Kuomba kwa muda mrefu!

maombi

Natamani kuomba kwa muda mrefu nifanyeje? pia natamani kuisikia sauti ya Mungu napo nifanyeje?

Erick kwizela

Advertisements

21 thoughts on “Kuomba kwa muda mrefu!

 1. Ndugu tambua ya kuwa Mungu huweza mambo yote tena Mungu hupa kila mmoja kipawa ka diri ya mtu aombavyo hivyo Mungu akutane na haja ya moyo wa zingatia kusoma neno la uzima kwa bidii,Mungu ameahidi hivi Isaya 43:26
  Ubarikiwe na Bwana

 2. Hongera kaka kwa huo msukumo uliopo ndani ya moyo..! Kwa hatua hiyo fahamu kuwa huyo ni Mungu anataka ufike hiyo “stage”.! Sijajua ni staili gani unayoitumia unapoomba yaani unapoomba huwa unakaa,unapiga magoti,au unasimama na nyinginezo…! Lakini nikushauri tafuta muda mahali ambapo pana nafasi tena unapoomba tumia njia ya kutembeatembea hapo ulipo…! Ucjaribu kutumia hisia zako na kufikiri kuwa labda kwa staili hii Mungu hawez kusikia maombi yako…la hasha..!

 3. Habari wapendwa ktk Bwana, Naombeni maombi yenu MUNGU anisaidie kufanikisha malengo yangu kielimu, azidi kuyanyoosha mapito yangu kama ninavyo tarajia. Namini MUNGU atajidhihirisha ktk hilo

 4. Ameen Michael,ndilo jambo nalo lifanya naanza kuon mabadiliko, Mungu akubariki sana

 5. NAKUSALIMU KWA JINA LA YESU.
  Nina kuomba upitie mafunzo ya Mwl. Mgisa Mtebe yaliyomo kwenye Blog yetu (NAMNA YA KUOMBA)
  Nimejifunza kuomba kwa muda mrefu kupitia hayo mafunzo.
  MUNGU AKUBARIKI SANA.
  AMEN

 6. Mwangomo N, m ungu akubariki mno kwa maelekezo mazuri ulonipatia.naamini nitafikia kiwango kile nilochokuwa natamani kukifikia.barikiwa sana

 7. Panua wigo wako wa kuombea mambo,utaomba tu kwa mda mrefu Isaya 54:1-20
  mfano
  @Nenda mbele za KuMungu kwa kusifu na kuabudi(zab 100:1-5)
  @mtukuze Mungu kwa uweza wake
  @Mtukuze Yesu kwa Ukombozi wake kwako
  @Roho Mtakatifu kwa kuwa na ushirika na wewe

  1. ombea familia yako(mama,baba,wadogo zako kaka/dada zako….nk)
  2. ofisi na wale wote unofanya nao kazi
  3. Kuna marafiki wanaitaji kumjua Yesu uliyenaye wapeleke mbele za Mungu ili Mungu ashughulike nao
  4.ombea maisha yako na mipango yako mbalimbali
  5……………….NK

  Mrudishie Mungu utukufu wake kwa kumshukuru
  Wakati unaombea hayo maeneo ingia ndani zaidi kwa kila unayemuombea au eneo unaloombea
  Ubarikiwe kwa KIU YAKO

 8. Kwanza Mungu akubariki sana kwakua hukutamani vya ulimwengu ila ulitamani kusema nakusikia kutoka kwa Mungu tamanio lizuri sana na huo nakuakikishia ndio mwanzo wa kukua kwako na kuomba hata kucha kwani Mungu atakupa tamanio la moyo wako…..Barikiwa sana

 9. M.J Siyi Mungu akubariki kwa ushauri mzuri,kw msaada wa Mungu yote ulonishauri nitayatendea kazi na jambo la muhimu ni mimi kujiepusha na dhambi ya aina yoyote mana hakuna Dhambi kubwa wala ndogo. barikiwa sana

 10. MABINZA L.S.Kwa uelewa wangu nikijua tabia yake,na lugha yake,na aina ya maomb ya nayo paswa kupelekwa kwake na amini shida yangu itakwisha.na kuhusu sauti ya Mungu tatizo langu ni kuzitofautisha kati ya sauti ya MUNGU NA YA ibilisi.katika yote ni kushukuru sana mana nimejifunza kitu kama nilicho jifunza kwa Mkandya,barikiwa

 11. Shalom,Mkandya nashukuru sana kwa maswali mazuri uloniuliza.kwa kweli nina kiu na shauku ya kuomba kwa mda mrefu nikijua kuwa ktk kuomba kwa mda mrefu nitakuwa zaidi karibu na Mungu,na kinacho patikana ktk kuomba kwa mda mfupi ndicho kipatikanacho ktk kuomba kwa mda mfupi.hATA HIVYO NIKUSHUKURU KWANI nimejifunza kitu hapa kuwa Kinachotakiwa ni nguvu ya Mungu niliyo nayo ndo itanipa kuomba kwa mda mrefu au mfupi kulingana na kile nilicho kibeba.BARIKIWA

 12. Erick,
  Kwanza, alichouliza Mkandya na mimi nakuuliza hivyo hivyo. Lakini nina swali la Nyongeza kwako; Wewe Erick ni kundi lipi kati ya haya mawili yafuatayo kwako, yanapaswa kutangulia kwako kuyajua kabla, iwapo una shida kubwa sana na unataka kumwambia Mtu mashuhuri ambaye unaamini au unafikiri kuwa akilipata tu ombi lako nawe shida yako imekwisha!:-

  1). Ni kujua tabia yake, Lugha yake na aina ya maombi yanayopaswa kupelekwa kwake?

  AU

  2). Kujua tu namna ya uwezo wake kiuchumi, hadhi yake na kumuomba tu kwa bidii?
  Nimekuuliza hivyo kwa sababu umesema kwamba licha ya kutaka uwezo wa kuomba kwa Muda mrefu, lakini na huyo Mungu ambaye angekujalia uwezo huo wa kuoma kwa muda mrefu, kumbe hata SAUTI YAKE HUIJUI! Ukijibu ndipo nitakushauri cha kufanya ambacho naamini ndicho bora.

 13. Erick umesema unataka kuisikia sauti ya Mungu.
  Jazwa Roho mtakatifu utaanza kuisikia sauti ya Mungu. Kitakachotakiwa tu baada ya kujazwa Roho mtakatifu ni wewe kujua kutofautisha sauti zingine na sauti ya Roho mtakatifu.
  Ubarikiwe.

 14. Erick Mungu akubariki kwa hiyo kiu uliyonayo.
  Lakini kabla sijakupa jibu kuhusu hili suala lako, ni vema nikakuuliza maswali pia:
  1. Kwa nini unataka kuomba muda mrefu?
  2. Kuna nini kinachopatikana katika kuomba muda mrefu ambacho hakipatikani katika kuomba muda mfupi?
  3. Unataka uombe kwa mfano masaa matatu mfululizo ukiwa unaombea nini?

  Nataka tu kukwambia kuwa kinachojalisha muda wako wa kuomba kuwa mrefu au mfupi ni kiwango cha nguvu ulichonacho ndani yako kulingana na ukubwa wa jambo unaloliombea.

  Kama una nguvu ya kutosha kutamka neno moja na jambo likatokea, kwa nini uombe muda mrefu? Na kama huna nguvu ya kulifanya jambo lifanyike mara moja kwa nini uombe masaa mengi?

  Na hiyo nguvu ninayosema ni ya Roho mtakatifu ambaye ndiye mwenye kujua uzito wa jambo unaloliombea na hivyo kukuongeza nguvu zaidi inayohitajika ili kufanya hilo jambo lifanyike. Huko ninakosema kukuongeza nguvu ni hali ya wewe kujisikia hamu ya/mzigo wa kuendelea kuomba unapokuwa uko kwenye maombi.

  Hivyo hauwezi ukaomba muda mrefu unaoutaka hata kama jambo unaloliombea linahitaji maombi ya muda murefu kama haujapokea nguvu za Roho mtakatifu ndani yako. Maana huyo ndiye chanzo cha hiyo nguvu ambayo unatakiwa kuwa nayo ndani yako.

  Kitu cha kwanza tafuta kujazwa Roho mt Erick.

 15. shalom…
  kwa uweza wa Mungu yote yawezekana.
  1. kua na ari / hamu ya kuomba, tamani sana kuzungumza na MUNGU
  2. unatakiwa uwe na ujazo wa roho mtakatifu ataeweza kukusaidia kuomba
  3. sasa ingia kwenye maombi kwa kuanza kutoa shukrani kwa mambo mbalimbali uliyotendewa na MUNGU
  4. fanya toba katika roho na kweli, omba utakaso wa damu ya Yesu, mweleze MUNGU dhambi zote ulizofanya ili akutakase.
  5.sasa peleka mahitaji yako mbele za baba yetu. mwite roho wa MUNGU (roho mt) akuongoze unapoingia katika kupeleka haja zako. mwambie we pekeyako huwezi bali yeye aonaye sirini akuongoze kwa yote.. hapo sasa utaona nguvu ya MUNGU ikikushukia kwa kasi ya ajabu na utapokea bubujiko moyoni mwako ambalo hujawahi pokea.
  halafu jitahidi kuomba katika roho, usitumie akili yako mwenyewe.,hapa mpe Roho mt nafasi kubwa ya kunena kwa lugha. japo waeza sali ktk roho kwa maneno ya kawaida ila ni yale ambayo roho mwenyewe anakupeleka.
  kwakufanya hivyo ndugu yangu masaa mawili yataisha na utaona kiu zaidi ya kuomba.
  na ili kufanya maombi ya muda mrefu pia nilazima uandae mazingira tulivu yasiyo na usumbufu wa hapa na pale na akili yako yote ielekeze mbinguni…
  haleluyah ushindi tuu
  BARIKIWA!

 16. Kwanza, muombe Mungu ili dhabi ikome maishani mwako.
  Pili, kuwa rafiki wa maandiko(Biblia) ukizifuatilia ahadi za Mungu-pray biblically
  Tatu, fanya kazi zake kwa uaminifu
  Nne, omba kutoka moyoni na kwa imani.
  Tano uwe na subira-uking’ang’aniza hapohapo, mashetani yatakufunika na kukugalagaza

 17. kuomba kwa muda mrefu ni hatua, inahitaji kujibidiisha katika kuomba jitahidi kuhudhuria mikesha mbalimbali ya maombi na kila semina au huduma zinazoitaji maombi unawez kujihusisha ili kupanua wigo wa maombi. Jibidiishe katika kusoma neno na kuomba maana ktk kusoma neno ni rais sana kusikia sauti ya Mungu.zaidi ya yote ishi maisha Matakatifu ujitenge na dhambi. isaya 58:9,Yohana 10:3-4.Barikiwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s