HALELUYA Wapendwa katika Kristo Yesu!

wapendwa

Shalom! 

Watu wa Mungu aliye hai, aliye Mungu wa uumbaji wetu katika roho na katika mwili pia! Na Mungu wa ukamilifu wetu ili kuuweka mbali udhaifu wetu maana katika yeye hatuko dhaifu, bali katika yeye tuko hai sawa sawa na neno lake kwa kuwa li hai ndani yetu, kwa kuyaishia mapenzi yake. 

Si katika kufarijiana, na kutiana moyo ili kupunguziana msongo wa mawazo na hali za maisha kwa tuyatamaniyo na kuyakosa, ama magumu tuyapitiayo, La! Hasha. 

Bali kwa kupeana uhai wa rohoni ambao kwa mwingine umekosekana, na haumo kabisa kwa namna moja ama nyingine, ili faida ya mwingine kuipata neema ya uhai wa rohoni imfufue na mwingine aliyekosa kabisa kama vile sote tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa ya dhambi zetu lakini tukawa hai tena kwa ile NEEMA ya BWANA wetu YESU KRISTO. 

Aliyotukilimia BWANA, Mungu wetu ili tuishi kama malaika walio katika umbo la mwili tukihuishana nafsi zetu sisi kwa sisi kama watoto tuliopendwa na BABA yetu aliye Juu Mbinguni kwa uweza wa Roho Mtakatifu kiongozi wetu na Mtawala wa mioyo yetu. 

Sikia; kwa sababu hiyo basi, na asiwepo hata mmoja mwenye kujivuna ama kujivunia kipawa alichopewa na Mungu ama kukinakshi kwa namna iliyo ya ulimwengu mbele za watoto wa Mungu; na kama vile UA lisivyojifunga atuapo nyuki ili kupata chanzo cha ASALI iliyo ya thamani basi hata wewe mwenye kipawa na karama ya Mungu ndivyo usivyopaswa kukunja uso wako na kuificha hiyo karama kwa wengine, bali itumie sawa sawa ili kwa hiyo na wengine wafanyike kama ile ASALI kwa tabia za UA kutoficha HAIBAZE kwa kumkilimu mgeni Nyuki hata naye akapata alichokilimiwa na kuwajaalia wengine iliyo sehemu ya kile alichokilimiwa na UA. 

Basi ndugu zangu ikiwa twaonyana na tuonyane kwa ajili ya MUNGU, maana kama kuna msafi miongoni mwetu ni msafi kwa uweza wa MUNGU walakini si kwa akili zake mwenyewe, naye hatapaswa kujisifu kwa ajili hiyo na kujitwalia kibri chenye kumletea majisifu naye akawa tena mwenye kukosa mbele za MUNGU. 

Basi ule usafi wake na ufanyike msaada kwa wengine ili nao wapate kufanyika ALAMA ya Utukufu wa MUNGU uliotukuka katika kuishi kwao, ili MUNGU aliye juu Mbinguni naye apate kujitukuza katika maisha yao. Nao wataishi kama Baraka, wala si kama laana. 

Tuweni makini na wenye kiasi katika kuleta masihara na karama tulizokilimiwa na MUNGU, kwa maana katika hayo twaweza haribu kujenga kwetu, kukawa si kujenga tena bali ni kubomoa na kuwa sehemu ya wahalifu ile kazi ya Roho Mtakatifu aliyowafunulia wengine kwa ajili ya wengine katika kusanyiko. Maana ndiyo utaratibu wa Mungu kumtumia mmoja kwa ajili ya wengi. 

Mwenye kufundisha na afundishe sawa sawa, na watu wafahamu, na mwenye kuelimisha pia aelimishe sawa sawa ili watu waelimike, kadharika mwenye kuonya na aonye ili watu wasiangamie, na mwenye kukemea pia, ili watu wajawe na HOFU YA MUNGU, Pia mwenye kukosoa na akosoe akitumia hekima ili kule kukosoa kwake kusifanyike dhihaka kwa mkosolewaji. Maana patakuwa na faida gani ikiwa kila mtu ataitumia Karama yake kana kwamba yu atafuta kujenga ufalme wake mwenyewe? 

Basi kila mmoja na atambue ya kwamba aliye Mwalimu ni Mwalimu kwa ajili ya MUNGU, na aliye Mwinjilisti ni Mwinjilisti kwa ajili ya MUNGU na Mchungaji, na Nabii, na Mtume, na Askofu, na mwingine na mwingine na mwingine wote ni kwa ajili ya MUNGU. 

Tuitambue thamani ya kusanyiko lolote, tutakalohusishwa nalo na kuwa sehemu ya wakusanyikaji, ili katika kulitambua kwetu tumtukuze Mungu kwa ajili hiyo, vivyo hivyo, pia yatupasa kuwa wenye maarifa maana katika kusanyiko lolote kwa ajili ya HAKI na wana Upotofu hawakosekani lakini yote katika yote ashukuriwe sana MUNGU aliyetutofautisha kuona na kuwaza kwao wale walio wana wa Upotofu kisha akatupa roho ya Utambuzi wa kazi za Upotoshaji wao kwa ajili ya usalama wetu kiroho. 

Basi na tuwe waaminifu mbele za MUNGU tukiwapenda watu wote kwa ajili ya BWANA. 

Mbarikiwe. 

JHU KYALA JHO NTIMI GWANGU

–Mwamfupe Anyisile

Advertisements

4 thoughts on “HALELUYA Wapendwa katika Kristo Yesu!

  1. Amen watu wa Mungu Jehova mwenye kustahili heshima na utukufu mwingi sana.

  2. n kwel kabsa haipaswi kujivunia vipawa wala chochote bali vyote tulivyo pewa viwe kwa utukufa wa baba.UTUKUFU UNA YEYE HATA MILELE AMINA

  3. Ubarikiwe Anyisile!

    Nadhani title halisi ya ujumbe huu ilipaswa iwe, “WARAKA KWA WASOMAJI SG”!! Maana nilidhani mt Paulo amerudi kazini upya!!!

    Mbarikiwe nyoote mlioupokea “waraka” huu!

    Ck Lwembe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s