Tuitafsiri 666

666

Leo nilikuwa nasoma mtandaoni juu ya kupitishwa kwa mswada wa Afya wa Rais Obama wa USA kuwa sheria ikanilazimu kusoma tena Ufunuo 13: 15 – 18 ili kuona kama unabii wa huo wa Yohana ndiyo huu wa sasa USA?. Hebu soma kwanza habari yenyewe nimejaribu kuitafsiri hapa kama ifuatavyo;

“Namba 666 = ni alama ya MPINGA KRISTO (Soma Ufunuo wa Yohana). Bunge la Marekani limepitisha Mpango wa Afya wa rais Obama kuwa sheria. Utekelezaji wake utaanza tarehe 23/03/ 2013. Sheria hii itahitaji Wamarekani wote kupandikizwa Kifaa cha mawimbi ya redio (Radio Frequency Identification (RFID) chip) ili kunufaika na mpango huu wa afya na kupata dawa. Kifaa hicho kitawekwa kwenye paji la uso au kwenye mkono na kitaunganishwa na akaunti za benki za raia mhusika.”

Jambo hili kwa [maoni yangu] linatimiza unabii uliomo katika kitabu cha Ufunuo 13:15-18 kuhusiana na ALAMA YA MNYAMA! Mwenzangu bado unatilia mashaka juu ya NYAKATI ZA MWISHO? KAA TAYARI! Wakati wa mavuno u karibu sana! Ufunuo 13 nadhani umeanza kuonekana wazi mbele yetu [Marekani si mbali]. Ingawa nadhani wengi hatujapata habari hizi na hata zitakapokuja rasmi pengine hatutajishughulisha kujiuliza maswali haya;

1. Kwa nini hiki kifaa kiwekwe kwenye maeneo yaleyale ya mwili ambayo Biblia imeonyesha kupitia Ufunuo. Kwa nini kifaa kiwekwe kwenye paji la uso au mkononi na siyo mahali pengine?

2. Kwa nini kifaa hicho cha mawimbi kiunganishwe na akaunti yako ya benki? Kumbuka Biblia inasema hautanunua wala kuuza bila kuwa na alama hiyo ya mnyama [asomaye na afahamu]. Na hebu fikiria kwa nini hicho kifaa kiwe na taarifa zako za fedha. Kinachoniumiza moyo ni kuwa watu wengi ndani ya makanisa wanadhani zile nyakati zingali bado sana na Yesu akija sasa wengi wetu tutaangamia? Najua wengi hapa tutasema ni maendeleo ya kiteknolojia lakini si vibaya tukihusisha na maandiko kisha tukajitathmini Je! Sisi tuko wapi leo.

–Moses

Advertisements

24 thoughts on “Tuitafsiri 666

 1. Wingu la mashaidi wa Kristo, pole sana.

  Lakini ukweli ni kwamba mlipigwa viboko na kuwekwa mahabusu kwa sababu ya ujinga wenu.
  Ukweli ni kwamba hata Yesu hakusema kuwa sisi tuitwe wakristo, bali ni watu pale Antiokia ndo walianza kuwaita wa-kristo wale watu waliomwamini Yesu. Kumbuka kuna wengine walikuwa wanawaita ‘wa njia ile’.

  Yawezekana kabisa tungeweza hata kuitwa wayesu, au vyovyote.

  Haibadilishi chochote wewe mbele za Mungu kusema dhehebu lako kama ni msabato, mpentekote, mrutheri, n.k. au kutokusema.
  Msingi wa Mungu ulio imara ni kwamba Mungu awajua walio wake, haijalishi kama wanasema madhehebu yao au la. Na katika hali ilivyo ya mambo ya kisheria na za serikali mbalimbali duniani huwezi kuepuka kuwa kwenye dhehebu fulani.

  Lakini pia mnavyotafsiri hiyo namba 666 ni kimawazo ya binadamu sana, ati kwamba kila anaposemwa mwanamke katika biblia inamaanisha kanisa. Just kwa sababu kanisa ni bibiharusi wa kristo?

  Haya Obama huyo hapo anamaliza muda wake, na wala hatujawekewa hiyo chip?

 2. CHAPA YA MNYAMA

  Ndugu William Branham alifundisha sana, kuhusu chapa ya mnyama, alisema kuwa kuipokea chapa ya mnyama ni kuukataa muhuri wa Mungu ambao ni Roho Mtakatifu, alisema kuna pande mbili tu, upande wa Mungu na upande wa shetani, hivyo ukikosa kuwa na Roho wa Mungu, maana yake ni una roho ya shetani ambayo ndio chapa ya mnyama.

  Kwahiyo roho ya mpinga kristo ambayo ndani yake imebeba chapa ya mnyama iliyozungumziwa kwenye kitabu cha Ufunuo 17:

  “1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi.
  2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
  3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
  4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
  5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
  6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”

  Hapa tunamwona mwanamke aliyeketi juu ya mnyama mwekundu sana, na juu ya paji la uso wake, alikuwa na jina limeandikwa la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI.

  Huyu mwanamke anayezungumziwa katika sura hii, ni kanisa fulani kwasababu mwanamke siku zote katika biblia anawakilisha kanisa na pia mwanamke huyu tunaona anaitwa mama wa makahaba, kwahiyo ni kanisa-kahaba mama, ikiwa ni mama basi ana mabinti, na hao mabinti ni makahaba kama mama yao. Kwahiyo kahaba ni mwanamke anayezini na wanaume wengi mbali na mume wake. Na tunaona kuwa kanisa pekee lililofanya uasherati kwa kuchanganya mafundisho ya Mungu na mafundisho ya kipagani ni kanisa Katoliki, kwahiyo yule mama wa makahaba aliyezungumziwa pale ni kanisa Katoliki, Na wale mabinti ni madhehebu mengine yote ya dini yaliyobakia, yaliyoacha uongozi wa Roho Mtakatifu na kuiga desturi zile zile za kipagani kama za mama yao kahaba yaani kanisa katoliki. Na sasa hivi tunaona madhehebu yote ulimwenguni na dini zote ulimwenguni zinaungana, pamoja na mama yao kahaba katoliki (ecumenical council) na kuiunda ile chapa ya mnyama. CHAPA YA MNYAMA INATENDA KAZI KWA NAMNA MBILI:

  Kwahiyo chapa ya mnyama ipo rohoni na mwilini, (nje na ndani). Na NDANI ni kwa mtu ambaye hana Roho Mtakatifu. Mtu huyo ameshaipokea ile chapa ya mnyama. Kwahiyo ndugu tafuta kuwa na Roho wa Mungu angali muda upo, maana Biblia inasema huo ndio muhuri wa Mungu, soma (Waefeso 4:30) na kuipokea chapa ya mnyama kwa NJE ni kama upo au umejiunganisha na mifumo yote ya madhehebu ambayo yameuacha uongozi wa Roho Mtakatifu, na kuweka mifumo ya kipagani, pamoja na taratibu za kibinadamu na desturi zisizoendana na neno la Mungu.

  Hivyo kuipokea chapa ya mnyama ni kujishona na madhehebu na kuwa na utambulisho mwingine wowote zaidi ya ukristo mfano, kujiita Mlutheri, Mwanglikana, Msabato, Mbaptisti, Mkatoliki, Mbranhamite n.k. badala ya kujiita Mkristo. (kumbuka maana ya haya majina sio mbaya, lakini madhehebu ambayo yamebeba hayo majina yana ile chapa ya mnyama ndani yake kwasababu yameshafanya uasherati kama wa mama yao katoliki na Mungu ameyakataa (Ufunuo 3:1 Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.) Kwahiyo kwa kujiita tu hivyo tayari umeshakwisha kuikubali ile chapa bila ya wewe mwenyewe kujijua. Na nguvu ya hii chapa itakuja kujidhihirisha sana katika kipindi cha dhiki kuu, baada ya kanisa(bikira safi) kunyakuliwa.

  Kwahiyo hii chapa ya mnyama kwasasa ipo sana katika roho na watu wanaendelea kuipokea kwa kukosa Roho Mtakatifu, lakini kwa nje, ipo ila itakuja kutenda kazi kwa Nguvu katika kipindi cha dhiki kuu. pale Mpinga kristo atakaponyanyuka na kupewa mamlaka na ulimwengu mzima, na mpinga kristo atakuwa sio mwingine zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki wa Roma.

  Tunaweza tukaona leo hii, mambo mengi ya ajabu, yakitokea ulimwenguni ikiwemo vitendo vya kigaidi vikizidi kukithiri, amani inazidi kutoweka duniani,watu wanaishi kwa hofu za machafuko na vita, siasa na umoja wa mataifa umeshindwa kuihifadhi amani ya dunia, dunia inatafuta suluhisho la mambo hayo na bado hawajapata, hivyo mtu atakayeonekana ana uwezo wa kurejesha amani duniani atakuwa si mwingine bali ni papa. kama tunavyomwona leo hii anajulikana ulimwenguni kote kama mtu wa amani(MAN OF PEACE). Hivi karibuni tunaweza tukaona jinsi kiongozi huyu wa kanisa Katoliki (papa Francis), akirejesha mahusiano kati ya Marekani na Cuba, ambayo yalikuwa yamevunjika kwa muda mrefu. Leo analeta dini zote ulimwenguni pamoja, anakubalika na kuheshimika na watu wote, Ni kiongozi mwenye ufuasi mkubwa wa watu kushinda kiongozi yeyote ulimwenguni.

  Kwahiyo katika kipindi cha ile dhiki kuu baada ya kanisa kunyakuliwa, atakuja na wazo la kukomesha ugaidi na vitendo viovu duniani akitaka watu wote, wasajiliwe kulingana na madhehebu yao na mashirika yao ya dini, kwasababu vitendo vinavyosababisha amani kutoweka vinasababishwa na dini. kwahiyo ni lazima tatizo litatuliwe kwa namna ya kidini kwahiyo itahitaji kiongozi wa kidini na tunamwona si mwingine anayekidhi hivi vigezo zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki. Leo hii duniani vita vya kidini vimeiweka dunia katika mtazamo mpya, mfano mabomu ya kujitoa muhanga, na vikundi vya kigaidi, kama ISIS, Alqaeeda, Alshabaab, Boko haram n.k.vimekuwa ni tatizo sugu kwa dunia nzima. Hii itatimiza ule unabii wa Daniel 9:27 (Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja).

  Agano hili la amani litafurahiwa na dunia nzima, kwani litadhaniwa kuwa litaleta amani duniani, Hapa ndipo utakapowekwa utaratibu mpya wa ulimwengu (new world order). chini ya uongozi wa papa(Mpinga kristo) baada ya kupewa nguvu na mataifa yote duniani. Kumbuka shetani ananyanyua vikundi vya kuvunja amani na ugaidi duniani kama mbinu yake ya sasa ya kutafuta kuwaangamiza wakristo, kama alivyofanya kwa wakristo katika kanisa la kwanza chini ya utawala wa kirumi chini ya Nero (AD 64),ambapo wakristo wengi waliuawa baada ya kusingiziwa kuwa wameuchoma mji, na hali sio wao waliofanya hivyo. Kwa njia kama hiyo shetani anawatafuta wakristo awaangamize, kwa vitu vya kusingiziwa, maana anajua hakuna namna yeyote mkristo anaweza akashitakiwa na kuuawa kwa makosa yeyote ya kihalifu.

  Hivyo sasa hivi ameunyanyua ugaidi katika uislamu na vikundi vingine ili baadaye aweze kuwasingizia wakristo kuwa ndio magaidi na kuwaangamiza wote. Wakati huo watu wote, watapaswa wahakikiwe taarifa zao muhimu zinazohusiana na dini zao, itahusisha pia na kazi mtu anayofanya, kwenye makampuni, na mashirika. Kila mmoja ni lazima atambuliwe yeye ni dhehebu gani au dini gani katika shughuli anayoifanya kwa dhumuni la kuwapata watu wachafuaji wa amani duniani, kwamfano waislamu wenye itikadi kali, wanaojihusisha na vikundi vya kigaidi.pamoja na vikundi vya kihalifu vinavyohusisha vita vya kidini na mauaji ya kikatili ya watu. Lakini nia ya shetani itakuwa sio kuleta amani wala kuwalenga waislamu bali ni kuwalenga wakristo ambao hawatakubaliana na huo mfumo wa yule mnyama ambao ni muungano wa madhehebu na dini.

  Mpinga kristo ataleta mfumo huu kwa kisingizio cha kuleta utaratibu mpya wa dunia. Mtu hataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa asipokuwa na huo utambulisho, Hataruhusiwa kuabudu kwenye kanisa ambalo halijasajiliwa na muungano wa madhehebu, ndugu Branham alitabiri akasema itafika wakati haya makanisa tuliyonayo sasa yatafungwa yote. Kwahiyo usajili utaanza karibu Duniani kote, katika kila nyanja na kila taasisi, kwa waajiriwa na wasio waajiriwa, katika vitambulisho vya taifa, kura na serikalini na taasisi binafsi kama mabenki, ATM cards, VISA n.k. Itakuwa ni sheria kila raia lazima ahakiki taarifa zake za kidini, na huo mfumo mpya. Watu wengi wataukubali na kuupenda na kuhakiki taarifa zao pasipo kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama, na mfumo huo utafanikiwa kukamata wahalifu wengi.

  Ni wazi kuwa itakuwa ni ngumu kwa mtu kufanya biashara yeyote ya kuuza wala kununua wala kuajiriwa usipokuwa na huo utambulisho wa kidini. kwahiyo ukishahakiki taarifa zako za dini/dhehebu lako utakuwa huru kufanya shughuli yako yoyote unayotaka. Lakini sio kujiita mkristo tu ambaye hajulikani na dhehebu lolote. Lakini wakristo wale ambao hawakwenda kwenye unyakuo watamfahamu yule mpingakristo na chapa yake, watakataa kuupokea huo utambulisho na usajili wake (chapa ya mnyama). Sasa hao ndio watakaotafutwa na kuitwa magaidi, na hao tu ndio watakaopitia dhiki kuu wakati dunia inaendelea kufurahi. Na hawa hawatauliwa ovyo ovyo tu, kama inavyodhaniwa, bali watachukuliwa na serikali,(maana serikali itawatambua kama wahalifu na sio raia wa kawaida). maana hawatakuwa wengi, na watapelekwa kwenye magereza maalumu ya mateso ya siri (concentration camps), huko ndiko kutakuwa na kilio na kusaga meno kama Bwana YESU KRISTO alivyosema. Watateswa kama magaidi, watasingiziwa wao ndio wanaotoa amani ya dunia kama sivyo kwanini wakatae kusajiliwa, lazima kuna mambo ya siri wanayo. Watakataliwa na jamii nzima, hata ndugu za hao jamaa hawatawaelewa.

  Tunaona kama vile wayahudi walivyofanyiwa na Adolf Hitler katika vita ya pili ya dunia kwenye zile concentration camps. Watu jinsi walivyokuwa wakiuliwa kikatili na mateso makali yasiyoelezeka ndivyo itakavyokuwa tena na zaidi ya hapo katika wakati wa dhiki kuu kwa wale wakristo watakaobaki, mpinga kristo atawaua wote, (Na dhiki hii kuu itawahusisha na wayahudi pia) na itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu ya mwisho wa lile juma la 70 la Daniel. Na kwa mataifa yote yaliyobaki ambayo yamepokea ile chapa (kwa kuukubali mfumo na utambulisho wa yule mnyama). wataingia katika ile siku ya KUOGOFYA ya BWANA ambayo itaanza baada tu ya ile miaka mitatu na nusu kuisha(baada ya dhiki kuisha). Hapo ndipo hukumu ya mataifa itakapoanza!

  USHUHUDA WETU

  Kuna ushuhuda tungependa kukushirikisha kwa uhakika zaidi na uhalisia wa hili jambo.
  Sisi, Denis na Devis, mwezi wa 4 mwaka 2015, Tulipokuwa tunaishi kule kigamboni, mahali tulipokuwa tumepanga chumba tulikuwa na rafiki yetu muislamu, anaitwa Hussein. alikuwa yupo na mpenzi wake ambaye ni mkristo wanaishi pamoja, siku moja ya mkesha wa Pasaka, walituomba tuwasindikize kanisani kwenye mkesha wa maigizo ya pasaka. Hilo kanisa lilikuwa ni kanisa kubwa maarufu la katoliki. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku, hawakujua shortcut ya kufika pale kwahiyo walituomba sisi tuwapeleke kwasababu sisi tu ndio tulikuwa tunaifahamu shortcut ya kufika pale. Basi tulienda tukawafikisha hadi getini tukawaingiza ndani.

  Wakati sisi tumewaacha tunatoka nje getini Walinzi wa geti wakatusimamisha wakaanza kutuhoji, kwanini mnaondoka kabla ya ibada kuisha, sisi tukawaelezea tumewaleta tu ndugu zetu na kuondoka, hatujaja kwenye ibada.

  Kulikuwa na mmoja ambaye ni kiongozi wa kanisa lile mahali pale akaja karibu, akatuuliza nyie ni dhehebu gani? ..Tukamwambia sisi hatuna dhehebu sisi ni Wakristo. Kitendo cha sisi kusema tu vile, tuliwasha moto, wakaitana wengine, wakaanza kutushambulia kwa maneno mengi, nikizungumza yote hapa muda hautatosha. Tulikuwa tunajaribu kuwajibu kulingana na neno kuwa Ukristo sio madhehebu, bali ni kuamwamini YESU KRISTO. Lakini jinsi tulivyozidi kuwaeleza ndivyo walivyozidi kutushambulia na kutukasirikia.

  Kulikuwa na vijana wengine pale, wakawaachia wote wapate nafasi ya kutugeukia sisi. Walikuwa hawana nia nyingine bali kusikia kutoka katika vinywa vyetu sisi ni madhehebu gani lakini tulipokataa kufunua madhehebu bali Ukristo ndipo vita vilipoanza, saa hiyo hiyo tulipigwa pingu. Tukakalishwa chini, defender ya polisi ikaitwa, simu ilipigwa kituoni wakisema tumewakamata ma-alshababu, tukafikishwa kituoni, tukapigwa na makuni, mapigo mengi. Tukasingiziwa kwanini tumeiba, wakatutupa ndani gerezani, ile sehemu ilikuwa ni chafu sana, wafungwa kule, walidhani sisi ni magaidi wa ajabu kwajinsi tulivyokuwa tunapigwa,ile alfajiri walitudekisha lile gereza.

  Lakini Mungu alitupa neema asubuhi alfajiri sana tukatoka kule, hiyo siku tukio hilo lilipotokea ilikuwa ni siku ya kupatwa kwa mwezi, (maarufu kama Bloodmoon duniani), hiyo ilikuwa ni uthibitisho wa somo Mungu alilotufundisha.

  Baada ya kutoka ndio Mungu alituthibitishia hili somo. Jinsi wakristo watakavyopitia katika dhiki ile kuu. Kanisa Katoliki ndio linaloongoza kwa kuwaua na kutesa wakristo wengi, na inakadiriwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68 katika historia ya kanisa. Na ndivyo linavyofanya hata sasa kwa siri na litakavyokuja kufanya katika kile kipindi cha dhiki kuu ambacho kipo karibuni kuanza. Na ndio maana yule mwanamke aliyeonekana kwenye Ufunuo 17 alionekana amelewa kwa damu ya watakatifu. Kuna wakristo wengi wanaoteswa na kuuawa kwa siri duniani kote, kwa ajili tu wao ni wakristo na sio jambo lingine.

  Shetani hapendi kuona mtu anajiita MKRISTO, kama vile asivyopenda kuona watu wakibatizwa kwa jina la YESU KRISTO, na ndivyo asivyopenda kumwona mkristo anautambulisho wa asilia. Hakuna mahali popote mkristo katika Biblia alikuwa anajiita Mpaulo au Mpetro au M-yohana Mbatizaji, au M-eliya au M-Timotheo, Biblia inasema wote walikuwa wanaitwa wakristo.

  Kwahiyo utambulisho mwingine zaidi ya huo unatoka kwa shetani, na hiyo ndiyo chapa ya mnyama. Amina!

  KUHUSU 666.

  Papa akiwa kama kiongozi wa kanisa katoliki ana nembo katika enzi yake inayojulikana na kusomeka kama VICARIUS FILII DEI. Tafsiri yake kwa kiswahili ni BADALA YA MWANA WA MUNGU.

  Kwahiyo Papa kulingana na kanisa katoliki anasimama hapa duniani badala ya mwana wa Mungu, anauwezo kama vile, kusamehe dhambi, kubariki, na kusujudiwa n.k. Haya ni machukizo mbele za Mungu,. Na hesabu ya hilo jina, kwa kirumi ni 666.

  Kwahiyo kutiwa chapa katika mkono wa kuume au kwenye kipaji cha uso, ni kukubaliana na ule mfumo kichwani kwako,(hiyo ni kwenye kipaji cha uso) na kukubali kuutumia huo mfumo kama kitu cha kujipatia riziki au chakula (hiyo ni kwenye mkono wa kuume) tunafahamu kama vile mkono tunautumia kwa kula, kukubaliana na kitu, kusaini mikataba n,k kwa wale watakaokubali kuuza na kununua ndio watapokea hiyo chapa (666). Na wala sio kugongewa kichwani au mkononi.

  TAFUTA ROHO MTAKATIFU, EPUKA KAMBA NA UTAMBULISHO WA MADHEHEBU.

  Ukiulizwa wewe ni dhehebu gani, sema mimi ni mkristo usione haya Bwana Yesu alisema katika marko 8:3; (Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu) Uvae Ukristo umfuate Yesu usiuvae udhehebu utakupeleka jehanum.

  Bwana Yesu anasema mathayo 16:24-26 (Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake)!!

 3. NI JAMBO LA MAANA TENA LA MUHIMU KUKARIRI NA KUTAFAKALI KWAMBA MUNGU ANATAKA NINI KWETU? tambua kua Mungu anakupenda hapendi uangamie pamoja na shetani.

 4. ALAMA YA MNYAMA , IBADA NA KUSUJUDU

  ASILI YA IBADA ZOTE NI UUMBAJI,

  “KWA NINI MUNGU AZUNGUMZIE ADHABU JUU YA WALE WANAOSUJUDU NA KUPOKEA CHAPA YA MNYAMA YA MFALME YULE /MNYAMA (DANIEL 17:7).

  KWANINI SHIDA IWE KUMSUJUDU NA KUPOKEA CHAPA?

  “NA MWINGINE, MALAIKA WA TATU AKAWAFUATA, AKISEMA KWA SAUTI KUU MTU AWAYE YOTE AKIMSUJUDU HUYO MNYAMA NA SANAMU YAKE, NA KUIPOKEA CHAPA KATIKA KIPAJI CHA USO WAKE, AU KATIKA MKONO WAKE,YEYE NAYE ATAKUNYWA KATIKA MVINYO YA YA GADHABU YA MUNGU ILIYOTENGENEZWA, PASIPO KUCHANGANYWA NA MAJI,KATIKA KIKOMBE CHA HASIRA YAKE NAYE ATATESWA KWA MOTO NA KIBERITI KIBERITI MBELE YA MALAIKA WATAKATIFU, NA MBELE ZA MWANAKONDOO.”UFUNUO14: 9,10

  ZABURI 95:6
  “NJONI, TUABUDU, TUSUJUDU, TUPIGE MAGOTI MBELE ZA BWANA ALIYETUUMBA”

  ZABURI 81:9
  “USIWE NA MUNGU MGENI NDANI YAKO; WALA USIMSUJUDIE MUNGU MWINGINE.”

  UFUNUO 4:10-11
  “NDIPO HAO WAZEE ISHIRINI NA WANNE HUANGUA MBELE ZAKE YEYE AKETIYE JUU YA KILE KITI CHA ENZI, NAO HUMSUJUDIA YEYE ALIYE HAI HATA MILELE NA MILELE, NAO HUZITUPA TAJI ZAO MBELE YA KITI CHA ENZI WAKISEMA,
  “UMESTAHILI WEWE,BWANA WETU NA MUNGU WETU, KUUPOKEA UTUKUFU NA HESHIMA NA UWEZA; KWA KUWA WEWE NDIWE ULIYEVIUMBA VITU VYOTE, NA KWA SABABU YA MAPENZI YAKO VILIKUWAKO, NAVYO VIKAUMBWA.”

  KUSUJUDIWA HUSTAHILI,
  1.ALIYEUMBA NA
  2.ANAYEISHI MILELE

  “MSUJUDIENI YEYE ALIYEZIFANYA MBINGU NA NCHI NA BAHARI NA CHEMCHEMI ZA MAJI.” UFUNUO14:7

  ESTA 3:2
  “BALI MORDEKAI HAKUINAMA, WALA KUMSUJUDIA”

  ESTA 3:5
  “HATA HAMANI ALIPOONA YA KWAMBA MORDEKAI HAINAMI WALA KUMSUJUDIA, ALIGHADHIBIKA SANA”

  MATHAYO 4:10
  “..KWA MAANA IMEANDIKWA, MSUJUDIE BWANA MUNGU WAKO, UMWABUDU YEYE PEKE YAKE”

  HIVYO TUNAPASWA KUKIINAMIA NA KIKISUJUDIA KILE KILICHOTUUMBA TU.

  JIULIZE KATIKA ESTA 3:2 KWA NINI MORDEKAI HAKUINAMA KUMSUJUDIA KIONGOZI WA BABELI.

  JIULIZE:“KWA NINI MUNGU AZUNGUMZIE ADHABU JUU YA WALE WANAOMSUJUDU NA KUPOKEA CHAPA YA MNYAMA YA MFALME YULE /MNYAMA (DANIEL 17:7).

 5. SIFA YA YESU KUWA NA MOYO MMOJA NA MUNGU NDIO TABIA/NA SURA HALISI
  YA MUNGU YAANI KUYATENDA MAPENZI YA BABA YAKE YAANI KUFUATA MAAGIZO SI MACHUKIZO,

  “AMBACHO MWANA WA ADAMU ATAWAPA, KWA SABABU HUYO NDIYE ALIYETIWA MUHURI NA BABA YAANI, MUNGU” YOHANA 6:27

  KWA MAJIRANI ZETU KUWA NA ALAMA NYEUSI KATIKA PAJI LA USO KUNAKOTOKANA NA KUFANYA IBADA HUITA TAA

  NINI HASA TAA HALISI?

  “MAANA MAAGIZO HAYO NI TAA, NA SHERIA HIYO NI NURU,” MITHALI 6:23

  ILI MTU AITWE WA MUNGU AWEJE?
  “ILI WAENDE KATIKA AMRI ZANGU, NA KUYASHIKA MAAGIZO YANGU NA KUYATENDA; NAO WATAKUWA WATU WANGU, NAMI NITAKUWA MUNGU WAO.” EZEKIELI11:20

  IPI NI SURA YA MUNGU?
  SURA YA MUNGU NI UPENDO

  “YEYE ASIYEPENDA HAKUMJUA MUNGU, KWA MAANA MUNGU NI UPENDO.
  1 YOHANA 4:8

  SURA HII NDIYO MFANO WA MUNGU AMBAO ADAMU NA HAWA WALIUPOTEZA PAALE EDENI. AMBAYE KILA ANAYERUDISHA KUFANANA NA MUNGU NDIO HUTIWA MUHURI.

  NINI MAANA YA KUMPENDA MUNGU?

  “KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU, KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE.” 1 YOHANA 5:2

  KWA NINI WATU HAWA HAPA CHINI WATIWE MUHURI WA MUNGU?
  JIBU: KWA SABABU WAMECHUKIA DHAMBI,KAMA MUNGU ANAVYOCHUKIA DHAMBI. MAANA AMEJAA UPENDO

  “BWANA AKAMWAMBIA,PITA KATI YA MJI, KATI YA YERUSALEMU,UKATIE ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO VYA WATU WANAOUGUA NA KULIA KWA SABABU YA MACHUKIZO YOTE YANAYOFANYIKA KATI YAKE” EZEKIELI 9:4

 6. NDUGU WAPENDWA TUNAYE PIA ROHO AMBAYE KUPITIA YEYE ANATIA USHAWISHI KATIKA TABIA ZETU. NA TUNAPOKUWA NA TABIA HALISI YA KUCHUKIA DHAMBI NA KUTENDA MEMA. TUNAKUWA TUMERITHI SURA HALISI YA MUUMBAJI WETU.

  ROHO NI MTIAJI MUHURI WA MUNGU SOMA HAPA CHINI.

  WAEFESO 1:13
  “NANYI PIA KATIKA HUYO MMEKWISHA KULISIKIA NENO LA KWELI, HABARI NJEMA ZA WOKOVU WENU; TENA MMEKWISHA KUMWAMINI YEYE, NA KUTIWA MUHURI NA ROHO YULE WA AHADI ALIYE MTAKATIFU.

  ROHO WA MUNGU NDIYO NAYETUTIA MUHURI.

  WAEFESO 4:30
  “WALA MSIMHUZUNISHE YULE ROHO MTAKATIFU WA MUNGU; AMBAYE KWA YEYE MLITIWA MUHURI HATA SIKU YA UKOMBOZI.”

  TUSIMHUZUNISHE ROHO MTAKATIFU/KUASI

  ISAYA 63:10
  “LAKINI WAKAASI, WAKAMHUZUNISHA ROHO YAKE MTAKATIFU; KWA HIYO AKAWAGEUKIA, AKAWA ADUI, AKAPIGANA NAO.”

 7. Lenda,

  Hii, Kumbukumbu 4:6 inayosema:
  “Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.”

  Haya Maandiko uliyoyanukuu, yangali yana nguvu iliyokusudiwa kwa asilimia mia moja kwa wote ambao hawajafikiwa na wokovu. Hao ambao bado wako ktk shule ya wokovu; Gal3:24 ” Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.” (“Wherefore the law was our schoolmaster to bring us unto Christ, that we might be justified by faith.”)

  Basi hizo Amri na Hukumu walizofundishwa, kazi yake ilikuwa ndiyo hiyo kuwaleta kwa Kristo, huku uliko Wokovu ili wapewe IMANI, hiyo yenye kumfunua Mungu, wamjue na KUMPENDA, hapa ndipo Sheria inapokomea, kwani Siri ya Mungu imefunuliwa kwao (Ufu 10:7 “… isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.)!!!
  25 “Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.” (But after that faith is come, we are no longer under the schoolmaster” Haleluyaaaa, hatupo tena chini ya Sheria!!!!

  Nazo chapa hawapigwi watu ktk Agano la Kale, wanapigwa huku inakomalizikia Injili hiyo yenye kuleta Imani!

  Sehemu gani unapopigwa chapa ndg yangu isikusumbue sana, unapigwa chapa sehemu ambayo inaonekana kirahisi, mfano wa sigida walizo nazo waisilamu wanaosujudu kwenye mikeka!

  Hata ukirudi Misri, damu ilipakwa ktk frame za milango, hiyo ndiyo iliyokuwa chapa yao kwa siku hiyo.

  Kwahiyo huyo malaika anapita hata sasa kuwatia alama watu wa Mungu, hao walio ktk Agano Jipya, hao ambao hawajaupigia magoti Utatu, hilo fumbo lisilo fumbuliwa; akimalizana nao ndio atawarudia watu wake Israeli, aliowaacha kwa kitambo, hao ambao hawakuingia ktk Agano jipya walibakia ktk hilo Agano kuukuu, wakiendelea ktk Sheria kwani hawakumpokea Kristo ili wavushwe upande wa pili wapewe mambo mapya, huo Wokovu!

  Basi chapa ya leo ni Utukufu wa Mungu unaomfunika mwaminio, kama ule ambao ulimfunika Musa alipotoka mlimani uweponi mwa Mungu, bali kwa leo ni wa rohoni ukiutiisha mwili hata kuwa waraka. Nayo chapa ya Mnyama ni utukufu wa Shetani unaoambatana na wasio iamini Injili ya mitume!

  Kwahiyo ktk wakati huu chapa zote mbili zinawahusu Mataifa maana hawa ndio waliomo ktk mchakato ambao unakwenda kufungwa karibuni, muda wao unapomalizika, ndio maana chapa zinatembea, na sasa hivi Shetani nae anawakusanya wote walioikosa Chapa ya Mungu, ule Muhuri, yaani RM.

  Ndio maana niliwaambia kuwa kudhani kwamba utawekewa chip, au kwamba malaika atapita na kopo la rangi atutie alama isiyofutika ni kujirejesha ktk Agano la Kale ambalo halituhusu kiagano bali ni mwalimu wetu wa kuijua dhambi ni nini ili tuijue na thamani ya wokovu tulioitiwa ambao ndio chapa ya Mungu! Maana Wokovu si wa mwilini kama tunavyofikiri mara nyingi, bali ni mambo ya rohoni yanayojidhihirisha katika mwili, ndivyo zilivyo hizo chapa zote mbili ni za rohoni! Mungu anawakusanya uzao wake kupitia Adamu, na ibilisi nae anawakusanya uzao wake kupitia nyoka; tayari kwa ile vita!!

  Mbarikiwe!

 8. TUTAMBUE PIA ALAMA YA MUNGU HUEKWA KWA WATU GANI KABALA YA KUJUA ALAMA YA MNYAMA.

  EZEKIELI 9:4
  “BWANA AKAMWAMBIA,PITA KATI YA MJI, KATI YA YERUSALEMU,UKATIE ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO VYA WATU WANAOUGUA NA KULIA KWA SABABU YA MACHUKIZO YOTE YANAYOFANYIKA KATI YAKE”

  UFUNUO 7:3
  “AKISEMA, MSIIDHURU NCHI, WALA BAHARI, WALA MITI, HATA TUTAKAPOKWISHA KUWATIA MUHURI WATUMWA WA MUNGU WETU JUU YA VIPAJI VYA NYUSO ZAO”

 9. “HAPA NDIPO PENYE HEKIMA. YEYE ALIYE NA AKILI, NA AIHESABU HESABU YA MNYAMA HUYO; MAANA NI HESABU YA KIBINADAMU. NA HESABU YAKE NI MIA SITA, SITINI NA SITA.”UFUNUO 13:18

  MUNGU ANASEMA HABARI YA HEKIMA NA AKILI NDIYO INAHITAJIKA HAPO
  ILI KUITAFSIRI LAZIMA TUJUE HEKIMA NA AKILI NI NINI? BILA KUTUMIA MANENO YETU ANASEMA;

  “ZISHIKENI BASI, MKAZITENDE, MAANA HII NDIYO HEKIMA YENU NA AKILI ZENU, MACHONI PA MATAIFA WATAKAOZISIKIA AMRI ZOTE, NAO WATASEMA, HAKIKA TAIFA HILI KUBWA NI WATU WENYE HEKIMA NA AKILI” KUMBUKUMBU 4:6

  “YEYE AISHIKAYE SHERIA NI MWANA MWENYE HEKIMA.” MITHALI 28:7

 10. Ukweli ni kwamba mwenye sikio na asikie. Una weza kuwa na elimu kubwa ukadhani umefika mbali katika elimu ya kiroho, kumbe upo gizani! Wana pinga ju ya habari za chip na kutoa maeleze kinyume na una bii, hao nao nimpango wa mnyama. Ikumbukwe kwamba ktk unabii si 1 ni sawa namia elf1 na miaka elf1 ni sawa na siku1. Asomaye afahamu

 11. Shalom, ndugu zangu ili niwe na la kuchangia, ningependa aliye na hiyo taarifa aitoe ili niisome na niweze kuwa na cha ku-coment!

 12. Mwisho wa dunia bado sana. Labda miaka 100 tena ijayo. Watu wengi wanajaribu kuchukua taarifa zisizohusiana na hali halisi na kama vinahusiana ukweli ni kwamba siyo kwamba Yesu ndo sasa anarudi.

  Hilo la Obama wa Marekani kama likiwa na uhusiano wowote na Maandiko ya Ufunuo basi haliwezi likawa ndicho kivutio cha Yesu kurejea duniani.

  Kwa mfano maandiko yanasema asiyekuwa na chapa hiyo hataweza kununua wala kuuza chcochote sokoni. Yaani hataweza kuandikisha mtoto shule, hataweza kupata matibabu, hataweza kupata tiketi ya ndege, basi treni, taxi,nk kama hana chapa ya mnyama huyo yaani namba 6 6 6.

  Ili swala hilo liwezekani kwa dunia yote ikiwemo vijivi vingi vya Bara la Afrika kama kule kwa barbaigi, wamasai, wakongomani, wanaijeria, nk haiwezekani ukawapa chip kama hizo za Obama wakati hata umeme hawana. Mpaka umeme uje kufika kwao na hizo chip za Obama ziwezekane kupachikwa usoni mwao itachukua miaka mia kama siyo zaidi.

  Ni lini watu wa mapolini na vijijini ambako umeme hakuna ili chip za Obama zifanye kazi maana hizo chip hazifanyi kazi mahali pasipo na umeme? Mifumo ya mabenki, mifumo ya redio, mifumo ya simu, itafika lini vijiji vyote vya Afrika, Asia, Amerika kusini ambako watu hata kupata huduma hizo bado ni ndoto?

  Maandiko yanasema mpaka Injili ihubiriwe kwa kila kiumbe ndipo ule mwisho utakapofika. Je, watu wanaoangalia swala hilo la Chip za usoni wamelitazama pia andiko hilo na kujiuliza kama vijiji vyote na watu wote wamefikiwa na Injili ili ule mwisho ufike? Je, kila kiumbe kimefikiwa na Injili? Je, kila mmasai, mbarubaigi, mmakonde, mjerumani, myahudi, muhindi, mkorea kaskazini, mkorea kusini, muiraki, muirani, Mwarabu, nk je ameshahubiriwa?

  Kuwahubiri wote hao hatuoni kwamba itachukua karne nyingine moja yaani miaka 100 au zaidi ndipo ule mwisho ufike?

 13. biblia haitafsiriwi kimwili japo linatimizwa mara nyingi kimwili na watu wengi, ni kweli kuwa siku za mwisho zimekaribia lakini pia tuwe maakini katika tafsiri zetu tusije tukawaukumu watu tukaukumiwa

 14. 666 ni mfumo wa biashara ya nafsi na si haya mambo ya chip hiyo mnayoizungumzia! Chip ambayo tutawekewa ni ya kiroho, “Utatu Mtakatifu”!!!
  Hii ndiyo chip inayopandikizwa katika kila nafsi. Yaani madhehebu yetu yote yataungana chini ya ukiri huo wa “Utatu Mtakatifu” na kutengeneza block moja yenye Nguvu kiuwakilishi katika utawala wa dunia kiroho na kimwili. Baada ya hapo hakuna dhehebu lolote lisilokuwamo katika Umoja huo ambalo litaruhusiwa kufanya biashara hiyo ya nafsi! Hakuna kuuza wala kununua mpaka uwe katika Umoja huo wenye Nguvu, wa makanisa duniani, yaani unaposikia neno “mnyama” jua kwamba hilo huwakilisha Nguvu, basi hao wanaoform block hiyo yenye Nguvu hupigwa ‘Chapa ya Mnyama’ kuwakilisha utambulisho wao, pamoja na washirika wao!!!

  Basi msitishike sana na mipango hiyo ya rais Obama, hiyo haina uhusiano wowote na hiyo Chapa ya Mnyama. Shughuli yenyewe ya Chapa ya Mnyama inaendelea, ni mchakato wa kiroho ulioanza siku nyingi sana, na ninaamini wapendwa wengi sana wanaufurahia, maana huo utawapa nguvu. Umeliona ‘Jukwaa la Wakristo’? Si, unaiona nguvu ya Umoja katika kupambana na chochote kile, hiyo ndiyo sampuli ya huo Umoja wa Makanisa Duniani. Yaani pale mnapoikosa Nguvu ya Roho Mtakatifu, basi Umoja wenu waweza kuziba pengo hilo, licha ya tofauti zenu za kimafundisho, at least at this while. Tofauti hizo ndizo zinazoshughulikiwa, sasa hivi madhehebu yetu yote yanakutanishwa kwanza katika Ukiri wa Mungu Mmoja katika dhana ya Utatu, baada ya hapo wataprune hiki na kile ili kufikia Umoja wa Roho wakielekea katika Umoja wa Imani!

  Hili ni jambo gumu kueleweka au kuaminika, kutokana na jinsi linavyovutia na hivyo kumpumbaza yeyote aliyelengwa, mithili ya swala aliyepigwa tochi na muwindaji! Hebu wafikirie Wasabato ambao wao huamini kuwa Muhuri wa Mungu si Roho Mtakatifu bali ni kuitunza Sabato, kwa hiyo wao hujihesabia kupigwa ‘Muhuri wa Mungu’, na kisha kuwaona wote wanaosali Jumapili wamepigwa ‘Chapa ya Mnyama’ halafu nao wamo katika Umoja huo ambao ndio wenye kuform Chapa ya Mnyama, nao HAWAJUI!!!

 15. Filbert si kwamba wapendwa hawako makini na nyakati, ulitakiwa kuiposti sehemu kama hii ndugu yangu!

 16. Hayo ni maandalizi si tu,bt alama hiyo siyo yenyewe. Na kama ni yenyewe, basi kanisa linatwaliwa muda si mrefu maana mpinga kristo9 kwa maana ya 666) hataanza kufanya kazi wakati kanisa lipo, kwa vile lina Roho mtakatifu ndani yake.

 17. Mimi nilishaisoma hiyo habari na nikaposti link twitter na facebook pamoja na swali, ” JE DUNIA BADO IPO?” kwa bahati mbaya wapendwa wenzangu marafiki ktk mitandao hii hawakuifuatilia wala kuuliza. Hii inamaana kuwa wapendwa hatuko makini na nyakati.

 18. Mimi nilishaisoma hiyo habari na nikaposti link twitter na facebook pamoja na swali, ” JE DUNIA BADO IPO?” kwa bahati mbaya wapendwa wenzangu marafiki ktk mitandao hii hawakuifuatilia wala kuuliz. Hii inamaana kuwa wapendwa hatuko makini na nyakati.

 19. Moses binafsi nakushukuru kwa hii taarifa, lakini ningeomba utupe na sisi hiyo source yako ya information ili tusome.
  Inawezekana unachokisema ni kweli, au ikawa vinginevyo.
  Give us the source please!

 20. Ni wakati wa kumtafuta mungu kweli ndugu katika Bwana moses!
  wanaosema mwisho bado wamo gizani bado ila tujue ni kwamba wakati wa hukumu katka nyumba ya mungu umeanza mwisho wake yeye asiye mucha mungu utakuweje?
  tuendelee kuhimizana ktk mema kwa maana wakati u karibu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s