Kwa wanandoa na wenye kujitayarisha kuingia kwenye ndoa!

Image

Mapenzi uliyonayo kwa mwenzi wako baada tu ya kuoana,huwa ni matamu sana,maana wengi hutamani sana kumuona mwenzi wake muda wote akiwa pamoja naye wakiwa nyumbani.

Lakini kadri ya muda unavyosogea,penzi hushuka,kama grafu inavyoshuka ,badala ya kupanda .

Wengi hupunguza upendo kwa mwenzi wake wa ndoa,Na wengine kama wameshaanza kupata mtoto wao wa kwanza,Utakuta; Upendo unarudi mahali pake kidogo, Kisha upendo ule unahamia kwa mtoto,

HAPO NDIO SHIDA INAKOANZA.

Sasa,mtoto huchukua nafasi yote ya mapenzi,utakuta wengine labda mama hampendi tena baba kama alivyokuwa anampenda na kuanza kumpenda mtoto tu,kwa mama wa namna hii,utakuta baadae anamuona baba kama lijanaumme lisilokuwa na maana yeyote (Hata wakina baba wengine nao ni hivyo ivyo siku hizi.)

Lakini hali yoyote ya ugomvi na haikuletwa Mungu bali ni shetani ndio mwenye kuleta magomvi katika familia.

TAZAMA KWETU SISI HALI KAMA HII HAINA NAFASI, MIMI NAMPENDA MKE WANGU NAYE ANIPENDA TANGU MWANZO HADI MWISHO,

WEWE JE ?

Mtumishi Gasper Madumla

Advertisements

5 thoughts on “Kwa wanandoa na wenye kujitayarisha kuingia kwenye ndoa!

  1. ubarikiwe mtumishi kwa mafundisho mazuri kwa sisi wanandoa Mungu atusaidie sana.

  2. Haaa… Mtumishi Gasper hapo kweli ila jambo moja nilitambua ni kwamba mtoto hawezi akafanya penzi lififie moto ila hiyo ni mbinu ya ibilisi tu kutowesha upendo.Kwanza mtoto ni baraka pili ndio kiunganishi halisi cha uhusiano wa baba na mama hivyo wapenzi wasimame imara kwa maombi kupinga mbinu hiyo ya ibilisi kwani patakapokua na upendo basi kutakua na mawasiliano na umoja na ushindi dhidi ya yote…….

  3. asante sana mama k ,kwa darasa la ukwelii .Mungu akubariki na aendelee kukutumia kwa huduma hiii

  4. Watoto ni baraka siyo rahana, wanapokuwa wamekuja ktk familia , upendo kwa baba na mama inabidi uongezeke na wala si kupungua, imeandikwa ktk mithali 10:22 kuwa Baraka ya Bwana hutajirisha wala achanganyi uzuni nayo, hivyo inabidi upendo uongezeke wala si kupungua, imeandikwa pia kuwa Mungu si Mungu wa machafuko bali wa amani, kwa hiyo wana ndoa jamani ukiona hakuna upendo au upendo unaanza kupungua mara mtoto anapozaliwa mvalie shetani njuga aondoe mikono yake michafu ktk familia yako, na ktk upendo wenu kati ya baba na mama, naungana na mpendwa aliyeandika wazo la mtoto kuwa pembeni kabisa asilale katikati ya mama na baba kitandani, hii ni muhimu sana maana hakuna ilipoandikwa ktk biblia kuwa mtoto anapozaliwa upendo upungue kati ya mama na baba, mimi na mume wangu mtoto wetu alianza kulala ktk chumba chake alipotimiza miezi mnne , na alipokuwa amezaliwa alikuwa na kakitanda kake kameunganishwa na kitanda chetu ,chumbani kwetu, baada ya miezi mnne mtoto alihamia chumbani kwake , nilikuwa naamka naenda kumnyonyesha chumbani kwake , narudi kitandani kwangu , lakini kama huna chumba cha mtoto , kama mfano una chumba kimoja na nyote mnatakiwa kuchangia chumba hicho, bado unaweza kununua godoro ukaliweka chini ,au kitanda cha mtoto kinachoitwa Crib, mkakiweka karibu na kitanda chenu. hii inasaidia sana sana , na wala hakuna kuogopa kuwa mtoto anapolala peke yake kuna kitu anakosa , mwanangu ana umri wa miaka karibu mnne lakini sioni kasoro yoyote kwake , ninayoweza kusema ilisababishwa na kulala peke yake alipokuwa na umri wa miezi mnne. hii ni muhimu sana asante Siyi kwa mchango wako. . Pia kama upendo unayumba baada ya mama na baba kuishi pamoja mda mrefu tumia sana maandiko ktk 1 wakolintho 13:4-8. huwa ninamsomea mume wangu maandiko haya kila mara na yeye ananisomea , ni maandiko ya upendo, na yana nguvu ndani yake. yatamke na kuyatafakari , na kuyahamini na kuyafanyia kazi kutenda kama yanavyosema, usiyasome ukaacha pale , hakika shauri la Bwana utaona likisimama ktk ndoa yako. Lakini Mungu ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo 1 wakolintho 15:57.. Love the only way to victory, Remember Jesus is Lord. Mama K.

  5. Vitoto vinapoatikana, visiwe vinawekwa kulala katikati ya Baba ba Mama pale kitandani. Viwekwe pembeni ili hawa wawili waendelee kuwa karibu. Nafikiri inaweza kusaidia kidogo. Hata mie nitajitahidi kufanya viile ili haya yasitokeee

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s