Unaamini Kuzimu ipo?

Tumekuwa tukisikiliza shuhuda nyingi za watu waliowahi kwenda kuzimu au mbinguni. Pata nafasi msikilize mama huyu Jane Kuria aliyeenda kuzimu na mbinguni kwa masaa mawili, na kuelezea Kuzimu ni kweli na Mbinguni ni kweli.

“Hell is extremely full of pain, palpable darkness, foul smell of burning bodies, cries of agony and total confusion. But heaven is extremely beautiful, calm, and full of unprecedented love” 

Je unaamini kuzimu na mbinguni vipo?

Advertisements

8 thoughts on “Unaamini Kuzimu ipo?

 1. Kaka Kabalo
  Mimi nijuavyo Biblia inasema haya juu ya wafu.Biblia na Wafu
  Kuna mkanganyiko mkubwa juu wa wafu katika imani za madhahebu mbalimbali pamoja na kwamba Biblia iko wazi sana juu ya hili. Ili kubaini nuru halisi juu ya jambo hili, ni vyema kumwomba Roho wa Mungu atuongoze kuyafahamu maandiko ya Mungu ( yaani Biblia). Katika matini hii, tutajaribu kujibu maswali yafuatayo ili yatuongoze kuelewa hali ya wafu ikoje hasa.
  1. Mtu ni nini ?
  2. Kifo ni nini ?
  3. Mfu anaweza kusikia ?
  4. Wafu huenda wapi ?
  5. Wafu wanaweza kuombewa na kusamehewa dhambi?

  Biblia inalo Jibu !!
  1. Mtu ni nini ?
  a. Ni dongo na pumzi ya uhai
  Mwanzo 2 :7
  Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
  Kwa hiyo mtu ni Mavumbi ya Ardhi
  + Pumzi ya Mungu(Roho)
  = Nafsi Hai (Mtu)
  Isaya 64 :8 Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
  Zaburi 103 :13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.
  14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

  b. Mtu ni nafsi hai. Tofauti na hapo haitwi mtu
  Kutoka 1 : 5 Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.
  c. Mara nyingine katika Biblia mtu hutajwa kama roho iliyo hai=nafsi hai kamili) Ayubu 33 :4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.

  1 Petro 3 :20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
  Matendo 241 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

  2. Kifo ni nini ?
  1. Ni kurejea tulikotoka
  Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

  2. Hali ya kukoma kuwa hai
  Mwanzo 7 :22 kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.

  3. Mtengano wa mavumbi na pumzi ya uhai
  Mhubiri 12 :7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
  Zaburi 104 :29 Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao,

  4. Ni usingizi tu
  Yoh 11 :11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.
  Mathayo 9 :24 akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.

  5. Ni pumziko la muda tu kwa walio katika Kristo
  Yoh 11 : 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
  26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?

  Fomula : Kifo ni Nafsi Hai (Mtu/Kiumbe hai)
  – Pumzi ya Uhai(Roho)
  = Mavumbi ya ardhi (Marehemu)

  3. Marehemu anaweza kusikia ?

  1. Mfu hajui neno lolote
  Mhubiri 9 :5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
  6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
  10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
  Zaburi 146 :4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
  2.
  4. Wafu huenda wapi ?
  Zaburi 146 : 4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
  Yohana 5 :28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.

  5. Wafu wanaweza kumsifu Mungu ?
  1. Hasha ! Biblia inasema
  Zaburi 115:17 Sio wafu wamsifuo Bwana, Wala wo wote washukao kwenye kimya;
  18 Bali sisi tutamhimidi Bwana, Tangu leo na hata milele.
  2. Kaburini hakuna kumbukumbu
  Zaburi 6:5 Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
  3. Sifa kwa Mungu ni kwa walio hai tu
  Ayubu 38 :17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?
  18 Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
  19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi?

  4. Wanaokufa hubaki kimya kaburini
  Ayubu 7:9 Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.

  Zaburu 146 :1 Haleluya.
  2 Nitamsifu Bwana muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.

  6. Wafu wanaweza Kuombewa na Kusamehewa Dhambi ?
  a. Wafu hawawezi kuombewa na kusamehewa.
  Hivi inawezekana kweli?? Kwani Yesu hakumwambia Yule jambazi msalabani kuwa tangu leo utakuwa pamoja name peponi!!!. Yesu alimaanisha nini hapa?? Jibu la Biblia.

  Angali Ombi la jambazi kwa Yesu;
  Luka 23 :42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
  43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.

  Inavyosomeka katika Biblia ni kana kwamba jambazi angeenda mbinguni saa ileile. Lakini kama ni hivyo, tutakuwa na utata wa aina tatu
  1. Jambazi hakuomba aende kwenye ufalme wa siku hiyohiyo.
  2. Yesu hakwenda siku ileile ya kifo chake, Yoh 20:17
  3. Jambazi hakufa siku hiyo aliyokufa Yesu, Yoh 19:30-34
  Pamoja na Yesu kuonekana kutokuwa na nguvu siku hiyo, alimwahidi Jambazi uzima wa milele tangu saa ile atakaporudi katika ufalme wake baada ya toba ya dhati ya jambazi huyo. Rejea swali la jambazi, linalenga kwenye wakati ujao…

  b. Kumbukumbu lao hutoweka….
  Hivi ni kweli?? Mbona roho huwa haifi. Na kama roho haifi, mtu huendelea kusikia, kuwa na kumbukumbu, utashi na uelewa wa kinachoendelea chini ya jua japo yeye yuko ulimwengu mwingine!!! Msamaha utakosekanaje???
  Jibu: Biblia inasema
  Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
  6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.

  c. Kama ni hivyo, kisa cha Lazaro na Tajiri kikoje?? Luka 16 :19-31
  19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
  20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
  21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
  22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
  23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
  24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
  25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
  26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
  27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
  28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
  29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
  30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
  31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

  Baada ya kusoma jiulize maswali yafuatayo!
  i. Biblia inajipinga yenyewe??
  ii. Ni kisa cha kweli hiki??
  iii. Je, kwa nini Tajiri anaomba rehema kutoka kwa Ibrahimu na siyo kwa Mungu au Yesu ??
  iv. Kama ni kisa cha kweli, mtu anaweza kuishi tena baada ya kifo kabla ya Yesu kurudi??
  v. Je, Ibrahimu huko jehanamu anasubiri kuwakaribisha wafu??
  vi. Roho za wafu huenda jehanamu??
  vii. Kama ni ndivyo au sivyo, Biblia inasemaje??

  Biblia inasema ;
  i. > Mungu hana kigeugeu, kiasi kwamba leo aseme wafu hawajui
  lolote halafu aje aseme wanajua…. Malaki 3 :6 Kwa kuwa mimi,
  Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi
  wana wa Yakobo.
   Daniel (12:1-2), Yesu (Yoh 6 : ), Mitume (1Korinth 15:51-57) wanasema wafu watafufuliwa kutoka makuburini ili wapate ijara yao sawsawa na matendo yao…
  Ufunuo wa Yohana 22:12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
  ii. Mtu hawezi kuishi tena baada ya kifo kabla ya Yesu kurudi mara ya pili. Ni hadi Yesu atakaporudi ili aamshwe usingizini.
  (Ayubu9: , )
  iii. Ibrahimu yuko kaburini anasubiri kuipokea ahadi ambayo hadi anakufa alikuwa hajaipokea.

  Waebrania 11:13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.

  iv. Roho za wafu haziendi jehanamu. Ni pumzi tu inayomrudia yeye aliyeitoa. Mhubiri 12:7
  v. Katika Luka 16:19-31, alitumia mfano tu kutoa somo maalumu kama tutavyoliona hapo chini. Hebu angalia wasifu wa wahusika hawa:
   Lazaro
  a. Maana ya jina hili ni Mungu husaidia
  b. Alikuwa ni mkoma
  c. Alikuwa masikini, ombaomba
  d. Hakuwa na mtu wa kumtunza
  e. Mwili wake ulijaa vidonda vya usaha
  f. Alikuwa rafiki wa inzi na mbwa
  g. Mpweke nk

   Tajiri
  a. Hakuwa mcha Mungu kwa dhati
  b. Hakuwajali sana watu Mf Lazaro
  c. Alidai kuwa nay eye ni mwana wa Ibrahimu
  d. Alikuwa na mali nyingi sana
  e. Alijishibisha mali yake yote yeye mwenyewe
  f. Hakurudisha chochote (1 ya 10) kwa Mungu
  g. Alikuwa na maarifa na talanta na karama lakini hakuzifanyia kazi

   Ibrahimu
  a. Anamwakilisha Mungu
  b. Anawakilisha mwamuzi wa mwisho
  c.
  Maana ya Mfano huu (Luka 16:19-31)
  Kwa uelewa sahihi wa mfano huu katika Biblia ni kwamba,
   Lazaro anamwakilisha Yesu ambaye alikataliwa, masikini(mwana wa seremala), aliyetengwa na kupuuzwa.
   Getini pa lango huwakilisha ugumu wa mioyo yetu ya kutompokea Yesu licha ya kubaini nuru halisi. Hadi leo Yesu anaendelea kubisha milangoni mwetu, lakini kwa sababu, tumebanwa na maisha, mali na anasa za dunia. Pendo lake la ajabu bado anatusihi tumfungulie…
  Ufunuo wa Yohana 3:20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
   Tajiri anawakilisha watu wanaodai kuwa ni uzao wa Ibrahimu pamoja na kwamba hawatendi ya Ibrahimu
  Yohana 8:39 Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu.
   Tajiri aliamini kuwa wokovu unapatikana kwa kuitwa mwana wa Ibrahimu peke yake. Watu wengi leo wanafikiri kumkiri Kristo peke yake inatosha. Wanasema tutakuwa na mafundisho yetu, misingi na miongozo yetu tofauti na ile ya Biblia ilimradi tunaitwa wakristo tu. Na haya yote ni ili kutimia yaliyosemwa na nabii Isaya
  Isaya 4:1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
  Salama yetu ni kuonesha upendo wetu kwake kwa kuyatii mapenzi yake na kuzishika amri zake 10.
   Jehanamu inawakilisha hali ngumu ya maisha kiroho (wasiwasi, hofu, maradhi, machungu nk.) kwa watu wasiomjua Mungu. Pamoja na kwamba matajiri wanaweza kufikiri kuwa wanamcha Mungu, wengi huwa hawafungui milango yao ya mioyo yao kumruhusu Yesu(Lazaro) atawale maisha yao badala yake hutegemea mali zao tu.
   Wanao Musa na manabii maana yake wanayo Biblia. Na waisome. Wasipoisoma, hakuna mtu yeyeyote atakayewafanya waamini kuwa wanapaswa kumfungulia Mwokozi milango ya mioyo yao

  Zingatia: Hiki ni kisa rahisi kuliko visa vyote ndani ya Biblia ndiyo maana Yesu
  hakuona hata haja ya kutoa maana yake kama ilivyokuwa kwa visa vingine.
  Naama hata wanafunzi walikielewa kwa haraka sana ndiyo maana hata
  hawakumwuliza Bwana wao maana ya kisa hiki. Wote walielewa maana ya
  jina Lazaro na sifa za Lazaro. Shetani amekipindua kwa fundisho lake la
  bustanini Edeni…Hakika hamtakufa….. maana yake kwamba mtakufa lakini
  si kwa uhakika, maana mtakuwa mnaishi sehemu fulani katika ulimwengu
  wa roho – Uongo mkubwa.

  Mungu alisema Utakufa hakika, na ndivyo Biblia inavyosoisitiza kuwa mtu akifa, hana kumbukumbu tena juu ya mambo yatendekayo chini ya jua.

  Ni nini hatima ya Wafu ??
  1. Wataendelea kubaki ndani ya makaburi hadi kwa wakati ulioamuriwa.
  Ayubu 14 :12 Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.
  13 Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!

  2. Watafufuliwa kulipwa sawasawa na matendo yoa wakati wakiwa hai
  Daniel 12:1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.
  2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.

  3. Watafufuliwa na miili yao ya mavumbi
  Isaya 26:19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
  20 Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.
  21 Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.

  4. Kama Yesu alivyokufa na kufufuka, nao watafufuli vivyo hivyo
  1Thesal 4:13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
  14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
  15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
  Yohana 5:26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
  27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
  28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
  29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

  5. Walio katika Kristo watafufuliwa kwanza ili waungane na walio hai kumlaki Bwana hewani…
  1Thesal. 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
  17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

  6. Yesu aliahidi mwenyewe kuwa atawafufua siku ya mwisho
  Yohana 6:39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.
  40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

  7. Yesu atatubadilisha, tusione kifo tena, tutaishi maisha ya ushindi na furaha milele, naam kifo tutakizomea….
  1Korinth. 15:51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
  52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
  53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
  54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
  55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?
  56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
  57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

  8.

  Hivyo, tunapaswa kumpenda Mungu wetu na wanadamu wenzetu bila kujali hadhi zao na zetu.
  Torati 6 :5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

  Marko 12 :29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
  30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
  31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

  Torati 6 : 17 Zishikeni kwa bidii sheria za Bwana, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza.

 2. Huo ni umizimi kaka Chiwango. Yesu lipokufa, hakuenda popote tofauti na kaburini na siku ya kwanza akafufuka. soma vizuri biblia yako. acha umizimu

 3. Ubarikiwe Mosile. Kimsingi luka 16 haizungumzii habari za kuzimu. Huo ni mfano tu ambao watu wengi sana huutafsiri vibaya kwa kujenga dhana za kuzimu. Tafsiri hii mbaya, husababisha watu waamini kuwa roho ya mtu afapo, yenyewe haifi!! Huo nao ni uongo mwingine.
  Ukiusoma vizuri mfano wa luka 16:20-31, utagundua kuwa huo ni mfano unaotuhusu mimi na wewe katika katika maisha yetu ya kila siku. Nasema hivyo kwa sababu, ukiisoma Biblia, habari za akina Ibrahim na Lazaro, utazikuta ziko tofauti sana na tafsiri hiyo ya kuzimu. Nijuavyo mimi Biblia iansema kuwa, kuzimu ni kaburini na siyo vinginevyo.

 4. Kimsingi kuzimu ipo na biblia inaonyesha kwamba ni mahali pa mateso, soma Luka 16:20-31 utaona. Jambo muhimu la kuangalia hapa ni kwamba hawa watu wanaodai kwamba wameenda kuzimu au mbinguni wote ni waongo na hatupaswi kuwaamini hata kidogo. Wanaota ndoto halafu wanadai wameenda huko. Kimsingi hatuana ufunuo mwingine wa mbingu au kuzimu tofauti na tunaoupata kwenye biblia, tusikubali kuaminishwa na watu wa jinsi hii kwa maana hautusaidii chochote, soma neno la mungu kwa bidii na ishi maisha yanayompendeza mungu na kuyatenda mapenzi yake ili siku moja upate kuingia mlango mwembamba tulioambiwa na Matayo 7:13.

 5. Sina cha kusema juu ya hao wanaotoa hizo shuhuda. wala siwezi kuthibitisha kama kweli huwa wanapelekwa huko au la. Lakini kama kweli kuzimu hakupo kwa nini Yesu alikuzungumzia kuwepo kwake(tajiri na Lazaro) na Petro naye katika nyaraka zake ijapo kuwa hakutaja kuzimu alidokeza kuwepo kwa roho waliopo kifungoni (Bwana Yesu aliwaendea roho waliopo kifungoni)

 6. M.J.N naona umeanza vizuri.
  Naomba msaada zaidi wa kimmandiko toka kwako uniwezesha kujua kuwa kuzimu siyo sehemu fulani. Na ningependa kujua pia ni wapi watenda maovu huwa wanaenda wakifa.

  Asante.

 7. Nadhani hao ni waongo sana. Wanachukuliwa na mapepo halafu wanawadanganya watu weeee!! Mara wao wamefika mbinguni au kuzimu!! Kwa uelewa wangu wa neno, huu ni uongo. Biblia haifundishi hivyo. Wale waliobahatika kwenda mbinguni, hawakurudi isipokuwa kwa miujiza(rejea Musa na Eliya pale mlimani wakiwa na Yesu). Lakini wengine wote, waliobahatika kwenda huko, hawakurudi. Na kuzimu kwa tafsiri ya kibiblia ni kaburini. Mtu akisema kuwa kuzimu ni mahali halisi pa roho kuungua moto, ni deceptions. Kama wanabisha, watuthibitishie kwenye Biblia.
  1 Yohana 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
  Bwana awabariki sana

 8. Watenda dhambi wote muache maovu kuzimu ipo. Mpokeeni Bwana Yesu muepuke sehemu ile mbaya ya kutisha

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s