Mungu hasikii maombi ya wenye dhambi?

maombii

Biblia inasema twajua Mungu hawasikii wenye dhambi, swali, je ni sahihi kwa mtu aliyeokoka kumwambia mtu hajaokoka (kuhukumu), kwa mfano, anasafiri au anaenda kufanya mtihani, ni mwenye maovu halafu aseme anahitaji maombi. Je Mungu atasikia nikimuombea?

Paul Andrew 

Advertisements

4 thoughts on “Mungu hasikii maombi ya wenye dhambi?

 1. Mpendwa Andrew,
  Kama sikosei, unamaanisha; Nukuu ya msitari uliyonukuu, umeulewa kwamba, Mungu HASIKII wenyedhambi wakiomba! Na hivyo unataka kujua kama Aliyeokoka akiomwombea Mtu mwenyedhambi, Mungu atasikiliza kuomba huko. Na pia unataka kujua iwapo ni sahihi kwa aliyeokoka, kumwambia mtu ambaye hajaokoka kwamba, ni mwenye maovu (ukimaanisha kuwa ni kumhukumu), Nasema hivyo kwasababu wewe umesema,

  “Biblia inasema twajua Mungu hawasikii wenye dhambi, swali, je ni sahihi kwa mtu aliyeokoka kumwambia mtu hajaokoka (kuhukumu), kwa mfano, anasafiri au anaenda kufanya mtihani, ni mwenye maovu halafu aseme anahitaji maombi. Je Mungu atasikia nikimuombea?”

  Nikwamba, Mungu hasikilizi maombi yaliyo Nje ya mapenzi yake tu basi, ujasiri wa katika kuomba kwa Mtu aliyeokoka kunatokana na kujua kuwa kile anacho kiomba kipo ndani ya mapenzi ya Mungu na si vinginevyo! Ukisoma ile 3Yh. 5:14 inasema,

  “14Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. ” Lakini ujasiri huo unatokana na tu kwamba Mwombaji ni AMEOKOKA (Mwana wa Mungu); Katika ile 1Yh. 3:9 inasema,
  “9Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

  ” Kwa hiyo katika swala la maombi, Mungu husikia maombi ya Watoto wake tu! Kwa hiyo, watoto wa Mungu, haki zao zipo kwa Mungu, na watoto wa Shetani haki zao zipo kwa Shetani. Neno linasema katika 1Yh.3:10 kuwa, “10Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.”

  Labda tujiulize kwa nini Mungu hamsikii mwenyedhambi? Sababu kubwa ni kwamba, pamoja na mambo mengine, maombi hayapati matokeo ya majibu yanayokusudiwa na mwombaji, yasipofanywa kwa Imani, Biblia inasema, Neno lolote lisilofanywa kwa Imani ni dhambi. Na kwa mjibu wa Biblia iyohiyo inasema Dhambi ni kutoamini Neno la Mungu, na tumekwisha jifunza kuwa, Mungu husikia maombi yaliyazingatia Mapenzi yake, na Biblia inasema Mapenzi ya Mungu ni ule ukweli uliyomo katika maombi husika, na kweli ni Neno lake na kweli hiyo inajulikana na kutimia kwa Imani; Sasa, kama maombi huthibitika mbele za Mungu kwa njia ya imani. Lakini tumejua pia kuwa Dhambi ni kutoamini Neno la Mungu, kumbe Mungu huyu atasikaje Maombbi ya Mwenye dhambi, yaani maombi ya Mtu asiye amini Neno la Mungu? Jibu ni kwamba haiwezekani, hiyo ndiyo sababu kubwa kuwa, Mungu hasikii wenyedhambi.

  Lakini katika Swala kumuombea Mtu mwenye dhambi, Jambo hili haliwezekani kabisa, ila tu umeambiwa hivyo na Roho mtakatifu. Maana wapo wanaoteswa na shetani lakini ni watoto wa ‘Ibrahimu’. Kimsingi, mwenyedhambi, ni wa shetani; Kwa hiyo kabla hujaanza kumuombea mwenye dhambi huyo jiulize kuwa, unachomuombea ni nini na kwa mungu yupi, ambacho shetani ambaye ndiye mungu wa huyo mwenyedhambi amekubali umuombee! Kwa kifupi mwenyedhambi asipotubu huwezi kumuuombea lolote kwa Mungu wa mbinguni. Kwa sababu, tunapoombea Mtu, tunapeleka shida za muombewaji kwa Mungu, sisi tunakuwa mawakala tu lakini hasa, mwenye ile shida inayopelekwa kwa Mungu ndiye anayeomba. Kwakuwa “mwombaji” huyo bado ni mwenyedhambi huyo ni mali ya shetani na hivyo mungu hawezi kusikiliza maombi ya huyo mtu wala ya “mawakala wake” yaani waombeaji wake, Mungu hamsikii mwenye dhambi!

  Kuhusu kumwambia mtu asiyeokoka kuwa ni mwovu, hiyo si hukumu kwani hukumu hufanywa na Mungu peke yake, Mungu anajuwa waliyowake na hivyo asiye wake pia anamjua. Kitendo cha Mungu kujua hatima ya mhusika hiyo ndiyo hukumu yenyewe, Neno linaema katika Korintho kuwa “Baada ya kifo hukumu!” Mwenyedhambi kuitwa mwovu, ni haki yake maana huo ndiyo ukweli wenyewe!
  Endeleeni kubarikiwa.

 2. kwanza kabisa ukiona mtu anaomba maombi huku matendo yake si mazuri ,hii inaonyesha mtu huyu tayari ndani mwake kuna mbegu ya neno la Mungu hivyo uovu ni roho ya shetani ndiyo inayotenda uovu ,unapomwombea Mungu anaweza akafanya kitu ,mfano paulo aliye itwa sauli ungemwona kabla hajaokolewa ungesema kuzimu ni yake lakin maombi ya mitume yalimwingia hata kama alikuwa mwovu.unaweza ukagundua paulo ndiye aliye kijua kitabu cha agano la kale hivyo aliokolewa ili ajue kuunganisha ya mwili kuwa roho so kuwaombea si tatizo maana unapo mwomba Mungu lazima utavunja njia za shetan kwake na kutaka Mungu amsaidie ,kwel wakat wa bwana ukifika ataokoka na akiokoka atasema Mungu alikuwa ananitafuta hivyo kwake ni ushuhuda kwa wengine.
  t a g njombe mjini

 3. Swali langu lilikuwa hivi, mtu ameokoka kuomba maombi kwa mtu hajaokoka ni sahihi ? Mfano unaenda kufanya mtihani umekutana na rafiki yako hajaokoka, halafu unamwambia naenda kwenye mtihani bwana,nahitaji maombi yako, mungu husikia maombi hayo? Au ni mazoea tu tumejenga?

 4. Kwa uelewa wangu ndg Andrew,
  Toba hufanyika kwa sekunde tu ndani ya moyo wa mtu. Hata kama ni mdahambi sana, lakini kama ataonekana kutubu ndani ya moyo wake, jambo ambalo wewe mwombaji huwezi kuliona kwa wakati, huo, wewe mwombee tu. Kama atakuwa ametubu kabisa ndani ya moyo wake na kutambua uweza na ukuu wa Mungu, Mungu atasikia maombi hayo. Lakini kama ndani ya moyo wake, hakutakuwa na toba ya dhati, maombi yale hayatajibiwa kabisa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s