Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa

burningbush

Shalom wana wa Mungu aliyejuu sana,

Ningependa leo nishirikiane nanyi katika kuhusu musa na maono ya Mungu kuokoa taifa lake Israeli

Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi/ wakristo hasa, kuna wakati tunakutana na hali Fulani au maono, au jambo au sauti ambayo kibinadamu yamekuwa yakituweka katikati. Lakini pengine hilo jambo au ono limeletwa ili kukuvusha hatua moja kwenda nyingine kihuduma na kimwili pia.

Nimejiuliza Musa asingekubali kugeuka na kutii (akasema Nitageuka sasa niyaone maono) asingeweza kukutana na kusudi la Mungu juu ya watu wake. Ebu angalia hapa  Kutoka 3:1-4, Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.  Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.

Akasema nitageuka sasa, ninachotaka kusema ni kwamba kuna mambo mengi sana hapa ambayo yamenifanya nifikiri mara mia moja,  kama yangenikuta nachunga ng’ombe kule kwetu. Naomba nieleze harakaharaka ambayo ningefikiria:

1.      Ningewezakuona kwamba huu ni uchawi, sio muijiza au maono toka kwa Mungu yamkini unaweza timua mbio: (ningekemea kwa bidiii sana kujiokoa au kuomba Mungu aniokoe.)

2.      Pili nahisi ile kusikia sauti ya malaika ningeyeyuka sana kuogopa, na rtpengine singeelewa hata anasema nini.

3.      Tatu ningeji compare kama kweli mimi ni nani hata niambiwe hivyo Imani

4.      Nne historia

Kwa nini ninge fanya hayo yote???

  • hilo namba moja, ni kwamba misingi ya imani tunaaminishwa sana kwamba uchawi unazidi nguvu ya Mungu, ndio maana tunakemea zaidi tukiamini nguvu ya shetani iko karibu yetu kuliko ya Mungu.  Mungu akikupa nguvu ya kufanyakazi yake kwa ishara na maajabu wakristo wengi bado wanadhani tu unatumia nguvu za giza. Maana nguvu ya Mungu haiwezi kuwasha kijiti.

  • hili la pili kama ningekuwa MUSA lingenikuta kwa sababu,ningehisi ile hukumu ya kuuwa watu na kukimbia labda ndio leo.kutoka212Mose akatazama huku na huko asione mtu ye yote, akamwua yule Mmisri akamficha mchangani. Maana wakristo wengi huchelewa kuamini kama Mungu kasamehe makosa yetu yoooote tuliyoyafanya.

  • la tatu ninge ji compare na wahubiri wakubwa wa leo kama yeye ambavyo angeweza jifananisha na watu maarufu wakati ule.

  • la nne ningekuwa Musa  ningeogopa ile dhambi ya kuuwa kwamba anawezaje kunitumia huku niliua??

Nikajifunza mengi sana katika imani hivi leo.  Napengine watu wengi twadhani hata tungeweza kufanya zaidi ya hao tunaojifunza kwao waliobeba imani. Lakini niseme tu leo kwamba kwa msaada Roho Mtakatifu Yohana 16:13 “lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli; atawaongoza awatie kwenye kweli yote…….” Tunatiwa nguvu zaidi. Japo waweza ona pia madhara ya shuhuda na mafundisho yenye elimu nyingi ya kuzimu kuliko ya tabia ya KIUNGU yanavyo athiri kwa kiasi kikubwa sana katika ufahamu wa muamini hasa kama mchanga.inamsababishia kukemea tuuuu hata kama ni sauti ya upole toka kwa BWANA. Pia msimamo binafsi kama huu wa Musa  kuamua kwa dhati kwamba NITAGEUKA SASA NIYAONENE MAONO. Yaani kwa Kiswahili sahihi udadisi wa kimungu. Nasema hili ukilinganisha na Petro alipoona upepo akaanza kuzama japo kwamba yeye ameambiwa atembee ktk maji. Matay0 14:30 na hata hivyo Yesu mwenyewe alikuwa akitembea juu ya maji pia.

Naona inabaki changamoto kwangu na wakristo leo, kuamua kwa dhati kuwa upande wa Mungu. Kuna wakati kabla ya kuokoka tumefanya madhambi meeengi sana,ambayo shetani hutukumbusha licha ya toba tulizofanya tukasamehewa bure bila gharama. Japo ipo madhara makubwa kwa dhambi zinazofanywa baada ya kuokoka linakua kama jembe la shetani/shoka la kunyongea. Hivyo ni kukaa vizuri na Mungu Muda woote.

Kujiepusha mafundisho ya kuzimu kama yale yatolewayo kama shuhuda ati kwamba nilikuwa kwa shetani kama mfungua geti la shetani nk, hasa kama bado neema ya kuukulia wokovu haijakaa ndani yako. Maana yakijaa ya kuzimu utahubiri ya kuzimu na neema ya Mungu iletayo wokovu hutaihubiri.

Ukiwa tayari ndani ya moyo wako, MUNGU YUKO TAYARI KUKUTUMIA haijalishi una umri gani, cheo chako kanisani, unaongeaji, usomi wako nk. Mungu huangalia utii, upole unyenyekevu na mengine mengi kama yalivyoorodheshwa kwenye kitabu kitakatifu soma maombi ya Hana ktk 1samuel2;7-8Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.

Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.

Mwisho tusimpe nafasi shetani kukumbusha dhambi zilizotubiwa. Jisamehe mwenyewe, epuka kujiingiza kwenye stress za kidunia pasi na sababu, Jitambue kama wewe ni nani,1corin7:23-24 tulinunuliwa kwa damu ya thamani; msiwe watumwa wa wanadamu. Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo. 

Barikiwa sana

–Anthony 

 

Advertisements

2 thoughts on “Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa

  1. Ahsate ndugu Athony kwa ujumbe wako mzuri umenijenga zaidi kiimani na kuona kuwa Mungu anamakusudi ya kila Mtu.Mungu azidi kukufunulia zaidi maono mengine.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s