Kwetu ni Kuzuri.

kwetunipazuri

Shalom SG,

Kati ya vitu vinavyoleta bubujiko la raha nafsini na utoshelevu wa kiakili na kimwili, ni mtu kua na KWAKE. Tafakari watu tunavyokazana kukopa mikopo bank, saccoss, kubana/kubajeti mishahara au kipato kutokana na biashara, kuchakarika huku na kule ktk shughuli za ujasiriamali, hata wengine kuuza vitu vyao ili mradi wapate viwanja na hatimaye kujenga nyumba ili mtu awe na KWAKE. Ni baraka ya ajabu na tamu sana  kutua mzigo mzito wa kulipa kodi na majaribu ya hatari kabisa ya kupanga ambayo naweza andika kitabu kwa habari ya masahibu mimi na marafiki zangu tunayo/tuliyopiti. Adha ya kupanga na kutokua na kwako ni kubwa na inatesa na kwakweli umchochea kila mmoja kumtaka sana Bwana, ikibidi asababishe shimo tu litokezee ghafla njiani unapotembea halafu humo kuwepo dhahabu/almasi/tanzanite(jiwe moja tu)- yaani kama muujiza wa samaki mmoja tu aliyeibuka akiwa mdomoni mwake na shekeli ya kulipa kodi ya Bwana na Petro.. Katika yote, tunapojua kua hatima yetu ni dhahiri kwa maana ya maisha baada ya kufa au kunyakuliwa yatakuawaje/wapi na mahali tunakokwenda, twatiwa moyo sana kuyaishi maisha haya ya uchaji na kujitesa/nyima/kubeba msalaba hata  ije mvua,moto, jua, tuna uhakika tutakuaje baada ya maisha haya na kua tunajua tunaenda KWETU, ni baraka kweli kua TUNA KWETU, na ukimbizi haupo.

Katika maandiko yafuatayo, karibu ufurahi na kutiwa moyo nami kufahamu kua ni ajabu Yesu na kisha Roho Mtakatifu, walichukua muda wa kutosha kabisa kuwahakikishia watoto wa Mungu swala la kua na KWAO na hata kuelezea jinsi KWAO/KWETU kulivyo kuzuri kupita maelezo. Inakua kama Yesu alijua tamaa/hamu/furaha/ shauku/sherehe/bubujiko la moyo na nafsi mtu anapokua na kwao au akahakikishiwa kua hasiwe na wasi kwa kua baada ya yote, kuna makaazi yameandaliwa kwa ajili yake. Na pia kwa RM kuelezea namna hata Mji/Kwetu kulivyojengwa na madini/materials zilizotumika na yaliyomo umo ktk Mji, namuona ROHO MTAKATIFU NI KAMA ANATUAMBIA…..COME ON SONS AND DAUGHTERS OF GOD, PRESS ON, YOU DON’T WANNA MISS ARRIVING IN/AT THIS HOME/CITY/HOUSE/PLACE….

Yohana.14:1-3..Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makaoNa nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo (KJV…In my Father’s house are many mansions: if it were not so, I would have told you. I go to prepare a place for you). Inakua kama Yesu ali-note huzuni fulani, kushuka moyo kwa aina fulani kwa wanafunzi wake ndiposa kuanza na..”Msifadhaike mioyoni mwenu’’…( sawa na kusema..Relax guys..dont worry, don’t mind ok…I know what I am doing/talking/thinking about you..)  for kwa Baba kuna nafasi za kutosha. Halafu naguswa sana na integrity ya Bwana, ni Mkweli kwa dhati ya moyo maana anawaambia kama kwa Baba kungekua hakuja kaa vema/hakuna chance, ofcoz nisingepoteza muda wenu au kua muongo, ningewaambia straight ukweli bila kulemba..ila sasa nakwenda kuwandalia makao (kwa kua kuna nafasi nyingi kwa Baba..you… lovely friends of mine are special, you deserve specially prepared place kati ya izo nafasi nyingi zilizopo kwa Baba). Lakini kuna kingine kimenibariki sana nilipotafakari kikaniji,  embu fikiri Obama/JK wengekuambia kua wanakwenda kukufanyia jambo fulani! ooh my God, sijui kama ningelala siku iyo lakini sasa hapa ni Master Yesu mwenyewe anasema kua anakwenda kutuandalia makao (ofcoz hata kama atatuma malaika kufanya kazi iyo lakini uwe na uhakika kua usimamizi/monitoring ya smart Jesus ni strictly perfect, no mistake ever, ili ahadi aliyoitoa iwe kweli kwa kua ni mtu wa integrity, He says what He means and means what He says.

Besides, ni blessings to think this way too …Ktk Kiingereza mstari huu.. ‘’Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi …nakwenda kuwaandalia makao unasomeka… In my Father’s house are many mansions….I go to prepare a place for you), note My Father’s HOUSE kuna many MANSIONS. Makao/makaazi wanayokaa/ishi Watu hua yana majina mbalimbali kama ‘majumba’, ‘mehekalu’, ‘mabangaloo’, ‘mamansheni’ , ‘jumba’, ‘nyumba’, ‘ghorofa’, ‘kibanda’ nk. Maana ya ‘’Mansion’ ni –a very large, impressive orstately residence, manor house, or a large building with many apartments na ‘Bungalow’a one-storied house with a low-pitched roof;also  a house having one and a half stories and usually a front porch na  ‘House’ ni a building in which people live; residence for human beings..a household. Kwa maana izo inaonekana ‘House’ ni makaazi/makao ndogo kulinganisha na mamansheni au bangaloo…Lakini Yesu alisema katika NYUMBA/HOUSE ya Baba kuna mamansheni mengi thus, nashawishika kusema iyo nyumba ya Baba yetu si ya kawaida na haipo definition yake ktk kamuzi izo za wanadamu kwakua NYUMBA( ambayo ni ni ndogo kwa dhana za hapo juu) yet ndio yenye kua na ‘mamansheni tena mengi’…HAKIKA IYO NYUMBA YA BABA YATISHA KAMA NINI KWA UKUBWA maana inazidi MABANGALOO, MAMANSHENI, MAJUMBA ,JUMBA, MAGOROFA, MAHEKALU..nk

Ufunuo.21:1-25…1  Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya….. 2  Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe…(soma mistari iyobaki)

Kwa kweli KWETU kuzuri..angalia sifa zake 13 zifuatazo kwa mujibu wa anadiko ilo:1-Umepambwa, 2-Una utukufu wa Mungu, 3- Mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri, 4- Ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli, 5- Ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.6- Mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake..ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa, ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika, 7- Ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi, 8- Misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna, Msingi wa kwanza ulikuwayaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;  wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto, 10- Milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja, 11- Njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu, 12- Mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo, 13- Milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. Embu piga picha tu ya city/town lenye madhali iyo na fikiri vito vya thamani vilivyopamba ukuta wa mji ktk sifa no.8…angalia/soma kwa makini vito ivyo, ni ajabu sana wandugu. Tukazane TUFANYE KAZI ZAKE KISHA twendeni KWETU, NI KUZURI MNO, BWANA ANATUPENDA NA KUTUTHAMINI KWELI NA MUNGU AMEPENDA TUISHI NAYE PAMOJA NYUMBANI KWAKE/KTK MJI WAKE ndio maana amesema sisi ni wenyeji nyumbani mwake Waf. 2:19 nani uzao mteule, ukuhani mtukufu, taifa takatifu, watu pekee wa Mungu tulioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyetuita kutoka gizani na kutuingiza katika nuru yake ya ajabu1Petro.2:9.

Songa mbele, Kwenu/kwetu kuzuri/kupo, hamna shaka,ametupenda upeo.

–Edwin Seleli

Advertisements

3 thoughts on “Kwetu ni Kuzuri.

  1. Siyi Michael , Amen.

    Yapi maswali hayo kwa hii text? maana hujauliza swali lolote zaidi ya kunibariki!

  2. Ubarikiwe kwa text nzuri Seleli. Tatizo lako huwa haujibu maswali ya watu, hasa yale magumu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s