Kanisa la Siloamu wanaamini nini?

nabiielia

Nabii Eliya, pichani

Wapendwa Shalom,

Ninaorodhesha machache ninayoyafahamu kuhusu Pool of Siloam Church ambalo lilianza mwaka 2003. (kwa maoni yangu walianza vizuri hadi ilipofika mwaka 2008 – ndipo U-Turn ilipotokea). Pia unaweza kusoma juu ya wanachokiamini kuhusiana na MWENENDO WA KANISA kwenye link hii; http://www.siloamgoshen.org/

MAMBO MACHACHE YA KANISA LA KIZAZI CHA NNE HAYA HAPA

1.   Pool of Siloam ilianzishwa rasmi 2003, na Mtumishi N. Munuo

2.   Mafunuo ya Nabii Eliya yanatambulika kuwa ni sahihi hutakiwi kuyahoji wala kuyaoanisha na Maandiko Matakatifu unapaswa kuyatii. Mojawapo ya ufunuo /maelezo ya ajabu ni hili Shetani aliuwawa na Nabii Eliya Novemba 2008. Hapa ndipo kwenye vile vitisho ya kuwa bubu, tasa kufa n.k.

3.   Imani yao imejengwa na kuongozwa katika ufunuo wa majira na nyakati na jambo hili ni muhimu sana. Hivi sasa wapo katika kizazi cha nne. Kizazi cha kwanza Adamu mpaka gharika, kizazi cha pili Nuhu hadi Yesu, kizazi cha tatu kutoka Yesu hadi Februari 2012. Kizazi cha nne kutoka Machi 2012 na kuendelea. Kwamba kwa kutumia Kalenda inayotumika sasa (Mwasisi wake akiwa ni Gregory – mwaka 1582) kanisa ilikuwa chini ya utumwa kwa miaka 430 kama Israel utumwani Misri. Kuanzia 2008 watu wa kizazi cha nne wana kalenda yao.

4.   Kanisa hivi sasa lipo katika kipindi cha miaka 1000 iliyoanza mwezi Machi 2012 (hii ni baada ya kupita kwa miaka 6000. Hesabu yao ni kuwa miezi yote (12) ina siku 28 na mwaka una siku 336). Yaani wenzetu tayari wamesha-spent mwaka mmoja katika ile miaka 1000 ya utawala wa Yesu hapa duniani, kama iliyoandikwa katika UFUNUO 20:1-5.

5.   Kwa kuwa Kristo anaishi na Kanisa hapa duniani hivyo hakuna magonjwa, dhiki, kudharauliwa na maonevu yote. Ni siku ya saba yaani miaka 1000 ya kustarehe na kutawala. Huenda hapa ndipo ile concept ya kutokufa inapokuja/ingia/ attach.

6.   Waumini wao hutakiwa kubadilisha hadi majina yao ya ukoo. Kwa sababu majina hayo yanabeba laana, kisha muumini hupewa familia nyingine (miongoni mwa washirika) na hutengwa na wazazi na ndugu wa kimwili.

7.   Maombi yao huomba kwa kushikamanisha na madhabahu ya Siloam /Mungu wa nabii Eliya.

8. Wanapomfanyia Deliverance mtu (mmoja wa wahudumu – huingiwa na pepo/mzimu ambao unamsumbua anayeombewa na kumweleza kilichokuwa kinamfunga). Biblically, mtu mwenye pepo/mizimu yeye ndiye hupagawa na kuongea, kisha huamuriwa kutoka ndani ya mtu.

Kila nilichokieleza hapo juu ina tafasiri yake ya ziada ambayo yeyote akipenda na akifunguka anaweza kutufafanulia.

–Mat

Advertisements

196 thoughts on “Kanisa la Siloamu wanaamini nini?

 1. nimesoma mahali kuwa Kiongozi wa Kanisa la siloam baada ya kufariki Munuo anaitwa MIAKA 1000 YA KUTAWALA NA KRISTO .

  Je kabla ya hapo huyu kiongozi aliitwa nani ?

  nataka kujua huyu miaka 1000 zamani aliitwa nani ?

 2. Upendo, Fruitful & Wanasiloam.
  Ni vigumu kuamini kuwa mmepagawa pepo.Kuthibitisha hili hata bila woga mnadiriki kusema huyo Munuo wenu ni Adamu wa pili.
  Pia mnamwita “Bwana wa majeshi” tena alimuua shetani mwaka 2008!!
  Huu ni zaidi ya Upagani, ni Ukengeufu wa hali ya juu.
  Mmelogwa, mmefungwa ufahamu na mnamwabudu IBILISI mkifikiri mnamwabudu Mungu.
  Huyo Mchaga wenu (Munuo) alifanikiwa kuwateka ufahamu na Munuo hana tofauti na akina KIBWETERE na Manabii wengine wa uongo.
  Hebu someni haya Maandiko kama yatawasaidia;
  2 WATHESALONIKE 2:7-12 ” 7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
  9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; 10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; 12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.”

  2 WAKORINTHO 11:13-15 ” 13 Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
  14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
  ***Ni kweli MUNUO ni mtumishi wa SHETANI na kwa kuwa ninyi wafuasi wake mnakataa Kweli na Neno la Mungu, Mungu amewaletea nguvu ya upotevu muamini uongo***

 3. naitwa Upendo unaokaa ndani ya moyo wa Mungu, niwashauri wakamilifu, kama wewe ni mkamilifu kwelikweli mfike mahali mjue kuwa Mungu amepiga marufuku kukaa ktk kituo cha kubishana na asiyeamini, kuna wengine ukweli wanaujua lkn hawataki kuamini kweli ya Mungu, kuna wengine wapo kukejeli tu na kuwasanifu wakamilifu, kaeni rohoni sana mnaibiwa mafuta hapo kwa ajili ya kituo cha kubishana. kweli ya Mungu inabaki pale pale kwamba Eliya amekuja kujenga msingi na anayemazia kwa ajili ya kupaua kuezeka yupo tsyari na ndiye ataondoka na kanisa, wakubari wasikubali. Maono ya Mungu kamwe hayawezi kuangushwa na yeyote yule. kama Mungu aliapa kwa Eliya kuwa yeyote atakayetaka kuangusha maono kufa na afe milele. Pia hao woote huko juu toka muanze mijadala wamekuwa wakikashifu siloamu na sijaona hata mmoja anayetaka kubadilika kutaka kujua ukweli, bali naona wakamilifu mnabishana na kerubi, pasipo kujua, kwani kerubi anajua ukweli kbs kuwa hili ndilo kanisa la mwisho. pia kwa wale wanaojiita wakristo lkn wanakataa kukubali majira sahihi za Mungu ni zipi, waseme wenyewe, kama Januari- hd desemba ni majira za Mungu waende huko. kama Abibu hadi Adari ni majira za Mungu waje huku. pia kama kwao Jumatatu-Jumapili ni Mungu anapatikana huko wamfuate huyo kalenda Gregori ya Mrumi. ukiangalia kwa ufahamu bila kuulizwa na Mtu yyt Mungu katk kitabu chake cha Mwanzo ameanza na siku ya kwanza hadi ya saba. Kuitwa Eliya adamu wa pili Mungu Mungu wa majeshi sio jambo la kubisha hapo, ni akili ya rohoni tu hapo itumike, kwamba tuliowengi tunatunatumia ubini za baba zetu, kwakuwa tunajua huyu ni baba yangu aliyenizaa, kwa hiyo Eliya naye alimjua Mungu ni baba yake aliyemtuma, naye akachukua jina la Mungu kwakuwa alijua huyu ni baba yangu aliyenituma, hivyo kuitwa Mungu wa Majeshi siyo kosa. tatizo la watu na wanadamu wanataka mpk kwanza waone ndiyo waamini. au walitaka itokee biblia nyingine iandikwe huyu ndiye Eliya Ad, waPili Mungu wa majeshi. ndiyo wangeamini bila kupinga. Yesu alisema heri yule anayeamini bila kuona. wengi wanaamini eliya atakuja wa kwenye biblia tena ni mzungu siyo mwafrika kwakuwa hata sisi waafrika hatujikubali kuwa tuna neema ya nabii kutoka kwetu au katika taifa hili, ambalo Mungu kalipenda. ANAYETAKA KUJUA UKWELI ATAFUTE UKWELI ULIPO AFUNGULIWE UFAHAMU.

 4. AMA KWELI TUPO MWISHONI!MTU ANAJIITA MUNGU WA MAJESHI?AISEE TUNAHITAJI KUFUNGUKA NA KULITAZAMA NENO.

 5. Wapendwa hawa ni matapeli wala msihangaike nao. Watafuta pesa waliogeuza neema kuwa biashara. Unaweza kuamini nabii aliwauzia watu maandishi ya kuchapisha tu stationary na kuweka frem sh Laki moja eti ni mafuta. Huu ni wizi mafuta/upako wa Mungu wa kweli hauuzwi kama njugu wapendwa.

 6. yesu alisema kizazi hakita badilika sasa nyie na nabii wenu mtasemaje kizazi cha nne? mnapingana na mwana wa mungu aliye hai(YESU KRISTO)? inamaanisha nyie ndo wale wapinga kristo?, yeye ndo alfa na omega(mwanzo na mwisho) alikuwepo,yupo,na ataendelea kuwepo……..mathayo inatosha kuthibitisha kuwa ndio waleeeee walioongelewa.HAKIKA MWANA WA ADAM YU KARIBU KURUDI

 7. Bezaleli Siloam ni lango la kuzimu, huwezi badili hilo labda uje kwa Yesu utubu na kuifuata kweli ya neno la Mungu. Munuo alikuwa tapeli na amekufa akiwa bado anaendeleza huo.
  Lugha ya matusi haikusaidii na haijawahi kukusaidia, ila inatusaidia wengine kuona roho iliyonyuma ya imani yenu. “Mtawatambua kwa matunda yao”. Hutabadili mtu kumuingiza kwenye imani hiyo potofu kwa lugha ya matusi. Mungu akusaidie utoke huko la sivyo utaendea jehanamu kwa ushabiki. Wakati wenzio wanatafuta pesa tu. Siunaona sasa mnasadaka ya kuhani kiongozi na mama siku saba, hiyo ndio ajenda kuu wala sio kuwapeleka mbinguni. Mwenda mbinguni hatukani wala kutapeli/kudanganya.

 8. DADA CLARA matapeli huwa hawajibu maswali yanayoweka wazi hadaa zao. Wala usijisumbue hawana majibu wanaburuzwa tu hawa na wala hawahui wanakopelekwa. Kama nabii wao aliwahi diriki kusema Yesu hakufanya vizuri ndio maana wakamsulubisha kuna nini tena hapo.

 9. DADA VAI
  BARIKIWA SANA.
  SAMAHANI DADA VAI NILIKUA NAOMBA MSAADA WA KUJIBIWA/KUFAFANULIWA MASWALI HAYA
  1.KWANINI SILOAM HAWATUMII JINA LA YESU KTK MAOMBEZI YAO?
  2.MADHEHEBU MENGINE YANATUMIA DAMU YA YESU KTK HUDUMA ZA KIROHO WAKATI SILOAM MNATUMIA DAMU YA HAKI KWELI NA HUKUMU JE MNAMAANISHA NINI NA IMEANDIKWA KTK KIFUNGU KIPI KTK BIBLIA?

 10. Maandiko matakatifu kwenye kitabu cha Math 24 ,yameweka wazi tabia na mwenendo wa watu wa nyakati hizi( hasa wanaojiita manabii). kikubwa wapendwa ni kukaa kwenye maandika na kumtazama Mungu na Yesu Kristo aliyemtuma, pia wafu hawana nafasi ya kuombewa, kinachofuata kwao ni HUKUMU, maakimu ataamua kitakachojiri.

 11. Yusufu Israel Elia ni nadhani akili zenu zimetenguliwa kwa kujazwa mapepo, huwezi kuwa na ufunuo unaopingana na neno la Mungu. Mfano Munuo alimwambia mzee Kimambo kuwa Mungu alimfunulia atoe kiwanja lijengwe kanisa HAPO MAKAO na kwenda kumwonesha kiwanja ambacho sio chake kule madale huo ni ufunuo au ni UTAPELI.
  Ndugu Pendael hawana majibu hawa matapeli wakubwa. WANASILOAM MMEPOTEZWA KWA USHIRIKINA MNADHANI MNA MUNGU MUNUO ALIKUWA TAPELI TU, HANA LOLOTE.
  Viapo milivyokula vitawatesa na msiopo sikia jiandaeni kwenda JEHANAM, mwenzenu walau alifaidi sadaka zenu mtaumia duniani na jehanam mtakwenda.

 12. YUSUF ISRAEL ELIYA & WANASILOAM
  TAREHE 19/11/2014 at 10:37 AM.
  NILIWAULIZA MASWALI YAFUATAYO.
  NI KWELI NAAMINI YUPO ELIYA AJAYE LAKINI SI Munuo.
  ” 1. Mmetumia VIGEZO GANI VYA BIBLIA kumuita Munuo ni Nabii Eliya? Naomba uthibitisho kimaandiko.
  2.Adam wa Pili ni nani?
  3.Huduma ya ELIYA ni ya DUNIA NZIMA au ni Ya Tanzania tu? Nchi zingine DUNIANI zinamtambua MUNUO KUWA NDIYE ELIYA ajaye?
  4.Nitajie sifa ZA NABII ELIYA.
  5.KILA MTU KWENYE BIBLIA alibadilishwa Jina kama ninyi mfanyavyo?
  6.Mnaamini Mungu ana NAFSI NGAPI?
  7.KAMA MNANG’OA KAVA JEUSI KWENYE BIBLIA ZENU, MTU MWEUSI MNAMFANYAJE? ADAM WA PILI MNAMJUA VIZURI AU MMERUBUNIWA UFAHAMU?
  8.SHETANI ALIUAWA NA MUNUO?
  Nipatie uthibisho wa kimaandiko.”
  Hayo ni maswali tu ya mwanzo kuhusu siloam
  KWAKO Yusuf ISRAEL ELIYA ,
  Umejibu MASWALI yangu KWA mtazamo WA kile ulichofundishwa na MUNUO.
  Kama ni kweli hutaki upotee mbona bado roho ya SILOAM imekung’ang’ania?
  Kama HUTAKI kupotea MBONA maswali unayajibu MASWALI kwa mtazamo WA SILOAM?
  Tafadhali jibu HAYO MASWALI muache Kuzungumza MANENO yasiyo na msaada kwa WENGINE.
  HEBU tumia UTHIBITISHO wa Kibiblia kwa MAJIBU yako.

 13. PIA KUNA SIKU NIKIWA KWENYE K3 NILIAMBIWA KUWA ELIYA NI MKUBWA ZAIDI YA YESU, HEBU SILOAM WENZANI NIONGEZEENI UFAHAMU WA NENO HILI, KAMA YESU NI MUNGU MWENYEWE NI NANI ALIYE JUU YA MUNGU? NASISITIZA LENGO LANGU SIO KUBISHANA BALI KUJIFUNZA KWA MAANA SITAKI KUANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA YA NENO LA KWELI LA MUNGU, NAJUA TOFAUTI KATI YA MAANDIKO NA NENO NA UFUNUO LAKINI UFUNUO UNAOMZIDI KRISTO SIPO TAYARI KUUJUA WALA KUUFUATA, KITU KINGINE KWA NINYI MNAOIPINGA SILOAM JINA MUNUO NA ELIYA SIONI TATIZO HAPO COZ MBONA JACOB ALIBADILISHWA JINA NA KUITWA ISRAEL? NA MKRISTO GANI AMBAYE HAJUI KUWA JINA NDILO LINABEBA HATMA YA MTU? HIVYO KUTOKA MUNUO MPAKA NABII ELIYA SIO ISHU HEBU TUANGALIE KINACHOFUNDISHWA KAMA KINA MSINGI WA KRISTO KWELI AU KINA MSINGI MWINGINE? TUPINGE PANAPOSTAHILI KUPINGA NA TUSAPOT PANAPOSTAHILI KUSAPOTI KWA MAANA WOTE HATUJA FIKA BALI TUNAKAZA MWENDO TUACHE USHABIKI TUSIMAME KWENYE NENO LA MUNGU PEKE YAKE

 14. ASANTENI SANA KWA MASWALI YENU MAZURI LKN KABLA YA KUJIBU ILI TWENDE PAMOJA NIANZE KWA KUULIZA SWALI MAANA NDIO MFUMO WA KIUNGU ULIVYO KWAMBA KUNA MASWALI YANAJIBIWA KWA SWALI, NAOMBA KUJUA NI NANI ALIYEMFUNDISHA INJIRI MTUME PAULO? INJILI ALIYOKWENDA KUIHUBIRI KWA MATAIFA? KAMA NI MUNGU MWENYEWE BASI SIO MAFUNDISHO BALI NI UFUNUO, NA UFUNUO NI NENO LA MUNGU MWENYEWE AMBALO HUTAMBULIKANA KWA WANAOENENDA KWA JINSI YA ROHO PEKE YAKE, BUT KWA ALIYE MWILINI HAWEZI KUELEWA MAMBO HAYO YA ROHO, HIVYO NABII ELIYA ALIKUWA ANAFUNDISHA MAMBO YA ROHONI AMBAYO MENGINE HAYAMO KATIKA UFAHAMU WA MWANADAMU ALIYE ANDIKA BIBLIA, NADHANI NIMEJIBU SWALI LA KWANZA, SWALI LA PILI KUHUSU MUNUO KUJIITA NABII ELIYA, NI KWAMBA MTU HAZALIWI AKIWA NABII BALI NI NEEMA TU YA BWANA AKIAMUA KUMTUMIA MTU FULANI HAIJALISHI ALIISHI MAISHA YA NAMNA GANI BALI MUNGU AKIAMUA KUKUTUMIA KAMA NABII WAKE UTATUMIKA TU, SINA HAJA YA KUELEZA SANA KUHUSU HILI COZ NAAMINI KAMA WEWE NI MKRISTO BASI UNA MIFANO MINGI SANA YA MANABII WALIOTUMIWA NA MUNGU UKIACHILIA MBALI UOVU WAO MF. MUSA, SAULI NK, KAMA NILIVYOKWISHA TANGULIA KUSEMA SISI SOTE NI WAKRISTO NA NIA YETU NI MOJA TU KUTAWALA PAMOJA NA KRISTO, LKN KUNA JAMBO AMBALO HATA MIMI BADO NINA MASHAKA NALO NA NINGEOMBA SILOAM WENZANGU WANISAIDIE KWA HILI KWANINI ELIYA ALIKUWA ANAITWA ADAM WA PILI MUNGU WA MAJESHI? MBONA MUSA AMBEYE MUNGU MWENYEWE ALIMFANYA KUWA KAMA MUNGU KWA FALAO NA AKAMPA NA NABII AMBAYE NI HARUNI KWANINI MUSA HAKUJIITA ADAM WA PILI MUNGU WA MAJESHI? HEBU TUSAIDIANE HAPO ILI TWENDE PAMOJA.

 15. SHIKA NENO MARAFIKI WA MUNGU WA ELIYA KIZAZI CHA 4!
  TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUFUNULIA PASAKA YA ROHONI NA YA KWELI AMBAYO IKO TOFAUTI NA PASAKA ZA DINI NA MADHEHEBU AMBAZO NI PASAKA ZA VILIO NA MAOMBOLEZO. NAWATAKIA MARAFIKI WOTE WA MUNGU PASAKA YENYE BARAKA ZOTE INAYOANZA LANGO LA 14 – 21 MWEZI ABIBU MWAKA WA 4 WA KANISA. TUNAUNGANA NA KUTOKA KWENYE UTUMWA WA KILA AINA ROHONI KWA DAMU YA HAKI, KWELI NA HUKUMU. MBARIKIWE MARAFIKI WA MUNGU, WASHIKA NENO, WATENDA NENO NA WALIOFUNULIWA KWA DAMU YA HAKI, KWELI NA HUKUMU.

 16. Inadaiwa sababu ya kifo Cha Eliya Adam wa pili kama alivyokuwa akijiita nikuchomwa na msumari wa tetenus na akakataa kwenda hospitali kwa sababu kanisa hilo haliamini katika tiba za hospitali. Waumini wa siloam acheni mambo ya ajabu.. Nendeni hospitalini mnapougua…
  Naamini huu mwaka mengi yaliyo sirini Mungu atayafichua..
  Yesu pekee ndiye njia ya kweli na uzima…hakuna mwingine jamani. Tujifunze pia kusoma neno la Mungu ili tusiyumbishwe na dini za kishetani zinazojiinua kila siku.

  Binafsi niliwahi kuabudu Siloam ila nilishindwa baada ya kuona wanatunga mpaka nyimbo zakumtukuza mwanadamu..Mungu hagawani utukufu na mtu. Nilitoka nduki na sikurudi tena…Mungu awafungue macho waumini wa Siloam mtoke kwenye hicho kikundi cha Occult kwa jina la Yesu..

  Ameeeen!

 17. Naombeni niwakumbushe alichoandika muumini wa siloam miezi iliyopita..

  Hakikazi ad2 Eliya says: 08/06/2014 at 3:15 PM MAASKOFU ! Eliya aliwatangazia “Kama wewe unaona Mungu wako ni wakweli na wa Eliya ni wauwongo basi njoo msimamishe mungu wako na Eliya asimamishe wake halafu tuone nani atakufa ! MBONA HAMKUJA ! Akasema basi mwiteni yeye aje hata uwanja wa taifa kila mmoja amuite Mungu wake halafu tuone wanani mwenye Nguvu ! MBONA HAMKU JITOKEZA !

  UNAPOKOSA UFAHAMU,UNAKOSA MUELEKEO , UNABAKI KWENYE KITUO CHA KULALAMA – LALAMA !

  UNAE MUNGU ! MUOMBE AMUUE ELIYA,

 18. SIKU MKIINGIA JEHANAM MTAYAKUMBUKA YOTE TUNAYOWAANDIKIA ENDELEZENI USHABIKI KAMA WANASIASA, NABII HANA NAMNA HAPO ALIPO, KAMA HAKUTUBIA UASI ALIOUANZISHA NA NYIE MNAUSHABIKIA MOTO WA MILELE HALALI YAKE.

  NI SUALA LA KUFANYA UPEMBUZI NA KUCHUKUA HATUA ACHANENI NA ULOZI WA KUDANGANYWA ETI DAMU YA KWELI HAKI NA HUKUMU YA KUTOKA KWA NANI, HUHITAJI KUGANGA KWA MAJI ILI YESU ADHIHIRIKE, MMEPUMBAZWA KWA KUTII UONGO WA SHETANI.

  MNADIRIKI KUSEMA MITUME WALIASI NDIO MAANA WAKAUWAWA, HIYO NI ROHO YA KUZIMU, NA NDIKO MTAKWENDA KAMA HAMTATUBU. MUNGU HADHIHAKIWI UNACHOPANDA LAZIMA NASEMA LAZIMA UTAVUNA.

 19. Na si Munuo tu. Kule Kenya kuna mtu anaitwa Mwenyezi Wanyonyi. Yeye anadai kuwa ni Mungu kabisa. na ana wake kibao. hehehehehehehehehehe Mungu tuokoe

 20. Mhh! Kaazi kweli kweli.. Kuchanganyikiwa hakujaanza leo. Ni tangu kale. Shika imani yako

 21. PENUEL Unashida kubwa ndugu yangu kama ndio ufahamu ulionao,nakupa pole. (kwa nini nasema haya binadamu tunaishi, tunasema, tunafanya na kuwaza sawasawa na kiwango cha ufahamu tulionao). Eti mtu kasema amemuua shetani ndio sababu ya kumfuata. Neno linasemaje kwenye kitabu cha ufunuo huyo joka atatupwa kwenye ziwa la moto, roho aifi, kifo cha kiroho lucifer alikufa alipomwasi Mungu (alitengwa na Mungu milele), hiki cha pili ni utapeli tu wakukamata watoto wasiotaka kukua wanaotakakuendelea kunywa maziwa miaka ishirini bado na kichupa cha maziwa. Kipimo ni neno linasemaje, ikingana na neno hata kama atakuja kama malaika hili halikubaliki. Ukristo ni maisha sio ngonjera kama musiki wa kizazi kipya mnapingana na neno mnalolisoma kila kukicha. Sasa motoni anatupwaga marehemu. Halafu shetani ni roho, walikutana wapi na huyo Munuo.

 22. hawa Siloam wana matatizo makubwa ya ufahamu… Mtume wao muongo na wao waongo wamefundishwa uongo na kuuamini… wamepotea.
  Haya ni majira ya Mvua za vuli na siku ya mazishi Bagamoyo mvua ilikuwa inanyesha tena kubwa sana na kwa upande wa Dar jua lilikuwepo na mawingi=u ya mvua ya upande wa Bagamoyo yakawa yanalikinga na kuleta miale inayoakisi mwanga kwenye mawingu. Na zaidi ya yote upinde wa mcua ukatokea angani kwaajili ya mchua eti wao wakaaanza kupiga mayowe kuwa jamaa yao katwaliwa hata akili ndogo ya kukumbuka majira ya mwaka ya mvua hawana, akili ya kukumbuka agano la Jehova kwa njia/alama ya upinde kuwa hatauangamiza tena ulimwengu hawana. Eeeh watu hawa ni hatari wanaweza kukuua manake sio wanadamu wa kawaida ni wehu wanaojua kufua nguo na kukalala vitandani…

 23. EE MUNGU Baba nakushukuru kwa udhihirisho wa kanisa la mwishi.Nasimamisha toba kwa ajili yangu mwenyewe na kwa watu na wanadamu wote niliowashuhudia na wakakaidi.

 24. YUSUF ISRAEL ELIYA & WANASILOAM,
  SHETANI ALIUAWA NA MUNUO?
  Nipatie uthibisho wa kimaandiko.

 25. YUSUF ISRAEL ELIYA & WANASILOAM,
  NI KWELI NAAMINI YUPO ELIYA AJAYE LAKINI SI Munuo.
  Yusuf Umekuwa mnyofu kwa sehemu kubwa, naomba niwaulize maswali yafuatayo;
  1. Mmetumia VIGEZO GANI VYA BIBLIA kumuita Munuo ni Nabii Eliya? Nomba uthibitisho kimaandiko.
  2.Adam wa Pili ni nani?
  3.Huduma ya ELIYA ni ya DUNIA NZIMA au ni Ya Tanzania tu? Nchi zingine DUNIANI zinamtambua MUNUO KUWA NDIYE ELIYA ajaye?
  4.Nitajie sifa ZA NABII ELIYA.
  5.KILA MTU KWENYE BIBLIA alibadilishwa Jina kama ninyi mfanyavyo?
  6.Mnaamini Mungu ana NAFSI NGAPI?
  Hayo ni maswali tu ya mwanzo kuhusu siloam!

 26. YUSUFU ISRAEL ELIA, UMEKUWAMSTAARABU WA KWANZA TANGU NIMEANZA KUKUTANA NA WANASILOAM. BAADA YA KUSEMA HAYO NAOMBA NIKURUDISHE KWENYE SWALI LAKO.

  KANISA LA SILOAM LIMEJAA UDANGANYIFU MWINGI MFANO NI KAMA IFUATAVYO
  1. NABII ELIA (A.K.A MUNUO) MUNGU WA MAJESHI, INAKUWAJE MNATUAMBIA MUNGU MWENYEWE AMESHUKA KUTAWALA NA KANISA MIAKA 1000
  2. HIKI SIO KIZAZI CHA NNE, SOMA MATHAYO 1:17. KIZAZI CHA NNE KIMETOKA WAPI.
  SITAKI KUKUJAZIA MAMBO MENGI TUANZE NA HAYA KWANZA, MIMI NAMI NATAKA KWENDA MBINGUNI KAMA NIKO KWENYE UPOTOFU I PROMISE UKIJIBU HOJA KWA USHAHIDI WA NENO MIMI NITAKUJA SILOAM, VERY SERIOUSLY.

 27. MUNGU ALIYESHUKA KUTAWALA NA KANISA MIAKA 1000 NAYE ANAKUFA KABLA YA MIAKA 10 KUFIKA, INAKUWAJE HII.
  NILIWAHI WAAMBIA HUKO NYUMA SHETANI MLIMPA WENYEWE UHALALI WA KUWATESA MAANA MLIINGIA MAAGANO KWA KUPENDA WENYEWE KWA SABABU YA UJINGA WA KUTOPAMBANUA ROHO, HUU NI USHIRIKINA PURE ILA UNAFANYIKA KWA JINA LA KANISA.
  MUNGU AWASIAIDIE NABII ALINYIMWA KURENEW CONTRACT AMEONDOKA NANYI MSIPO TUBU, HAKIKA MTAANGAMIA MILELE. MNAJUA KUWA MUNGU HATANII, MNACHOPANDA HAKIKA MTAVUNA, KAMA ALIVYOVUNA NABII. KAGOMA KUCHOMA SINDANO YA TETENAS HAYA TETENAS IMEMWONDOA. MSIJIDANGANYE KWA UONGO WA KUTUNGA TUNGA.

  HAMNA MUNGU WA KWELI MMEDANGANYWA, TOKENI HUKO MAPEMA, NENO LINASEMA BAADA YA KIFO NI HUKUMU NABII WENU KAMA KWELI ALIACHA MAAGIZO MNAYOTANGAZA BASI HUYO NI WA WAJEHANAM, MAANA HAKUTUBU.

 28. Washika neno na marafiki wa MUNGU ka mkijua mnapoteza mafuta yenu kwa kubishana na watu na wanadamu walioko kizazi cha tatu watawaibia mafuta ya rohoni kama wamekaidi pamoja na ishara na miujiza iliyotokea waacheni kwani hata kipindi cha nuhu watu waliambiwa watengeneze njia lkn wakakaidi na waliotekeleza waliokolewa ndan ya safina na wale waliomtukana na kumthiaki walikwenda wap? Mtajijibu wenyewe

  Natubu kwa ajili yenu kwani sahv ni kipinfi cha toba na kushukuru

 29. Namshukru sana MUNGU WA MAJESHI kwa maana amejitetea mwenyewe,Kitendo cha mjumbe wake kuita makuhani wote na wazazi wake kabla hajafariki kwamba MUNGU angemchukua siku ya pili kwa gari la moto na kweli ikatokea ni ushuhuda mkubwa kwa kanisa kuwa lilikuwa na Nabii aliyebeba Roho ya MUNGU.
  kitu cha pili ni Ishara ya jua la haki Malaki 4.1-3 ambalo limelizukia kanisa la mwisho wakati ule mwili unaenda kulazwa ni HAKI KWELI NA HUKUMU zimesimama na aibu kwa kanisa imefutwa HONGERA KWA USHINDI MAKUHANI NA WASHIKA NENO WOTE.

 30. SHIKA NENO MLIYOPEWA NEEMA KUBWA NA BWANA HAKIKA KWA ISHARA KUBWA ILIYOONEKANA JANA KWENYE KUMLAZA MJUMBE NI WAZI KUWA MJUMBE ALIKUWA NA AGIZO HIVYO MWENYE MACHO ALIJIONEA NA WAPINGAO SILOAM PIA WALIJIONEA HIVYO NAPENDA KUKALIBISHA MASWALI YENU SHIKA NENO TENDA NENO.

 31. NAPENDA SANA MJADALA HUU COZ INAONYESHA WAZI KUWA WATANZANIA NI WAMOJA NA TUNA LENGO MOJA KIIMANI YAANI KUMTUMIKIA MUNGU MMOJA TENA WA KWELI PEKE YAKE NA MABISHANO HAYA YANATUFUNDISHA NA KUTUONGEZEA UFAHAMU WA NENO LA MUNGU, BAADA YA KUSEMA HAYO SASA NAOMBA KUJUA KUTOKA KWENU WADAU KWANINI MNALIPONDA KANISA LA SILOAMU? NIPO HAPA KUJIBU MASWALI YENU YOTE NA PIA TUTUMIE KITABU CHA NENO PEKE YAKE KAMA REFERENCE TUELIMISHANE BILA KUTUKANANA NA HOJA ZENU ZIKIWA NA MASHIKO NIPO TAYARI KUHAMA SILOAMU, NASISITIZA TUTUMIE USHAHIDI WA NENO LA MUNGU KUBISHANA.

 32. Hapana, hapana… No way! Hii SILOAM siyo Wakristo!

  Nashangaa ni kwa Nini Wanatumia Bibilia?

  Matunda 9 Elya ameandika “HERI YA KUINGIA MWEZI ADARI KWA DAMU 1”

  Hii ni ELIMU NYINGINE!

 33. SILOAM,
  POLENI,
  KAMA MNANG’OA KAVA JEUSI KWENYE BIBLIA ZENU, MTU MWEUSI MNAMFANYAJE? ADAM WA PILI MNAMJUA VIZURI AU MMERUBUNIWA UFAHAMU?
  KUNA KUFURU ZA AINA NYINGI DUNIANI!!
  ****MTU AKISHA KUFA KINACHOFUATIA NI HUKUMU***

 34. Yusuf Israel Eliya,
  Huwezi kumlinganisha BWANA YESU na Munuo.KUWA MPINGA NENO NI KUWA MPINGA KRISTO NA KUWA MPINGA KRISTO NI KUWA MPINGA YESU.
  UNAJUA ALIKORUDISHA MAJIBU?
  NASHANGAA HUO MSEMO WENU “SHIKA NENO TENDA NENO”. SI AJABU NI NENO LA SILOAM WALA MSIFIKIRI NI NENO LA MUNGU ALIYE HAI.
  SHETANI ALIKUFA,2008 KWELI NI ZAIDI YA KUCHANGANYIKIWA!!
  Hebu kwa jambo hili Mungu awafungua macho IKIWEZEKANA.

 35. SHIKA NENO MLIOPEWA NEEMA KUBWA NA BWANA
  NABII ELIYA HAJAFA KAMA WAPOTOSHAJI WANAVYOJARIBU KUPOTOSHA UMMA, NENO MJUMBE MAANA YAKE ULIYEBEBA UJUMBE AMBAYE AKISHAKUUFIKISHA BASI SHARTI ARUDISHE MAJIBU KWA ALIYEMTUMA, HATA YESU ALIRUDISHA MAJIBU BAADA YA KUMALIZA KAZI YAKE, HIVYO MJUMBE AMERUDISHA MAJIBU YA KAZI ALIYOKWISHA IMALIZA
  SHIKA NENO TENDA NENO

 36. SHIKA NENO WAKAMILIFU KIZAZI CHA NNE! KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUPATIA KITUO KIPYA CHA UKAMILIFU KWELI KANISA TUKO JUU YA DINI, MADHEHEBU, MILA, DESTURI, DUNIA NA ULIMWENGU. TUNAMSHUKURU MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU BABA YETU WA ROHONI KWA KUKUBALI KULIBEBA AGIZO LA MUNGU WA KWELI MPAKA AMETUTOA KWENYE KILA AINA YA UOVU, UASI NA DHAMBI. HERI YA KUINGIA MWEZI ADARI KWA DAMU 1

 37. AHAA SHIKA NENO ULIYEPEWA NEEMA KUBWA NA BWANA.. HATA YESU ALIPOKUJA KIZAZI CHA TATU WALIMPINGA KWA HIVYO WALA HATUSHANGAI NINYI KUMPINGA ELIYA W KIZAZI CHA 4… LABDA TU NIANZE KWA KUMSHUKURU MUNGU, PILI KUWASHUKURU WOTE AMBAO HAWANA UFAHAMU NA AKILI YA MUNGU KWA KUWA UGONJWA SIO MALARIA PEKE YAKE BALI HATA KUKOSA UFAHAMU NI UGONJWA VILE VILE. . . NA UGONJWA KWA KAWAIDI USIPOTIBIKA BASI LAZIMA UFE NDIO MAANA MUNGU ALISEMA “WATU” WANGU HUANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA, HAKUNA DINI WALA DHEHEBU LOLOTE AMBAKN LIMEJENGWA PASIPO MSAADA WA WAZUNGU ( ) KAMA LIPO NINNESHE, HIVYO WENGI WALIKAA AU WALIFANYA AMBACHO MUNGU HAKUWAAGIZA. 1) HUWEZI KUKUBALI KUWA SHETANI KAFA KWA SABABU INAWEZEKANA NI BABA YAKO, WHY? KWasababu kama amekute7a miaka yete alafu ukasikia kunaaliyejitokeza kumuua kwanini usimfata huyo alafu ukatafuta ukweli ili ujue kiundani lakini kwa sababu ya ujinga mnabaki kulaumu na kupiga kelele na kukashifu, kama hamtaki nendeni kwa waganga na wachawi maarufu mkawaulize kuwa babao marehemu shetani yuko

 38. Dickson,
  “Nguvu ya Upotevu” si mchezo!

  Hao hapo, wamekula viapo vya utii mbele ya madhabahu ya Upotevu na nafsi zao zimefungiwa huko kuzimu kwa hiyari yao, kwahiyo hawa hapa si wao tena bali ni zile roho za kufuru zikitenda kazi ndani yao!!

  Hebu fikiria, wameaminishwa kwamba kulikuwa na Edeni alimoishi Shetani na Adeni alimoishi Adamu! Halafu wanakupa maelezo hayo kwa furaha kabisa, Biblia zao walizozing’oa magamba wanazo kwapani, halafu wanajipongeza kwa “SHIKA NENO!!”
  Ukiwaletea Biblia ya kizungu ambayo sehemu hizo mbili zilizokosewa ktk tafsiri ya Kiswahili kwa hizo herufi za mwanzo wa jina hilo ambazo wao kwa kule kuwa kwao makasha matupu waliamishwa kuwa ni mahali pawili tofauti; basi wakiona ktk kingereza kuwa ni sehemu moja hiyo hiyo, wanabaki wanakushangaa kama mazezeta, ambavyo ni kweli, ni mazezeta wa dini!!!

  Gbu!

 39. SHIKA NENO ULIYEPEWA NEEMA KUBWA.Nina kila sababu kumshukuru Mungu wa Eliya ninaye mwabudu kizazi cha nne.Kwa Neno aliloweka kinywani mwa ELIYA Nabii kumwabudu Mungu katika Roho na kweli na kuvunja misingi yote mibovu ya dini na madhehebu.
  Kila kitu chini ya mbingu Mh 3.1 kina majira yake utendaji wa Mungu wakati wa nabii MUSA ni tofauti na wakati wa nabii ELIYA mtishibi na pia tofauti na wakati wa kipindi cha Roho ya Eliya ndani ya Yohana kazi ambayo Yesu alikuja kuimalizia.
  Tunafunuliwa kuwa Yesu alikuja na toba ya kweli na kuleta ufalme wa Mungu duniani maana kabla ya hapo hakukuwa na toba wala ufalme wa Mungu kutawala.
  Hapa utaijua kuwa wale wote waliotangulia kabla ya Yesu au kanisa walikuwa ni wezi na wanyang;anyi Yoh 10.10 Hata pale MUNGU alipomtuma mwana wake walimua wakamtupa nje ya shamba.Math 21.33-41 lakini sasa Mungu anasema anaumba mbingu mpya na nchi mpya mpya Isaya 65.1- nchi ambayo ni moyo uliosafi ibada ya kweli,
  Rejea Math 21.33-41 kuna vipindi vinne ndani ya shamba la Mungu watumishi, manabii. mwana -Yesu , na sasa baada ya kuisha kipindi cha Yesu kutawala ameshuka MUNGU mwenyewe anatawala.pamoja na kazi zingine Yesu alikuja kujenga msingi ili mitume na manabii wajengee kazi za dhahabu fedha.chuma -ambazo ELIYA,Lakini dini nyingi zimejengwa juu ya msingi wa wachungaji, wainjilist. maaskofu. Hawa Wakiona huduma yoyote ya kinabii wanakimbilia kusema manabii wa uongo kitu hiki si sahihi maana hata Neno linasema Kumjua mtakatifu ni ufahamu.kama huna huo ufahamu utajuaje nabii wa uongo kwa taarifa tu , Kitabu kimesema pia wachungaji. wakristo wa uongo mbona hawa hawasemwi.
  Siku zimeeenda majira haya MUNGU anatawala pamoja na watakatifu rohoni ,ufalme wa Mungu ni haki, amani furaha. kama una huzuni majonzi, hofu, magonjwa. kuwaza kufa. kuwazi kifo,mauti si wakati wake. kama unawaza hivyo huna ufalme wa Mungu.YESU anasema njooni………mtapata raha nafsini mwenu siyo mtapata shida au uchungu.Tunamshukuru MUNGU WA MAJESHI kwa kupitia nabii Eliya tunatembea na ufalme wake kiuhalisia.
  ZAIDI YA YOTE NAINUA TOBA KWA AJILI YA WOTE AMBAO WAMEAMUA KUSEMA WANAVYOWEZA KUHUSU NABII WANGU ELIYA ADAM 2 MUNGU WA MAJESHI. SHIKA NENO TENDA NENO

 40. Hizi ni nyakati ambazo zaidi ya asilimia 80 ya wateule wa Mungu aliye hai wanaishi
  kwa IMANI inayotokana na kusikia NENO LA MASHETANI na MAFUNDISHO YA WANADAMU.Wengi wanasikiliza ROHO ZIDANGANYAZO NA MAFUNDISHO YA MA
  SHETANI!!!(1Timotheo 4:1,Mathayo 15:7-9).Kwahiyo wanategemea IMANI ILIYO KUFA!IMANI ILIYO HAI ni ile inayotokana na kusikia NENO LA KRISTO.

  Chanzo cha imani iliyo hai kujengeka ndani ya mtu ni UTII wa lile NENO LA KRISTO
  analolisikia(Warumi 10:17).Wengi wanajengewa UTII ULIO KUFA kwa kusikiliza neno la shetani ndani ya wajumbe wake.Wengi wanaapa mbele ya madhabahu za shetani kwamba
  watatii sauti yake impaka atakapowanyonga kabisa na kuwapeleka KUZIMU!!

  Mungu aliye hai alishayaona haya yote ndiyo maana ameamua kuongeza MAARIFA kwa wateule wake(Habakuki 2:14) ili wawe HODARI NA KUFANYA MAMBO MAKUU(Danieli 11:32).WAJUMBE WA SHETANI(Watumishi wa uongo) wanajitahidi kuiba na kuyatumia maarifa ya Yesu kwa UOVU KUPITIA HUDUMA AU MAKANISA YAO AMBAYO NI KUTA ZILIZOPAKWA CHOKAA ISIYO KOROGWA VYEMA.NI KUTA AMBAZO UKIZITAZAMA KWA MACHO YA ROHONI UTAONA JINSI
  ZINAVYOENDELEA KUANGUKA KILA KUKICHA(Ezekieli 13:10-15,Isaya 23:24-32).

  MAARIFA YA MUNGU ALIYE HAI yanapoongezeka ni ishara kwamba vita baina ya wateule na wajumbe wa shetani INAZIDI KUWA NA UTAMU WA MOTO ili wateule wanaoendelea kukosa maarifa na kuogelea ndani ya maangamizi ya shetani wapewe TIKETI ZA KWENDA JEHANAMU MAPEMA.Haya mambo yote Yesu alishayaweka wazi kwetu(Hosea 4:6,Mathayo 24:4,10-14,24-25,28).Naomba tumshirikishe Roho Mtakatifu KUTAKAFARI VIFUNGU VYOTE KWA MAKINI.Tusisome ujumbe huu wa Yesu bila kutafakari NENO LAKE.

  Wateule wengi wameibiwa MACHO NA MASIKO YA ROHONI (Isaya 42:18-22).Ni maarifa ya YESU YANAYOPATIKANA NDANI YA UNYENYEKEVU WAKE NDIYO YANAYOWEZA KUWARUDISHA WATEULE katika MIKONO YA MUNGU ALIYE HAI
  ILI WAANZE KUUKOMBOA WAKATI(Waefeso 5:15-33).Binafsi kabla sijaya tambua
  haya nilipoteza muda mwingi na imenigharimu sana kuufidia.

  HAKUNA SILAHA NYINGINE INAYOWEZA KUTUKOMBOA .NI UNYENYEKEVU
  WA YESU TU NA UNATAKIWA UISHI NDANI YETU.

  ASANTE YESU KWA UJUMBE WAKO MZITO.TUNAOMBA REHEMA ILI TUWEZE
  KUUISHI.NI UJUMBE UNAOKWENDA KUHUISHA NAFSI ZILIZO KUFA.

 41. nina swali kwa STRAIGTH GOSPEL; Mbona comments zangu ninazotoz siku hizi hazionekani kwenye list ya wachangia mada? Tatizo hili limejitokeza zaidi ya mara 2 sasa. Kwani kuna tatizo gani?

 42. Dada Esta,

  Nikiirejea kauli yako kuhusu huyu kipofu, unaniambia;
  “” Lwembe ninachokueleza nataka usiwe kama yule kipofu aliyekuwa ameketi kando ya njia akiwa amevaa mavazi machafu, Lakini baada ya kusikia habari za yesu alipata ufahamu kuwa nitaona na akamwita YESU KWA SAUTI NA AKAMSIKIA NA AKAYAVUA MAVAZI MACHAFU AKAPATA KUONA.””

  Pia umenipa na maana ya jambo hilo kama hivi:
  “”NINI MAANA YAKE: MAANA UKIWA HUNA UFAHAMU WA NENO LA MUNGU NDANI YAKO NI SAWA NA KIPOFU NA UNATEMBEA NJE YA NENO YAANI KANDO YA NJIA LAKINI UKIJIFUNZA NENO LA MUNGU NDIPO UNAWEZA KULALUA MAVAZI MACHAFU YAANI KUACHA DHAMBI NA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KUTENDA SAWA SAWA NA NENO, UWE NA IMANI, UTAKATIFU YAANI KUKAA KWENYE TOBA SIKU ZOTE NA UTII, UTII YALE YOTE UNAYOAMBIWA NA MUNGU KUPITIA MTUMISHI ALIYE MSIMAMISHA. KWAHIYO MIMI NAFURAHI SANA LWEMBE KWAAJILI YAKO MAANA NAJUA NITAKAVYOENDELEA KUKUFUNDISHA UTAPATA UFAHAMU NA UTAMJUA MUNGU WA ELIYA.””

  Haya ni mafundisho mazuri sana na yenye kusisimua! Katika hali yoyote ile, unapokutana na maelezo matamu kama haya, ni lazima uvutike; na ninaamini hivyo ndivyo ilivyokuwa kwako, kama unavyouleta mrejesho huu kwangu, ili nami nilione jambo hili kubwa na la kusisimua nipate na Ufahamu!!

  Nimelipenda zaidi jambo hili la “UFAHAMU” kutoka ktk haya unayonieleza, ndipo nikaona nijifunze zaidi hilo kutoka kwako uliyeipokea hiyo “NEEMA KUBWA YA MUNGU WA ELIYA MAANA UNAMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI”

  Ktk kulifuatilia hilo, nikaanza na huyo kipofu, nikarudi ktk Neno, kweli nikamkuta, anaitwa Bartimayo, na maelezo yake ndiyo haya hapa, Mk 10:46-52:
  “Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. YESU AKASIMAMA AKASEMA, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita. Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.”

  Umeniambia kuwa huyo kipofu alikuwa “AMEVAA MAVAZI MACHAFU”, lakini sijaliona jambo hilo ktk Maandiko yote yanayomhusu huyo kipofu unayeniambia “nisiwe kama huyo”!

  Pia, umehusisha “kuyavua mavazi machafu” na kuona alikokupata jambo ambalo sijaliona ktk Maandiko. Nilichokiona humo ni furaha ya kuitwa kwake iliyomfanya alitupe hilo vazi la nyongeza lililomtia uzito bila kujali atalipataje tena, na “akaruka” kumkimbilia Kristo; nasi twafahamu ilikuwa ni desturi kuvaa jinsi ya hayo mavazi kama tunavyosoma hapa ktk Mt 5:40 “Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia …”, kwahiyo tuna kila sababu ya kuamini kwamba hilo vazi alilolitupa lilikuwa ni hilo joho linalovaliwa juu ya kanzu na si vazi chafu kama unavyofundisha!

  Jambo jingine, unasema kwamba kipofu huyo hakuwa na UFAHAMU mpaka hapo aliposikia habari za Yesu ndipo akapata ufahamu kwamba ataona na akamwita Yesu. Mandiko yanashuhudia tofauti kabisa na hili unalonifundisha!

  Tazama yanachosema, ” Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu.” Mandiko yanasema Yesu alikuwa ameandamana na mkutano mkubwa, kwa leo tungesema ni maandamano, na twafahamu kwamba maandamano hayawezi kuwa ni ya kimya kimya, kwa kawaida huwa na muungurumo wa hizo sauti za watu, ambazo ndizo alizozisikia kipofu huyo na kuuliza kunani, akaambiwa huyo ni Yesu Mnazarethi! Ndipo kutoka UFAHAMU alionao kuhusu habari za huyo Yesu, “Mwalimu”, akamwita katika nafasi yake ya Ufalme, hapo atakapokikalia Kiti cha Ufalme akiwa ni “Mwana wa Daudi” ingawa ktk kipindi hicho alikuwa ni Mwana wa Adamu, yule Masihi, bali Bartimayo alimwita Mfalme wake ili amweleze shida yake; huo ni zaidi ya Ufahamu wa kawaida wa dini!

  Mara nyingi dini haimfikishi mtu ktk kiwango cha kuwa na imani, kwa sababu “… imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Rm 10:17). Basi iwapo moyo wako utajaa mambo kama haya unayonifundisha, ambayo si Neno la Kristo, hiyo imani kama iliyomponya Bartimayo nitaipata wapi? Tena basi, iwapo nitatoka nami niwafundishe watu mambo haya ambayo hayamo ktk Biblia, hilo Neno la Mungu, dada yangu, huoni kwamba ni kujipalia makaa ya moto kichwani; maana Neno linasema “Usiongeze wala kupunguza …”!

  Neno la Mungu pekee ndilo ambalo ndani yake imewekwa “TRANSFORMING POWER” ambayo hukufanya uwe mwana wa Mungu, maana hilo Neno ndilo Roho. Lakini Neno la Mungu linapochanganywa na mafundisho ya dini, huzalisha watoto chotara, hybrid ambao huifanania dini na hivyo kukosa hesabu ktk Ufalme wa Mungu kutokana na unyonge waliourithi kutoka mafundisho hayo!

  Ishara na miujiza ni vitu vizuri sana, tena humtukuza Mungu, maana Mungu alipo, mambo hayo ni LAZIMA yawepo! Lakini ishara haziwezi kulitangulia Neno, hilo ambalo twapaswa kulipokea loooote; Mt 4:4 “Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Jilinde na michanganyiko ya Neno na hekima za watu, kwani vipawa havina majuto; pia elewa kwamba yule “inner man” atadumaa na mwishowe kufa kabisa, maana yeye hula KWELI ya Mungu pekee!

  Katika kila hali, bado ninaamini kwamba napaswa niwe kama huyo kipofu, hebu zifikirie zile kelele za makutano, unadhani ni kelele yake ndiyo iliyomfanya Kristo ASIMAME na kumwita? Hapana, Yesu hasikiagi kelele za watu, yeye huisikia Imani tu, imani ndani ya kipofu huyu ndiyo iliyomsimamisha Kristo kama alivyosimama kwa yule mwanamke mwenye kuvuja damu!

  Kuna hadithi ya Bartimayo, nadhani hiyo inaweza kukufundisha kitu zaidi cha kukusaidia kuliko hili fundisho linalokuua, maana linalichafua Neno la Mungu; nitakuletea hiyo!

  Gbu my sister!

 43. Esta umefunga mjadala wakati hoja zangu hujajibu? Usikimb,jibuie kaa tupige kazi ,jibu hoja na maswali yangu.

 44. Dada Esta,

  Ninakushukuru kwa maelezo mazuri, yanayoonesha jitihada uliyonayo ktk kumfanania Bwana, ile nia.

  Pia, imekuwa ni jambo zuri kwamba umelisemea hilo la mauaji, na kwa vile ni jambo la habari, ninapaswa nikuamini wewe kwa kauli yako hii ya kwamba mchungaji hakuua, maana wewe ndiye uliye karibu zaidi na kundi hilo, labda ikithibitika tofauti!

  Pia ninakushukuru kwa kunikaribisha huko Siloamu, asante sana, lakini kuna jambo dogo ambalo niliomba nipate maelezo yake ktk usahihi wa Maandiko ili mnithibitishie “tendo” la kushika kwenu Neno, ngoja ninukuu tena kama hukuliona, nilisema:
  “”Msipate tabu ya kunialika nije niyaone hayo mliyonayo, mimi mkinionesha tu ni wapi katika Biblia mlipopewa ahadi ya ujio wa:
“Mjumbe wa Mapenzi ya MUNGU Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi HakiKazi12″, ninawahakikishia kwamba mtaniona huko Siloamu na nitajitambulisha mbele yenu na nitazirejea kauli zangu zote nilizoziandika hapa na kuzimeza, kisha nitayakana Maandiko kwa kuchukua jina la “Eliya” badala ya Jina la Yesu, hilo ambalo familia yote ya mbinguni na ya duniani inaitwa!””

  Labda ktk hili nikuache kidogo utafakari kwanza.

  Ila ninapokusubiri, basi ngoja tuutazame huo mfano wa kipofu aliyekuwa ameketi kando ya njia …!

  Gbu!

 45. Unapofunga mjadala ESTER ninakuasa yafuatayo:
  1. Acha kuongea chochote kwenye hadhara au kuandika kwenye mtandao kuhusu lolote kama hukijui vizuri na huna uwezo wa kukitetea, hii itakupunguzia udhia mwingi.
  2.Usipate mhemuko wa mafundisho au mahubiri ukadhani unaufahamu wa kuwafundisha na wengine. Kwani sio wote wanaishi kwa mihemuko.
  3.Mtafute roho mtakatifu akutie kwenye kweli yote ya Mungu wanadamu watakupeleka usikokujua, maana sikuhizi huduma nyingi zinakimbiza maslahi ya matumbo ya watu, na tunawatumishi wengi wanaomiliki huduma hizi kama duka la mangi.

  Mungu akusaidie utoke kwenye upotofu huo.

 46. NARUDIA TENA KILIMBA MIMI SIYO KIPOFU MAANA NINAMJUA NINAYE MUABUDU KUWA NI MUNGU ALIYE HAI MAANA NAONA SASA UNACHOANDIKA KIKO NJE YA NENO SITAKI KUENDELEA KUBISHANA NA WEWE KILA MMOJA ASHIKE ANACHOKIAMINI ILA ANGALIE USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA WEWE MAANA HATA NENO LINASEMA MUNGU ANGALIHESABU MABAYA NANI ANGESIMAMA. MANENO MABAYA YOTE ULIYOANDIKA HAPO JUU AMBAYO HUNA HAKIKA NAYO MUNGU AMEKWISHA KUKUSAMEHE NAMI NATUBU KWAAJILI YAKO.

  NIMEFUNGA MJADALA

  SHIKA NENO

 47. Hakikazi sina sababu ya kusukumana na dini zinazoabudu watu badala ya kumwabudu Mungu. Unajua kwa uhakika hatiya ya wa mwabuduo mtu ni wapi hilo sitaki kujadili. Niambie wale watu mliowazamisha Kagera ilikuwaje mchungaji naye asizame kama ukishindwa kutupa maelezo yanayojitosheleza tutajua ilikuwa ni mkakati wa kafara tu.
  Ndio maana mnahangaika na mambo ya nyota hayo yalikuwa mambo ya shehe Yahaya, Yesu lini alitufundisha mambo ya nyota. Mmeaminishwa uchawi mpaka sasa mnaupractice na hamuoni shida, Kwa kudanganywa eti ni damu ya Yesu, Yesu asingekuja duniani kama maji tu yangekuwa yabadilishwa kuwa damu, huo ni ushirikina pure, mkiomba Mungu wenu hasikii mpaka mfanya manyanga kama waganga wa kienyeji.
  Wiki kama mbili zimepita mkamleta huyo mnayemwita askofu ambaye hata nauli ya kumtoa kijijini kuja Mbeya mjini hakuwa nayo. Huyo askofu wawapi kama sio utapeleli wenu tu wa kuuhadaa umaa wa watanzania. Halafu kijijini lini kukawa na umoja wa makanisa ya kipentekoste, hicho kitakuwa kijiji cha kwanza. Mzee ndio kakomalia kwenye mimbari eti askofu askofu hakuna kitu hapo huo ni utapeli wenu tu.
  Nakuhakikishia huyo hajatumwa kajituma mwenyewe kwa shida zake mwenyewe na kwa kuwa kapata wajinga lazima ale, Yesu aliyetumwa hakuwahi sema uongo mbona huyu wenu uongo ni sehemu ya mafundisho ya kila leo. Hakikazi na wewe ni kipofu kama Ester ndio maana mnakubali kuwa mko kizazi cha nee wakati kabla hata ya kuja kwa Yesu vizazi zaidi ya arobaini vilikwisha pita Mathayo 1:17.

  Siloam huwa hamnaga hoja ila mmefundishwa kuwa wabishi tu, hivyo tumewazoea hivyo ILA MSIPO TUBU NA KUACHANA NA UDANGANYIFU HUO MMEBEBA TIKETI YA JEHANAMU.

 48. SHIKA NENO MLIYOPEWA NEEMA KUBWA NA BWANA

  KILIMBA MIMI SIYO KIPOFU NIMEINGIA KWENYE MADHABAHU YA SILOAM NILIKUWA KIPOFU SASA NAONA KWAHIYO NAOMBA NIKUHAKIKISHIE KUWA MIMI SIYO KIPOFU NINAO MWISHO KABLA YA MWANZO.

  UKITAKA KUJIFUNZA KUHUSU MAJIRA NJOO SILOAM MAANA HII SIYO MAJIRA YA MANENO BALI NENO KWA UHALISI WAKE

  SHIKA NENO TENDA NENO

 49. Esta,

  Kwa kuwa umeniambia maneno mazito kwamba niliondoka kwenye ibada zenu kwa sababu ya mizimu ya ukoo wetu, sasa kaa vizuri usikimbie mjadala, ili baadae tujue mimi na wewe nani ana mizimu.

  Kwanza nataka unipe maelezo/majibu ya wala watu mliowaua mkiwabatiza kule Kagera, maana naona mmjefanya kama hamjaliona hilo swali. Nipe jibu lake

  Pili, hebu niambie huyo ndugu Munuo alianzia wapi kabla hajaanza hiyo huduma yake ya Pool of Sloam?

  Tatu, Je laana za ukoo huwa zinaondolewa na jina, na je wale wanaokuja sloam wote majina yao yana laana za ukoo?

  Nataka ujjue pia hili, mpaka nikaamua kuja hapo Mbezi kwenu, kuna mtu kutoka kwenu aliniletea barua ati kwamba Mungu amemuagiza aje aniambie kuwa mimi natakiwa kumtumikia Mungu hapo Sloam.

  Ndo nikaamua kuja siku moja kuona mnachofanya, nilikaa nusu saa tu, nikaona jinsi ambavyo ni kupoteza muda hata kukaa mpaka ibada yenu iishe. Kwanza ile theolojia iliyo ndani ya nyimbo zenu yenyewe tu ni majanga. (Mimi ni song writer and singer)

  Kuna mtu mmoja nilimkuta hapo niliwahi kufanya nae huduma aliniona siku nimekuja , baadae aliniandikia e- mail akanimbia ”Sungura nilikuona kanisani kwetu, hapo wewe hupawezi, mpaka sisi tuliozoea”)

  Ati unaniambi labda nilifuata muujiza, mimi mwenyewe natambea na miujiza kama ulikuwa hujui.

  Esta , kaa tujibizane maana inawezekana hapo unasali hata hupajui kwa undani!

 50. SHIKA NENO
  Asante sana Hekima aonavyo mtu ndivyo alivyo, Lwembe ninachokueleza nataka usiwe kama yule kipofu aliyekuwa ameketi kando ya njia akiwa amevaa mavazi machafu, Lakini baada ya kusikia habari za yesu alipata ufahamu kuwa nitaona na akamwita YESU KWA SAUTI NA AKAMSIKIA NA AKAYAVUA MAVAZI MACHAFU AKAPATA KUONA. NINI MAANA YAKE: MAANA UKIWA HUNA UFAHAMU WA NENO LA MUNGU NDANI YAKO NI SAWA NA KIPOFU NA UNATEMBEA NJE YA NENO YAANI KANDO YA NJIA LAKINI UKIJIFUNZA NENO LA MUNGU NDIPO UNAWEZA KULALUA MAVAZI MACHAFU YAANI KUACHA DHAMBI NA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KUTENDA SAWA SAWA NA NENO, UWE NA IMANI, UTAKATIFU YAANI KUKAA KWENYE TOBA SIKU ZOTE NA UTII, UTII YALE YOTE UNAYOAMBIWA NA MUNGU KUPITIA MTUMISHI ALIYE MSIMAMISHA. KWAHIYO MIMI NAFURAHI SANA LWEMBE KWAAJILI YAKO MAANA NAJUA NITAKAVYOENDELEA KUKUFUNDISHA UTAPATA UFAHAMU NA UTAMJUA MUNGU WA ELIYA.

  NARUDIA KAMA NILIVYOANDIKA PALE MWANZO MSIPENDE KUHUKUMU MCHUNGAJI HAJAUA UKWELI UPO NA UMETHIBITIKA. KITU KIMOJA NATAKA NISEME NINA UFAHAMU MKUBWA AMBAO HAUWEZI UKANIRUDISHA NYUMA MAANA MUNGU ALISEMA NAMI KABLA SIJAINGIA MADHABAHU YA SILOAM MAANA WALIO WAKE NA WENYE NEEMA KUBWA MUNGU ANAWAJUA NAKUHAKIKISHIA SIJAPOTEA NA NITAKAA NDANI YA HII HUDUMA MAANA NAMUONA MUNGU KWA UHALISI WAKE.

  LWEMBE KARIBU SANA SILOAM UJE UPOKEE NEEMA KUBWA YA MUNGU WA ELIYE MAANA TUNAMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI NA SIYO MJUMBE ELIYA MAANA YEYE AMEFANYIKA DARAJA FOR TRANSFORMATION NOTHING ELSE.

  SHIKA NENO TENDA NENO

 51. kilimba usitake kulisukuma basi lililokwama ukiwa ndani yake sanasana utang’oa viti na bado halitatoka mpaka ukubali kushuka! na wewe ujiitaye pastor danieli uliwahi kufikiri unajiita Mchg lakini huna hekima? unaweza kunipa maelezo yanayojitosheleza kuhusu ibada ya kishetani na ibada ya Mungu? na wewe sungura nimefurahi sana kwaajili ya swali lako kuhusu ubin wetu ujue hata kipindi cha ibrahimu yakobo mwanzo 17:1-8+mwanzo 30,31,32,na 33: yote ili MUNGU aweze kuwabariki aliwabadilisha majina ni kwa sababu jina lako linabeba Baraka zako, hatima yako, nyota yako,na maisha yako. kipindi cha Yesu Yohana 1:12-13 “¹² Bali wote waliompokea yaani wale waliaminio jina lake aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. “¹3 waliozaliwa si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya Damu, wala si kwa mapenzi ya mtu bali kwa Mungu” wakolosai 1:13 unaokolewa na unahamishwa kila aliyekubali kuokoka ubin wake sio mizimu tena ndio maana ukisoma ufunuo 5:8-12 imeweka wazi kwamba YESU alikuja kutununua kwa Damu yake tutoke kwenye makabila, lugha, jamaa, na makabila na ukoo.

 52. Shika neno mliopewa neema na BWANA! ama kweli dini hata uwapigie kengele hawaelewi,(wanaelewa sana) katika matayo 13:16-17 Neno limesema “heri macho yenu kwakuwa yanaona nature masikio yenu kwakuwa yanasikia Kwa maana manabii wengi nature wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona wasiyaone na walitamani kuyasikia mnayoyasikia wasisikie” Je, ni kitu gani kilikuwa kinazuia? wakati tunaona ni wenye haki na ni manabii? jibu tunalipa katika Zaburi 11:3 “Kama misingi ikiharibika mwenye haki atafanyaje?”„„„„ inamaana kinachosababisha wengi kutokuelewa na kutokumwelewa aliyetumwa ni misingi mibovu kwenye nafsi ambayo no kichaka cha dhambi, uovu, na uasi.

 53. kiukweli hizi imani zimeshika kasi sana hivyo cha msingi nikwatu kumtafuta roho mtakatifu coz haya makanisa ya sasa watu hawamwabudu Mungu wanamwabudu mtu hiyo ni hatari kubwa mno, ila kwa wote mliopotoka huko siloam nawapa pole, coz eti mnatoa maganda ya bibilia eti yana laana maana mengine ni meusi mnayatakasa kwa kuyajaladia hembu nionyesheni ni wapi imeandikwa kwenye bible kuwa jalada lake ni laana nyeusi na ni wapi bible imeonyesha kuwa mtu ubadilishwe jina la mwisho liwe la kwanza huko ni kukosa maarifa bibile inasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kweli nawasikitikia wote wana siloam mnaomwabudu eliya ila si YESU ila “YESU ATABAKIA KUWA YESU” pia mtambue ni nyakati za mwisho

 54. Hekima Eliya,

  Msipate tabu ya kunialika nije niyaone hayo mliyonayo, mimi mkinionesha tu ni wapi katika Biblia mlipopewa ahadi ya ujio wa:
  “Mjumbe wa Mapenzi ya MUNGU Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi HakiKazi12″, ninawahakikishia kwamba mtaniona huko Siloamu na nitajitambulisha mbele yenu na nitazirejea kauli zangu zote nilizoziandika hapa na kuzimeza, kisha nitayakana Maandiko kwa kuchukua jina la “Eliya” badala ya Jina la Yesu, hilo ambalo familia yote ya mbinguni na ya duniani inaitwa!

  Nitajifanya sijui kabisa kwamba, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo ndilo linalopaswa litukuzwe ndani yetu, nasi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo. (‭2 THE.‬ ‭1‬:‭12‬ SUV), badala yake nitalitukuza jina la Eliya huyo “Mjumbe wa Mapenzi ya MUNGU Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi HakiKazi12″ ambaye hayumo ktk Maandiko bali nitakomaa kama aliyepagawa mapepo niking’ang’ania kwamba yumo ktk Maandiko na ametumwa na Mungu!

  Pia, sintajali jambo la kwamba Jina la Yesu ndilo Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; (‭FLP.‬ ‭2‬:‭9-10‬ SUV) nitajiunga na kundi lenu, kwa jeuri, tutaendelea kulitukuza jina la “Mjumbe wa Mapenzi ya MUNGU Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi HakiKazi12″ na kuwafundisha wengine kufanya hivyo licha ya kujidai kwetu kwamba hatumwabudu huyo, ktk hilo tutajitahidi kuendelea kuwavuruga wote wanaotupinga kwa kuwashushia mambo yasiyoeleweka, bali tukiliitia jina la Mungu wa majeshi kupitia “Mjumbe wa Mapenzi ya Mungu Eliya Adamu wa Pili Mungu wa Majeshi HakiKazi12” ili kuwachanganya walio nje ya imani yetu tukiwang’ang’aniza waje wajionee wenyewe ili kama nasi tulivyokuja tukaishia humu, nao waje na hivyo kuwavuta wooooote ambao majina yao hayajaandikwa ktk Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo!

  Haya Hekima Eliya, “Fanya jambo unalolijua”, nipe hiyo rejea ya ahadi ya nabii wenu kama mnavyomtambulisha;
  Nami nitayatimiza yote niliyoyasema!

  Ninakusubiri “utende hilo neno ulilolishika”!!!!

  Gbu!

 55. “Shika neno mliopewa neema kubwa ya Mjumbe wa Mapenzi ya MUNGU Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi HakiKazi12” Huwezi kufanya jambo usilolijua, vilevile huwezi kuishi maisha usiyoyajua hii ina maana upo jinsi ulivyo kutokana na ufahamu wako. RUM 8:5 wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale tuifuatayo Roho huyafikiri mambo ya Roho. Neno la MUNGU linasema ukijifanya unajua, haujui kama inavyokupasa kujua. hata siku moja SILOAM hatujamwabudu MJUMBE(ELIYA AD2) tunayemwabudu ni MUNGU atendaye kazi ndani yake, kama na ivyo ni kosa basi na wewe unayeyatetea maandiko utakuwa umekosea kama tunavyosoma kwenye 1FAL.18:36 ELIYA alimwita MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Israel. Ninatubu kwa maneno yote mliyotoa pasipo kuwa na ufahamu. MUNGU wa Majeshi awabariki.

 56. Dada Esta,
  Usiwe nawe kama wale mabinti za Lutu na waume zao waliokataa kuondoka Sodoma; hilo si kanisa ni ngome ya pepo la dini, hilo linaojiita “Eliya, Adamu wa Pili, Mungu wa majeshi”, huyo Munuo anatumika tu kama chombo!!! Biblia yako si unayo, kwanini huyakagui hayo kuuona ukweli wake? Usikubali kuwa mjinga!!!!

  Kimbia dada yangu, kungali kweupe, saa ya mateso yaja ambayo hutaweza kufanya chochote zaidi ya kubakia humo utumwani ukilia na kusaga meno hapo utakapoyakumbuka haya tunayokuambia leo hii yaliyo Kweli ya Mungu!

  Unaambiwa mchungaji wenu kaua watu wawili “akiwabatiza”; hata hausimami kujiuliza ni mungu gani huyo anayewaua wanaomwendea? Hauoni kuwa hiyo ni tabia ya yale mapepo (jeshi) yaliyo waingia wale nguruwe na kuwatumbukiza mtoni yakawaua wote, ila leo hii, ndiyo hayo baada ya kuondoka makuburini, sasa yako kanisani kwenu, hilo kubwa lao ndio linajitambulisha kama mungu wa hilo jeshi la mapepo!!! “Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.” (‭MK.‬ ‭5‬:‭9‬ SUV)

  Dada jitahidi usiwe nawe mmoja wapo wa hilo jeshi mnaomuabudu huyo “Adamu wa Pili, Mungu wa majeshi”; kumbuka, Mungu hadhihakiwi; utashangaa nawe siku utakapotumbukizwa mtoni na kushikiliwa huko chini ya maji mpaka kuzimu!!!

  Gbu!

 57. SUNGURA SIJAKUJIBU SWALI LAKO LA PILI UMESEMA UBINI WENGI TUNATUMIA ELIYA, HII INAMANISHA KUWA TULIZALIWA NA WAZAZI WETU NA WAKATUPA MAJINA AMBAYO MENGINE NDANI YAKE YAMEUNGANISHWA NA LAANA YA UKOO, MIZIMU NK. KWA MFANO, MAMA ANAMPA MTOTO JINA TABU UKIMMULIZA ANASEMA NILIPATA TABU SANA NA HUYU MTOTO MAISHA YAKE YOTE ANATEMBEA KWENYE MATATIZO MENGI NA JINA LA BABA NI MASUMBUKO AU LINGINE LOLOTE AMBAYO SIYO MAJINA YA KIUNGU UNAKUTA HATA KAMA UMESOMA AU UNAFANYA BIASHARA UNATUMIA NGUVU NYINGI AMABAYO WENGI IMEWAPELEKEA KUKATA TAMAA, KWAHIYO BASI KUTUMIA JINA LA ELIYA MAANA YEYE NDIYE BABA YETU WA ROHONI NA NI JINA LILILOJAA NEEMA KUBWA YA MUNGU SASA ILI UPOKEE HAYO MAFUTA NI LAZIMA UWE NA JINA AMBALO NI LA KIUNGU. KAMA UNASOMA KITABU CHA NENO LA MUNGU KWANINI ABRAHAMU ALIBADILISHWA JINA NA MUNGU NA KUITWA IBRAHIMU BABA WA MATAIFA MENGI MUNGU ALIONA AKIENDELEA KUTUMIA ABRAHAMU HATABARIKIWA NA SISI TUNA SHIKA NENO NA KULITENDEA KAZI ILI TUPOKEE YALE YA UFALME WA MUNGU.

  SHIKA NENO TENDA NENO!

 58. Sungura usinichekeshe ulitoka kwasababu ulikimbizwa na mamizimu ya kwenu ambayo haitaki umtumikie Mungu. Penye Mungu wa kweli upinzani ni mkubwa na kama humaanishi lazima ukimbie. ILA SASA SUNGURA NAKUKARIBISHA KWA MARA NYINGINE UJE UONANE NA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU. NA KITU KINGINE MADHABAHU YA ELIYA HAITEMBEI KWENYE MAJIRA YA MIUJIZA, NA KAMA ULIFUATA MIUJIZA PALE HAMNA MIUJIZA MAANA MADHABAHU INATEMBEA KWENYE UFAHAMU AMBAYO NI MAARIFA YA MUNGU.

  NENO LA MUNGU LINASEMA WANANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA, SASA USIINGIE SHIMONI KWA KUKOSA MAARIFA. MAANA HATA WAKATI WA YESU, YESU ALIWAULIZA WANAFUNZI WAKE NINYI MNANITAMBUA MIMI KAMA NANI, NI PETRO PEKE YAKE NDIYE ALIFUNULIWA NA MUNGU WENGINE WOTE WALIKUWA HAWAJUI KUWA WANATEMBEA NA YESU. HII NI SAWA NA KIZAZI HIKI WATU HAMJAMTAMBUA NABII NA WENGINE KUWA NA MASWALI MENGI HUYU NDIYE ELIYA ALIYEMSEMA YESU AU BADO ANAKUJA. KAMA HAMUAMINI BASI ZIAMININI KAZI ZAKE. KWASASA KANISA LA SILOAM KILA MKOA, WILAYA LIPO NA SASA KUNA MATAWI KENYA, UGANDA, DRC, MALAWI, ZAMBIA, MSUMBIJI HIZO KAZI TU ZINALITETEA KANISA NA MAKANISA HAYO YOTE YANAANZISHWA KWA NENO NA MAFUTA YA MUNGU MWENYEWE. NA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU HARUHUSU KABISA KUTEGEMEA MISAADA HAKUNA KANISA LILILOJENGWA KWA MISAADA YA KUTOKA NJE.

  NAWAKARIBISHA WOTE MADHABAHU YA ELIYA YENYE NGUVU YA MUNGU NA WIVU WA KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI

  SHIKA NENO TENDA NENO!

 59. Ester we ni kipofu japo unajifanya unaweza kuona, majira sio jina la siku wala mwezi. Nimewahi uliza maana ya majira humu huwa hamjibu mnakuja na vimaelezo virefu visivyozingatia mwelekeo wa mjadala.

 60. Esta,
  Binafsi nilishaingia na nikatoka, hata saa moja sikumaliza!
  Unasemaje?

  Halafu mbona wote naona kama bini
  username) zenu zote ni Eliya, hiyo ina maana gani?

 61. Ukitaka kujua what is inside then go inside and u will find the truth, yote mlioandika hapo juu ya kuipinga SILOAM hayana ukweli ndani yake na wengine mnaandika kwa ushabiki tu kama ilivyo simba na yanga. Ukweli ni kwamba mmehukumu sana lakini nawashauri msome mathayo 7:1- 3 Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi na Mungu maana kipimo mpimiacho ndicho mtakachopimiwa. Ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza ndio uondoe kibanzi ndani ya jicho la mwenzio.

  Neno la Mungu linasema usipoona huwezi kupata maana upofu ndio unawafanya wengi kutokumuamini mungu wa kweli, SILOAM hamna ibada ya kupandisha mapepo kama maada ilivyoandikwa, NATUBU KWAAJILI YENU MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU ELIYA NI MTUMISHI WA KWELI MAANA YEYE HAPENDI UCHAFU NA WOTE WALIOONDOKA SILOAM NI KWASABABU WAMESHINDWA KUACHA DHAMBI NDIO MAANA WANAKIMBIA HALAFU WANATAKA KUMCHAFUA NABII, SISI TUNAWAPENDA WOTE NA NDIO MAANA TUNASIMAMA KWAAJILI YENU KUTUBU ILI MUNGU ASIANGAMIZE MAANA NENO LINASEMA MMOJA AKISIMAMA MUNGU HATAANGAMIZA. TOBA NI UFUNGUO AMBAO UNASABABISHA MUNGU AKUFUTIE HUKUMU ZOTE NA KUKUHESABIA HAKI. NA YESU KRISTO ALISEMA NAWAPENDA WENYE DHAMBI NAWACHUKIA WANOKUFA NA DHAMBI KWAHIYO INATUPASA TUTEMBEE SAWA SAWA NA NENO MAANA MUNGU ANATUWAZIA YALIYO MEMA SIKU ZOTE.

  KUHUSU MAJIRA KUANZIA SIKU NA MWEZI, SOMA MWANZO 1:1-31 NA MWANZO 2:1 KUNA MAJIRA HALISI YA MUNGU. JUMATATU MPAKA JUMAPILI NI MAJIRA AMBAZO ZILIANZISHWA NA WATU NA ELIMU ZAO MAANA HIYO NI MIUNGU. KILA MMOJA ANAHITAJI KUFANIKIWA ROHONI NA HEKALUNI SASA KAMA HUJUI NI MAJIRA IPI UTAFANIKIWA VIPI. MIEZI YA KIUNGU UKISOMA KITABU CHA ESTA UTAONA JINSI KERUBI ALIVYOCHEZA NA MAJIRA ILI KANISA LISIONEKANA LIKAFUNIKWA NA KUONA ALIYEOKOKA NI YULE MWENYE SHIDA, MASKINI, MNYONGE WAKATI SIYO UKWELI NA KAMA NI HIVYO MATAJIRI WASINGEKUWA WANAKUFA. LAZIMA TUJIULIZE TUKO HAPA KWASABABU TUMEJIUMBA WENYEWE AU NI MUNGU ALIYETUUMBA. NAOMBA NIWAULIZE KWANINI UKIWA MJAMZITO (MJAMWEPESI) HOSPITALI (MATENGENZO) WANAHESABU MWEZI NI WIKI 4 SAWA SAWA NA SIKU 28, TAREHE 29, 30 & 31 ZIMETOKA WAPI NA KWANINI MWANAMKE ANAPATA SIKU ZAKE KILA BAADA YA SIKU 28 NA SIYO 29, 30 AU 31. MSIHUKUMU NI MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU ELIYA NDIYE AMBAYE MUNGU AMEMFUNULIA HII SIRI KUBWA AMBAYO IMEREJESHA UUMBAJI WA KANISA KUMILIKI NA KUTAWALA. MSIISHAMBULIE SILOAM NJOONI MJIFUNZE MPATE UFAHAMU ILA MKUBALI KUACHA DHAMBI KABISA MAANA MUNGU HACHANGAMANI NA UCHAFU. SIJAWAHI KUONA MTUMISHI AMBAE HACHANGAMANI NA UCHAFU NA ANAIKEMEA DHAMBI KAMA NABII ELIYA NA UKIJA KANISANI ANAYEWAHI NDIYE ANAKAA MBELE MAANA YEYE HAANGALII WENYE FEDHA KUWAWEKA VITI VYA MBELE MAANA KAZI YAKE NI KUHAKIKISHA KILA MMOJA ANAMUONA MUNGU NA HAYUPO KWENYE TAMAA YA FEDHA. MIMI MWENYEWE NI USHUHUDA NIMEPITA KWENYE MATESO MENGI LAKINI BAADA YA KUJIFUNZA NENO NA KUWA NA IMANI KUWA MUNGU ANAWEZA NIMEFUNGULIWA NAWEZA KUSOMA NENO NIKALIELEWA NA KUWASAIDIA WENGINE. NAWAOMBENI SANA MSIHUKUMU PASIPO KUJUA NJOONI MJIFUNZE NA KAMA MANASOMA GAZETI LA NEEMA KUBWA MMEONA USHUHUDA WA ASKOFU KUTOKA MBOZI HAPO NDIPO NIMEAMINI KUWA TUAHITAJI KUJUA SANA NENO ILI TUONE FURAHA YA KUMTUMIKIA MUNGU.

  TATIZO AMBALO WENGI LINAWASUMBUA NI KUTOKULIJUA NENO VIZURI LAKINI UKISOMA NENO VIZURI UTAPATA UFAHAMU AMBAO UTAKUONDOLEA UTATA AMBAO MNAUONA KUHUSU MADHABAHU YA SILOAM Soma Mithali 8: 14-15, PASIPO UFAHAMU WA NENO LA MUNGU HUWEZI KUMILIKI MAANA WENGINE HUAMINI KUPITA KWENYE MATESO NA UTAABISHAJI WA MAGONJWA NA UMASIKINI NA MENGINEYO HUSEMA NI MAPITO HAYA NDIO MAFUNDISHO POTOFU MAANA MUNGU WA ELIYA SAWA SAWA NA NENO ANASEMA MUNGU HAKUUMBA MAGONJWA UHARIBIFU WOTE ULILETWA NA KERUBI BAADA YA KUIBA NAFSI HAI YA ADAM WA KWANZA NA NDIO MAANA YESU ALISEMA KWENYE Math 17:11-12 kuwa Eliya yuaja kwanza ili kutengeneza yote yalioibiwa na kerubi kwenye bustani.

  NAOMBA NIISHIE HAPA ANAYETAKA KUJIFUNZA ZAIDI NJOO SILOAM UKIONA YALIYOANDIKWA HAPO YAPO UNARUHUSIWA KUONDOKA HAKUNA ANAYEKULAZIMISHA LAKINI NAKUHAKIKISHIA UKIINGIA SILOAM HUWEZI KUTOKA.

  MUNGU WA MAJESHI AWAFUNGUE NAFSI ZENU MPATE KUONA ILI MUISHI SAWA SAWA NA MAKUSUDI YA MUNGU

 62. Kwa kweli dini hii ni kati ya zile zilizotabiriwa na Uongo.Dini gani inayojitenga na jamii.Mch mmoja wa kibaigwa kafiwa na kaka yake wa toka nitoke mwezi wa nne mwaka huu kasusia msiba akidai kuwa aamini juu ya kufa.wanaokufa ni wenye dhambi.mama yake kafariki wiki hili hakushiriki hata ibada wala chochote cha familia.Alijifungia ndani na mke wake na kuacha maelefu ya waombolezaji nje.Anadai imani yao aiamini juu mtu kufa,na wao hawafi wala hawaugui hivyo awezi kujihusiha na mwenye dhambi.Amesahahu kuwa Yesu ndiye mwenye kanisa na alikuja kwa wenye dhambi kuwaokoa na sio wenye haki.Kimsingi kushindwa kumsika mama yake mzazi tena mama yake alikuwa ni mchungaji anayeamini mambo ya wokovu katika kanisa letu.Na amekumchungaji(Mch Sara Oforo) mwenye kuheshimika na aliye mtumikia Mungu kwa uamini hapa dodoma.Kwa kweli hii haikubaliki na huku ni kupotosha neno La Mungu.Serikali kwa kweli inapaswa kufuatilia yendo za madhehebu haya mapya.yanapotosha jamii.Hata Yesu mwenye alihudhuria msiba wa Lazaro.Ndugu zetu wanaamini wao hawafi wala hawaugui.Watanzania wote tunaoumwa ni wenyedhambi.Wanasahau kuwa Yesu alisema mtaweka mikono juu ya wagonjwa na watapona.wao wametowa wapi imani hii kama sio ila za shetani kuwapotosha.
  Deusi wa Mnadani Dodoma

 63. Elisha na Vai,
  Mnasemaje kuhusu mchungaji wenu aliyeua watu wawili juzi kule Bukoba akiwa anawabatiza kisha akala kona kukwepa mkono wa dola?

  Huwa mnabatizaje kiasi cha mbatizwaji kuzama na kufa na mbatizaji kubaki salama?
  Na ilikuwaje akafa mtu wa kwanza mchungaji akaendelea kubatiza mpaka na wa pili akafa?

  Hebu nisaidieni kujua!!

 64. Aliyetumwa na Mungu lazima aseme sawa na neno la Mungu linavyosema, sasa leo hii wanaojinadi wametumwa ndio wapotoshaji wa kwanza wa kweli ya neno la Mungu. Hapo unajiuliza wametumwa na nani hawa. Kwenye hili Elisha hata kiongozi wako hana uwezo wa kulikanusha, ninyi mnakubali kwa kuwa mmetiwa hofu, basi.

  Elisha umenishauri “USIPENDE KUBISHA BILA UTAFITI NENDA SILOAM UONE MUNGU WA KWELI KUPITIA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU” kwa taarifa yako nimesha hudhuria sana ibaada za siloamu, nimeongea na wachungaji kadhaa wa kadhaa, na washirika wa kutosha tu, sasa utafiti huo labda nipe mongozo ufanyike je iliuamini kuwa siongei bila taarifa sahihi au nipe objectives za utafiti huo ilinikuletee taarifa na wewe ukahakiki.

  Tatu nimesoma sana vitabu vya nabii wenu, na magazeti yenu, na makala zake, mfano Gazeti la NEEMA KUBWA la tarehe 22 June 2014, page 15 makala inayosema WOKOVU WA KWELI, kwenye sehemu ya mbingu ya III, niuongo kusema eti Yesu aliporudi toka mlimani alirudi nyuma, huo ni utapeli.

  Na hata jina la gazeti limekaa kitapeli, sijawahi soma kwenye neno kuwa kuna NEEMA KUBWA NA NDOGO, exaggerations zinafanywa na wadunia, Rumi 12:1-2 unasemaje.

 65. Elisha nashukuru sana, lakini sijawahi kuwa na jaziba ninachokiandika cha weza onekana kama jazba labda kwa kuwa lugha yangu imenyooka tu, sijui kumremba mtu kinafiki.
  Elisha ujue huo ni utapeli wa mchana kweupe kizazi ni kizani wingi wake ni vizazi sasa uanachomaanicha kwenye mathayo 1:17 unataka kusema nini hapo, umekanusha pasipo kutoa maelezo. Toa maelezo kukataa hoja bila maelezo hakuonyeshi ukomavu Elisha.

  Kizazi chenu cha nne ni cha kitapeli tu, halafu mnajidhania kuwa mnatisha, hamna lolote mnalotisha, mmedanganyika na kutapeliwa. Watu wanawadharau kwa kuwa mmepoteza hata uwezo mdogo wa kutofautisha pumba na mchele umewatoka.

  Halafu hapa simuwakilishi mtu; mimi sio mchungaji useme ninawakilisha dhehebu au dini, ninawakilisha jinsi ninavyolielewa neno mimi binafsi.

  Kwa nini mnasema lugha vitu vilivyo kinyume na ukweli wa mambo hizo lugha za kitapeli na uongo halafu mnaita lugha ya mbinguni, uongo ni lugha ya Lucifer kwa taarifa yako maana yeye ni baba wa huo.

  Mimi huwa nauliza maswali tu ila mmeshindwa kuyajibu kwa hivyo mnaniweka kwenye watu wenye jaziba kwa lipi sasa. Ninyi sio wa Yesu ninayemsoma kwenye neno na ndio maana hata Roho mtakatifu hamjazwi. For your information Roho mtakatifu anakaa mahali palipo safi, sasa kwa kuwa kiongozi wenu anajua alivyo wachafua mioyo kurahisisha mambo kawaambia hamumuhitaji Roho mtakatifu, eti mna roho saba, Otherwise mnishawishi kuwa Elia wenu anaufahamu mkubwa kuliko Yesu aliyewakataza wanafunzi wasitoke kwenda kwenye huduma mpaka wajazwe Roho Mtakatifu.

  Soma Mathayo 5:33-37 Yesu anasemaje kwa habari ya viapo. Mmekariri neno wala hamjalishika ndio maana mnadanganyika kirahisi. Wewe umeshakula viapo vingapi kwa kiongozi wako.

  Elisha na wanasiloamu mnaishi kwa hofu tu hapo mlipo ya kumwogopa Elia lakini nawahakikishia hawezi kuwafanya lolote, matapeli wote wanatumia gear hiyo kuwa ukimsema ghadhabu ya Mungu itakushukia, hata matapeli wa uganga wa kienyeji siwanafanya hivyo kwani hamjawahi sikia. Mnatishiwa kwa maneno mazito mazito, NEEMA KUBWA, Mungu ana Neema tu hana neema kubwa wala ndogo.

  Mfano wa Yesu kutumia tope kumfungua kipofu haufanani hata kidogo na kuchukua udongo na kwenda nao huko kwenye matambiko yenu. Lete hoja zenye mashiko.

  MSICHONIELEWA WANASILOAM NINATAMANI SAANA KUMPENDEZA YESU, LAKINI SIO KUFURAHISHA MTU ANAYETAFUTA MASILAHI YAKE BINAFSI.

 66. SHIKA NENO TENDA NENO, UFAHAMU WA NDUGU YETU KILIMBA NI MDOGO MNO NA INASHANGAZA SANA KUONA ANAJIWEKA MBELE KUWAWAKILISHA DINI NA MADHEHEBU ANAWAPOTOSHA SANA.

  NAMUOMBA NDUGU KILIMBA AJE KTK BIRIKA LA SILOAM ANAWE NA AONE. KUCHUKUWA UDONGO SIO MATAMBIKO, YESU MWENYEWE WAKATI ANAMPUNYA MTU ALIYE KIPOFU ALITUMIA MATE YAKE KUCHANGANYA NA UDONGO NA KUMPA MWENYE YULE KIPOFU APAKAE MACHONI NA KUMWAMBIA NENDA KTK BIRIKA LA SILOAM AKANAWE NA ALIPONAWA AKAONA, JE YESU ALIFANYA MATAMBIKO?

  PIA NDUGU YETU KILIMBA ANATUMIA SANA LUGHA YA JAZBA NA MANENO YASIYOFAA, KWELI DINI NA MADHEHEBU UPOTOFU NI MKUU. NAKUSHAURI USIPENDE KUBISHA BILA UTAFITI NENDA SILOAM UONE MUNGU WA KWELI KUPITIA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU

  KUHUSU VIZAZI, UMETOA ANDIKO MATH 1:17 HATA MAANA YAKE HUJUI, VIZAZI VILIVYOTAJWA HAPO NI UZAO.

  KIZAZI CHA NNE KINATISHA CHINI YA KUHANI AFUNDISHAYE MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU, HIKI NI KIZAZI CHA UFAHAMU KUAMILI HILO ANGALIA NDUGU ZANGU WA SILOAM WANAVYOTOA NENO KWA UFASAHA WAKIJUWA FIKA UUMBAJI WOTE NA KUSUDIO LA MUNGU.

  SHIKA NENO TENDA NENO

 67. Kweli nilwahi kwenda mojawapo ya makanisa hayo nikiwa mchanga sana kiroho, niliyoyakuta huko nililia bila kupenda,
  nilikuwa sijui taratibu zao,sadaka zinatolewa kwa awamu na upako unatolewa kwa kiwango chako cha sadaka!!!!??
  nilishushwa madhabahuni na elfu moja yangu ya sadaka eti kwa sababu mchungaji ameita wenye elfu kumi!!!!!!

  mh! hali inatisha lakini hakuna kuogopa maana maandiko yanatimia, kutokata tamaa ndio mpango mzima.

  tokeni tena mchana kweupe tena msihiriki maovu, usijali ulikokea hapo ukiona ibada zao haziendani na neno okoa roho yako kabla haijaja ile siku parapanda.

 68. Gema unang’aka kwa alichokisema pastor kwa kuwa mnavyofanya vingi vinasura ya kishirikina. Mnachezea wajasiria mali nyie. Unataka neno soma Mathayo 7:15-20. Neno lilishatuonya mapema kuwa wengine watakuja wakijiita mie ndiye kristo (AD 2). Endeleeni maana hata waswahili waliliona wakasema wajinga ndio waliwao.

 69. Ninyi wana Siloamu,
  Kwamba juu ya maelezo na rejea zote za Maandiko mlizopewa na wapendwa wenye kuwatakia mema, bado hamjakamata chochote ili mchomoke toka huko kifungoni, ni hali inayotisha saaaana, sana!

  Kumbe kwa kadiri unavyolibeza Neno la Mungu, ndivyo unavyozidi kuzama mautini! Kwa jinsi ya mwenendo wenu, inadhihirisha kwamba nafsi zenu zimekwisha kufungiwa katika ngome hiyo inayofanya kazi ya kuyakusanya magugu, na hivyo HAMTATOKA tena humo mpaka utakapoletwa ule M……!!!

  Inasikitisha saaaana, lakini ndio hivyo, Neno sharti litimie, basi kutimiliwa kwenu na Neno hilo ni Utukufu kwa Mungu maana ni kwa hiari yenu kama Yuda, mmelikufuru Neno la Mungu, kwa kumuita huyo binadamu mwenzenu aliyezaliwa katika dhambi kwamba ni “Adamu wa Pili, Mungu wa Majeshi” na uchafu mwingineo, mmeonywa lakini hamtaki kusikia chochote kile zaidi chorus hiyo ya kuzimu; ama kweli Lusifa na jeshi lake!!! Basi Mungu awafanyie nini zaidi ya kulitimiza Neno lake juu yenu!!!??

 70. pastor Daniel ,huoni nakushauri kanawe kwanza kwenye birika then urudi mtandaoni nao kondoo unaowaongoza ndio waliokutuma hujatumwa na mungu kutoa hiyo huduma

 71. HOSEA 4;6 IKO WAZI
  WE UNABISHANA NA MTU AMBAE UFAHAM WE NENO HANA
  MARKO 9;11 IKO WAZI
  HAWAENDELEI BILA MISAADA, WAKATI NENO LIMESEMA ALAANIWE AMTEGEMEAYE MWANADAMU.
  ILAMRADI NENO MMEWAPA SASA NI WAO KULISIKIA NA KULITENDA
  COZ MATH13;9-MWENYE MASIKIO NA ASIKIE,
  JAPO MATH13:14-15 NA MATH15:-10 NA YOH4:22 INAWAFANYA WASIIELEWE TH POOL.
  ILA SISHANGAI COZ YOH 8;43-44 IMEWEKA WAZI
  SASA CHAGUA KUNAWA UONE AU UENDELEE KUWA KIPOFU
  NB UKIERPLY COMMENT REPLY KWA UFAHAM WA NENO SIO KWA SENTENCE200 BILA NENO COZ
  NENO LINASEMA NENO LA KRISTO LIJAZWE KWA WING NDANI YENU

 72. Hakikazi ad2 Eliya tunataka aokoke aende mbinguni, shetani muuji, na ndio maana anawafanya muwaze kuua ua tu, Mungu anataka kila mtu afikilie toba apatanishwe naye. Hatutaomba afe ila tunaomba Yesu amuokoe, aache uajenti wa kuzimu.

  Kuenea kwa kasi ni kutimiza neno tu waendao upotovuni ni wengi, kwani ulidhani mtakuwa wachache.

  Kwa taarifa yako hakuna neema kubwa wala ndogo kwenye neno, kuna neema ya Mungu tu, hiyo kubwa ni ya utapeli tu.

 73. Asante Mchungaji Daniel kwa kuliweka wazi, Munuo na hao manabii wauongo ni malango ya kuzimu, hili halina mjadala. Kanisa lazima tufike mahali pa kuwaambia hawa watu waziwazi, mbona tunaujasiri wa kuwaambia makahaba, wezi na walevi, iweje leo hawa wanaopindisha neno na kuleta udanganyifu tuwaonee haya.

 74. Jamani hebu tuweni makini kipindi hiki cha sasa! UGANGA WA KIENYEJI UMEHAMIA KANISANI! nataka nitoe rai kwetu wote; jambo la kuangalia si uponyaji tu bali ni nani amekuponya! Siloam ni ibada ya kishetani kabisa. Ngoja niwatajie ibada za Kishetani: 1. Kwa mch. Gwajima 2. Huyo Munuo 3. Nabii Bendera 4. Nabii Malisa.
  Ukubali usikubali hizo ni ibada na mafundisho ya kuzimu

 75. POLE VAI, ELIA MSANGI NAYE ALIJIITA HIVYO NA KUTUMIA MISTARI HIYO HIYO, AKAPATA WAFUASI WENGI TU, LAKINI ANGALIA ALICHOKIACHA NYUMA, NAMTAKA YESU NA SIO ELIA.
  NYIE MMEKAA KWA VITISHO VYAKE KUWA MKIMSEMA VIBAYA MTAPATA GHADHABU YA MUNGU. HATA WANGA WANAGHADHABU ZA MIUNGU YAO AU HULIJUI HILO.

 76. MUNGU ANISAMEHE MIMI KWA AJILI YAKO KWANI HUJUI ULISEMALO WALA ULITENDAO! LAKINI UJUE KUWA ELIYA SIYO MTU BALI NI MUNGU NDANI YA ELIYA! HIVYO ANAYEMTUKANA NABII ELIYA AMEMTUKANA MUNGU! MUNGU AKUJALIE USIFE KABLA HUJAFUNULIWA KUWA MWANA WA MUNGU NA KUUPATA WOKOVU WA KWELI NA SIO ULOKOLE

 77. VAI MNGEKUWA ROHONI USHIRIKINA MNAUPATIA WAPI, UAGUZI WA UDONGO, NA MAZINDIKO YA KUMIMINA VITU VYA KISHIRIKINA, HUO SIO ULOZI.
  MNGELISHIKA NENO LINGEBADILI MAISHA YENU KWA KUMFANANIA YESU NA MSINGEINGIZWA KWENYE MTEGO WA KUFANYA USHIRIKINA HUKU MKIJINADI MNA YESU. SHIDA MMEKARIRI KAMA TULIVYOKUWA TUNAKARIRI BIOLOGY AU WANAVYOFANYA WENZENU KUKARIRI KORANI.

 78. MPAKA SASA HIVI SILOAM IMEENEA TANZANIA NZIMA NA MATAIFA (KENYA,MALAWI,RWANDA,BURUNDI,ZAMBIA,UGANDA,DRC….) NA HAPA TZ PEKEE KUNA WANA WA MUNGU WA ELIYA WASIO PUNGA ELFU ISHIRINI INCHI NZIMA ! SILOAM SASA TUNA GAZETI (NEEMA KUBWA [kwa jina]) RADIO ILIYOPO MOROGORO [ikiwa kwenye majaribio yamwisho] KAZI HII YOTE IMEFANYIKA NANI YA MIAKA KUMI TU, BILA MSAADA WA WAZUNGU AU VATCAN. Je, dini mna miaka mingapi ? mbona mnapitwa hivyo ? simnasema mna mungu ombeni na mfunge amuue Eliya ! simnasema sio nabii wa kweli ?

 79. MAASKOFU ! Eliya aliwatangazia “Kama wewe unaona Mungu wako ni wakweli na wa Eliya ni wauwongo basi njoo msimamishe mungu wako na Eliya asimamishe wake halafu tuone nani atakufa ! MBONA HAMKUJA ! Akasema basi mwiteni yeye aje hata uwanja wa taifa kila mmoja amuite Mungu wake halafu tuone wanani mwenye Nguvu ! MBONA HAMKU JITOKEZA !

  UNAPOKOSA UFAHAMU,UNAKOSA MUELEKEO , UNABAKI KWENYE KITUO CHA KULALAMA – LALAMA !

  UNAE MUNGU ! MUOMBE AMUUE ELIYA,

 80. KWELI NI KWAMBA !
  Mti usiokuwa na matunda hata siku moja haupigwi mawe !
  PIA:
  Vilivyo hai ndio vinaongelewa, sio vilivyo kufa,
  PIA:
  Ukirusha jiwe gizani atakae piga kelele ndio limempiga !

  DINI NA MADHEHEBU MSIJISUMBUE, MTAPIGA KELELE HADI MCHOKE SILOAM TUNAZIDI KUFANIKIWA NA KWENDA MBELE !

 81. SHIKA NENO WANA WA MUNGU MLIOPEWA NEEMA KUBWA! KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU KWA PASAKA YA ROHONI YA MWEZI ELULI. MBARIKIWE NA BWANA YESU!

 82. Huna neno uliloshika wewe umeshika matango mwitu unayolishwa. Sasa Vai na wenzio mlioshiba matango mwitu mnamfanya Yesu ni mwongo au.

 83. 2NYAKAT 20: 20 NENO LINASEMA UKIMWAMINI MUNGU UNADHIBITIKA MBELE ZA MUNGU NA TUKIWAAMINI MANABII WAKE (WA KWELI) TUNAFANIKIWA. IKUMBUKWE KUWA MUNGU ALIPOTAKA KUWATOA WANA WA ISRAELI UTUMWANI ALIANZA KWA KUMTAFUTA NABII (MUSA) ILI AMPE AGIZO LA KUWATOA UTUMWANI. HIVYO BILA NABII WA KWELI HAUWEZI KUTOKA UTUMWANI! HII NI KANUNI YA UFALME WA MUNGU NA IMEFUNULIWA KWA KANISA PEKE YAKE. KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUPA NABII WA KWELI ELIYA WA KIZAZI CHA 4 AMBAYE AMETUTOA KWENYE UTUMWA WA DINI NA MADHEHEBU NA MAJIRA ZA GREGORY AMBAZO NI MAJIRA ZA FREEMASON! ASANTE MUNGU WA ELIYA! KWAKWELI NINAKUSHUKURU MNO KWA UFAHAMU MKUBWA WA NENO LILILOFUNULIWA NA MUNGU MWENYEWE KUPITIA ROHO YA ELIYA. HONGERA WANA WA MUNGU KWA KUVUKA PAMOJA NA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU/ NABII MWEZI ABU NA KUINGIA MWEZI ELULI. SHIKA NENO!

 84. VAI HIYO REHEMA YA NABII UNAYO NA YA MUNGU WAKE UNAYO, ILA YA MUNGU MUUMBAJI NA YA YESU KRISTO HUNA.

  WALA SITISHIKI VAI HATA MAPEPO NA MIZIMU HUWA INAJIFUNUA SI NDIO MAANA WATU WANAIGOPA AU ULIKUWA HUJUI HILI.

 85. NAOMBA REHEMA KWA AJILI YA MANENO YOTE YA UOVU NA UONGO YALIYONENWA NA HUYU MTU KWA AJILI YA KANISA LA MUNGU WA MAJESHI KWANI HAJUI ALISEMALO. UPO WAKATI MUNGU WA ELIYA UTAJIFUNUA KWAKE WAZIWAZI MAANA HATA MIMI MWANZONI NILIPOKUWA MJINGA SINA UFAHAMU WA NENO BALI NILIKUWA NA UFAHAMU WA DINI/ KILOKOLE NILIKUWA NAONGEA MANENO MACHAFU JUU YA NABII ELIYA LAKINI ULPOFIKA WAKATI WA MUNGU WA KWELI KUJIFUNUA KWANGU AKAJIFUNUA. KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA GAZETI LA NEEMA KUBWA NIMEONA LIKIWAFUNGUA WENGI NA WALE WALIOKUSUDIWA NA MUNGU KUINGIA KIZAZI CHA NNE WAMEPATA NEEME KUBWA YA WOKOVU WA KWELI. MUNGU TUNAKUSHUKURU KWA KUTUPA KANISA LA KWELI, NENO LA KWELI, NABII WA KWELI, MADHABAHU YA KWELI, MAJIRA NA NYAKATI ZA KWELI. SHIKA NENO!

 86. LIZY Kuna mwanasiloam aliwahi niambia wao hawahangaiki na kutoa mapepo, nikajiuliza Yesu aliyesema toeni pepo pozeni wagonjwa alikosea au wao wanamfuata nani jamani watu hawa. Wamebadili majina lakini umbea haujawaacha, chuki hazija waacha, uongo ndio namba moja, majidai na kujitapa ndio namba moja, nadhani hii ni branch nyingine tu ya freemason, na ilikujiosha wanajifanya kutulaghai kutoa nembo za maji. Nini nembo si bora wasingekunywa maji kabisa ilitujue wako serious. Ningekuwa mimi hata maji hao sinywi. Wanapenda muonekano wa nje lakini ndani wamejaa kutu. Nabii kawadanganya eti ISBN na namba ambazo product hupewa kama utambulisho kuwa zimekuwa approved ndio freemason.

 87. Kuja dada alinishawishi niende Siloam kuombewa, mmh kwa kweli nilishangaa. Kwanza mapepo hayakutoka, maji wanatoa nembo eti ya Freemason, wakanibadilisha jina eti la mwanzo linabeba laana, mafundisho yao nilitoka kapa. Kwa kweli mpk sasa sipati jibu khs hilo kanisa.

 88. Hakikazi Eliya “Ufalme wa Mungu hautangazwi bali unatawala” Unasemaje kuhusu Mathayo 28:19, unawafanyaje mataifa kuwa wanafunzi bila ya kutangaza habari za ufalme. Huo ni ujinga uliopindukia ndugu yangu, wewe hutawali bali umetawaliwa kifikra, na huna unalojua hapo ulipo ukiambiwa kesho utembee uchi na nabii utafanya hivyo maana wewe ni kama mzoga tu unapelekwa kila anakotaka huyo bwana wako.

  Shetani anachohangaika ni kukamata ufahamu tu halafu unakuwa kama zezeta, unabishania kitu usichokijua, mara vazi jeupe, basi waislamu waliwatangulia kwenye vazi jeupe. Poleni sana

 89. Hakikazi Eliya, endelea kufuata utapeli huo Mungu hatapeliwi, analiangalia neno linasemaje na wewe unaliishi neno kama lisemavyo basi. Huyo nabii ni tapeli, anawadanganya mchana kweupe na kwa kuwa mlisha jazwa ujinga kuwa hakuna mwingine na vitisho kuwa ukimsema vibaya utakufa, mnakubali kila anachosema. Eliya Msangi naye alitumia ujanja huo huo lakini, aliishia kuzini na wamama na mabinti zao, huku wababa wakiwaruhusu wake zao kwenda kupewa nguvu/maombezi na nabii. Tunaushaidi wakutosha kusema nabii wenu ni mwongo na Mungu hawezi tembea na mwongo. Ya huyo wa kwenu tutajua zaidi akisha ondoka maana hapo mlipo mnahofu, hamuwezi nyanyua midomo. Mfano soma gazeti lenu la neema kubwa uone jinsi anahangaika kudanganya watu kwa nini anasema mko kizani cha nne.

  YESU NI MPOLE NA WALA HAKUTISHA JAPO KUWA ALIKUWA NA UWEZO HUO WAKATI ANALIANDAA KANISA, ILA AJAPO MARA YA PILI ATATISHA, SASA MATAPELI WOTE WA KIIMANI HUTUMIA VITISHO KAMA DEFENSIVE MECHANISM WATU WASIJE HOJI WAKAGUNDUA UTAPELI WAO. MMEDANGANYWA KUMILIKI NA KUTAWALA WEWE UNAMILIKI NINI HAPO ULIPO, UTAKUFA MASIKINI UKIWA NA UKIRI WENU WA KITAPELI.

  Kukubali kila unaloambiwa hiyo ni aina nyingine ya utoto pia. POLENI NA SHUPAZENI SHINGO SHETANI ANACHEKELEA KUWA AMEWAPATA.

 90. Nyie wajoli wa “nabii eliya” Msangi au Mtishbite?
  Hahahaha… Mmenasa, chezea ngome nyie!!!!

  Mnaona aibu ama haswa ni waoga hadi mmeshindwa kujiondoa mautini!!! Si ajabu mnavyozidi kuharibika akili zenu kiasi kwamba hamuioni hata hatari mnayoikimbilia!

  Amewatisha kuwa mkijaribu kwenda kinyume naye ‘mtakufa’! lakini ukweli ni kwamba mkiendelea kukaa hapo mtaishia kama Sabato Masalia!!!!

 91. Bezaleli,
  Usijisumbue kupiga kelele huku,
  Kumbuka Kizazi cha nne,
  Ufalme wa Mungu hautangazwi bali
  unatawala !
  Kizazi cha nne Mungu wala Yesu wala Eliya hawatetewi,
  Wote tunajua kuwa Ukishupaza shingo yako kifuatacho ni kuvunjwa !
  Atakae taka kumfuata Mungu na Amfuate ! Asiye taka Kumb 28:15-68 imejibu kitakacho kutokea ! DINI MADHEHEBU achana nao hata kwa Yesu hawakumsikiliza ! kutoka na Nafsi ya Mema na Mabay

 92. Wapunch, 

  Shetani anavijua vilima vyote from where you can behold his great splendour, 
  “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake” (MT. 4:8)
  Its just a mirage! The whole thing is a hoax!!
  Amewapandisha kilimani huko mnakodhani faraghani, kisha AMEWAPOFUA macho yenu ya kiroho, akawatia tamaa ya mambo yasiyoeleweka wala kushikika, nanyi kwa upofu mmeyapokea bila rejea, ndio maana mnajiita kila aina ya majina, ile “fahari” mliyodanganywa!!!

  Huyo nabii wenu amejipachika u Eliya wa Yohana Mbatizaji huduma iliyokwisha kumalizika, wala hamshituki mlikague jambo hilo; kaendelea kuwakoroga kuwa yeye ni yule Eliya ajaye, mnameza tu! 

  Ndg zangu, mbona Maandiko yako wazi, kagueni muone iwapo huduma ya Eliya ni kwa ka kusanyiko kalikojichimbia huko kitongojini au ni huduma inayoletewa Kanisa lote la ulimwenguni! Ama kweli ktk siku za mwisho watajirundikia walimu, “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” (2 TIM. 4:3, 4)
  Wapunch, jaribu kujikumbusha uone ni lini ulipokuwa na uwezo wa kuitafakari kweli ya Maandiko ambayo Kilimba amekuletea ikuokoe? HUJAWAHI, nakuona unavyojiepusha nayo!!!

  Mkimbieni huyo mwalimu wenu aliyewachukua mateka kama Biblia ilivyosema kuwahusu nyote:
  “Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. (2 TIM. 3:6, 7 SUV)

  Unajua, “wanawake” wanawakilisha kanisa, basi ninyi mnakidhi namna ya Maandiko haya, kama Biblia ilivyotabiri, kwamba ni vipofu tena mu uchi na hamjui! Neno la Mungu pekee ndilo lenye kutusitiri aibu yetu, nanyi Neno hilo mmenyang’anywa na kupewa hadithi za kusisimua badala yake, kama: “Kizazi cha nne; Adamu wa pili, Mungu wa majeshi; nabii Eliya; Mjumbe wa mapenzi ya Mungu kupitia toba ya kweli iliyoniweka juu ya madhehebu na dini; na upuuzi mwingineo mwingi sana, ambao kwa uhakika mnapaswa kuungama ili mziponye roho zenu, uvumilivu wa Mungu unapowasubiri msiangamie kwa upumbavu wa dini mnaodhani mko juu yake kumbe mko shimoni!!!!

  Jaribu kuwaza, kwanini kwa kujifunza kwako kwa bidii umeweza kukariri marundo ya semi zisizo na maana yoyote, halafu umeshindwa kuelewa jambo dogo na la msingi kwamba Kristo pekee ndiye Adamu wa pili kwa jinsi ya uumbaji alioufanya Mungu kwa Neno lake??? Huku ndiko “”kutokuweza kabisa kuufikia ujuzi wa kweli”” Biblia ilikokutabiri kuyahusu makundi ya Cults kama hili lenu!

  Kimbiiiiia Wapunch!!! Mnazidi kuzamishwa ktk KUFURU, hakuna Neema inayoizidi hii anayokuletea ndg yako Kilimba, run for your life, its no joke brother, its abt to rain fire & brimstone, by then it will be over!!!

 93. Ninyi ni wadanganyifu ndio maana mnatumia majina feki. Wapunch is this your real name. Mko feki kama baba yenu alivyo feki. IMEKULA KWENU, MTAJITIA MOYO KWA KUWANUFAISHA WENZENU. MIAKA 430 ILIKUWA YA WANA WA ISRAEL UTUMWANI ACHA KUNDANDIA MADA USIZOZIELEWA MPENDWA.
  Sijawahi soma mtu akiongelea dini na madhehebu humu isipokuwa wanasiloamu, mmelishwa tango mwitu.
  POLENI NA MBINGU YA MUNGU MTAISIKIA NA KUISOMA HAMTAIONA NG’O LABDA MTUBU NA KUIFUTA KWELI.

 94. Am about18years old ASHUKURIWE MUNGU WA MAJESHI ADAM WA PILI MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU KUPITIA TOBA YA KWELI ILIYONIWEKA JUU YA DINI NA MADHEHEBU MAHALI AMBAPO JICHO HALIJAWAH KUSIKIA WALA MACHO HAYAJAWAH KUONA WALA AKIL HAIJAWAH FIKIR NDUGU ZANGU WAPENDWA KwA UPENDO WA MUNGU TUSOME kut6:2-3 ukisoma kwa ufahamu ambao unakuweka kuwa wa tofaut kuliko chochote utamjua mungu wa eliya ni nan sawasawa na mwanz15:15 mungu anasema na ibrahm kuhxu kizaz cha nne kwa sababu ya uovu wa waamori bado yesu anawakubalia wanafunz wake kwa kuulizwa kuhusu eliya marko 9:11-12 tena bado ukisoma malak4:5-6 bado tena yesu anawambia math17:10-12 hv mnajua tatizo linalowafanya hamuelew ni kwakutopanda juu mliman faraghan kufumbuliwa macho ya rohon math17 .tofaut yangu mim na wewe n kwamba na nabii wa kwel afundishae na tena amepewa agizo la mungu mwenyewe kutujenga sis katka roho na kwel tumetoka kwenye utumwa wa miaka 430 utumwan tupo kwenye majira na nyakat mpya ya kutawala na kristo mwenyewe miaka 1000 .

 95. Ni mwezi sasa tangu nilipo post hiyo post ya hapo juu kuuliza maswali yahusuyo ukiri wa wanasiloam kuwa wao wako kizazi cha nne, tangu wakati huo wamekuwa kimyaa. Hii nikuwa wamekuwa na wingi wa shughuli au ndio kuficha ukengeufu na udanganyifu wanaotumia kuwalaghai watu. Wapendwa mbinguni hatutaingia kwa kughushi neno ili tuonekane tuko bora kuliko wengine, kughushi ni uongo, kama uongo mwingine tu.

  Mpaka hapa ninashawishika kuamini kuwa HAWA WATU NI WAONGO MAANA WAMESHINDWA KUTUELEZA NASI TUJUE KUWA INAKUWAJE KIZAZI CHA SASA KUWA KIZAZI CHA NNE. HATUULIZI KIUSHABIKI TUNATAKA KUJUA KWELI ILI ITUWEKE HURU.

  USHAURI WANGU WA BURE MAFUNDISHO YENU YAMECHAKACHULIWA, NA KWA KUWA MUNGU SIO MUONGO NA HACHANGAMANI NA UONGO NINAWASHAURI MTAFUTE KWELI, MTUBU NA KUTANGUA MAAGANO YA KITAPELI MLIYOINGIA MAANA YANAZIPA UHALALI ROHO MBAYA KUTAWALA NAFSI NA MIOYO YENU. MUNGU NI MWINGI WA REHEMA, ATAWAREHEMU. BAADA YA HAPO MJIKITE KUMTAFUTA MUNGU, ACHENI KUKIMBILIA INJILI ZA KUAMSHA MIHEMUKO NA HISIA, MUNGU HATEMBEI KWA MIHEMUKO BALI ANATEMBEA KWA KANUNI ZILIZOPO KWENYE NENO LAKE.

  MATAPELI WENGI KAMA WAGANGA WA KIENYEJI TU WANAJUA JAMII INATAKA NINI NA NDICHO WANACHOWALETEA KATIKA MAHUBIRI YAO YALIYOJAA UDANGANYIFU NA HILA ZA MWOVU.

  KANUNI ZA KIMUNGU HAZINA TIJA UNAPOZIKARIRI KAMA SOMO LA BAYOLOJIA, ZINATIJA ZINAPOKUWA SEHEMU YA MAISHA YAKO (KUZIISHI).

  MUNGU AWABARIKI

 96. AMILTON hujui unachokisema, nitakuonyesha hatua kwa hatua kwa nini ninaujasiri wa kusema mnatudanganya kwa mafunuo ya uongo, uongo na ukweli ni sawa na giza na nuru haviwezi kaa pamoja, sasa niambie mnajiita mko kizazi cha nee unajua kuwa huo ni uongo mtupu, kuthibitisha hili soma Mathayo 1:17, halafu uniambie kizazi chenu cha nne kinatoka wapi.
  Utape huu umetengenezwa kwa umakini wa hali ya juu, ili uendane na neno toka kitabu cha Mwanzo15:16 wakati Mungu anamwahidi Abrahamu kwamba yeye atalala na Israel wataenda utumwani na kizazi cha nee kitarudi nchi ya ahadi. Soma pia Mwanzo 15:13, Kutoka 12:40 inaongea habari za miaka 430 ya wana wa Israel utamwani misri.
  Nipe maelezo ya kina kizazi cha leo kuwa cha nne kinauthibitisho gani wa neno kama sio utapeli wa kudanganya wakristo wachanga. TWENDE HOJA KWA HOJA TUTAFIKA TU.

 97. Bigups Kilimba simama ktk kweli usiogope vitisho vyao. Hakuna aliye juu ya Bwana Yesu.Yeye ni Alpha na Omega si nabii wala mtume. Bwana Yesu ndio jiwe kuu la pembeni. Huu si wakati wa kufichaficha wala kuogopaogopa ni muhimu watu waambiwe kweli ili iwaweke huru naamini wapo watakaochomoka huko kutokana na michango ya watu wa Mungu kupitia blogu hii.Hivyo roho hizo zitakuwa zimeokolewa na hukumu ya Mungu na jehanamu ya moto. Maana wapo ambao hawajui kitu na wanahitaji kusikia kweli lakini wamebanwa na kufungwa huko.

 98. NAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YENU WOTE MAANA NINAONA WAKATI AMBAO YESU ALIUTABIRI KWAMBA NI LAZIMA KILA MTU ATALISIKIA NENO SASA WAKATI HUO UMEFIKA. KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU WA ELIYA KWA AJILI YA WOTE WALIOKUWA WAMEPOFUSHWA NAFSI ZAO NA MAREHEMU SHETANI (DINI NA MADHEHEBU)ILI KWAMBA WASIZUKIWE NA NURU YA INJILI YA YESU(NENO) SASA LAZIMA WAIJUE KWELI YA YESU (NENO) KATIKA JINA LA YESU LILILOFUNULIWA! KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU WA ELIYA KWA KUTOA GAZETI LA KANISA SASA LINALOITWA NEEMA KUBWA! KWELI SASA KANISA TUKO JUU YA VYOTE, YOTE NA WOTE KWA UHALISI WAKE KUPITIA TOBA YA KWELI NA DAMU YA HAKI, KWELI NA HUKUMU. SHIKA NENO WANA WA MUNGU MLIOWEKWA JUU YA VYOTE WOTE NA YOTE!

 99. Mimi nadhani hujasoma maandiko ktk mistari niliyokuonyesha usome,ungesoma kwa umakini huku ukiongozwa na Roho Mtakatifu,ungeweza kuelewa vizuri,nakushauri soma halafu uje upya.na pia bwana Kilimba mbinguni hatufiki kwa majibizano haya,naamini Siku Moja Mungu atakupa ufahamu huu,na usipende kujibu kitu pasipo maandiko kwa uthibitisho.Na ukisema nimeleta maneno mbona hujatoa utetezi Wa kimaandiko kupinga hayo niliyosema?

 100. AMILTON Tukishindwa kuwaambia watu dhambi zao watatubu vipi. Ninachojua mkristo yeyote anatakiwa kuwa mfuasi wa Yesu na maelezo yake yote yawapeleke watu kwa Yesu na sio kwa mwanadamu. Yesu alimaliza yote pale msalabani na Roho Mtakatifu anatusaidia kuijua kweli yote. Mengine ya mtu kuwa na nguvu zaidi ya Yesu na Roho Mtakatifu tunawaachia wapiga debe maana yako nje ya neno.
  Watafuta pesa na waongo wapo kazini wewe husomi neno sasa utawezaje kulishika kama hulisomi.
  Mamlaka na ujasiri nilionao unatoka kwa Yesu aliyeniokoa.

  AMILTON leta hoja zenye mashiko na wala sio maneno maneno tumedhamiria kwenda mbinguni hivyo tutalinda mioyo yetu kuliko yote tuyalindayo.

 101. Jambo lingine bwana kilimba Mimi si mpiga debe,kama we we unampenda Mungu hutakiwi kutumia maneno kama haya hili naonge kwa upendo na mungu akupe hekima zaidi ya Suleiman 1fal 10:23. Luka2:52 na Luka11:52unachotakiwa nikuonyesha unanini ktk ufahamu Wa neno la Mungu,Unajua jambo linalohusu imani soma Ebrania 11:1-40 nisuala linalogusa moyo Wa mhusika na inpotokea unamhukumu masihi Wa bwana vibaya we nani amekupa kinywa na mamlaka ya kuhukumu,na kutumia majina kama muongo,mtafuta pesa,unamamlaka gani,maana hata neno LA Mungu linasema msiwaguse masihi Wa Bwana,na Mwenye mamlaka ya kuhukumu ni Mungu mwenyewe.soma hata yesu mafarisayo walimhukumu pasipokujua kuwa ni mwana Wa Mungu,soma Yohana 9:1-41.

 102. Nambariki Mungu mwenye rehema na upendo,Nikweli mnayozungumza hapa hatubishani lengo ni kuweza kukua kiimani,jambo moja ambalo kwa ufahamu nao jua nikwamba Mungu ktk kila kizazi alikuwa anatuma kiongozi Wa kuwaongoza watoto wake,ukiangalia,kunamtumishi kama Musa,Eliya,Yesu mwenyewe,lengo nikuwa na Kongozi,Mungu ametupa kibali cha kuwatii na kuwafuata wale wanaotuongoza,kwakuthibisha haya someni Mathayo 10:40-41,Ebr 6:12- na 2nyakati20:20

 103. Bwana Yesu asifiwe wapendwa
  “Hiki ni kipindi cha dhiki kuu,shetani alikufa 2008 sijui mwezi wa 11 na tarehe wanaijua,nabii eliya adamu wa pili mungu wa majeshi”

  Hapo juu nimenakiri baadhi ya maneno yao.Hivi haya mafundisho potofu wanayatoa wapi? halafu hawa watu wanaonekana kama wameleweshwa ni kama vile hawaeleweki na hasa cha zaidi ninachokiona wanampigia debe nabii wao ambaye wamemweka juu utadhani ni Mungu.Karibuni kwa BWANA YESU tokeni kwa nabii.

 104. Amen Kilimba,

  Majina ya dini, madhehebu na huduma zote zilizopo duniani hata sasa zote hazipo katika biblia na ‘Hakuna anayeweza kusema ipi ni sahihi’ LAKINI tunatambua uwepo ‘wa wafuasi wa Kristo (wa-Kristo) tu ambao wanatenda yale aliyoagizwa na YESU na hata yale waliotenda mitume wa kwanza katika Biblia (ambao tunauthibitisho kuwa walimpokea Roho Mtakatifu na hivyo walitenda kama YESU alivyoagiza. Hata ukijiita m-Pentekoste, m-Katoliki, m-efatha, m-TAG, mlutherani n.k halafu hutendi aliyoagiza YESU haitusaidii kitu. Ni sawa na mtu akuite malaika haitakufanya ugeuke kuwa malaika, litakuwa ni jina tu lisilo na uhalisia wowote ndani yako wala kukupa faida.

  Ebu angalia hiyo dini, dhehebu au huduma yako kama inatenda yaliyoagizwa na Yesu au kulingana na neno? ama mnafanya mapokeo na taratibu ambazo kinyume kabisa na maagizo au hazina msingi wa neno au kwa mazoea tu? THEN kaa chini uombe Mungu akuongoze katika kundi ambalo linahubiri injili halisi na misingi ya imani yao inatokana na neno, na ambao wanakaza mwendo kuutafuta utakatifu, kutenda yaliyoagizwa na MUNGU BABA kupitia YESU na kutafuta kufanana na YESU then tulia hapo.

  Yohana 17; 1-11
  Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
  Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

  Unakumbuka wafuasi wa mitume wa kwanza walipoanza kuvutana katika Biblia kisa mimi wa mtume huyu, mie wa yule???? Soma hii

  1 Wak 3;4-9,
  Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
  Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

  1 Wak 3;21-23,
  Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu;
  kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

  Ebu tuangalia akina Petro, Apolo, Paulo walivyoenenda, kuna mengine walifanya kwa tukio fulani sawa na Roho alivyoongoza, hata miujiza yao haikuwa ya maonyesho, au kujitafutia kufurahia anasa za dunia, au kushindana na watu BALI kwa utukufu wa Mungu.

  -Leo kuna kauli kali za watumishi kuwa ni wao tu wametumwa, ukihama huduma ‘UTAKUFA’ au ‘UTALAANIWA’ imagine Yesu alisalitiwa na Petro na Yuda. Hakuwatamkia maneno magumu bali tena akaja kumuombea Petro asimame tena na awasaidie wengine. Yuda kiburi kilimponza, naamini angeenda kwa Yesu kuomba msamaha angesamehewa na angeweza kuwa mtumishi mkubwa tu.

  -Stefano alipigwa mawe mpaka kufa, lakini hakulaani wala kuwaombea mabaya waliomuua na mwisho aliomba Mungu awasamehe (japo aliuawa kwa ajili ya kuitangaza kweli na watu hawakutaka kuipokea).

  -Paulo alipowahubiria watu wa ‘Beroye’ (kama sijakosea spellings), wakamuomba awape fursa wakayahakiki kama hawapotoshi, naye akawaruhusu kwa upendo, Imagine…..Upendo na uhuru wa watu kulinda roho zao (si udikteta na kutokuwa tayari kukosolewa).

  Wapendwa hakuna kificho tuna mifano hai tulioachiwa na Yesu na mitume wa kwanza jinsi ya kuenenda ipo wazi na inatosha, ebu tusijibebeshe mizigo inayotuchosha bila sababu. Hv kuna ugumu upi wa kufuata yale YESU aliyosema na kuanza kung’ang’ana na mapokeo ambayo hatuna uhakika nayo?

  ‘TUMEPEWA JINA LA YESU TU AMBALO PEKEE NDILO LITUPASALO KUOMBA KWA BABA YETU ALIYE MBINGUNI’ Tunautoa wapi ujasiri wa kuomba kupitia majina ya binadamu wengine waliokufa, walio hai, picha zao na kuwaabudu??

  Mdo 4; 10-12

  jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAPANA JINA JINGINE chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

  Mie binafsi hata kama kunakitu kiongozi wangu atasema na nikajikuta sina uhakika na nimeomba nakosa amani sifanyi sababu napaswa kuwa mkweli mbele za Mungu na si unafiki wa kuogopa binadamu wakati roho yangu inazorota. Makanisa mengi ya kiroho yanarudi kulekule ambako mwanadamu akisema watu lazima wafuate bila kujali kama linaendana na neno? Lina utukufu kwa Mungu ama?

  Tunatakiwa kulitetea jina la YESU na kweli ya injili isiyochakachuliwa, wala si kutetea sini, dhehebu, huduma au mtu fulani.

  Mbarikiwe zaidi, tukaze mwendo kutafuta kuijua kweli kila siku na kuitenda ili tuusogelee ukamilifu na kufanana na YESU.

  Dada Imani

 105. Shalom Shalom Shalom
  Namshukuru Mungu kuniruhusu kujifunza mengi zaidi kuhusu imani ya Pool of Siloam Church ambalo lilianza mwaka 2003. Imani hii sikuijua kabla lakini katika miaka mitano hivi iliyopita ndipo kilipoanza kizaaza cha kundi hili hata kwa makanisa mengine kila kanisa yalianza kulia uwiwii uwiii Siloam, Siloam..!!!
  Katika Mkoa ninaoishi mimi niliona washirika kadhaa wamechukuliwa na imani hii na kukawa na sintofahamu ya baadhi ya makanisa ya kipentekoste na mengineyo (Siyataji). kwani washirika (wanachama) wa makanisa walianza kuyakimbia makanisa yao haooo kwenda Siloam.

  Namkumbuka mchungaji mmoja wa imani hii alikuja kanisani kwetu kama mpendwa na kasali wetu kwa wiki kadhaa. Washirika wakamwelewa kama mpendwa Asifiwe ikatembea kama kawaida ya walokole, kumbe kaingia mtaalam mchambua habari za kiimani baada ya ibada anawafuata washirika na kuwapa vipande wa imani hii mpaka wakaondoka hata bila kuaga.
  Mimi mwandishi wa habari hii unayoisoma sasa jina ugomvi na Jina la Siloam kwa kuwa lipo ki-Biblia, nimegundua kuwa baadhi ya watu walioamini imani hii na wakaingizwa mafundisho haya sijui wanakuwaje nashidwa kueleza mwonekano wao wapo wapo tu!.

  Sijasahau mmoja kati ya waliokuwa waumini wa kanisa letu alipojitoa na kuyaingia mafundisho hayo akabadilika kabisa hata tabia. Akawa mkali wa hasira alipoulizwa kulikoni mwenzetu hakuwa anapenda ushauri zaidi ya hayo kila alichoambiwa kwa upole alikuwa na hasira mpaka mchungaji wa kanisa langu akamsihi yule bwana kwa upole aonyeshe japo heshima. Mimi nilimshangaa mtu yule ambaye alikuwa mpole anakuwa mkali na mwenye hasira kiasi cha kutokumtii hata mchungaji wake wa awali. Hee, nikajifunza kitu hapo.

  Kuna dada mmoja alikuwa katika kanisa letu, dada huyo alikuwa mwimbaji sana akiimba utapenda. Pasipo kuelewa kulitokea nini tukasikia amehamia hilo kanisa na baada ya muda akawa kichaa kabisa aliombewa, aliombewa, na kuombewa wapi! Sisi tuliojua umahiri wake katika uimbaji tukashikwa butwaa mpaka sasa hali yake haijatengemaa na mme wake hawako nae tena.
  Mfano mwingine mwanangu (binti yangu aliyenisaidia kufanya kazi za ndani kwa miaka kumi na minne kama binti wangu wa ndani) Binti huyu aliposwa na kijana wa kanisa letu ambaye baadaye alihamia imani hiyo. Baada ya harusi binti yangu huyo amefika kwangu mara moja tu hadi leo hajafika tena huu ni mwaka wanne hivi, inaonekana kama kazuiliwa na pengine huo ndio upendo wa “Shika Neno, Tenda Neno”

  Kuna kiongozi fulani nilimsalimia Bwana Yesu asifiwe akakataa akasema “Aaaa hapana “Shika Neno Tenda Neno” nikaduwaa hapo tena. Salaam za “Shika Neno Tenda Neno” ni nzuri sina kinyongo nayo kwa kuwa inamuasa mtu alishike Neno la Mungu na kukitendea kazi.

  Salam hii ya “Shika Neno Tenda Neno” inatofautiana na Bwana Yesu Asifiwe, Bwana Yesu ainuliwe, Bwana Yesu atukuzwe nk. kwa kuwa inamlenga moja kwa moja Mungu wetu kupitia Jina la Bwana Yesu kwa Kuinuliwa kwake, Kuheshimiwa kwake , Kutukuzwa kwake nk. Lakini Salaam ya “Shika Neno Tenda Neno” haina mahusiano ya kumtukuza au kumuinua Mungu wetu kwa kuwa mtu hawezi kumwambia Mungu “Shika Neno” Yeye akuambie “Tenda Neno”. Tunalishika Neno la Mungu sisi (wanadamu) na Tunalitenda Neno sisi (wanadamu) kwa nguvu za Mungu.

  Namshukuru Mungu kwa mwandishi mwanzilishi wa habari hii kwani ametupa mwanzo wa utafiti kuhusu imani hii. Bado nazidi kujiuliza maswali kadhaa kuhusu imani hii! Watu hawa wana tabia ya kuwatafuta washirika wa makanisa hasa ya kipentekoste na wakristo wengine na kuwaambia wazivunje madhabahu (mafunzisho ya awali ya wokovu wetu na kushikamanisha na madhabahu ya Siloam /Mungu wa nabii Eliya. Unavunjaje madhabahu za Roho Mtakatifu iliyowafanya watu wabadilike kabla? Ati waokoke na kujishikamanisha na madhabahu nyingine? Hivi Eliya na Yesu nani ni bosi wa mwingine? Kati yao ni nani anaabudiwa? Aaah Sijui…Nasikitika!!!

 106. AMILTON C wewe ni mpiga debe wa nabii hivyo huwezi toka nje ya box hilo, sina ushabiki wa dhehebu wala dini, sidhani kama nimewahi hata kusema ninaabudia wapi, HILO SIO LA MSINGI, ABUDU UTAKAPOABUDIA LAKINI UWE SAFARINI KWENDA MBINGUNI, NA SIO UTAPELIWE NA WATU WENYE TAMAA ZA KUTIMIZA MAMBO YAO KUTUMIA KIVULI CHA IMANI. Niliwahi kusema humu kuwa mnadanganya watu kuwa kwa nabii kuna wokovu wa kweli hili mmelipata wapi. Nijuacho mimi wokovu hupatikana kwa mtu kuamini na kumkiri Yesu basi na sio kuwa kwa nabii Rumi 10:9-10. Neno halijaweka condition kuwa lazima ukakiri ukiwa kwa nabii au kwa mtume. PIGA DEBE UKIJUA KUWA YESU NDIYE ATATOA UJIRA SIO NABII, MCHUNGAJI, ASKOFU AU MTUME.

  Dada Imani umesema iliyokweli. Imani ni tegemezi kwa mwanadamu haiendi popote, (NENO LINASEMA YESU NDIYE NJIA KWELI NA UZIMA LEO HII WATU WAMEWEKA IMANI KWA MITUME NA MANABII WALA SIO KWA YESU. UKIWASIKILIZA WAMEFIKA MAHALI PA KUWAABUDU JAPO KUWA HAWASEMI KINAGAUBAGA KUWA WANAWAABUDU.
  Imani inayosimama ni ile iliyowekwa kwa Yesu na kwa msaada wa roho mtakatifu pekee yake. Wapendwa imani ya kikristo imeingiliwa na hayo tulionywa mapema Mathayo 7:15, Mathayo 24:24, 1 Yohana 4:1. Yesu pekee yake ndio njia kweli na uzima. Sitaishi kwa kutegemea Mchungaji kasema nini, chochote asemacho nitakipima kwa neno la Mungu na ushuhuda wa roho mtakatifu ndani mwangu utasema.

  Sina sababu ya kupigia debe dhehebu maana halikuniokoa na haliwezi kuniokoa likiingiza ukengeufu naachana nalo, mbinguni hakuna sehemu ya dhehebu kuna sehemu ya wale waliotakaswa kwa damu ya mwana kondoo peke yake. Hakuna damu ya nabii wala msaada wa nabii utaingiza mtu mbinguni ni damu ya Yesu na msaada wa roho mtakatifu.

  Yesu alimtuma msaidizi alipokwenda kwa Baba Mbinguni, ndiye tunayemuhitaji baada ya kuokoka na sio nabii, nikiwa na roho wa Mungu nitajulishwa hata yajayo.
  Manabii wakati wa agano la kale walitabiri waliposhukiwa na roho, sasa leo hii roho mtakatifu amefanya makazi ndani mwetu, tunaingiaje kwenye huu udanganyifu kama sio wafuata mikate na samaki kama wakati wa Yesu?
  Tatizo la wakristo wa leo tunataka ready made, kizazi cha dot com every thing fast fast fast, hatutaki mchakato kujifunza kutembea na roho mtakatifu (KUJIFUNZA KWA NENO NA MATENDO) ndio maana tumekuwa tukikimbiza na miujiza tunayosikia kila kona na shetani kwa kujua hilo ameinua matapeli wanaokuja kwa jina Yesu (manabii wa uongo wengi zama hizi na bado wataendelea kutokea).

  KILA MTU ATAUCHUKUA MZIGO WAKE MWENYEWE, MAAMUZI UNAYOFANYA LEO YANAATHIRI HATIMA YAKO YA UMILELE, UVIVU WA KUMTAFUTA MUNGU NA KUJIFUNZA MANENO GHARAMA YAKE NI HIYO.

 107. Shalom wapendwa,

  Nafikiri kuna haja kubwa sana ya kuomba ‘Kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu’ tuijue na kuifuata kweli ili katika kila jambo tundende inavyopasa. Tusiishie kuwa watu tunaotumia akili, hisia, uelewa au ushawishi wa watu au wachungaji. Sababu YESU alituahidi ‘Roho Mtakatifu’ Yeye tu ndiye atakayetufundisha kweli yote, namna ya kutenda na kuenenda. Tutaipataje kweli kama hatuitafuti? Wapi tutaitafuta na namna gani tuitafute?

  Unajua hapa kuna makundi tofauti kulingana na upeo, kiwango cha kukua kiroho.
  -Kuna wengine bado wapo gizani
  -Wengine wapo katika mapambano ya kutoka gizani
  -Wengine wameshaingia nuruni.
  -Wengine hawajui walipo, au kama wapo sehemu sahihi

  Ndo maana mnaweza ku-‘argue’ kwa namna isiyoleta matunda na badala yake kufanya watu wajae hasira, chuki na ushindani ambao si mpango wa Mungu pia. Kuna wakati ni ngumu sana sawa kumwambia kipofu aamini kuwa gari linaliwapigia honi hapo pembeni lina rangi nyekundu. Kuna wakati ni ngumu pia kwa mwenye ufahamu kueleweka au asiye na ufahamu kupokea.

  Binafsi ninaamini kila mmoja wetu ana wajibu na haki kamili ya kujibidiisha kutafuta kuijua kweli na kuitenda ili kulinda usalama wa roho yake. Ni kweli tuna wachungaji na viongozi wetu makanisani LAKINI tusisahau kuwa nao ni binadamu na kondoo kama sisi nao wanahitaji kupata mwongozo toka kwa Mungu kila sekunde kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

  Sasa tujiulize usalama wetu na ‘conviction’ ya imani yetu inatokana na tuna ujasiri kwamba tumeijua kweli (personal encounter with JESUS) au ujasiri wetu ni wa kupitia yale wachungaji au viongozi wanasema.
  -JE ikitokea na Yeye (Mchungaji au kiongozi wako) amelegea, amebadili msimamo au ameacha kuutafuta uso wa Mungu na akaanza kutumia akili yake Je ‘Tuwe victims’ na tupotete pia sababu wao ndo macho yetu na dira yetu?
  -JE umejitosheleza kujua neno na uongozi wa Roho Mtakatifu kiasi cha kwamba hautayumbishwa?

  Yohana 14:16, 17.
  Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui. Bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu

  Yohana 14:26.
  Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia

  Yohana 16:7; 12 – 15.
  Lakini mimi nawaambia iliyo kweli – yawafaa ninyi mimi niondoke. Kwa maana, mimi nisipo-ondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. … Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote. Kwa maana, hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu, kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasheni habari

  Tito 2; 11-14
  Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.

  YESU hakutumia nguvu nyingi sana kuconvince watu, wala hakupoteza muda kubishana na watu LAKINI aliwaambia kweli bila kugwaya HALAFU akawaachia uhuru wa kuamua kutii au kuacha ILA alihakikisha anawapa FAIDA na HASARA ya maamuzi watakayoamua kufanya. Kuna watu wapo tayari kusikiliza maneno ya watu, viongozi wao KULIKO hata ya YESU mwenyewe, wanaamini maneno na taratibu fulani kuliko yale aliyotenda YESU.

  PAULO ni Mtume ambaye ni role modal mzuri sana, ambaye ninapenda sana vitabu vyake. Safari yake ya utumishi ilijaa changamoto sana haswa ilipokuja issue ya kudeal na watu wa aina zote na alijua nini cha kuwaambia na kufanya kwa wakati gani na kwa kundi lipi? Mtume PAULO alikuwa na kiu sana na kilio kikubwa watu waijue kweli, kuna wakati alikuwa mkali na alikaripia, kuna wakati aliwarejesha kwa upendo na kwa uvumilivu mkubwa.

  Kitu kingine kikubwa ambacho PAULO ananifurahisa kamwe hakusahau alipotoka, hakusahau YESU alivyomtoa uovuni. Hilo lilimpa kuwa na unyenyekevu, uvumilivu na upendo kwa wengine. Wapendwa kuna wakati huwa tunasahau tulipotoka, tunasahau watu walivyotuvumilia kabla hatujaijua kweli.

  Mbarikiwe wote, Roho Mtakatifu atusaidie kuijua, kuipokea na kuitendea kazi kweli.

  Dada Imani

 108. kilimba,kanisa hili halifundishi uongo wowote kwa sababu chochote kinachofundishwa kinatoka ktk maandiki matakatifu,kuonyesha kusudi LA mungu toka mwanzo,wapi tulikosea,wapi kusudia mungu Kwangu mimi na wewe liliibiwa.pia mafundisho ya unayofundiswa Leo si hayo utamayofundishwa kesho,kanisa linahama kituo kila siku,sasa lipokituo cha upendo,sikuombea wagonjwa kwakutumia watu wengine kama mnavyodhani.

  Mungu hataki porojo anataka kuona umemfanyia nn ktk ufalme wake?hv Leo him bwana kilimba ukaizwa umeleta faida gani ktk ufalme Wa mungu utasemje?soma Ezekia 38:1-,pia soma hesabu 23:23, yohana 15:16,yohana15:1,yoh 5:17utaona umuhimu Wa kuleta faida ktk ufalme Wa mungu na so mane no yasiyo na Neno LA Mungu

  Mungu alimpenda sana Daudi kwa sababu ya moyo wenyeshukrani na toba,kwahiyo kupitia hapo tunaona jinsi toba na shukrani vinatufanya Mimi nawewe kuwa huru,wengi mnajadili kwa kutumia Mawazo yenu,yaani akili za theologia na Mawazo ya kibinadamu,soma 1kor 2:6-10,jambo jingine ni juu ya dini na dhehebu ndo vinawaumiza wengi lakini naweza kukuonyesha Kazi ya dini na dhehebu ni IPI,soma matendo 5:17- lakini ukiweza anzia 1 nakuendelea utapatakitu hapo.

 109. AMILTON C ASANTE KWA KUYAONA HAYO ” NIKAKUTA TOFAUTI NAYAYISEMWA HUMU NI BAADHI TU NDO KWELI” SASA HAYO BAADHI NDIO UDANGANYIFU NA MTEGO WENYEWE TUNAOUSEMA. HATA SHETANI ALIMJARIBU YESU KUTUMIA NENO LILILOPINDISHWA KWA KUWEKWA MRENGO WA KUMJARIBU MUNGU, KUWA TEGEMEZI KWA VITU, LAKINI HAYO YOTE YAMEANDIKWA.

 110. NAMBARIKI MUNGU KWA UZIMA JAMANI UKISOMA YOHANA 9:1-11,UTAPATA NINI MAANA YA SILOAMU,LAKINI TUACHE KUZUNGUMZA KWA KUSIKIA UNAWEZA KUJAJI KITU VIBAYA KUMBE NDIYO MUNGU MWENYEWE AMECHAGUA,CHANSINGI NENDA KASIKILIZE UPATE KUONA MWENYEWE UONE HAYO YANAYOSEMWA,HAKUNA KANISA ZURI KAMA SILOAMU KWA MTU ANAYE JIFUNZA NENO LA NUNGU MIMI NIMEENDA NIKAKUTA TOFAUTI NAYAYISEMWA HUMU NI BAADHI TU NDO KWELI

 111. Wamefungwa fahamu zao, kwa ukiri wa midomo yao wenyewe, kwa maagano waliyoweka bila ya wao kufahamu. Hizo roho potofu zinawatawala kwa uhalali walioutoa wao wenyewe kwa ukiri wa midomo yao kupitia maagano waliyoweka. Shetani ni baba wa uongo na ukicheza tu umeliwa, iweje leo watu wanaingizwa kwenye maagano na huyo nabii wao wala sio maagano na Yesu aliyewakomboa. Huu ni utapeli wa kiwango cha juu sana ambao unazipa roho za udanganyifu nafasi ya kukutawala kwa ukiri wako mwenyewe. Wanamiungu mingine na ndio maana wako tayari kupingana na neno la Mungu wakati wakijinadi kwa slogani ya shika neno tenda neno.

  Tuwaombee kwa Mungu yeye bado anaweza kuwafungua toka kwenye hilo kongwa na udanganyifu.

 112. SHIKA NENO WANA WA MUNGU MLIOPEWA NEEMA KUBWA YA KIZAZI CHA 4! TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUVUSHA MWEZI ZIVU NA KUTUINGIZA MWEZI SIWANI AMBO UMEBEBA UNABII WA USHINDI MKUBWA WA KANISA JUU YA VYOTE, WOTE NA YOTE KWA KANISA KATKA JINA LA YESU. TUNAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA NABII ELIYA MAHALI AMBAPO AMELIFIKISHA KANISA KUWA JUU YA VYOTE, WOTE NA WOTE.

 113. “SHIKA NENO WANA WA MUNGU MLIOPEWA NEEMA KUBWA YA NABII ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI”

  Ndugu Vai unamaanisha nini hii sentensi yako?nani Mungu wa majeshi? una maana kiongozi wako wa dini amekuwa Mungu wa majeshi? au unamaanisha nini?Inaonekana wazi kuwa huyu kiongozi wenu anawachanganya akili kwelikweli, hivi mwanadamu anaweza kuwa Mungu wa majeshi?Hii umeitoa wapi? Ndugu yangu kwa mtindo huu mtaanza kumwabudu na kumsujudia mwanadamu ambaye naye ni kiumbe tu aliyeumbwa na Mungu. Hii inasikitisha sana kuona kuwa mnaiacha kweli na kudakia imani zingine za mitume na manabii, kweli hamuitaki mnataka kusikia tu mafundisho yasiyo ya kibiblia yanayopambwa na uongo wa mashetani.Eti shetani Alishakufa siku nyingi! biblia ipi imeandika hili? Shetani ni baba wa uongo wengine anawaambia kuwa yeye ni Mungu hivyo kuna shetani mwingine na wengine anawaambia kuwa yeye alishakufa siku nyingi. Ooh Bwana Yesu tusaidie.Sisi je tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii? Eti “mliopewa neema kubwa ya nabii eliya adamu wa pili”! du hii nayo sijui umeitoa wapi?! Neema inatoka kwa binadamu aliyezaliwa kwa mbegu iharibikayo?Bwana Yesu amekaribia sana kurudi, time is fast running out/Le temps court très vite!

 114. Matayo 7:15-20
  15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma?17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”

  2Timotheo 4:3-4.
  Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe, watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wanamasikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za Uongo”

  MIUJIZA YOTE SHETANI ANAWEZA KUIGIZA LAKINI SIO KUBADILI MAISHA YAMFANANIE YESU, HAPO NDIPO CHANGAMOTO ILIPO “mtawatambua kwa matunda yao.”.

 115. SHIKA NENO WANA WA MUNGU MLIOPEWA NEEMA KUBWA YA NABII ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI. KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KULIPAKA KANISA MAFUTA YA KUWA JUU YA VYOTE, YOTE NA WOTE KUPITIA NENO LAKE LILILOFUNULIWA KIZAZI CHA 4. SASA NENO LA ZAB 8:6 LIMETIMIA KWA KANISA/ WANA WA MUNGU KTK JINA LAYESU. HONGERENI KWA SIKU YA 4 YENYE UNABII WA MAJIRA NA NYAKATI ILIYOFUNULIWA KWA AJILI YA KANISA. TUNAMSHUKURU KWA AJILI YA MWEZI ZIVU AMBAO UMEENDELEA KUTUWEKA JUU ZAIDI. ABARIKIWE NA BWANA ELIYA NABII KWA KUKUBALI KULIBEBEBA AGIZO LA MUNGU LA KULIJENGA KANISA LINALOMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI

 116. Mareto, sisi tu nani tupingane na neno la Mungu. Yesu hatakuja kuwaambia watu kweli kwa mara ya pili ametuacha sisi. Tunaweza chagua ustarabu wa kidunia (civilization) ambao sehemu nyingine dunia yetu hiihii ukimwambia mtu uzinzi dhambi atakupeleka barazani wewe ni mbaguzi. Timotheo aliagizwa na mkufunzi wake Paul kukemea dhambi sijui hakuwa na hekima. Jamani utapeli umeingia kanisani lazima tuambizane ukweli au la tutadaiwa kwa kutowaambia.

 117. shaloom watumishi mungu awabariki kwa kutafakari na alau kusema mawili matatu juu ya mungu palipo na wawili watu mungu yu pamoja nao,
  mimi napenda tu tuondoe tofauti za kiimani tulizonazo kwani hapa naona watu wanakinzana sana lkn lengo ni moja kuujenga mwili wa kristo so mimi naomba sana tuelekezane wapi umepitia na changamoto ulikutana nazo kama mdau tunkut nimependa ufafaunuzi wake sana ni mzuri,tuache ubishi madhehebu yote misisngi ilikuwa mizuri kwa makusudio ya kuwaleta watu kwa mungu lkn mpaka sasa wameacha njia na kuangalia kwingine kama hao the pool so tuache ubishi wote tumepotoka neeema ya mungu nitusaidie ili tuufikie mwish mzuri

 118. Bezaleli kasome Mathayo 1:17, utaona kuwa hiki sio kizazi cha nee kama mnavyotapeliwa, neno liko wazi vizazi vingi vilipita kabla hata ya kuja kwa Yesu Mwokozi, sasa hiki cha nne chenu ni kutoka injili mpya au ni elimu ya mashetani. Usituzuge kwa mafunuo niliwahi toa ushauri humu ndani mafunuo yoyote yasipokubaliana na neno hiyo ni elimu ya mashetani.

  Mnatubu kwa vizazi vyote, iliiweje ilihali neno linasema mwana hata uchukua uovu wa baba yake na roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa, haya hiyo injili yenu mwaitoa wapi?
  Bezaleli endelea kuisubiri jehamu wakati unatiwa moyo kwa uongo usiokuwa hata na ushahidi wa neno la Mungu, na ndio maana kukudanganya wewe na wenzio mliodanganyika mkaghilibiwa kwa slogani SHIKA NENO, TENDA NENO, ni roho mtakatifu peke yake ndiye anayeweza kukusaidia ukalitenda neno nje ya hapo hamna nabii au mtume anayeweza kukufanya iliishi neno la Mungu.

  Tafuta kuijua kweli inayokubaliana na neno la Mungu acha ubishi unaelekea kubaya.

 119. Bezaleli DC,
  Mwana wa kizazi cha Nne, chini ya uongozi wa Adamu wa Pili, Mungu wa Majeshi, Nabii Elia; kumbe upo kaka!!!!!

  Majira yanasemaje???

  Kwa kweli nilidhani umefanikiwa kuchomoka, lakini naona the tomb is sealed!!!

 120. MWISHO WA SIKU….WAPO WENGI WANAMPOKEA YESU KUPITIA WOKOVU WA KWELI ,SI KUPITIA ULOKOLE….MAANA KIZAZI HIKI CHA NNE MUNGU ANAANGALIA KAZI….ONYESHA KAZI ZAKO ULIZOFANYA TANGU UPATE ULOKOLE WAKO…. NA KANISA LITAKUONYESHA KAZI ZILIZOFANYIKA TANGU HUDUMA YA NENO LILILOFUNULIWA KIZAZI CHA NNE ILIPOFUNULIWA KUPITIA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU…..

  UPENDO UNATANGULIA NDIYO KANUNI….KATIKA KIZAZI HIKI CHA NNE MASHINDANO YAMEFUTWA….NA KILA KITU KINAELEA KWENYE TOBA YA KWELI VIZAZI VYOTE VINNE… MAANA KERUBI HAKUTUBU, ADAMU HAKUTUBU, KIZAZI CHA PILI NA CHA TATU HAWAKUTUBU… NDIYO MAANA YOHANA NA YESU WOTE WALIHUBIRI ”TUBUNI UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA”

  KIZAZI CHA NNE TUNATUBU KWA VIZAZI VYOTE VINNE…

  NDIYO MAANA MUNGU ANASEMA ”MUWAREJESHE KWA UPENDO” , HATA MTU NA MWANADAMU ANAPOHAMAKI AU KUKEJELI AU KUDHARAU , TOBA YUPO KAZINI….MWISHO WA YOTE KILA NAFSI ITAMJUA MUNGU WA ELIYA…

  ”MAANA NI NINI KITATUTENGA NA UPENDO WA MUNGU???
  JE NI UCHI? AU DINI, AU DHEHEBU, AU KABILA? AU ELIMU???

  NAKWAMBIA HAKIKA HATA UKIKIMBIA UKIFIKA KWENYE KONA UTAMKUTA UPENDO WA MUNGU ANAKUSUBIRI…HATA UKIWA MBISHI MPAKA UZEENI HAPO UZEENI UTAMKUTA UPENDO WA MUNGU ANAKUSUBIRI….HATA UKIJIFICHA KWENYE DINI YAKO NA DHEHEBU LAKO….HUMOHUMO UTAMKUTA UPENDO WA MUNGU ATAKU NYOFOA….MMOJA MMOJA….KWA WAKATI WAKE….

 121. Kilimba endelea kugonga injili watu wapone wacpotaka basi tena coz wewe kazi utakuwa umeifanya.Ujuwe sumu ni mbaya!yaani watu wamenyweshwa sumu na ipo kazi kuzimaliza.Bt am sure one day watafunguliwa macho na kuijua kweli.

 122. Karamu hakuna toba ya kweli wala nini bali nyie mmetekwa ufahamu na huyo nabii wa uongo anaejifanya kuja kama malaika wa nuru. Hana lolote, wala hana Mungu muumba wa mbingu na nchi ila anamiungu migeni na huenda ni ya kinaigeria ndo maana mmeiga na mavazi yao, eti vazi jeupe. Toba ya kweli iko wazi Warumi 10:9-11. Mtafuteni roho mtakatifu sio nabii huyo ana ajenda yake na miungu yake migeni, hana nia ya kueneza ufalme wa Mungu muumbaji.

  Mtalumbana saana, msaidieni mwenzenu apete maisha ya hapa duniani wakati nyie mkiishi kwa matumaini, lakini jehanamu mtakuwa na mujahidina kama hamta rudi kwenye kweli maana hapo mlipo hamna tofauti nao.

 123. Toba ya kweli inafuta dhambi na damu ya haki kweli na hukumu ina kusafisha na kukuweka huru

 124. mmwambieni aache uongo, kazi zake haziendi kama Yesu alivotuagiza, akajifunze neno la Mungu upya, wajua dhambi (roho wa mafundisho yaendayo kinyume na Neno la Mungu) ndiyo inayomsumbua, hajaleta habari za Yesu Kristo bali habari zake yeye mwenyewe, na chakushangaza bado watu wanaskiza mafundisho yake na kuyaamin

 125. VAI umejificha kunieleze udongo wa viwanja na mashamba mnaufanyia nini kanisani. Ninajua upeo wako kwenye imani hii ni mdogo saana ila unafuata mkumbo tu kama walivyo wengi, sasa utakwenda jehanam kwa ujinga wa kuikataa kweli, sisi tunanawa kwa kukueleza iliyo kweli uamuzi ni wako.

  Kama ni mafunuo, ushauri wa bure mafunuo yeyote yasiyoendana na neno la Mungu ni mafunuo ya mashetani hayo yakimbie la sivyo yatakuwa ticket yako ya jehanamu.

 126. Kuzaa sio dhambi soma context ya sentensi, Byera. Uzani Mungu alishatupa kanuni Byera, mke mmoja. Sasa ukizaa na kila mshirika wako dhambi ya uzinzi unaweka wapi> Ukiwekwa kwenye maono basi mmekwisha maana maono ya wenzetu hayapimwi kwa neno la Mungu as long as Nabii kasema.

 127. EVA yatosha ndugu, leo nikuulize swali moja tu

  HIVI UDONGO WA KWENYE VIWANJA NA MASHAMBA YA WATU UNAOPELEKWA KANISANI MNAUFANYIA NINI KANISANI KAMA SIO KUUFANYIA MAZINDIKO, TOFAUTI YENU NA WAGANGA WA KIENYEJI IKO WAPI, NI WAPI YESU ALITUFUNDISHA KUFANYA HAYO.

  Eva Nabii Elia Msangi alizaa na wake za watu, akazaa na mama na mtoto wake, lakini mpaka leo hii kunawafuasi wake bado wanaamini alitumwa na Mungu, hivyo sishangai saana KUKUONA UMENG’ANG’ANA umefungwa.

  UTAYAKUMBUKA HAYA UKIWA JEHANAMU KAMA HUTAGEUKA NA KUFUATA KWELI.

 128. NAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YAKO KILIMBA KWAKUWA YEYE ANAKUWAZIA MEMA SIKU ZOTE! UKIMWAMINI MUNGU UNADHIBITIKA LAKINI UKIWAAMINI MANABII WAKE UTAFANIKIWA (2nyakti 20:20). Unapaswa kufahamu kuwa NABII WA KWELI ni KITI CHA MUNGU, na Mungu hafanyi kitu bila kupitia Nabii. ukitaka kuamini hili angalia wana wa Israeli ili waweze kutoka utumwani Misri Mungu alibidi amtafute Nabii (Musa) ili awatoe utumwani. Sisi Kanisa tunamshukuru Mungu kwa kutupa NABII WA KWELI ALIYEPEWA AGIZO LA KUJENGA KANISA LINALOMUABUDU MUNGU KTK ROHO NA KWELI na ametutoa kwenye utumwa wa dini na madhehebu/ulokole, mila, desturi, sheria ya dhambi,matendo ya mwili, ametutoa kwenye utumwa wa majira na nyakati za Jumatatu-Jumapili, Januari – Decemba. KWAKWELI KANISA BADO TUNAENDELEA KUMSHUKURU MUNGU WA ELIYA KWA KULIKUMBUKA KANISA LAKE NA KWAKUWA SASA MUNGU AMELITOFAUTISHA KANISA NA DINI NA MADHEHEBU NDIO MAANA WALIOKO KWENYE DINI NA MADHEHEBU/ULOKOLE HAWAELEWI

 129. Mtumishi Lwembe ni kweli nimwambia vai aendelee na msimo wake kwani siloam ni dhahiri ni mlango uliowazi kwenda kuzimu, na ukweli tumemwambia na nafsi yake inamshuduhudia hivyo lakini ameng’ang’ana tu. WAPENDWA KWA HILI SINA UKAKASI NA WANA KUTAFUNA MANENO VAI NA WAFUASI WENZAKE WAMEPOTEA NJIA WANAYOPITA NI YA UPOTEVUNI. MTU KAWAFANYA SHAMBA NA KUWAPUMBAZA ETI WAO SIO WATU NA WANADAM, WANAMFANYA MUNGU MWONGO ALIYESEMA NATUFANYE MTU KWA MFANO WETU. SASA HUO NABII AGIZO ALILIPATA WAPI KAMA ANAMPINGANA NA NENO LA MUNGU MUUMBAJI. HILO AGIZO ANALOLINADI KILA SIKU AMEPEWA NA NANI SASA? NISAIDIENI KUELEWSHWA HAPA MAANA SIJAWAHI KUONA BALOZI ANAYEPINGANA NA MAMBO YA NCHI ANAYOIWAKILISHA NA BADO ABAKI KUWA BALOZI.

 130. Kilimba,

  Unamwambia Vai, “Endeleza msimamo ndugu maana pia hilo ni kutimiliza maandiko”, hili ndilo jambo linalonishangaza kuliko hata kuihubiri Injili, kule kutimiliwa na Maandiko mchana kweupe, tena watu wakiyang’ang’aniza yawatimilie, yaani wakijipofua macho yao ya kiroho kwa makusudi ili wakatumbukie kwenye lile shimo reeeeeeeeeeeeee……fu, lisilo na mwisho!

  Hebu iangalie kufuru hii waliyoaminishwa na kujazwa ndani ya mioyo yao, hivyo kutiririshwa bila kikomo ili kuhakikisha kwamba hawapati nafasi ya kuyatubia hayo waliyoingizwa:
  “”NABII wa kweli ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI””
  Basi utasemaje kuhusu kauli kama hii, ni CULTISH by all measures!

  Kuhusu hao, huko kuwatimilia Maandiko, ndio hawa hapa, 2Tim 3:6-9:
  “Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani. Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.”

  Unaona, ni roho zilizowateka na kuwafungia ktk ngome, by their own volition!!!

  The Gospel is for the savable, if they are not ordained, they will trample it!

  Gbu!!!

 131. VAI nimesema iliyokweli na ndio maana huna cha kukanusha. NAOMBA MTAFUTE YESU NA SIO NABII NABII HAWEZI BADILI MAISHA YAKO ILA YESU ANAWEZA. WALIKUWEPO MANABII WENGI TU NA WENGINE WALIJIITA ELIA MFANO ELIA MSANGI. ALIFANYA MIUJIZA NA ISHARA PIA LAKINI MWISHO WAKE NI AIBU UKISIKIA. LAKINI PAMOJA NA HAYO YOTE KUNAMFUASI WAKE ANASEMA MPAKA LEO ANGEFUFUKA ANGEMKUMBATIA. HIVYO SIONI AJABU KWA WEWE KUENDELEZA MSIMAMO JAPO UKWELI NAAMINI UNAUJUA KWA SEHEMU.

  Fanya utafiti maisha yenu kwa nini yanakwenda opposite na maisha ya Yesu. Mnaweza kujikweza tu lakini maisha halisi ya kikristo hamna. Hii ni dalili tosha kuwa MNA NABII LAKINI HAMNA YESU.
  Endeleza msimamo ndugu maana pia hilo ni kutimiliza maandiko.

 132. Kilimba wewe wasema!
  Namshukuru Mungu kuwa huu sio wakati wa kubishana kwa maneno bali ni wakati wa kujifunza NENO na KULISHIKA NENO na KULITENDA!
  Neno linasema wazi kabisa kuwa Kumjua mtakatifu ni UFAHAMU! Kwa hiyo kama huna ufahamu wa Neno huwezi kumjua MTAKATIFU. Hata wanafunzi wa Yesu walitembea na Yesu miaka 3 mfululizo lakini Yesu alipowauliza kuwa wao wanamfahamu yeye kama nani walishindwa wote kumjibu isipokuwa Petro peke yake ambaye alifunuliwa sio kwa damu na nyama bali alifunuliwa na Mungu mwenyewe (Math 16). Na sisi wana wa Mungu wa kizazi cha 4 tumepata NEEMA kubwa ya kufunuliwa na Mungu mwenyewe kumfahamu NABII wa kweli ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI aliyepewa AGIZO la kweli na MUNGU mwenyewe. Hivyo ni mpaka ufunuliwe ndipo utaweza kufahamu mambo makubwa ya kizazi cha 4! Namshukuru Mungu wa Eliya kwa kuifunua TOBA YA KWELI AMBAYO IPO KAZINI IKIENDELEA KUFUTA UOVU, UASI NA DHAMBI KATIKA JINA LA YESU. SHIKA NENO!

 133. HUNA JIPYA VAI, MNARUDIARUA TU YALE YALE. TUMIENI UWEZO ALIOWAPA MUNGU NA ROHO MTAKATIFU NJE YA HAPO MTAISHIA KUWA KAMA BINTI WA HERODIA MARKO 6:22-27. VAI UNAMUHITAJI ROHO MTAKATIFU YOHANA 16:12-14 NA WALA SIO MANABII WANAJITUKUZA NA KUTAFUTA KUTUKUZWA MATHAYO 24:4-5; MATHAYO 24:23-25.. SOMA PIA YOHANA 14:26. WAKATI WA KUDANGANYIKA UMEPITA. SLOGANI TUMEZIPOKEA KWA WANASIASA YESU HAKUWA NA SLOGANI NA NDIO MAANA MNASEMA KILA WAKATI TENDA NENO NA BADO HAMLITENDI NENO LOTE BALI MNACHAGUA BAADHI ILIKUJINADI (hata waduni waliostaarabika wanafanya hayo tofauti yenu iko wapi sasa) MMEDANGANYWA NA WEWE NI SHAHIDI WA NAFSI YAKO. HATUTAFURAHI KUONA WATU WAKIENDA JEHANAMU KWA KUDANGANYWA NDIO MAANA TUNAWAAMBIA TUSIPOFANYA HIVYO TUTAKUWA NA HATIA MBELE ZA BWANA (TUTADAIWA NA BWANA).

  Macho ya mioyo yenu yafunguliwe.

 134. HERI YA SIKU YA 3! SIKU YA THAMANI, FAIDA NA UBORA (Mwanzo 1: 9-13)KANISA TUNAMSHUKURU MUNGU WA ELIYA, MUNGU WA KWELI KIZAZI CHA NNE KWAKUWA AMETUTOFAUTISHA KABISA NA DINI NA MADHEHEBU. NDIYO MAANA HAWATUELEWI YALE TUNAYOWAAMBIA. WANATUONA WANA WA MUNGU KAMA TUMEPOTEA AU KUCHANGANYIKIWA. NI SAWA KABISA KWAKUWA VILE AONAVYO MTU NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO YEYE. MUENDELEE KUONA HIVYOHIVYO KWAMBA TUMEPOTEA LAKINI SISI TUNASONGA MBELE DAIMA KATIKA JINA LA YESU! WANA WA MUNGU TUKO JUU KWAHIYO HATUOGOPI KWAKUWA TUNAYE NABII WA KWELI ALIYEPEWA NENO LA KWELI NA MUNGU NA UFUNUO WA KWELI. SIKU ZOTE MTI ULIO NA MATUNDA NDIO HUWA UNARUSHIWA MAWE. SILOAM TUNA MATUNDA YANAYOONEKANA WAZIWAZI NDIYO MAANA WANATUTUPIA MAWE LAKINI HAYO MAWE HAYATATUPATA WANA WA MUNGU KWAKUWA TUMESIMAMISHWA JUU YA MSINGI WA TOBA YA KWELI KUPITIA DAMU YA HAKI KWELI NA HUKUMU. KANISA TUNAENDELEA KUOMBA TOBA KWA AJILI YA WOTE WANAOLIPINGA KANISA MUNGU ATUSAMEHE KWA AJILI YAO.

  MBARIKIWE NA BWANA YESU WANA WA MUNGU

 135. Msoma huwezi kuwa na nafsi hai ya Mungu na maisha yako yakapinda, mmejazwa uongo ili mkiambiwa ukweli muone mnapingwa, hatuna sababu yeyote kwani dini ni siloam peke yake. Hamna majira mapya ila ni udanganyifu tu mkienda benk, kazi na nyaraka zote bado mnatumia kalenda hiyo inayojifanya kuipinga. KAMA NI WA KWELI BASI TUMIE HIZO KALENDA ZENU MBONA MNAKUWA KAMA VIVYONGA, MNATAKA VYOTE. leo hii nilikuwa namsaidia mdada wa siloam lkuandika barua ya kazini katumia tarehe ya leo na mwezi huu wa kumi na kataja aliajiriwa tarehe 31 January. Nyie si mnasiku 28 hiyo ya 31 anaipata wapi kwenye majira zenu?

  Msoma unasema “dini na madhehebu ni mapenzi ya watu na wanadam” na kwa taarifa yako Munuo kasajili dini ya kikristo na dhehebu la siloam serikalini. Iweje leo mnajifanya kuponda dini na madhehebu, hamna lolote nyie waongo wakubwa msio na haya. Shida mmefungwa kuhoji kila mnalosikia, hivyo mnalibeba kama lilivyo. Kuweni kama watu wa Beroya hata waliposikia ujumbe wa watumishi wa Mungu waliyachunguza maandiko kujua kama kweli walichohubiriwa ndio neno la Mungu nje ya hapo hamuwezi kukwepa kula matango mwitu.

 136. shika neno mliopewa neema kubwa; nawauliza nyie mnaopinga siloam majira mnazo tembea nazo au kuamini ni za mungu au ni mtu na mwanadamu kaziweka.sisi tuna majira ya Mungu mwenyewe miezi ya kiungu na siku za kiungu tunaishi katka siku 7 za kiungu na zimebeba unabii wake na miez pia ambayo nikuanzia ABIBU-ADARI na inaptikana katka kitabu cha NENO ambacho ni kitabu cha HAKI KWELI NA HUKUMU nyie mnaita biblia kwa hiyo msiendelee kuburuzwa hamjui wap mnaenda. dini na madhehebu ni mapenz ya watu na wanadam bali KANISA NI MUNGU MWENYEWE .na mniishi hamna nafsi hai ya MUNGU ndo maana mnatupinga SILOAM tuna nafsi hai yaMUNGU

 137. Usharika mtakatifu SG,

  Nawasalimu kwa jina la Bwana Yesu

  Namtukuza Mungu, Baba wa Bwana yetu Yesu Kristo kwa mibaraka ya rohoni aliyotubariki ktk ulimwengu wa roho ndani yake Kristo.

  Tukiendelea kudumu ktk neema hii ya Mungu,maana ndani yake yeye tunaishi tunakwenda tukiwa na h uhai wetu.

  Mtu wa Mungu hebu tafakari nami habari hii niliyoileta……….
  Wakristo wa mwilini ni mfano halisi wa kanisa la koritho ugiriki la wakati wa mtume Paulo.
  Wakristo wa mwilini uvutiwa na ujuzi kwa kuwa wana masikio ya utafiti wanataka kuona/kusikia/kuambiwa ambavyo vitawasisimua mwili,

  Mara nyingi kama si zote utawakuta wakati wakusifu au mhubiri anapohutubu na anapowatabiria wanaruka na kucheza kwa msisimko lakini wakitoka nje ya kusanyiko lile urejea huzuni yao kwanza,
  Furaha yao ni ya bandia,hawana furaha ya kweli ya Roho Mtakatifu

  Wakristo wa mwilini wao hawana habari na safari kwamba sisi tu wageni na wapitaji hapa duniani,
  Mkristo wa mwilini anataka kusikia na kuona miujiza na kufunuliwa neno tu,pasipo hayo hapo hakuna uwepo,anatafuta kanisa la ufunuo, na kutabiriiwa.

  Ujivuna mno kwa vipawa na mafunuo upelekea kuwatukuza au kuabudu watumishi wao.
  Wayunani walivutiwa sana na ujuzi,mimi wa Apolo/Paulo!!kwa sababu walikuwa wakristo wa mwilini wakienenda kama watu wa asili.

  Kipawa ni kitu chema lakini tunaona ktk maandiko watumishi wote waliokuwa na vipawa walikuwa na Tunda la Roho samabamba kama Bwana Yesu,(mf…Mdo6:3,16:24)

  Vipawa vya udhirihisho wa Roho (viko:9) na Tunda la Roho(matunda:9)lazima viende sawia.maana tunatambulika kwa matunda mchongoma hauwezi zaa zabibu,

  Vipawa havituingizi Mbinguni wapendwa tusipokuwa naTunda Roho(Gal5:22-23)
  Bwana hatutambui kwa sababu hatuenendi ktk Roho kama tusipo kuwa na Tunda(siku ile atasema tokeni kwangu sikuwajua tangu mwanzo)usisahau hata kidogo kuwa watu wa mwilini nao wanafanya miujiza kwa jina la Yesu

  Bwana Yesu anasema hilo tawi lisilo zaa ukatwa,utupwa na kuchomwa moto hata kama ulikuwa ni mjuzi wa maandiko sijui na neno lililofunuliwa.(Mt7:17-22,Yak1:22-25,2:14,11,17,24,26)shimo la moto.

  Wenye kujali vipawa peke yake mara nyingi ni watumwa binadamu(watumishi)

  Mtume Paulo anawaandikia wakoritho….
  “Je, wewe ulikuwa mtumwa wakati ulipoitwa? Sawa, usijali; lakini ukipata fursa ya kuwa huru, itumie.
  Maana yeye aliyeitwa na Bwana akiwa mtumwa huyo huwa mtu huru wa Bwana.
  Hali kadhalika naye aliyeitwa akiwa mtu huru, huwa mtumwa wa Kristo.”1Cor7:21-22,Exodus21:1-6(SNT)

  Tutafakari hizi elimu na mafundisho potofu uturejesha na kutufanya kuwa watumwa si wa shetani bali binadamu.
  Pamoja na kwamba tumekombolewa kutoka utumwa wa dhambi kwa kutakaswa kwa damu kama ya kondoo asiye na hila(Kristo),
  Wapendwa wengi baada ya kumpokea Bwana wameangukia ktk utumwa Hatupaswi kuwa watumwa wa mtu kama israel wakati wa siku za sheria “Kut21:6”ukipata fursa ya kuwa huru itumie.usikubali kutobolewa sikio malangoni mbele za Bwana,MWANA ametuweka huru…tu huru kweli.

  “Nyote mmenunuliwa kwa bei(thamani); kwa hiyo msiwe tena watumwa wa watu(binadamu)”.1Cor7:23(SNT),msisitizo ni wangu

  Maana kuwa mtumwa wa shetani ni kitu kingine na kuwa mtumwa wa binadamu nacho ni kitu kingine,Binadamu anakufungia nje kwa mafunuo/mafundisho ili usilijue neno la kweli umwonee yeye shauku,Yeye anakuwa Nabii/mtabiri wa maisha yako na hata ufikia kujifanya kuwa Roho (Mungu)kukutishia maisha.

  Niliwahi kuhudhuria ibada sehemu moja nikamsikia mtumishi anamwambia mpendwa mbele ya hadhara ya kusanyiko kuwa atakufa kwa sababu aliondoka bila kuaga kwenda kusanyiko lingine na sasa amerudi pale na yeye hamtaki..nikasema mbombo jilipo

  Wapendwa tunaye Roho wa Kristo,Hatuko na roho wa utumwa

  Barikiwa mtumwa wa Kristo,

  Mjoli Haule

 138. Ndugu livinus likweti hatukimbizwi na miujiza kumwamini nabii kwani hata shetani anaweza kutenda miujiza. Tunapima kwa kipimo cha neno la Mungu inakuwa je maisha yenu yanakwenda kinyume cha neno la Mungu. Mnashika neno na maisha yenu yanakwenda kinyume na neno la Mungu ilikupumbaza watu mmeweka slogani ya kutenda neno. Mtenda neno hahitaji kujitangaza maisha yake yatafanana na neno na ndio maana Paulo anatuita sisi ni barua, maisha yetu yanasomeka kabla hata hujaanza kujinadi kama bidhaa.
  Kutokuona kwa utendaji wa Mungu kwako hapo awali kulitokana na maisha yako machafu na pia hukuwa na imani mbona hili liko wazi.
  Tatu mafanikio (nyumba, magari) sio kipimo cha kuwa na Mungu, mbona waduniani ndio wanamafanikio ya kutisha, Baharesa ana Mungu, huo ni uchanga wa kuchambua utendaji wa Mungu, kwwni wote waliojenga na kununua magari wana Mungu.
  Pili wewe sio wa kwanza kutamkiwa kuwa hutafanikiwa, kuna watu walitamkiwa mashuleni/sekondari kuwa walikuja shule wakiwa na uwezo wa kupata division one lakini kwa kuwa walijifanya kuwa watumishi wa Yesu na wanapoteza muda mwingi kwa kazi za Mungu watapata zero. Ninavyoandika mojawapo ni waziri katika serikali ya sasa, unasumbuliwa na vitu vidogo sana kwani aliyetamka ni Mungu, daktari sio Mungu ni mwanadamu kama wewe japo kuwa nimesikia siloam mnajiita sio wanadamu.
  Nadhani, maisha yenu yangekuwa kigezo cha kwanza cha kuwafanya watu wavutwe kuja kuwasikiliza la sivyo watu watakuja tu kwa kuwa wanashida hata kwa waganga wa kienyeji watu huenda wawapo na shida, japokuwa hakuna atakayependa kutambulika kuwa anaendaga huko. Kwa hu\iyo wingi wa watu kujaa huko usije ukachukua kama kigezo cha uwepo wa Mungu.
  La mwisho mimi sio mshabiki wa dhehebu au dini yoyote ila mimi ni mshabiki wa kweli tu. Kunamoja wa waumini wa huko aliniambia wokovu wa kweli uko siloam. Nijuacho mimi ukimwani Yesu moyoni na kukiri utaokoka. Hiyo version nyingine ya wokovu wa kweli ni pale tu unapokuwa kwa nabii mimi naona ni upotoshaji wa neno Mungu, na yapo mengine mengi yaliyopindishwa yaliyonifanya nione hii ni imani potofu.

 139. ma name is livinus likweti ukweli nikwamba yoyote ambaye njaa haija muuma awezi kuitaji chakula UKWELI SILOAM NIMEINGIA NA KUPATA UPONYAJI WA HALI YA JUU WALIOSOMA NA MIMI CHIDYA BOYS,KILOMBERO DAY NA IFAKARA HIGH SCHOOL WATAKUBALIANA NA MIMI NILIKUA NA ROHO YA UZINZI AMBAYO SIYO YAKAWAIDA,NILIKUA ROMAN NILIPOKEA MAFUNDISHO,KIPAIMARA NA BAADAE NILIINGIA UFUFUO NAUZIMA PALE UBUNGO NIKITAFUTA UPONYAJI WANGU KUACHA DHAMBI NILISHINDWA BADO NILIINGIA T.A.G KIBAONI IFAKARA NA MAZIMBU MOROGORO BADO UOVU ULIKUA PALEPALE, NILIPATA NEEMA MWAKA 2007 KWA MARA YA KWANZA KULIONA KANISA LA SILOAM NIKIWA ARUSHA KIMANDORO BAADA YA MAMA YANGU KUNIOMBA TUMSINDIKIZE RAFIKI WA MJOMBA WANGU KATIKA KANISA LA SILOAM ILI AOMBEWE ALIKUA ANASUMBULIWA NA UTI WA MGONGO NA ALIKUA NI DAKTARI PROFESIONAL WA WAKINA MAMA ANAITWA DOCTOR SWEKE,UKWELI TULIVYOFIKA KWENYE KANISA HILO TULIFUNDISHWA NENO NA BAADA YA NENO MAOMBI NA KATIKATI YA MAOMBI DOCTOR ALIANZA KULIA KWA SAUTI YA KUMSHUKURU YESU KUA ALIKUA ANASIKIA UPONYAJI UKIINGIA NDANI YAKE MWANZONI KABLA YA MAOMBI ALIKUA AMEVALISHWA MKANDA WA CHUMA AMBAO ALIUVUA BAADA YA MAOMBI NA KUINAMA NA KUINUKA NA KURUKARUKA KUA AMEPONA HILO LILINICHANGIA MIMI KWA ASILIMIA ZOTE KUAMINI MUNGU YUPO NA KUCHUKUA HATUA YA KUJIUNGA NA KANISA HILO SAWA NA KUMB 12:5-7 MAALI AMBAPO MUNGU AMEPACHAGUA TUENDE HUKO,UKWELI HAKUNA ANAYEPENDA KUPOTEA AU KUPOTEZWA ILA UKWELI BAADA YAKUJIUNGA NA KANISA HILO NIMEFUTIWA KIU YA ZINAA,NILIKUA NA LAZWA ST FRASINC HOSPITAL WIKI BAADA YA WIKI MALARIA ILIKUA HAIISHI,NILIWAI KUTAMKIWA LAANA NA JAMII WAKIWEMO BAADHI YA WALIMU WANGU SHULE NILIZO SOMA KWAMBA NIMJINGA NA SITAFANIKIWA KAMWE ILA SASA BAADA YAKUINGIA KANISA LA SILOAM MAJIRA ZAO MANENO YAO YAMEFUTWA NA SASA NAKARIBIA KUJENGA KWENYE KIWANJA CHANGU NILICHO NUNUA MWENYEWE NA SASA NA MILIKI GARI LANGU MWENYEWE HAYO NIMAFANIKIO AMBAYO NIMEYAPATA KUPITIA MADHABAHU YA NABII ELIYA,MAMA YANGU MZAZI ALIWAI KUTAMKIWA NA MADAKTARI WA ST FRANSINC NA MUHIMBILI KWAMBA HATA FIKA MDA MREFU KUA ATAKUFA NA ALIKUA AWEZI TEMBEA TUNA MBEBA KWENDA CHOONI LAKINI BAADA YA MAOMBI YA NABII ELIYA KUFUTA MAJIRA ZA MAGONJWA NIMZIMA WA AFYA KABISA,;;USHAURI WA BURE..;;;;;;KILA ANAYETAKA KUJUA JAMBO ASIWE MUULIZAJI WA PEMBENI NJOO KWENYE KANISA ULIZA MASWALI YAKO YOTE KAA MWEZI AU MWAKA ALAFU JIFUNZE KWABIDII KISHA UTAJUA SIRI AMBAYO TUNAJIVUNIA UKWELI NIKWAMBA TUMEMPATA NABII WA KWELI NA ANALO NENO LA KWELI KUMB 18:18,KILICHONIVUTIA ZAIDI KWA NABII ELIYA ALIKUA ANAFUNDISHA WATUMISHI NA MIMI NIKIWEMO KWENYE DARASA HILO 2008 ALISEMA YEYE SIO MGANGA HIVYO NGUVU YA MUNGU ILIYOKO NDANI YAKE KWA YOYOTE ANAYETAKA KUTENDA KAZI ZA MUNGU KAMA YEYE GHARAMA NI UTAKATIFU KULISHIKA NENO NA KULITENDA HIVYO ALIRUHUSU WATUMISHI KUWAOMBEA WAGONJWA HUKU NIKIWA NA ELIMU YAZAMANI YAKUOGOPA MAPEPO NA NGUVU ZA GIZA LAKINI NILIPO OMBEA WENGINE WALIFUNGUKA MAPEPO YANAKIMBIA HILO JAMBO AMBALO SIKULIONA HATA UFUFUO NA BAAADHI YA DINI NA MANABII AMBAO TUNAWAANGALIA KWENYE TV WAO NDIO KAMA MUNGU NA WANASIRI KUBWA HAWANA UAMBUKIZO,WOTE TUNAFAHAMU MTOTO WA NYOKA NI NYOKA SI NDIO SASA KWA NINI HAWA MANABII HAWAFANANI NA WAOWASAIDIA KIUDUMA?WAKATI KWENYE KANISA LA SILOAM MIMI MWENYEWE AMBAYE HATASIJAWAI KUKAA KITI KIMOJA NA NABII ELIYA AU KUONGEA NAE MUNGU WAKE YANI MUNGU ALIYEUMBA MBINGU NA NNCHI AMESHANITUMIA KUFANYA MAMBO MAKUBWA NA YA AJABU KAMA VILE WAPO WAGONJWA WALIOLETWA KUTOKA LOLIONDO WAKILETWA JUU YA MACHERA KATIKA KANISA LA SILOAM NILIWAI MWOMBEA MAMA MMOJA NA ALISIMAMA SAA HIYOHIYO,NIMEWAI MWOMBEA MCHUNGAJI WA DHEHEBU MOJA MOROGORO AMBAYE ALISHINDIKANIKA KUPONA HATA HOSPITALI NA ALIPELEKWA KWA BAADHI YA MANABII WA UONGO IKASHINDIKANA AKALETWA SILOAM AKIWA NA WADOGO ZAKE NA MKE WAKE NILIVYOMWOMBEA ALIINUKA SAA HIYOHIYO NA SASAIVI AMEAMUA KUWA MCHUNGAJI WA SILOAM NA YUKO SINGIDA NI MCHUNGAJI WA SILOAM, UKWELI USIO FICHIKA SINA UKOO WALA UNDUGU NA NABII ELIYA ILA KAZI AMBAZO MUNGU ANAFANYA NA AMEFANYA KUPITIA YEYE NIKUBWA NYINGI NA ZINATISHA KAMA NINI. ;;;; huyo anae dai siloam watumishi wanapandisha mizimu kwanza ndio waombe sio kweli na naomba toba kwa ajili yake na natubu pia kwa wote wasio amini na wote walio tukana na kumtukan nabii hao ni wachafuaji,kama walivyo msingizia yesu ana pepo ila ukweli halisi nimeuona nasasa nauwezo wakuwajua manabii wa uongo, manabii wa uongo utawatambua kwa kazi zao kama waganga wa kienyeji, asipo kuwepo yeye inabidi wamsubir au waweke video zake lakini kanisa la siloam anayefanya huduma ni MUNGU MWENYEWE, yeyote anayekubali kutii neno na kuacha uovu na kumwamini nabii sawa na 2NYAKATI 20:20 MUNGU anamtumia hata awe mtoto mdogo akikutamkia jambo ukaamini linakua na hiyo nikila eneo maali ambapo siloam hipo nnchi zote.;;;;;;;;;;YOH 9:7,MIMI SIKO KWENYE MASHINDANO, HUO NIUKWELI WANGU MBELE ZA MUNGU NA VIPO VINGI VIKUBWA SIJAVISIMULIA BADO. hekima moto hapa kama auamini hata nuhu awakumwamini sasa njoo siloam uone Mungu anavyotubariki nyie kaeni kwenye maneno,hakjuna anyejua utendaji wa mungu isipokua ni yule ambaye mungu amependa kumfunulia sasa ni hivi kanisa la siloam liko maali ambapo mambo ambayo jicho halijawai kuyaona wala sikio halijawai sikia wala kuingia ndani ya moyo ya mwanadamu,ili uyajue haya uje kwa nabii eliya ambaye MUNGU amemfunulia soma 1kor 2:6-10

 140. SILOAM NI IMANI POTOFU WALA HILI HALINA MJADALA. WANATEMBEA KWA MAWAZO YA NABII NA WALA SIO NENO ILIHALI WAKIUHADAA UMAA KWA SLOGAN YA SHIKA NENO TENDA NENO. HAWANA WALITENDALO SAWA NA NENO WANAIMBA TU.

 141. FERDINAND
  TUSOME 2NYAKATI 20;20 NA WAEBRANIA 6;12 NA INAONESHA WAZI KUWA BILA NABII UWEZI KUFANIKIWA JE HAPA UMESOMA MALAKI 4;1-7 BASI KIPINDI CHA MUSA WANAGESIMAMA WAO KAMA WAO NA IMANI INATOKANA NA KUAMINI UNACHO KIJUA IVYO NA SIKU NIKIASI SILOAM NA NIFE KABISA ILA WEWE NITAKUKUMBUKA KUPITIA TOBA YA KWELI MPENDWA

 142. Haki,
  YESU alisema Mt5:9 “heri afanyiae kazi amani kwa maana ataitwa mwana wa MUNGU. hii ndio njia pekee yaku itwa mwana wa MUNGU. na mimi ninavyo jua kutoka kwenye neno. YESU ndiye kuhani pekee kwa mfano wa yule Melkizedeki. si mwingine, wala si binadamu kwani yeye sadaka yake ndiyo ilikuwa kamilifu. Toba ya kweli ni ile tu tunayopewa kupitia sadaka ya mwana kondoo wa MUNGU.

  Ushauri wangu kwako, Haki ni kwamba usifwate sheria sana. sheria zitumike pale tu kuona kama umekosea. lakini badala yake, sikiliza imani. imani kwa YESU tu!. kwani yeye ndiye njia ya ukweli kwa MUNGU, ukweli wa MUNGU na uhai kwa MUNGU. amini tu neno la MUNGU sahau yote yaki binadamu. tengeneza misingi yako mwenyewe kwa msaada wa ROHO MTAKATIFU.

  kama uta hitaji kujua makosa yako; MUNGU yupo na neno lake lipo, litumie. kwani mwongozo wake ni mzuri kuliko wa huyo “eliya” na anakupenda zaidi yake na yuko tayari kukusaidia kuliko yeye.

  simama mwenyewe kiimani kama utakavyo ambiwa na ROHO MTAKATIFU

 143. NAMUSHUKURU MUNGU KWA YOTE NILIYOSIKIA ILA NENO LA KWELI LIPO SLOAM NA MUNGU WA KWELI NA KUHANI AFUNDISHAYE DINI NA MADHEBU WANACHANGIA TU KWA SABABU WANAISHI MAJILA YA DUNIANI YA JUMATATU -JUMAPILI NDIYO MAHANA UNAONA WANAPINGA WANAWAMUNGU TUWAKUMBUKE KUPITIA TOBA YA KWELI

 144. Nadhani huu ndio uongo uliokithiri kwa kanisa hili hasa kwa kuepuka kanuni ya kufasiri maandiko na kutumia mafunuo na ndoto zao za uongo. Kupitia imani hii wenzetu walichomwa moto na aliyejiita Eliya(kibwetere) na kwa kuwapa Ufunuo wa kuvaa nguo nyeupe na kuwa tayari kwenda Mbinguni kwa kuchomwa moto. Kila mtu anapaswa kujua kuwa kuna Nguzo kuu tano za kujua.
  1: Maandiko pekee ndio Mwanga mkuu na sio Nabii na mafunuo yake.
  2: Imani pekee ndio iletayo wokovu na sio matendo.
  3: Neema pekee ndo njia ya msingi wa wokovu wetu
  4: Yesu pekee ndiye Mwokozi wala sio mafunuo na ndoto za Nabii feki wengi.
  5: Utukufu ni kwa Mungu Pekee wala sio kwa Mwingine awaye yote.
  Kwa Nguzo hizi nadhani inatupasa kuepuka kudanganywa na wahuni wanaojenga Uongo kwenye msingi wa kweli.

 145. Yohana…..

  Napenda kutumia nukuu anayoipenda mno ndugu yangu Lwembe…..”yatatimiaje Maandiko?” Utawapotezaje wateule kama usipokuja na mafundisho kama haya hayo….?

 146. NILIYO YAONA NILIPO ABUDU SILOAM
  Napenda kusema hawa wenzetu wapo nje ya mstari
  a) Nilipata fuesa ya kuuliza kwanini wanasema wapo kipindi cha kutawala miaka 1000 na Kristo, waliniambia kuwa YESU amesha rudi ndiyo wanatawala naye. Cha kushangaza nilikaa mezani kuhoji ushahidi wa kimaandiko au wa kinyakati majibu hakuna. Sasa ninawaomba watu kuachana na imani potofu kama hii.

  b) Tena niliwauliza kwanini kiongozi wenu anajiita nabii Eliya Adam wa pili Mungu wa Majeshi? tazama walivyolishwa sumu. nikaambiwa eti Mungu amemwambia aitwe hivyo ili maadui na waovu wasimwone wakimtafuta jina lake Munuo…jamani hii si brainwash hata wafuasi wake hawawezi kufikiri kuwa wanadanganywa? aibu sana

  c) Kuhusu shetani kufa 4/8/2013 eti niliambiwa ni ufahamu wanawasaidia watu wachanga ili waamini shetani amekufa…..je hii inaingia akilini si kuwapoteza kabisa na kuwaangusha shimoni gizani.

  d) Ni kweli nimehudhuria ibada zao mafundisho yao, na hata vitabu vyao ninavyo kwa maana ni majirani kwa kweli mafundisho ya kiongozi wao ambayo huyaita mafunuo yana nguvu kuliko neno la Mungu na hupaswi kuhoji wala kuuliza ni kutii tu kwa kuwa nabii kasema. mbaya sana watu wamekuwa vipofu hawaoni wanako elekea wamekuwa mateka.

  e) Kingine wanatoa nembo za maji au kinywaji wanasema ni freemasons halafu wanayaombea na kunywa. sasa kama wanaweza kuyaombea maji na kuyageuza kuwa damu ya YESU kwanini wasiyaombee yakiwa na nembo. Tena cha ajabu MENGINE WANAJIMIMINIA KICHWANI NA MWILINI KAMA UGANGA PAMOJA NA MAFUTA.

  Ni hayo kwa leo, Mbarikiwe

  e) Cha ajabu kiongozi wao anaimbiwa nyimbo za kuabudiwa na kutukuzwa na kushukuriwa…..tunakuabudu Mungu wa Majeshi, Mungu wa Eliya Adamu wa pili…hakuna kama wewe….lala lala…jamani hii ni extrem na watu wamekuwa zuzu wanaelekea shimon. Wakuabudiwa ni YESU pekee

 147. Mama K, Bwana akubariki sana!
  Kuugua na kulia kwako, kwa ajili ya wapendwa wenye kuyapenda sana ya dunia na dini zake, ule mchanganyiko maalumu unao unajisi Utakatifu aliotukirimia Mungu kwa Neema, nimekuona unavyougua! Ile mioyo ya nyama aliyotuwekea Mungu, wapendwa wengi tumeitoa na kuirudisha ile mioyo migumu ya mawe! Hatuna tena uwezo wa kuipokea Injili na Kweli yake, mioyo yetu imekakamaa kwa mafundisho ya Uongo, viriba vyetu ni vikavu sana, haviwezi kuupokea Mvinyo Mpya maana vitapasuka, puff! Mafundisho ya kidhehebu yameyakausha Mafuta yote, ule Uhai wa Mungu ndani yetu, viriba vimepoteza ule ulaini unaoviwezesha kulitanukia Neno la Mungu, tumerudishwa utumwani!

  Hatutaki kabisa kusikia habari za kuachiliwa kwa Kristo, ile INJILI; tunamtaka Baraba, mafundisho yetu ya kidhehebu, hayo yenye kulifisha Neno la Mungu! Si unaona, huyu anakwambia nabii Eliya wa Siloam ndiye Adamu wa Pili, ni aibu kiasi gani kwa kanisa lililonunuliwa kwa Damu ya Thamani, linapoyarudia matapishi yake, wamerudi kuiabudu miungu yao ya kipagani iliyojipachika majina na sifa za ki Biblia! Mwingine anakuambia sabato ndio Muhuri wa Mungu, nao wote hawako tayari kuyaruhusu Maandiko yawatawale katika maisha yao, inasikitisha saana!!!

  Basi tufanyaje? Tumshukuru Bwana kwa yote, nawe endelea katika huko kuugua na kulia alikokupa Bwana, maana hakuna jambo linalojifanyikia tu chini ya mbingu isipokuwa kulitimiza kusudi la Mungu. Ndipo huenda wakati wowote akapita yule malaika aliyetumwa na Bwana:
  “BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.” Eze 9:4
  Mambo ya Mungu yako katika urahisi wa jinsi hiyo kwa wale wenye kumuamini, huenda amekwisha kupita nawe ulikwisha kutiwa alama!!

  Umeliona jiji letu? Dini zetu!!! Akimaliza, huyo aliyekutia alama Mama K, nyuma yake wanakuja malaika wengine, hebu itazame amri waliyopewa: Eze 9:5-6
  “Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.”

  Kisago kitaanza na wazee walioko mbele ya nyumba, hao manabii na mitume na maaskofu na wachungaji na viongozi vinara wa mafundisho ya Uongo!

  Ndugu zangu, tujinyenyekeze kwa Neno la Mungu, tusiwe wepesi wa kulibishia, safari hii haji Mungu, bali malaika ambao hatuwezi kuwasomesha watuachie, hao wanachukuaga Amri moja tu!!!

 148. NABII ELIA NI NABII ALIYETUMWA NA MUNGU NINAPOSEMA HIVI NAMAANISHA KWAMBA KUNA MANABII WALIOTUMWA NA WATU NA WANADAM, KUNA NABII ALIEJITUMA MWENYEWE NA PIA KUNA NABII ALIETUMWA NA MUNGU. DINI NA MATHEHEBU HAWANA NENO BALI SILOAM TUNALO NENO

 149. Kwa kweli ninamshukru sana Mungu wako Lwembe nahamini kabisa Mungu wa Lwembe ndiye Mungu Mungu wangu , hayo unayosema ni ukweli mtupu , anayebisha akatafute mda wa ziada asome neno na kulitafakari, akishamaliza atakuja kwako Lwembe na kukuunga mkono, tuzidi kuomba kwa Mungu maana anasema hataki mtu yeyote apotee anataka wote waokolewe, nawe Lwembe naomba uungane nami mimi na mtume Paulo tutamke na kuomba kama alivyoomba mtume Paulo ktk warumi 10:1 akasema ndugu zangu nitakayo sana moyoni mwangu na dua yangu,nimwombayo Mungu ni kwa ajiri yao hili waokolewe.Dini hizi na mapokeo yake yameharibu watu wa Mungu , tusimame tuangamize, tubomoe , tuvunje, tuharibu sawa na Yeremia 1:10 , mambo haya yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu kwa watu wake, Usiasaau kuomba Mungu afanye neno kwa habari ya ndoa ya jinsia moja maana watu wanajiamulia mambo kienyeji na hata baadhi ya viongozi wanaweka utaratibu wa Mungu pembeni, tangu mwanzo Mungu aliumba mme na mke , maana hiyo alikuwa na makusudi ya kufanya vile, hakuwa mjinga wala hakukosea alivyofanya hivi, leo watu wanamuweka Mungu kando wanatenda wanavyotaka Hii aikuwa ktk mada lakini nimeunganisha umo umo , lakini nasema kuwa siku zaja walio chini watajua kuwa aliye juu ndiye anayetawala juu ya ufalme wa wanadamu. Daniel 4:17,25-26 . maana imeandikwa kuwa sharti amiliki yeye, 1 wakolintho 15:25.Imeandikwa pia ktk Zaburi ya 65:2 kuwa wewe usikiaye kuomba wote wenye mwili watakujia. Ukweli ni kwamba kila siku ninaingia ktk maombi na ramani ya dunia, nasema Mungu baba shauri lako likasimame kwa watu wako, mapenzi yako yatimizwe, kwa watu wako, utakalo ndilo lifanyike kwa watu wako,Kila goti lipigwe na kila ulimi ukiri kuwa Yesu ni Bwana kwa utukufu wa Mungu baba, hapa sasa ninaita wapagani, waislamu, waromani, waruteri, na wote ambao hawamuhabudu Mungu ktk Roh na kweli. Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe juu ya nchi kwa mda wa miaka mitatu na miezi sita mvua aikunyesha, akaomba tena mvua ikanyesha. Mungu wa Eliya ndiye Mungu wetu Yakobo 5;17.Ubarikiwe sana Lwembe maana unaona ninachokiona. Mama K.

 150. Matunda tisa ya Roho Mtakatifu,
  Hivi huwaga mnayakagua mafundisho mnayopewa katika Maandiko au mnayameza tu?

  Angalia kauli yenu:
  “Huu wakati wa kizazi cha nne na ndani ya majira sahihi ya kanisa yaani miaka 1000 ya kutawala na Kristo Yesu ndio wakati ambao Mungu wa kweli anaabudiwa katika roho na kweli.”
  Jaribuni kuwa waangalifu kidogo, rudini katika Maandiko muangalie ni lini jambo hili unalilipigia debe kuwa tayari limeanza, linapaswa kuwa kulingana na programu ya Mungu na si mambo ya manabii wa uongo wanaowafanya vituko!

  Bwana awasaidie!

 151. Majo Best
  Kwanza nikupe pole kwa kukwazika.

  Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa umenisikitisha sana kwa kuliweka Neno la Mungu nyuma ya taratibu za dini, yaani ukiutanguliza Ukatoliki na kuuhesabia Haki badala ya Neno la Mungu!

  Unapozungumzia idadi ya watu na kuifanya hiyo ndiyo kigezo kwa Mungu katika maamuzi yake, sidhani kama wazo la jinsi hiyo lafaa kukuongoza. Maana unapowaona 1.2 bn kuwa wanatosha kumshawishi Mungu kuliacha Neno lake, labda kabla ya kujiaminisha katika hilo, kwanza ungetafuta idadi ya watu waliopoteza maisha na nafsi zao katika gharika ya Nuhu kwanza ndipo uone huko kujiaminisha kwako katika idadi ya watu kama kuna manufaa au ni kufukuza upepo!

  Tunapozungumzia kanisa Katoliki, ni lazima ujue pia kulitofautisha na waumini waliomo katika kanisa hilo. Wengi wa waumini hao, ni wale waliozaliwa kwa wazazi Wakatoliki na pengine pamoja na wazazi wao, wote hawaujui hata Ukatoliki wenyewe zaidi ya kuyakariri mafundisho wanayopewa na taratibu za ibada wasizozijua kiini chake, hata hao watu maarufu uliowataja. Ndio maana kutoka humo humo Katoliki Mungu atawaita wanae watoke waje kumfanyia ibada iliyo safi badala ya hizo “Salamu Maria…” na ibada za Watakatifu waliolala, na kuabudu sanamu zilizojaa katika majumba yao ya ibada pamoja na ibada za wafu, na kumsujudia ‘mtu’!

  Kwani wewe ukiingia katika jumba la mapepo nawe ndio unakuwa pepo? Hebu jaribu kuifuata historia ujifunze mengi kuhusu kanisa Katoliki, kuliko kuwa mlalamikaji usiye na rejea. Papa Yohane wa mwisho aliomba msamaha kwa Waprotestant kwa tendo la kanisa hilo la kuwaua watakatifu zaidi ya milioni 60 kwa kulipinga, yaani walipozikataa ibada za kuzimu, sasa wewe sijui utakatifu wa Katoliki unauona katika kigezo gani? Maana hata kama utachukua wasaa kidogo tu wa kuzikagua ibada zao katika Biblia, ungeliona jambo hilo la kwamba hao si Kanisa la Kristo kabisa! Au majengo yao mazuri ndio yanayokuchanganya?

  Kuhusu Waprotestant, shida yao kubwa ni hayo madude waliyotoka nayo Katoliki walipowakimbia. Hayo ndiyo yanayoendelea kuwaparaganyisha, maana wamekuja na miungu ya Kikatoliki hiyo ya UTATU MTAKATIFU na mifumo ya uongozi inayomtoa Roho Mtakatifu (yaani zile Huduma Tano) nje ya ulingo. Basi unapobaki na hekima ya kibinadamu kukuongoza ni rahisi sana hila kujipenyeza na kuleta mitafaruku katika tafsiri ambazo hawana ujuzi nazo. Kwa hiyo usilalamike sana, wala hakuna anayehukumu isipokuwa Neno lenyewe ndilo linalohukumu, basi linaporejewa hilo jaribu kulikazia macho hilo badala ya kujiridhisha katika uongo ambao Mungu atahitaji hesabu yake kesho, nawe ukiwa ni sehemu ya uongo huo!

  “Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.” 1Yoh 5:21

 152. Bwana YESU,asifiwe nimefuatilia mjadala huu,kwa umakini,ukweli ni kwamba,kuna WAKRISTO wapagani katika miaka hii,wanaogeuza maandiki NJIA sahihi ni Kumuamini MUNGU kupitia YESU..Yohana 3:16

 153. Matunda tisa ya Roho Mtakatifu;Inavyoelekea kwako wewe siloam ndiyo Yesu wako!Nakushauri kipimo chako cha kumjua aliyetumwa na Mungu kiwe Biblia pekee na siyo mbwembwe za watu!Kama kilivyo kipimo sahihi cha uzito wa kitu fulani ni mizani, basi kipimo cha Ukristo ni Biblia!Mafunuo yaliyo kinyume na Biblia yanatoka kwa shetani,yachunguze kwa umakini wa rohoni kwa msaada wa Roho Mtakatifu!

 154. Nduggu Baraka;yatazame matumizi ya maneno haya: Mungu na mungu ni tofauti Mdo.7:43,nk. hata Roho Mtakatifu na roho mtakatifu ni tofauti vivyo hivyo Yesu Kristo ni tofauti na yesu kristo!Barikiwa!

 155. Namshukuru Mungu kwa ajili yenu wote mliojitokeza kuchangia mawazo mlioayo juu ya kanisa la SILOAM. kiukweli kanisa la siloam sio dini wa dhehebu bali ni kanisa. Dini na dhehebu ni mpango au utaratibu uliowekwa na watu au wanadamu kumtafuta au kumwabudu Mungu wakati kanisa ni mpango wa Mungu mwenyewe kuwatafuta watu au wanadamu. Dini na madhehebu yalikuwepo duniani hata kabla ya Bwana Yesu hajaja. Yoh 4: 22- 24 tunaona Bwana Yesu akisema kuwa watu walikuwa wanaabudu wasichokijua na kwamba Mungu alikuwa haabudiwi katika roho na kweli ndiyo maana akasema utakuja wakati ambao Baba ataabudiwa katika Roho na kweli. Huu wakati wa kizazi cha nne na ndani ya majira sahihi ya kanisa yaani miaka 1000 ya kutawala na Kristo Yesu ndio wakati ambao Mungu wa kweli anaabudiwa katika roho na kweli. Dini Mungu aliisha zikataa Amosi 5:21 kwa sababu hazikuanzishwa na yeye. . Hata kama yeyote anapinga ukweli unabaki palepale. Mtume na Nabii Eliya wa kanisa la kweli la SILOAM ndiye amepewa Agizo na Mungu kumjengea kanisa linalomwabudu Mungu katika roho na kweli.

 156. Ndugu yangu CK Lwembe, Tumsifu Yesu kristu. Kilichonikwaza ni hukumu zako kwa Kanisa Katoliki lenye watu wapatao 1.2bn duniani.

  : Wako ndani ya mauti ya Kikatoliki
  :Wako katika kanisa(jumba la papepo!)
  :Wako atika Kanisa ambalo ndilo lililoua Kanisa la Kwanza

  Kwa maelezo yako watu wote waliotangulia ndani ya Kanisa hili wako Jehanamu ya moto,na Mungu hana huruma kila anayefunguliwa,badala ya kukaa ndani ya Kanisa akawa mwanga kwa wengine anaenda kufungua Kanisa lake. Lakini mimi naona afadhali ya wakati wa hilo Kanisa la mapepo,Kuliko wakati wa sasa wa Makanisa ya Kiroho wa Mungu yaliyopo sasa, dunia inaenda kubaya,mpaka kuna watu wanaona injili ya Yesu ni USANII MTUPU! . Ndugu CK kwa mtu mwenye mtazamo wa kweli na usio na upendeleo anapaswa kulishukuru japo kidogo Kanisa ambalo ndilo walilofia wazazi wetu waliotanguliaaki, kwani wao ndani ya Kanisa la mapepo(Katoliki) walipendana, waliheshimiana, walisaidiana ,waliombeana, walivumiliana, walionyana kwa upole, kulikuwa na watu wenye hekima kidogo hata kama ni ya kidunia eg. Mlm J.K Nyerere, D .Tutu, Mama Tereza wa Calkuta na wengine ambao cjwajui,hapakuwa na matabaka ya kidini,kikabila,vipato,madhehebu na machukizo mbele za Mungu kama sasa wakati tuna makanisa ya kiroho mengi sana! soma 2Tim:3:2-9. Ck tuangalie kauli tunazotoa,maana tutazitolea hesbu mbele za Mungu. MAWAZO YA MUNGU SIO KMA YA MWANADAMU. tumuachie yeye atawahukumu Wakatoliki, huoni wao wako kimya? mara nyingi huwa si wepesi wa kujibishana,nami nahisi sikutumia busara kukubishia. Nakutakia kila la heri,tuombeane HEKIMA YA MUNGU.

 157. ktk kila jambo ulifanyalo ulisikialo kwa mtu usiwe mwepes wa kuliamini bal lipime lko sawa na mandiko maana manabii weng wa uongo wametokea toka ez za manabii kwa mf manabii wa baali ez za nabii yeremia walikuwepo hata ez za mikaya walikuwepo.hawaja aza leo. hivyo tuwe makn na ufunuo tunao letewa yakuapasa kuangalia je uko sawa na maandko au la.maandko yako wazi hupaswi kuongeza wala kupunguza yaliyo andikwa kwa matakwa yako mwenyewe. tuijue kweli ambalo n neno la mungu lpate kutuweka huru. mbinguni hatuta ingia kwa sababu ya kuwa unasari kwa nabii fulan au mchungaja fulan au mtume fulan.bal n wale walio andko ktk kitabu cha uzima wa milele walio oshwa mioyo kwa damu ya pekee ya bwana wetu yesu kristo walio saf mwili na roho. ndg wapendwao sana na bwana yesu kristo yatupasa kumjua mungu na kumtafuta mungu kwa nafsi zetu na kuomba kila siku ili umjue mungu tusiyumbishwe na mafundisho mengne ya mashetan yanayo kuja kwa njia ya mungu tumgeukie mungu 1 tim 4;1-8, 2the 2;10-12, 2tim 3;1-17, 1kor4;6-13,1yahana 4;1 mathayo 7. wapendwa tujihadhari tujiweke tayar kwa siku ya bwana wala tusidanganyike maana shetan ni mwonga na baba wa huo anakuja kwa mfano wa malaika wa nuru kumbe mbaya balaaaaaaaaaaaa! usipo kuwa na neno na macho rohon c atakuteka jaman
  namuomba mungu atie roho ya hekima na ufunuo ktk kumjua yeye macho ya mioyo yenu yatiwe nuru mpate kuijua kweli ya kristo ambayo huweka huru mbali na dhambi mbarikiwe wapendwa ktk kristo bwana wetu

  TENA MTAIFAHAMU KWELI, NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU
  YOHANA 8;32

 158. shalom
  Ohh mtumishi, Ndg, Majo Best, km hutajari andika email yako hapa ili nipate kuwasiliana nawe…. Mungu wangu na akubariki.

 159. Majo Best, naona umenipa pole sana kwa kumuaibisha Mungu wangu wa Pentekoste! Pia umenishauri nimuombe Mungu anipe hekima! Ninakushukuru kwa hayo. Lakini mbele tena umeniomba msamaha kwa maneno makali uliyonitolea!

  Labda niseme kwamba, mimi sijakwazika kwa jinsi yoyote ile, kwani nimeyachukulia maneno uliyoyasema kama onyo lililojikita katika upendo, kulingana na ufahamu wako katika hayo niliyoyaandika. Kwahiyo napenda kukuhakikishia kwamba HUJANIKWAZA kabisa, bali umeniongezea shauku ya kutaka kujua ni yapi haswa katika hayo niliyoyaandika ambayo yamekukwaza.

  Unajua, Neno linasema, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Halijasema Imani huja kwa kusoma Biblia! Ndipo ni lazima tukubaliane na Mpango wa Mungu wa Wokovu ambapo anasema ametuwekea Huduma Tano makanisani mwetu, wachungaji, wainjilisti, mitume, walimu na manabii ndani ya makusanyiko yetu. Nazo Biblia hutusaidia kumjua zaidi Mungu na kuwakagua hao wanaotuhudumia ili kuwa na uhakika kwamba wamewekwa na Mungu. Iwapo utagundua kuwa mambo yaliyopo hapo hayaendani na Neno la Mungu, nawe ukaendelea kukaa hapo eti ukijiridhisha kwa kusoma Biblia, basi utakuwa umeamini nini? Neno linasema TOKENI katikati yao! Usipotoka basi kaa ukijua kuwa unakusanyika kwa HASARA!!!

  Sijaona lugha laini inayoweza kumzuia mtoto anayetaka kuvuka barabara bila ya kuangalia magari zaidi ya kumshtua ili asimame na kuigeukia hiyo sauti kali; wala kwa kusoma kwangu Biblia siwezi kukiri kuwa imejaa lugha laini, labda uwe unaisoma kama hadithi kama alivyosema Tunkuh; vinginevyo katika kuisoma kwako inapaswa Maandiko hayo yageuke yawe Sauti ya Mungu ndipo lile jambo la Imani huweza kuzaliwa, na likakuongoza katika matakwa yake!

  Basi nigekuomba ndg yangu Majo Best, tuyalete mambo yote katika kipimo cha Neno la Mungu na si mafundisho yetu ya kidhehebu, hata ikiwa ni unyenyekevu, pia ni lazima uendane na Neno na si wa kinafiki wa kidini, tukiutanguliza huo ili kuinyamazisha sauti inayopingana na mafundisho yetu. Labda nikuulize jambo kuhusu unyenyekevu, Je, kuna unyenyekevu unaoweza kuuzidi ule wa Kristo alipozipindua zile meza za wafanya biashara pale hekaluni??

 160. Tunkuh, Tumsifu Yesu Kristu,
  Sina budi kumshukuru Mungu wa Bw. wetu Yesu kristu aliyeiweka ndani yako roho ya hekima, asante sana kwa ajili ya ufafanuzi wako wenye mionjo ya unyenuekevu wa kweli,mimi binafsi nafurahi kukutana na mawazo ya watu kama wewe,kwani nahitaji sana HEKIMA YA MUNGU. Ivyo nakuomba uniandikie kwa kinaganaga njia uliyotumia mpaka kufikia hapo ulipo, pili naomba uniombee kwa Mungu nami anipe roho wake kunifundisha neno wake si kwa ajili ya ubishi,sifa na wala kijifanya najua bali kwa ajili ya kuutafuta uso wake.Naomba maelezo hayo nitumie kupitia E- mail yangu . Mwisho naomba msamaha kwa ndugu CK Lwembe kwani nimemtolea maneno makali.

 161. Shalom watumishi.
  Binafsi nimeshiriki ibada za madhehebu mbalimbali, hii ni kutokana na mazingira niliyopitia ktk makuzi yangu. nataka tushirikiane huu uzoefu niliouptata

  1-Karibu ibada zote nilizohudhuria Biblia ndio kitabu kinachotumika kutoa muongozo wa ibada husika, inaweza ikasomwa na kiongozi, au waumini wote kwa pamoja au mteuliwa kulingana na utaratibu uliowekwa..

  2-Kiongozi ni mmoja, anayetumika kuitafsiri ile mistari ya biblia, haijalishi hiyo mistari inatafsiriwa kwa uwezo wa Roho MT. au ni kwa mtazamo wa kiongozi husika, au anawasilisha kile kilichokwisha tafsiriwa, kutokana na utaratibu wa kanisa.

  3-Taratibu hizi hazitofautia saaana, mf; unyenyekevu ibadani, vipindi vya sadaka, kusifu na kuabudu n.k..

  4-Ktk ibada zote, maswali hayana nafasi labda nje ya ibada, hasa kwa wale wanaodhuria mafundisho ktk kanisa husika..

  5-Kuna wengine wanaamini uwepo wa mapepo na wanayashughulikia…ibada zingine hazishughuliki kabisa na hilo.. pia ziko ibada zinazohusisha maombezi ya mtu mmojammoja au makundi fulani n.k, na zingine hazihusishi hilo..

  6-Kuna wanaoamini Yesu ni mwana wa Mungu, wengine Yesu ni Mungu mwenyewe. Kuna wanaoamini juu ya Utatu mtakatifu yaani Baba Mwana na RohoMt. na wengine ktk Mungu mmoja.

  7- Kuna wanaoamini ktk sala za wafu, watakatifu fulani, Maria mama wa Yesu, sabato na torati, n.k na wengine hawana imani hiyo kabisaaa…Na wengine ndio km hao Siloam na taratibu zake..

  Cha ajabu imani zote hizo muhimili wake ni Mistari iliyopo ktk Biblia. Haijarishi nguvu ipi inatumika kulilinda kanisa iwe ya giza au nuru, mistari ya Biblia lazima itatumika, ili kuimarisha uhakika wa imani za washirika wa kanisa husika.

  Wakristo wenyewe kwa wenyewe tumekuwa tukikosoana kila kukicha, kila mtu akiona kuwa dhehebu lake ni sahihi kuliko la mwingine. Hata viongozi wa madhehebu, wanatumia muda mwigi wawapo ibadani kutoa kasoro wenzao baada ya kuhubiri injili…. Na ni Mistari hiyihiyo ya biblia inatumika ktk hutoaji wa hizo kasoro. Mbaya zaidi hata wasio Wakristo wanatumia mistari hii kukashifu na kuhoji juu ya Ukristo…

  Hii ilinipa changamoto saaana ya kutaka kujua juu ya siri iliyopo ktk maandishi ya Kitabu hiki Biblia…

  Uchunguzi wa awali niligundua kuwa Biblia ni kitabu chenye vitabu vingi ndani yake, na kila kitabu kina kusudi kwa yule anayekitumia(anayesoma) kwa wakati huo anaosoma au uliompita au unaomjia. Na baadhi ya maneno yake yamejirudia zaidi ya mara mbili, ili kumsaidia msomaji kuoanisha na kupata maana iliyokusudiwa kwa wakati na somo husika. Na pia imegawanyika ktk Sehemu mbili, ambazo zina tegemeana nazo ni……….

  Agano la kale (Torati), ambalo ndani yake tunaona uumbaji wa Mungu, Uteuzi wa Mungu juu ya Taifa la ESRAEL, Sheria na taratibu ambazo Mungu alizipanga kupitia Musa na wenzake, maisha ya Manabii, Makuhani, watakatifu na Wafalme wa wakati huo, laana na baraka n.k

  Sehemu ya pili ni Agano Jipya (Imani) hapa tunakutana na injili ya Mathayo, Luka, Yohana n.k zote zikielezea juu ya kuzaliwa mpaka kifo cha Yesu na Mafundisho yake, ambayee alitabiriwa na manabiii tangu ktk Agano la kale…Mtume Paulo amefafanua sana juu ya utakatifu, sheria na imani pia tunaona Ufunuo wa Yohana jinsi hali itakavyokuwa hapo mwisho…

  Hizi sehemu mbili za biblia pia zimesababisha mgawanyiko mkubwa sana ndani na nje ya UKRISTO …ni kama zinakinzana na wakati huohuo zinategemeana.

  Pia nikagundua kuwa Biblia ni Kitabu kinachosomwa na watu wengi
  ulimwenguni kuliko kitabu chochote, na usomaji wake umegawanyika ktk makundi matatu muhimu…naweza kusema haya makundi ndio yanayosababisha kwa kiasi kikubwa mgongano uliopo hii ni kutokana na matokeo ya taswira iliyopo juu ya Ukristo.

  1-kundi la kwanza na ndilo kubwa ni lile linalosubiri kiongozi wa madhabahu asome vifungu kisha atafsiri, kundi hili huwa halina maswali vichwani mwao wala kudadisi juu ya mistari hiyo…. ni km wanakaririshwa na husomaji wao ni mpaka iwe siku ya ibada. Yaani wapo kimapokeo zaidi. Na km watasoma nje ya ibada basi watasoma km Hadithi mf; kitabu cha Ester, Daniel,Samwel Vinapendwa sana na watu wa aina hii…

  2- kundi la pili ni wale wanashughulika na mstari mmoja mmoja ndani ya kitabu hiki bila kujua kiiini na madhumuni husika juu ya huo mstari, na hapa ndiko wanakokamatwa wengi kiimani. na mara nyingi hawa ni wale wanaotafuta
  (a) Maneno ya faraja ili waweze kuwafariji wanaowahubiri au wao wenyewe kwa faida za kimwili zaidi…
  (b)ushindani kutaka kutoa kasoro wengine au kukashifu,hawa uoanisha mistari ya Biblia na vitabu vya imani nyingine, au sayansi na mazingira n.k
  (c)wako wanaokariri mistari ili kuonekana kuwa wanaijua Biblia ktk hawa ndiko wanakopatikana washindani wengi, yaani wabishi na wajuaji.

  3- kundi la tatu ni wale walopata maarifa toka kwa Bwana Wanaomcha Mungu wa kweli … wao husoma Biblia mara kwa mara, kutaka kuongeza maarifa ili kumkaribia Mungu, si kwaajili ya ubishani au kumkosoa mwingine Na hawa Roho Mt. ndio anayetumika kama mtafsiri na muelekezaji. Kundi hili huwa alipati shida juu ya muingiliano uliopo kati ya Agano Jipya na Agano la kale, alipati taabu ya kujua vya nuruni na vya gizani, sikuzote huongozwa na Amani ya Bwana iliyopomioyoni mwao.

  Hili kundi la tatu ni la watu wachache sana, maana hawalengi saana maslahi fulani, hata hushuhudiaji wao ni wa unyenyekevu na upole na si kwa ushindani, hawavuti kondoo ili tu wajae nyumba wanazoabudia kwa maslahi yao, bali huwaleta kondoo mbele za Mungu wa kweli, kwa kuwafundisha ile kweli waliyofunuliwa na Roho wa Mungu ktk Biblia..

  Nashauri……Kama tu wakristo wa kweli na tunataamani kuishi maisha ya ushindi chini ya jua na hata kufikia uzima wa milele, tujiunge na hili kundi la tatu,tuache kukosoana kwa kukebehiana na kushutumiana. Kila mmoja wetu achukue jukumu la kusoma maandiko kwa kumuomba Roho Mt. awe mtafsiri wake. Na tusiache kujichunguza km tuko mahali sahihi kiimani.?

  Ni hivi mpendwa ukiwa msomaji mzuri wa neno la Mungu na ukitafsiriwa na Roho, ni rahisi kujua juu ya misingi ya imani uliyonayo juu ya YESU na kanisa lake hawezi mtu yoyote kukuyumbisha.

  Binafsi nilipokosa muelekeo niamini lipi niache lipi juu ya imani na madhehebu, maana ilifikia wakati niliona kila Mhubiri yuko kimaslai zaidi …..Niliutafuta uso wa MUNGU kwa maombi ya kumaanisha ..Ndipo nilipooneshwa cha kufanya… kwa kuanza kusoma Biblia kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo nilichukua mwaka mzimma na miezi miwili kuimaliza…Kitabu hiki huwa hakiishi hamu na kinaeleweka vizuri sana unapokuwa na mtafsiri Roho,. Huko nyuma nilikuwa nasoma km hadithi inayomuhusu mtu mwigine hivyo sikuelewa namna Mungu alikuwa anaongea na mimi ktk yale maaandishi.. Baada ya hapo nilianza kuhudhuria kanisani bila manung’uniko na maswali mengi na Upendo wa Mungu ukaniunganisha mimi pamoja na madhabahu ninayoabudia….hii ni kutokana na kuijua kweli..

  Yaliyoyangu nayafungia ktk chumba changu cha moyo na kutenda sawa na Mungu atakavyo… yasiyo yangu nayarusu yapeperushwe na upepo.

 162. BWANA YESU ASIFIWE.NDUGU WAPENDWA KTK KRISTO YESU. yatupasa kuwa makini sana na ulimwengu wa sasa tunaoishi, tusome na kulielewa neno na kutafakari Roho mtakatifu atatufunulia na kutukumbusha yote ambayo YESU KRITO ALITUAMBIA NA KUTUFUNDISHA, 1yohana 4:1. tunasisitizwa kujabu kila roho ie tujihadhari sana na mafunuo. pia ukisoma vitabu vya injiri nb Mathayo 24:10-11,24-25 Inatupa tahadhari na kutueleza wazi wazi vitu ambavyo vitatokea nyakati za mwisho. imani yako ktk KRISTO ndiyo itakayo kuongoza huku ROHO MTAKATIFU AKIKIONGOZA. jambo la msingi zaidi kila jambo unaloliuna muulize MUNGU kwanza akueleze vizuri ili uzidi kuwa jasiri. Yoshua 1:9. MUNGU AWABARIKI. Naomba MUNGU atutie nguvu na shauku ya kusoma na kulitafakari neno lake ili imani zetu zisiyumbishwe.

 163. CK KWembe, inabidi nikupe pole sana, kwani umemwaibisha sana Mungu wako wa Pentekoste, kwani inaonyesha huna hekima, nakushauri umuombe Mungu wa kweli akupe hekima. yote uliyoandika yanaonyesha kiasi gani umepungukiwa hekima. Hakuna jinsi unaweza kuniconvince kuwa wewe unamjua Mungu wa kweli wakati umejaa dharau na majivuno. Omba msamaha na utubu maaana hujui unaloliongea. Nami nakuombea japo Baba yetu moja.

 164. Ck Lwembe nakubaliana sana na maoni yako, Mungu akubariki kwa ujumbe wako. Hiki ni kipindi ambacho kila mkristo anatakiwa awe macho sana kama kweli anataka kuurithi uzima wa milele. Wadanganyifu wamekuwa wengi duniani. Mbaya zaidi ni pale anaedanganya na wanaodanganywa kama hawajui kuwa huo ni uongo. Wokovu ni kwa njia ya Imani ktk Jina takatifu la Yesu kristo. Baada ya kutubu dhambi na kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu, tunatakiwa kuendelea kuishi maisha yanayoendana na kutubu kwetu kwa maana ya maisha ya utakaso. Tukiwa ktk hali hiyo tunapokea ahadi ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Baba. Mtu kabla hujajiunga na dhehebu lolote ni muhimu kujua kama misingi ya imani yao kama haipingani na Biblia takatifu. Lengo kuu la Mungu kutuokoa tuurithi uzima wa milele. Hivyo Mwanadamu aliyeokolewa na Bwana afahamu kuwa Lengo kuu ni kuurithi uzima wa milele. Ukiwa ndani ya kristo wajibu wako baada ya kuokolewa ni kujilinda na dunia pasipo mawaa, kuwatembelea yatima, wajane na maskini kwa ujumla na kuwasaidia katika dhiki zao, pia kuihubiri injili kwa kila kiumbe. Kama dhehebu lako halisimamii mambo hayo basi fikiria kwa makini uhusiano wako na Kristo upoje. Hatukatai baraka za mwilini zipo lakini hilo sio Lengo la msingi la injili ya Kristo.
  Kama kweli yupo nabii wa Bwana, kwa mujibu wa Biblia atawaelekeza watu kwa Yesu Kristo waokolewe, waishi matakatifu, wajazwe Roho. Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo yote mtazidishiwa.

 165. Wapendwa,
  Ni vizuri kuzijua Huduma au makanisa kuwa yanasimamia nini kimafundisho, lakini ni vizuri zaidi ukiyajua yanahudumu katika milki gani!

  Kimsingi, hakuna huduma yoyote ile iliyo nje ya mpango wa Wokovu kwa kadiri Mungu alivyoupanga, huduma zote zinautimiza mpango huo maana unapozungumzia Kuokoa, ukamilifu wa kuokolewa uko katika Maangamizi! Ndipo twapaswa kujua kuwa tumeokolewa kutoka ktk makundi yanayoangamia!

  Kwa kifupi hatua za Msingi za kuufikia wokovu ziko tatu:
  1. Kuhesabiwa Haki kwa Imani
  2. Kutakaswa
  3. Ubatizo wa RM
  Hizo ndizo hatua zilizopitiwa na Kanisa katika Kufufuka kwake kutoka katika Mauti ya Kikatoliki. Yaani Ukatoliki ndio ulioliua kanisa la Kwanza, na juu yake kujisimika lenyewe nalo kuwa ndilo Kanisa! Lakini hilo ni jumba la mapepo!!!

  Kwahiyo katika hatua ya Kwanza ya Ufufuo wa Kanisa la Kristo, hao wameitwa kutoka katika Mauti ya Kikatoliki kwa Imani, malaika mbeba Sauti ya Mungu, ile iliyomuita Lazaro kutoka kaburini akiwa ni Martin Luther. Likaamka kundi kubwa kwa Sauti ile ya Kuhesabiwa Haki kwa Imani, kinyume na mafundisho ya Kikatoliki yaliyowahesabia haki waumini wake kwa sadaka zao, sadaka kubwa, haki zaidi!!

  Basi hilo ndilo kundi la kwanza, hao walioipokea ile Sauti ya Mungu kupitia Luther, ndio hawa hapa Waluteri wakiendelea katika Neema ya Kuhesabiwa Haki kwa Imani. Sasa ukumbuke kwamba Martin Luther hakuwa nabii bali mwana Matengenezo tu. alipewa sehemu tu ya Neno, katika kazi ya kuijenga upya Madhabahu ya Bwana iliyoharibiwa na Wakatoliki.

  Hatua ya pili ya Kanisa ni hapo hilo kundi lililo Hesabiwa Haki, sasa likipelekwa mbele zaidi katika Kutakaswa. Mjumbe wa Neno hilo la Utakaso akiwa ni John Wesley. Huyu ndiye aliyeibeba ile Sauti, akiwahubiri Walutheri na kuwaingiza katika maisha safi. Neno likiwaondolea uchafu woote kati yao, sigara, pombe, uzinzi, uasherati, nk. Hawa ndio haya makundi ya Wamethodist na wengineo unaowaona leo hii. Pia Wesley hakuwa nabii bali mwana Matengenezo.

  Kutoka katika kundi hili, kakawepo kakundi kadogo ambako kalijitazama katika kioo cha Neno na kujiona kanastahili sawa na ndugu zao walioipokea Injili ya mitume! Kwahiyo kakundi hako kakaisubiri Ahadi ya Ubatizo wa RM pia, maana ni stahili yake!!! Hako ndiko kakundi ka wale waliohesabiwa Haki na kisha Kutakaswa, sasa Mungu akiwatimizia kulingana na alichokiahidi katika Neno lake, akawashushia Roho Wake, nao wakapokea na vipawa!

  Basi hata leo hii makundi ya Kipentekoste yanajiwakilisha katika Neno kulingana na tukio hilo la Azusa, ambalo makundi hayo yalilitengenezea Fundisho la Kunena kwa Lugha! Pia ifahamike ya kwamba kuliendea tukio hilo la kihistoria, alikuwepo pastor William Seymour ambaye alilikamata ono hilo hata kulifikisha kundi hilo katika pinnacle ya Ahadi hiyo ya Mungu. Pia Seymour hakuwa nabii.

  Basi uyaangaliapo madhehebu yetu yoote, kwa kadiri utakavyo yarudisha katika Neno la Mungu, kulingana na programu ya Wokovu, yote ni lazima yaangukie katika mojawapo ya nafasi hizo tatu. Hizo nafasi tatu ndizo zilizofunikwa kwa Neema ya Wokovu. Yaani humo katika hizo hatua limo Neno liokoalo, ambalo kwalo mtu alipokeaye ndani yake mchakato wa kuzaliwa mara ya pili huanza na kuendelea, kama package! Na katika hatua zote tatu, Mungu hakumsimamisha nabii!!

  Basi, kwa kifupi, unapomuona Mpentekoste leo hii, basi jua kuwa huyo ni yule Mkatoliki aliyefufuliwa kwa ile Sauti ya Kuhesabiwa Haki kwa Imani, kisha akaipokea Sauti iliyomuitia Utakaso, na mwisho Ubatizo wa RM uliomkirimu vipawa! Mlutheri, ni yule aliyekwamia katika hatua ya Kuhesabiwa Haki, yaliyoendelea mbele, hayajui; hajui chochote kuhusu utakaso, yeye anaendelea na sigara zake! Naye Mmethodist ni yule aliyekwamia katika hatua ya Utakaso, hawakuendelea mbele kuvipokea vipawa, kwahiyo akikukuta unamuombea mgonjwa, yeye hujua una mizimu!!!

  Kwahiyo, Upentekoste ndio hatua ya mwisho ya Kanisa. Hakuna tena hatua nyingine kwa kanisa zaidi ya hiyo. Upentekoste ndio mwisho, kinachofuatia kwa Kanisa ni urejesho wa Neno Kamili, mafundisho potofu yakitolewa na kutupwa huko nje, ili kulirudisha Kanisa katika Imani Halisi inayoambatana na Neno, kama walivyolifundisha mitume!

  Katika hatua hii ya Urejesho, inayoambatana na Kunyakuliwa kwa Kanisa, Katika kulileta Neno Kamili, kulingana na utaratibu wa Mungu, ni lazima amsimamishe nabii, maana huyu ndiye humuwakilisha Mungu kikamilifu, naye huja na “Bwana Asema”, lile Neno, sio tena sehemu ya Neno bali Neno Kamili hilo liwezalo kuumba Imani ya Kunyakuliwa ndani ya muaminio. Ndio maana kuna Ahadi ya kusimamishwa nabii ili arejeze yote yaliyopotoshwa na kulifunga Neno lililo kamili kabla ya ile Siku ya Kuogofya ulimwengu unayoiendea.

  Basi tukiwa tunaishi mwisho wa wakati, huko ambako kuna Ahadi ya nabii, ndipo Shetani kwa kuyasoma Maandiko naye analifahamu hilo. Hivyo basi, licha ya Ahadi kwa Kanisa ya kuletewa nabii, Shetani naye ameruhusiwa kuwainua manabii wake katika kipindi hiki, Mt 24:24 hao manabii wa uongo. Ndio huu mfumuko wa manabii wanaohudumu nje ya zile milki 3 nilizokutajieni. Ni huduma zisizo na rejea yoyote katika programu ya Wokovu, hazina msingi wowote ule. Kwahiyo ndani ya Huduma hizo huwezi kulipata Neno lenye Upako wa Kuokoa zaidi ya miujiza na upako wake wa kujikusanyia mali na mafanikio mengine ikiwa ni pamoja na Kuvunja Laana za mababu na mambo ya jinsi hiyo ambayo kiuhalisi hupatikana. Lakini kuhusu Neno, hilo hawajui hata kuwa ndio nini!!!

  Mnaona, hatua ya kwanza mnayoweza kuitumia kuzipima hizi Huduma ndio hii, kwamba wamesimamishwa kuwa manabii kwa jambo gani kulingana na hatua liliposimama Kanisa katika Upentekoste, ambao kimsingi wamesheheni vipawa vyoooote, maana nguo uliyonayo sandukuni bado ni ya kwako, kwahiyo akiibuka mtu na kuitukuza nguo hiyo ambayo nawe unayo, si una haki ya kumwambia niondolee kelele hapa!

  Basi ndio kusema, huduma zooote za kinabii zilizo simama leo hii, ziko nje ya Upentekoste ingawa zinaonekana hivyo kwa jicho lisilo na ujuzi wa Neno, kwani Upentekoste haukusimamishwa kwa Neno la kinabii, bali huo ni kipeo cha matengenezo ya madhabahu ya Bwana, ambapo juu yake, i tayari sasa kuipokea sadaka, ibada iliyokamili. Yaani juu ya madhabahu ya Kipentekoste ndipo nabii anainuliwa ili kulikamilisha Neno, hilo libebalo ibada, ile Injili safi ya mitume inayobeba manukato safi, humo ndani liko jina moja tu, la Bwana Yesu Kristo, Hiyo ndiyo Ibada anayoisubiri Mungu!

  Lakini kinyume cha jambo hilo, haya mahuduma yoote ni maroho yadanganyayo, hayana jambo lolote yanalofundisha zaidi ya miujiza na uinjilisti wa kawaida hapo inapowabidi kusoma Biblia. Maelezo yao mengi ni ubabaishaji wa dini, wenye nukuu zisizolingana na maudhui ya wanacho kifundisha, zaidi ya kuutengua ufahamu wako. LAKINI, wanao Upako wa kuzikamata nafsi ziangamiazo, pia huwashawishi na wengine ambao majuto yanawasubiri!

  Huduma hizi zinajumuisha na makanisa kama ya Siloamu na utitiri wa makanisa mengine yanayoongozwa na “mitume na manabii” hapa kwetu na ulimwenguni kote, pamoja na makundi kama ya “nabii” Ellen White. Hawa wote wako hapo kwa ajili ya kuukamilisha Wokovu, huduma zao zikiyahudumia makundi yanayoelekea huko kwenye maangamizo, ndipo ninyi mlioondoshwa katika njia hiyo kwa ile Neema iliyosambazwa katika zile hatua tatu, sasa mtakuwa na wimbo wa kumwimbia Mwanakondoo aliyeshinda!!

  Ngoja nikomee hapo kwa leo!

  Ck Lwembe

 166. Hii inasikitisha sana, yaani kumbe hilo ndio chimbuko la injili ya kizazi cha nne!

  Wote hao kuanzia huyo kiongozi wao wanahitaji kuijua Kweli ili wawekwe huru.

  Kama uongozi haujabadilika tokea walipoanza basi nina wasiwasi na usahihi na uimara wa msingi wao tokea hiyo 2003. Unajua hata kama msingi uko off by a few degrees jengo linapoanza siyo rahisi kugundua bali linapozidi kwenda juu basi kule kupinda kwa ukuta kunazidi kuwa dhahiri na ndivyo ilivyokuwa kwa hawa ndugu zetu na “ukuta umeonekana kupinda” hiyo 2008.

  Mungu awarehemu, awafungue macho yao ya rohoni wakapate kuiona kweli wapone.

  Patrick.

 167. Ndg zangu, nami imenishtua kikweli juu ya misingi yao, naam, sijui, labda mimi ndo sina elimu, hata hivyo, tumsubiri D.C. BEZZA, maana, ameahidi kuja baadaye, lkn pia, nina hoja ya kuhoji, haswa pale kwenye UASISI. Nimewahi kumsikia mtumishi Mtume na Nabii Mwingira akielezea juu ya historia ya uanzilisho wa Efatha Ministry, tangu nadhani, 1997, lkn, AKISIKITIKA kuwa, baadhi alioasisi nao hiyo huduma, walipokonywa na shetani baadaye, lkn, asiwataje majina, ila, nalikuja kusikia wkt ffulani kwa baadhi ya washirika mule Efatha ya kuwa, huyo, aliyedakwa na shetani na kwenda kuanzisha huduma yake ni huyo Munuo, sasa, ktk ile namba moja uliyoi mention, kuonyesha alibadili muelekeo toka 2003, ndicho kielelezo chenyewe yasemekana. Sasa, ninaomba msaada hapo, je, yeyote ajuaye aweza kunithibitishia haya??? Nimeuliza hilo kwakuwa, hitoria hapo yasema kuwa alianza vizuri sana kabla ya kupotoka baadaye. Mubarikiwe. Oguda J.E.

 168. Mmmh! Kwa kweli mimi mwenyewe mwanzoni nilikuwa nikijua Pool of Siloam ni kama makanisa mengine ya Kiroho. Ila nilipokuja kupewa maelezo na mmoja wa Waumini wanaosali huko nilishangaa sana.. Any way, Ngoja tusubiri maelezo ya wahusika wenyewe..

 169. Mh haya nayo makubwa jamani na ndiyo kwanza nayaona tangu nizaliwe.Kumbe kuna mambo mengi yanaendelea ndani ya kanisa bila kufahamu.Huu si ushirikina wa kiroho jamani????????//

 170. Bwana Yesu apewe sifa ndugu yangu Bazaleli,

  Umetoa ufafanuzi na sijataka kuusoama wote kwa sababu kuna maneno ambayo siyo ya Mkristo lakini hata hivyo kuna vipengele vingi ambavyo ungewaelimisha watu ili wajue msingi wa huduma hii. Mojawapo ya vipengele hivyo ni hiki hapa namba nane. Naomba ufafanuzi kama ni kweli au uongo na inakuwagaje, naomba kuujua ukweli ili niwe huru.

  8. Wanapomfanyia Deliverance mtu (mmoja wa wahudumu – huingiwa na pepo/mzimu ambao unamsumbua anayeombewa na kumweleza kilichokuwa kinamfunga). Biblically, mtu mwenye pepo/mizimu yeye ndiye hupagawa na kuongea, kisha huamuriwa kutoka ndani ya mtu.

  Rev. Damasus F. Mkenda

 171. This is new theology from our fellows,nabii unapotoa unabii usitimie,umekwisha tena wewe ni nabii wa uongo,watu wengi wameshindwa kutambua sauti ya Mungu,look saul three times,anatafakari,anapembua,ili apate uhakika,siku hizi mtu akiota ndoto siku moja,Mungu kazungumza nami,is it?kumbe that dream cames from lot of activities,Nabii na mtume,we unacheza na jina mtume,look paul,we ukizunguka vi mikoa vitatu we mtume,tena ukiwalemea watu,paul alishona mahema kupata pesa ya safari sometimes.Nabii we look Eliah,no afraid aliwapa ukweli hata wafalme,we umepeleka ujumbe mara ngapi kwa Rais?je kwa nchi?mbona magorofa yanaanguka ulikuwa wapi?sasa ndo haya zinaibuka doctrines za ajabu ajabu tu,kila kipindi ambacho kanisa limepitia kinaonekana kwa macho ya kiroho na kimwili pia,mimi ukiniambia tofauti ya machi na sasa au mwaka jana ili nipate kugawa sesson sipati msingi wake,doctrine zote ulizoziweka hapo juu is nonsense.Msilipotoshe kanisa kwa mafundisho ya uongo wanasoloam

 172. Kachumbari tu hii::

  Kanisa la SILOAM si Dini wala dhehebu, Limefunuliwa si kwa Mapenzi ya mtu yoyote, Bali Kwa Mapenzi ya MUNGU. (Yoh 1:13-14).

  Ufanyeni mti kuwa Mzuri na Matunda yake kuwa mazuri hali kadhalika ufanyeni mti kuwa Mbaya na Matunda yake kuwa Mabaya. (Mathayo 12:13), mtawatambua kwa Matunda yao, kila mti mwema huzaa matunda mazuri.,mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya.Kila ayafanyaye Mapenzi ya Baba ndiye ataingia katika ufalme wa MUNGU, si kila alitajaye jina la BABA.( Mathayo 7:16).

  Huo mti mzuri uzaao matunda mazuri ni mimi na wewe (OGUDA) kama unazaa kama unamatunda ,onyesha umezaa nini au unalitajataja BURE tu jina la Baba kwa MOYO usio na NAFSI hai…(Isaya 61:-)

  KANISA la SILOAM ( Bwawa la Siloam, unawe uso wako nawe utaona). Mahali alipopachagua Bwana ,elekezeni nyuso zenu hapo. ( Kumb 12:5).

  KILICHOKUWA NDANI YA GARI KINASABABISHA GARI HIYO IITWE JINA: gari la Rais, Gari la Taka, Gari la wagonjwa, Gari la Polisi. Lakini Gari ni gari tu.

  KILICHO NDANI ya MOYO husababisha mwenye MOYO azae matunda mazuri au Mabaya..

  UNACHOSEMA ndicho kilichoujaa MOYO wako,

  MOYO wa UMBEA- umbeya
  MOYO wa Uongo-uongo
  MOYO wa Mwilini-Nafsi ya Mwili
  MOYO wa Ukabila-ukabila
  MOYO wa Lugha -Lugha na jamaa na Mapokeo
  MOYO wa Ukoo- Mapenzi yako mwenyewe.

  Warumi 8:5 waufuatao mwili huyafanya mambo ya ufalme wa Mwilini.

  Moyo wa asili (1 kor 2:14) hauwezi kuyapokea Mambo ya MUNGU wala hauwezi kuyafahamu kwa KUWA yanatambulikana kwa Jinsi ya ROHONI.

  (DINI na chochote kilichowahi kuwa Kabla ya YESU KRISTO na Adamu wa Kwanza siyo cha MUNGU mahali ambapo hapakuwa na Nafsi hai.YESU alipokelewa na DINI wakamuua:NI MOYO usiyoyafanya Mapenzi ya MUNGU-

  Moyo wa dini, dhehebu,Nchi,Kabila,Taifa,Malalamiko,Lugha,Kukumbuka mambo yaliyopita,Ufahamu wa Dunia,Akiba mbaya,Usio na Nafsi ya MUNGU, kando ya njia,hofu,mashaka,Nabii wa Uongo,Nabii Mzee,Madanganyo matupu,Mapokeo.

  NI MOYO WA UPENDO ni MOYO WA UDHIHIRISHO wa NGUVU za MUNGU ambao unakupa :
  -FURAHA
  -AMANI

  Unapatikana katika 1 KOR 2:6-10 ndiyo moyo unaosababisha :
  _Matengenezo
  -marejesho
  -Uponyaji
  -Utumishi
  -kuwapenda wengine
  -kuwahudumia wengine
  -kujenga
  -kupatanisha.

  USIIACHE AKILI YAKO IWAZE HOVYO NA KUZURURA HOVYO KAMA BILINGISHA MAVI, mdudu anaye kokota uchafu popote akiuona kuzurura nao popote alipo na UCHAFU anao.

  Asante kwa Kachumbari hii, ikuweke vizuri kulijua KANISA…

  Bezaleli DC.

  Mwana wa MUNGU kizazi cha nne.

 173. Duuu!! Ha aha aaa!! Kumbe ningekuwa huko mie hata jina langu Nzala jamaa angelibadilisha eee!!
  nzala

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s