Ukweli ni kwamba Yesu aliitangua Torati!!

torat

Wapendwa wa SG,

Naomba mnisaidie kupata mjadala utakoleta mwafaka kuhusu kutangua au kutotanguliwa kwa Torati.

Ukweli ni kwamba nionavyo mimi Yesu alikuja kutangua TORATI. Wapo watu wasiokubaliana na kauli hii kwa maneno ingawa kwa vitendo wanadhihirisha hilo.

Biblia imesema kwamba Yesu hakuja kutangua Torati wala manabii bali kutimiliza yote na kwamba hakuna hata nukta moja ingeondoka kwenye torati mpaka yote yatimie.

Kauli hii ya mwisho kwenye Mathayo 5:17-20 ndiyo imekuwa ikiachwa na wasomaji wengi wa andiko hilo. Naomba kunukuu tena andiko hilo:

“Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii;  la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.  Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, HATA YOTE YATIMIE” (Mathayo 5.17-20)

Ukisoma kwa makini utaona kwamba Yesu alimaanisha kuwa akiwepo duniani kabla ya kifo chake ilikuwa lazima Torati iendelee kutawala hadi yote yaliyotabiriwa na kunenwa na Musa yatime ndipo TORATI IFIKIE MWISHO.

Ukisoma kwa makini andiko hilo ambalo watu wengi hulitumia kuendeleza na kuhimiza watu washike maagizo ya Agano la Kale kwenye Torati na kutaka WATU wayafanye kama sheria, utaona kwamba siyo sahihi. Andiko hilo linamaanisha kwamba  Agano la Kale lilitakiwa litimizwe kwanza na ndipo Agano Jipya liweze kuanza na hapo ndipo Yesu aliposema “HATA YOTE YATIMIE.

Naomba nitoe mifano ya mambo yaliyokuwa ni lazima muumini wa Agano la Kale afuate ili ahesabiwe haki ambayo leo hii ukiyafuata hauwezi kuhesabiwa haki mbele za Mungu:

1. Kutahiriwa; Katika Agano la Kale muumini asiyetahiriwa hangeweza kuhesabiwa haki hata kidogo. Katika Agano Jipya kutahiriwa siyo lazima ili uhesabiwe haki na Mungu (Mwa 17:9-10, Gal.6:15).

2. Katika Agano Jipya tunaweza kula vyakula vyote isipokuwa vilivyotolewa sadaka kwa sanamu au vilivyonyongwa bila kuchinjwa, lakini wakati wa Agano la Kale kulikuwa na kuzuiliwa kula baadhi ya vyakula hasa baadhi ya wanyama kama vile sungura, nguruwe, samaki wasio na magamba, nk. (Mdo 26:12-18).

3. Katika Agano la Kale kulikuwa na utaratibu wa kutoa sadaka za wanyama ili mtu aweze kuhesabiwa haki. Hii ilikuwa sheria. Katika Agano Jipya Yesu amelitangua kabisa hilo halipo tena. Damu yake iliyomwagika inatosha kuondoa dhambi ya kila amwaminiye Yesu.

4. Katika Agano Jipya Kuhani alipaswa kuwa mtu mmoja tu amabaye alipaswa kuendesha ibada yote na kutoa sadaka za kuteketezwa. Hilo nalo Yesu alilitangua baada ya Kifo chake Msalabani kila amwaminiye anakuwa kuhani wa Mungu na anaweza kufanya ibada ya kuongea na Mungu moja kwa moja bila kupitia kwa mtu mwingine.

5. Wakati wa Torati ya Musa siyo watu wote waliokuwa wanaweza kumwagiwa Roho Mtakatifu ilikuwa ni kwa makuhani au manabii tu. Lakini hilo naalo Yesu alilitangua na watu wote wenye mwili wanamwagiwa Roho Mtakatifu.

Mwisho kabisa kuna vitu vingi sana Yesu alivyotangua na leo hii siyo tena maagizo ya sheria kwamba usipoyafuata umevunja Maandiko.

Naomba wapendwa wenye mawazo zaidi na ufafanuzi wa andiko hilo ambalo limekuwa likileta utata wajitokeze kuweza kujadili hoja hii; YESU ALITANGUA TORATI AU HAKUITANGUA? Kama aliitangua au hakuitangua unaweza kutupatia hoja za msimamo wako?

Asanteni.

Mr. Milinga 

Advertisements

78 thoughts on “Ukweli ni kwamba Yesu aliitangua Torati!!

 1. Hello,

  Mada hii hiituliiacha bila kujibu vitu ambavyo Nene, alivisema, lakini si vizuri kuuacha uongo ukae bila ukweli juu yake kuwekwa wazi.

  Nene alijaribu kuleta hoja za udadisi wa kiufuatiliaji wa maandiko na historia ya Biblia, akasema kuwa siku ya kwanza ya juma inayosemwa katika Mdo 20:7 siyo Jumapili bali Jumamosi jioni. Na hii yote ni kujaribu kupinga kabisa kuwa Jumapili haitakiwi watu kukusanyika kufanya ibada.

  Kuna matoleo kama manne hivi ya biblia ambayo Nene alitushauri tukarejee ili kuthibitisha kuwa ile ilikuwa ni siku ya Jumamosi jioni na siyo Jumapili.

  Kwanza katika hayo matoleo aliyosema (” (GNT), (ERV), (GW) ni toleo moja tu la GNT ndo limesema ilikuwa Jumamosi jioni, mengine yote yamesema Jumapili. Kwa hiyo kwa sehemu kubwa Nene katudanganya. Na sitaki kuingia kwenye kusema habari za hilo toleo ni la kina nani hasa.

  Pili, hakuna mahali mimi nimesoma maandiko yanapokataza kuwepo na kusanyiko la ibada siku ya Jumapili. Mara nyingi wasabato husema kuwa Jumapili mnaweza kukusanyika lakini si kwa ibada ya siku nzima. Hata Nene kwenye comment yake kasema hivyo hivyo, tena akaongeza kuwa lile lilikuwa kusanyiko kwa ajili ya sherehe ya kumuuaga Paul.
  Lakini cha ajabu katika hii habari, watu walikusanyika usiku mzima, mpaka asubuhi.

  Tatu, hebu tufikiri sote; Kwamba watu hawa walikuwa wamekusanyika asubuhi kwa ajili ya ibada ya sabato mpaka jioni inapokwisha sabato, sasa je waliunganisha au waliondoka kurudi nyumbani ndo wakarudi tena hiyohiyo jioni kukusanyika kwa ajili ya hiyo ibada ilikesha mpaka asubuhi? Waliwezaje kuandaa hiyo sherehe kabla ya sabato kumalizika? Ina maana walishinda ibadani Jumamosi nzima kuanzia asubuhi wakaunganisha mpaka Jumapili asubuhi!
  Hebu tulifikirie hilo tuone kwa kiasi gani linawezekana.

  Nne, kulazimisha kuwa hiyo inayosemwa siku ya kwanza ya Juma kuwa ilikuwa Jumamosi jioni, ni kutaka kulazimisha kitu ambacho hakina uthibitisho, kuwa ilikuwa ni jioni ya Jumamosi kumalizika. Biblia imesema tu kuwa ilikuwa siku ya kwanza ya juma, kwamba ni jioni asubuhi, alasiri au mchana ya saa ngapi haijasema. Wanaweza kuwa waliksanyika saa tisa alasiri, mambo yakaendelea mpaka usiku wa manane- mpaka asubuhi.

  Tano, lugha ya Kigiriki iliyotumika kwenye hilo andiko yenye kumaanisha ‘siku ya kwanza ya juma’ ni ileile iliyotumika kwenye Marko 16;2 – hata asubuhi ilipokwisha kupambazuka, siku ya kwanza ya juma…..
  Kigiriki: MIA TON SABBATON’- This is the common expression for “First day of the Week’

  Kama kusanyiko la akina Paul lingekuwa Jumamosi jioni, angalao tungekuta maneno kama yaliyo katika Mark 16:1- Hata sabato ilipokwisha kupita…., jioni hiyo tulikutana/tulikusanyika kuumega mkate. Lakini hii iko kavu kabisa kuwa ‘Siku ya kwanza ya Juma tulikutana kuumega mkate, haina dalili kabisa ya kujaribu kuonesha kuwa siku hiyo ndo sabato ilikuwa inamalika(jioni ya Jumamosi)

  Sita, Nene kasema kusanyiko hilo halikuwa la ibada kwa maana ya ibada kama tufanyavyo leo, bali lilikuwa kusanyiko kwa ajili ya kuumega mkate, kwa hiyo ilikuwa sherehe fupi. Haikuwa ibada ya kuhubiri/ kufundishana/kunena neno la Mungu. Sijui kwake neno ibada lina maana gani kuumega mkate siyo ibada.

  Mfumo wa ibada za kanisa la kwanza ukisoma utakuta walikuwa wanakutanika kufundishana, kuomba, kuumega mkate, au vyote kwa pamoja kama ambavyo Paul alifanya hapa. Walimega mkate na wakafundishana mpaka kukacha.

  Tumshikeni kristo, tusing’ang’ane na mambo ambayo kimsingi Mungu hayumo kwayo.

 2. Nene,

  Umejianda kukisimamia ulichokisema au umeona tu huna cha kufanya ukaamua kuongea?

 3. Watu
  Wengi wanajidai ni wakorofi wa dini, na hata ukorofi wenyewe, hawauwezi!! Kupambana na Mungu hawataweza. Wanahangaika tu. Kama kweli wao ni vidume ngoja tuone Mungu atawaangamiza siku ya mwisho. Wengine kwa akili finyu na mitazamo ya kijahidina,wameitafsiri Mdo 20:7 kutetea uasi wao huo wa mari ya saba =sabato. Leo nataka tuiangalie kidogo hiyo sehemu;
  Inasomeka hivi;
  “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane”.-SUV
  “And upon the first day of the week, when the disciples came together to break bread, Paul preached unto them, ready to depart on the morrow; and continued his speech until midnight” -KJV.
  Biblia imetumia neno siku ya kwanza ya Juma –jumapili, kwamba wanafunzi/mitume wa Yesu (kanisa la Kristo huko Troas) walikutana kuabudu. Hebu twende polepole kulichunguza jambo hili;
  Kwanza, wapendwa, Kwa mujibu wa Biblia, siku huanza jioni na kuisha jioni ya siku inayofuata, “Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu”-Mwanzo 1:13. Jumamosi huanza ijumaa jua linapozama na kuisha jumamosi jua linapozama. Jumapili huanza jumamosi jua linapozama na kuisha jumapili jua linapozama. Sasa anaposema kuwa jumapili watu walikutana tena hadi usiku wa manane, hii ina maana kuwa, kwa mujibu wa Biblia, ilikuwa ni Jumamosi usiku katika maana ya siku za leo. Ndiyo maana katika tafsiri za kawaida kwa leo, baadhi ya matoleo ya Biblia, yametaja kabisa kuwa ilikuwa ni jumamosi jioni. Soma …
  “ On Saturday evening we gathered together for the fellowship meal. Paul spoke to the people and kept on speaking until midnight, since he was going to leave the next day” (GNT), (ERV), (GW).
  Kwa hiyo, siku hiyo haikuwa jumapili (mchana, jioni au usiku wa jumapili, ambao kwa kipindi kile, ingekuwa jumatatu). So, Mdo 20:7, huzungumzia tukio lililofanyika jumamosi jioni (mwanzo wa siku ya jumapili) na wala haikuwa jumapili mchana wala usiku wa kuamkia jumatatu.
  Pili, wale hawakukutana kufanya ibada kama vile ya kuabudu siku nzima kama wanavyofanya watu leo. Lilikuwa kusanyanyiko kwa ajili ya maandalizi ya Paulo kusafiri kesho yake. Ilikuwa ni dhifa (shehrehe fupi) ya kumuuga Paulo ambayo kwa kawaida, ilikuwa ikiambatana na ulaji wa Pasaka, -“breaking of bread”. Kwa kawaida, taratibu zilizokuwepo, ilikuwa ni kushirika vyakula pamoja na baadaye kula meza ya Bwana, leo tungesema communio, -kuumega mkate-Mdo 2:42, 46. Kuumega mkate, maana yake, ni kula pasaka. Siyo kuhubiri neno kama Lwembe anavyotukokota!! Kitendo cha kula Pasaka, kilikuwa ni jambo la kawaida (agh. baada ya chakula) kwa kila nyumba au kanisa alilokuwa akipita Paulo. Paulo “alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula” Mdo 27:35. Utaratibu wa kula pasaka, sharti huenda sanjari na neno (maelekezo kiasi), kama alivyofanya Kristo akiwa na wanafunzi wake. Kunena kwa Paulo, kulikuwa ni kuwapa maelekezo (mafundisho kidogo yanayohusu ulaji wa Pasaka) na kisha kuwapa salama za heri ili kesho yake asafiri. Hoja kuu hapo ilikuwa ni kuumega mkate na siyo kuhubiri neno usiku huo wa jumamosi kuamkia jumapili. Hasha!! Na kama wewe unabisha, jaribu kusoma Bible Commentary yoyote, ile, itakwambia ukweli wa mambo!!
  Kwa hiyo, ukitumia matedo 20:7, kuhalalisha ibada za siku ya kwanza ya juma –jumapili, elewa kuwa ulishaenda na maji. Usidanganyike kuwa eti unamwabudu Mungu katika Roho na Kweli huku uko kinyume na Kweli (biblia) yake. Ndiyo maana wasabato tuko makini kiasi kile. Soma Biblia ili uwe smart. Acha kubahatisha kijana!!

 4. Watu wabishi wanatetea dini zao…nyie wasabato ni kweli mnaitii sabato kama inavyotakiwa? na mnajua nani ni Bwana wa Sabato? Na je mnamfuata? acheni maneno maneno mliyojazwa na nabii mke Hellen ambaye alitoa nabii nyingi hazikutumia.

 5. Hakuja kutangua.
  Kwa mtazamo tuu, alieleza yote yaliyoandikwa na manabii na wengineo kuhusu yeye .
  Na yote aliyoandikiwa yalitimia.
  Mtazamo tuu.

 6. ASANTE KWA MADA YAKO.PIA NAWASHUKURU WACHANGIAJI WA MAWAZO YAO.TWAPASWA KUJIULIZA NINI MAANA YA TORATI KTK BIBLIA?TUNAPOSEMA TORATI KTK MAANDIKO MATAKATIFU TWAPASWA KUJUA KTK HATUA NNE,1TORATI AU SHERIA ZILIZOHUSU MAMBO YAHUSUO TARATIBU ZA KIIBADA KWA WAEBRANIA.2TORATI AU SHERIA ZILIZOHUSU MAMBO YA KIUTAWALA.3TORATI AU SHERIA ZILIZO HUSU MAMBO YA KIAFYA.4TORATI AU SHERIA YA KIMAADILI(AMRI KUMI)KWA HIYO YESU ANAPOSEMA KUTIMILIZA ALIKUWA ANALENGA SHERIA ZA KIIBADA ZILIZOKUWA ZIKIMLENGA YEYE.LUKA 22:20NA TUJUE KUWA TARATIBU ZOTE ZA IBADA YA WAEBRANIA ILIHUSIANA NA KUMWAGA DAM.WAEBRANIA9:22 NA KWAMBA HAKUJA KUTANGUA TORATI WALA MANABII ALIKUWA ANAMAANISHA KUWA SHERIA ZA MAADILI,SHERIA ZA KIUTAWALA NA SHERIA ZA KIAFYA HIZO ZITADUMU MILELE HADI MWISHMN WA WAKATI.NDIO MAANA UTAONA KUWA BIBLIA KTK UFUNUO 12:17NA 14:12 INASISITIZA SANA JUU YA KUTII AMRI ZA MUNGU NA YOHANA KTK 1YOHANA2:3-6;5:1-3.NA PIA UKWELI NI KUWA TORATI ASILI XAKE NI ROHONI WARUMI 7:14 KWA HIYO YESU ASINGEWEZA KUITANGUA.

 7. Looo!
  Kumbe kuna mijadala mizuri hivi halafu watu jamani mko kimya tu!!! Nitapitia mmoja baada ya mwingine ili na mimi niliyechelewa kuiona, nifaidi kidogo. Ubarikiwe sana ndg MD kwa ufafanuzi wako. Binafsi nimekuelewa.
  Ushauri,
  Kwa wanaouliza maswali mengi kama mimi, maswali yao muwe mnayaondoa kama majibu ya maswali hayo yatakuwa yanapelekwa sehemu/link nyingine, badala ya kuwa na maswali tu bila majibu yake kuonekana. Tena ikiwezekana, maswali na majibu yahamishiwe yote huko na taarifa kwa mwulizaji itolewe ili ayatafute majibu yake huko. Ni ushauri tu.
  Ubarikiwe kwa kazi ngumu sana

 8. Bwana Yesu asifiwe ndug Siyi na Lenda…maswali na majib yenu ambayo hatukuruhusu ni kuhusu Kunena kwa Lugha, hapa si mahala pake yanaingilia mada husika. Comments zenu tumezihifadhi ili kuzihamisha kwenye mada husika ya kunena kwa Lugha, hata hivyo ilishawahi kujadiliwa sana kwenye blog.

  Tafadhali fuatilia links hizi kuhusu kunena kwa Lugha na Faida za kunena kwa Lugha.

  https://strictlygospel.wordpress.com/2012/03/05/ni-lazima-kuzungumza-kwa-lugha-mpya/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2009/07/01/sababu-na-faida-za-kunena-kwa-lugha/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2012/12/24/tumetoa-wapi-hii-wakati-wa-kuombewa-ili-kunena-kwa-lugha/

  Samahani kwa usumbufu wowote uliotokea. Hata hivyo comments zenu zitaruhusiwa kwa masharti zinalenga kuujenga mwili wa Kristo.

  Barikiweni.

  –MD

 9. Shalom wapenzi.
  HAINA MAANA YA KUWA MNAYAACHA MASWALI YA WATU KWENYE BLOG HAPA ILHALI MAJIBU YA MASWALI HAYO MNAYAFUTA. KUMBUKENI KUWA KUNA MUDA UNATUMIKA KUANDAA MASWALI NA MAJIBU HAYO…
  SIDHANI KAMA NI SAHIHI KUYAFUTA TU BILA HATA YA KUTOA MWONGOZO WOWOTE. MUNGU ATUSAIDIE SOTE. AMINA

 10. Ndugu Siyi kuna maswali yako ya tarehe 29/04/2013 sikuwa nimeyajibu.

  Swali kuhusu mji unaosemwa katika Isaya 65. Nataka nikujibu kwa namna fulani ya kifupi na yenye kufikirisha ila utakuwa umelielewa jibu kwa uzuri sana.

  Unatakiwa ufikirie sana kama unaamini kuwa Isaya aliposema simba na kondoo alikuwa ana maanisha kweli mnyama simba na kondoo.

  Mimi najua katika mbingu mpya na nchi mpya inayosemwa kwenye ufunuo, kwa sababu ya kwemye ufunuo biblia inasema hakutakuwa na kifo (Ufu 21:4), lakini hii ya kwenye Isaya inasema kutakuwa na kifo (Isa 65:20)

  Halafu kumbuka makao yetu Bwana mwenyewe ndiye kaenda kutuandalia,kwa hiyo huo mji wa sisi kukaa unaosemwa katika ufunuo utashuka ukiwa tayari. Lakini katika hiyo Isaya biblia inasema tutajenga wenyewe.

  Kwa naomba na wewe Siyi sasa ujiulize ni mji gani huo uliokuwa unaongelewa, baada ya kuwa nimekuonesha kuwa siyo ile mbingu mpya na nchi mpya ambayo tunaitarajia watakatifu.

  Halafu umeniuliza suala la Yesu kushika amri za Baba yake. Kwanza unatakiwa ujue Yesu alikuwa nani kabla ya kuvaa mwili.(hiyo tafuta mwenyewe). Na kitu ambacho nimekuona unakichanganya sana kwenye mjadala huu ni Yesu kushika sabato.

  Unapaswa kujua kuwa ilikuwa ni lazima Yesu aitimize torati yote waliyopewa waebrania ndipo a-qualify kuleta agano jipya. Hivyo ilikuwa ni lazima aende kwenye sinagogi siku ya sabato, atahiriwe siku ya nane,nk. Ndiyo maana hakuzalwa kwingineko duniani, ila kule ambako Mungu alikuwa ameamuru torati itunzwe.

  Nafikiri suala zima la Yesu kumpenda Baba alianza lini unatakiwa kujua kabla hajawa Yesu alikuwa nani, ndipo utajua kama alikuwa anamwabudu Baba kabla hajawa katika mwili.

  Na jibu lake pia liko kwenye Yohana 1:1-5 Hapo mwanzo alikuwako Neno…….. Then niambie kama unaweza kumtenganisha huyo Neno na Mungu.

  Pia hukunijibu kama wasabato juwa mnanena kwa lugha mpya.
  Asante Siyi.

 11. Siyi, umesema umerusha yale mafundisho yako ya Kisabato, hayajatoka! Ninadhani sababu kubwa ni yale machati mnayotumia kuigawa Torati mafungu mafungu, watakuwa wameshindwa kuyatoa humu maana hata kwenye simu yanaparaganyika, pole saana! Sasa utafanyaje? Ninakushauri usisumbuke nayo sana maana hayo machati yenyewe hayana rejea ya Maandiko, kwani ni mafundisho mnayotumia akili zenu tu, hayana maana yoyote katika Wokovu zaidi ya kujipima kwenu kama mmeiva vizuri katika Usabato!

  Halafu jambo jingine nikuulize, hivi wewe huwaga unajifunza chochote katika michango ya wapendwa? Ninalazimika kuuliza hivyo baada ya kuona kuwa majibu yako mengi ni rejea za masomo yenu, ambavyo mara nyingi hayaendani na kinachozungumziwa katika wakati huo. Mada inaongelea Torati, lakini wewe na Lenda mmeipindisha mpaka imekuwa issue ya sabato, yaani nilichokiona kwenu ni kwamba ufahamu wenu wote wa Torati, kwenu ninyi ni hiyo Amri ya Nne, mkijisogeza saaana basi mtaishia kwenye vyakula!

  Basi niwaombe wachangiaji wengine kuwa wasiwachoke wala wasiwaone kuwa ninyi ni wabishi, hapana, ninyi mko safi kabisa, tatizo ni uelewa tu! Kwahiyo wawavumilie, waendelee kuizunguka hiyo ngome ya Yeriko wakizipuliza tarumbeta za Neno!!!

 12. Kaka Mabinza,
  Binafsi sina ubavu wa kuibishia Biblia kaka. Ila naweza kuchallenge tafsiri za aya za Biblia zisizo sahihi kwa kutoa aya za Biblia pia na siyo kubisha kubisha tu. Kama kuna mada yako nimebisha tu bila kufuata utaratibu huu, naomba usisite kuniamboia, huenda nilipitiwa tu. Si unajua kuwa na mimi ni mtu tu!! Ilete ili tena tuiangalie upya kaka.
  Barikiwa sana

 13. M. J. N. Siyi,
  Nabaki na kazi zangu hasa ninapoongea nawe ndugu yangu Siyi, na maanisha kwamba, kila nikikueleza unapinga tuuuuu, hata maandiko nayo unayabishia kha!

  Mabinza LS.

 14. Siyi kusema kweli suala la siku ya kuabudu limefafanuliwa sana huko nyuma. Isingekuwa busara kuanza kulirudia tena.

  Kuhusu suala la ujazo wa Roho mtakatifu umesema mnajazwa kama walivyojazwa mitume. Biblia inasema walikuwa wamekaa katika chumba cha juu siku ya pentecoste zikawatokea ndimi zilizogawanyika kama ndimi za moto….. wakanene kwa lugha mpya (Mdo 2: 1-4).

  Je unamaanisha kwamba na ninyi mnajazwa hivyo ndugu Siyi?
  Asante!

 15. Kaka Kabalo.
  Nakushukuru sana kwa hoja, japo umepangua hoja bila ya kutoa reference za kimaandiko kusupport hoja zako za kipi kinaanza, wokovo au kuyatenda mapenzi ya Mungu?
  Na kuhusu suala la siku, sidhani kama ni sahihi kufuata mitazamo ya watu. Ingekuwa vyema zaidi kuangalia kama kweli Biblia haisemi chochote juu ya siku ya ibada ni ipi!! Natambua kuwa, wakati wote tunatakiwa kuwa connected with Jesus. But pamoja na hayo, kuna siku (the whole day) ya ibada tu na siyo kufanya mambo yetu mengine kama ilivyo kwa siku zingine 6. Mungu ameibainisha vyema kabisa siku hiyo. Ni siku kwa ajili ya maadhimisho ya Mungu na kazi zake! Mungu aliitunza, Yesu aliitunza na hata mitume(kanisa la kwanza), liliitunza. Reference za hoja yangu hii, jaribu kuipitia michango yangu ya mwanzoni kabisa kwenye mada hii. But ukisema kuwa Yesu hakusema, sidhani kama umefanya utafiti wa kutosha na kupata hoja za kusupport mtazamo wako huo. Tungependa kujifunza na sisi.
  Na kuhusu swali lako, kuwa na sisi tunajazwa Roho Mtakatifu? Jibu lake ni rahisi sana. Ni NDIYO. Tunajazwa Roho Mtakatifu kama walivyojazwa mitume. Tunafanya matendo ya ujazo wa Roho Mtakatifu kama walivyofanya mitume. Wewe je?
  Barikiwa

 16. Siyi kuna kitu umesema, nakunukuu ”Wokovu hupatikana kwa wale tu wayatendayo mapenzi ya Mungu”. Mimi najua kuwa wokovu unaanza kwanza ndipo mtu anapate uwezo wa kutenda mapenzi ya Bwana. Labda kama hujui maana ya wokovu.

  Lakini naona pia suala la siku ya kusali limeongelewa vizuri sana huko nyuma na wachangiaji wengine. Hakuna siku ambayo Yesu kasema ndio maalum kwa watu kusali, ispokuwa wanatakiwa kusali siku zote, kwa sababu kinachoazimishwa siyo siku fulani, bali kinachoadhimishwa ni Mungu.

  Ivi wasabato mnaamini na ninyi katika ujazo wa Roho mtakatifu?

  Barikiwa.

 17. Mabinza,
  Una maana gani unaposema matoleo ya kazi zako unabaki nayo mwenyewe? Kazi zako hazijibiwi au una maana gani? Nieleweshe plz

 18. Kabalo,
  Nina tabia ya kucheka tu mtu anaponifurahisha, aidha kwa hoja zenye nguvu ama hoja nyonge. Sasa, inabidi nianze mazoea ya kutocheka ili nioneshe userious, maana kumbe wengine kicheko changu wanakitafsiri vibaya. Sasa twende kwenye hoja zako.
  Nikubaliane na wewe kuwa, Msabato anaweza kuishika vizuri sana sabato na kuzingatia aina ya vyakula kwa mujibu wa Biblia na bado akawa si mkamilifu. Na hasa atakapoamua kuyashika yote hayo kwa nguvu zake mwenyewe. Kupwaya ni kwingi sana kaka. Hii ni kweli kabisa. Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Kwa nini nakubaliana na wewe?
  1. Kushika sabato tu, ukavunja sheria zingine 9, ni kukosa juu ya yote. Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
  Sheria hizi ni sehemu ya NENO la MUNGU kaka Kabalo. Sasa jaribu kuangalia na wewe kwa kutunza j2, unasalimika kweli kwa hizo zingine 9? Sisi tunajitahidi kumwomba MUNGU atuwezeshe kuziishi amri zote 10. Sisi wenyewe hatuna uwezo huo wa kuziishi. Ndiyo maana tunaomba msaada kutoka kwa Yesu ili tuyaweze yote katika YEYE anayetutia nguvu. Kwa msabato aliyejazwa Roho Mtakatifu, pendo lake kwa Kristo limekamilika, kushika amri 10, hatumii nguvu hata kidogo, bali ni matokeo ya matendo ya upendo wake kwa Kristo. Kinachoanza, ni upendo, ndipo kushika amri huja kama matokeo ya upendo huo. Yohana 14:15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Yohana 14:21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
  Hivyo kaka, Roho Mtakatifu anapokuwezesha ktk haya yote, dhambi kwako haitatajwa tena. Na huo ndio ukamilifu ktk Kristo ambao kila mtu anautafuta. Ukisema kuwa wanaosali j2 hawajakosea, binafsi sikubishii, ila nitakuomba unifundishe imeandikwa wapi ndani ya biblia kuwa watu wanapaswa kusali j2?
  2. Kuhusu vyakula, sisi kaka hatuli kitu kisicho chakula. Kwa maneno mengine, kuna vitu alivyoviita Mungu vyakula kwa mwanadamu, hivyo ndivyo tunavyokula sisi. Vile ambavyo Biblia haijaviita kuwa ni vyakula, kwa nini sisi viumbe vyake(wanadamu), tuviite vyakula? Ina maana sisi tuna akili sana kuliko Mungu? Ndani ya Biblia, binafsi, sijapata aya yoyote inayoruhusu watu kula vitu visivyo vyakula, ila inatoa maonyo makali sana kwa watu wanaokula vitu visivyo vyakula. Isaya 66:17 Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana. Isaya 65: 2 Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe; 3 watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali; 4 waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao; 5 watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa.
  Zingatia mstari wa nne. Sasa kaka Kabalo, kama Biblia imesema tusijihalalishie vyakula, sisi tu nani hadi tuibadilishe ili kukidhi matamanio/haja zetu? Labda kama wewe una aya yoyote inayoruhusu watu kula kitu kisicho chakula kwa mujibu wa Biblia, nionyeshe na mimi nipate kujifunza, maana mimi ni mwanafunzi wa Biblia tu.
  Hivyo kaka, kuitwa msabato tu peke yake, na kutokula nguruwe, eti ukajihesabia haki, Biblia imekataa kata kata. Wokovu hupatikana kwa wale tu wayatendayo mapenzi ya Mungu. Na mapenzi ya Mungu, hayatendwi na mtu yoyote tu bali ni mpaka yule azishikaye amri/sheria za Mungu. Zaburi 40:8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
  Hili ndilo NENO la Bwana kaka.
  Barikiwa sana

 19. Mabinza mfano wako uko ‘so relevant’ kwa yeye asomaye na kufahamu.

  Lakini Siyi kamaliza kuusoma kisha akacheka, na akakwambia kuwa yeye haumhusu ila unakuhusu wewe. Tena kacheka kabisa kwa kuonesha kuwa yeye yuko sahihi 100% na mfumo wa imani anaouamini na kuuishi.

  Lakini kwake (Siyi) ningependa kumwambia kitu kimoja kwamba tukiachana na masuala ya sabato na vyakula ambayo tumeyaongea sana tukaamua pia kuangalia kweli zingine zinazomhusu mkristo, yako mambo tunayopaswa kuyaona pia.

  Siyi suala na sabato na vyakula hata kama yangekuwa ya muhimu kuyashika na mtu akayashika na kuyatenda,kuna uwezekano mkubwa wa mtu huyo kuyaweza hayo lakini bado akakosa quality za ndani za mkristo.

  Quality hizo ni kama usafi wa moyo, nguvu za Roho mtakatifu, ushindi dhidi ya dhambi, nk.

  Siyi ningependa kukwambia kuwa kama wewe na wasabato wengine mnazo hizi quality katika maisha yenu, believe me’ kusali kwenu J’mosi na kutokula vitu fulani hakuwapunguzii wala kuwaongezea sifa yoyote ya ninyi kumwona Mungu baada ya maisha haya.

  Lakini kama wasabato hamna hizo quality; yaani hamna usafi wa moyo (purity of heart), hamna nguvu za Roho mtakatifu, hamshindi dhambi nk, ukweli ni kwamba kusali kwenu J’mosi na kutokula vyakula fulani hakutawasaidia baada ya maisha haya.

  Kusali kwenu J’mos si kitu kinachowapunguzia wala kuwaongezea kitu chochote machoni pa kristo, kwa hiyo nanyi mtahukumiwa kwa mujibu wa hicho mnachokiamini na kukifanyia mapatano.

  Lakini msidhani kuwa wanaomwamini kristo bt hawasali J’mos ati wamekosea njia, never, hawajakosea.

 20. M. J. N. Siyi,

  Mpendwa wewe niandikie tu, mimi hupenda kujua vitu vingi, shida yangu Neno niwe nalo kwa wingi. Na usidhani kuwa napuuza hoja zako, zote nazifanyia kazi, ila tu kibaya ni kwamba, matoleo ya kazi niifabyayo nabakia nayo mwenyewe!

  Mabinza L.S

 21. Ha ha haaa!! Nahisi mada hii inakuhusu wewe wmenyewe kaka Mabinza. Unajaribu tu kuwashawishi na wengine kufuata maazo yako. Majibu niliyoyatoa kwenye hoja yako kabla ya hii, yangetosha kuumaliza mjadala huu. Mshukuru …… maana hayaruhusiwi hapa. Nimekuwa nikiyarusha tangu april 2 hadi leo bila mafanikio. Aidha, kwa sababu, nina email yako, nitakurushia wewe mwenyewe. Shida ni kwa wengine. sijui itakuwaje.

 22. @ Mkandya,
  Wapo wanaojua kuwa wanajua kumbe hawajui, hao achana nao!
  Fikilia upo Posta ya zamani Stand, pale Dar es salaam, mpo wengi mkingojea usafiri kila mtu aende anakokwenda. Wewe unakoenda usafiri unakuwa wa shida kidogo, lakini karibu na wewe kuna jamaa ana Begi kubwa na vifurushi vingine vidogovidogo vitatu au vinne hivi, ana kifurushi cha kama Debe mbili hivi cha mchele katika Kiroba, pamoja naye ameambatana na watoto wawili cha kike ndicho kikubwa kina kama miaka saba hivi na kidogo ni kivulana nacho kina kama miaka mitano hivi.

  Unashikwa udadisi uliochangamana na Huruma ya Kristo, unamsogelea Mtu yule na kumsalimia na unavisalimia pia vile vitoto navyo vinakujibu kwa furaha. Kisha kwa kuona kama watoto wale wamechoka kwa safari, unawachukulia “Azam embe” mbili na kuwagawia moja moja huku ukichekacheka kilokole. Watoto wale, nao kwa pupa wana pokea na kuanza Kunywa kwa Furaha, unawatazama watoto wale, moyoni unamshukuru Mungu kwa wewe kuwa pale kwa wakati ule!

  Unaanza kwa kumuuliza yule Mtu ambaye anaonekana kama Mgeni Jijini hapo, na mwenye kuonekana akitoka Safari huenda Mkoani nje sana ya Dar es salaam yenu (ni mfano tu si maanishi kuwa wewe upo au ni mkaazi wa Dar.). Kaka samahani, wewe unaelekea wapi, naona kila Daladala lijalo hupandi na sasa ni karibu usiku? Mtu Yule kwa uchangamfu mwingi uliojaa urafiki, akacheka kidogo, akasema, Aaaaa……Mimi na watoto wangu hawa pamoja na Mizigo niliyonayo naelekea Kigamboni, nataka nipate Gari la moja kwa moja kuepusha usumbufu wa kushuka na kushusha mizigo mara kwa mara! Huku ukionyesha kuijua Dar es salaam vizuri, unamwelekeza, loo, kaka, hapana, kama ni hivyo utakesha Bro. Una muuliza, kwani lile Daraja la Magufuri ilishakamilika? Naye anakujibu, sijui, labda nikuulize wewe! Ndipo unagundua kuwa Mtu huyu ni mgeni kabisa hapa mjini; unasema, Kaka hakuna Daladala la moja kwa moja hadi Kigamboni hapa. Unachoweza kufanya ni kuchukua Daladala (Town bus) iendayo Feri, toka hapo utapanda Kivuko ambacho kitakupeleka hadi ng’ambo ya pili kisha utaenda sasa kule uendako, kama ni mji mwema haya!

  Mtu Yule anakujibu, Aaaa…Bwana wewe kama vipi nenda tu kaka, mimi si mgeni ki hivyo hapa mjini, juzi tu kulikuwa na Madaladala lukuki yakienda huko huko Kigamboni moja kwa moja, leo unaniambia hakuna usafiri kama huo?! Kaka, kapumzike nashukuru kwa kuwajari wanangu na kunipa kampani yako ambayo ambayo nimeifaidi na kiukweli si wengi wenye moyo kama wako! Unaamua kumuacha, ukiwa pale watoto wale wanakuwa wakikutazama kwa zamu kama wanakuhitaji kwa msaada fulani. Baada kama ya Nusu saa hivi, unamsogelea tena Mtu yule unamwambia huku ukichekacheka, Sasa mkubwa, unaonaje labda nikuchukulie Taxi ili katika hiyo, unaweza kuvuka nayo! Lakini moyoni umeguswa zaidi na hali ya watoto ambao kwa ujinga na ubishi wa Baba yao watateseka bure mahali pale na hasa usiku sasa unaanza kuingia. Jamaa ana kujibu kwa uchangamfu, usijari kaka, mimi hapa mwenyeji, gari itakuja tu! Wewe utafanyaje Mkandya tofauti na wazo la ya kuachana naye?!

  Kila mwenye Roho ya Kristo hupenda wote wapone, waishi kwa furaha. Wanaumizwa sana kuwaona wenzi wao wamebebeshwa mizigo na Shetani na kwa ujinga wakionyeshwa kwa vipi wataachana na adha ile, wao hujibu kuwa wanajua sana namna ya kuachana na Mizigo yao hiyo. Lakini kila ukienda unawakuta wanayo na inazidi kuongezeka, kwa kifupi Mtu kama huyo HUJUA KAMA ANAJUA, KUMBE HAJUI; huyo achana naye, usibishane na mbishi atakuponza!

 23. Lenda sasa naona umeamua kuanza kutumia hoja ya nguvu. Kama fafanuzi zote hizo ambazo tumetoa katika mjadala huu bado hujataka zikuelee, basi wewe umelishwa unga wa ndele(kama umesoma fasihi).

  Nafikiri wadau katika mjadala huu tumesema sana kuhusu torati kutanguliwa, halafu wewe wakati huu tunapoelekea kuhitimisha huu mjadala unaturudisha nyuma tena tuanze kusema yaleyale tuliyokwisha sema.

  Uliniuliza maswali nikakujibu, mbona huongelei hayo uliyoniuliza nikakujibu?

  Kuna majibu mengi mazuri sana yametolewa na akina Mhina, Mabinza, John Mtangoo, Millinga, Neema, Anthony nk. Naomba tuzingatie hayo majibu tusiendekeze ushabiki tu wa kidini.

  Nafikiri alichosema Anthony ni cha kweli kuwa nyie wasabato ni wabishi sana!

  Basi bwana, Mungu mwenyewe anajua jinsi atakavyowasaidia maana aliwafia na ninyi pia.

  Barikiwa.

 24. Ndg zangu Siyi na Lenda, itawachukua eternity ili kujua maana ya “Habari Njema”; yaani mnaweza fika Hukumuni na mkaendelea kubishana na Hakimu kuhusu jambo hilo!

  Habari zinakuwa Njema hapo zinapozifunika Habari Mbaya! Torati ni habari mbaya inayofungamana na Laana. Hakuna hata mtu mmoja aliyefaulu kwa Torati. Inasikitisha sana mnavyojidanganya kuhusu Torati. Mnajaribu kuifanya kana kwamba si kitu cha kutisha kwamba eti mnaiweza, huku mkiigawa mafungu ili mbaki na Sabato ya Kiyahudi, halafu hiyo ndiyo muishikie bango! Mmeambiwa hakuna hata “yodi” moja itakayoondoka, ukiiondoa hata koma, inakuwa siyo Torati! Amri 10 ni sehemu ya Torati, basi mnapaswa mvitimize vipengele vyote 613, vinginevyo mnakuwa ni wale waliolaaniwa, haijalishi mnajiongopea vipi!!!

  Siwashangai mnaponishangaa hapo ninaposema mkristo hatendi dhambi. Ninaufahamu ugumu mnaokumbana nao katika kujaribu kwenu kuyapambanua mambo haya. Maana kila kukicha mnazisikia habari za uzinzi na uasherati na uasi mwingineo kati ya makundi yenu na ya jamii nyinginezo za kikristo zinazowazunguka, hao wote ni wale wanaokiri kujazwa na kuongozwa na RM. Kujidanganya kuwa unaongozwa na RM kunawafanya kuwa sitting ducks katika mawindo ya Ibilisi! 

  Hakuna hata mtoto mmoja wa Mungu aliyejazwa RM anayetenda dhambi. Kujiongelesha kuwa umejazwa RM hakukufanyi kuwa umejazwa, inawezekana ukawa umejazwa roho wa dhehebu lako na kudanganywa kuwa huyo ndiye RM!

  Mungu hajawahi kufanya Maagano mawili kwa wakati mmoja na watu wake. Agano la Kale lilikuwa na kazi yake, ambayo ilikuwa ni kutuleta kwa Kristo. Basi hebu jaribu kuwazia jambo hili kuwa wewe ulikuwa na Torati hata ikufikishe hapo kwa Kristo? Basi hao waliotokana na Torati na kisha kuletwa kwa Kristo, ndio walio na ujuzi wa mambo hayo, hao ndio wametumwa kwetu, mitume! Hao ni Wayahudi tena ni Wafarisayo, kwahiyo unapowaona wakijikusanya na watu wao siku ya Sabato ya Kiyahudi kuyatimiza yapasayo, sioni kama kuna jambo jema linalozidi hilo. Tumeona ktk siku moja wakivuliwa Wafarisayo zaidi ya 5000 kuujia Wokovu! Chumvi ikibaki peke yake haiokoi, ni lazima kuwe na contact na kinachookolewa! Kwahiyo kuishabikia Sabato ya Kiyahudi na kuifanya ndio Sheria kwa misingi kwamba Kristo aliitimiza na mitume wake, ni ufinyu wa uelewa wa maisha ya kijamii na desturi zake. 

  Lakini kutoka jamii hiyo ya Kiyahudi, imezaliwa jamii mpya, inalo jambo jipya, ina hadithi mpya, kaburi liko wazi!! Ninawahakikishieni Siyi na Lenda, nguvu ya Torati haikufia msalabani, pale iliongezeka mara dufu, ndio maana Yuda alijinyonga baada ya kumaliza kazi yake kwa mafanikio! Sabato iliyofuata kulikuwa kumetulia kimyaaa, hakuna hata sauti ya mzushi iliyosikika. Kila mwanafunzi alikuwa anawaza jinsi ya kurudi kwenye mzunguko wake wa maisha wa zamani, akatafute kondoo wa sadaka arudi hekaluni akatengeneze mambo yake. Hiyo ndiyo hali ya ushindi wa Torati iliyotawala Sabato ile aliyokuwamo KABURINI Kristo, Kanisa nalo lilikuwa Kaburini!!! Bwana wa Sabato alikuwa Kaburini, ni nani atakayeyapokea maombi na sadaka zenu enyi Wafarisayo? Au hamjasoma kuwa Mkristo huzikwa na kufufuka na Kristo? Au hamuelewi ina maana gani? Mnasomaga tu kama gazeti au liturgia! Jumamosi, wenzenu huwa tumo makaburini, na Jumapili makundi yetu hufufuka!!! Hii ndiyo siku ambayo Torati ilifutika, yaani Kristo asingefufuka, basi ushindi usingekuwepo, wala wokovu! Hiyo ndiyo siku yetu ya Bwana sisi kundi jipya, hiyo ndiyo Sabato yetu ya kimwili na kiroho, tunakuadhimisha kufufuka kwake pamoja nasi, ilianza kwa siri na sasa ni kamili kwa Mwili wa Kristo! Mnaong’ang’ania huko nje, shauri yenu, kwanza Mungu hana ahadi yoyote na ninyi, Wayahudi watakaporejewa wataungana nasi katika Sabato hii iliyokamili wakiwaacha nyie maporini kwenu mlikojipeleka!

  Uongo wa Wakatoliki hauwezi kuubadili ukweli wa Injili. Wasabato ni sehemu ya uongo huo, wakiutukuza ili kuyashawishi makundi yaliyookolewa, yarudi katika utumwa na Laana ya Torati, wakitumia kigezo cha udhaifu wa mafundisho humo makanisani, kuwarudisha dhambini  kinyume na Injili. Hiyo ni michezo ya kuzimu, nairudia tena kauli yangu, Dhambi ya Uzinzi hailihusu Kanisa! Tafsiri yako Siyi kwamba eti, 
  “wakristo leo wako huru kutamani tu na kuwaka tamaa juu za mabinti, wake/maume za watu?? Je, huu ndio uhuru tulio nao katika Kristo wa kuwa huru kutamani wake/waume yaani kuzini?? Kwa maelelezo mengine, unasema kuwa leo hakuna dhambi tena ambazo zinaweza kutendwa na watu!! Na kama hakuna dhambi, hakuna haja ya kuwa na mwokozi.”
  Maelezo yako haya yanadhihirisha jinsi ambavyo ulivyo mbali sana na Injili! Intelectual Faith haina uwezo wa kukufanya uzaliwe mara ya pili ndg yangu, na bila kuzaliwa mara ya pili hutaelewa chochote kuhusu Injili, utabaki na madude yasiyoeleweka maisha yako yoote! Hivi kuna yeyote kati ya mitume aliyekuwa mzinzi? Au siku hizo kulikuwa hakuna wanawake? Ama kweli acha mt Paulo awashangae mlivyorogwa!

  Tambueni kwamba Hakuna Sheria juu ya Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, huyo aliyezaliwa kwa Roho wa Mungu; huyo Mkristo ndiye Sheria yenyewe!! Basi jitahidini nanyi katika utii ili mfanyike wana wa Mungu, muondokane na utumwa mliouzoea!

 25. MKANDYA
  Umesema kirohoni inakuwa usimtazame+ke kwa kumtamani. Lakini hapa unakili neno katika Warumi kuwa torati ni hai maana inasema.

  “TUSEMAJE, BASI? TORATI NI DHAMBI? HASHA! WALAKINI SINGALIITAMBUA DHAMBI ILA KWA SHERIA; KWA KUWA SINGALIIJUA KUTAMANI, KAMA TORATI ISINGALISEMA, USITAMANI? WARUMI 7:7

  (Kwa hivyo umejua kutamani ni dhambi kwa sababu ya Torati? Sasa unafikiri torati ilitanguliwa? si sahihi)
  TII INJILI NDUGU, YESU NDIYE NENO USIPOTII NENO HUJAMTII KRISTO.

 26. M. J.N. Siyi mpendwa,
  Usihofu kabisa, sikwaziki kirahisi hivyo, naijua tabia ya ‘Dibeiti’ vizuri sana kiasi kwamba simuchukii au kumuogopa ‘Opoza’. Uwe huru sana tu, hii ni kazi ya Mungu si yangu, nikwazike kwa lipi? Kama kuna umhimu atakwazika mwenye kazi yake, si mimi!

  Nimekusoma ndugu yangu, nimekupata kuwa unadhani kuwa Sabato ni SIKU, na pia unafikiri Sabato ni MOJA tu! hasa unaposoma “…ikumbuke siku ya sabato uitakase…” Sabato ni ISHARA, unapoitekeleza unaadhimisha ishara. Umesema mimi ni Muongo! Hebu ona, ulivyosema nanukuu,
  “Ukisema kuwa sabato ni starehe ya kila siku HUO NAO NI UONGO TENA UONGO MWEKUNDU” mwisho wa kunukuu.
  Hebu ona, Mungu hapa anaainisha sababu ya kuileta sabato, anasema “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ISHARA kati ya mimi na wao, WAPATE KUJUA yakuwa MIMI NI BWANA, NDIMI NI WATAKASAYE Eze. 20:12”.
  Angalia, Neno linasema, Sabato ni Starehe (Pumziko) Kut. 20:10. Biblia inaelekeza kwamba Sabato ni siku ya ‘Mema’wala hupaswi kuwa mtu wa njaa njaa siku hiyo, Mrk.2:24-26, Mt.12:1-5. Mimi nadhani kuniita muongo ulikuwa umesahau, pengine ulimaanisha kuwa Mungu ndiye muongo maana, Neno hili sijasema mimi; Aliyesema hayo ni Yesu na ndiye mwenye hiyo Sabato Mt.12:8. Labda usema Mungu ndiye muongo, au unaogopa, ukaona unisingizie mimi? Hebu niambie, maandiko yanasemaje, sisi watoto wa Mungu tuishi kwa furaha na kwa starehe au tupumzike na shida za Dunia kwa siku moja tu katika wiki? Kama sivyo, hiyo sabato ipo ili tuihudumie sisi au yenyewe ndiyo ipo ili kutuhudumia sisi? (Yaani iliwekwa kwa ajili ya nani?)

  Kwakuwa mambo yote naona ni kama umeyarudia yaleyale tu. Maelezo yako karibu yote yamejaribu kuonyesha umhimu wa kwenda kusali jumamosi, Jambo ambalo si la msingi wa kuja kwa sabato! Kinachotakiwa nikuliangalia Neno lituambie hasa Sabato ipo kwa nini, inapaswa kutekelezwa lini na kwa namna gani! Biblia inasema kuwa Sabato haikuletwa kwa ajili hiyo tu. Labda nilisemee na hili uliosema mkanganyiko, eti nimekuongopea! Umesema nanukuu,
  “Ukisema kuwa Sabato ni Starehe ya moyoni tu ambayo haipaswi kuoneshwa kwa matendo huo ni UONGO MKUBWA SANA KAKA”
  Umepata wapi maneno hayo ndugu yangu? Hebu ipitie upya hiyo ‘komenti’ yangu uone kama nilisema kwa kumaanisha hivyo!
  Mpendwa Siyi, wewe huwa unaelewaje maneno ya Mungu lakini? Hebu ona ulivyosema, nanukuu “ Hivi kama Mungu mwenyewe, Yesu, na hata mitume wake, hawakuziita siku zote sabato wala hawakujichagulia siku ya kuabudu, wewe u nani hadi ufikie hatua hiyo? Ooohhhh!! Neno la Mungu litabaki palepale, TII uishi, ASI ufe, fullstop!” mwisho wa kunukuu.

  Kushikilia mapokeo ni upofu na ni pingu ya ufahamu ‘Enyi Wagalatia ni nani aliyewaloga?’ Kwani, Jumamosi kama siku ya saba katka wiki ndiyo inayoitwa Sabato? Ndugu, ukiwa porini mara ghafla ukaona jua linatokea Magharibi, jua kuwa tayari umepotea! Tafuta mti wenye kivuli ukae chini utulie hadi akili ikukae sawa, ukifosi utajikuta upo Tegeta wakati safari yako ni ya Mbagara! Sabato siyo SIKU (yaani siyo jina la siku kama vile, jumatatu, jumanne, jumatano……), bali ni TENDO lililotendwa na Mungu kwa mara ya kwanza katika ile siku ya Saba, alipomaliza kazi ya uumbaji. Siku hiyo ni ambayo leo kwa sababu nisizozijua inajulikana kama jumamosi! Tendo hilo liliitwa “Pumziko au starehe” tendo linalofanywa na mtu baada ya kazi. Kwa hiyo ukikaa tu bila ama kabla ya kufanya kazi huwezi kuita unapumzika! Kwa hiyo, kupumzika huko ndiko kunakoitwa Sabato, lakini elewa kwamba Pumziko hilo liitwalo Sabato, si pumziko la kama mkulima, mfugaji, mfanyakazi serikalini, mjasilia mali au mvuvi wa samaki ni pumziko la MUNGU. Sisi tunalishiriki kwa sababu ni WATOTO wa Mungu! Mpendwa, inawezekana kabisa nikawa nakuchanganya zaidi, iko sababu, unajua, Mtu asiye Msukuma hawezi kujua mila za kisukuma! Kwa hiyo kung’ang’ania kuwa Sabato ni siku ni kuona jua linatokea Magharibi badala ya Mashariki, yakupasa ukae chini katika kivuli hadi akili ikae sawa. Bila hivyo utajikuta upo Tegeta badala ya kuwa Mbagara! Pasaka njema.
  Mabinza L.S.

 27. Mungu awabariki Mkandya na John Mtangoo.. Wasabato ni wabishi sana na wanadhani wanajua bibilia kuliko wengine. Roho Mtakatifu aseme nao kupitia maoni ya wachangiaji walio na Roho wa Mungu wa kweli

 28. Kwanza lazima nikiri kwamba nilipoingia kwenye mjadala huu sikujua utajikita katika sabato. kuhusu Mungu Yesu Kristo kuja na kuitangua torati msimamo wangu utabaki pale pale kwamba TORATI UKAMILIFU WAKE NI UPENDO. Jamani mistarii hii maarufu kweli tunajifanya hatuijui? kwamba “SIKU ZINAKUJA AMBAZO WAMWABUDUO MUNGU HALISI WATAMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI! Hivi Jumamosi ni ya kiroho au ya kimwili? Maneno haya “MTU ASIWAHUKUMU JUU YA VYAKULA, MWANAMO WA MWEZI, SABATO n.k (siwawekei mistari maana najua mnaijua lakini mnajifanya makauzu!)
  Kitu ninachokiona hapa kuna watu WAMESHIKILIA DINI ZAO kuliko kumshika MUNGU! kumbuka jamani “DINI ILIYOSAFI NI KUWAJALI YATIMA NA WAJANE! mara ngapi unakuta mtu anamsimamo wa dini yake lakini maisha hayampi Mungu utukufu? kusali jumamosi na huku hujali kama jirani yako amekula au ana njaa ni kazi bure! kusali jumamosi huku umeajiri watu halafu unawalipa msahahara mdogo usiotosheleza mahitaji yao ni unyonyaji! kusali jumamosi huku unazini ni upuuzi mtupu! KUSALI JUMAMOSI HUKU HUTIMILIZI UPENDO WA MUNGU KWA WATU NI UBATILI MTUPU NA KUJILISHA UPEPO!
  sasa hapa naomba nilete swali.
  “KAMA MUNGU ALIPUMZIKA, MUNGU AKIPUMZIKA HUWA ANAFANYA NINI! ANALALA? ANAKULA? ANAENDA KUSTAREHE? STAREHE YA MUNGU NI NINI? HIVI MUNGU HUWA ANAPUMZIKA KWELI? HIVI MUNGU AKIPUMZIKA TUTAKUWA SALAMA?
  Maandiko yananithibitishia kwamba Mungu huwa hapumziki. jicho lake liko kila mahali likiwaangalia wabaya na wema. TORATI INAYODUMU MILELE NI KUMPENDA MUNGU KWA MOYO WOTE, NA JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
  Mungu anataka ibada ya kweli na siyo ibada ya siku. Mungu kwake hana jumamosi wala jumapili. Na chakula kinachoishia chooni hakimkwazi bali unajisi unaokaa ndani ya moyo ndio utakao hukumiwa.

 29. Bwana wa pumziko anakuwa amefanya makao ndani yako, wala hayuko hekaluni au milimani tena ambako walilazimika kwenda kumwabudu.

  Siyi hebu fikiria; Baba na Mwana wako ndani yako, unayemfuata kwenda kumwabudia hekaluni ni nani wakati tayari uko nae ndani yako siku zote,na keshakupa pumziko la milele?

  Na akisha kukupumzisha kwa kule kmwamini na kumpokea kinachobaki ni kuendelea kumwabudu muda wote,siku zote,milele,wala si kusubiri J’mos.

  Siyi kwan sasa hivi Mungu huwa hafanyi kazi J’mos? Tafakari

 30. Kwamba ili utimize sheria ya usizini mwilini, unatakiwa usilale na mwanamke. Lakini rohoni ili uitimize unatakiwa usimtazame +ke kwa kumtamani. kwa hiyo wa mwilini wao hutazama tu na kutamani haina shida.

  Usiibe; katika mwili ni mpaka uchukue hicho kitu, rohoni ukishania tu kuchukua umeshakuwa kwenye hatia tayari.

  Kwa sabato; ktk mwili kuitimiza lazima usiende kazini kimwili J’mos, lakini rohoni ni kumwamini na kumpokea Yesu, tangu siku hiyo hata milele unakuwa umepumzika, maana yeye mwenyewe bw

 31. Siyi hujasema chochote lakini kuhusu majibu yangu kwa maswali ya Lenda ya juzi.

  Kwa hili la sasa kumbuka nilikuwa namjibu Lenda, na kasema mwenyewe kwa sawali kuwa kwa nini tunaadhimisha J2 badala ya J’mosi? ndo nimemwambia mimi siadhimishi siku.
  Na pia ungekuwa umejibu swali la ndg Mhina kuhusu sabato ya kimila ingekuwa vema sana maana nami nalihitaji hilo jibu. Tusiwe tunaacha vipolo.

  Kuhusu kutimiza sheria rohoni na mwilini ni rahisi sana jibu lake.
  Kwa mfano sheria ya kuzini kimwili…

 32. Ooooh, ndg Lenda,
  Samahani kwa kuchelwa kujibu pachiko lako. Na kuna mapachiko yangu mengi nimeyaandika kwa wajoli wa Bwana, sikujua kama na wewe umerusha pachiko makini kama hili. Anyway, kile nilichokisema huko, rejea yake itakuwa ni PACHIKO LAKO HILI ZURI. Huo ndio ukweli usiopendwa na watu wengi ndg yangu. Bwana akubariki sana sana.
  Sasa niende kwenye hoja zako. Mimi nitajibu kidogo tu maana najua wajoli wa Bwana wengine uliowataja watakushushia nondo nzuri tu. But, Haya nitakayoyasema mimi na wengine, yahakiki kama yako sanjari/sambamba na NENO la Mungu.
  Umeuliza kuwa huelewi kuhusu, warumi 7:12, WAGALATIA 3:24. Paulo alipozungumzia hiyo TORATI, nijuavyo mimi haikumaanisha AMRI ZA MAADILI. Paulo alijua kabisa kuwa sheria za Maadili hazibadiliki milele. Ni tabia ya Mungu ile. Alichokuwa anakirejelea hapo ni sheria ambazo zilikuwa ni kivuli cha Kristo mwenyewe-yaani sheria za maagizo/kafara. Nyaraka za Paulo zimeandikwa kwa hekima kubwa sana na watu wavivu, wasiyo na hekima ya kuyasoma maandiko hayo, na huyapotosha kwa upotovu wa mioyo yao wenyewe. 2 Petro 3:16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
  Na kwenye ile hoja ya mkutano wa Vatican II, binafsi, sijui kama na wasabato nao walikuwepo kwenye huo mkutano wa kumwidhinisha Papa awe msemaji wa Wakristo duniani. Nijuacho ni hiki, Papa ni msemaji wa makanisa yoooote ya j2 isipokuwa kanisa la wasabato. Makanisa ya jumapili, hawana la kufanya juu ya hili, majuzi tu, Kadinali Pengo alikuwa Kwa Papa aliyepita. Na kama hajaenda tena kwa huyu mpya wa sasa, najua atakuwa mbioni tu kwenda kuhiji tena. Wasabato ndiye adui mkubwa wa Mpinga Kristo-Yaani mfumo wa Rumi-Upapa. Makanisa ya j2 ndiyo hasa watoto wa MAMA-Rumi-Upapa japo watabisha weee!! Rumi ilianzisha ibada za jua, na wao wakafuata bila kuhoji, Rumi ikaanzisha Krismas, watoto hawa bila hiana wakasogea kushiriki, Rumi ikaanzisha, Easther ambayo haipo Kibiblia, Leo wanaiita mara nyingine Pasaka, Watoto wa MAMA hawa wapo katikati. Rumi akaanzisha umoja wa madhehbu, watoto hawakubaki nyuma wakafuata, tangu mwanzo Rumi alizikanyaga sheria za Mungu, na wao pia wakajumuika kwa kigezo cha kuwa rohoni. Akaanzisha ibada za wafu, eti watu hawafi, maana anafundisha kuwa Mama wa Yesu yuko mbinguni na hakufa-uongo mkubwa. Na Waumini wengi wanafahamu hivyo ndiyo maana huwa wanaomba kwa mama maria wakifikri kuwa mama maria yuko mbinguni… kumbe ni uongo tu. Ni uongo kwa sababu, kaburi la mama wa Yesu liko hapo Israel hadi leo na watu huenda kuhiji hapo. Sasa kama mtu kaburi lake liko Israel na yeye yuko mbinguni, kama siyo uongo ni nini hiki? Na watu wengi hawajui. Wanakokotwa tu. Rumi kaanza yeye kutetea ndoa za jinsia moja, watoto wake nao wakafuata tu. Mama akaanzisha mapambo ya mwilini kwa wanaume na wanawake, watoto nao wakafuata tu bila kuhoji, wakijifariji kuwa Mungu anaangalia ndani na siyo nje – wakasahau kuwa kilichoko nje, ni matokeo ya kile kilichomo ndani ya moyo wa mtu. Taabu kweli.
  Yaani kwa mtindo huu, sijui shetani anatupeleka wapi- Motoni eeee!! Kweli.
  Mimi naomba niachie hapa.. Wengine watakuja kukusheheni vizuri ndg yangu Lenda. Barikiwa sana.

 33. Mabinza,
  Maelezo yako mtu akiyasoma kwa ulewa wa elimu dunia, unaonekana kama umeandika hekima sana, lakini mtu akiyasoma katika ulimwengu ra roho ni deceptions+truth kaka. Samahani sana kama nitakukwaza, lakini ngoja nikuoneshe kuwa ni deceptions zilizochanganywa na kweli, ambazo jawabu lake ni deceptions tu. Zero result!!
  Umekiri wewe mwenyewe kuwa, SABATO NI MOJAWAPO YA SHERIA ZA MUNGU, ambazo kwa hakika zote zinapaswa kutiiwa kuanzia kwenye bottom ya moyo wa mtu-yaani rohoni. Na sheria inapotiiwa kuanzia rohoni, matokeo yake hujidhihirisha kwa matendo ya mwili. Mpaka hapa unabisha kaka Mabinza? Kwa kuzitii kuanzia rohoni, tutakuona hautendi mabaya hasa kama unamjua Mungu! Kwa nini? Utii umeanza ndani ya roho(mioyo) wako ndiyo maana hatukuoni kuzini, kuiba, kuua, nk. Na huu ndio ukamilifu wa imani, naam utimilifu wa sheria. Yakobo 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

  Sasa ukisema kuwa sabato nayo ni lazima ianze kutiiwa kutoka ndani ya moyo, kwa mantiki ya Biblia utakuwa sahihi. Mkanganyiko uliotupa ni kuitii tu moyoni halafu hauioneshi kwa matendo ya kupumzika STAREHE. Starehe kwa maana ya sabato ni PUMZIKO la kiroho, kimwili, kiakili na hata kisaikolojia. Ukisema kuwa Sabato ni Starehe ya moyoni tu ambayo haipaswi kuoneshwa kwa matendo huo ni UONGO MKUBWA SANA KAKA. Ukisema kuwa sabato ni starehe ya kila siku HUO NAO NI UONGO TENA UONGO MWEKUNDU. Kama unavyozitii sheria zingine kuanzia rohoni na kisha ukazidhihirisha kwa matendo ya mwili, vivyo hivyo unapaswa kuitii na sabato na kuidhihirisha kwa amtendo ya mwili pia –kwenda siku ya sabato kupumzika kimwili, kiroho, kiakili na hata kisaikolojia.
  Sheria ya sabato shetani anaijua vizuri sana umuhimu wake ndiyo maana watu wengi amewafunika wasiitambue na kujiona wako sahihi tu wanapoivunja sabato kwa kisingizio kuwa wao wako rohoni zaidi. This is Fatal teachings!! Hivi kuwa rohoni ni kuwa above the law of God?? Kwa maneno mengine, kuwa rohoni, ni kuwa na mamlaka ya kujichagulia siku ya kustere kama sabato ama kuziita siku zote sabato?? Hivi kama Mungu mwenyewe, Yesu, na hata mitume wake, hawakuziita siku zote sabato wala hawakujichagulia siku ya kuabudu, wewe u nani hadi ufikie hatua hiyo? Ooohhhh!! Neno la Mungu litabaki palepale, TII uishi, ASI ufe, fullstop!
  Ukiwaambia watu kuwa mambo ya rohoni ni kama mambo ya watoto, nayo hii ni deception!! Fatal teaching!! Si fundisho la Biblia kwamba mtu anayeko rohoni huwa ana luksa ya kuvunja sheria za Mungu. Mafundisho yako kaka Mabinza ya kuwa rohoni hadi unakosa conscious ni deceptions!!
  Yesu alikuja kuunganisha moyo na mwili katika suala zima la utii wa sheria kuliko ilivyokuwa hapo awali. Yesu alikuja kuufanya utii wetu wa sheria uanzie mioyoni(rohoni), then utii huo udhihirishwe kwa amtendo ya mwili. Kama ni kutozini, hofu ya kutozini inapaswa ianzie moyoni kaka na siyo sisi kutokukuona unazini tu kwa macho ya kibinadamu. Kama moyoni hautii sheria hiyo ya usizini, yaani hata usipoonekana kwa macho yetu kufanya hivyo, bado mbele za Mungu hauna tofauti na yule aliyezini kimwili kabisa. Kadhalika, usipoitii sheria ya sabato kuanzia moyoni, na siku ya sabato ukaja kusali kanisani-(kudhihirisha kimwili kile kilichomo ndani ya moyo wako), bado utakuwa ni mvunja sheria tu mbele za Mungu. Na mbaya zaidi pale utakapoamua kujichagulia siku yako mwenyewe eti ukadhani nayo ni STAREHE TAKATIFU kwa BWANA, hapo napo hautakuwa tofauti na mwabudu sanamu.
  Tuacheni masihara tunapojadili NENO la Mungu.
  Barikiwa

 34. Oohh, kaka Mkandya,
  Mimi ngoja nijibu hoja yako ya siku ile kuwa mbingu na nchi unazozijua wewe, hakutakuwa na mchana wala usiku na hivyo kukufanya urefute hoja yangu ya sabato hadi sabato na mwezi hadi mwezi ambazo mbinguni tutamwabudu Mungu.
  Kwa kujibu hoja yako hii, napenda nikuulize swali la tafakari. Je, unaweza kuniambia kwa kurejea majibu yako kwa ndg Lenda, ule mji atakaojenga Bwana(isaya 65-66), mji ambao Simba na mwanakondoo watalisha pamoja, watu watajenga na hatakaa mtu mwimgine, mji ambao watu watamwabudu Mungu sabato hadi sabato nk ulikuwa ni mji gani katika historia ya Biblia kwa taifa la Israel? Hebu nifundishe na mimi kaka nipate mambo mapya kwa vile sote tunajifunza.
  Na kuhusu jibu kuhusu suala la Sabato ulilompa ndg Lenda, mimi sitaki kulipinga wala kulikubali jibu lako. Nakubaliana na wewe kwenye kipengele hiki kwamba, Biblia zenye tafsiri makini kama KJV, baadhi ya sehemu zimetumia neno REST kumaanisha SABATO. Hiyo ni kweli kabisa. Na kama unakumbuka, tangu mwanzo wa mjadala huu, nilitoa maana ya sabato, nikasema kuwa ni PUMZIKO. Hivyo hakuna shida ninapoona reverse hiyo ikitumika ndani ya Biblia. Sasa naomba unibainishie mtanzuko huu; katika luka 4: 16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
  Yesu inaonekana kuwa alikuwa na desturi ya kuabudu siku ya sabato tangu mwanzo. Je, desturi hiyo aliianzia hapa duniani pindi alipokuja kumkomboa mwanadamu au alikuwa nayo tangu hapo mwanzo? Na katika kitabu cha Luka 18:20, Na yohana 15: 9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
  Nikihusisha na kauli ya Mungu Baba, bado nabaki na maswali mengi sana juu ya majibu yako kaka Mkandya. Mungu alipokuwa akitoa kauli mbalimbali za “HUYU NDIYE MWANANGU MPENDWA NIPENDEZWAYE NAYE, MSIKIENI YEYE”.. Naomba mjibu kwa haya; Je, unajua Yesu alianza kumpenda Babaye tangu lini kaka Mkandya? Je, ni tangu zamani au ni baada ya Yesu kuvaa mwili wa kibinadamu? Na ni amri gani hizo (za Babaye) alizozishika Yesu hadi akapendwa na Babaye kiasi cha kumfanya hata BABAYE kulithibitisha hilo kwa kinywa chake mwenyewe mbele za binadamu? Naomba kujifunza kwako katika hayo pia!
  Ni kweli yawezekana kuwa unaijua vizuri misingi ya mafundisho ya wa wasabato, ambayo msingi wake mkuu ni Biblia. Sikubishii. Na katika mjadala huu, utaonekana kama hubahatishi kweli au unatudanganya tu, kumbe ni mbahatishaji mkubwa!! Umeniuliza kuwa habari za Roho Mtakatifu kuwa tunajazwa/tunaamini ama la! Jibu fupi sana ni hili; WASABATO TUNAJAZWA NA ROHO MTAKATIFU NA TUNAAMINI SANA JUU YA ROHO MTAKATIFU NA KARAMA ZAKE ZOTE.
  Nafikiri swali lako nimelitendea haki. Twende kazi kwa maana ya kusonga mbele…
  Asante!

 35. Mimi nitakuomba unieleze utimizaji rohoni na mwilini wa sheria zingine tisa kama unavyodai kaka Mkandya then uhusianishe na utimizaji wa sabato. Wengi ambao huwa hawaelewi, hufikiri kama unavyofikiri kaka Mkandya, kuwa wasabato tunaadhimisha siku. Jambo ambalo ni tofauti kabisa.
  Siku hazina tofauti kaka, ila Mungu alichoifanyia siku ya Saba ni kitu tofauti na siku zingine ndiyo maana na sisi kama YEYE, mwanaye, na mitume wake wote, tunamwabudu YEYE kama alivyoagiza na si vinginevyo. Pumziko la Kiroho, eti huku unaweza kwenda kazini na then kurudi, that is not a HOLLY TOTAL REST. Unachojaribu kujidai hapa, ni kumlazimisha Mungu akubaliane na matakwa yako. Kumbuka kunijibu hilo swali la kwanza hapo juu.

 36. Ooh, Siyi ndugu yangu niwie radhi,nimekuzoe sana tatizo.

  Badala ya kumwadress Lenda nimekuadress wewe. Nilikuwa namwambia Lenda kuwa yuko ‘out of context.

  So Lenda kitu kingine ambacho waadventist mmekosea ni kutumia muda wenu mwingi kutaftiliza makosa ya wengine, hasa wa-Catholic. Kwa hiyo mnajikuta mnajikuta mnajifunza zaidi kile ambacho ninyi mnaamini ni kazi ya shetani(utendaji wa kanisa katoliki) kuliko mnavyouelewa utendaji wa Mungu.

  Mjifunzeni Kristo zaidi kuliko adui!!

 37. Nitaenda ibadani kwa sababu ‘a day has got nothing to do with the rest of Christ’. Hii ni kwa sababu pumziko la Yesu ni la rohoni na siku ni ya mwilini.

  Ni kweli wayahudi waliomwabudu Mungu ktk mwili sabato yao ilikuwa J’mos, bila shaka hata leo wasiomwamini(wayahudi) kristo wanaendelea nayo.

  Siyi kwani kuna amri gani nyingine unayoitimiza ktk mwili leo mbali na kushika sabato ya J’mos?

  Hebu jitoe ktk mapokeo ya akina G.White uwaze kama ‘idependent thiker’ kwa dakika chache uone tofauti.

 38. Siyi, now u are completely out of context,gone astray.
  Hata sijui usaidiweje sasa.

  Tena nimeshtushwa sana baada ya kuelewa kuwa kumbe wewe unaadhimisha siku,yaani J’mosi. Kwa hiyo unadhani na sisi tunaadhimisha siku yaani J’pili!
  Sikia Siyi,mimi siadhimishi siku yoyote ispokuwa naadhimisha lile pumziko la rohoni la milele ambalo Kristo kanipatia (wokovu).

  Kuna wakati J2 huwa naenda kazini,na nkienda ibadani huwa hatushindi huko. Hata pastor wangu akiamua ibada tufanye J3 nitaenda ibadan….i

 39. ndugu wakristu niwapendao
  SIYI
  MKANDYA
  MILINGA
  LWEMBE
  MHINA
  MAGRETH MOKIWA

  NAHOFU SANA NA NAMNA TUNAVYOCHANGANYA MANENO YA BIBLIA NA FIKRA ZETU.
  WAPENDWA MUNGU AMETUONYA HIVI:

  “MBWA HAO WANA CHOYO SANA, HAWASHIBI KAMWE; NA HAO NI WACHUNGAJI WASIOWEZA KUFAHAMU NENO;WOTE PIA WAMEGEUKA UPANDE, WAZIFUATE NJIA ZAO WENYEWE, KILA MMOJA KWA FAIDA YAKE, TOKA PANDE” ISAYA 56:11

  MI SIFURAHII MANENO MENGI ILA UHALISIA MFANO NAWAFURAHIA WAKATOLIKI KWA KUWA WAMESEMA WAO WANAWEZA KUBADILI AMRI ZA MUNGU;

  Nakili ya 1957 ya Concerts Catechism ya Wakatoliki inajibu kuwa wao ndi wamehamisha utukufu wa Jumamosi kwenda Jumapili hapo sina shida na ndugu zangu hawa naowapenda , wako wazi wanasema:

  Swali: Sabato ni siku ipi.?
  Jibu: Jumamosi ndiyo Sabato.
  Swali:Kwa nini tunaiadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi?
  Jibu: Tunaiadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa katoliki liliuhamisha utukufu toka jumamosi hadi Jumapili. (KATEKISM YA WAONGOFU YA 1957 YA WAKATOLIKI)

  HONGELENI WAKATOLIKI KWA UWAZI.

  PAPA NIKOLAS WA V ANASEMA ANA MAMLAKA YA KUBADILI TORATI?
  In 1455 Pope Nicholas V ,Decretal De Translat Episc.Cop.
  “ I have the authority of the kings of Kings. I am all in all and above all. Where fore if the things that I do be said not to be done of man,but of God, What can you make me but God?….wherefore, no marvel if it be in my Power to change Times And Times: to alter and ABROGATE LAWS, to dispense with all things, yea,with the precepts of Christ… The pope has power to change times, to abrogate laws, and to dispense with all things, even the precepts of Christ. He can pronounce sentences and Judgements and contradiction to the rights of nations, to the law of God and man..HE CAN FREE HIMSELF FROM COMMANDS OF THE APOSTLES, HE BEING THEIR SUPERIOR, AND FROM THE RULES OF THE OLD TESTAMENT”

  Kwa ufupi anasema yeye ni Yote katika Yote na Juu ya Yote, na anaweza kubadili amri na nyakati na hafungwi na mafungo ya amri za mitume na sheria za agano la kale.

  Barua moja kwa Kadinali mmoja inasema
  Chancellor Albert Smith for Cardinal of Baltimore Archdiocese, letter dated February 10, 1920:
  “If Protestants would follow the Bible, they should worship God on the Sabbath day by God is Saturday. In keeping the Sunday, they are following a law of the Catholic Church.”

  “The pope can modify devine law” Prompta Biblio theca,’ “Papa,”art.2
  Yaani ;Papa anaweza kurekebisha/kuboresha amri za kimbingu

  NIKASOMA KAMUSI YA KISWAHILI YA OXFORD IKANIAMBIA
  Sabato nm (kd) siku ya Jumamosi ya Kumuabudu Mungu kama itumikavyo na Biblia.

  lakini magungu haya yakanichanganya zaidi

  “BASI TORATI NI TAKATIFU, NA ILE AMRI NI TAKATIFU, NA YA HAKI, NA NJEMA.” (WARUMI 7:12)

  “HIVYO TORATI IMEKUWA KIONGOZI KUTULETA KWA KRISTO, ILI TUHESABIWE HAKI KWA IMANI” (WAGALATIA 3:24)

  YOTE HAYA MANENO YANANIFANYA NIWAONE WENGINE NI MAKUSUDI YAO ILA WATUMISHI SIJAJUA MSIMAMO WA WAUMINI WA KIZAZI HIKI CHETU CHA MUUNGANO WA MAKANISA TUKIZINGATIA TULIKUBALI KATIKA MKUTANO WA VATIKANI II PAPA AWE MSEMAJI WA MAKANISA YA KIKRISTU DUNIANI..HUYU KANISA MAMA ANASEMA YEYE TORATI ANA MAMLAKA YA KUBADILI NAYO WATOTO JE INAKUWAJE WATUMISHI?

  MNISAIDIE WAPENDWA NIELEWE KAMA NINYI.

 40. Wapendwa Wana na Binti za Mungu,
  Kwanza niseme kwamba, Mpendwa wangu Milinga nimethamini salamu yako kwangu, nimshukuru Mungu kama umeona na kuthamini kile Bwana alichonijalia kutia na kuongeza katika ufahamu wako, Mungu aendelee tu kukubariki, tujue tu kwamba tuyafanyayo hapa ni FAIDA lakini pia Yaweza kuwa HASARA yenye kutisha sana maana, lipo andiko linaloainisha matumizi na nguvu ya Ulimi katika Neno!

  Neno huhuisha au kuua, na Mtu anapoamini uongo hupewa kuamini huko! Kila nikiufuatilia vizuri, mjadala huu naona kama ulishakwisha mapema tu ulipoanza kwa sababu, kwanza, hakuna anayeikata Sabato, pili kila mmoja anakili kuiheshimu na kuthamini uwepo wa Sabato. Lakini kilicho kikubwa sana kuliko maneno yoooote tuliyoyazungumza hapa wote TUNAOGOPA KUPATIKANA NA HATIA YA KUIVUNJA SABATO! Tunachokieleza wachangiaji wote hapa, nimeona JAMBO MOJA TU kwamba, Kila mmoja anajaribu kwa uwezo wake wote kuonyesha ambavyo hahukumiwi na uvunjaji wa Sheria hii MASHUHURI ya Sabato! Kwanini hofu hii ipo? Ipo kwa sababu MWANAFUNZI HAOGOPI MTIHANI, ILA HUOGOPA MATOKEO YA MTIHANI, HIVYO HUUPENDA MTIHANI NA KUICHUKIA KALAMU YA MSAHIHISHAJI! Amri kama Amri kamwe si Mtihani ni Kalamu (PEN); Bali Matendo yenye kuilingania Amri ndiyo Mtihani!

  Shetani haigopi Amri, Bali huogopa matokeo ya ile Amri, nimekwisha sema kuwa Amri ndiyo Kalamu ya kusahihishia, na tayari shetani kwa vile hajaufanya mtihani ipasavyo, anayajua vilivyo majibu yaliyokwisha bandikwa katika ile “Anser sheet” yake! Shetani bila shaka anajua kuna watu wapumbavu wenyekujua kuwa wanajua, kumbe wapo hola, wajinga waliokaa kizembe hawana bidii katika kutaka kuijua kweli ili wawe huru, wakiamini kivivu kila waambiwacho huko waliko na kuona kuwa ni sawa tu wakisema yanini kutafiti wakati Mungu hachunguziki, ingawa Biblia mbilimbili mikononi wanazo, wavivu wa kujisomea Neno la Mungu, wasiotaka kujifunza chini ya Roho mtakatifu miguuni pa mitume, watukutu wa shule ya Bwana waliong’ang’ania Maudhui na mafundisho potofu ya Dini zao, watoro katika mafunzo, waliong’ang’ani ubishi, wenyekujiona na kujisikia vizuri kwa mali zao, wenye kulalamika na kutaka sana kukalishwa mbele kama wakuu kumbe watumwa wa Mtu masikini asiye na hadhi popote, wenye vichwa visivyelewa kabisa Neno la Mungu, wasio na ile Mbengu ya Mungu ndani yao, hao ndiyo Shetani huwatafuta ili awape ile “Answer Key” ya uongo, nao huipapania na kuigombea ili kuitwaa, na wakiipata huondoka mbio, huku wakishangilia kama mazuzu kuwa wao wamekwisha fauru! Lo, huruma! Sasa, ngojea majibu yatoke, kulia watataka na kucheka watataka sawia; Biblia inasema hali hiyo kitakachowapata ni kilio na kusaga meno!

  Kwa Tafsiri iliyo rahisi na nyepesi Sabato ni STAREHE, Yesu ndiye Bwana wa Sabato! Bila Yesu hakuna Starehe hata kidogo. Kama ni hivyo, kwa nini Neno Sabato ni gumzo? Ni gumzo kwa sababu mbili, moja nikuwa, inatokana na mafundisho ya Thiolojia za kidini pili ni uelewa upatikanao tokana na mafundisho ya Roho Mtakatifu. Tatizo linalowasumbua watu ni, SIKU IPI HASA NI YA SABATO jambo ambalo ni la kimwili; Kumbe wanachotakiwa kuelewa ni kwamba SIKU ZOTE NI SABATO ( Neno linasema, Sasa imebaki Raha ya Sabato kiroho!)

  Tatizo lingine kuhusiana na Sabato, watu wanadhani Sabato ni Siku kama siku, kumbe Sabato ni Sheria! Tunajua kwamba, mambo yote yaliyokuwepo kwa mjibu wa torati kimwili ilikuwa ni kivuri cha mambo haya ya Rohoni, maana Mungu hajipingi. Wapendwa Sabato ni Ishara inayotakiwa kuangaliwa kila siku, ni mkataba unaotakiwa kutekelezwa kila siku.

  Utekelezaji wa Sabato ndilo jambo mhimu hapa kwa sababu Kiroho kila siku ni sabato! Kwa nini Sabato itekelezwe kila siku, sikiliza, kwenda kusali jumamosi si kwamba unaitekeleza sabato! Ona Mungu kwanini alitupa sabato, Neno linasema, “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ISHARA kati ya mimi na wao, WAPATE KUJUA yakuwa MIMI NI BWANA, NDIMI NI WATAKASAYE Eze. 20:12”. Kwa Neno hili ni kila siku tunapaswa kukaa ndani ya sabato ili tutakasike, kwa sababu, tunatakaswa kwa Neno la Mungu. Na Neno ndiye Yesu na Yesu ndiye Mungu Kwa hiyo Mungu ndiye aliyeifanya hiyo Sabato. Ndiyo maana anasema, Sabato ni Ishara ya kututambulisha kwake kuwa Yeye ndiye Bwana mwenyekututakasa; Kama Sabato ni sheria ipaswayo kutekelezwa kila siku, Je, NANI KATI YETU AWEZA KUSEMA KUWA ANAYO LAZIMA KWA SIKU MOJA TU KATIKA WIKI YA KUMTAMBUA MUNGU KWAMBA NDIYE MWENYEKUTUTAKASA, LAKINI KATIKA SIKU ZILE SITA ZILIZO BAKI KATIKA WIKI HALAZIMIKI KUTAMBUA HIVYO?!

  Wapendwa mara zote jueni kuwa Mambo ya Roho mwili hauyawezi! Muonekano wa mambo ya Roho ni kama ya kitoto, hayana ujuzi wa kielimu, wanaoyajua ni wale wanaokubali kutokutegemea Elimu na ujuzi wao wa kimwili.

  Swali la Msingi, ni Je, tunaitekeleza Sabato ipasavyo kiroho?

 41. Siyi nimeshamjibu Lenda, bila shaka na wewe ulikuwa na maswali hukuniuliza kwa vile uliona tayari Lenda keshaniuliza.

  Siyi nawajua wasabato vizuri na mfumo wa imani yao ulivyo, kwa hiyo sibahatishi.

  Umegusia suala la Roho mt. Hebu sema sasa nyie wasabato mnajazwa na Roho mt/ mnaamini katika Roho mt?

  Asante!

 42. Ndugu Lenda kwanza ili uelewe kinachoongelewa na Isaya unapaswa kusoma kuanzia Isaya 65.

  Na utagundua kuwa mbigu mpya na nchi mpya zinazoongelewa hapa si zile zinazoongelewa katika ufunuo wa Yohana. Hii ni kwa sababu katika hii inayoongelewa hapa kwa Isaya bado tunaona kuna kifo na kuna wenye dhambi ambao wamelaaniwa (Isa 65:20), wakati katika nchi mpya na mbingu mpya ya kwenye ufunuo wa Yohana hatuoni kama kuna wenye dhambi watakaokuwemo wala hatuoni kama kuna kufa.

  Kitu cha pili utagundua kuwa habari hii inawahusu wana wa Israel/ uzao wa Israel.

  Tatu, sabato inayoongelewa hapa katika Isaya inaambatana na sikukuu za mwanadamo wa mwezi (new moon), amabazo kwa mujibu wa biblia leo zote hazipo maana zilikuwa kivuli.
  Ona hapa Paul anavyosema: ( Colossians 2:16 – 17 Let no man therefore judge you in meat, or in drink, or in respect of an holyday, or of the new moon, or of the sabbath days:
  17. Which are a shadow of things to come; but the body is of Christ.)

  Kuhusu huo uasi unaousema, nakushauri uwe msomaji mzuri ujue ni nini hasa kinaongelewa kwenye hizo sura za Waebrania 3 & 4.

  Hapo mwandishi anawaongelea waebrania ambao alikuwa amewahubiria neno la Kristo akijaribu kuwaonya kuwa wasiwe na moyo wa kutokuamini kama wale wana wa israel (waebrania pia) ambao walishindwa kumwamini Mungu matokeo yake hawakuingia katika ile nchi ya maziwa na asali ambayo kwa maneno mengine ameiita pumziko (rest),ispokuwa Joshua na Kaleb.

  Kwa kiswahili rahisi zaidi ni kwamba mwandishi anasema tusije na sisi tukawa na moyo wa kutokuamini kama wale waliotoka Misri, tukajikuta na sisi tunashindwa kuingia katika pumziko ambalo Yesu Kristo ametuletea. Nalo ni hili hapa: (Mt 11: 28 Come unto me, all ye that labour and are heavy laden, and I will give you rest)

  Ndio maana anasema kuwa pumziko lililobaki kwa watu wa Mungu ni hili, amabalo tunaliingia kwa njia ya imani, maana wale waliotoka Misri hawakuliingia kwa sababu hawakuwa na imani (Hebr 4:6 Seeing therefore it remaineth that some must enter therein, and they to whom it was first preached entered not in because of unbelief:)

  Kabla ya kurukia tu mstari wa 9 ni vizuri kugundua kilichosemwa katika mstari wa 8. Anamaanisha kuwa, kama hao waebrania waliotoka Misri wangekuwa wamelipewa hilo pumziko la Yesu basi leo kusingekuwa kumebakia pumziko jingine. Hebr 4;8 For if Jesus had given them rest, then would he not afterward have spoken of another day.
  Kwa hiyo kumbe Yesu hakuwapa hilo pumziko, na hakuwapa kwa kuwa hawakuwa wanaamini.

  Na kwa kuwa kumbe wao hilo pumziko hawakupewa, basi ndipo anasema sasa katika mstari wa tisa kuwa limebakia hata
  leo hilo pumziko kwa ajili ya watu wa Mungu. (Lakini wale wanaoamini). Hebr 4:9 There remaineth therefore a rest to the people of God.

  Lenda mimi natumia King James Versio. Nakushauri ukaisome kwa utulivu mzuri hiyo mistari utagundua kuwa kinachosemwa pumziko hapa siyo siku ya Jumamosi wala nini, bali ni pumziko la milele la rohoni ambalo linapatikana kwa njia ya kumwamini Yesu kristo. Na kwa bahati mbaya zaidi tafsiri nyingi za asili zimetumia neno pumziko badala ya neno sabato kama ilivyo tafsiri ya kiswahili.
  Asante.

 43. ndugu siyi sawa….nakubaliana na maelezo yako ya awali…umeniuliza yale maneno ya mungu aliyomwambia Adamu asile lile tunda kama ni torati au siyo torati na je,ni ya musa au ya mungu?..sijakuelewa ulitaka kuhoji nini hapo….lakini kwa ufupi ni kwamba ile ilikuwa ni sheria ya mungu dhidi ya Adamu kwa wakati ule…sheria zote ni za mungu mwenyewe ila ninaposema sheria za musa maana yake ni kwamba zimepitia tu kwa mkono wa musa lakini mungu ndiye anaemuongoza nabii musa kuandika sheria mbalimbali kwa ajili ya watu wake…hakuna kitu kama ulichosema eti sijui torati ya musa na sheria za mungu!..mungu ndiye mtoaji na muongozaji wa sheria zote kupitia manabii wake.Sheria za mungu zilikabidhiwa rasmi kwa ajili ya wanadamu wote pale mlima sinai.Pia umelitafasiri neno MAZOEA nililolitumia huko juu kwa tafsiri isiyofaa nimesikitika kwelikweli lakini nakuomba uwe mwepesi wa kuelewa mambo vinginevyo tutakesha hapa!!….neno MAZOEA nililotumia huko juu kwenye hoja yangu nilimaanisha KUDUMU KATIKA SHERIA ZA MUNGU KWA WATU WA ISRAEL CHINI YA UTARATIBU AU UONGOZI WA NABII MUSA KAMA MUNGU MWENYEWE ALIVYO WAAMURU KWA WAKATI ULE KATIKA TORATI YAKE.Sasa sijui kulikuwa na tatizo gani kwa waisrael kuishi chini utaratibu au mazoea maalumu ya kushika njia za mungu? Kama nilitumia neno ‘mazoea’ vibaya badala ya neno jingine m badala basi naomba ieleweke hivi…lakini nakuomba uwe mwepesi wa kuelewa mambo!…mimi siyo muandishi wa habari wala mtangazaji wa Radio…jitahidi kusoma mambo kwa utulivu ili uyaelewe kwa maana halisi inayofaa.Kaka siyi nimalizie na sabato sabato sabato kama wewe mwenyewe unavyoitetea kwa nguvu zote!!!…nilitoa ushahidi wa wazi kabisa kwamba BWANA YESU NDIYE BWANA WA SABATO…Hayo hayakuwa maneno yangu bali yalikuwa ni ya bwana yesu mwenyewe akimaanisha yeye ndiye kanisa anayekaa ndani ya roho zetu akituongoza,yeye anasema pasipo mimi nyinyi hamuwezi jambo lakini wewe bado huelewi umeshika sana dini na dhehebu wewe badala ya neno la mungu!.Ukisoma kwenye ufunuo,Yohana anakiri kwa kusema NAIFURAHIA SABATO YA ROHO…Wewe bado watafuta sabato ya mwili…je,bwana yesu hakufa kwa ajili yako ili umtumikie kwa hiari ya roho yako?..Sabato siyo mchezo ndugu siyi kwa kuwa ukikosea kidogo tu mungu anaamuru wewe kuu wawa!…hebu fikiri katika biblia inatuonyesha kuwa binti mmoja aliuliwa kwa kosa la kukusanya kuni tu katika sabato!! Soma(hesabu 15:32-36).Sasa ujiulize wewe unaefuata sabato ungeponaje katika mazingira yetu haya ya siku hizi.Hii ndiyo maana baada ya kuongezeka kwa maovu na mauaji ya hali ya juu kwa sababu ya sabato…mungu kupitia nabii isaya aliamuru kuvunjwa kwa sabato,soma(isaya 1:13-16).Halafu kaka siyi ulipinga kuwa ile sabato aliyoiongelea mtume paulo siyo sabato yenyewe…ukasema ile ilikuwa ni sabato ya kimila ya wana wa israel lakini huo pia ni uongo wa wazi kabisa!!.Fahamu kuwa hakukuwa na sabato ya kimila na sabato ya kweli ya mungu na kama ile ilikuwa ni ya kimila hebu nionyeshe katika biblia hiyo ya kweli iko wapi?…tena uthibitishe kimaandiko pasipo kutafuta elimu yoyote ya ziada kwenye mitandao ya kijamii kama google kama ulivyotaka nifanye kwa kuwa biblia inajitegemea yenyewe na hairuhusu mawazo mengine ya kibinaadamu,soma (ebrania 13:9)….sikiliza na uelewe kaka siyi sabato ya mungu ni moja na ni ileile lakini maovu yalipoongezeka kwa wana waisrael ndipo wao wenyewe wakawa wanaichanganya sabato ile ya mungu na taratibu zao za kibinaadamu ikawa haiwezekani tena kutofauthsha sabato ya mungu na mila na desturi mbaya za wana wa israel ndipo mungu akamtuma yesu kristo ili kuitimiza kwa ukamilifu wake wa mwili ili sisi wote tuenende kwa kumuamini yeye.soma kwa makini (mathayo 12:1-10).Bwana yesu aliifuta kabisa ile hati ya mashtaka pale msalabani,soma(kolosai 2:14-17).Bwana yesu asifiwe…Bwana yesu asifiwe…basi mimi niishie hapo nakushukuru kwa changamoto zako kaka siyi…nikuache uendelee na hoja nyingine na mwenyezi mungu akubariki.Ukijisikia kujibu hoja mimi niko tayari kwa hilo.ubarikiwe.

 44. Mkandya
  Ha ha haaaa!! Sikucheki kaka, ila nafurahi tu kwa jinsi ulivyojibu pachiko langu. Nikwambie tu kuwa, situmii nguvu nyingi kama unaavyofikiri. Ni kawaida sana. Baada ya kusoma pachiko lako, nilitaka kukuuliza maswali bahati nzuri ndugu Lenda ameshafanya hivyo tena maswali mazuri sana. Jibu kwanza maswali ya Lenda. Na ukisema kuwa mimi naitunza sabato kimwili tipiko, sikushangai, maana huelewi kuwa kushika/kutunza sheria za Mungu hakutokani na jitihada za mwili bali ni matokeo ya upendo wa mtu kwa Mungu wake na wanadamu wenzake. Nimesikiliza wahubiri wengi sana wa makanisa ya j2 wanavyowadanganya watu, kuwa wasabato ni watu wa mwilini. Hawana roho. Wakavu –hawana mafuta ya Roho Mtakatifu nk. Ninahisi na wewe unawasikiliza sana hao na unaamini maneno yao hayo licha ya kutokuwa na ushahidi wowote wa Kibiblia ama kuwasikiliza wasabato wenyewe wanasemaje. Na kwa vile unayaamini sana maneno ya mitume na manabii wako kuliko Biblia, utahangaika kweli kubaini uongo na ukweli unaosemwa na viongozi wako wa dini. Ndiyo maana nilikwambia, sikushangai.
  Nakusubiri ujibu kwanza maswali ya ndg Lenda.
  Tuzidi kusonga mbele…

 45. Mkandya naomba unisaidie fungu hili umelielewaje?

  “KAMA VILE MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, NITAKAZOFANYA, ZITAKAVYOKAA MBELE ZANGU, ASEMA BWANA, NDIVYO UZAO WA JINA LENU LITAKAVYOKAA. NA ITAKUWA MWEZI MPYA, NA SABATO HATA SABATO, WANADAMU WOTE WATAKUJA KUABUDU MBELE ZANGU, ASEMA BWANA.” ISAYA 66:22-23,24

  -NISAIDIE NA HILI

  Kwa nini Mungu anasisitiza juu ya uasi akaitaja Sabato kuanzia Waebrania 3:12-19 na 4:1-13 na anazungumzia Sabato 4:9. Lakini Pia kaita uasi wa Sabato “NAO WATATOKA NJE NA KUITAZAMA MIZOGA YA WATU WALIONIASI; MAANA FUNZA WAO HATAKUFA, WALA MOTO WAO HAUTAZIMIKA NAO WATAKUWA CHUKIZO MACHONI PA WOTE WENYE MWILI.” ISAYA 66:24

  -NA HAPA CHINI ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?

  Na kinachonichanganya zaidi anasema
  “IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU” Waebrania 4:9
  Ntafurahi ukinijibu ndugu yangu katika Kristu.

 46. Bwana Seyi pole sana, naona unatumia nguvu nyingi sana.

  Ila kwa kweli unanifurahisha, kwamba mbinguni tutakuwa tunaabudu siku ya Jumamosi! mimi najua mbinguni siku zote ni mchana,sasa sijui utajuaje kuwa leo ni ijumaa jioni na kesho ni Jumamosi, wakati hakutakuwepo na usiku unaotuletea mchana.

  Bila aibu unasema mimi narudi kwenye dini ya kiyahudi basi wewe sijui nikwiteje sasa, labda zaidi ya farisayo wa mafarisayo!
  Bado unamwabudu Mungu katika mwili tipiko

  Inaendelea….

 47. Aaaaa, Lwembe,
  Mimi naona sichanganyi mtu ila labda unataka kuchanganyikiwa wewe mwenyewe. Na utachanganyikiwa kweli usipokuwa makini. Siyi, haongezi wala hapunguzi chochote kwenye Biblia. Nenda taratibu utanielewa tu.
  Nimesema kuwa hukunielewa na hutanielewa kamwe isipokuwa umerudi nyuma kidogo kutafakari maandiko upya. Si unaona sasa unavyojichanga Lwembe. Yaani unasema dhambi ya uzinzi hailihusu kanisa? Kweli kabisa?? Je, wakristo leo wako huru kutamani tu na kuwaka tamaa juu za mabinti, wake/maume za watu?? Je, huu ndio uhuru tulio nao katika Kristo wa kuwa huru kutamani wake/waume yaani kuzini?? Kwa maelelezo mengine, unasema kuwa leo hakuna dhambi tena ambazo zinaweza kutendwa na watu!! Na kama hakuna dhambi, hakuna haja ya kuwa na mwokozi.
  Kristo (torati mpya kama unavyodai) anaposema tukimpenda tutazishika amri zake, ni amri zipi hizo kaka Lwembe? Najua unataka kuhalalisha na kuwadanganya watu kuwa leo hakuna dhambi maana torati haipo. Na kama torati, haipo, maana yake ni hakuna dhambi, maana bila sheria/torati, utalitambuaje kosa/dhambi? Ngoja nikuoneshe kitu kamanda wa Yesu usiyeona…
  Umesema kuwa sasa hivi hatuko chini ya sheria, yaani torat na ukasema kuwa tumsikilize Yesu na mitume wake jambo ambalo ni sahihi kabisa, maana kwa maneno mengine ni kuliangalia agano jipya kama linasupport hoja zako hizo kaka Lwembe.
  Huyo unayetwambia tumsikilize YEYE yaani Kristo, ni mshika torati. Yesu na Baba yake, ni wanatorati tangu mwanzo na hata milele. Angalia, Yohana 15:10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Unaona? Huwezi kumtenganisha Yesu/Mungu na torati kama kweli wewe ni mwanafunzi mzuri wa Biblia anayeongozwa na Roho Mtakatifu.

  Mwangalie huyu mwanafunzi mahiri wa Yesu ambaye unatuambia tujifunze kwake pia-Paulo anasema nini? Warumi 3:20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
  Unaona Lwembe, Paulo anachosema hapa ni kweli tupu. Sasa jiulize, Yesu alipokufa msalabani, dhambi ziliisha kutendwa na watu? Je, leo ndani ya kanisa hakuna dhambi zinazotendwa na muumini mmojammoja au kanisa zima? Je, Paulo naye analikubali hilo suala la kutokuwa na dhambi leo kama unavyojaribu kutulaghai wewe Lwembe? Angalia Paulo anavyosema tena hapa; Warumi 3:31 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria. Unaona? Sasa kama tunaithibitisha sheria katika imani, hii ina maana gani? Ndiyo kusema kuwa sheria inapothibitika, inaondoa dhambi?? La hasha! Acha kudanganya watu kaka.

  Hebu, mwangalie tena Paulo anavyosema hapa, Warumi 7: 15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. 17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

  Unaona Lwembe? Kumbe Paulo pamoja na mbwembwe zooote za kuandika nyaraka nyingi ndani ya Biblia, kuongozwa na Roho Mtakatifu kwingi sana, bado alikuwa na dhambi ndani ya moyo wake. Rudia aya hiyo ya 17 na 20 kuisoma tena! Kaka, Lwembe, Yesu hakuja kuondoa torati ya maadili katu. Acha kuchanganyikiwa na falsafa za walimu wako hao. Wanakupoteza tu. Ruhusu Biblia chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, ikuongoze kaka.
  Tumwache Paulo, twende kwa Yohana mwanafunzi wa Yesu. 1 Yohana 2:4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Je, Lwembe na wengine(SG), unafikiri hizi amri ni nini kama siyo Torati? Angalia tena hii; 1 Yohana 2:3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 2 Yohana 1:6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.

  Lwembe na wengine, kama utamsikiliza Kristo, ina maana utamjua YEYE-Kristo. Sasa kumjua kwako huko kuko wapi kama huzishiki sheria? Hebu jaribu kufikiria, ni watu wangapi walisoma hiyo text yako ya uongo. Ni watu wangapi walichukua hayo madanganyo yako uliyoyaandika tena bila hiana!! Unafikiri huna sababu ya kuomba msamaha kwa Mungu kwa sababu umelikosesha kundi lake? Zaidi ya hapo, rudi, kaa chini, tafakari halafu angalia hicho unachotaka kusema kwa watu kama kiko sawasawa na neno la Mungu. Kama hakiko sawa, ni heri unyamaze kimya.
  Ushauri wangu kwako, isome vizuri Biblia yako. Iko wazi sana. Roho Mtakatifu atakuongoza vyema na hautapotea kamwe. Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, hawapingani NG’O! Njoo tu kwa wasabato tuburudike katika utakatifu wa sheria za maadili ikiwemo na sabato, ambazo kwa msingi mkubwa, zimejengwa chini ya PENDO la Kristo. Na katika PENDO hilo, tunazitimiza sheria.

  (basi pendo ndilo utimilifu wa sheria-warumi 13:10).
  Barikiwa sana.

 48. Mmh, kaka Mkandya,
  Naona bado unaniijia kwa maswali mengi sana, japo mengine ni maswali ya mtego. Nami ngoja nijaribu kukujibu safari hii kwa ufupi zaidi huenda utanielewa. Kuna maeneo mengi katika mchango wako, umechanganya sana sana . Siyo kwamba hujui kitu. La, hasha. Una mambo mengi tu kichwani, tangu mwanzo nimekuwa nikiyaona. Twende sasa kwenye maswali yako;
  1. Swali la kwanza, umeuliza nini maana ya ibada? Sidhani kama huelewi kabisa maana ya ibada. Nafikiri napo unaniangalia akili tu kuwa ninaelewa nini kuhusu ibada. Nikushauri kuwa, JITAHIDI KUWA UNAANGALI HICHO NILICHOKISEMA KAMA KINAENDANA NA BIBLIA AMA LA NA SIYO KUNIANGALIA NINAJUA NINI! Niende sasa kwenye kujibu swali. Ibada ni tendo la kumwabudu Mungu. Kumwabudu huko kunaweza kuhusisha maombi(sala), nyimbo, kujifunza neno nk. Ibada inaweza kufanyika kila siku. Hata mimi kaka Makandya, huwa nafanya ibada kila siku. Na ninafanya hivyo kwa sababu ya upendo wangu KWAKE. Ninapotambua fadhili zake zilizo nyingi maishani mwangu, huwa sina budi kuanguka magotini na kumshukuru kwa wema huo.
  2. Umeuliza kuhusu sabato na wanafunzi wa Yesu kukata masuke ya ngano siku ya sabato!! Umeuliza kuwa huo ndio utakatifu? Makandya, niseme tu hivi, Sabato maana yake ni pumziko. Pumziko takatifu. Pumziko alilolianzisha Mungu mwenyewe bustanini Edeni. Pumziko ambalo mtu yeyote duniani, anapaswa kupumzika, kimwili, kiakili, kiroho na hata kisaikolojia. Mwanzo 2:1-3, kutoka 20:8-11. Pumziko hili, huwa ni pumziko kwa ajili ya kumwabudu Mungu siku nzima. Ni pumziko kwa ajili ya wanadamu wote. Yaani kutenga siku nzima kwa ajili ya Mungu. Siku hiyo, mtu yeyote hapaswi hata kufikiri mambo ya biashara, kilimo, elimu dunia, nk isaya 58:13-14. Ni siku ambayo hatufanyi kazi zetu na mambo yetu binafsi kama binadamu. Ibada hii, huwa haina maana kwamba watu wanakaa tu hapo siku nzima bila kumove kwenda hapa na pale kama kwenda kuwaona wagonjwa, wasiojiweza, kwenda mahali/nyumbani kula chakula kilichoandaliwa siku ya sita-ijumaa na kisha kurudi tena kwenye ibada nk.
  Wanafunzi wa Yesu walichokifanya siku ya sabato, lilikuwa ni jambo jema la kuokoa nafsi zao. Kumbuka wale walikuwa kwenye movements na Bwana wao. Njaa zilipowazidi, ulitaka wafeint kwa njaa kaka Makandya? Suala la kuokoa afya zao zisidhurike kwa njaa kwa mazingira hayo waliyokuwa nayo-mbali na makwao, lilikuwa ni jema. Ndiyo maana mimi msabato, ikitokea emergence yoyote siku ya sabato ya kwenda kuchimba dawa kwa ajili ya mgonjwa, kutibu mtu, kumpeleka hospiatli nk naifanya kazi hiyo na hiyo siyo dhambi. Sabato siyo mzigo kama unavyoifikiria kaka Makandya. Sabato ni tunda, tokeo la upendo ulio nao kwa Bwana/Mungu wako. Na ndiyo amri hiyo ya kwanza iliyokuu ya mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, nafsi yako yote….ambayo kwa hakika, inajumuisha amri ya 1-4 kwenye zile amri 10.
  3. Umeuliza kuwa wapi pameandikwa ndani ya amri za Mungu kuwa siku ya sabato watu wasipike? Mmmh! Ukianza kuwa unafirkiri kuwa kila jambo ni halali tu kama lipo kwenye amri kumi za Mungu, Makandya utaanza kuvuta sigala, kunywa pombe, na mambine ambayo ni illegal kimaadili, kisa tu hayamo kwenye amri za Mungu. Hii nayo ni hatari kubwa sana kaka. Mimi sifuati amri peke yake, bali nafuata Biblia nzima. Biblia haisemi wasipike tu, bali wasiwashe kabisa hata huo moto. Kutoka 35:3 Hamtawasha moto katika nyumba zenu kwa siku ya Sabato. Mbali na kutowasha moto siku ya sabato, waliambiwa waandae chakula cha sabato siku ya sita-ijumaa, maana siku ya sabato, kisingeonekana. Kutoka16(soma sura nzima) Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana-aya ya 26. Kipindi cha wana wa Israel, Mungu aliwaambia watu wakusanye pishi mbili siku ya sita-ijumaa kwa ajili ya ijumaa na siku ya sabato, manna sabato ilikuwa ni starehe takatifu. Kutoka 16: 23 Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi. Na wale waliokiuka amri hiyo na siku ya sabato wakatoka kuokota manna, wasiione… Angalia Mungu alivyowaambia. Aya ya 27 Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione. 28 Bwana akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini? Mungu alikuwa na makusudi yake, Sababu zake. Wewe ukianza kuhoji mawazo ya Mungu, hoji tu, lakini Mungu hafikirii wala hawazi kama tunavyofikiri/kuwaza sisi, Isaya 55:8-9. Kuna waliohoji wakaprove zero-wana wa Israel. Na wewe Makandya endelea kuhoji tu japo sikushauri ufanye hivyo. Ni hatari sana kaka. Maana shida niliyoiona kwako ni hii, yaani unafikiri watu wasiimbe wala kupiga vinubi, gitaa, zeze, kinanda nk siku ya sabato eti hizo nazo ni kazi!! Watu wasifungue Biblia maana nayo ni kazi tu. Wasihubiri siku hiyo maana nayo ni kazi ya kutoa sauti tena kwa nguvu na wengine huwa wanasweat kabisa, sasa hii nayo ni kazi tu. Wasiinue mikono, wala kumove, maana nayo ni kazi. Yaani hata kula wasile au kuwahudumia wenye shida/wagonjwa wasiwahudumie kwa maana watafanya kazi. Na hao maserafi huko mbinguni hawapaswi kumovuzisha mabawa yao sita siku ya sabato wakiimba, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu…. maana nao watakauwa wanafanya kazi siku ya sabato!!…nk. Hii ndiyo shida yako kubwa kaka Makandya!! Unarudi agano la kale tena ndani ya utamaduni wa taifa la wayahudi katika suala zima utekelezaji wa sheria za maagizo. Unarudia dini ya mafarisayo na masandukayo. Sasa sijui nitakusaidieje ili uelewe maana, unasema una uelewa sana na hata mimi nauona, but huelewi mambo madogo tu kama haya kaka!!! Natafuta namna nyingine ya kukuelewesha kama na text hii hautaielewa tena.
  4. Swali lingine umeuliza kama kuhusu amri zinazozilinda amri 10 . Ni dhahiri kuwa hapa ndg hukunielewa kwenye makala yangu ya kwanza kwenye mjadala huu. Nakurejesha tena kwenye makala hiyo, na ile niliyoipost majuzi ikibainisha sheria zilizoishia msalabani ambazo kwa hakika, ndiyo aliyekuwa mlinzi wa Amri 10. Sasa hivi mlizi wa amri 10 siyo sheria za maagizo tena, bali ni upendo wetu kwa Kristo peke yake.
  Mwisho, kama unafikiri kusali jumapili haina tatizo, au mtu anaweza kusali siku yoyote ile kama siku yake nzima ya ibada badala ya siku ya saba-jumamosi aliyoiteua Mungu, akapumzika, akaibariki na kuitakasa, wewe acha kwenda hiyo jumapili then nenda jumatano ukasali. Utaniambia kama utafanikiwa kwa hilo. Labda nikwambie tu kuwa, ibada zingine tofauti na siku ya sabato ni ibada za sanamu(usikwazike tafadhari). Na huo ndiyo ukweli. Kuna siri kubwa imefichika kwa kuadhimisha jumapili. Najua kabisa kuwa hujui katika hili. Ibada ya jumapili, ni ibada kwa mungu Lucifer-jua. Na Biblia iko wazi sana kwa hili. Yaani sijui unatumia version gani kaka!! Jumapili ni takwa la Lucifer na siyo takwa la Mungu. Wanadamu chini ya uongozi wa Lucifer, ndiyo waliyoiweka jumapili kuwa siku ya ibada. Jumapili iliwekwa na wanadamu na siyo Mungu walaYesu. Na walioiweka jumapili, ukiangalia kwenye zile amri 10 za Mungu, amri ya pili waliiondoa kabisa, maana walijua itawashtaki kwa kuabudu sanamu. Ukitaka ushahidi wa kibiblia ni mwingi kuliko maelezo haya. Nitakupa tu ukitaka. Wengi wa wanaosali jumapili hawajui. Lakini kuna ole kwako wewe uliyetahadharishwa tayari!!. Sabato kama mojawapo ya amri 10 za Mungu ipo hadi siku zote.Siku ile nilikwambia kuwa, hata huko mbinguni tunakoenda, tunaenda kumwabudu Mungu siku ya sabato. Jumapili wala ijumaa kama siku za ibada hakuna kule. Tangua agano la kale, hadi jipya, ukweli kuwa sheria za Maadili itaendelea kuwepo. Jitahidi tu kusoma Biblia yako. Utagundua mengi. Lakini kama ni mtu wa kusikiliza tu..HILI NDILO NENO LA BWANA…AAAMEN!!!-, utaliwa mpaka utaisha tu.
  Msemo wako, tunaendelea…

 49. Milinga na Mkandya, nawashukuru wajoli wa Bwana. Naomba tuvumiliane ili tufikie mwafaka mzuri. Biblia ina kila kila kitu ila sisi wenyewe ndiyo wavivu wa kuisoma. Sabato ipo na itadumu kuwepo kama zilivyo amri zingine tisa, amabzo kwa ujumla wake, ukijumlisha unapata ten commandments.
  Aidha, kaka Makandya nimekona kwa hiyo correction yako. Usijali. Huwa siangalii sana makosa ya tahijia(spelling errors) bali ujumbe zaidi. Twende kazi mjoli wa Bwana

 50. Milinga nimekuona ndg yangu, nashukuru sana.
  Pia Lwembe rafiki yangu nimekuona, ubarikiwe mno.
  Amina!

 51. Wapendwa wote na hasa Mpendwa Mkandya,

  Navutiwa sana na jinsi unavyojenga hoja za maandiko na mantiki ya akili na uelewa mkubwa. Ubarikiwe sana. Umenijenga vyema sana kwenye mjadala huu. Nimeupenda mjadala wote toka mwanzo. Kaka endelea zaidi na zaidi. Napenda sana the way you have contributed in this spiritual debate. Umechangia mambo mazito sana ambayo kwa kweli yanaeleweka labda tu kama kuna mtu hataki kukuelewa kwa sababu alishalogwa kama Wagalatia waliotaka kurudia mafundisho manyonge ya Torati na Mt. Paulo akahoji, “Enyi wagalatia msio na akili ni nani aliyewaloga……?” Kwa hiyo mtu asiyeelewa maelezo yako atakuwa kama wagalatia walioonekana kama waliologwa hadi wakawa hawaelewi kutenganisha Agano la Kale na Agano Jipya au Torati ya Mussa na NEEMA ya Kristo.

  Mpendwa CK Lwembe, ubarikiwe sana kwa maelezo yako ya kina na yanayoeleweka kwa ufasaha kabisa. Mungu azidi kukufunulia maana ya maandiko zaidi ili nasi tubarikiwe zaidi.

  Mabinza LS, Mungu azidi kukutia nguvu kimwili na kiroho. Nimevutiwa sana na jinsi ulivyochangia mada hii.

  Mpendwa Siyi, nashukuru sana kwa changamoto zako ulizochangia kwenye mada hii nakuifanya iwe motomoto. Ubarikiwe zaidi na Mungu azidi kukufunulia ukweli wa Injili ni upi na ukweli wa Sabato au Torati ni upi. Nimependa sana ulivyochambua hoja zako kimaandiko na logic.

  Mpendwa Magreth Mkiwa na Neema Msabila na wengineo wote walioshiriki kuchangia mada hii na wale wanaoemndelea kuchangia mada hii, Mungu awabariki sana. Nimejifunza mengi toka kwenu. Asanteni sana.

  Mjadala unaendelea kwa wale wote wenye hoja za kulisaidia kanisa la Tanzania na dunia kwa pamoja ili kukua kiroho, kiimani, kiidadi na kimtazamo.

  Majadiliano au mjadala unaendelea.

 52. Ndugu Seyi huwa kuna ‘key points’ katika hoja, hizo mimi ndio hufuatilia. Halafu usidhani kabisa hata kidogo kuwa mimi ninayejibizana nawe ni maamuma (mjinga) au sijui kama unavyojaribu kudhani. Nimekuuliza tu maswali mepesi ili niuone ufahamu wako juu ya suala hili.

  Ngoja nikuoneshe kitu hapa: Ona ulivyojichanganya hapa ndugu Seyi, nakunukuu ”Hata mimi huwa nasali asubuhi, mchana na jioni. Na hufanya hivyo kuanzia siku ya 1-6. Siku ya saba, hupumzika kabisa yaani hufanya kusanyiko takatifu kwa ajili ya ibada ya kumwabudu Mungu muumbaji tu. Hakuna kazi siku hiyo”

  Umesema kuwa siku ya saba hupumzika kabisa, halafu unaseme siku hiyo huwa unafanya kusanyiko takatifu kwa ajili ya ibada.( What is ibada Seyi?)
  Na ukishasema maana ya ibada uniambie sasa kile ambacho huwa unakifanya siku ya kwanza mpaka ya sita ni nini?(yaani huko kusali asubuhi na jioni ni nini?)

  Kwa tafsiri nyingine ya ulichokisema ni kwamba kwako maana ya kutunza sabato ni kukudanyika siku ya Jumamosi. Na kwamba siku ya kwanza mpaka ya sita unaposali asubuhi na jioni huwa si kumkumbuka Mungu muumbaji. Sasa niambie huwa unamkumbuka nani hizo siku.

  Na kama maana ya kuitunza sabato na kuitakasa ni kufanya kusanyiko siku hiyo, niambie wakati wanafunzi wa Yesu wanakata masuke huko nako kulikuwa ni kukusanyika?

  Lakini Seyi umesema kuwa wasabato wanaopika siku ya Jumamosi ni sawa na kenge katika msafara wa mamba. Lakini kumbuka hakuna mahali katika amri kumi panasema usipike siku ya sabato. Na wewe katika kufafanua kwako huko nyuma ulisema alichotangua Yesu ni zile sheria za kulinda amri kumi, ambazo ni pamoja na kutofanya kazi wewe, wala mnyama wako, wala mgeni wako,wala mtumwa wako nk.

  Sasa kama hizo zimetanguliwa kama ulivyosema, umepata wapi ‘ubstance ya kumhukumu anayepika siku ya jumamosi kuwa anakosea?

  Seyi tunaposema kupumzika, tunamaanisha nini kinachopumzika mwili au roho?

  Halafu wewe ati unasema siku ya Jumamosi huwa unapumzika kabisa!
  Ndio maana nikakwambia muulize mpiga gitaa wa kanisani kwenu kama kutembeza vidole kwenye scale za gitaa siku ya Jumamosi ni kupumzika huko.

  Tunaendelea.

 53. Kwa wale wanaojua kimombo naomba wasome maelezo yafuatayo:

  DO NOT THINK THAT I CAME TO DESTROY THE LAW BUT TO FULFILL IT.

  Law keepers always try to justify their 10 commandment keeping by Matt. 5:17-19. Lets look at what Jesus intent is when He states, “Do not think that I came to destroy the Law or the Prophets. I did not come to destroy but to fulfill. “For assuredly, I say to you, till heaven and earth pass away, one jot or one tittle will by no means pass from the law till all is fulfilled.”
  In the greater context of his sermon Jesus is giving contrasts of his correct interpretation of the law in contrast to the Pharisees interpretation. The Pharisaic traditions destroyed the law because they reinterpreted the law, not presenting it in the way Moses had intended. As long as Jesus was alive He had to keep the law the way it was written by Moses. He would fulfill the law as Moses had written it. Once He died and rose again He ratified what was needed to be kept under the law of Christ (not Moses). This law was either given directly by Jesus or through the apostles after the resurrection (Acts 1:2). The Sermon on the Mount is used to prove one is still under the law but Jesus is only explaining the true intent of the law in contrast to what the Pharisees taught.

  In this section quoted (Mt.5:17-19) He goes on to say “Whoever therefore breaks one of the least of these commandments, and teaches men so, shall be called least in the kingdom of heaven; but whoever does and teaches them, he shall be called great in the kingdom of heaven.”
  What would be the least of the commandments? This is not the Sabbath or the 10 but all 613. The smallest “jot or tittle” of “the law and the prophets” will not pass away. The jot or tittle is the smallest stroke of the pen in the Hebrew alphabet. This would include all the ceremonial laws as well! If one insists on keeping the 10 then this means we would have to keep all the Torah laws that Israel kept, there would be no change from the new covenant. If the law is still in effect then so are the penalties for breaking the law. If one separates the penalties then the commands have no authority or justice on an individual. But Jesus also mentioned the prophets, that all they have prophesied will be accomplished.

  Jesus fulfilled all the laws requirement by his perfect obedience, taking upon himself the penalty and the curse of the law and with his dying rendered it inoperative for the believer (Rom.10:4-5; Heb. 8:13). To say one is going to keep the Old Testament law because of requirement is to ignore the work that Christ did in our stead in the New Testament covenant.

  As far as the word “fulfill” which many abuse, it does not mean to continue or reinforce. Matthew consistently used the word fulfill in a specific manner, once something is fulfilled there is not a future fulfillment. He quotes Isa.7:14 for the fulfillment of the virgin birth. Where he was to be born Micah 5:2, there is no awaiting for this to re occur in the future. To fulfill something means to bring it to a completion. It is used consistently this way through Matthews gospel (Mt.2:17,23, 12:17, 13:13,35, 27:9,35)

  Here are a few examples: Matt 2:15 “and was there until the death of Herod, that it might be fulfilled which was spoken by the Lord through the prophet, saying, “Out of Egypt I called My Son.”

  Matt 8:17 “that it might be fulfilled which was spoken by Isaiah the prophet, saying: “He Himself took our infirmities and bore our sicknesses.”
  Matt 21:4-5 “All this was done that it might be fulfilled which was spoken by the prophet, saying: “Tell the daughter of Zion, ‘Behold, your King is coming to you, lowly, and sitting on a donkey, a colt, the foal of a donkey.’“
  Matt 26:56 “But all this was done that the Scriptures of the prophets might be fulfilled.” Then all the disciples forsook Him and fled.

  All the Scriptures that Matthew writes about being fulfilled all mean a completion of something that is said. That something was prophesied or written and he fulfilled it or made it happen, bringing it to its end, having it come to pass.
  Jesus’ last words before he left are found in Matt. 28:20 “teaching them to observe all things that I have commanded you; and lo, I am with you always, even to the end of the age.” Amen. Jesus after the resurrection continued with the apostles for 40 days. We find in Acts 1:2-5 “Until the time he was taken up after he through the Holy Spirit had given commandments to the apostles he had chosen.” “To whom He also presented Himself alive after His suffering by many infallible proofs, being seen by them during forty days and speaking of the things pertaining to the kingdom of God. And being assembled together with them, He commanded them not to depart from Jerusalem, but to wait for the Promise of the Father, “which,” He said, “you have heard from Me; “for John truly baptized with water, but you shall be baptized with the Holy Spirit not many days from now.”

  An interesting correlation is that Jesus stayed with the apostles 40 days giving instruction, the same amount of time Moses was on Sinai receiving the commandments from God. Was he teaching them the same thing he had taught them prior? No, these were new instructions through a new covenant.
  Acts 1:8 “ But you shall receive power when the Holy Spirit has come upon you; and you shall be witnesses to Me in Jerusalem, and in all Judea and Samaria, and to the end of the earth.”

  As we can see, some commands are temporary and only for a certain time. This is also true for the Old Testament laws, many of the Old Testament laws are given new meaning in the New Testament. Whatever came through the cross and taught by the apostles were the teachings for the Church.

  Commands can be something God gives at a certain time. They are not to be confused as to always being kept at all times in the way they are said. Otherwise we would all have to go to Jerusalem to receive the Holy Spirit. Some commands are specific and one time events. Some are temporary such as the sacrifices, others still continue. Some are to certain individuals others are to the whole Church. For example: Jesus did not tell the disciples not to sacrifice animals during this time they were still under the law before his resurrection. Its obvious after he died the veil was rent and his sacrifice was once for all, they no longer had to do continue this. So when Mt.28 states to observe all things that I have commanded you it must mean and include what he spoke to the disciples after His resurrection, which could explain the very fact of why he stayed 40 days and did not ascend to heaven immediately after His resurrection.

  Some examples of these temporary commandments are: Mt. 10:5-8 “These twelve Jesus sent out and commanded them, saying: “Do not go into the way of the Gentiles, and do not enter a city of the Samaritans. But go rather to the lost sheep of the house of Israel.” Jesus told the disciples not to go to the gentiles but afterwards in Mt.28 he tells to do so and this is where he says to teach them to observe all I commanded you. Acts 8:5 “Then Philip went down to the city of Samaria and preached Christ to them.” Acts 9:15 “But the Lord said to him, “Go, for he is a chosen vessel of Mine to bear My name before Gentiles, kings, and the children of Israel.” Acts 18:6 “From now on I will go to the Gentiles.” Was Paul disobedient? Of course not, the command of Christ had changed from what was previously given.

  In Acts 15 [T]he gentiles are told that they do not have to be circumcised or keep the Law of Moses. The Old Testament consequence for not keeping the Sabbath was the death sentence (Ex. 31:14-17). God sought to kill Moses before he was going to Pharaoh because he neglected to circumcise his son.
  Num. 28:9-10 states there is to be a sacrifice on each Sabbath. In the New Testament the sacrifices ceased.

  Heb.7:12: “For the priesthood being changed, of necessity there is also a change of the law.”
  Heb.10:1: “For the law, having a shadow of the good things to come, and not the very image of the things, can never with these same sacrifices, which they offer continually year by year, make those who approach perfect.” If the sacrifices were taken care of by one sacrifice and an eternal priesthood was installed instead of a continual changing of one. Doesn’t it make sense the law of God was also changed? Well that’s exactly what it says in Heb.7:12 “For the priesthood being changed, of necessity there is also a change of the law.”
  So we see the priesthood as well as the sacrifices, in the law were changed yet Jesus upheld these during his 3 years of his ministry on earth. So his command “teaching them to observe all things that I have commanded you,” is focused on the instructions after the resurrection not on all the ones before, unless applicable.

  The Old Testament Covenant was never intended to be permanent. (Gal.3:17-18, 22-25) Jesus used two examples in a parable to show the new is not to be joined with the old, (Luke 5:36-39) V.36 “No one puts a piece from a new garment on an old one; otherwise the new makes a tear, and also the piece that was taken out of the new does not match the old.”Heb.8:13 “In that He says “a New Covenant,” He has made the first one obsolete…”. Paul describes the Mosaic covenant in 2 Cor.3: 7 the HOLY SPIRIT tells us, is “passing away” and is “abolished” (verses 11,13), in its place we have the “ministry of the Spirit” and “the ministry of righteousness” (verses 8,9).
  Jesus did not come to destroy the law but to fulfill it. To have it put aside. If continued it would become much the worse, even for the purpose for which it was intended; Jesus did not come to patch up Judaism, he came to fulfill it by his life teaching death and resurrection, not to patch up the old. Jesus’ purpose was expanded beyond Israel, to all mankind through his spirit something that could never be done under the old administration of the law.
  V.37 “And no one puts new wine into old wineskins; or else the new wine will burst the wineskins and be spilled, and the wineskins will be ruined. v.38 “But new wine must be put into new wineskins, and both are preserved. The old wineskins were stretched out to their limit and any more fermentation would burst them. To try and mix the old (law) with the new (gospel) would destroy both. You are not saved by Jesus plus Moses, neither is one sanctified by Jesus plus Moses. V.39 “And no one, having drunk old wine, immediately desires new; for he says, ‘The old is better. ”
  Once the wineskin was used and stretched it could not be stretched more, it was useless and a new wineskin was needed. The Pharisees held on to the old law but those who found Christ to be their all in all found life in the new, they left the old for the new.

  We are under the new law of Christ NOT the law of Moses. Some of the Old Testament laws are ratified in the new covenant and some are not. He did not polish up the Old Testament laws to shine better. The moral laws continue, as they are reaffirmed in the New Testament because they preceded the law of Moses (you shall not kill, no adultery, no lying or stealing). Man was created in the image of his maker and so had a moral likeness in his nature, though now flawed. These moral laws were relative to mans moral nature that was made in God’s image.

  Rom 3:19-20: “Now we know that whatever the law says, it says to those who are under the law, that every mouth may be stopped, and all the world may become guilty before God. Therefore by the deeds of the law no flesh will be justified in His sight, for by the law is the knowledge of sin.”
  In Romans 7 (which makes a good study on this topic), he makes the argument of a bride to her husband. That if one dies the other is not longer bound. Rom 7:4: “Therefore, my brethren, you also have become dead to the law through the body of Christ, that you may be married to another– to Him who was raised from the dead, that we should bear fruit to God.” V.6 “ But now we have been delivered from the law, having died to what we were held by, so that we should serve in the newness of the Spirit and not in the oldness of the letter.

  This is why Paul could say “the life which I now live in the flesh I live by faith in the Son of God, who loved me and gave Himself for me. I do not set aside the grace of God; for if righteousness comes through the law, then Christ died in vain.”
  Therefore, if Christ fulfilled all the law why do some try to bring people back under its bondage? I have found that it is because they have not studied the covenants carefully enough to discern which one to live under, therefore their confusion continues.

 54. Siyi, umeulizwa maswali rahisi sana na Mkandya, mf “Wapi katika wakati wa Edeni kulikuwa na amri ya usizini kwa mfano?” Umeshindwa kutoa jibu badala yake unaleta stori! Sema inachosema Biblia yako acha kuongeza ongeza, unaulizwa Edeni, unaanzisha stori za Sinai na Ukaldayo, sijui Mungu wa baba zako, Hivi Adamu alikuwa na baba yake mwingine huko Edeni? Unafanya makusudi kutuchanganya!??

  Jambo kama hili la Mathayo 5:28 “…lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”, ambalo ni sehemu ya kule kutimilizwa kwa Torati, yaani sasa limekuwa magnified, kwamba badala ya kumkamata mzinzi mmoja huko kwenye Agano la Kale, sasa wanakamatwa kwa mamilioni kila dakika kuanzia mitaani mpaka kwenye maruninga; hivi mnadhani kuwa hiyo Torati iliyotimilizwa inawahusu Kanisa? HAIWAHUSU hata chembe, yeyote anayefikiri kwamba Kanisa wanahusika, basi hajaelewa kilichofanyika msalabani; “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rum 8:14), hao ndio Kanisa ambao Laana ya Torati imeondolewa kwao!

  Kwahiyo hao wanaoendelea katika Torati, hao ndio inawahusu hiyo Torati iliyotimilizwa, “…maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.” Kwahiyo ukimuona mtu anayejidanganya kwa kuigawa Torati mafungu mafungu ili kukwepa kuitimiza yote, basi jua mtu huyo akili zake zimelala! Mungu hakuzuii kubaki katika Torati kama unaipenda, ila unatakiwa kuyatimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, hakuna mambo ya mipango mipango, eti oh hii ya maadili, hii ya kafara; endelea kutoa kafara kama wenzio kule Israeli, vinginevyo unaangukia katika Laana!!!

  Wengi wanang’ang’ana na jambo hilo pasi uelewa kamili wa madhara wanayoyaendea. Aliyeileta Torati na magumu yake ni Mungu, na sasa anaifanya kuwa NGUMU zaidi kwa wote watakaobaki katika hiyo, maana wanawe amewawekea ‘Moyo mpya, na roho mpya, na kuwajaza Roho wake’ akiwaongoza katika maisha mapya, maono mapya, yaani ni viumbe wapya, uliwahi kusoma popote pale kwamba Kristo alimtamani mwanamke?! Basi sasa Kristo yumo ndani ya Kanisa lake akiliendesha, huo ndio MUUJIZA MKUBWA kuliko yote iliyowahi kutendeka duniani!!!

  Nikimnukuu ndg mmoja mwenye kuyapenda sana Maandiko, yeye katika tafakari ya Mt 17:1-8 mambo yaliyotokea pale mlimani, “Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.” Basi akasema, Musa aliwakilisha Torati, Eliya aliwakilisha manabii; kwa hiyo hizo zote zilikuwa ni sauti ya Mungu katika nyakati zake, naye Petro amezitii hizo maisha yake yote, kama yule kijana Tajiri, na kulithibitisha hilo, anataka kujenga vibanda vitatu, ili azisikilize sauti zote tatu! Lakini anaambiwa, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; MSIKIENI YEYE”! Hii ndiyo ORDER MPYA, msikilizeni Kristo! Basi Kristo yumo ndani ya mitume wake, hivyo tunapaswa kuwasikiliza hao, kama wametuambia Agano la Kale ni kuukuu, ukiwa na Roho aliyekuwa ndani ya huyo anayekuambia hilo ni kuukuu, utaelewa hivyo kwa kuuona Upya wa hilo Jipya, kama uko kidini saana, basi utabaki na wale Wafarisayo waliolishona pazia lililopasuka wakijiaminisha kuwa Mungu yumo kwenye hekalu lao, mpaka alipowafikia Titus!!

  Kristo ndiye TORATI MPYA, fuata wanachofundisha mitume, mambo ya rohoni ni vigumu kufahamika mwilini, tutazunguka sana jangwani bila RM, maana hapatikani isipokuwa tuitii Injili iliyohubiriwa na mitume! Tu Jinyenyekeze wapendwa!

 55. Kaka Mhina,
  Mungu akubariki kwa majibu yako mazuri. Binafsi nimejifunza mambo mengi sana kutokana na majibu yako. Ni kweli ulivyosema kuwa japo hatuonani kimwili but tuko pamoja katika ulimwengu wa roho. Bwana akubariki sana rafiki. Labda nitoe rai kwako na wengine. Najua kuwa hudhamirii ila tu ni kujisahau. Naomba tunapoandika majina haya, ya mungu na yesu, kama tunamaaminisha Mungu na Yesu yule mwokozi. Tafadhari nawaomba, tuweke hiyo tofauti, maana kuna mungu wengi na yesu wengi sana leo duniani.
  Baada ya maneno hayo, niseme kuwa, sijachanganya mambo hapo kaka. Naomba nieleweke kuwa, kuna torati iliyoondoka ambayo ni sheria za maagizo, sheria ambazo zilikuwa za KIMWILI TU. Hizi ndizo zilizoondoka kaka Mhina. Nitakutumia ushahidi wa kimaandiko ili nikueleweshe kaka. Mgawanyo wa torati huu unafahamika kwa mwanatheolojia na mwanafunzi wa Biblia yeyote.
  Uhuru unaouzungumzia kaka Mhina, uko sahihi. Maana unasema tunaishi chini ya uhuru, uhuru wa kuzifuata sheria takatifu za Mungu. Hakuna adhabu yoyote ya papo hapo utakayopata kutoka kwa Mungu kwa sababu umeiba, umezini, umevunja sabato, umeabudu sanamu nk. Sheria za maagizo, hazipo tena. Kilichopo leo, ni ile hali ya kwanza/awali ya kutii uishi au kuasi halafu ufe!! Adamu alipoasi, hakufa palepale japo sheria ilisema hakika utakufa. Mungu leo anatuhitaji tumpende kutoka mioyoni. Upendo huo wa mioyoni, utadhihirika kwa matendo yetu ya nje ya kila siku, maana upendo au imani bila matendo imekufa. Yakobo 2:17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.Yakobo 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
  Kwa hiyo, kinachohitajika leo, ni kuonesha matendo yetu kwa Mungu kuhusu hicho kilichopo mioyoni mwetu yaani upendo. Na upendo kaka Mhina Biblia inasema kuwa ndiyo utimilifu wa sheria (basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.Warum 13:10).
  Upendo wa kweli kaka Mhina, daima huongoza kwenye utii. Huwezi kusema unampenda mtu halafu huyafanyi akutakayo kufanya. Na anasema wazi kabisa, kwamba, ili nijue kuwa Mhina unanipenda, shika amri zangu yoh 14:15. Utashika kivipi? Kuanzia rohoni, ambako kutadhihirishwa nje yaani kwa matendo. Najua bado hujanielwa hapa!! Sikiliza kaka, angalia mf. huu: Mathayo 5:28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Ukiangalia kwenye zile sheria za KIMWILI, yaani sheria za maagizo, kwa kauli hii ya Yesu, haikuwa na tatizo kwa mtu anayetamani tu ila ni mpaka kwa yule atakayekamatwa kabisaa akizini. Yesu alikuwa anasema nini hapa? Yesu alikuwa nasema kuwa, dhambi huanzia moyoni. Kabla mtu hajaonekana anaiba, anazini, anavunja sabato, nk, akishawaza tu moyoni kufanya hivyo, tayari hana tofauti na yule aliyefanya kabisa kwa mwili. Na hii ilikuwa na maana kwa Mungu, maana YEYE huangalia moyo bali binadamu huangalia mwili tu. Yesu alikuja kuiandika torati ya maadili ndani ya mioyo ya watu wake. Mungu alitaka watu wake wawe safi kuanzia mioyoni mwao.
  Sasa kushika kwa sheria hizi mioyoni mwetu, kunatufanya tuzidhihirishe kwa amtendo yamwili. Kivipi? Kwa sababu hautamani mabinti/wake/waume za watu, automatically hautazini. Kwa sababu hautamani vya watu, automatically, hautaiba, kwa sababu moyoni mwako kuna sabato, siku ya sabato utapumzika kumwabudu Mungu siku nzima na siyo siku ya kwanza ya juma. Kwa sababu ndani ya moyo wako kuna upendo wako kwa wazazi, ndg nk, automatically, wazazi utawatunza, ndg utawatendea yale upendayo wewe utendewe. Na hii ndiyo maana ya Pendo kuwa ni utimilifu wa sheria. Kama kweli tunampenda Kristo, ni sharti tutii sheria zake za maadili. Na huu ndiyo uhuru tulio nao katika Kristo, kwamba, hatutii sheria za maadili kwa kulazimishwa. Tunatii tu kama matokeo ya upendo ulio ndani yetu. Sheria kufanywa kuwa za moyoni, haikuwa na maana kwamba, mwili haupaswi kuzitii!! Yaani haiwezekani ukasema kuwa, tunazitiii sheria kwa uhuru wa rohoni, lakini hapohapo mwili wako unawaka tamaa. Utii wa rohoni, hujidhihirisha katika utii wa mwili.
  Aidha, kwenye tafsiri yako ya torati kwenye walawi 18:4-5).(kutoka 19:8)…., napenda nikuulize kuwa, hivi Mungu alipomwambia Adamu kuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usiyale; lile agizo lilikuwa ni torati au halikuwa torati? Na kama ilikuwa ni torati, ilikuwa ni torati gani ile? Ya Musa au ya Mungu mwenyewe? Na kama haikuwa torati, agizo lenyewe lilikuwa ni nini/sheria gani? Maswali haya yatakuongoza kwenye kuijua torati ni nini na isiyo torati ni ipi. Peruzi peruzi tu, utaona…
  Kaka Mhina, kilichobadilika pale msalabani, ni adhabu ya papo hapo kwa mdhambi, lakini matokeo ya dhambi bado yako palepale. Mtu asipompokea Yesu na kuenenda kama anavyotaka, bado adhabu kwa mtu huyo iko palepale. Agano la jipya, halilipingi agano la kale.
  Kaka, ukisema kuwa kushika sheria ni mazoea, mimi sikuelewi. Hivi unataka kuniambia kuwa, Mungu alikuwa alifanya mazoea katika mwanzo 2:1-3? Je, na katika kutoka 20:8-11 Mungu aliwaambia waisrael wafanye mazoea? Akina Ibrahim, Isaka, Yakob nk walifanya mazoea katika ibada? Yesu naye alikuwa na mazoea tu ya kwenda kusali siku ya sabato? Na kama alikuja kutangua torati hiyo, kwa nini asingesema kuwa haya ni mazoea tu, bali inatakiwa watu wasali j2-siku ya kwanza ya juma? Mitume nao walikuwa na mazoea vilevile? Hivi, kushika sheria za Mungu kumbe ni mazoea kaka? Sasa hata kama yatakuwa ni mazoea, wewe unaposali j2, unafuata mazoea ya akina nani? Anyway kama Biblia imeandikwa kusali jmosi ni mazoea, wewe unasoma wapi kusali j2 ni mazoea ili na wewe uyaendeleze hayo mazoea? Najua kuwa unatafakri nzuri sana kaka Mhina. Iweke pia na hapa ili ikupe jibu toshelevu na makini.
  Kuhusu sabato za Kol 2:16-17, hizi zilikuwa ni sabato za kiutamaduni za wayahudi. Hazikuwa sabato za Amri ya nne!! Zilikuwa ni sabato miongoni mwa sabato za kijadi zilizotokana na sheria za Musa. Mf, kulikuwa na sabato za miandamo ya miezi(sijui leo ungeiitaje na hiyo nayo), sabato za mwaka, sabato za mavuno, za kuhifadhi nafaka, nk. Ukitaka kuelewa vizuri, nenda hata google tu uandike background ya epstle of colosians, utajifunza mengi. Aidha, Andika tena neno mishna utaziona sabato hizi ninazokueleza hapa kuwa zilikuwa ni tofauti kabisa na ile sabato ya amri ya nne-sabato ya kumwabudu Mungu.
  Kuhusu vyakula, Kwanza inabidi uelewe kitu kiitwacho chakula kwa mujibu wa Biblia. Halafu uangalie muktadha uliokuwa ukitumiwa na nyaraka nyingi za Paulo na Yesu mwenye kuzungumzia vyakula. Hakuna chakula ndani ya Biblia ambacho Mungu alikiita chakula, kilibadilika na kutokuwa chakula. Hakuna kitu/kiumbe ambacho hakikuwa chakula tangu mwanzo, na eti ujio na kifo cha Yesu msalabani ulikifanya kitu hicho kiitwe chakula. Katika nyaraka za Paulo anaposema msihukumiane kwa vyakula, alikuwa anazungumzia vyakula (nyama) vilivyokuwa vikitolewa kwenye kafara, kama vilikuwa vinafaa kuliwa na wacha Mungu. Mf. mbuzi mweusi uliyekuwa unampeleka kwenye matambiko, halafu akachinjwa huko usiku na kesho yake nyama ikaletwa ili watu wengine wale. Kwa wacha Mungu, hii ilileta shida, kama leo watu wanavyohoji nyama zilizochinjwa na ndg zetu waislamu-kwa maana wao kuchinja kumbe ni ibada. Kuna wakristo wameamua kuacha kula nyama hizo na kuna wengine wanazitakasa tu kwa jina la yesu halafu wanakula. Hali kadhalika kwa watu wale. Hapa ndipo mzozo ulikuwa unatokea. Nenda tena google tu uone backgrounds za hizo nyaraka, utajifunza mengi.
  Yesu hakuja kuifanya nguruwe, sungura, paka, mjusi, kambaremamba, mumi nk kuwa safi ilhali ni wanyama najisi. Mungu hajatuumbia miili hii kwa ajili ya kuipakiza tu kila kitu almradi hakidhuru papo hapo. Miili yetu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu. Mungu hapendi tuingize vitu najisi ndani ya mahekalu yake. Kama mawazo machafu tu hayatakiwi ndani ya miili hii, iweje vitu najisi? Soma vizuri Biblia yako kaka, Yesu hakufa msalabani ili nguruwe na vitu/viumbe vingine najisi viwe chakula. Huko ni kuhafifisha kusudi la Kristo kufa msalabani.
  Mambo uliyaandika ni mengi kaka Mhina. Nami nipumzike tu kwa kukushukuru kuleta insights nzuri zenye tafakari. Kama unaweza waweza nitumia email yako nikakutumia ule mchanganuo wa sheria ipi iliishia msalabani na sheria ipi bado ipo na itaendelea kudumu. Nahisi kurasa za blog yetu zinaweza zisidisplay vizuri japo nitajaribu kufanya hivyo. Nakusubiri pia kwa hoja kama utakuwa bado hujaelewa. Lete hoja, maana hata mimi nachota mengi kutoka kwako. But make sure kila tunachozungumza, ukihusianishe na Biblia-kiongozi wetu mkuu chini ya usimamizi wa Roho Mtakatifu.
  Barikiwa sana

 56. Ndg Mkandya!!
  Mimi nashukuru sana kwa kuniijia kwa hoja. Ni kweli nikubali kuwa, shida iliyoko kati ya wanaosali j2 na wasabato, iko kwenye amri ya nne tu-Sabato. Kwingine hakuna shida maana kila mtu anajua kuwa kuiba ni dhambi, kuzini ni dhambi, kuua ni dhambi nk. Tatizo huwa ni watu wangapi wanatambua kuvunja sabato nayo ni dhambi kama ilivyo kwa amri zingine Makandya? Kwa nini unafikiri hapa kuna mgogoro sana? Shida siyo kuiweka mbele jumamosi. Makandya, siku zote ziko sawa kwa urefu nk. Mungu alizipa saa 24 kila moja. Jua ni lilelile. Sasa kama ni hivyo, shida iko wapi sasa?
  Mkandya, baada ya uumbaji, Mungu alitoa utaratibu wa namna ya kumwabudu. Ili kufanya kielelezo, aliamua kupumzika siku ya saba-jumamosi. Biblia inasema kwamba, siku hiyo ya saba-Mungu alistarehe, akaibariki na kuitakasa. Mambo makuu matatu yanajitokeza hapo Makandya. Siku ile nilikwambia hivi;
  Kwanza, Sabato maana yake ni pumziko(ni neno la kiebrania shabbath means rest). Ukisoma Biblia yako hiyo Mwanzo 2 inakueleza jinsi alivyopumzika Mungu. Alistarehe siku hiyo akaacha kufanya kazi zake zoote alizozifanya kwa siku 6. Tangu Adamu hadi vizazi vya Yakobo, siku ile nilikuthibitishia kuwa, walikuwa wakipumzika siku ya sabato, hadi wanatwaliwa utumwani Misri. Misri huko walisahau taratibu zote za kumwabudu Mungu. Mungu alipoamua kuwatoa huko, Farao alijua kuwa kizazi hiki tangu mwanzo, kilikuwa na tabia ya kutunza sabato ya YAHWE. Farao anamuuliza Musa swali katika kutoka 5:5 Kisha Farao akasema, Tazameni, watu wa nchi sasa ni wengi, nanyi mnawapumzisha, wasichukue mizigo yao. Katika Biblia ya kiingereza inasema; “You make them rest from their labor” (NKJV). Kumbuka sabato nimekwambia ni nini? “Sabbath/shabbath means REST” . Farao aliifahamu vizuri historia ya Taifa la Mungu “Israel”, kuwa kupumzika siku ya sabato, lilikuwa ni mojawapo ya amri za Mungu. Nakumbuka nilikupa hadi amri zote 10. Na pale mlimani Sinai, Mungu anawaambia kwenye ile Amri ya nne, kwamba, siwapi pumziko jingine tofauti, bali ni lilelile la tangu zama za mababa zenu. Nalo halikuwa jingine kweli, maana Mungu aliwaambi, “IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE…” Maana yake nini? Siku hiyo ilikuwepo tangu mwanzo enzi za mababa zao. Haikuwa siku mpya. Na waisrael walipaswa kuenenda kama mababa zao wa zamani.
  Aidha, bwana Lenda alizungumzia vizuri sana na yeye katika mchango wake. Nina wasiwasi kama huwa unasoma maoni ya kila mtu kwenye mada hii ndg yangu Makandya.
  Pili, kitu kilichobarikiwa, ni tofauti na kile ambacho hakijabarikiwa. Mf, hivi Yakobo na Esau walikuwa sawa baada ya Yakobo kubarikiwa? Kaka Makandya, Mungu akibariki kitu, mwanadamu hawezi kutangua!! Baalamu alilijua hilo pia Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa(hesabu 22:12). Mungu hana kigeugeu kaka Makandya, kwamba abariki siku hii, halafu kesho kutwa aseme sasa nimetangua baraka juu ya kitu kilekile…Malaki 3:6). Kwa hiyo, kama Mungu aliibariki siku ya sabato, sisi nasi twapaswa kufanya vivyo hivyo. Mungu alifanya hivyo, Yesu akafanya hivyo, Mitume wote walifanya hivyo, kadhalika na sisi hatuna budi kufanya vivyo hivyo.
  Jambo la tatu ni kuitakasa siku hiyo. Kutakasa maana yake ni kukifanya kitu kiwe safi, kukitenga kwa makusudi fulani tu. Mungu aliitenga siku ya saba kwa ajili ya kumwabudu YEYE na si vinginenvyo. Jumamosi siyo siku ya kufanya mambo mema tu, bali pia ni siku iliyotengwa na Mungu mwenyewe kwa ajili ya ibaada kwa watu wake. Ni ishara ya utambulisho wa watu wake-ezekiel 20:12, 20. Na amesema kuabudu jumamosi, ni kufanya kumbukumbu/sherehe ya kutambua kuwa Mungu ndiye muumbaji wa vyote. Ukiangalia mwanzo 2:1-3, kutoka 20:8-11, ufunuo 14:6-7 nk , utagundua kuwa, wanaomwabudu Mungu, ni sharti watambue kuwa YEYE ni muumbaji wa vyote, mmiliki wa vyote na mtawala wa vyote. Na ili ufanye hivyo, ni sharti upumzike siku ya jumamosi ya kumwabudu pamoja na kutenda hayo matendo mema.
  Nilikwambia kuwa kaka Makandya, kama una ushahidi wowote ndani ya neno la Mungu, unaokuunga mkono kusali/kupumzika siku ya j2 kama siku ya ibada, ulete huo ushahidi tuuone sote. Kusali halafu tukaendelea na kazi zetu za kila siku, nina imani kila mtu hufanya hivyo kwa wale wanaomcha Mungu. Hata mimi huwa nasali asubuhi, mchana na jioni. Na hufanya hivyo kuanzia siku ya 1-6. Siku ya saba, hupumzika kabisa yaani hufanya kusanyiko takatifu kwa ajili ya ibada ya kumwabudu Mungu muumbaji tu. Hakuna kazi siku hiyo. Mimi nilikupa aya nyingi sana kussuport hoja zangu. Kama na wewe unazo kaka za upande wa pili, zilete tuzione. Lete walao hata mbili tatu tu hivi kama huna kabisa…
  Kaka Mkandya, ushahidi wa akina Ibrahimu na wengine woote wa agano la kale kuwa waliitunza TORATI ya maadili kwa ujumla wake, nilikupa siku ile. Labda kama unataka nirudie tena. Mafarisayo wao walijidai kuwa wao ni watoto wa Ibrahimu, Yesu aliwaambia, kuwa, mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngeyafanya aliyoyafanya Ibrahimu yoh 8:53…). Ibrahimu alifanya nini? Mwanzo 26:5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu. Aidha Yesu aliwaambia pia kuwa, mngemwamini Musa, mngeliniamini na mimi…Kwa nini?; kwa sababu yeye aliandika habari zangu(Yohana 5:46).

  Mkandya, sikushurutishi uje uabudu siku ya jumamosi, ila nakushauri tu maana tofauti na kumwabudu Mungu siku ya jumamosi, kaka unatukuza mamlaka ya mungu mwingine japo hujui. Kama unabisha, sema nikupe data zote na jinsi alivyouteka ulimwengu mungu huyo mnayemwabudu kwa kudhani kwa mnamwabudu YEHOVA-Mungu muumbaji. Walimu na viongozi wenu wanalifahamu hili vizuri sana. Wewe kama unataka wakupe live, wabane tu kwenye kona, nina uhakika, watakufungua akili. Kuhusu baadhi ya wasabato kupika siku ya sabato, hao wanaopiga, ni udhaifu wao binafsi. Kwenye msafara wa mamba, kenge hawakosi.
  Karibu tena
  Asante

 57. Wapendwa ndg. Zangu katika SG,
  Nimevutwa na hoja hii mashuhuri, kwa ujumla wake hoja ipo wazi na inaeleweka kimtazamo. Ila ni kujikanganya sisi wenyewe tunapochanganya mafundisho ya Dini na Neno la Mungu. Wapendwa, Dini imejaa mambo ys Mwilini bali Mungu kumjua ni mambo ya Rohoni; Biblia inasema, “Mkiijua kweli nayo kweli itawaweka huru Yh.8:32” Lakini tunajua kuwa ile Kweli ni Neno la Mungu.

  Labda niachane na hilo, nije tu kwenye ile Maada, Maana wasukuma husema, tembo mchune kama alivyoanguka, kujaribu kumgeuza nikujichelewesha! Kwakifupi kabisa, HAKUNA TORATI ILIYOTANGULIWA WAKATI WOWOTE, NA HAITATANGULIWA KAMWE! Tuyatazame maandiko.
  Kwanza, nipingane na ndugu yangu M. J. N. Siyi yeye kasema kuwa, “….Ni torati ambayo Mungu aliitoa tangu Edeni yaani kabla ya dhambi. Torati hii ipo hata kabla ya wana Israel kuwepo….” Mwisho wa kunukuu. Hilo si kweli maana, Sheria haiwezi kulitangulia kosa. Ni kosa kwanza kisha Sheria; Neno linasema, “Maana kabla ya SHERIA dhambi ilikuwemo ulimwenguni, Rum. 5:13”

  Kiukweli Torati au sehemu ama Nukta ya Torati ambayo inayoifanya Torati nzima ikamilike, haitaondolewa kabisa, kwakuwa Neno halipo nje ya unabii! Katika Uf. 22:19 inasema, “Mtu atakaeondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima,…. “ Neno katika Zab. 19:7 Linasema Sheria ya Bwana ni kamirifu.

  Neno linasema, kwenye Mathayo 5:17-20 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yadi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie”

  Hapa ndiyo kwenye mkanganiko wa wengi. Yesu katika ile Mt. 22:36, alipokuwa akieleza ipi katika Torati ni Amri kubwa kuliko zote alisema, yakwanza, MPENDE Mungu wako….na ya pilil yafanana nahii, MPENDE jirani yako…Katika Amri hizi mbili hutegemea TORATI na MANABII” kwa hiyo Torati kumbe imashikamanishwa na upendo, angalia ile Gal. 5:14-21, tunajifunza kuwa, Torati yote imefungwa na Upendo, na huo upendo ndiye Mungu mwenyewe. Nakupitia Mungu akiwa Roho mtakatifu anaiandika Torati yote ndani ya mwamini mwenyewe Yer. 31:31-34. ili tupate kufanikiwa kuzishika na kuzitenda sheria za Mungu kwa njia ya imani Rum. 14:13, kwakuwa Sheria sasa ipo ndani yetu, basi tunajihukumu wenyewe kwa kujikubali Rum. 14:22

  Tuna jua kuwa ulimwengu uligawanyika katika Mauti na Uzima, kama ambavyo Rum. 5:12 inavyothibitisha, kwa hiyo ni lazima mambo hayo yahukumiwe. Haiwezekani kuhukumiwa bila Sheria inayosimamia hukumu husika, Mhu. 12:14 inasema, Mungu ataleta Hukumuni kwa kila Kazi. Kwa hiyo Sheria ipo palepale! Kama ambavyo nilisema mwanzo, kwa mjibu wa Mt. 22:36 tunaona kuwa, sheria (Torati) imeshikamanishwa kwa Sheria (Torati) ile ya Mwanzo, mwanzo mungu kama alivyo yeye kuwa ni Roho, vivyo hivyo na Sheria zake zilikuwa za kiroho tangu mwanzo! Ieleweke tu kwamba, Mwanadamu baada ya kuasi akawa mwilini, lakini mwanzo alikuwa mfano wa Mungu, alikuwa wa kiroho kama alivyo Mungu. Torati ni sheria za Mwilini na Torati ni sheria za Rohoni! Lakini ukamilifu wa torati yote upo katika Upendo.

  Bwana Yesu, alipokuwa akijibu swali moja wapo juu utekelezaji wa mambo ya Taraka katika swala la Ndoa alisema katika ile Mt.19:7- 8,9 na 10 inasema, “….Musa kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; LAKINI MWANZO HAIKUWA HIVI,…..” Kiukweli Torati ni Sheria ya kimbingu, na haitaondoshwa kabisa, kinacho wachanganya Watu wengi wanaitazama Torati kimwili tu wakati wote, Bila kujua kuwa Mungu ni Neno, yeye ni Yule Yule jana na hata milele, habadiliki, si sura bali Neno lake! Pamoja na kwamba Torati wakati hivi sasa inatumika kiroho! Torati ilikuja na ikawa kwanza itumike kimwili kama Kivuri cha mambo ya Rohoni. Unajua, upokeaji ki matendo wa Neno la torati kwa mwanadamu ni kwamba, Torati katika Mwili NGUVU YAKE KIUTENDAJI IMO KATIKA DHAMBI 1Kor. 15:56, na Torati katika Roho NGUVU YAKE KIUTENDAJI IMO KATIKA IMANI Rum. 14:23, na Imani, imo katika upendo kwakuwa Mungu ni Pendo. Mungu ni wa mipango, hufanya mambo yake kwa utaratibu, ndiyo maana ana sema upo wakati wa kulia na upo pia wakati wa kucheka, ikiwa upo wakati wa kutawanya vivyo hivyo upo wakati wa kukusanya nk..Ulipofika wakati wake, mwenyewe akaifanya torati iyo hiyo, ikafunuliwa kiroho na kuhama isitumike kwa namna ya Mwili. Kwa sababu mambo ya Rohoni mwili hauyawezi; ukisoma ile galatia 4:4-5 inasema, hata ulipowadia utimilifu wa wakati ,mungu alimtuma mwanae ambaye amezaliwa na mwanamke,amezaliwa chini ya sheria kusudi awakomboe hao walio chini ya sheria ili sisi tupate hali ya kuwa wana. Neno linasema haiwezekani kumpendeza Mungu kwa matendo ya Sheria, kwa hiyo ilimbidi aje afe msalabani ili afanye patanisho na kutuhamisha katika nguvu za Dhambi ambayo ni mauti inayohuhishwa na Torati kimwili na kutuingiza uzimani kwa jia ya Imani kwa Torati inayosimamiwa na upendo!..

  Hebu msikie Yesu mwenyewe hapa, “…lakini kila mtu atakayemwacha mkewe isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine azini, naye amwoaye aliyeachwa azini.” Anagalia jibu la wanafunzi wake, wakati wangali wamo katika Torati ya mwilini, katika ule mstari wa 10 kwenye hiyo Mt. 19 walivyojibu, “mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivi, haifai kuoa. Tazama Bwana Yesu akiwa katika Torati ya Rohoni, alivyowafundisha, ”,…Si wote wawezao kulipokea Neno hili, ila WALIOJALIWA” unaona? Hapo kuna kutangua kokote? Sheria ni ile ile, ila upande huu ilikuwa kimwili na upande huu sasa inatumika kiroho! Kwa maoni yangu naamini kuwa Torati ipo kamili na haijatanguliwa kabisa. Ila Kama lipo andiko linalosema wazi kuwa Torati ilitanguliwa mnionyeshe ili name nipate kujifunza jambo jipya.

 58. Seyi sina vacum yoyote kama ulivyojaribu kusema, nilikuuliza maswali mepesi but logical kwa makusudi. Na kwa sehemu kubwa nilikuwa najua utakavyojibu.

  Kwa ujumla Seyi mgongano wa wakristo wengine na wasabato huwa hauko sana kwenye vitu vingine,ispokuwa kwenye suala la sabato, hapo kwa kweli mmekamatwa,kiasi kwamba mmepeleka Jumamos mbele kuliko hata ushindi dhidi ya dhambi.

  Seyi utakuwa ni mtu usiyejua kabisa kuelewa mambo kama utadhani kutunza sabato maana yake ni kukusanyika kusali siku hiyo. Mimi husali karibu kila siku ikiwemo siku ya Jumamosi.
  Na mimi nijuavyo ni kwamba maana ya kuitunza sabato ni kutenda mema siku hiyo.

  Halafu kuna jambo la ajabu kweli umesema, ”Rafiki, hakuna hata aya moja ndani ya Biblia inayokuruhusu wewe kukusanyika j2 kuabudu/kupumzika/kusali”. Hebu wewe nipe hiyo aya ambayo imenizuia kukusanyika J2 kuabudu/kupumzika/ kusali, nami nitakupa aya ambayo inaruhusu kukusanyika siku ya kwanza ya Juma.

  Halafu Seyi unataka kusema kuwa wewe husali J’mos tu na siku zingine zote huwa husali? Mbona mimi nikiwa sekondari na chuo nimekuwa nikiwaona wasabato wanasali kwa pamoja (wanakusanyika) siku ambazo si J’mosi?

  Kwani wewe ulishasoma mahali kwamba Ibrahim alikuwa anakusanyika siku ya Jumamosi kufanya ibada?

  Seyi zamani hata kupika mlikuwa hampiki, siku hizi vipi mnapika?

  Tafuta tena maana ya kupumzika kwa kutumia tafsiri asilia za biblia kisha ulinganishe na alichokisema Yesu hapa – Mathayo11: 28. Come unto me, all ye that labour and are heavy laden, and I will give you rest.
  Asante.

 59. Kaka siyi nashukuru sana kwa hoja na changamoto zako za msingi sana.Nimetafakari maelezo yako na nilichogundua ni kwamba unachanganya sana mambo….yani unachanganya mafundisho ya injili na torati kwa pamoja!.kwa mf:umechukua kauli za mungu katika (ezekiel 20:19) alivyokuwa anawaambia israel katika agano la kale ukaja kuhalalisha sabato kwenye injili…mtazamo huo sio sahihi kabisa!.Tena umejaribu kuigawanya vipande vipande torati ya mungu katika agano la kale ili uendelee kuhalalisha baadhi na nyingine useme bado zipo!.Lakini biblia inasema bwana yesu aliitimiza yote kwa ajili yetu ili tupate kumtumikia mungu kwa sheria ya uhuru.Lakini uhuru ninaouzungumzia mimi hapa ni wakufuata sheria za mungu ndani ya mioyo yetu tukiachana na adhabu za mwili kama torati ya musa ilivyokuwa ikitekelezwa LAKINI SIYO ETI KUISHI BILA SHERIA ZA MUNGU KABISA KAMA MNYAMA!!…Naomba nieleweke kuwa sikumaanisha hivyo…Amri kumi za mungu ndiyo msingi wa sheria ya mungu utakaosimama daima…tena pasipo sheria za mungu HAIWEZEKANI JAMBO,nafikiri tumeelewana hapa,maneno Mwisho wa sheria na sheria ya uhuru hayamaanishi kuishi bila kufuata sheria za mungu zilizo takatifu bali ni namna ya kuziishi au kuzifuata ikimaanisha KUZIFUATA KWA ROHO NA SIYO KWA ADHABU ZA MWILI…huu ndiyo uhuru wetu sisi wakristo aliyotupa bwana yesu kwa kuumia kwake yeye katika mwili kwa niaba yetu kwa ukamilifu wake wa mwili…ili sisi tuwe watoto wa mungu tukienenda kwa roho kwa kuwa baba mwenyewe(mungu) ni roho.Tuje kwenye hoja yako ya kushika sabato…kaka siyi umekazania sana sabato katika maelezo yako yote na hoja zako zote,je ni kweli kuna mambo ya sabato na mambo ya tule nini na nini tusile?..biblia itatujibu…fahamu kuwa mambo yote ya vyakula na sabato yalikuwa na lengo la KUUTAWALA MWILI KATIKA TORATI YA MUSA.Hebu tujiulize basi torati ni nini? Torati ni kile ambacho mwanadamu aliahidi kumlipa au kumfanyia mungu kwa kila atakacho au aagizacho.soma(walawi 18:4-5).(kutoka 19:8)….wakati injili ni kile ambacho mungu ameahidi kumfanyia mwanadamu baada ya mwanadamu huyo KUSHINDWA.soma(yeremia 31:31)(hosea 2:11)(mithali 11:22,23)(zaburi 111:9).Hivyo basi usipoelewa misingi na maana halisi ya haya maagano utachanganya mambo na kufundisha elimu isiyo sahihi kwa 100% …japo si vibaya kwani wote sisi akuna ajuae sana bali tunagaiana maarifa zaidi..labda baya ni kwamba unaweza kumsingizia mungu kua mbona hapa kasema hivi na pale kabadilika kumbe ni wewe HUKUELEWA VIZURI.Elewa kuwa Bwana yesu katika injili hakufanywa kuhani kwa mambo ya mwili na sheria bali kwa mambo ya roho akionyesha upendo wa mungu na asili yake ,ndiyo maana upendo ukawa ni mwisho wa sheria.(1yohana 2:7-10).Sasa uliuliza kwanini yesu na mitume waliendelea kufuata sabato?…mazoea ya sheria na sabato zake yalikuwa yameenea sana tangu zamani hata kabla ya bwana yesu na mitume wake kuhubiri injili…hivyo basi kutokana na mazoea yale yaliyojumuisha taifa zima la israel isingewezekana kabisa kuwabadilisha watu wote kwa maramoja ndiyo maana paulo kwa wagalatia aliwakemea baadhi ya waumini kuendelea kushika mambo fulani fulani ya mwili katika torati ya musa.(galatia 3:1-3) na ndiyo maana pia kwa hekima mitume wale hawakukurupuka na kuchagua wakati ule kubadilisha kila kitu kwa maramoja!.hata bwana yesu mwenyewe,biblia inasema aliishi chini ya torati ili awakomboe hao walio chini ya hiyo torati.ukisoma kwa makini barua za mtume paulo anasema..NILIKUBALI KUISHI KWA HALI ZOTE NA WATU WOTE ILI NIWAPATE NA KUWAPELEKEA INJILI YA KWELI YA KRISTO.Kwa hiyo ndugu siyi hiyo mistari uliyotoa haihalalishi au kuonyesha kuendelea kwa sabato cha msingi ni kuielewa injili kwa ujumla.hebu tuichambue hiyo mistari..ulitoa (matendo 15:21)…inasema: kwamaana tangu zamani za kale musa anao watu wahubirio mambo yake katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi…hapo tumeona kumbe ulikuwa ni utaratibu wa torati ya musa tangu zamani watu uhudhuria sabato! Sasa tujiulize angewezaje paulo kuwahubiria neno la injili bila kujumuika nao kila sabato ,wakati hata yeye mwenyewe alikua chini ya huo utaratibu? Utanisaidia mawazo kaka siyi.tena( matendo 18:4) inasema”AKATOA HOJA ZAKE KATIKA SINAGOGI KILA SABATO AKAJARIBU KUWAVUTA WAYAHUDI NA WAYUNANI…umeona hapo…kumbe paulo lengo lake kubwa lilikuwa ni kutoka mji hadi mji nyumba hadi nyumba,Sinagogi hadi sinagogi ili kuwapelekea watu hoja na injili ya bwana yesu!!.pia soma (matendo 13:44-46).Nimalizie na vyakula ambapo karibu mitume wote wa bwana yesu na bwana yesu mwenyewe walifundisha na kutukataza kabisa kumhukumu mtu kwa mambo ya vyakula ijapokuwa mimi mhina sili kitimoto kwa sababu ambazo ni zakimazoea lakini lazima nieleze ukweli kuwa kula au kutokula kwa wateule wa mungu hakuwapunguzii wala kuwaongezea chochote.Kwanza tumuangalie bwana yesu mwenyewe kasemaje?…(mathayo 15:11) “SIKILIZENI MFAHAMU SICHO KIINGIACHO KINYWANI KIMTIACHO MTU UNAJISI BALI KITOKACHO KINYWANI NDICHO KIMTIACHO MTU UNAJISI…Sasa basi pombe sumu na vitu vyenye kuleta madhala ya mwili na roho havifai lakini kitu kisichoweza kutuathili kwa mujibu wa maandiko ni ruhusa,kwa hiyo basi kila mtu na apime matumizi yake mwenyewe na si kuhukumiana.Mtume paulo nae(1wakorintho 8:8) aweka wazi kabisa pale anaposema”LAKINI CHAKULA HAKITUHUDHURISHI MBELE ZA MUNGU MAANA TUSIPOKULA HATUPUNGUZIWI KITU WALA TUKILA HATUONGEZEWI KITU.Pia soma (warumi 14:14-17).Pia msowe tito kwenye (tito 1:15).Halafu ongezea maneno zaidi ya bwana yesu kwenye (marko 7:14:23).Umethibitisha wazi wazi kaka siyi.Na kuhusu sabato pia nakupa changamoto kuwa HAKUNA SIKU YA SABATO MAALUMU KWA WATEULE WA MUNGU..kama j’mosi au j,pili nk…haitudhuru kitu kwa kuwa sabato wetu sasa ni kristo mwenyewe unatakiwa usiku na mchana ujifunze injili neno la mungu ili upate uzima wa milele.Ndugu yangu siyi lazima uelewe kuwa sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu,si mwanadamu kwa ajili ya sabato..Hivyo basi unatafuta nini wakati Yesu kristo ndiye bwana wa sabato!.thibitisha hili kwenye (marko 2:27-28).Hata paulo alimuunga mkono bwana yesu pale aliposema”BASI MTU ASIWAHUKUMU NINYI KATIKA VYAKULA AU VINYWAJI AU KWA SABABU YA SIKUKUU AU MWANDAMANO WA MWEZI AU SABATO MAMBO HAYO NI KIVULI CHA MAMBO YAJAYO BALI MWILI(SABATO YENYEWE) NI WA KRISTO.Soma(wakolosai:2-16-18).Pia ongezea na(rumi 14:5).Nimalizie na kukushukuru sana sana kaka siyi kwani hata mimi najifunza mengi kutoka kwako hivyo basi majibu yako mazuri yatanisaidia zaidi kunijenga na mungu akubariki na kukupa moyo huohuo wa kufundisha na kuifafanua vyema tena kwa bidii sana injili ya bwana wetu yesu kristo..nafahamukuwa kimwili sikuoni lakini kiroho sisi tu pamoja kuutwaa uzima wa milele.Ubarikiwe.

 60. KAKA Mtangoo, majibu yako separte haya hapaaa….
  Ha ha ha ahaaa!! Nimefurahi sana ulivyoileta hii ndgu Mtangoo. Ubarikiwe sana. Umesema vyema kabisaaa kuwa TORATI (YA MAADILI) haitaondoka kamwe. Hadi mbingu na dunia ziondoshwe. Uko sahihi sana.
  Na ukiangalia TORATI hii UPENDO utagundua kwamba, amri ya 1-4, huzungumzia upendo wetu kwa Mungu na ile 5-10, huzungumzia upendo wetu kwa ndugu zetu wote. Hata ukiangalia kwenye zile mbao mbili za mawe, zilitenganishwa hivihivi- ubao wa kwanza amri 4 na ule wa pili amri 6. Kwa hakika zotezinalenga kwenye upendo tu, kwa maana kwamba, ukimpenda Mungu automatically tu (bila shuruti) utatii utajikuta unamtii Mungu kwa kuabudu hata siku ya sabato-jumamosi kama vile utakavyowapenda ndg zako wengine na kutowafanyia hiana.
  Ukisali siku nyingine tofauti na sabato, ukala vitu najisi, ukaiba nk, utakuwa bado hujampenda Mungu kiukweli. Ndiyo maana Yesu alisisitiza kauli hizi akisema kuwa,
  Yoh 14:15(mkinipenda mtazishika amri zangu)
  Yohana 14:21 (Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake).
  Yohana 15:10 (Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake).
  Wapendwa na kaka Mtangoo, haiwezekani kushika amri 9 tu, tukaacha moja(sabato). Kama tunampenda Yesu kweli kweli, anaendelea kusisitiza ktk neno lake;
  Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
  1 Yohna 2:3-5 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
  1 Yohana 5:2-3 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
  NA HILI NDILO PENDO LAKE, TOFAUTI NA HAPO, HAKUNA PENDO.

 61. Hoja si mabishano hapa. Ila majadiliano tu yenye lenye la kueleweshana na hatimaye kufikia mwafaka. Niseme tu wewe bado hujaelewa jambo moja muhimu liitwalo TORATI. Ukiliielewa hili kwanza, utajua ni torati ipiiliyogongomelewa msalabani na ni ipi bado ipo hadi milele zote. Jaribu kuangalia mwanzoni mwa majadiliano ya mjadala huu, utapata jibu huko – sehemu ambayo mgawanyiko wa torati umefafanuliwa kwa wazi na kuonesha ni TORATI haipo na ipi IPO.
  Wanaosema kuwa siku ya Ibada ni jumamosi, kimsingi wao hawasemi ila Biblia ndiyo inayosema hivyo. Maana kama Kristo alivyotuahidi Roho Mtakatifu atakayetuongoza katika kweli yoote yaani Biblia(Yoh 17:17), bila shaka utakubaliana na Biblia kuwa siku ya ibada ya ibada Sabato-pumziko ni jumamosi. Wewe ukiabudu siku nyingine tofauti na hiyo, nina uhakika kuwa hautakuwa na unaongozwa na Roho Mtakatifu aliyeaahidiwa na Kristo kuwa atawaongoza watu wake katika KWELI(Biblia) yote. Changamsha akili tu, hili ni rahisi sana. Rejea majibu yangu ya mjadala huu kwa wapendwa Neema na Mhina hapo juu ili ujifunze zaidi. Biblia iko wazi sana ila watu tumechanganyikiwa sisi wenyewe na kufikiri Mungu anaweza kukubaliana na matakwa yetu. Mungu hana kigeugeu rafiki, kile alichosema ndicho atatekeleza…
  Karibu tena kama utakuwa na maswali. Lakini hakikisha unapitia kwanza ile makala yangu hapo juu ndipo unirejeekwa maswali yako.
  Bwana akubariki sana

 62. kwa ujumla mjadala ni mzuri sana,binafsi naweza kusema kuwa yesu alikuja kuitangua torati,mfano no pale alipopita na wanafunzi wake shambani walifanya nini,mafarisayo(viongozi wa kidini)walipo muuliza yeye alijibu nini MATHAYO 12:1-8,Torati haikuruhusu watu kuponywa siku ya sabato yesu alifanya nini MATHAYO 12:9-13,lkn mafarisayo walifanya nini MATHAYO 12:14,biblia inasema nini kuhusu siku na sabato na kung’ang’ania vyakula?biblia yangu inalo jibu,MARKO 7:1-24,RUM 14:1-9,KOLOSAI 2:16-19, Torati ilikuwa kiongozi cha kutuleta kwa kristo, GAL 3:1-29 Ndo kusema hatupo chini ya sheria maana yesu ndie mjumbe wa agano lililobora zaidi,EBRANIA 8:1-13,Pia hawa wanaosema jmosi ndio ck sahihi ya kuabudu huu ijasiri wanaupata ktk biblia gani?Mungu alisema ck ya 7 ni pumziko wao mbona wanamsingizia Mungu eti kibiblia ck ya sabato ni jmosi au wamesahau kuwa Mungu wetu wetu ni Roho YOHANA 4:24,Kaka milinga ni kweli kabisa kuwa Yesu aliitangua torati wanaobisha endeleeni kubisha,ni hayo tu,Asanteni.

 63. Lenda, bado naipitia makala yako. huenda kesho nitakuwa na majibu.
  Barikiwa sana

 64. Oooh, Kaka Mkandya,
  Mwanzo 2:16-17,
  Hii ilikuwa ni sheria ya tii uishi au asi ufe!! Sasa unaweza kuona utaiweka wapi kwenye hizo amri 10. Maana na wewe una utashi, hebu fanya hivyo.
  Wapi katika wakati wa Edeni kulikuwa na amri ya usizini kwa mfano?
  Nami nikujibu kwa kukuuliza swali, kama amri 10 hazikutolewa tangu mwanzo, Je, Yusufu(na wengine), alijuaje kuwa kuzini ni kumkosea Mungu(mwanzo 39:7-9)?? Fafanua na wewe hapa kaka.
  Halafu Seyi, ivi sabato ni sawa na Jumamosi, tena ni sawa na siku ya saba? Hebu nipe tafsiri ya sabato, siku ya saba, na siku ya kupumzika.
  Sabato maana yake ni pumziko. Kwa mujibu wa Biblia, pumziko hilo linapswa kufanyika jumamosi na si vinginevyo. Siku ya saba ni siku ya mwisho wa juma-kibiblia ni jumamosi lakini kidunia ni jumapili. Siku ya kupumzika kwa kwa mujibu wa Biblia kaka Makandya, ni siku ya jumamosi na siyo jumapili. Unaposali jumamosi hauazimishi siku ila ni ishara au alama kati ya Mungu na watu wake(ezekiel 20:20). Kama wewe ni mtu wa Mungu, sharti upumzike jumamosi ili mbingu zikutambue kupumzika na ibada zako. Kupumzika jumamosi ni kumtangaza Mungu kuwa Yeye ndiye muumbaji na mtawala wa vyote. Mwanzo 2:1-3, kutoka 20:8-11, ufunuo 14:16-17 nk .
  Seyi ni nani ambaye unadhani amevunja sabato? je ni sisi ambao tunakusanyika Jumapili kwa ajili ya kusali?
  Haswaa, unapokusanyika siku ya jpili, umeshavunja sabato ya Mungu. Maana Mungu alipumzika siku ya saba, na wewe unaamua kupumzika siku ya kwanza ya juma kwa mujibu wa Biblia. Jpili siyo siku ya ibada kwa Mungu. Ni ibada kwa mungu jua-mamlaka ya mpinga Kristo.
  Kwani kutunza sabato ni kukusanyika siku hiyo kwa ajili ya kufanya ibada/kusali? Au maana ya kupumzika ni nini?
  Maana yake ndiyo hiyo japo inaweza kutoishia hapo tu maana kuna matendo mengine mema ambayo hufanyika siku ya sabato. Waimbaji wanafahamu sana kuwa yote ambayo huyafanya, ni sehemu ya ibada. Hata kama nina dereva, siku ya sabato akiendesha kwenda kanisani kuabudu siyo dhambi na atakuwa hajavunja sabato. Yaelekea una vacum kubwa sana ya maarifa ya namna ya kuitunza sabato.
  Huwezi ukaziondoa sheria zinazolinda sabato halafu ukasema ati unaitunza sabato. Utajuaje sasa namna ya kuitunza? eg. sheria ya sabato inasema siku hiyo usifanye kazi, usitembee zaidi ya mrusho wa jiwe nk.
  Sabato na sheria zingine za maadili, tangu mwanzo watu hawakuziishi kwa msaada wa hizo sheria ndogondogo(by laws). By laws zilikuja tu baada ya dhambi. Zamani, watu walimtii Mungu kama matokeo ya upendo wao kwake. Na waliokaidi, miisho yao tunaifahamu sote. Baada ya mwanadamu kuanguka dhambini, ndipo hizo by laws zikaletwa. Yesu alikuja kuziondoa zote. Sasa tuko chini ya neema ileile ya mwanzo ya kutii uishi au kuasi ufe. Ndiyo maana leo mtu asiyemjua Mungu, Biblia inamwita ni mfu, na ukishampokea Yesu, unakuwa hai ndani yake-kiumbe kipya. Na hakuna hata aya moja ndani ya Biblia inayosema kuwa sheria ya zamani(by laws iliwapasa watu watembee mrusho mmoja wa jiwe siku ya sabato. Haipo aya hiyo ndani ya Biblia. Kama unayo wewe, ilete tuione maana tunajifunza sote.
  Lakini kwenye mchango wako wa kwanza ulisema hizo sheria za kulinda amri ndio zilizotanguliwa na Yesu. Sasa niambie kama zimetanguliwa wewe umejuaje jinsi ya kuitunza sabato.
  Hili ni rahisi sana. Kwani Adamu na wanawe, walijuaje kuitunza sabato? Kama by laws zilikuja kwa sababu ya dhambi, je, unaposoma mwanzo 2:1-3, huwezi kupata maana na namna ya kuitunza sabato?
  Rafiki, hakuna hata aya moja ndani ya Biblia inayokuruhu wewe kukusanyika j2 kuabudu/kupumzika/kusali.Tangu mwanzo hadi ufunuo, Biblia inaelekeza watu wasali siku ya saba-sabato-jumamosi. Mungu aliitunza sabato, Yesu aliitunza sabato na mitume wooote waliitunza sabato, naam amri zote kumi, wewe ni nani unakaidi maagizo ya Mungu ya kumwabudu? Aidha, nipatie aya ypoyoyte ya ndani ya Biblia, inayosema kuwa Yesu au mitume waliibadili sabato. Nami nitakupa zawadi yoyote utakayosema. Ubarikiwe sana. Jaribu pia kupitia majibu ya kaka Mhina na dada Neema niliyowapeni leo asubuhi. Yatakusaidia sana na kuondoa baadhi ya maswali yako.
  Karibu tena rafiki kama hujaelewa sehemu.

 65. Naomba nianze kwa msisitizo huu:
  “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, HATA YOTE YATIMIE” (Mathayo 5.17-20)
  YESU anaposema mpaka MBINGU NA NCHI ZITAKAPOONDOKA hivi ni kweli ameongea habari ya yeye kufa na kufufuka? sio mwisho wa dunia? kumbe ina maana kwamba mpaka mwisho wa dunia hakuna torati hata moja itakayoondoka! lakini ukomo wa torati unakuja hapa
  LUKA 10:27- Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na jirani yako kama nafsi yako!
  Hii ndiyo amri kuu na ndiyo utimilifu wa torati. Ndani ya kufuata torati kama hamna Upendo ni bure. Hata kama utashika sabato mpaka ukapitiliza kama huna upendo ni kazi bure! hata kama utabatizwa na maji mara mia tano lakini kama huna upendo ni kazi bure! hata kama hutakula nguruwe wala sungura lakini kama huna upendo ni kazi bure. UPENDO NDIYO AMRI KUU NA YA KIPEKEE AMBAYO HAITAONDOKA MPAKA UKAMILIFU WA DUNIA!
  Kwenye mijadala ya kikristo utashuhudia mijadala mingi ikiegemea kwenye ubinafsi wa mtu anachokiamini. Kwenye kanisa la kwanza hata kupeleka injili kwa watu wa kigeni ilikuwa ni kujitia unajisi lakini KRISTO alitaka INJILI IHUBIRIWE mpaka mwishowa nchi. Ukitaka ukosane na watu hubiri Upendo!
  Leo hii Mpentekoste anajiona bora kuliko mlutheri na wote wanaabudu Mungu mmoja. Mkatoliki anamdharau Msabato na wote wanaamini katika Yesu! LAKINI MBAYA ZAIDI MPENTEKOSTE WA TAG ANAMUONA MWENZAKE WA FPCT NI MUASI! AMA KAKOBE ANAMUONA MAMA RWAKATARE HAJAOKOKA NA MAMA RWAKATARE ANAMUONA KAKOBE NI MSHAMBA! MWINGIRA ANAMUONA MZEE WA UPAKO HAJUI KUFUNDISHA!
  Kama unampenda Mungu hautaona thamani ya miungu mingine na utamtengea siku nzima kwa juma ili kumuabudu. Kama unampenda jirani yako hutazini naye ili umuambukize ukimwi ama umpe mimba isiyo na baba! kama kweli una upendo utaheshimu wazazi wako! hutatamani kuiba cha jirani yako bali utajituma upate cha kwako halali. KAMA UNAMPENDA JIRANI YAKO NDIVYO UTAKUWA UNAMPENDA MUNGU.
  Matokeo yake kanisa limeshikwa na mafundisho yasiyo na msingi wa kusimamisha kazi ya Mungu bali kuligawa kanisa. Torati kuu ni upendo! UPENDO NDIYO TORATI KUU NA YA MILELE NA HAITAONDOKA MPAKA ULIMWENGU UKIONDOKA.

 66. Bwana Siyi,ukweli ni kwamba sijakubaliana na wewe. Haujaweza kabisa kuthibitisha kuwa amri kumi zilikuwepo tangu Edeni. Kwa mfano unaposema kuhusu alichoambiwa Adam katika Mwa 2:16-17 kuhusu kula matunda sioni kama unaweza kukihalalisha kuwa hiyo ilikuw ni amri ya ngapi katika amri kumi za Mungu.

  Wapi katika wakati wa Edeni kulikuwa na amri ya usizini kwa mfano?

  Ukiangalia mambo mengi uliyoolozesha yako baada ya Edeni, lakini cha ajabu umetumia muda wako mwingi kweli kuyasema hayo.

  Halafu Seyi, ivi sabato ni sawa na Jumamosi, tena ni sawa na siku ya saba? Hebu nipe tafsiri ya sabato, siku ya saba, na siku ya kupumzika.

  Seyi ni nani ambaye unadhani amevunja sabato? je ni sisi ambao tunakusanyika Jumapili kwa ajili ya kusali?

  Kwani kutunza sabato ni kukusanyika siku hiyo kwa ajili ya kufanya ibada/kusali? Au maana ya kupumzika ni nini?

  Ivi unadhani mnapokusanyika siku ya Jumamosi na kusali huko ndiko kutunza sabato kwa kutofanya kazi? Hebu waulize waimbaji na wapigaji wa vyombo wa kanisani kwenu kama huko kuimba huwa ni kupumzika. Jiulize pia wewe kama una gari au dereva yeyote ambaye huendesha gari lake kwenda kanisani siku hiyo kama kuendesha gari si kazi ila ni kupumzika.

  Huwezi ukaziondoa sheria zinazolinda sabato halafu ukasema ati unaitunza sabato. Utajuaje sasa namna ya kuitunza? eg. sheria ya sabato inasema siku hiyo usifanye kazi, usitembee zaidi ya mrusho wa jiwe nk.

  Lakini kwenye mchango wako wa kwanza ulisema hizo sheria za kulinda amri ndio zilizotanguliwa na Yesu. Sasa niambie kama zimetanguliwa wewe umejuaje jinsi ya kuitunza sabato.

  Nipe majibu ndugu yangu.

 67. NA TUITII INJILI KATIKA JINA LA YESU AMINA .
  1. Matatizo Ya Dunia Ya Sasa Yanatokana Na Kuasi Amri Za Mungu
  DUNIA INAOMBOLEZA, INAZIMIA; ULIMWENGU WADHOOFIKA, UNAZIMIA, ULIMWENGU UNADHOOFIKA, UNAZIMIA; WATU WAKUU WA DUNIA WANDHOOIKA. TENA DUNIA IMETIWA UNAJISI KWA WATU WANAOIKAA; KWA MAANA WAMEZIASI SHERIA, WAMEBADILI AMRI WAMELIVUNJA AGANO LA MILELE. (ISAYA 24:4)
  2. Torati ni kiongozi kutupeleka kwa kristo kwa ajili ya toba. Hivyo imetuweka huru na mauti ya kupigwa kuuwawa kama wakati wa Musa.
  “HIVYO TORATI IMEKUWA KIONGOZI KUTULETA KWA KRISTO, ILI TUHESABIWE HAKI KWA IMANI” (WAGALATIA 3:24)
  3. Mungu si kigeugeu akisema hajatangua ni kweli hajatangua kweli.
  “MIMI SITALIHALIFU AGANO LANGU, SITALIBADILI NENO LILILOTOKA MIDOMONI MWANGU (ZABURI 89:34)
  4.Biblia inasema inasema Yesu ndiye kuhani.
  “KISHA AMETAJWA NA MUNGU KUWA KUHANI MKUU KWA MFANO WA MELKISEDEKI.”(WAEBRANIA 5:10)
  5.Amri za Mungu hazibadiliki milele.Tukisema sheria hakuna basi dhambi pia hakuna. Sheria ni kioo kinachotuwezesha kuona dhambi zetu ili tuende kwa kuhani Yesu atupatanishe na Baba.
  “ KWA SABABU SHERIA NDIYO IFANYAYO HASIRA;MAANA PASIPOKUWAPO NA SHERIA, HAPANA KOSA.”(WARUMI 4:15)
  6. Kitu ambacho wanadamu tumepewa ni Agano la kuandika Sheria mioyoni mwetu kwa njia ya Upendo. Yaani Mungu anataka tuzaliwe katika upendo ndio amri zake tutazishika bila shuruti kutoka moyoni ndio maana hata anasema. Kama enzi za Musa mpaka watu wauawe ndi wengine waogope na kutii.
  “NITATIA SHERIA ZANGU MIOYONI MWAO, NA KATIKA NIAA ZAO NITAZIANDIKA” WAEBRANIA 10:16
  “KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU, KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE.” (1 YOHANA 5:2)
  7. Si kweli kusema unamjua Mungu halafu hushiki Amri zake.
  “NA KATIKA HILI TWAJUA YA KUWA TUMEMJUA YEYE, IKIWA TUNASHIKA AMRI ZAKE.” (1 YOHANA 2:3)
  7(A) Yesu bado atatumia sheria kuhukumu
  “BALI MKIWAPENDELEA WATU, MWAFANYA DHAMBI NA KUHUKUMIWA NA SHERIA KUWA WAKOSAJI” (YAKOBO 2:9)
  7 (B) KUVUNJA AMRI NI KUASI KAMA WANA WA ISRAELI WALIVYOASI NA KUFA NJIANI KUTOINGIA KAANANI HIVYO TUKIASI SHERIA NA MAAGIZO KAANANI YA MBINGUNI HATUWEZI KUFIKA.
  “TENA NI AKINA NANI ALIOWAAPIA YA KWAMBA HAWATANGIA KATIKA RAHA YAKE, ILA WALE WALIOASI? BASI TWAONA YA KUWA HAWA KUWEZA KUINGIA KWA SABABU YA KUTO AMINI KWAO.” (WAEBRANIA 3:18) // “KILA ATENDAYE DHAMBI AFANYA UASI; KWA KUWA DHAMBI NI UASI.”(1 YOHANA 3:4)
  8.Ukisema unamjua halafu hushiki amri zake wewe ni mwongo.
  “YEYE ASEMAYE NIMEMJUA, WALA HAZISHIKI AMRI ZAKE, NI MWONGO, WALA KWELI HAIMO NDANI YAKE.” (1 YOHANA 2:4)

  9.Unaposhika Amri ndio unakaa katika Pendo lake.
  “MKIZISHIKA AMRI ZANGU, MTAKAA KATIKA PENDO LANGU KAMA VILE MIMI NILIVYOZISHIKA AMRI ZA BABA YANGU NA KUKAA KATIKA PENDO LANGU” (YOHANA 15:10)
  NA YESU HAKUVUNJA TORATI YEYOTE : NDIO MAANA MAFARISAYO WALISHINDWA KUMSHTAKI KWA KUVUNJA AMRI NA MAAGIZO YA MUNGU WAKAISHIA KUSEMA “AMEWAKATAZA WATU WASILIPE KODI KWA KAISALI”
  10.Kama Yesu alishika amri na anasema tuenende kama Yeye basi imetupasa kushika amri za mungu kama Yeye alivyozishika.
  “YEYE ASEMAYE, YA KUWA ANAKAA NDANI YAKE IMEMPASA KUENENDA MWENYEWE VILEVILE KAMA YEYE ALIVYOENENDA” (1 YOHANA 2:6)

  “KWA SABABU NDIO MLIOITIWA; MAANA KRISTO NAYE ALITESWA KWA AJILI YENU, AKAWAACHIA KIELELEZO, MFUATE NYAYO ZAKE.” (1 PETRO 2:21)

  “MPATE KUYAKUMBUKA YALE MANENO YALIYONENWA ZAMANI NA MANABII WATAKATIFU, NA ILE AMRI YA BWANA YA BWANA NA MWOKOZI ILIYOLETWA NA MITUME WENU.” (2 PETRO 3:2)

  “BASI WALIPOKUWA WAKIPITA KATI YA MIJI ILE, WAKAWAPA ZILE AMRI ZILIZOAMRIWA NA MITUME NA WAZEE WALIOKO YERUSALEMU ILI WAZISHIKE” (MATENDO 16:4)

  “NISIKILIZENI, NINYI MJUAO HAKI WATU AMBAO MIOYONI MWENU, MNA SHERIA YANGU; MSIOGOPE MATUKANO YA WATU, WALA MSIFADHAIKE KWA SABABU YA DHIHAKA ZAO.” (ISAYA 51:7)

  “MAANA INGEKUWA HERI KWAO KAMA WASINGALIIJUA NJIA YA HAKI, KULIKO KUIJUA, KISHA KUIACHA ILE AMRI TAKATIFU WALIYOPEWA.” (2 PETRO2:21)

  “HAKI YAKO NI HAKI YA MILELE, NA SHERIA YAKO NI KWELI.” (ZABURI 119:142)
  11. Kama hauenendi kwa sheria na ushuhuda wa Yesu hamna asubuhi kwako.
  “NA WAENENDE KWA SHERIA NA USHUHUDA; IKIWA HAWASEMI SAWASAWA NA NENO HILI, BILA SHAKA KWA HAO HAPANA ASUBUHI” (ISAYA 8:20)
  “JOKA AKAMKASIRIKIA YULE MWANAMKE, AKAENDA ZAKE AFANYE VITA JUU YA WAZAO WAKE WALIOSALIA, WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, NA KUWA NA USHUHUDA WA YESU; “ NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI” (UFUNUO 12:17)
  12. Imani haiondoi sheria ila inathibitisha sheria.

  13.Kwa kuwa ndani ya Kristo matendo yote yanayozaliwa huwa mema hivyo, dhambi hushindwa. Na sheria kwetu si mzigo bali. Upendo wa kristo umetubidisha kuitii bila shuruti.
  “KWA SABABU HAKUNA MWENYE MWILI ATAKAYEHESABIWA HAKI MBELE ZAKE KWA MATENDO YA SHERIA; KWA MAANA KUTAMBUA DHAMBI HUJA KWA NJIA YA SHERIA.” (WARUMI 3:20)
  14.Pia tunaithibitisha sheria.
  “BASI, JE TWAIBATILISHA SHERIA KWA IMANI HIYO? HASHA, KINYUME CHA HAYO TWAITHIBITISHA SHERIA.” (WARUMI 3:22)
  15. Ukigeuza sikio na kukwepa amri za Mungu Hata sala zako ni chukizo Kwa Mungu.
  15 (B) Kama hata Yohana aliona sanduku la agano mbinguni akiwa patmos. iweje leo tuasi sheria ya mungu na ndio agano (UFUNUO 11:19)
  15 (C) SHERIA NI KIOO. ILI TUJUE TU WACHAFU WAPI TWENDE KITI CHA REHEMA TUTUBU KWA YESU.
  ANGALIENI SHETANI ASIIBE KIOO KAMA ALIVYO WABIA ADAM NA HAWA.
  “LAKINI ALIYEITAZAMA SHERIA KAMILIFU ILIYO YA UHURU, NA KUKAA HUMO, ASIWE MSIKIAJI MSAHAULIFU, BALI MTENDAJI WA KAZI HUYO ATAKUWA HERI KATIKA KUTENDA KWAKE. “(YAKOBO 1:25) SOMA PIA (WARUMI 2:13)

  “YEYE ALIGEUZAYE SIKIO LAKE ASIISIKIE SHERIA HATA SALA YAKE NI CHUKIZO.” (MITHALI 28:9)

  16. Tafsiri ya Tunaokolewa Kwa Imani ni pamoja na kuwa tukiamini tunatii sheria na maagizo kwa upendo bila shuruti kwa sababu tumelipenda na tumempenda aliyelitoa. Acha kuchukia agizo la Mungu maana ni tamu tukimpenda. Igeni mfano wa Ibrahimu aliyehesabiwa haki kwa Imani.

  “KWA SABABU IBRAHIMU ALISIKIA SAUTI YANGU, AKAYAHIFADHI MAAGIZO YANGU, NA AMRI ZANGU, NA HUKUMU ZANGU, NA SHERIA ZANGU. (MWANZO 26:5)

  15. Watu wengine wachungaji huwa wasisitiza kwa waumini msizini,msiibe n.k na waumini wao kuwa wasikilizaji tu, lakini anahubiri amri zimefutwa msalabani ukimwambia tuzini anasema “hapana mtumishi hiyo ni dhambi.” Ukimwambia umejuaje ni dhambi bila sheria ndio anakubali na kujing’ata midomo.Kumbe alipata Pesa Saccos akanunua Sub-Woofer na Maiki akaanzisha kanisa bila kusoma na kutii injili kwanza na kuhubiri “NEW AGE GOSPEL DOCTRINE YA MUUNGANO WA MAKANISA AMBAYO INASEMA AMRI IMEGONGELEWA MSALABANI” ambao wanataka kuweka dini moja duniani. Na mafundisho yale yanayotoa tafsiri tofauti ya Biblia ya tunaokolewa kwa Neema ili watu wadumu katika dhambi wasijibidishe kutii kwa Imani na kutaka Yesu awashindindie dhambi. Torati ndio inayotuongoza kwa Yesu tukaipate Neema (Wagalatia 3:24) Basi amri Mungu anawaambia hivi;
  “KWA SABABU SIO WALE WAISIKIAO SHERIA WALIO WENYE HAKI MBELE ZA MUNGU, BALI NI WALE WAITENDAO SHERIA WATAKAOHESABIWA HAKI” (WARUMI 2:13)

  “KUTAHIRIWA SI KITU, NA KUTOKUTAHIRIWA SI KITU BALI KUZIHIFADHI AMRI ZA MUNGU” (1 WAKORINTHO 7:19)

  “HIVYO TORATI IMEKUWA KIONGOZI KUTULETA KWA KRISTO, ILI TUHESABIWE HAKI KWA IMANI” (WAGALATIA 3:24)

  Tafsiri ya Mtakatifu katika Ufunuo ni Yule anayezishika Amri za Mungu na Imani ya Yesu.
  “HAPA NDIPO PENYE SUBIRA YA WATAKATIFU, HAO WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, NA IMANI YA YESU” Tukiwa na imani kwa Yesu atatuwezesha, halafu tutatenda matendo mema kwa sababu tumempenda, tukitenda mema tumesihinda dhambi na sheria tutakuwa tumeishika.
  1 YOHANA 3:18

  16.Laikini Pia Tunakuwa Huru Kwa Maana Hakuna Atakayetupiga Mawe Tukikosa Ila Kwa Imani Tutamtumikia Yeye Kwa Uhuru/Hiari Lakini Tusipoamini Na Kuchagua Dhambi , Atapaoiangamiza Dhambi Na Sisi Tutaangamizwa Na Dhambi Kwa Maana Alitaka Kuiangamiza Dhambi Peke Yake Na Sisi Tumeikumbatia Hivyo Tunakuwa Tumechagua Kufa Na Dhambi Zetu.

  “BASI TORATI NI TAKATIFU, NA ILE AMRI NI TAKATIFU, NA YA HAKI, NA NJEMA.” (WARUMI 7:12)

  “BASI JE! ILE ILIYO NJEMA ILIKUWA MAUTI KWANGU MIMI? HASHA! BALI DHAMBI, ILI IONEKANE KUWA NI DHAMBI HASA, ILIFANYA MAUTI NDANI YANGU KWA NJIA ILE NJEMA, KUSUDI KWA ILE AMRI DHAMBI IZIDI KUWA MBAYA MNO.” (WARUMI 7:13)
  “LAKINI NI NYEPESI ZAIDI MBINGU NA NCHI VITOWEKE, KULIKO ITANGUKE NUKTA MOJA YA TORATI.” (LUKA 16:17)

  HII NDIYO JUMLA YA MANENO; YOTE YAMEKWISHA SIKIWA; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU. (MHUBIRI 12:13)

  “HIVYO TORATI IMEKUWA KIONGOZI KUTULETA KWA KRISTO, ILI TUHESABIWE HAKI KWA IMANI” (WAGALATIA 3:24)
  ROHO WA MUNGU ATUONGOZE SISI WENYE DHAMBI.AMINA.

 68. Shalom Dada Neema na kaka Mhina!
  Nimefurahishwa na majibu yenu mazuri. Yamejaa HOJA za kimaandiko vizuri. Tatizo nililoliona katika majibu yenu, bado umnajumuisha torati zote. Aidha, nawapa changamoto ili na ninyi mjaribu kufikiri zaidi ya hapo. Ikiwa TORATI ZOTE ZILIISHIA MSALABANI, je, kwa nini Yesu aliifundisha sana baadhi ya TORATI hizo? Mf. Torati ya maadili ikiwemo sabato, Yesu aliifundisha kwa maneno lakini pia kwa matendo. Angalieni aya hizi.
  Marko 1:21 Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.
  Marko 6:2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
  Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
  Luka 4:31 Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;
  Luka 13:10 Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.
  Luka 6:6 Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.

  Mitume wa Yesu nao baada ya Yesu kupaa kwenda zake mbinguni, waliendelea kuziishi hizo baadhi ya hizo TORATI? Mfano
  Siku ya sabbato(ambayo ni mojawapo ya torati), waliendelea kwenda kanisani. Angalieni haya hizi;
  Matendo ya Mitume 13:14 Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi.
  Matendo ya Mitume 13:42 Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.
  Matendo ya Mitume 13:44 Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.
  Matendo ya Mitume 15:21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.
  Matendo ya Mitume 16:13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
  Matendo ya Mitume 17:2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
  Matendo ya Mitume 18:4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani
  Paulo bado anasisitiza
  Waebrania 4:9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
  Dada Neema na Kaka Mhina, Luka 24:44, Warumi 10:4, 8:3,4, hazimaanishi kuwa kuondolewa kwa TORATI ZOTE. Hizi hurejelea kuondolewa kwa suluhisho kaimu wa dhambi(sheria za maagizo-rejea kwenye hoja zangu hapo juu), kwa maana Suluhisho mwenyewe halisi(Yesu Kristo) alikuwa amekuja. Baada ya kifo cha Yesu, hakuna taabu tena ya kutafuta kondoo wa kafara, mbuzi njiwa wala kupondwa mawe kwa sababu mtu ameiba au amezini. Yesu aliondoa shida ile na kuifanya sheria (torati nyingine iliyosalia), iandikwe ndani ya mioyo ya watu-kuitimiliza. Kwa maana kwamba, unapompokea Yesu na kumjifunza ukamjua, huhitaji tena kushurutishwa (na sheria za maagizo) kutozini, kutoiba, kutoabudu sanamu nk kwa sababu ulishamjifunza huyo Pendo na huwa unatenda kama matokeo ya upendo wako kwake. Kumpokea na kumjua Kristo kiundani kabisa, kutakufanya automatically, utii torati ya maadili, vyakula na zingine zote zilizosalia. Maana Yesu mwenyewe anasema,
  Yoh 14:15(mkinipenda mtazishika amri zangu)
  Yohana 14:21 (Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake).
  Yohana 15:10 (Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake).
  Dada Neema na Mhina, na haiwezekani kushika amri 9 tu, tukaacha moja(sabato). Kama tunampenda Yesu kweli kweli, anaendelea kusisitiza ktk neno lake;
  Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
  1 Yohna 2:3-5 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
  1 Yohana 5:2-3 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
  Wapendwa, nabii Isaya na Yohana mwanafunzi wa Yesu walioneshwa kuwa mbinguni tunakoenda, watakatifu watatunza sheria zote za maadili ikiwemo sabato. Nabii Isaya alioneshwa watakatifu wakienda mbele za Mungu kuabudu siku ya Sabato mbinguni. Yohana naye alioneshwa sanduku la Agano (la Amri 10 ikiwemo sabato) liko hekalu la mbinguni.
  Isaya 66 :22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
  Ufunuo 11 : 19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
  Hitimisho langu kwenu, Mungu anasema;
  Ezekiel 20 :19 Mimi ni Bwana, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda;
  20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

  Bwana awabariki mnapotafakari maandiko haya.
  Karibuni tena kwa hoja tusemezane katika pendo la Kristo.

 69. Shalom Mkandya.
  Nakushukuru kwa kuleta hoja nzuri. Niende kwenye maswali yake moja kwa moja..
  Je unaweza kulithibitisha hilo, ukatuonesha kwenye maandiko hiyo torati ya tangu Edeni?
  Ndugu yangu Mkandya, Soma kwanza kutoka 20 halafu, angalia uthibitisho huu huku ulinganisha na hizo
  Amri Kumi Kabla ya Mlima Sinali
  Baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kuhusu Amri kumi za Mungu kuwa walipewa Waisrael tu pale Mlimani Sinai na zilikuwa ni kwa ajili ya Waisrael tu. Kwa leo Amri hizo hazina kazi tena maana sisi ni mataifa watu wa Agano jipya, agano la Neema. Hoja hizo huwa siyo kweli kabisa. Na huu ni ushahidi wa baadhi ya vielelezo yakinifu vikionesha kuwa Amri 10 zimekuwa kabla ya mlima Sinai.
  Amri 10 za Mungu
  1.
  “Usiwe na miungu mingine ila MIMI”
  Mwanzo 2: 16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
  Mwanzo 15: 7 Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi. Mwanzo 17: 1 “…. Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu”. Kutoka 3: 6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. Mungu alitaka kuheshimiwa YEYE tu na si miungu wengine!!

  2.

  “Usijifanyie sanamu za kuchonga-ibada za sanamu…”
  Mwanzo 35: 2 Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu.
  3 Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea. 4 Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu. Mungu aliwataka watu wamwabudu YEYE tu.

  3.
  “Usilitaje Bure jina la Bwana Mungu wako”
  Lawi 18: 21 Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana. 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi

  4.
  “Ikumbuke Siku ya Sabato uitakase…”
  Mwanzo 2: 2-3 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Kutoka 16: 23 Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi. 30 Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba. Ndiyo maana sisi wasabato tunaamini kuwa kupika chakula/ au kununu chakula/chochote siku ya sabato kwa makusudi ni dhambi.

  5.
  “Waheshimu Baba yako na Mama yako…”
  Adamu ni mwana wa Mungu (luka 3:38). Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; Hata leo usipomtii mzazi ndg yangu, tarajia laana na masaibu maishani.

  6.
  “ Usiue”
  “Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako” Mwanzo 4:8,10.

  7.
  “Usizini”
  Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?(mwz 39:7-9).

  8.
  “ Usiibe”
  Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? (Mwanzo 3:11) Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.(Mwanzo 30:33) Awaye yote utakayemwona kuwa nayo miungu yako, yeye asiishi. Mbele ya ndugu zetu ukitambue kilicho chako kwangu, ukakichukue. Maana Yakobo hakujua ya kwamba Raheli ameiiba.( Mwanzo 31:32). Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu? Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu.(Mwanzo 44:8-9). Wapenzi, tangu mwanzo wizi ilikuwa ni ishu kubwa. Kubwa sana iliyowapeleka watu/wakosaji kwenye umauti tu.

  9.
  “Usimshuhudie jirani yako Uongo”
  Katika Agano Jipya Yesu anamtaja shetani kama muongo na baba wa huo uongo tangu mwanzo. Why?? Kwa sabau alimshuhudia Mungu uongo kwa Hawa….. “lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.(Mwanzo 3:3-5). Angalia, Hawa naye alimshuhudia Mungu uongo…. anasema “Msiyale wala msiyaguse….” Kwani Mungu alimkataza hata kuyagusa kweli??

  10.
  “Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako”.

  Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. (Mwanzo 3:6) . Tamaa ni mbaya sana wajoli. Mungu aliijua tangu mwanzo.

  Nafikiri umeuona, na kama hujalizika nao, nirudie tena rafiki. Sheria ni katiba ya Mungu. Hii haibadiliki kama zilivyo katiba za wanadamu. Mungu hana kigeugeu.
  Ubarikiwe sana.
  Karibu tena.

 70. Dada neema umechangia vyema kwelikweli!…kwa ujumla ni kwamba bwana yesu hakuitangua tourati bali ameitimiza kama maelezo ya dada neema yalivyofafanua na kueleza vizuri kwa ujumla.Biblia kwenye (galatia 4:4-5) inasema:HATA ULIPOWADIA UTIMILIFU WA WAKATI ,MUNGU ALIMTUMA MWANAE AMBAYE AMEZALIWA NA MWANAMKE,AMEZALIWA CHINI YA SHERIA KUSUDI AWAKOMBOE HAO WALIO CHINI YA SHERIA ILI SISI TUPATE HALI YA KUWA WANA.Hapa inamaanisha kuwa torati ilikaa kama mwalimu au kiongozi kwa wakati ule ili kutuleta wote kwa bwana yesu na kama bwana yesu alikwisha tukomboa kwa kuitimiza torati yote basi hatupo tena chini ya torati bali tumekua WATOTO WA MUNGU KATIKA YESU KRISTO KWA NJIA YA IMANI.(Galatia 3:23-24).Hivyo basi,ukiniuliza kuhusu mambo yote ya torati ya musa katika mwili nitakujibu hayapo tena kwa kuwa mungu mwenyewe ndiye aliyelitimiliza agano lile la kale kwa kutuletea agano jipya ili tuwe wana mbele zake na si watumwa wa mwili tena.,.na hii ni kutokana na udhaifu wetu wa mwili ili sheria zake aziandike katika ubao wa roho zetu yani tuenende kwa roho.Soma(yeremia 31:31-34).Kwa hiyo HAKI ya Mungu iliyokuwa ikipatikana kwa matendo ya sheria ya mwili…Sasa mungu kwa kumtuma yesu kristo kwa mwili uliomkamilifu aliitimiza torati ile takatifu ya mungu ili watoto wote wa mungu wajinyenyekeze kwa imani mbele zake huku wakionyesha uadilifu na utiifu wa roho wakiwa ni barua halisi ya sheria ile.Soma(2wakorintho 3:2-6).Kwa hiyo basi,kwa kuwa tumekwisha kuwa watoto wa mungu kwa roho ,mambo yale ya torati ile yanayohusu mwili hatunayotena kwa sababu sasa tumekuwa wateule wa mungu halisi yani wana wa mungu…kwa hiyo kama mtume paulo alivyofundisha haitupasi kusemana vibaya au kuhukumiana vibaya kwa mambo ya mwili kama vyakula nk.lazima tufahamu kuwa kunatofauti kubwa sana kati ya watumwa wa maagano na wateule halisi wa mungu yani SISI WAKRISTO…ni kwamba sisi tumekwishadhihilishwa mbele za mungu tukisubiri wakati tu wa kufunuliwa ile kweli ya mungu.

 71. Bwana Milinga kwanza nikupongeze kwa kuleta hii hoja, na kuonesha kile kipengele ambacho wengi huwa wanakisahau katika suala zima la torati kutimizwa na Yesu.

  Kisha naenda moja kwa moja kwako ndugu Siyi.
  Umesema kuwa amri kumi zilikuwepo hata kabla ya dhambi( ”Hizi hazikutanguliwa na Kristo. Ni torati ambayo Mungu aliitoa tangu Edeni yaani kabla ya dhambi. Torati hii ipo hata kabla ya wana Israel kuwepo. Ipo kabla ya mlima Sina ”)
  Je unaweza kulithibitisha hilo, ukatuonesha kwenye maandiko hiyo torati ya tangu Edeni?

  Na kama unakubali kuwa amri kumi leo zimefanya kuwa za kiroho katika kuzitekeleza ( ” Yesu alipokuja, alizifutilia mbali sheria zoote za maagizo na kuzifanya zile za Maadili kutiiwa kiroho zaidi. Kwa mf. Yesu aliwaambia, Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake(mtt 5:27-28) ”), unakubali pia kuwa sabato sasa ni pumziko la rohoni, yaani mtu kutoka kwenye utumwa wa dhambi, kama Yesu alivyosema kuwa njooni kwangu ninyi nyote msumbukao….. nami nitawapumzisha?

  Lakini nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa katika ule mgawanyiko wa torati Seyi.

  Asante.

 72. Shalom Mr Milinga
  Mimi naomba nichangie hii mada kwa mtazamo huu

  Tukiangalia Mathayo 5:17, Bwana Yesu alisema hajaja kutangua torati bali amekuja kuiitimiza. Akaongeza kusema kuwa hakuna hata yodi moja wala nukta moja ya torati itakayo ondoka hata yote yatimie yaliyo andikwa katika torati (Mathayo 5:18). Nadhani utakubaliana nami kuwa Bwana Yesu alichosema ni kwamba hapo ambapo torati itakuwa imetimizwa yote kwa ukamilifu wake, basi itaoondoka! Vinginevyo asingezumngumzia swala la hiyo torati kutimizwa wala swala la hiyo torati kuondoka. Na hapa alikuwa akizungumza na watu waliokuwa watendaji wa torati, lakini akawaambia ni lazima haki yao iwe zaidi ya waandishi wa sheri na mafarisayo kama wanataka kuurithi Ufalme wa Mungu (Mathyo 5:19-20).
  Swali la msingi ni nani aliyeweza kuiitimiza hiyo torati? Na kama ilitimizwa ni wakati gani na nini matokeo yake kwa mwamini wa leo hii? Katika Luka 16:16 tunapata dokezo linalotupa mwangaza, kwani inasema torati na manabii vilikuwapo au vilitumika mpaka kipindi ambacho Yohana mbatizaji alikuja na tangu wakati huo alipokuja Yohana hata leo hii habari njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa. Na kimsingi ukiangalia agizo la Bwana Yesu kwa wanafunzi wake na wale wanao mwamini ni waende ulimwenguni mwote na kuhubiri habari njema za ufalme wa Mungu kwa kila kiumbe (Marko 16:15 na Mathayo 18:18-20) na si kwenda na kufundisha watu kushika torati.
  Uthibitisho mkubwa zaidi wa ya kwamba torati ilitimizwa ni maneno yake Bwana Yesu mwenyewe aliyoyasema katika Luka 24:44 “…… Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii na zaburi”.
  Natumaini mpaka hapo hakuna utata wowote kuhusu kutimizwa kwa torati au sheria! Na kama imetimizwa yote, na Bwana Yesu mwenyewe kutoa uthibitisho kwa maneno yake basi ni dhahiri kwamba imeondolewa na kwamba haiitumiki
  tena. Warumi 10:4 inasema “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria [torati], ili kila aaminiye ahesabiwe haki”. Mungu alimtuma mwanawe [Yesu Kristo] katika mwili ili ahihukumu dhambi katika mwili (Warumi 8:3) ili maagizo ya torati yatimizwe ndani ya wale wanaomwamini [Yesu Kristo] ambao wanaenenda si kwa kuufuata mambo ya mwili, bali mambo ya Roho (Warumi 8:4). Hivyo basi wanaomwamini Yesu Kristo na kuenenda katika roho [neema na kweli]hao wanakuwa nao wametimiza torati yote!
  Neema

 73. Bwana Yesu asifiwe wajoli wa Bwana SG?
  Nimshukuru bwana Milinga kwa kuleta hoja ambayo leo watu weeengi huichanganya na kudhani Mungu hufikiri kama wanavyofikiri wao. Niende moja kwa moja kwenye hoja za msingi za ndg yangu Milinga.
  Kwanza, unaposema kuwa Yesu alikuja kutangua TORATI inabidi utuambie ni torati ipi iliyotanguliwa? Ukweli ni kwamba kuna TORATI zilitanguliwa na TORATI zingine bado zipo hadi leo na mpaka kesho. Wasomi wa Biblia, wamejaribu kuzibainisha TORATI hizo katika makundi matatu (japo baadhi yao wana makundi manne au zaidi).- Torati za Maadili(Amri 10), Toarti za Maagizo(Sheria za kafara) na Torati za vyakula(sheria ya kula), Torati za mahusiano(taratibu za maisha ya kila siku) nk. Sasa twende kwenye mchanganuo wake kidogo.
  1. Torati au Sheria za Maadili(Amri 10).
  Hizi hazikutanguliwa na Kristo. Ni torati ambayo Mungu aliitoa tangu Edeni yaani kabla ya dhambi. Torati hii ipo hata kabla ya wana Israel kuwepo. Ipo kabla ya mlima Sinai, japo Mungu kaiweka bayana kwenye kutoka 20. Mungu anairudia tena kwa kizazi cha Israel baada ya kukaa utumwani kwa miaka mingi wakiabudu miungu-sanamu za wamisiri. Mungu alipoamua kuwatoa huko Misri, alitaka warudi kwenye taratibu zake za ibada ya kumwabudu YEYE- YAHWE, Mungu muumbaji. Ndiyo maana aliamua YEYE mwenyewe kuwaandikia kabisa kwa kidole chake. Hizi ndizo sheria amabzo waumini leo, hawapaswi kuziishi kimwili bali kiroho zaidi. Kivipi? Twende kwenye kipengele kifuatacho kitatuelezea namna ya kuziishi kiroho zaidi na si kimwili.
  2. Torati za Maagizo (sheria za kafara).
  Hizi zilihusu taratibu zoote amabazo watu walitakiwa kuzifanya baada ya kuonekana kuzivunja zile Amri 10. Kwa maneno mengine, kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu(uasi), Mungu aliamua kuanzisha taratibu za upatanisho kwa mtu aliyekuwa ametenda dhambi-kuvunja sheria za maadili. Zoezi hilo, lilianzia bustanini Edeni, pale Mungu alipowachinjia Adamu na Hawa kondoo kama ishara ya upatanisho kati yao na Mungu wao tena. Hadi kipindi cha Musa, Mungu alimwambia Musa, kuziandika tena kwa kizazi kile kilichokuwa utumwani maana hakikujua taratbi hizo japo mababu zao wa kizazi hicho kama akina Ibrahimu, Isaka, Yakobo nk ambao walikuwa wakizifanya sana taratibu za kafara.
  Katika kipindi cha Musa, Mungu anamwambia Musa aziandike na kuziweka pembeni mwa sanduku la TORATI ZA MAADILI(Amri 10)-Torati 31:24-27. Na kwa wakati huo, sheria hizi za maagizo zilijulikana kama sheria za Musa. Zilikuwa ni sheria ndogondogo(by laws), zilizokuwa zinawazuia watu wasivunje zile za maadili. Mf, mtu akizini, adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe hadi kufa. Hivyo ilibidi watu waogope kuvunja amri ya usizini kwa sababu ya kuogopoa kupondwa mawe. Kwa mantiki hiyo basi, utii wa Amri 10, ulikuwa wa kimwili zaidi kuliko kiroho. Yesu alipokuja, alizifutilia mbali sheria zoote za maagizo na kuzifanya zile za Maadili kutiiwa kiroho zaidi. Kwa mf. Yesu aliwaambia, Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake(mtt 5:27-28). nk. Yesu alikuja kuziondoa sheria za maagizo na kuwafanya watu watii sheria za maadili kutoka ndani ya mioyo yao na si kwa kushurutishwa na by laws. Na hii ndiyo dhana halisi ya kauli ya Yesu “ KUITIMILIZA SHERIA/TORATI”. Kuiandika ndani ya mioyo ya watu. Watu walipaswa kumwabudu Mungu na siyo sanamu, kwa sababu wanampenda, upendo wa moyoni-Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, akili zako zote….. Watu walipaswa kutowatendea wenzao mabaya kwa sababu wanawapenda kama wanavyojipenda wao wenyewe-Mpende jirani yako kama nafsi yako…. Vile wewe unayopenda wewe utendewe, watendee na wengine vivyo hivyo.

  3. Torati za vyakula.
  Hizi ni sheria za vyakula. Na zenyewe zilikuwa na by laws zake. Sheria za vyakula, zilihusu watu wale nini na wasile nini!! Na kulikuwa na sababu ya Mungu kufanya hivyo. Kwa sababu Mungu ndiye aliyetuumba, ndiye anayefahamu nini kinafaa kwa ajili ya afya zetu na nini hakifai. Ndiyo maana tangu gharika, Mungu alimwambia Nuhu aingize wanyama safi sabasaba kwa ajili ya chakula baada ya gharika kwa sababu hakutakuwa na mbogamboga, matunda wala mimea; na wanyama najisi wawiliwawili tu kwa ajili ya mbegu. Soma mwanzo 7 na 8. Na by laws zake zilikuwa ni kutokula nyama na damu yake, kutokula mafuta ya wanyama nk kwa hao wanyama safi ambao Mungu alimruhusu Nuhu kula tangu kipindi kile.
  Ukija kwa wana wa Israel, Mungu anamwambia Musa tena kuwa kuna taratibu za vyakula viwapasavyo kula. Ukisoma walawi 11 utaona anaelezea nini kiliwe na nini kisiliwe. Sheria hizi, bado zipo na zitaendelea kuwepo hadi mwisho wa wakati. Yesu hakuja kufa ili nguruwe na sungura wawe chakula. Yesu hakuja kuwafanya wafae(wawe safi) kwa afya za binadamu. Yesu alikuja kumkomboa binadamu kutoka dhambini na siyo kumletea uhuru wa kula na visivyo vyakula.
  Tangu mwanzo hadi ufunuo, Biblia imekataza watu kula wanyama najisi na vitu visivyo vyakula kama vile sungura, nguruwe, paka, punda, mijusi, panya nk.
  4. Torati za mahusiano-
  Hizi nazo bado zipo. Ndiyo maana leo waumini wakigongana wao kwa wao, usuluhishi hufanyika ndani ya kanisa. Ukisoma vitabu vitano vya Musa, utaelewa vizuri.

  Kwa kuhitimisha, ndugu Milinga, Mungu alitupatia taratibu zoote ambazo watu wake tunaweza kuishi tukimpendeza YEYE. Taratibu hizo zipo hadi leo japo baadhi ziliondolewa-yaani torati za kafara. Lakini Torati zingine kama Amri 10, Vyakula, na mahusiano hizi zipo hali leo. Na watu wanapaswa kuziishi. Kwa sababu ya watu kumpenda Mungu, wanapaswa kutoabudu sanamu ila YEYE tu, kuitunza sabato ya siku ya saba ya juma na siyo jumapili-siku ya kwanza ya juma, nk Watu wanapaswa kuwapenda wenzao na kutowaribu mabinti/vijana wao wa kiume kwa sababu wanawapenda, kutowaibia, kutowasingizia uongo nk. Na huku ndiko kumpenda Kristo-yaani kuzishika amri zake na amri zake siyo nzito.
  Ubarikiwe sana.
  Karibu sana
  nzala

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s