa Geita pia kashiriki katika upatanishi huu, naye ni mshirika wa makanisa yetu ya Wokovu, nadhani anaitwa Loyce Bisanda (???). Najua sababu hasa ni kwa kuwa yeye hapo alipo ni mbuge aliyepigiwa kura na wote, Waislamu na Wakristo.

  Swali na Pili: Je! iwapo kuchinja bado ni ibada kwa Waislamu, je! ni sawa kwa Wakristo kukubali upatanisho huu?

  Jibu langu: Nami najibu kwa kujiuliza mwenyewe, hivi ni lini jambo hili halikuwahi kuwa ibada kwao? Mbona tangu nimezaliwa, nikaokoka ukubwani, nikafundishwa, nikaanza kumtumikia Mungu katika nafasi mbalimbali, na hata leo hii mbona jambo hili limekuwa hivi, na hata sasa hapa Dar es Salaam sijaona bucha hata moja ya kuuza nyama ambayo haikuchinjwa na hawa ndugu zetu, na wapendwa tunaenda buchani tunanunua na tunakula na familia zetu? Na mbona jambo hili litokee Mwanza na hadi mauaji yametokea, na hali miji mingine, ikiwemo Dar ambayo imejaa “Wakiroho” malaki kwa malaki kama sio Mamillioni wanandelea kununua nyama buchani kama kawaida?

  Swali la tatu: Je! inawezekana tukachinja na kuwa na mabucha yetu wenyewe?

  Maoni yangu: Inawezekana, lakini pia inategemea unachinja nini. Kwa mfano, kama ni kuku mimi na familia yangu tunajichinjia wenyewe kwa miaka mingi tu, na wala haihitaji vikao wala kumuomba ruhusa mtu yeyote. Lakini iwapo ni uchinjaji wa kibiashara, mfano ng’ombe wa kusambaza mabuchani, hapa naomba nitumie kidogo taaluma ya business management (administration) ili tupime uwezekano wa jambo (feasibility), maana linahusisha pia usambazaji wa nyama hii ili kuwafikia walaji, ambao ni wenye mabucha.

  Jambo hili kwanza linahitaji machinjio rasmi iliyoandaliwa na kupitishwa. Miji karibu yote Tanzania ina machinjio moja, hivyo pengine itahitaji kugawanywa. Pili, uchinjaji wa ng’ombe sio jambo jepesi la kuamua leo na kuanza, ingawa kwa Mwanza hali ni tofauti kwa sababu wenyeji ni wafugaji. Hivyo wameona na kujifunza tangu wakiwa wadogo. Lakini hapa Dar tukisema tumchague Mwenyekiti wa Vijana wa kanisa Y akatuchinjie, badala ya kupata nyama ya ng’ombe tunaweza kumkuta kijana wetu kavunjwa mbavu kadhaa na huyo ng’ombe. Halafu badala ya yeye kumdhibiti ng’ombe ili amchinje, yeye ndiye inawezekana watu wakamuona anatimua mbio anakimbizwa na ng’ombe Vingunguti nzima huku akipiga mayowe, anakimbizwa na kitoweo

  Namaanisha kuwa ni jambo linalohitaji mafunzo ya muda mrefu, vijana wetu waione hiyo kama ndio ajira yao, waikubali n.k. Narudia tena, kwa Mwanza wapo, Dar je? Mmh, sina uhakika.

  Pili, usambazaji wa hiyo nyama utahitaji wafanyabiashara wenye nia na hamu ya kufanya biashara ya bucha. Si jambo la kumlazimisha mtu aanze leo kuwa na bucha bila ya yeye mwenyewe kuamua, kufanya feasibility study, kuwa na mtaji, na mambo mengine, vinginevyo itabidi tuzifuate nyama vingunguti. Inawezekana ukatoka Tegeta kufuata kilo mbili za nyama Vingunguti? Au itabidi kuondoa nyama katika “menu” ya nyumbani kama mtaani kwako hakuna bucha ya namna hiyo?

  Ilikuwa rahisi Geita, kwa sababu wilayani unaweza ukaweka bucha moja watu wote wakaifikia, hata kutoka vijiji vya mbali wakaja kwa baiskeli. Dar tutaiweka wapi? Ukiiweka Kinyerezi, wa Kigamboni vijibweni atafuata kilo mbili huko?

  Yaani biashara ya bucha ni biashara, anayefungua anafungua ili apate faida. Au itabidi makanisa yafungue mabucha? Is this option feasible? Hapana.

  Lakini pia naomba niingie ndani zaidi kidogo. Hivi Myebusi ni nani, ni Mwislamu tu?, au hata kwa anayeitwa Mkristo lakini hajaokoka? Tukisimamia mafundisho ya wokovu ni kuwa yeyote ambaye hajaokoka anakuwa bado hajawa sehemu ya Kanisa, yaani Mkristo. Huwa hakuna Mkristo wa kuzaliwa, yaani Ukristo haurithishwi, unaamini, unaokoka ndipo unakuwa Mkristo, unakuwa sehemu ya Kanisa. Hakuna cha kusema “nilibatizwa nikiwa na miezi mitatu!”

  Matendo 2:46-47
  Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

  Kwa hivyo kwa sisi walokole hawa Wayebusi pia wanajumuisha na wanaoitwa Wakristo lakini bado hawajaokolewa. Sasa hiyo haki ya kuchinja tujibakizie walokole tu?

  Maoni yangu: Sisi tulioanza kwa Roho tusitake kukamilishwa tena katika mwili.

  Wagalatia 3:2-6
  Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?

  Iwapo wao kuchinja wanafanya ni ibada, hivi ibada yao ina nguvu gani kwangu mpaka initie mimi hofu?

  1 Yohana 4:4
  Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.

  Kwetu tuliookoka ibada yeyote kinyume na kumwabudu Bwana Yesu haina nguvu, kwa sababu yeye aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Nikienda buchani kununua nyama ili nile na familia yangu, nikamshukuru na kumwomba Mungu akibariki chakula kile, ibada yangu inazifuta ibada zote zilizowahi kufanywa juu ya nyama au mnyama yule. My authority is high above all those other people waliosali kokote au kwa namna yeyote juu ya nyama ile.

  Ninamshukuru Mungu kwa sababu ndiye aliyeumba mifugo hii tunayokula nyama yake. Mimi peke yangu najua siwezi kununua ng’ombe mzima kila siku ili nijichinjie mwenyewe, ni lazima ku-share na wanaohitaji kidogo kidogo kama mimi, hivyo tunaenda buchani kila mtu kwa imani yake.

  Natambua aliyemfuga ng’ombe huyo alitambikia mifugo yake, natambua anayefanya biashara ya kununua ng’ombe kwa jumla kutoka kwa wafugaji ametambikia biashara yake, natambua mchinjaji anasema sala kwa imani yake “ibada”, natambua mwenye bucha nitakayenunua nyama kwake katambikia bucha na biashara yake, lakini LILILO LA MUHIMU NI KUWA NATAMBUA YEYE ALIYE NDANI YANGU NI MKUU KULIKO YEYE ALIYE KATIKA DUNIA.

  Nitakaposema sala yangu “Baba naomba ukibariki chakula hiki, ukitakase kinifae …….., kwa jina la Yesu Kristo, Amina.” Inakuwa! Chakula kinatakaswa dhidi ya hayo matambiko yote na hizo ibada zao zote zinafutwa juu ya nyama ile.

  Hakuna lolote walilofanya hao niliowataja hapo juu ambao ndio kwa ujumla wao wanakamilisha ‘value chain’ ya nyama mpaka inifikie, ambao tendo lolote wanalofanya linawapa haki ya uumbaji wa mfugo ule, bali haki ile ni ya Mungu aliye ndani yangu.

  NIMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NYOKA, NGE NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI (Luka 10:19). Kwa hivyo ninayo kazi nyepesi ya kukanyaga nguvu zote za yule adui katika nyama ile. Mungu wangu ananiona, ninapokwenda kununua nyama ile nia yangu ni kununua chakula, sio kushiriki ibada zao, ambazo kimsingi kwangu hazina nguvu yeyote.

  Na ndio sababu nimejaribu kufuatilia sana wazee wetu akina Moses Kulola nijue mambo waliyoyahubiri miaka na miaka mpaka leo tupo kizazi hiki chetu, mbona suala hili la uchinjaji halikufunuliwa kwao kwa kipindi kirefu namna hii? Mbona walipohubiri waliendelea kula nyama zinazouzwa mabuchani kama kawaida? Mbona hata sasa watumishi wa Dar hawajafunuliwa jambo hili, wakitoka kuchapa Injili, wanaketi na kula nyama kama kawaida? Mbona Mwanza limekuwa kubwa kiasi kwamba Mchungaji kachinjwa.

  Nimepata jibu (ninavyodhani). Jambo hili halikuanzia ndani, bali ni majibu ya mafundisho ya uchochezi wa viongozi fulani wa imani hiyo nyingine huko Mwanza, kwamba hawawezi kula nyama iliyochinjwa na wanaowaita wao ‘makafiri’, ingawa nadhani hawajui hata maana ya neno hilo. Hivyo ni “reaction to that”, ndiyo hoja ya Wakristo kuanza kuchinja ilipoanza. Kwa kweli napenda nikiri hivi ndivyo ninavyafahamu juu ya chanzo cha jambo hili huko Mwanza.

  Kwa maoni yangu, ilikuwa ni ‘reaction’ nzuri, kwa sababu imefanya Serikali iamke kupambana na wale wachochezi ambao ilikuwa ikiwaona lakini ilikaa kimya. Sasa baada ya watumishi kusimama katika zamu yao, ingawa kwa gharama ya maisha ya mmoja wao, ni wakati wa kutafuta tena amani. Hivyo Shigongo nampongeza amefanya jambo zuri.

  What is the way forward?
  Wapendwa tule nyama. Kwa kweli hakuna jema kama kula na kunywa kile kitu unachokipenda, tena ambacho Mungu kakupa uwezo wa kununua.

  Mhubiri 2:24
  Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu.

  Sasa kwa kuwa napenda nyama, na sifugi ng’ombe na ili nile njia iliyopo ni mimi kuinunua buchani, na inakuwa imechinjwa na watu wa imani nyingine, na tena wanafanya kuchinja kuwa ni “ibada”. Sasa nafanyaje?

  Hivi ndivyo nitakavyofanya. Nitawaona hawa watu kuwa ni watumishi wangu, wote wanaohusika kuileta nyama karibu yangu ili niinunue, yaani mfugaji, mnunuzi wa ng’ombe kwa jumla kuwaleta mjini, msafirishaji, mnunuzi wa ng’ombe momoja mmoja ili achinje, mchinjaji na mwenye bucha, wote hawa ni watumishi wangu. Kwa sababu pasipo hawa sitaweza kuipata hiyo nyama.

  Kabla ya kuila nyama ile nitafanya maombi ya kumshukuru Mungu kwa kunipa nyama, kisha nitaitakasa na nitaibariki na itabarikiwa. Maombi yangu yatafuta ‘ibada’ zilizofanywa huko nyuma.

  Wakolosai 2:16-17
  Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

  Ndugu zangu Wakristo, tusiicheze ngoma hii kwa stahili ambayo Shetani anataka. Tusipigane daima bila kutaka suluhu kwa sababu moja tu, haki ya kuchinja. Jambo hili lisitumiwe kuwa kisingizio cha vita na vurugu zisizoisha. Hivi yupo atakayeenda mbinguni kwa sababu tu kala nyama iliyochinjwa na Mkristo?

  Narudia tena, “reaction” ya viongozi wetu Mwanza juu ya mafundisho ya upande wa pili kuwa sisi hatupasi kuchinja kwa sababu kwao ni ibada ilikuwa ni nzuri na ya muhimu ili upande wa pili wachunguze upya mwenendo wao.

  Lakini wakijirudi kwa kupatana na wakaomba waendelee na kazi ya kutuchinjia inapokuwa ni kibiashara, mimi ambaye sina muda wala uwezo wa kwenda Vingunguti ili nijichinjie mwenyewe kwa nini nikatae? Nadhani hii ndio busara ambayo viongozi wa Kikristo wa Geita wameitumia katika kukubali mapatano, nadhani hivyo.

  Wakolosai 2:20-23
  Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

  Nashauri tukubali na tuwashauri watu wapatane, si tu huko Geita, bali Mwanza yote na kila mahali ambako jambo hili lilileta tabu kubwa.

  Tutie bidii katika kuziokoa roho, si miili yenye kuharibika. Hao wenye kuchinja wahubiriwe Injili waokoke, ili badala ya kuchinja kwa kusema sala zao za awali, waliitie jina la Bwana Yesu wakati wakitimiza kazi zao.

  Nakaribisha ushauri na kukosolewa au kurekebishwa kwani ndio sehemu ya kuyakulia mafundisho ya Roho Mtakatifu. Isipokuwa ndugu Nzala nakuomba sana usinijibu juu ya hili kwa kuwa sijakukusudia wewe.

  DM

 15. Hili swala wangeshirikishwa Maaskofu na wachungaji wengine Shigongo ana fungu gani kati ya dini hizi mbili? yeye hata akila vya madhabahu za miungu migeni hana hatia maana nisehemu yake,na ni fungu alilo chagua,je! kwetu sisi tununue nyama kwa wayebusi? au niishie kula samaki? cha msingi tunamhitaji Mungu awe suluhisho letu.

 16. Tuangalie AMOS 3:3

  Je wawili hao wamepatana katika msingi upi wa Mungu! Limbiko lipi la Mungu na chanzo kipi cha Mungu kuhusu kuchinja, au la hapana makubaliano hapo bali kuna msingi mbovu unaoendelea na limbuko bado ni bovu na chanzo kibovu kinaendelea…

  Wataendaje pamoja ikiwa wanakubaliana nusu hawapatani nusu..

  Kaa rohoni, utaona kwa sasa kanisa halitukanwi tena, tunatawala na kumiliki enzi na Bwana Yesu miaka 1000.

  Bezaleli DC

 17. Mimi naomba Maaskofu wetu na mababa wa Imani waongee kuhusiana na suala hili kwani mbele sioni nuru kwa sababu, naingia kwenye ibada ya mtu ambaye anamwabudu Mungu ambaye hatuchangamani hata kidogo. Sasa huo upatanishi una maana gani?? Pia inaingia akilini Wapentekoste kupatanishwa na mtu ambaye hajaokoka??? Kweli mimi nimejazwa na roho na ninamtumikia Mungu nikubali kuyafanya yasiyo mapenzi ya Mungu kirahisi namna hiyo. Haya mimi naomba WAKUBWA ZETU WATUSAIDIE VINGINEVYO KUNA MAHALI TUTAKAMATWA.

  Rev. Damasus

 18. Dear ALL
  Kwenye ustaarabu kabisa kuna maduka ya nyama yameandikwa HALLAL ili wale jamaa waende kununua na kula kwa amani vilivyochinjwa kwa mutkadha wa mahitaji (pengine ya kiibada) ya imani zao.
  Butcher zingine huachwa huru kwa kila aliyewekwa huru na DAMU YA YESU kula na kunywa baada ya kushukuru kwa UTUKUFU wa MUNGU.Lakini kwa nini tufike mahali pa kuchinjana na kuuana kwa ajili ya chakula na tumbo ambavyo MUNGU anasema KUWA MIILI HII na nyama HAVIWEZI kurithi ufalme wake?
  Kilicho tatizo hapa nchini tunatembea kama kuku aliyekurupushwa akakatwa kichwa akaachwa akafie iwezekanapo katika suala la uongozi.Viongozi hawasemi KWELI kwa sababu hiyo hawako HURU maana wamekula nadhiri na upande mmoja kulinda IBADA,na kinachoitwa HAKI zao NA SASA VIONGOZI-(SOMA WATAWALA) WANASHINDWA KUTIMIZA NADHIRI ILHALI KURA WASHAPATA 2010.Hii ndiyo tatizo ya AFRIKA ni UNAFIKI power of 100!
  Mapatano over SHED BLOOD?wale YATIMA waache kumlilia MUNGU ,BABA wa milele kwa kuwa SHIGONGO au mpatanishi yeyote kapatanisha basi wakiwa hawana Baba tena MCHUNGAJI?

  Mbarikiwe kiaina msiyotarajia
  Kombe,Elly

 19. WAPATANE TU JAMANI WAISLAM NA WAKRISTU,MANA UPENDO NDIYO TUNDA LA ROHO, UNAAMBIWA PALIPO NA UPENDO NDO PALE MUNGU YUPO,
  AMINA KWA WATU WA GEITA JINA LA BWANA NI KUU NA DAMU YAKE YESU INANENA MEMA KILA MARA.

  BARIKIWA

 20. Ndugu Oguda,

  Umesema vyema na kwa kweli concern yako ni muhimu sana. Mimi naomba nisiongeze sana maneno bali niweke maandiko kama alivyoorodhesha mtumishi wa Mungu huyu, labda pengine tutazidi kuelewana vizuri zaidi.

  1 Wakoritho 10:25-27
  Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo. Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.

  Sasa mabucha si ndiyo masoko ya nyama? Sasa tuulize-ulize nini tena badala ya kula kama Biblia inavyoongoza? Ndugu zanguni hivi kweli tumewahi kutembelea hayo mabucha tukawaona jamaa wanaochinja, hivi wanafanana ni hiyo ibada inayosemwa, au zaidi sana wanaelekezea mahali fulani tu(tena kama wanakumbuka). Sasa kwangu hii niione ni ibada ya kunifanya nigeuke kuwa vegetarian niachane na nyama?

  Tunachopaswa kukitaa ni hiki, kwamba ukiambiwa hiyo nyama imetolewa sadaka, labda ni nyumbani kwa muuini wa dini hiyo anatoa nyama hiyo kwa sababu ni sadaka yake, hapo Mtume Paulo anasema kataa kwa ajili ya dhamili yako. Soma hapo chini.

  1 Wakorintho 10:28
  Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.

  Kwa hivyo wandugu, nyama ambayo ninatumia pesa yangu kuinunua hiyo siyo sadaka. Nanunua kwa pesa ninayoipata kwa uweza wa Mungu wangu, Bwana wangu Yesu Krsito. Yule anayeuza ile nyama anauza ili apate faida, hatoi sadaka. Na pengine mwenye bucha ni Samsoni, Mkristo.

  Luka 10:7-9
  Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.

  Sasa tukianza kuhoji katika nyumba tulizotembelea, mfano, “Mzee Ezekieli, hivi hii nyama mliyonipakulia imechinjwa na nani?” Naye anamwita mkewe, “Hivi we mama Jose hii nyama kule buchani walikuambia nani alichinja?”. Hotelini Dodoma Hotel, unaletewa menu, unahitaji na maelezo ya aliyechinja.

  Jamani nirudie maoni yangu, kwamba ‘it is not feasible’ kwa ghafla biashara ya mabucha ya nyama za wanyama waliochinjwa na Wakristo zifunguliwe na kuenea kote kulingana na mahitaji. Sasa iwapo Mungu alishawapa majibu wenzetu ambao naamini walimuuliza Mtume Paulo moja kwa moja kwa vile walikumbana na shida kama yetu, ni kweli kuna jibu lililo bora zaidi ya hilo?

  Maana tukitumia nguvu kubwa sana kuwahamisha watu wasile ambacho hakikuchinjwa na mlokole, halafu mabuchani hazipatikani hizo ambazo ndizo zinatakiwa, matokeo yake itakuwa utaona taratibu yanazaliwa mafundisho ya kuonyesha jinsi ilivyo vizuri kula mboga za majani. Yaani watu wata ‘adopt’ mafundisho ya kirastafari na ma-vegetarian ili kuhakikisha nyama iliyochinjwa na wasioamini hailiwi.

  Au pengine kuna watakaoweka sheria kali, mfano: “tutawatenga wote watakaonunua nyama zilizochinjwa na wasioamini”. Matokeo yake wapo watakaokuwa wakinyata usiku kwenda kununua nyama ili wasionekane, wanaingizwa kwenye mtego mwingine wa dhambi ya kusema uongo. Kwa nini tufike huko kote? Hivi kweli hatujui walaji wakubwa wa kitimoto ni akina nani, lakini sheria yao inasemaje?

  Tuichukulie hali ya Mwanza kuwa ni exceptional case. Watumishi wetu walikuwa wanajibu hoja kudhihirisha kuwa suala la sisi kuruhusu wao wachinje lisitumiwe na wachochezi ‘radicals & exteremists’ kama hoja ya kuutukana Ukristo. Joto lilikuwa limepanda sana sana, na hatimaye suluhu zimeanza kutafutwa.

  Matendo ya Mitume 10:14-15
  Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.

  Nathibitishiwa ndani yangu ya kuwa Mungu aliyetuweka nchi yetu isiwe ya Wakristo pekee au Waislamu pekee, ndiye anayejua kuliko hata sisi ya kwamba yatupasa kuachiana baadhi ya mambo ili kila mtu ajione ana haki yake ya ku-exist. Hata nyau akiona kawekwa kona na hana pa kutokea huwa mkali sana na anaweza kufanya shambulio baya sana liwezalo hata kuua, ili tu atetee haki yake ya kuwepo.

  Ndiye anayetakasa vyakula tunavyokula na hasa kila tukimwomba afanye hivyo.
  Wapendwa ibada zetu sisi ziko juu ya ibada zote. Sisi tulishatoka siku nyingi kwenye ibada ya kumwaga damu na kuchinja tangu siku ile Mwana Kondoo alipochinjwa, yaani Yesu Kristo aliposulubiwa. Leo hii damu gani iatakayoweza kufanya agano juu yetu itakayoizidi nguvu damu ya Yesu Kristo?

  Lakini, hivi kweli ni ibada????
  Huyo mfanyabiashara wa nyama anachotaka ni faida, na kamwe ibada haitakuwepo iwapo hataitoa nyama hiyo kuwa sadaka. Akiuza tu, hakuna ibada hapo!

  Haya na huyo mchinjaji anafanya ibada gani kwa ng’ombe na mbuzi wasio wake? Kawanunua yeye? yeye si anachinja tu, hata hakumbuki idadi yao kwa siku? Jamani mafundisho yanatuambia nini juu ya hizo zilizokuwa ibada za kuchinja wanyama? Hivi ilikuwa mtu anadaka tu mnyama juu kwa juu anachinja inakuwa sadaka?

  Hapana! Ulihitaji kummiliki yule mnyama, kama hauna ukamnunue awe wako, ndipo ukitoa sadaka itakuwa umefanya ibada. Jamani, wachinjaji wetu hawa hao ng’ombe tunaouziwa ni wao? Hapana. Ni ibada? Hapana.

  Hivi hao wachinjaji wanachinja bure, si wanalipwa kwa kila mnyama wanayemchinja? Sasa hawa jamaa wanafanya ibada gani hapo, au akili yao si ni kupata “mshiko’ wa kula na vipande kadhaa vya nyama? Yaani hofu yangu mimi ni juu ya usafi wao wa mwili iwapo wananawa mikono, kuliko kuniambia wanafanya ibada kwa ng’ombe za wenzao!

  Hata kama wanasema ni ibada, sisi si tunajua si ibada? Kusema kamwe hakufanyi jambo lisilo la kweli liwe kweli.

  Ndiyo maana ya kauli ya Mtume Paulo, Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, maana kiuzwacho sokoni kwa ajili ya faida, anayekinunua kinakuwa chake, na ndiyo mwenye haki nacho, haki zote za aliyekiuza zinafutwa, yaani ni juu yako sasa iwapo unataka kukifanyia ibada, kifanyie. Mimi hapo ibada yangu iliyobakia ni kumshukuru Mungu kwa kunipa nyama ile tamu, na kukibariki na kukitakasa chakula changu, kisha hicho mdomoni, kisha tumboni!

  kwa taaluma ya biashara mtu akilipia kitu kwa bei halisi iliyowekwa na muuzaji, naye akakubali kukiuza kwa kupokea bei ile, basi inatokea ‘transfer of ownership.’

  Mtoto wangu angekuwa na magari mengi sana mpaka tusingepata pa kuyaweka, maana kila gari linalopita anasema lake? Sasa nimchape kwa kusema magari ya watu ni yake? Benz, lake, VW Polo, lake, Peugout, lake, vitara, lake, du! Kusema si ni kusema, tu. Wewe unayesikia si unapaswa kuchambua kulingana na mafundisho yako juu ya linalosemwa?

  Tusiingie kwenye mtego, in the first place hao wanaosema wanafanya ibada yaani hakuna cha ibada hata kidogo. Mtitiriko mzima wa nyama tunayonunua buchani umebebwa na msingi mkuu wa kupata faida kwa kila aliyehusika mpaka hiyo nyama imfikie mlaji. Ikishauzwa tu hakuna cha ibada hapo, sisi tunatoa pesa kununua nyama ya mnyama aliyeumbwa na Mungu, tunabariki, tunatakasa, tunamshukuru Mungu kishwa tunakula.

  Mimi nadhani hapa hofu ibaki kwa yule ambaye ana mashaka na mamlaka aliyo nayo. Au labda kuna wenzetu ambao kwao kuchinja pia ni ibada, hivyo wanahitaji wasipoteze haki ya kufanya ibada! Sina maana mbaya, bali nahitaji tu kupata ufafanuzi.

  Oguda, karibu mtu wa Mungu nipate mawazo yako. Kaka Edwin, bado nipo na wewe katika maelezo haya?

  DM

 21. Binafsi, ninampongeza sn ndg yetu Shigongo kwa jitihadaa kubwa hz za kibinadamu ili kufikia malengo ya kiroho, yaani, amani kwa watu wote. Naomba kujua, je, hao inaosemekana kuwa ni wachungaji, ama, ni Maaskofu, je, ni wa makanisa ya kiroho, ama, just wa Protestanti?? Lkn pia, niseme jambo moja mahala hapa, ALIMRADI HUKO KUCHINJA BADO NI IBADA KWA Waislam, hili ndg zangu, ni mpaka liwekwe sawa kwanza kwenye jamii ya Tanzania, vinginevyo, litabakia kuwa, km Sauli alipoamua kutokumuua Mfalme na Vinono vyake, km alivyoagizwa na Bwn asisaze chochote hai, matokeo yake, leo hii Issrael wanasumbuliwa mno na Wapalestina. Hilo jambo ndg zangu bado halina equillibrium, ni jambo ambalo linataka jamii ya Kikristo kuji submit under Islamic laws, Culture, and, Norms, may be kwakuwa, pengine President wetu ni Muislamu, hivyo, ht watu wenye uwezo wa kutatua haya kwa hekma ya kiroho na kimwili kuogopa, may be watarudiwa na serikali. Akhsanteni, naye, Mungu awabariki.

  Oguda J.E.

 22. Shalom wapendwa
  Basi ndugu EUCALYPTOS mambo unaposema ni sawa . lakini tujuwe kama adui yote kama iko mbali na wewe itakuwa nguvu ya yeye kukuweza. wandugu wetu waislam ni watu waliumbwa na Mungu. Sasa Imani yao iko tofauti sana na sisi moja hawabatizwi. hawamwamini Roho Mtakatifu.na kuna mambo mingi iko tafauti sana na wao . Kitu inabaki nikuomba Mungu juu ya mambo iyo sio vita ya kimwili ni vita ya kiroho

  Mbarikiwe ……………………………………

 23. Haleluya!

  Kuna hekima ninaiona kwenye kauli hii ya Godbles Lema (MB),

  “Hali hii ilipelekea Mbunge wa Chadema Godbless Lema kutoa tamko lifuatalo “Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani”

  Ni kweli na vyema kuwaheshimu, kuwaajali na kuwapenda watu wote pasi na kujali imani yao ama kigezo kingine chochote kwakuwa “amri mpya tuliyopewa ni UPENDO” na upemdo wa kweli hautoki kwa watu bali kwa Mungu mwenyewe.
  Katika hali hiyo tunatakiwa kuwa “wapole kama hua na werevu kama nyoka”, tuwe makini kujinasua kwenye hila “wile” kwani adui (Shetani) hakuwahi kuja kwa aina na namna tuijuayo.
  Twahitaji neema ya Kristo Yesu kung’amua.

  Mbarikiwe!

 24. haya ni majira mapya yenye kibali tele. ndugu na ndugu kupatana, jirani na jirani kupatana, nchi na nchi. haya na yawe majira ya amani popote ulimwenguni katika jina lenye mamlaka yote JESUS Christ of Nazaret. Amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s