Faustin Munishi na siasa kwenye mitandao ya kijamii!

munishi

Mwimbaji wa Injili aliyepata umaarufu mkubwa kupitia album ya MALEBO. Mbali na ndoto ya kuwa Raisi wa Tanzania, ameonesha dhahiri kujikita kwenye siasa kukosoa serikali si Tanzania pekee hata Kenya pasipo woga amekuwa akieleza hisia zake ambazo zimezua maswali mengi kwa watumishi wa Mungu na kuuliza vipi kuhusu mashairi ya nyimbo zake alizowahi kuimba kupinga kuchanganya Injili na siasa?

Baadhi ya maneno yaliyo kwenye wimbo wake wa Injili na siasa havichanganyikani:

……siasa ya wanasiasa ni uwezo wa wanadamu, uletao maendeleo kwa kila ajitahidiye, usijaribu kuchanganya vitu viwili tofauti, Injili ya Mwokozi Yesu, na maneno ya wanadamu, Neno la Mungu ni tosha, lina Roho na mwili, Injili siasa pamoja ni kama mafuta na maji ukijaribu kuvichanganya na wala havichanganyikani, Siasa huwa ni maneno, yanayosemeka vizuri, yavutia kusikia, yanashawishi akili, yamesemwa na wa kale yataendelea kusemwa siasa injili pamoja ni kama mafuta na maji ukijaribu kuvichanganya havichanganyikani.

Baadhi ya maneno aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa facebook;

RAIS JAKAYA KIKWETE AAMURU MKANDARASI NA MWENYE JUMBA LILILOPOROMOKA DAR AKAMATWE. HIYO AMRI INGETOKA KWA WAZIRI WA UJENZI AU KWA RAIS? TANZANIA RAIS NDIYE KILA KITU. HATA BODABODA HUKAMATWA BAADA YA AMRI YA RAIS.

————————————————————

UHURU YUKO TAYARI KENYA NA WAKENYA WAANGAMIE KULIKO AKOSE MADARAKA AEPUKE ICC.SI HAYO TU. KULIKO MJALUO ATAWALE KENYA.MFALME SULEIMAN ANGEAMUAJE KESI YA UHURU NA RAILA?

1WAFALME 3:16 Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake.
17 Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. 18 Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa
mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu. 19 Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. 20 Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. 21 Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. 22 Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.23 Ndipo mfalme akasema,
Huyu anasema, Mtoto wanguyu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema, Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu. 24 Mfalme akasema, Nileteeni upanga. Wakaleta upanga mbele ya mfalme. 25 Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu. 26 Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue
kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na akatwe. 27 Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake.

———————————————————-

DAR ER SALAAM TANZANIA: KUKAMATWA KWA MKUU WA USALAMA WA CHADEMA NI KOSA LA JINAI? AU UHASAMA WA KISIASA?MAHAKAMA TANZANIA ZIKO HURU KIASI GANI KUHAKIKISHA BWANA LWAKATARE HASULUBIWI KWA SABABU ZA KISIASA?ANASHTAKIWA KWA TUHUMA ZA KUPANGA NJAMA ZA KUMTEKA NYARA MWANDISHI HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI TANZANIA AMBALO NI GAZETI LINALOMILIKIWA NA NATION MEDIA GROUP YA KENYA.

JE MEDIA KENYA NA TANZANIA MNASEMAJE? CCM HAWATUMII MEDIA KUMSULUBISHA LWAKATARE? AU NI KWELI ALIHUSIKA NA MIPANGO YA KIGHAIDI?

————————————————————

KAGAME ATUMIA GENOCIDE KUWANYIMA MEDIA UHURU WA KUSEMA RWANDA. Ni marufuku Rwanda kutaja Neno “MTUSI AU MHUTU.” Kosa ni Kagame anataka wote waiter Wanyarwanda badala ya kuwataja kwa makabila yao.Lakini ukiingia kwenye maofisi ya Serikali Rwanda utawakuta watu warefu wenye pua ndefu pekee kila ofisi. Lazima utashawishika kuuliza hawa warefu wenye pua ndefu ni Wasomali? Utajibiwa ni Watusi. Utauliza Mbona ni wao tu kila Ofisi? Utajibiwa Rais ni wa kabila lao Mtusi kama wao ndiyo maana.

Sasa anayekosea ni huyu anayetaja Mtusi? Au ni Kagame anauwabagua Wahutu?

KAMA ANATAKA MAKABILA YASITAJWE AWAPE HAKI SAWA

———————————————————— 

UHURU KIBAKI NA NSIS WANAWEZA KUDHANI WANALINDA MASLAHI YA WAKIKUYU KWA SASA LAKINI WATAKUWEPO MIAKA MIA MOJA IJAYO KUIBA KURA?Kama hawatakuwepo wanawaharibia wakikuyu sifa kwa maslahi yao ya sasa.Watakaoumia ni Wakikuyu waliotapakaa kila mahali. Ruto alipowatimua wakikuyu Rift Valley wakawa IDPs Uhuru aliwapa shamba? HAPANA.

Je Kibaki aliyeiba kura 2007 Akasababisha Ruto awatimue Wakikuyu Bonded la Ufa alitoa shamba lake kuwapa Wakikuyu? Hapana. Na wengine ni IDPs hadi leo. Wakikuyu wanapaswa kuwa wa kwanza kutetea haki kwani wizi wa kura utawaumiza wao wakati hawakuhusika kuiba kura.

MUNISHI MTAMUONA ADUI LEO LAKINI YAKIWAPATA MUWE IDPs MTASEMA KUMBE MUNISHI NI RAFIKI WA KARIBU KWETU.

–Facebook

Advertisements

9 thoughts on “Faustin Munishi na siasa kwenye mitandao ya kijamii!

 1. Munishi ulianza na ROHO unamaliza na mwili kwa nini?Umeenda siasa?Tamaa ya uongozi ilikuweko wakati wa Noah kama tu sasa.WATEULE TUWE Macho!

 2. katiba ya Tanzania inamruhusu kutoa maoni yake ibara ya 20;1 sijui ya Kenya ila namshauri arudi Tanzania agombee ubunge kwa siku hizi wachungaji wengi wapo dodoma kuchunga kamati za bunge ingawa bado nasikia machangudoa huhamia Dodoma wakati wa vikao vya bunge na cc ya ccm sijui za cc za akina chadema cuf au udp

 3. Wapendwa,

  Tusidanganyane! Chagua kimoja kuwa Baridi ama kuwa Moto. Siasa za Dunia na Neno la Mungu ni vitu viwili tofauti, huwezi kumtumikia Mungu na Dunia. Siasa huongozwa na Katiba ambayo ni muongozo wa kibinadamu lakini Neno la Mungu huongozwa na Roho Mtakatifu, Biblia ndimo humo kulimowekwa Neno hili lenye uvuvio wa ajabu. Neno la Mungu humuongoza Mwanadamu afikie uzima katika Ufalme wa Mungu milele, lakini Katiba za Siasa huwaongoza watu kufikia ufanisi na uhuru wa kimwili wenye mwisho hapa Duniani.

  Wachungaji na watumishi wengine wa Mfano wa kama alikofikia Mnishi, siwatofautishi na MBWA MWITU KATIKA NGOZI YA KONDOO! Maana hujifanya waonekane tofauti na uhalisia wao, Biblia inasema Majaribu hutoka katika tamaa ya mtu mwenyewe. Watu wanaposema kuwa Mungu anawaheshimu na kuwachagua viongozi wa Mataifa kisiasa za kidunia, hawajui maana halisi ya Jambo hilo. Mungu anao wafanyakazi wa aina mbili, moja ni kutoka uzao wa Nyoka na mwingine ni kutoka uzao wa Mungu, wote hawa ni wafanyakazi wa Mungu amewachagua yeye, kumdharau mmoja ni kumdharau aliyewachagua na kuwapa hiyo kazi, ambaye ni Mungu. Ndipo andiko la Mungu linaposimama kuwa “Watu waziheshimu mamlaka” na sehemu nyingine Neno linasema, “Usimnenee mabaya mtumishi wa Mungu” Watu wengi wanaposikia Mtumishi wa Mungu, wanaangalia upande mmoja tu kuwa mtumishi huyo lazima awe mwema, Mtakatifu na kamwe shetani hawezi kuwa mtumishi wa Mungu huko ni kujidanganya kwa mwenye kupotea! Yesu anawaambia wanafunzi wake nini juu ya watumishi wake?…..” soma katika ile Yh.6:70 inasema, “70Ndipo Yesu akajibu, ‘‘Je, mimi sikuwachagua ninyi thenashara na mmoja wenu ni shetani?…..’’ (SNV-1997)

  Si kila Mtumishi aitwaye mtumishi wa Mungu ni Mtakatifu, lakini watumishi wa Mungu awe mtakatifu au asiye mtakatifu wote lazima waheshimiwe na watu, kutokana na ukuu wa aliye wachangua wamtumikie ambaye ni Mungu!

  Siasa ni kumkataa Mungu, hayupo mwanasiasa akawa sawasawa katika Neno la Mungu, kwa sababu Mwanasiasa ni mwanataasisi, siasa si mtu mmoja. Mwnasiasa hutekeleza Sela za taasisi yake, hawezi kwenda nje ya matakwa ya wenzake kisha akafanya Siasa. Sikiliza Mungu anasemaje, juu ya watu wa Mungu wanapoamua kuingia katika Siasa za Kidunia; Soma,

  1Sa:8:4-7 inasema, “4Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. 5Wakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuwekee mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.’’
  6Lakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,’’ hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba BWANA. 7Naye BWANA akamwambia “Sikiliza yale yote watu wanayokuambia, si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao.”

  Kwanini Siasa za Kidunia ni mbali na Mungu, endelea mbele kidogo usome ile 1Sam.8:8-18

  “8Kama vile walivyofanya tangu siku nilipowapandisha kutoka Misri mpaka siku hii ya leo; wakiniacha mimi na kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokufanyia wewe. 9Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.’’
  10Samweli akawaambia wale watu ambao walikuwa wakiomba wapewe mfalme maneno yote ya BWANA. 11Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake. 12Baadhi yao atawaweka kuwa majemedari wa jeshi wa maelfu na majemedari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake. 13Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji. 14Atayachukua mashamba yenu yaliyo mazuri, mashamba ya mizabibu na mashamba yenu ya mizeituni na kuwapa watumishi wake. 15Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake. 16Atawachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike na ng’ombe wenu walio wazuri sana na punda zenu atawachukua kwa matumizi yake mwenyewe. 17Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake. 18Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye BWANA hatawajibu.”

  Munishi na wenzake hawakosi ‘Sababu’ utawasikia wakisema, eti wakiwezeshwa na kuitawala Nchi ‘kilokole’, watayaendesha mambo kwa haki, bila dhuruma, ubabaishaji ama ufisadi. Hata wale wa kale ambao ndiyo mfano wa safari ya mkristo walisema hivyo hivyo, wakiwa wamejaa ubishi na sababu za kimwili, hebu ona katika ile 1Sam. 8:19-20 inasema,

  “19Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala. 20Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.’’

  Kilichoendelea baada ya wao kutaka kuishi kwa mjibu wa Siasa za kidunia, Mungu hakuwasikiliza katika taabu zao zilizosababishwa na utwala wa Sauli, hata Sisi leo tunapomwacha Mungu, na kuegemea zaidi Siasa ka Suruhisho la matatizo yenu, Mungu anakaa kimya. Ndipo utasikia Mafuriko, machinjano ya kidini, migogoro ya kuchinja Nyama, kukojolewa kwa Kruani na kuwa Ishu ya wakristo na mali zao, kupigwa malisasi kwa mapadri, dhuruma za viwanja na mshamba, migongano ya wakulima na wafugaji nk.

  Utasikiwa wapendwa anatangaza kufunga na kuomba kwa ajili eti ya Taifa liwe na suruhisho la matatizo yanayolikumba, bila ya wao kwanza kujiuliza kama wamo ndani ya Neno!

  Bwana na aendelee kutufundisha.

 4. Nikweli uongozi wa Tanzania unashida zake kwa ninavyofahamu kila sekta na kiongozi wake ila si kwaTanzania amri ya mmiliki wa jengo lililoporomoka ilitakiwa itoke kwa waziri husika

 5. Wakati anasema kuwa ‘injili na siasa ni kama mafuta na maji…’, alikuwa bado mjinga juu ya ukweli wa suala hilo. Sasa ndio ameerevuka.

  Na bado kuna watumishi wa Mungu tu wengi wanaendelea kuwadanganya watu kuwa wasichanganye siasa ma dini au injili, kama ambavyo Munishi alifanya katika huo wimbo.

  Ukweli ni kwamba huwezi kutenganisha siasa na dini, au niseme kuwa si kweli kwamba siasa na injili havichanganyikani.

  Kama unataka kuelewa vizuri ninachosema hapa chukua muda utafakari hotuba za Martin Luther King, then ujaribu kutenga siasa na injili toka kwenye hizo hotuba kama utaweza. Hotuba zile zinaweza kusikilizwa kanisani zikaleta ukombozi na zinaweza kusikilizwa kwenye jukwaa la siasa zikaleta ukombozi vilevile.

  Nimalizie kwa kusema kuwa watu wengi wakiwemo na wapendwa hasa Tanzania wamedanganywa na maneno ya mzaha kuwa ati siasa ni uongo uliochanganywa na ukweli. Na hiyo imewafanya wengi waogope hata kugombea nafasi za uongozi wa nchi, matokeo yake wakija viongozi wabaya tunakuwa wa kwanza kulaumu na kutangaza maombi ya kufunga kuombea watawala hao waovu.

  Tutafunga sana na kuomba na hakutakuwa na mabadiliko, twendeni wenyewe kwenye siasa, maana sisi tukiingia naamini tutafanya siasa safi.
  Anachofanya Munishi kukosoa watawala ndicho manabii walifanya zamani. Hawakuwa wa kwenda kunywa chai Ikulu kama maaskofu wetu wa leo.

  Big up Munishi!

 6. Kumsikia Mungu akisema ni muhimu kuliko kusikiliza hisia na mawazo yetu,

 7. Munishi mambo mengi anaongea kweli lkn naona kama uchungaji kwa sasa ameacha. mtazamo tu

 8. Mwinjilisti Munishi ni mmoja wa watu wa awali sana walionijenga kupitia nyimbo zao wakati nikiwa nimezaliwa mara ya pili, JAPO KWA WIMBO WAKE HUU SIJAWAHI KUKUBALIANA NAYE. Nadhani yeye mwenyewe ameelewa alikosea.

  Niliwahi kusema mahala fulani, sikumbuki kama ni huku SG ama pengine.
  Hapa narudia tena “INJILI NA SIASA HUWEZI KUZITENGANISHA HATA YODI MOJA”. Jambo la msingi hapa ni kujua siasa hii niizungumziayo sio “SI-HASA”.

  Kama Mungu mwenyewe ndiye aliyeanzisha mahusiano kati yake na mwanadamu, na pia ndiye aliyeanzisha mahusiano kati ya huyo mwanadamu na mwanadamu NA HATIMAYE AKAANZISHA KUWAPAKA MAFUTA NA KUWAWEKA WANADAMU WENGINE KUWA VIONGOZI JUU YA WANADAMU WENGINE, je leo hii tutasemaje Mungu hahusiki na siasa?

  Katika maandiko tunaona uhusiano mkubwa sana kati ya INJILI NA SIASA, kama siasa ya taifa ni mbovu ama watawala wa nchi ni wabovu “INJILI INAYUMBISHWA NA SIASA ZAO MBOVU” ndio maana utamsikia “mchungaji ama askofu ama mtume ama nabii” akisifia kazi za mtawala fulani ama chama fulani “madhabahuni” JAPO MTAWALA MWENYEWE NI MCHAFU AMA MWOVU HATA HICHO CHAMA CHAWEZA KUWA KIMEMTAKIRIMU KWA NAMNA FULANI”. Na watu watu kwa hakika wanajua “udhaifu huo”.
  Pamoja na hao “watumishi dhaifu” wanaopelekeshwa na wanasiasa wapo watumishi thabiti wasioyumbishwa, wao huwaelekeza na kuwafundisha watu wao kweli juu ya nchi na siasa za nchi. Kwanini wawafundishe? Ili wajue hatua za kuchukua ikiwemo maombi na tahadhari za namna mbalimbali.

  Mbarikiwe!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s