Torati Vs Neema

bwana-wa-sabato

Tunapoliendea jambo hili, kuhusu Torati inapobadilika na kuwa Neema, ni vizuri tukianzia hapo kwenye mkanganyiko kwa swali la msingi:

Je, kuna Andiko lolote linalotuambia na kutuamuru kuadhimisha Jumapili kama tu Wayahudi walivyoadhimisha Jumamosi? 

Jibu ni hakuna. Hakuna Andiko lolote katika Biblia, haswa Agano Jipya, kwetu sisi Kanisa, linalotuamuru kuadhimisha Jumamosi wala Jumapili. Lakini kusudi la kuadhimisha Jumapili, ni ukumbusho wa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristo!

Sasa, kuna makundi yanasema, “Katoliki ya Kirumi ndio walioigeuza siku hiyo kutoka Jumamosi kuja Jumapili.” Nao Katoliki wanadai kulifanya jambo hilo, bali ni uongo mtupu. Kama ni wao walilifanya, basi mtakatifu Paulo atakuwa alikuwa ni Mkatoliki wa Kirumi, na hata Petro pia, Yohana, na Yakobo na wengineo wote, kwa kuwa wao walikutanika siku ya kwanza ya juma kwa ibada (Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, … Mdo 20:7). Na, kulingana na historia, njia pekee wangewatofautisha kati ya Wayahudi Wakristo na wale Wayahudi wa kiasili (orthodox), ilikuwa ni siku zao za ibada, orthodox walikutanika Jumamosi (waliokataa kufufuka kwa Kristo), na hawa wengine, Wakristo, wao walikutanika Jumapili (walioamini kuwa Yesu alifufuka katika wafu). Na hiyo ilikuwa ni alama ya utenganisho kwao. Na bado inaendelea kuwa ni alama, na huenda ikaja kuwa ile chapa ya ya mnyama!

Sasa, ndugu zetu Wasabato wao wanaamini kuwa kuitunza sabato, katika maana ya siku ya Jumamosi, huo ndio muhuri wa Mungu. Wao wanasema, “Unatiwa muhuri kwa kuadhimisha sabato.” Lakini hakuna Andiko hata moja katika Biblia lisemalo hayo. Yaani kimsingi tunaweza kusema kwa uhakika kuwa hilo ni fundisho lililo kinyume na Maandiko. Kwa faida gani? Roho aliyelibuni atakuwa anajua zaidi, ila halina uhusiano wowote ule na mbingu!

Lakini ukitaka kujua kuhusu muhuri wa Mungu, hebu lifananishe jambo hilo la muhuri wa Wasabato na Andiko hili katika Waefeso 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.” Ubatizo wa Roho Mtakatifu, Huu ndio muhuri wa Mungu! Unaona, ukienda katika Isaya 28 anasema, “Amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, huku kidogo na huku kidogo.” Usikurupukie neno lolote bila kupata uhakika wa Maandiko katika Hekima yake!

Tazama, watu wanajaribu kufanya jambo fulani ili kujiokoa, wengine wanaacha kufanya kazi, wanajaribu kuacha kula nyama, wanajaribu kuadhimisha siku ya sabato ya Kiyahudi, wanajaribu hiki na kile, unaona, lakini hakuna kitu unachoweza kufanya kuhusu kujiokoa. Hivyo ndivyo ilivyo tabia ya mwanadamu wa mwilini, “Kama ungalifaulu kuacha pombe, au uzinzi, au kuvuta sigara, au ukiitunza sabato…”, hakuna utakalo fanya liwezalo kukuokoa! Tunaokolewa kwa Neema. Mungu hutuita, Mungu hutuokoa. Tunapaswa kuzifuata nyayo za Mungu, Neno lake, hicho tu. Naye Mungu kwa neema hutupatia Uzima mpya, huo Uzima wa milele. Nao Uzima wa milele ni Ubatizo wa Roho Mtakatifu! Sasa iwapo umedanganywa kuwa kwa kuitunza kwako sabato ya Kiyahudi ndio umetiwa muhuri, itakuwaje? Unaiona hasara hiyo, au umedanganywa kuwa ulipoNena kwa Lugha ndipo ulitiwa muhuri, hakika kama hautayafuata Maandiko UTAPOTEA!!!

Basi, Sabato ni nini? Sabato maana yake ni “Raha” ndipo Sabato yapaswa kuwa ni siku ya “raha!” kwahiyo unapoliona neno sabato, jua maana yake ni ‘raha’. Basi kwa vile jambo hili la sabato limo katika zile Amri Kumi, ambazo kimsingi ndizo zinazoleta mkanganyiko katika madai ya kuzitimiza kwake, kulingana na zilivyotolewa na kukabidhiwa Israeli, naye Kristo kwa kauli yake akisema kuwa hakuja kuitangua Torati, nazo Amri hizo zikiwa ni sehemu yake, hilo likimaanisha kuvushwa kwake kutoka Agano la Kale kuja Jipya. Ndipo makundi ya kikristo, hao wanaokutanika siku ya Jumapili huonekana ni wenye kuivunja Amri hiyo ya Nne, ambapo sababu zake nilizielezea huko juu. Nako kuvunjwa kwa Amri yoyote kati ya hizo, huhesabika ni kuvunjwa kwa zote.  Ndipo sasa, nataka tulitazame jambo hili katika ujumla wake wa hizo Amri Kumi, ili kuona kwamba, tunapozizungumzia hizo Amri Kumi baada ya kumpokea Kristo, je, huwa tunazizungumzia hizo Amri katika maana ya zile walizopewa Israeli au zilizotimilizwa?

Kwa kadiri ya ile alama ya utenganisho, kule kukukataa kufufuka kwa Yesu kutoka katika wafu, kwa upande mmoja, na huko kuamini kuwa Yesu alifufuka katika wafu, nayo alama ya utenganisho huo ikijiwakilisha katika siku za kukutanika, Jumamosi kwa wanaokataa na Jumapili kwa walioamini, ndipo hata Amri hizo zimegawanyika kulingana na utenganisho huo. Kundi la waliokukataa kufufuka kwake Yesu likiendelea katika zile Amri Kumi za Agano la Kale, na hili kundi jingine lililokupokea kufufuka kwake, likiendendelea katika Amri zilizobadilishwa, yaani zilizotimilizwa! Basi mara nyingi tatizo huwa hapa, sote hudhani tunaongelea jambo moja lakini ukweli ni kwamba sisi huongelea vitu viwili tofauti, only similar!

Haya, na tuyatazame mambo yalivyo katika Agano Jipya. Kristo, katika Mathayo mlango wa 5 anaweka msingi wa jambo hili, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.” Sasa Andiko hili linatudhihirishia kuwa Torati aliyoikuta Kristo, hiyo iliyokuwepo, katika ujumla wake, toka ilipotolewa na kutumika katika kuyaongoza makundi ya Israeli, ilifaa katika kazi hiyo ya uongozi (schoolmaster), yaani ikiwafundisha kuhusu dhambi na adhabu zake hapo inapowapeleka kwa Kristo. Hiyo ndiyo safari ya kiroho ya Israeli, kutoka utumwani hadi kuwa wana katika Kristo! Kwahiyo twaweza kusema kwa uhakika kuwa Torati au zile Amri, zimedumu hadi Kristo alipozitimiliza. Kwahiyo kundi lolote ambalo linaendelea katika hizo Amri zisizotimilizwa, hilo linahesabika pamoja na hao waliokataa kufufuka kwake Kristo, haijalishi kelele zao, matunda yao ndiyo yanayothibitisha kile walicho, nayo miti huzaa kulingana na pando au mbegu!

Lakini kwa upande wa pili, hawa wako katika torati iliyotimilizwa. Twaweza kuona kutimilizwa kwake kwa kuviangalia vifungu vichache vya Maandiko ili kuibaini maana kamili ya KUTIMILIZWA kwa Torati, yaani AGANO JIPYA! Basi Kristo anaanza hivi:

Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, ““Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.”” Ati, hii ilikuwa ni nini? Torati, zile Amri.

Bali mimi (Yesu) nawaambieni, ““Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.”” Akaigeuza hiyo Torati, sivyo? Huko kutimilizwa!

Mmesikia kwamba imenenwa, ““Usizini””; lakini mimi nawaambia, Aliigeuza, sivyo? Wadhani yeye hakuigeuza Torati? Vema, yeye alisema “”Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.””

Haya hayakuwepo kule nyuma katika Agano la Kale, haya ni Agano Jipya! Yeye alivuka ng’ambo na kuendelea kutoa Amri hizo, “Mmesikia wakisema, wale watu wa kale, ‘Usi…’ nami nawaambieni vinginevyo. Mmesikia wakisema, ‘Jino kwa jino na jicho kwa jicho,’ lakini mimi nawaambia…!

Sasa mwishoni mwa hayo yote, Yeye aliiacha ile Amri ya Nne, hiyo ilihusu, “Ikumbuke siku ya sabato na kuitakasa.” Sasa tazama, “Kila aziniye hana budi kupigwa mawe,” iliwabidi wawe katika tendo la kuzini. Sivyo? Na ilibidi wakamatwe katika tendo hilo. “Kila auaye,” ilibidi awe muuaji, awe ameua kihalisi.

Lakini Yesu anasema, “Kila amtazamaye mwanamke,” nafsi yake, roho, hakuna lolote katika mwili wake sasa, Nafsi yake ikiwa imekombolewa sasa, bali huko nyuma katika Torati, haikuwa imekombolewa wakati huo, kwani Torati ilikuwa ni kiongozi katika kuwaleta na kuwafikisha katika huo ukombozi wa Nafsi zao. Ndipo Yeye sasa akasema, “Kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Akasema, Mmesikia wakisema ‘Usiue,’ bali nasema kila amuoneaye ndugu yake hasira, amekwisha ua.” Unaiona Torati inavyotoka mwilini na kuhamia rohoni?

Basi Yeye alisema, yaani kuhusu sabato:

Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha… ; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

Umeiona hiyo sabato au pumziko au raha inayoahidiwa kwa Nafsi zetu? Si kwa mwili huu unaoonekana, Nafsini mwako!

Haya hebu msikilize Paulo sasa, akiwaandikia Waebrania, watu wa Torati, waadhimisha sabato. Sasa, anawaleta Wayahudi, kwa vivuli na mifano, akionesha kile Torati ilikuwa kwa mfano. ”Torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuja,” naye aendelea mbele kuinyonyesha kama mwezi na jua. Kama mwezi ulivyo kivuli cha jua, jua likiangaza sehemu fulani ya nchi, nao mwezi ukipokea kutoka kwa jua na kuangazia sehemu nyingine mwanga hafifu nk unaweza kuyaona hayo katika Waebrania 9. Lakini katika Ebr 4, anaingilia jambo la sabato. Sasa tazama,

Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.

Paulo akinena na watu wa sabato, hao walioiadhimisha sabato. “Basi na tuogope ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika siku ya sabato” kwa maneno mengine!

“Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao (nyuma kule chini ya Torati)… Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.”

Sasa, hayo ni kule nyuma chini ya Torati. Hawakuwa na Imani, sababu hakukuwa na msingi wa kuiwekea. Umeona? Torati haina uwezo wa kuleta Imani, “Imani huja kwa kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo

“Maana sisi tulioamini tunaingia katika (sabato) raha ile; kama vile alivyosema, …” 

Sasa, raha “Yake”. Sasa “Yake” ni Raha ya Kristo. Raha yake, “Sabato” Yake! Si mnakumbuka tulikubaliana kuwa neno Sabato maana yake ni ‘raha’; kwahiyo kila palipoandikwa ‘raha’ tutatumia neno sabato ili tuupate ufahamu kuhusu kuadhimisha siku fulani. Haya,

“Maana sisi tulioamini tunaingia katika (Sabato) raha ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia (Sabato Yangu) rahani mwangu:… (Sasa, tazama ujumbe wa Paulo wa siku iliyotakaswa)…  ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Kwa maana ameinena(katika Torati) siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote.”

Hiyo ilikuwa ni siku Yake ya saba. Sasa, Paulo anakubali kuwa Mungu aliwapa wao, hiyo ilikuwa siku ya saba. Na Mungu alistarehe siku ya saba, akaibariki siku ya sabato, akaitukuza, na akaitakasa, akifanya siku ya kustarehe. Mungu akafanya hivyo, akaacha kazi Zake zote. 

 Na hapa napo, Hawataingia (Sabato Yangu) rahani mwangu (Yesu akinena).

Sasa, kuna sabato nyingine mahali fulani, iko wapi?

Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, …

Aweka tena siku fulani, … 

Aweka siku hapa. Ni ipi? Sabato, sivyo? Aweka siku ya saba ya juma hapa kama sabato katika mahali hapa.

Aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; (hata Yesu alipokuja, ule wakati wa kwanza) … kama ilivyonenwa tangu zamani (Torati), Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu. (Mimi na wewe! Hapa kuna raha / Sabato nyingine ijayo; si ya kimwili, ya kiroho!)

Sasa, tungeweza kusema kwamba tuna siku ya saba pia. Twende taratibu, tuzifuate hatua Zake atuongozaye. Hebu tusome kifungu kinachofuata, tuone zaidi kuhusu hilo:

“Maana kama Yesu angaliwapa (Sabato) raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.

Kristo alipoigeuza Torati, kutoka hiyo Torati hadi kuwa Neema, si angaliwapa siku nyingine ya ‘raha’ au sabato, siku fulani ya raha, siku fulani? Lakini Yeye hakusema lolote kuhusu sabato. Hakusema lolote kuhusu Jumapili, hakusema lolote kuhusu Jumamosi. Bali alisema hivi, Paulo kasema. Haya fungua hayo macho yako ya rohoni, usome na Mungu akupe ufahamu wake:

Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. (Hiyo ni leo!)

Kwa maana yeye (mimi au wewe) aliyeingia katika raha yake (Raha ya Yesu, au sabato ya Yesu; “Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”) amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. (hapo mwanzo).

Amina! Ndiyo hiyo sabato yetu, Ubatizo wa Roho Mtakatifu!!!

Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi. (kwa kung’ang’ana na siku, na kwingineko)

Tazama, Mungu alistarehe siku ya saba, akaiumba siku ya saba, akawapa Wayahudi kwa ajili ya ukumbusho, ikiwa imefungwa ndani ya Torati. Naye Paulo akiwa ni Myahudi, basi twadhani kuwa yeye alikuwa akiizungumzia siku hiyo waliyopewa? Angehesabiwa Haki kwa lipi? Maana twafahamu kuwa kwa Torati usingeHesabiwa Haki, bali yeye anayafundisha haya yote kwa uongozi wa RM. Ndipo unamuona akiyatia muhuri wa RM mafundisho haya, sawa sawa na Neno la Kristo hapo aliposema, “…bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao”, naye mt Paulo anasema, “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.” Huo ndio udhahiri wa Injili!

Basi ukipenda kujua Raha ya Wakristo ni nini, nenda katika Isaya 28, isomeni sura yote. Yeye alisema, ““Amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, huku kidogo na huku kidogo…” Shikilia sana yale yaliyo mema.

La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa; ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia. 

Hii ndiyo sabato, ile raha ambayo walipaswa waingie. Bali kwa haya yote walifanya mioyo yao migumu na kutikisa vichwa vyao kuikataa. (Jambo lile lile tu walilolifanya siku ya Pentekoste, RM aliposhuka juu ya watu Azusa, na RM alipotolewa kwa watu kwa mara ya kwanza nyuma kule katika siku ya Pentekoste. Hiyo ndiyo Raha, sabato kwa watu wa Mungu)

Kwahiyo, sababu pekee tuadhimishayo Jumapili, ilianzishwa na baba zetu wa imani, Biblia, mtakatifu Paulo, Yohana, Mathayo, Marko, Luka na wengine wote, walienda nyumba kwa nyumba, wakifanya ushirika siku ya kwanza ya juma, mitume walipokusanyika na iliitwa, si sabato, bali siku ya Bwana. Yohana alisema, kwenye kile kisiwa cha Patmo, “nalikuwa katika Roho siku ya Bwana.” Sasa siku ya Bwana ni hiyo aliyofufuka, na ndipo yeye Yohana aliyaona hayo!

Hata ukiwarudia wana historia, kama Josephus na wengineo wengi wa mashariki, au wanahistoria wa kanisa, na wengineo wengi tu, waweza kuliona jambo hilo la kundi hili la Wakristo kukutanika katika siku hiyo ya Bwana. Katika kuwatofautisha, mmoja wao aliwaita ‘cannibals’ yaani “wala watu,” hao walikuwa ni Wakristo. Wao walisema, “Kuna mtu aliyeuawa na Pontio Pilato na wanafunzi wake wakaja na kuiba mwili wake. Nao wakauficha, na kila Jumapili wao huenda kula sehemu yake.” Lakini wao walikuwa wakifanya ushirika tu, wao walikuwa wakila mwili Wake na kunywa damu Yake! Wao walisema walikuwa wakila mwili wa Bwana, ushirika. Nao hawakujua ilikuwa ni nini, ndipo wakasema, “Walikuwa wala watu”, wakisema, “Wao huenda kuula kwenye siku ya kwanza ya juma, wao hukutanika pamoja na kuula mwili wa mtu huyo”

Nayo njia pekee ambayo ungetambua kama walikuwa waadhimisha sabato na wakanushaji kabisa wa ufufuo, ama walikuwa ni Wakristo na waaminio ufufuo, wengine walienda kanisani Jumamosi na wengine walienda kanisani Jumapili, hiyo ndiyo ilkuwa ALAMA kati yao, huko nyuma, na ingali ALAMA leo hii!!!

Mbarikiwe nyoote!

Ck Lwembe

Advertisements

43 thoughts on “Torati Vs Neema

 1. Matonya,
  Kwa maelezo yako hayohayo, siuji huelewi wapi!! Hivi dhambi ya kuzini-kile kitendo kinaanzia wapi? Ni mwilini au rohoni? Je, kuna jambo lolote waweza kulifanya bila kuanzia rohoni? Kama Yesu alisema usizini kiroho na torati ikasema usizini kimwili, huoni kwamba kwamba Yesu alikuja ku-rise the standard of keeping the Laws?
  Watu wa zamani, walijua kuwa kushika sheria kimwili yaani kutoiba, kutozini nk hata kama mioyoni mwao wanatamani kufanya hayo mabaya, maadamu tu hawakuonekana kwa macho ya kibinadamu, kwa mawazo yao walifikiri wako sahihi mbele za Mungu jambo ambalo sivyo. Hicho ndicho Yesu alichokuja kukirekebisha vizuri.
  Kwamba licha ya kutenda kile kitendo kimwili, hupaswi hata kukifikiria. Huoni kuwa Yesu alikuja kurejesha kile alichokisema Mungu kupitia nabii wake Yeremia 31:33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
  Sheria zinapokuwa moyoni, hujidhirisha katika mwili. Kwa mfano, usipofikiria kuzini-usipotamani kuzini, mwili utapata wapi msukumo wa kuzini.
  Usipotamani kuiba, mwili utaibaje ilhali moyo na mawazo yako hayakudhamiria kufanya hivyo?
  Hivyo, basi, unapotii sheria kiroho, sharti udhihirisho huo, uonekane katika mwili. Hiyo ndiyo standard aliyokuja kui-rise Kristo. Huwezi kusema eti unatunza sheria za Mungu rohoni ilhali mwili unatenda vinginevyo…Yaani, kwa mfano, unavunja amri za kumi za Mungu kwa kisngizio bubu eti unashika rohoni ilhali matendo yako hayaendani na kile kilicho rohoni mwako.
  Kama ni suala la sababto, hupaswi kwenda siku ya jmosi tu kanisani bila ya msukumo wa kuwa na hilo pumziko takkatifu kuanzia moyoni, utakuwa mnafiki mbele za Kristo, maana unadai kuishika sababto lakini moyoni haimo. Unashika sabato ya siku ya saba, sharti sabato hiyo ianzie moyoni, halafu ionekanane katika mwili- yaani kwa kwenda kusali siku ya sabato na si vinginenvvyo.
  Hali kadhalika na sheria zingine. Na hiyo ndiyo imani, yenye matendo. Imani iliyo hai.
  Ubarikiwe.

 2. Torati yasema usizini,na injili yasema UKIMTAZAMA MWANAMKE KWA ”KUMTAMANI” ni dhambi.KUZINI ni kitendo cha mwilini,na KUTAMANI ni rohoni.Yesu alikuja kutimiliza kwa kuwa torati ilikuwa na upungufu,ni kivuli si kitu halisi. Kwahiyo unaposhika amri kumi ambayo ni torati bado utakuwa na upungufu,maana hata Yesu alisema ”mmesikia kwamba imenennwa,”USIZINI” lakini mimi nawaambia UKITAMANI TU NI UMEZINI. Kushika amri kumi bado utakuwa na upungufu aliousema Yesu,watu wa kale waliambiwa ”USIUE” lakini Yesu alisema kuona hasira tu ni dhambi.Kushika amri kumi ni sawa na bado kuwa na hali yakusubiri mpaka uzini maana kwako hujakuwa na ile hali yakutotamani.

 3. Kumbuka kuhusu sheria, Yesu alisema kwa mwanasheria yule kuwa UMEJIBU VYEMA…. SASA KAMA NA YESU ANAWEZA KUSEMA UMEJIBU VYEMA, LEO LWEMBE ANAKATAA KUWA YESU ALIKOSEA,… DUUUU!! HIYO KALI KAKA. HEBU TAFAKARI TENA … HALAFU UJE.
  KARIBU SANA

 4. Ha ha ha ha haaa!! Wewe unachekesha kaka!!
  Anyway, ni mitazamo tu, lakini ukweli utabakia kuwa ukweli. Kuhusu shheria, hizo ni amri za milele kaka wala hazibadili na wala hazitabadilika. Yesu mwenyewe alizitii na kuzisisitiza sana.
  Luka 10:25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
  26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?
  27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
  28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
  Sasa kama kuishi kunakuja kwa kutii sheria za Mungu, sijui kwako itakuwaje…..!!!

  Kuhusu suala la utatu mtakatifu, nikkikuulizaga maswali huwa unakimbia na wewe siku hizi kama Seleli, au Mathew au Mabinza. Mbiyoooo, mwanaume wewe!!! Teh teh teh… Haya sasa kama wewe unakataa juu yutatu mtakatifu kama nafsi moja ya Uungu, hebu toa fafanuzi ya aya hizi;
  Mathayo 7:21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

  Mathayo 8:21 Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu.

  Mathayo 10:32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

  Mathayo 10:33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

  Mathayo 11:27 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

  Mathayo 12:50 Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

  Mathayo 15:13 Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.

  Mathayo 16:17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

  Mathayo 18:10 Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

  Mathayo 18:19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.

  Mathayo 18:35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

  Mathayo 20:23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.

  Mathayo 25:34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

  Mathayo 26:29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

  Mathayo 26:39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

  Mathayo 26:42 Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.

  Mathayo 26:53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?

  Marko 8:38 Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.

  Marko 10:29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,

  Luka 2:49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?

  Luka 9:26 Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.

  Luka 9:59 Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende nikamzike baba yangu.

  Luka 10:22 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

  Luka 15:17 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.

  Luka 15:18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;

  Luka 16:27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

  Luka 22:29 Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi;

  Luka 22:42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.

  Luka 23:46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.

  Luka 24:49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

  Yohana 2:16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

  Yohana 5:17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.

  Yohana 5:43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.

  Yohana 6:32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni.

  Yohana 6:40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

  Yohana 6:65 Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

  Yohana 8:19 Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.

  Yohana 8:28 Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.

  Yohana 8:42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.

  Yohana 8:49 Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu.

  Yohana 8:54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.

  Yohana 8:56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

  Yohana 10:18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.

  Yohana 10:25 Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia.

  Yohana 10:29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

  Yohana 10:37 Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini;

  Yohana 10:38 lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.

  Yohana 12:27 Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.

  Yohana 12:49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.

  Yohana 14:2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

  Yohana 14:10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

  Yohana 14:11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

  Yohana 14:20 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

  Yohana 14:21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

  Yohana 14:23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

  Yohana 14:24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

  Yohana 15:1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

  Yohana 15:8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.

  Yohana 15:10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

  Yohana 15:15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.

  Yohana 15:23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.

  Yohana 15:24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.

  Yohana 16:15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.

  Yohana 16:32 Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.

  Yohana 17:21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

  Yohana 20:17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
  HAYA;
  Zingatia aya hii ya mwisho;
  1 yoh 5:8 Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.

  Sasa, usilale mbele tena, hebu nifundishe na mimi ili nielewe niachane na utatu mtakatifu huenda kweli niko chaka.
  Kazi kwako mjoli na mtoto wa Baba.

 5. Rafiki yangu Siyi, safari hii umenigusa sana katika tafakari yako, nimekuelewa vizuri sana!

  Unasema, “Mimi najaribu kutafakari sana kwa kina juu ya watu kama ninyi mnaoliasi neno la Mungu …” Basi kauli yako hii kwangu nami imeamsha tafakari ya kina kuhusu watu kama ninyi. Nilichokiona katika tafakari hiyo ni kwamba mmekubuhu katika UNAFIKI!!!

  Tazama unachosema kwa sehemu,
  “Bila kufuata sheria kwa sisi binadamu, ni sawa na kusema vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu vikaidi utaratibu vilivyowekewa tangu uumbaji, halafu uone nini kitatokea…Ukiondoa sheria, ni sawa kusema hakuna maisha!!”

  Basi ni jambo hili ndilo lililonionesha kuwa ninyi mtakuwa aidha ni “ngunguri’ wa UNAFIKI au ni vipofu kupindukia! Ila naona Unafiki ndiyo sifa yenu sahihi, maana ninyi wenyewe kwa ukaidi, ndio vinara wa uvunjaji wa Sheria ya Mungu, zile Amri 10 za Maadili, zile zilizoandikwa kwa Kidole chake Mungu, ambazo ziko na kwenye Hekalu la Mbinguni, halafu mnageuka na kupiga kelele saaana kwamba watu wote wanaoivunja Amri ya Nne watahukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto, basi huo kama si unafiki ni nini??

  Hii hapa Amri ya Kwanza (Kum 5:6-7):-
  “Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.”

  Ndipo nikikuuliza Siyi, kwa huko kuwa kwenu na miungu watatu, yaani Mungu Baba, halafu Mungu Mwana na wa mwisho Mungu Roho Mtakatifu, je, si uvunjaji wa dhahiri wa Amri hiyo ya Kwanza? Mmeziinua Biblia zenu juu mkijisifia kuitii, na hapo hapo mna miungu mingine!

  Pia Maandiko yanasema ukiivunja moja, umezivunja zote; nasi twafahamu kwamba Mungu ni Amri zake, ndio kusema siku zote mnazoendelea katika ibada zenu na maisha yenu yote, mmekuwa mkitembea bila Mungu, yaani, “Ukiondoa sheria, ni sawa kusema hakuna maisha!!” ndiyo kusema ninyi ni WAFU mnaotembea. Umekiona kilichotokea kwenu baada ya kukaidi kuzishika Amri 10? mmekuwa wafu, nao wafu hawajui neno lolote!!!

  Pole saana ndg yangu, lakini iko Sauti ifufuayo wafu wa jinsi yenu, INAKUITA!

 6. Lwembe,
  Mimi najaribu kutafakari sana kwa kina juu ya watu kama ninyi mnaoliasi neno la Mungu kwa kulisingizia kuwa linasema amri zote zilishapitwa na wakati(eti tuko chini ya neema tu). Ninaposema neno la Mungu, mf. mwanzo 1 inaelezea uumbaji wa vitu vyote vilivyoumbwa kwa amri(kauli shurutia). Nikisoma Zaburi 33:6 Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Tena nikisoma mstari wa 9 Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama…. DHANA NINAYOIPATA HAPA, NI KWAMBA, KILA KITU KILIAMRIWA NA MUNGU KIKAWEPO. KITENDO CHA KUAMURU, NI KUTUMIA AMRI/SHERIA KUKIFANYA HICHOKITU KIWEPO AU KIWE KTK HALI UNAYOTAKA.
  Sasa kaka Lwembe, fikiri kidogo, kama mbingu na nchi, jua mwezi, na nyota, anga, maji nk viliamriwa kukwepo na kukaa katika hali hiyo iliyopo leo, mbona vyenyewe havijaasi na kufanya ndivyo sivyo? Ulishaiona dunia inalizunguka jua tofauti na ilivyoamriwa? au ulishawahi kuona kazi ya mwezi/nyota inafanywa na jua au kiyume chake? They are still in order!!
  Leo watuwanasema eti amri kwao tu ndo hakuna!! Kichekesho kweli!!! Watu wanazichanganya sheria za Mungu na zile za Musa(temporal laws) na kuzifutilia mbali zote. Hatari mno!!
  Ujumbe wa agano jipya, huwezi kuuelewa kama hujakaa vizuri kwenye agano la kale. Agano la kale ni msingi wa agano jipya. Huwezi kulielewa agano jipya kabla ya kulielewa agano la kale. Utababaisha tu. Nakutia moyo ujifunze kwanza vizuri sana agano la kale ndipo utaliewa vizuri na agano jipya.
  Sheria za Mungu zadumu milele. Bila kufuata sheria kwa sisi binadamu, ni sawa na kusema vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu vikaidi utaratibu vilivyowekewa tangu uumbaji, halafu uone nini kitatokea…Ukiondoa sheria, ni sawa kusema hakuna maisha!! Najua huenda hujanielewa!!!
  Karibu sana.

 7. Siyi, unaniuliza, “Wewe ukiisoma unaiona kuwa ni mpya kweli?”, Mimi nadhani utakuwa unanionea, swali hilo unayepaswa kumuuliza ni Roho Mtakatifu, maana ndiye aliyeyasema hayo! Ninaamini amekusikia na atakujibu!

  Bali mimi kazi yangu ni KUAMINI yooote aliyoyasema!

  Kama unakumbuka niliwahi kukuambia kuwa jitahidi uliamini Agano Jipya katika mafundisho yake yooote, uyapokee hayo ili UJAZWE Roho Mtakatifu wa kweli, upewe na “kunena kwa lugha” na zaidi ufunguliwe UFAHAMU wa Neno la Mungu, ndipo ukirudi katika Agano la Kale utayaelewa mengi pamoja na sabato na haya uliyoyanukuu bila ujuzi!!

  Karibu ndugu yangu!

 8. Wewe unakielewaje? Akisema si amri mpya kwa vile iko agano la kale, na akisema ni mari mpya kwa vile kaileta kwa mfumo mwingine tu kaktika agano jipya, wewe waiona kuwa ni mpya kweli?? Wewe ukiisoma unaiona kuwa ni mpya kweli?

 9. Hahaha…! Umenifurahisha sana Siyi kwa kuniletea nukuu kutoka kwa mt. Yohana. Unajua Neno la Mungu lina Nguvu sana pale utakapoigundua Nguvu ile ilipo, kama vile nguvu za Samson zilivyokuwa katika nywele zake!

  Hebu nipe tafsiri ya vifungu hivi ulivyovinukuu ili usiniache mbali!
  1 Yohana 2:7 Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.

  1 Yohana 2:8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung’aa.

  Hebu nisaidie, univushe kisiki hiki: cha “siwaandikii amri mpya” halafu tena “nawaandikia amri mpya”

  Ubarikiwe!

 10. Ndg yangu Siyi,
  Haya mambo matatu unayonitaka nikufafanulie, mimi nadhani ungechukua muda kidogo kuutafakari ule mfano wa msafara wa rais, kama ulivyo uleta wewe mwenyewe, ukiwa katika uhuru wa kufikiri, yaani ukiwa umejitoa katika kibano cha mafundisho yenu, ungeliona jambo hilo la Sheria ya Kifalme kwa urahisi sana! Mambo ya Mungu si magumu kama walivyokudanganya. Mungu amejishusha mpaka chini sana, kama nawe unavyojishusha ili uelewane na mwanao wa mwaka mmoja!

  Lakini ngoja nijaribu tena kama itasaidia. Sheria ya Kifalme inafanya kazi ndani ya ukoo wa Kifalme ikiwaongoza. Pia huwezi kuwa Mfalme bila subjects, yaani watwana. Sheria za Maadili, kama unavyoziita, hizo huwatawala na kuwaongoza watwana. Rais anapotoka na msafara wake, ile Sheria ya Kifalme ndiyo inayomuongoza. Ndipo king’ora hupigwa, ikiwa ni ishara ya Upendo kwa raia wake waondoke barabarani wasidhurike na huo msafara kutokana na kasi au chochote kile. Nayo Sheria ya Maadili imewafunza watwana kusimama mpaka Mfalme apite! Akiwepo mjeuri kama Siyi, basi wale “malaika” walinzi wa sheria hiyo ya Maadili, humkamata huyo na kumpeleka ahukumiwe!

  Maandiko yanapotufunza kuwa Kristo ndiye mwisho wa sheria, tunapaswa kuamini hivyo, ndipo Mungu huwajibika katika kulifunua hilo tuliloliamini. Mungu ni Neno lake, nimefurahi kuwa nawe umekiri hivyo, hata kunikosoa na kunifunza, ukiniweka sawa: “Neno la Kristo maana yake ni BIBLIA. Neno la Mungu. Maana Kristo ni Mungu.” Sasa kama Kristo, huyo aliye Neno la Mungu, anapotuambia kuwa “Yeye ndiye mwisho wa sheria”, yaani Sheria hiyo anayosema yeye ndiye mwisho wake au ukomo wake, ni hiyo Torati ambayo imewaongoza Israeli tangia walipotoka Utumwani huko Misri na sasa wakitengwa kwa ajili ya maisha mapya; Je, itakuwaje kwa makundi yetu sasa bila Torati ile tuliyoambiwa ni Agano la milele? Inataka ufunuliwe jambo hilo. Mungu akupe kulielewa. Kama Mungu amesema Kristo ndiye mwisho wa Sheria, hiyo yenye kubeba laana, hivyo ndivyo ilivyo! Yeye Kristo ni MWISHO WA SHERIA; basi huyo akiwa ndani yangu, au nikiongozana naye kama wale wanafunzi wake siku ile walipovunja masuke na kuyala siku ya sabato, hilo hudhihirisha ukomo wa sheria hiyo, na mwanzo wa Sheria Mpya ya Kifalme.

  Halafu jaribu kuchunguza ili ujiweke sawa katika ufahamu, watu wengi hudhania neno “forever” au “forever and ever” ni sawa na “eternity.” Nimewasikia watu wakitufundisha kuwa moto wa Jehanam ni wa eternity! Na ni katika context hiyo hiyo nanyi huichukulia sabato, katika maana ya ile amri ya nne kuwa amri hiyo ni ya eternity, na hivyo kuukosa uelewa wa jambo hilo. Lakini milele, yaani forever, ni kipindi cha muda unaokomea mahali fulani tu, yaani kutoka point A hadi B katika wakati. Jehanamu ina muda wake wa kuwakirimu wapendwa wake, baada ya hapo itatoweshwa, kama ilivyotoweshwa Torati katika ujio wa Kristo! Eternity maana yake “Bila Mwanzo wala Mwisho”; kwahiyo kama Hell ni eternal, jambo hilo lingeyavuruga Maandiko! Au lile Fundisho la Kikatoliki lililosambalia katika madhehebu yetu, likiuthibitisha Uungu wa Yesu Kristo, ile Nafsi ya Pili ya Mungu, ambalo linasema, ‘Jesus Christ is the Eternal Son of God”, likituleta katika kuamini kuwa ‘Uana wa Mungu’ wa Kristo hauna Mwanzo wala Mwisho, jambo ambalo si kweli!

  Unaona ndg yangu, uongo wa kidini umesambaa sana kama kansa ya damu ndani ya kanisa, ni vizuri kuyapitia pitia mafundisho yetu ili kuwa na uhakika kama ni Neno la Mungu!

  Ubarikiwe!

 11. Nami ngoja nioneshe zaidi,
  Sitatoa majibu, ya moja kwa moja lakini nitakupa assignment na wewe ya kujifunza hizo Sheria za Maadili(Moral Laws) Ndani ya Biblia, hakuna hiyo phrase nzima ya Sheria za Maadili, but ukijifunza hata wewe binafsi, utagundua kuwa kuna aina za sheria ndani ya Biblia.
  Nina uhakika, utakutana na sheria za maadili kama mojawapo ya aina za sheria hizo ndani ya Biblia.
  Ni kweli unaweza ukawa unajitahidi kuzitii sheria hizo ijapo unaweza kupungua ktk moja au mbili kwa shingo ngumu, kibiblia, utakuwa umezikanyaga zote. Watu wengi hufikiri wana Mungu ktika maisha yao pindi wanapoona miujiza na matendo makuu yakitokea. Ukweli ni kwamba, hivyo sivyo vigezo pekee vya kujihesabia haki mbele za Mungu na kujiona kuwa uko kwenye njia sahihi. Ktk historia za biblia, hata ibilisi naye, alifanya maajabu na miujiza mingi kwa baadhi ya watu hadi wakaamini kuwa wana Mungu wa kweli kumbe wana baal tu. Chunguza vizuri kama unazitii sheria zote za Mungu-sheria za maadili-amri 10.
  Na ukigundua kuwa umepungua ktk mojawapo au mbili….. mwombe Mungu akusaidie na wewe uchukue hatua ya kuzitii zote. Kwa nguvu zako wewe utakesha, huwezi!! Utakuwa farisayo tu, mtu wadini…. But ukiruhusu RM aingie ndani yako, sheria za Bwana siyo nzito.
  Ubarikiwe.
  Nakusubiri kwa ahadi ya uchanganuzi wa maneno yetu yaleee

 12. Aise ngoja niulize zaidi !
  Siyi hilo neno ”sheria za maadili” liko kabisa kwenye bible au ni ufafanuzi wa walimu baada ya kuona fungu fulani la sheria linahusiana na maadili?

  Kwani kuna ipi ambayo sisi hatuitii bwana Siyi? Maana kama tungekuwa hatuzitii tusingeweza kuwa tuna tembea na Mungu na kupata uwezo wa kumshinda shetani na dhambi kama tunavyoshinda.

  Usijali nitakutofautishia hayo maneno Siyi!

 13. Hello kaka Mkandya,
  Shalom mtumishi? Nimefurahi sana kaka, umenipa changamoto nyingine ya kutaka kujua kwa kujifunza zaidi tofauti iliyopo kati ya chuki na hasira!! Sasa kwa vile wewe unafahamu vizuri, unaweza kunitofautishia kati ya maneno haya mawili kibiblia na kimaana za kawaida tu? Ni kweli naona kama kuna tofauti hiyo, but hebu nijuze kiundani kaka. Nitashukuru sana.
  Kuhusu sheria za maadili, siziiti mimi kaka. Bali Biblia ndiyo inayoziita hivyo na ndiyo inayosema kuwa, zipo hadi mbinguni. Na mbinguni wanaishi kwa kufuata sheria hizo!! Ndiyo maana lucifer aliposhindwa kuzitii, aliondolewa kwenye himaya hiyo ya mbinguni. Hata wewe mkanda na wengine msipozitii hizo sheria, hakika yake ni kupotea tu. Nadhani umemsoma mtume Yohana vizuri, na umemwelewa. Kilichobaki ni wewe kufanya uamuzi sahihi kaka. Kuchagua nuru au giza.
  Barikiwa

 14. Hello ndugu yangu Siyi,
  Sijui kama unajua kuwa kuna tofauti pana tu kati ya chuki na hasira.
  Haisira kama hasira si dhambi kama unavyojaribu kusema. Ndio maana katika kueleza kwako umejikuta unaongelea chuki ukidhani unaongelea hasira.

  Kuwa na hasira siyo kuwa ndiyo dhambi bali matokeo ya hiyo hasira, hasa kama huyo mtu atakuwa mpambavu mwenye kuibeba hasira katika kifua chake.

  Ivi Siyi hizo sheria unazoziita za maadili mpaka mbinguni wanazo, kwamba na wao wanatakiwa kuishi kwa kushika sheria hizo?

  Lwembe ulijibu vizuri sana ule mfano wa raisi na sheria za barabarani, ubarikiwe.

  Amina.

 15. Ubarikiwe na Bwana Lwembe.
  Nimefurahi kuniletea somo zuri la kutoa na kujumlisha. Kwa kweli umenikumbusha mbali sana. Hata hivyo kuna mtu mmoja alishawahi kulichambua somo hili, japo si udadavuzi wa kina, lakini amejaribu kidogo. Leo nitakurushia wewe na wengine, mlisikilize mlete mchango yenu.
  Aidha, nakuona pia unachanganya vitu viwili hapa. Neno la Kristo. Unarejea neno la Kristo kwenye vitabu vya mitume…. Halafu haohao ndiyo waliopewa neno hilo!!! Labda nichabgie kidogo hivi, Neno la Kristo maana yake ni BIBLIA. Neno la Mungu. Maana Kristo ni Mungu. O course, mitume ndio waliopewa neno walisambaze/kulihubiri, lakini hawana mamlaka ya kulibadili!! Hawana mamlaka ya kulipunguza wala kuliongeza. Sasa kama walipewa na kazi yao ikawa na kulisambaza/kulihubiri, nini sasa kinachokuchanganya hadi unapotea wewe?? Tuseme wewe Lwembe, unalijua neno kuliko mitume? Ha ha ha haaa!! Mbona hulifuati kama walivyolifundisha mitume? Ngoja nikupeleke kwa mtume mmoja tu aliyekuwa na Kristo uso kwa macho…
  1 yoh 1: 1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;
  2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
  3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
  Umemwona huyo jamaa(yohana) anavyosema? Yeye alisikia, yeye aliona, akapapasa nk. Ndiye anayetuambia sasa. Unayaamini maneno yake kama mtume wa Kristo?
  Angalia tena mistari hii ya 1yoh1.
  8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
  9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

  Lwembe huyu ni miongoni mwa wanafunzi wa Yesu. Tena alikuwa ndg wa Yesu damu. Leo anatusimulia na kutufundisha alichokisikia kwa Bwana wake, ndg yake.
  Anaendelea kusema, (JITAHIDI USOME AYA ZOTE KWA MAKINI SANA)
  1 Yohana 2:3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

  1 Yohana 2:4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.

  1 Yohana 2:7 Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.

  1 Yohana 2:8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung’aa.

  1 Yohana 3:22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

  1 Yohana 3:23 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.

  1 Yohana 3:24 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.

  1 Yohana 4:21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.

  1 Yohana 5:2 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.

  1 Yohana 5:3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

  2 Yohana 1:4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.

  2 Yohana 1:5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.

  2 Yohana 1:6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
  Umeona HAYA MAMBO yalivyo rafiki yangu? Ukisema kuwa chini ya NEEMA, hii ndiyo habari yake ya kwamba, WAMPENDE MUNGU-2yoh 1:4 na kuwapenda ndg zao 1 yoh 3:23 nk. Sasa kuwa chini ya NEEMA kunakokufanya uzikanyage sheria za Mungu, umekutoa wapi? Kati ya mimi na wewe, unafikiri ni nani atarudishwa na SONARA, eti dhahabu yake ina kutu? Unajua unatia huruma sana kipenzi changu Lwembe!!
  Najua una uelewa mkubwa sana rafiki yangu. Tafakari haya, ulinganishe na hicho unachokielewa na haya maneno ya Yohana. Ndiyo maana huwa nakwambia rafiki kila mara, kwamba, changamka. Nafasi bado ipo rafiki yangu… Acha kusinzia!!

  Kuhusu wanawake kulihubiri neno mimbarini, binafsi sina uelewa wa kutosha juu ya hili. Ninachoelewa ni kwamba, sisi sote(wanaume na wanawake) tumepewa kazi ya kuhubiri injili ya Kristo. Habari ya mipaka ya maeneo kwa kuangalia jinsia hapo kwa kweli sielewi rafiki.
  Kitu kingine ninachojua kuhusu wanawake, hawapaswi kuwa wachungaji, maaskofu, makasisi, wala wazee wa makanisa. Hawapaswi kuwa na mamlaka yoyote ndani ya kanisa la Mungu. Ila kwa habari ya injili, hapo tamko la Yesu enendeni, halikubakiza jinsia ndiyo maana hata ukiangalia kwenye nyaraka za mitume, utakuta wanawake wakishughulika na uinjilisti. Anyway, nitafurahi kujifunza kutoka kwako pia kama una nuru zaidi rafiki yangu.
  Karibu sana.

 16. Lwembe
  Nashukuru kwa kuniona kama najaribu kuusogelea wokovu. Na hii ndiyo adhima yangu. Kwa vile sasa ni mchanga, hatimaye nitafurahi kuufikia ukamilifu. Maelezo yako ni mazuri. Sasa naomba unieleze;
  1. Maana ya sheria ya kifalme na ufafanuzi wake.
  2. Unipe tofauti iliyopo kati ya sheria ya kifalme na sheria za maadili?
  3. Hivi, unapompenda Mungu, ni matokeo ya utii wa sheria za maadili au sheria ya kifalme?
  Natamani kujifunza katika haya kutoka kwako.
  Ubarikiwe na Bwana.

 17. Siyi!
  Hauko mbali sana na ukweli, ingawa wewe mwenyewe hujui!
  Hebu tuliza munkali wa ubishi, irudie tena kauli yako hii pole pole:
  “Au ingekuwaje, rais anapopita barabani-msafara wake usivyozingatia sheria za barabani, kuwa baada ya rais kupita tu na watu nao wasizingatie sheria hizo za barabani kisa rais kapita bila kuzingatia sheria? Hiki ndicho mnachong’ang’ania ninyi akina Lwembe!!!”

  Haleluya! Siyi sasa hivi umefunguka! “rais anapopita barabani-msafara wake usivyozingatia sheria za barabani”; hii ni kweli kabisa, sheria za barabarani huwa hazimuhusu kabisa si kwamba anazivunja! Hizo tumewekewa mimi na wewe ili zituongoze kwa kukosa kwetu Upendo! Au haujaona kwenye makutano ya barabara, taa za kuongozea magari zikiwa zimezima na askari hayupo, jinsi madereva wanavyo lazimisha kupita, kila mmoja akimzuia mwingine asipite mpaka yeye apite kwanza, na wakati mwingine magari huishia kugongana na kusababisha jam kubwa zaidi!

  Basi, rais anatawaliwa na Sheria ya Kifalme ambayo watumwa hawaielewi, maana si yao, “Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.” Yak 2:8. Bali watumwa, hao huitii Sheria hiyo ya Kifalme, kwa kuzitii zile sheria za maadili zinazoambatana na adhabu! Walioingia katika Neema, hao ndio wako katika hiyo Sheria ya Kifalme, yaani Roho Mtakatifu! Basi hicho ndicho tunachong’ang’ania ndg yangu Siyi, sisi ni marais, sheria za maadili hazituhusu, sisi ni wale tulio katika Sheria ya Kifalme!

 18. Kimo cha mtu mkamilifu: 2Petro 1:5-7
  “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.”

  Msingi unaokibeba kimo cha mtu huyo ni IMANI!! Nayo Imani twafahamu huja kwa kusikia, nako kusikia kwaja kwa Neno la Kristo. Basi Neno la Kristo walikabidhiwa nani, askofu mkuu wangu, au nabii na mtume wangu, au mchungaji wangu, ni nani haswa aliyekabidhiwa? Walikabidhiwa mitume, hao ndio wanalo lile Neno safi na pure! Ni Neno hilo pekee liwezalo kukupa KUSIKIA ili Imani izaliwe ndani yako kwanza, ndipo juu ya msingi huo imara, pajengwe Wema, na juu yake Maarifa, halafu Kiasi, na juu yake Saburi, kisha Utauwa, na mwisho kukikamilisha kimo hicho, panajengwa Upendano wa ndugu; Basi huyo aliyesimama mbele yako, aliyejengeka katika kimo hicho, huyo anaitwa UPENDO, yaani Kristo, ule MWILI wake!!!!!!!!

  Kwahiyo unapozungumzia dhambi na Mkristo, unapaswa kuli reflect jambo hilo kwa mtu aliye katika kipimo hicho, huyo “Upendo”. Huyo ndiye ile kazi ya Msalaba iliyokamilka!

  Sasa iwapo mtu amelisikia Neno lililochanganywa na hekima ya kibinadamu, ambayo imeligawa Neno kwa kulichanganya na mitazamo yao, labda mchanganyiko huo umewapelekea kuitilia shaka Injili waliyoihubiri mitume, kama vile inaposema “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha”, halafu kwa hekima yao, wakawaruhusu wanawake kufundisha, na wengine wakatawaliwa na wanawake manabii, basi ni dhahiri kuwa hao watakao lipokea neno hilo mchanganyiko, ndani yao haitazaliwa Imani kamilifu kulingana na kigezo kilichowekwa, maana kusikia kwaja kwa Neno la Kristo na si mchanganyiko! Wengi wetu tunaishia kuwa na mfano wa Imani, ambayo haina uwezo wa kuvibeba vipawa hivyo sita, ambavyo kwa uzito wake, maghorofa yanaanguka kila kukicha; dhehebu fulani limemeguka, waanzilishi wamegombana, wengine wamedhulumiana, mwingine naye kapata kipawa kaondoka kwenda kuanzisha lake!

  Shida kubwa iko katika ile dhahabu ya kuchovya! Si kwamba eti inapauka upesi, au kwamba kwa kuiona tu waweza kuigundua kuwa ni ya kuchovya, la hasha, muonekano wake ni wa dhahabu kamili, na ukiitunza vizuri unaweza uka kaa nayo kwa muda mrefu sana, wakati mwingine maisha yako yote, maana kila unapokwenda kwa wale wauzaji, iwe ni jumapili au sabato au saa kumi na moja alfajiri ya kila siku huko Pool of Siloamu, wao huipolishi na kuiongezea mng’ao; mpaka siku utakapotaka kuibadilisha iwe pesa! Naye Mbadilishaji huwa HABADILI mpaka AIPIME kwanza!!

  Basi ukifika kwa Sonara, ndipo unamkabidhi kito chako cha thamani, ile IMANI uliyoitunza maisha yako yote, ukijua kuwa itakusaidia, na sasa wakati huo ndio umefika. Haya, lete hiyo Imani yako:

  SIYI: “Namwamini Mungu mmoja mwenye Nafsi Tatu zinazounda UTATU MTAKATIFU; ambazo ni Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Watatu hawa si jinsi ya mtu mmoja bali ni watatu walio tofauti lakini wote ni Mungu mmoja!”

  SONARA: “Umekuja na kito hiki tu?

  SIYI: “Ninako na haka kengine, haka hapa, ‘Ninaamini kwamba yule mwanamke mchawi alimpandishia Sauli mzimu uliojifanya kuwa ni Samweli, kwahiyo hata ule unabii uliotolewa licha ya kwamba ulitimia mimi siuamini kabisa, itakuwa Msimulizi wa tukio hilo alijichanganya!”

  SONARA: Vizuri, subiri kidogo tuvipime. (Baada ya kuviingiza katika Kipimo, BIBLIA, anauliza), Unayo risiti uliyonunulia vito vyako?

  SIYI: (Kwa furaha kubwa anatoa machapisho yao aliyopewa yenye hayo mafundisho akitegemea kuvuna pesa), Hii hapa!

  SONARA: Ndio maana! Vito vyako ni vyuma vilivyochovya katika dhahabu, hatupokei, maana havina thamani yoyote, labda urudi kwa hao waliokuuzia. Unaona, wamevichovya tu kwenye Biblia, lakini ndani ni chuma chenye kutu! Pole sana ndg yangu!!

  Sonara anakurudishia mavito yako!!! Nawe ukitoka hapo unamcheeeka Sonara yule, kuwa hujawahi kuona Sonara asiyeijua kazi yake kama huyo, amekataa vito original!!!

 19. Lwembe,
  Kibarua ulichonipa ni kikubwa sana. Lakini itabidi nikifanye tu kwa malengo ya kujifunza na mimi. Huenda nitachota vitu huko. Nitakuijia mtu wa neema isiyokuwa na sheria. ha ha ha haaaa!!
  Hebu fikiria, hivi ingekuwaje Tanzania tungekuwa tunaishi bila sheria? Au ingekuwaje Rais wa nchi anapotoa msamaha kwa wafungwa fullani, halafu hao wafungwa wakishatoka nje ya gereza, wanaanza kuiba, kuua nk maana hawako chini ya sheria-rais kawapa neema/rehema? Au ingekuwaje, rais anapopita barabani-msafara wake usivyozingatia sheria za barabani, kuwa baada ya rais kupita tu na watu nao wasizingatie sheria hizo za barabani kisa rais kapita bila kuzingatia sheria? Hiki ndicho mnachong’ang’ania ninyi akina Lwembe!!! Nanyi mnaona mko sahihi kabisa!!! Kah!! ha ha ha haaa
  Kama tunavyoishi kwa sheria nchini Tanzania/duniani, kadhalika na mbinguni kuna sheria-sheria za maadili/amri 10. Usidanganyike kijana.

 20. Mkandya,
  Nakushukuru kaka kwa kurudi tena baada ya kupotea sana kwa muda mrefu. Aidha, niseme tu kuwa, kama imeonekana nashambulia mtu badala ya hoja zake, basi utakuwa ni udhaifu wangu ambao inabidi niurekebishe mara moja. Niombee pia. Hata mimi sipendi kushambulia mtu, kudharau mtu, kubeza mtu au kumfanyia lolote lisilofaa mbele za Mungu na wanadamu pia. Baada ya kusema hayo, niende sasa kwenye maswali yako kaka, japo umeniambia niwe naandika kidogo tu badala ya kuandika mikeka mirefuu. Nitajitahidi ndg yangu…
  Naona hoja yangu ya kuwa kila aliyezaliwa na mwanadamu ni mdhambi umeipinga. Nikiri kuwa, mtu anapompokea Kristo, kiuhalia hubadilika na kuwa ni kiumbe kipya. Ya zamani, huisha na mapya huanza kwenye ukurasa wake. Hoja yangu ya kusema mimi na wewe bado ni wadhambi tunaohitaji rehema za Mungu, haikuwa na maana kwamba nilkuwa nafutilia mbali kafara ya Kristo pale msalabani. Nilichokuwa najaribu kusema hapa, ni kwamba, mtu anapompokea Yesu, ninyi mnaita kuokoka, kuna hatua Fulani ambazo mtu huyu hupaswa kuzipitia ili aufikie ukamilifu(kuwa mwana wa Mungu halisi) asiye na dhambi hata tone.
  Hatua hizo ziko tatu. Lwembe alijaribu kuzidonoa siku ile, nikamwomba azielezee kidogo but amelala mbele tena na kuniletea links tu nisome. Sijui nitamaliza lini!!!
  Napenda nidonoe ile hatua ya tatu, hatua ya UONGOFU. Katika agano la kale, hii ni hatua iliyofikiwa na akina Henock, Ibrahimu, Eliya, Elisha, vijana watatu wa kiebrania wa Daniel 3 nk. Kwenye agano jipya, utawakuta akina Stefano, na mitume wote wa Yesu katika hatua za maisha yao ya mwisho. Ndiyo maana hadi leo, wamepewa sifa ya wafia dini. Kabla ya hapo, ukifuatilia maisha yao, yalikuwa ni maisha ya kuanguka na kusimama-yaani maisha ya kuomba msamaha wa dhambi kwa Kristo kila wakati. Kama utazihitaji hizo hatua zingine mbili za awali, sema nikupatie, japo nilishawahi kudondoa kwenye mjadala huu na ule wa kutanguliwa kwa torati. Unaweza kurejea.
  Hivyo basi kusema kuwa mtu anapompokea Kristo tu tayari hana dhambi, ni sahihi kwa maana hii; dhambi zake zote za mwanzo hufutwa. Lakini bado hubakia na ile hali ya uovu iliyo ndani yake yaani asili ya dhambi. Uovu ndio unaosababisha mtu kutiwa unajisi-yaani kuwa na mawazo mabaya, tamaa mbaya, nk ambayo kibiblia hasa kwa mujibu wa agano jipya, mambo haya, ni dhambi tayari.
  Hivyo kaka, mtu anapozidi kukua ktk Kristo, daima huwa ni mtu wa kuanguka na kusimama…hadi atakapofikia ukamilifu-UONGOFU. Na uongofu huu huja kwa muumini anapojikabidhi kwa Kristo saa zote. Kwa hiyo naweza kukubaliana na wewe kuwa, inawezekana leo tukawa na watu waliofikia UONGOFU kwa maana ya kufikia hatua ya kutowaza hata mabaya kabisa-yaani kutembea na Mungu saa zote, japo kundi hili linaweza kuwa ni la watu wachache sana. Na wengine waliosalia, wako kwenye zile hatua mbili za awali. Changamoto kwangu na wewe, je, tulishafikia hatua ya UONGOFU? Kama, bado, tuchangamke kaka.
  Na habari za kuwa hasira, hiyo ni dhambi tayari. Ni sawa na mtu anayetamani mke wa mtu, kibiblia huyo tayari ni mzinzi. Hii ni Biblia na siyo maneno ya Siyi. Haya soma baadhi ya aya hizi; 1 Yohana 2:11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.

  1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
  Unaona sasa kaka? Unafikiri kuna usalama unapomchukia ndg yako? Kwani uuaji siyo uvunjaji wa sheria za Mungu-Usiue?? Na ile ya kutamani, ni Mathayo 5:28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
  Nafikiri umeelwa hapa.
  Kuhusu sabato na sheria zingine kwa akina Ibrahimu, jaribu kupitia makala yangu niliyoirusha kwenye mjadala wa torati kutanguliwa. Huko nimeonesha UWEPO WA AMRI KUMI ZA MUNGU KABLA YA MLIMA SINAI-YAANI TANGU ADAMU. Soma huko kaka utapata majibu yake vizuri.
  Na kuhusu majina ya Baba, Mwana na RM, jaribu kupipta makala zangu juu kidogo kwenye mada hiihii. Utayaona kaka.
  Ubarikiwe sana.
  Karibu tena

 21. Ha ha ha ha haaa!! Sikucheki Lwembe, Nacheka maneno yako tu!!! Naandaa majibu ya hoja zako. Naona hutaki kabisa kuleta majibu ya maswali yangu yaleee. Badala yake unanipa link tu. Najua kuwa wewe unapokuwa huna majibu kwa wakati huo, huwa unapinga chengaa weeee, mpaka utakapopata hayo majibu. Lakin pamoja na hayo, wewe endelea kukusanya nguvu na uelewa wa Biblia but utaishia kwenye hoja ya Mungu mmoja katika nafsi tatu. ngoja nipiptie link hizi kwanza
  Ubarikiwe

 22. Mkandya, mwalimu wao akina Siyi, Lenda na Nashon alipo safiri, aliwaacha kwenye somo la sabato na sheria za maadili na Amri kumi alizoandika Mungu mwenyewe kwa kidole chake ambazo ziko kwenye Hekalu la mbinguni! Kwahiyo kwa kadiri utakavyo ongea nao, basi wao huwa kama santuri iliyochubuka na hivyo ifikapo sehemu hiyo hujirusha nyuma na kuanza upya wimbo wa sabato na sheria za maadili na habari hiyo ya kidole cha Mungu, utadhani sio Musa aliyewasimulia!

  Ukisikia PASUA KICHWA, ukitaka klijua hilo kutana na CULT member, hata akiwa mlei!!!

  Ila mimi nimemzoea rafiki yangu Siyi, aliwahi kunihubiria kuwa Yohana Mbatizaji alihubiri Injili kabla ya Yesu kuzaliwa!!! Ndio maana najaribu kumshawishi aje kanisani kwetu tumpe uchungaji au akileta mafunuo safi, basi atakuwa mtume na nabii Siyi! Hahahahah….!

 23. Siyi, acha uoga mtoto wa kiume! Link tuliwekewa na moderator kwenye mail siku nyingi, ila wewe kazi yako ni kujifanya huzioni! Nakumbuka uliwahi kuniambia kuwa wewe huwaga unapata mafunuo, njoo nayo basi huku kwenye hizi links!!

  Kwa mfano ule ufunuo wako wa UTATU MTAKATIFU wa Kikatoliki ulioniambia kuwa ni : Mungu Baba, Mungu Mama na Mungu Roho Mtakatifu, kwa kadiri nilivyoutafakari, nimeona hata ninyi hamko mbali sana na Utatu huo kwani nanyi mnaye Mama Ellen ambaye kwenu ninyi nafasi yake ni sawa na ya Mama Maria. Kila alilolisema mama Ellen kwenu ni Neno la Mungu, haijalishi Biblia inasema nini!

  Haya Siyi, link hizi hapa nimezikopi kutoka kwenye mail zako, tafuta kisingizio kingine!

  https://strictlygospel.wordpress.com/2012/02/27/mtu-asipozaliwa-kwa-maji-na-kwa-roho/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2008/07/16/swali-8/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2009/11/02/mwingira-afunuliwa-ubatizo-mpya/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2013/01/21/ubatizo-kwa-watoto-wadogo/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2012/02/09/utatu-mtakatifu/

  Asante Siyi

 24. Unajua rafiki yangu Siyi, kusema kweli mimi naona aibu juu yako. Kwanza najua kuwa wewe ni mtu mzima tena unatoaga ushauri kanisani kwenu, lakini kwa hizi “off”, inaonekana umerudi, umekuwa mtoto mdogo, halafu utakuwa ni wale wenye akili lakini wanafeli kwa kuendekeza kiburi kwa walimu wao!

  Kiburi huondoa ufahamu, hebu angalia ufahamu wako ulivyojilock huko nje, unasema, “Wewe mwalimu anakwambia kuwa formula ya pai ni 22/7, wewe unasema inaweza kuwa 21/7, hivi bado kweli utakuwa mwanafunzi mzuri wewe? Hatima yako utafeli tu mtihani.”

  Sasa tukiuchukua huo mfano tukauleta katika uhalisi wa jambo tunaloliongelea, hapa tutapata picha kamili ya hatima ya mwanafunzi huyo, ambaye kwa leo utakuwa ni wewe Siyi, ambaye unaonekana umelielewa vizuri somo!

  Haya, tumepewa Pai kuwa ni 22/7 ambayo kulingana na Biblia hiyo ingekuwa ndiyo ile Mt 28:19 “… mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu”

  Sasa imefika saa ya mtihani, jibu ulilolitoa ndio hili hapa: “Siyi anamwabudu Mungu mmoja mwenye nafsi tatu. Baba, jina lake ni YAHWE, Mwana, ni Yesu, na RM linabaki vilevile”, ambavyo ni dhahiri kuwa umebatizwa “kwa jina la YAHWE, na la Yesu, na la Roho Mtakatifu”!!! Hii ndiyo ile Pai 21/7, …hahahahahahaha…!!!

  UMEFELI MTIHANI WA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU; “… Ondokeni kwangu”!!!

 25. Siyi kuna kitu huwa nakuambia mara nyingi, kuwa unaandika maneno mengi sana ambayo kwa kweli huwa yamejaa utupu mwingi, na yanachosha kusoma. Punguza kumshambulia Lwembe badala yake ushambulia hoja zake kwa hoja.

  Nami ngoja niseme kidogo kuwa kusema kuwa ulichokisema kuhusiana na Rumi 7:15-20, umepotosha. Kama wewe unaijua vizuri fasihi andishi utagundua tu kuwa Paul alikuwa anajitumia yeye kama mfano kumwelezea mtu ambaye ni mtumwa wa dhambi, na wala si kwamba alikuwa anasema yeye ndiye mtumwa wa dhambi.

  Na unaposema kuwa kila mtu ni mdhambi hujui unachosema. Mtu anapoungama dhambi zake anakuwa si mwenye dhambi tena bali mwenye haki. Sasa kama dhambi bado inaendelea kukaa ndani ya huyu aliyeziungama dhambi zake na kuziacha, basi kazi ya msalaba ni bure. Kwani nani alikwambia kwamba kuwa na hasira ni dhambi, basi na Mungu ana dhambi maana ya yeye kuna wakati huwa ana hasira. N a tena kwa nini unalazimisha kuwa kila mtu ana chuki na ana mawazo mabaya. Kwa taarifa yako Siyi wengine hawana hivyo vitu.

  Halafu sijui kama unajua kuwa wewe umeshakuwa mtumwa wa sabato, yaani imekuwa kwamba wewe uliumbwa kwa ajili ya sabato wala si sabato kwa ajili yako. Siyi suala la sabato tuliwajibuni vizuri sana wewe na Lenda, lakini naona katika hoja zako hata huonesha kwamba tulikujibu hoja zako na ukakaa kimya.

  Ivi kweli kwa ujasiri unasema kuwa Adam na akina Ibrahim nao walitunza siku ya sabato ya Jumamosi au amri kumi kwa ujumla? Hebu nioneshe mimi kwa mfano, mahali ambapo Ibrahim aliitwa mzinifu, maana alikuwa na wake zaidi ya mmoja au mahali ambapo alikwenda kusali Jumamos siku ya sabato.

  Kwa suala la ubatizo wewe unasema unabatiza kama Yesu alivyosema, yaani kwa jina la baba, na mwana na roho mt. Ok, jina la mwana tunalijua ni Yesu. Je jina la baba ni lipi na la roho mt. ni lipi? maana ni kweli baba, mwana na roho mt. ni sifa.

  Anyway, Siyi punguza uandishi wa kumshambulia mwingine kwa vichejo na dhihaka kana kwamba wewe unachokisema ni sahihi mno,hata wewe mengi unayoyasema hupatii kama unavyodhani unapatia

  Asante.

 26. Kaka Lwembe,
  Bwana akubariki rafiki. Najua saa yaja utaelewa tu. Umejibu hoja zangu out of contxt kabisaa. Yaani kutaja sheria za kafara tu, tayari nimekuwa mtu wa sheria!! Sheria za kafara!! Mmh, kama bado niko kwenye sheria za kafara, sina haja ya Kristo, jambo ambalo sivyo. Sheria za kafara zilikuwa kivuli cha Kristo. Dhambi zilizokuwa zikisamehewa, zilikuwa zikiondolewa kabisa, japo wadhambi hao mara nyingine walikuwa wakijikuta wamezirudia tena. Na wanapozirudia dhambi hizohizo ama zinazofanana na hizo, iliwalazimu kutafuta mnyama wa kafara kwa ajili ya msamaha tena. Kwani hili nalo ni gumu kulielewa? Kwani wewe Lwembe, hujawahi kuwa na udhaifu ktk jambo fulani, na kwa hilo ukaanguka zaidi ya mara moja, japo sasa huenda ulishapona? Hali hiyohiyo ndiyo ilikuwa ikiwatokea waisrael. Sheria za kafara, Yesu alikuja kuziondoa. Ndiyo maana leo hatuna haja ya kuchinja mnyama ili tuondolewe dhambi. Damu ya Kristo yatosha! Tunapoanguka dhambini, saa yoyote, hatuna haja ya kugharimika kutafuta mnyama wa kafara au kulipa fedha/sadaka kwa padri/mchungaji eti atuombee sala ya toba, badala yake tunamwendea Kristo sisi wenyewe mwanakondoo wa Mungu ili atusafishe dhambi zetu zote. Na kama ukitenda dhambi hiyohiyo ama nyingine, huna budi kurudi tena kwake. Ndiyo maana nikakwambia kuwa, pamoja na kwamba tulishampokea Kristo, bado asili ya dhambi imo ndani yetu, NOTE, siyo dhambi ya asili!! Tu wakristo, but sometimes tunaweza kudanganya, kuiba, kushuhudia uongo, nk. Na dhambi hizi, sharti tukatubu kwa Kristo.
  Tatizo lako wewe, unafikiri dhambi hazipo kwa sababu, unakwepa kukubali kuwa SHERIA ZA MAADILI bado zipo. Jiulize, kama kweli sheria hazipo, mbona kuna maovu mengi leo ndani na nje ya kanisa? Tunayatambuaje kama si kwa kutumia kioo-amri 10 za Mungu? Unatia huruma mwanaume wewe!!
  Na kama unadhani wokovu hupatikana kwa mtu kuwa rohoni bila ya kudhihirisha kwa nje yaliyo rohoni, UMEPOTEA KWELI NDG. Neno likiwa rohoni, sharti matunda yake yaonekane kwa nje. Acha kuchanganyikiwa, kugeuza maandiko na kujifariji kwa kupumbaa!! Utapotea wewe!!
  Kuhusu utatu kaka, sijawa mwepesi kuamini fundisho, but nimekuwa mwepesi kama nini kuiamini Biblia. Tafsiri yako ndiyo inayokupotosha. Nazidi kusikitika kuwa mpaka sasa na wewe pia kama Mabinza, bado unalala mbele kujibu hoja zangu juu ya UTATU!!! Unapiga chenga weee twende kwenye link, link wapi kaka?? Kama siyo usanii tu?, si ungeionesha hiyo link? Imani yako wewe na Mabinza, yaani mnatia huruma kweli wajoli wa Bwana. Watu makini, lakini mnatia huruma sana juu ya hayo mnayoyaamini.
  Na kuhusu dhambi na Paulo, hata mimi najua kuwa Paulo alikuwa mwalimu na sifa nyingi unazoweza kuzitaja. But naona napo unachenga weee!! Almradi tu Biblia ikubali mawazo yako dhaifu. Ha ha haa!! Pole sana. Wewe mwalimu anakwambia kuwa formula ya pai ni 22/7, wewe unasema inaweza kuwa 21/7, hivi bado kweli utakuwa mwanafunzi mzuri wewe? Hatima yako utafeli tu mtihani. Na hii ndiyo hatima yako kaka, utapotea kabisa usipoangalia. Changamka nafasi bado unayo.
  Pamoja na ubishi mwingi, nashukuru huwa unaelewa japo huwa hutaki kuonesha waziwazi kuwa umeelewa. Sasa kama umefikia kwenye uelewa wa hatua hizo tatu za wokovu wa mwanadamu tofauti na ulivyokuwa hapo mwanzo, hebu zifafanue hizo hatua. Lete mchanganuo wake tafadhari, maana naona kama vile bado unachanganya mambo tu tena. Kuubeba msalaba, ni hatua za awali za wokovu kwa Paulo????????? Mmmh!! Hebu lete kwanza, nijifunze then nitakuijia.
  Mungu wangu na akubariki
  . Karibu ndg yangu.

 27. Siyi, unapopambana kuhusu IMANI unasema:
  “Na kuhusu imani napo naona bado hujanielewa pia. Imani ilikuwepo tangu mwanzo kaka. Zamani imani hiyo hiyo ilijengwa katika sheria. Mf. mtenda dhambi aliamini kuwa damu ya kondoo/mbuzi/njiwa nk wa kafara inaondoa dhambi zake zote. Ni imani iliyokuwa inahitaji gharama(matendo ya sheria za kafara).”

  Ingawa unaijitetea saana kwamba wewe si mtu wa dini anayejidanganya kuwa anaifuata Biblia, lakini kauli yako hiyo inadhihirisha hilo unalolikataa! Iwapo mtenda dhambi wako wa huko Kale, aliamini kuwa damu ya kafara aliyoitoa “INAONDOA DHAMBI zake zote” kama unavyofundisha, basi kulikuwa na haja gani kwa Kristo kuwafia hao ambao dhambi zao zimeondolewa? Tena, hao watenda dhambi wako walioondolewa dhambi zao kwa hizo kafara walizozitoa, mbona walirudi tena kutoa kafara hizo hizo kwa dhambi kama hizo hizo ambazo wamezitenda tena mwaka unaofuatia, ilhali ZILIKWISHA ONDOLEWA? Siyi na wenzio, changamsheni akili hizo, Injili siyo hadithi za Abunuwasi au alfu lela ulela! Sheria haina uhusiano wowote ule na Imani, Sheria inaambatana na Adhabu, hauibi kwa sababu unaogopa kufungwa jela au kukamatwa na polisi nk. Sheria inazalisha roho ya kuogopa adhabu, kwa hiyo hata sadaka za kafara ziliambatana na jambo hilo!

  Mtazame hapa Bwana wa Torati, Bwana Yesu Kristo, ndani ya Paulo anachokuonesha kama unayo macho ya kiroho (maana Agano hili ni la Rohoni!); Ebr 10:4 “Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.” Basi kama hao wa Kale, ninyi wa Kale mnaoishi leo, kwa hizo kafara walizozitoa, mwadhani walikuwa na Imani, hilo ladhihirisha kuwa hata Sheria hamuijui licha kuin’gang’ania kwenu! Unaelewa Siyi? Endelea mstari wa 6, “Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo.” Mtapasua vichwa vyenu kwa kutumia akili zenu katika Neno la Mungu, Mwenye Neno lake hajatutaka hata mara moja tutumie akili zetu ndiyo sababu anatupa Roho wake atuongoze katika Neno lake.

  Angalia akili yako, sijui ni yako au ya walimu wako, inavyozidi kukupeleka porini, unasema:
  “Leo imani ileile, haihitaji gharama tena. Yesu alishagharimia zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Sasa hivi, tunaweza kumwendea Kristo ambaye ni NEEMA bila gharama yoyote, just kwa imani tu. Na kama haujaelewa bado, soma waebrania 11 uone hiyo kwa KWA IMANI, MUSA….., KWA IMANI IBRAHIMU….. nk huenda utaelewa rafiki.”

  Kama jambo hili la Imani lingekuwa katika urahisi kama huo unaousema, basi hata wewe pamoja na mafundisho yako yasiyo na kichwa wala miguu, ungekuwa nawe umejazwa RM badala ya huyo Roho Mwingine ambaye wewe wadhani kuwa ndiye! Lakini umeshindwa kuingia gharama ya kuachana na mafundisho ya uongo ili uambatane na Neno la Mungu, Mt 10:38 “Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.” Hiyo ndiyo GHARAMA YA WOKOVU anayopaswa anayeujia WOKOVU katika Kristo. Hao akina Musa waliisikia mioyoni mwao sauti ya Mungu, wakaitii, halafu Mungu kulifunga jambo hilo akasema, “Kwa Imani Musa ali…” akakuchanganya kwa makusudi ili usilielewe jambo hilo, hahahaha…! Angalia hapa anachosema, Rum 10:17 “So then faith cometh by hearing, and hearing by the word of God”, kitafakari kifungu hiki ndicho kinachoushikilia ufunguo wa Kuzaliwa mara ya Pili kwa mkristo, maana bila ya Imani huwezi kumpendeza Mungu!

  Tazama sauti ya Mungu hapa akiendelea kuongea na wanae, Mdo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Neno la Mungu huwa haliendi bure, huwaendea hao waliokusudiwa, wote, wa kuokolewa na wa kuhukumiwa au wa kupotea; ndipo siku hiyo walikuwepo hapo, Injili inatoa ushuhuda huu, Mdo 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.”!!! Biblia haisemi “wote waliokuwepo siku hiyo wakalipokea neno lake”, walikuwako wengine pia, hao wa kupotea, walikuwa na maelezo kama yako Siyi, “Siyi anamwabudu Mungu mmoja mwenye nafsi tatu. Baba, jina lake ni YAHWE, Mwana, ni Yesu, na RM linabaki vilevile. Na huyu Mungu mmoja katika utatu, kila nafsi unaweza kukuta ina majina zaidi ya moja. Na nafsi zote hizi, zinahusika sana katika wokovu wangu na wako pia”! Hebu wewe mwenyewe jaribu kujiuliza, ni kwanini umekuwa mwepesi kuyaamini mafundisho hayo uliyonayo kuliko kuliamini Fundisho la Mitume? Ni Ujeuri wa dini tu unaokusumbueni, “… Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” Mwa 4:9

  Kuhusu Paulo na Dhambi, nimekuona mara nyingi sana mtume huyu amekuwa kielelezo chako cha wana wa Mungu kuendelea katika dhambi licha ya kuzaliwa kwao mara ya pili. Sasa, nataka ufahamu kuwa huyo mtume alikuwa ni mwalimu. Naye mwalimu aliyefuzu katika somo analolifundisha, huzileta uweponi mwa wanafunzi wake hali zote zinazohusiana na somo hilo, hata somo hilo likiwa ni wokovu. Nilikuambia huko nyuma kuwa kipeo cha wokovu ni kuzaliwa mara ya pili, yaani kujazwa Roho Mtakatifu. Lakini haujazwi RM katika siku yako ya kwanza ya kuhubiriwa Injili. Nikakuambia kuwa Ukamilifu wa Ukombozi wako au Wokovu uko katika hatua Tatu, Kuhesabiwa Haki, Kutakaswa na mwisho Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Basi hiyo dhambi unayoirejea katika mafundisho ya Paulo, inahusiana na hatua hizo mbili za mwanzo, hizo zinazobeba ile gharama ya Wokovu, kule kuubeba msalaba wako. Hebu yarejee Maandiko yanayokueleza kuhusu siku ile Kristo alipoubeba Msalaba wake, halafu endelea mbele umtazame kama aliendelea na msalaba huo alipofufuka! Basi vivyo kwa mkristo Aliyezaliwa mara ya Pili, hatendi dhambi tena kama Maandiko yanavyoshuhudia, kutokuelewa kwako jambo hili hakulibalishi!!!

  Mwisho niseme hivi uliponiambia kwamba niyasome majibu ya Mabinza, sikukuelewa vizuri, basi mimi nikadhani kuwa Mabinza naye yumo katika Biblia, lakini leo ndio nimekijua ulichosema, nimeyaona hayo uliyoyaandika, asante! Bali kwa habari ya kuyajibu mimi naona ni bora twende kule kwenye zile link husika ili tuendelee kutokea hapo, tutapata mtiririko mzuri.
  Yaani kuhusu mambo ya UTATU Mtakatifu, twende kwenye mada yake na pia Ubatizo, nadhani ni “Swali Kuhusu Ubatizo” nk Usiogope, twende huko ukanoe ufahamu wako, usibweteke tu na maombi kumbe uko kwenye ibada za mizimu!!!

  Karibu ndugu yangu!

 28. Lwembe,
  Bwana akubariki ndg. Nimejaribu kuunganisha majibu ya makala zako zote mbili hapa. Jaribu kupitia tu taratibu kaka, utaona nilivyotoa maelezo japo kwa kifupi sana. Twende kazi….
  Kuhusu Hawa na kula tunda naona hukunielewa. Ndiyo maana umeishia na wrong understanding.
  Na kuhusu imani napo naona bado hujanielewa pia. Imani ilikuwepo tangu mwanzo kaka. Zamani imani hiyo hiyo ilijengwa katika sheria. Mf. mtenda dhambi aliamini kuwa damu ya kondoo/mbuzi/njiwa nk wa kafara inaondoa dhambi zake zote. Ni imani iliyokuwa inahitaji gharama(matendo ya sheria za kafara). Leo imani ileile, haihitaji gharama tena. Yesu alishagharimia zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Sasa hivi, tunaweza kumwendea Kristo ambaye ni NEEMA bila gharama yoyote, just kwa imani tu. Na kama haujaelewa bado, soma waebrania 11 uone hiyo kwa KWA IMANI, MUSA….., KWA IMANI IBRAHIMU….. nk huenda utaelewa rafiki.
  Kuhusu dhambi, naona unailazimisha Biblia ikubali mawazo yako. Kwani Paulo hakuwa mwana wa Mungu? Nakuona hata huelewi maana ya KUFANYIKA KUWA MWANA WA MUNGU. Unachojua ni mwana wa Mungu tu tena kwa wrong understanding. Kilichoandikwa ndani ya Neno, hicho peke yake ndicho nikiaminicho tena kwa msaada wa RM ktk kukielewa. Zingine porojo tu kaka. Hivi unaelewa maana ya mtu wa dini? Na unaweza kueleza maana ya kuwa mwana wa Mungu?

  Na kuhusu Baba, Mwana na RM napo sijui nitumie lugha zipi uelewe. Labda niseme hivi tu kwa kifupi. Siyi anamwabudu Mungu mmoja mwenye nafsi tatu. Baba, jina lake ni YAHWE, Mwana, ni Yesu, na RM linabaki vilevile. Na huyu Mungu mmoja katika utatu, kila nafsi unaweza kukuta ina majina zaidi ya moja. Na nafsi zote hizi, zinahusika sana katika wokovu wangu na wako pia.
  Nikushukuru sana kwa kuleta maelezo yako mengi japo hukujibu maswali yangu niliyokwambia uyajibu kwanza kwenye makala ile ya Mabinza. Umejidai kana kwamba hukuyaona kabisa. Naomba uyajibu hayo maswali kwanza, ili tuondoe mzizi wa suala la UBATIZO kwa jina la Yesu ama Baba, Mwana na RM. Acha hadithi kaka. Lete majibu kwanza ndg yangu.
  Ubarikiwe

 29. Maswali mawili matatu uliyoniuliza, ngoja nijaribu kuyajibu kwa faida ya nduguyo Lenda maana najua kuwa nyote yanawahusu.

  Kuhusu Hawa, maelezo yako yanaonesha jinsi ambavyo anayelikataa neno la Mungu anavyouvaa upofu, na hivyo kushindwa kabisa kuyapambanua Maandiko! Yaani huelewi hata kuwa Hawa ndiye aliyetangulia kula lile tunda na kisha akarudi kwa mumewe na kumpa, baada ya mumewe kula ndipo “WAKAJIONA WAKO UCHI”!! Sasa kama hata jambo lililowazi kiasi hiki nalo linakuwa issue, ama kweli upofu anaopigwa mtu wa kupotea si mchezo! Nimekuombea ufunuliwe hayo Maandiko, hebu yasome tena!

  Kuhusu Sheria kutokuwa na Imani ndani yake, najua itakuwia vigumu kulijua hilo, lakini iwapo Sheria ingekuwa na Imani, basi Kristo asingesulubiwa. Ndio maana huko nyuma nilipoona kuwa hamuijui hata Sheria kuwa ni nini, nikasema itawachukua eternity ninyi kuletwa katika ufahamu, ambavyo mtakuwa mmekwisha chelewa! Hebu visome tena vifungu hivi kwa utulivu, vitakuondoa katika mzunguko wa mauti uliojiingiza, Ebr 4:2 “Maana ni kweli sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao, lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia” hivi ndivyo ilivyo unapoizungumzia Torati. Bali unapowaleta akina Ibrahim, Henoko na wengineo, sina jinsi bora ya kukuelewesha mambo ya rohoni ilihali uko mwilini ukiendelea na juhudi ktk Mungu bila Maarifa! Lakini Imani ni mawasiliano ya siri kati ya Mungu na wanae, bali kwa kukosa kwako Maarifa nawe unajitahidi kuwa na Imani, ndio maana niliwahi kukuambia huko nyuma kuwa Intellectual Faith will not regenerate you!

  Kuhusu dhambi, ndio kama nilivyokuambia, ni KUTOKUAMINI. Hayo mambo ya hasira, tamaa nk ni matunda ya dhambi. Kwahiyo usishangae sana, maana ulipoukataa Ubatizo uondoao kutokuamini, basi mmekuwa ni pango la mapepo ya kidini, ndio maana huwezi hata kuelewa unapoambiwa kuwa wana wa Mungu hawatendi dhambi, hata huelewi ni lini walikuwa na dhambi na ni lini wamekuwa si wenye kutenda dhambi tena maana Mungu huyo unayedhania unamuabudu, yumo ndani ya wanaye, basi utayajuaje hayo nawe ni mtu wa dini?

  Kwamba wewe unamuhitaji Yesu kila dakika, hilo ni kweli, maana wewe mwenyewe unakiri “Maisha ya muumini ni maisha ya kujiona umepungua kila dakika ” na utaendelea katika mzunguko huo mpaka moto utakaposhuka! Huo ndio mzunguko wa dini, maana hujapata ubatizo wa RM, nako kuigiza kujazwa RM hakukufanyi uwe umejazwa; inapofika saa ya kweli ya uhitaji ndipo unaposikia kupungukiwa nawe ungejibidiisha katika maombi na mifungo na kusaidia masikini na wajane na mashoga na wasagaji na mwisho kutoa sadaka na zaka!

  Lakini kwa akina Henoko, wao wanaye Kristo ndani yao akiwaongoza na wanalijua hilo, basi hebu fikiria furaha yao ikoje? Wakati mnatimua mbio kuyakimbia mabomu ya Gongo la mboto kama watu mlioota mbawa, wao wametulia tuli wakisubiri maelekezo!!!!

  Labda mwisho nikwambie hivi, kwamba, kwa kuwa wewe u tofauti na wale Wakristo unaowasoma katika Biblia hao waliobatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo, basi kujihesabu kuwa nawe ni mmoja wao ni zaidi ya ufinyu wa kufikiri, au ni umbumbumbu wa kupindukia, kwamba ndio lile jambo la mwanamwali MPUMBAVU! Unajua ni afadhali MJINGA, huyo anaweza kuelimika, lakini huyo aliyegubikwa na shuka la dini linalozalisha Mwanamwali Mpumbavu, hana nafasi ya kujifunza lolote!!! Hebu itazame kauli yako hii:
  ““Kuhusu ubatizo kwa jina la Baba, Mwana na RM, wewe umesema kuwa uelewa wa wale mitume ulikuwa juu sana ndiyo maana walimwelewa Bwana wao. Yesu aliposema wakabatize kwa majina hayo matatu, wao walimwelewa kwa jina moja tu. Na wewe umeufuata uelewa huo. Sisi ambao tunafuata nyayo za Kristo, acha tubatize tu kama Yesu alivyosema. Kama ni majina Baba, Mwana, na RM si majina halisi(yaani sifa), acha tu tubatize kwa kutumia hizo sifa maana zinamlenga YEYE huyohuyo. Hakuna tatizo katika hilo. Ni sawa na kumwapisha mtu kwa kutumia jina la Kikwete na badala yake ukatumia sifa zake, kama vile Rais, amiri jeshi mkuu, mkuu wa nchi nk, automatically, utakuwa umemlenga Kikwete huyohuyo. Hivyo haina shida.””
  Kweli , unaweza ukajiaminisha ujinga kama huu? Umeona kwanini mtume Paulo aliwakatia tamaa watu wa jinsi yako? 2Tim 3:6 For of this sort are they which creep into houses, and LEAD CAPTIVE SILLY WOMEN LADEN WITH SINS, LED AWAY WITH DIVERS LUSTS” umeona kwa kuukataakwako Ubatizo uletao ONDOLEO la dhambi, jinsi dhambi zako zinavyoendelea kujirundika mpaka umekuwa mtumwa wa injili za udanganyifu!

  Hebu wazia hili, kwamba unakutana na mtu mtanashati kama Siyi, kavaa suti safi na buti inang’aa mpaka nawe unajitengeneza kola yako kwa kujiangalia kwenye buti yake, mkononi ana Biblia ya leather genuine, baada ya kusalimiana naye unamwambia:
  WEWE: Nimekutana na baba hapo njiani,
  SIYI: (naye upesi anakuuliza) Baba yangu au baba mkwe?
  Unajifanya hujamsikia unaendelea,
  WEWE: tena wameongozana na mwana,
  SIYI: Mwana yupi, mtaje jina basi, halafu hujasema sawa sawa ni baba yupi uliyekutana naye??

  Mbele akikutana na Lwembe anakomaa kabisa kuwa baba ni jina na mwana pia ni jina!!!

  Lakini dunia ndivyo ilivyo, karibu ndg yangu tuikamilishe Injili!

 30. Unajua ndg yangu Siyi, Mungu ni wa utaratibu. Mungu haendi akibahatisha kama wanadamu walioanguka! Basi unapaswa ujue kuwa katika Utaratibu alioupanga, alianza na Agano la Kale, humo aliyaweka maagizo yote yampasayo mwanadamu aliyepangiwa Wokovu Wake. Na kwa kadiri utakavyolitazama Agano hilo, utauona mkondo wa Wokovu ulivyopita na hao waliohusika mpaka kulifikia taifa la Israeli. Ndio maana mtume Paulo, huyo mjuzi wa Torati, huyo aliyesoma chini ya mwalimu maarufu , Gamalieli, anasema, “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.” Basi wokovu wa Myahudi umo katika Injili na Myunani pia! Rum 1:16.

  Ujio wa Kristo ndio uliolifanya Agano hilo kuwa kuu kuu. Naye messenger anayelifunga Agano hilo ni Yohana Mbatizaji, huyu ndiye anayeichukua mioyo ya watu wa Agano hilo na kuigeuza imuelekee Kristo. Lk 1:16-17
  “Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa”

  Sasa, Kristo kuwa mwisho wa sheria, hebu litazame jambo hili: Mdo 19:2-3
  “…akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.” Unaona, hao ni wale watu wa Torati walioupitia Ubatizo wa Yohana. Sasa, NGUVU iliyokuwamo ndani ya Ubatizo huo, ndiyo iliyomtayarisha huyo aliyeitii sauti hiyo ya mtu aliaye nyikani, hiyo ambayo ilikuwa na UPAKO wa Mungu kwa ajili ya kazi hiyo kulingana na utaratibu alioupanga, ikawakamata wote waliokusudiwa, licha ya kwamba hawakuelewa kisawasawa, lakini walijikuta wakiitikia sauti hiyo! Ukisoma Mat 11:7-13 unaweza kupata picha kamili.

  Mstari wa 13 unasema hivi, ukimzungumzia Yohana Mbatizaji, nafasi yake katika programu hiyo ya ukombozi,
  “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.”
  Ndipo ukilichukua jambo hili na kulirudisha pale Mdo 19:2-3 hapo juu ili kuliona kikamilifu linavyotimia kwa hao walioitembea Njia hiyo, yaani waliopita katika Programu hiyo, kwamba hadi kufikia Huduma ya Yohana Mbatizaji, yaani manabii na Torati, hawajawahi kumpokea RM na wala hawamjui! Kwanini? Neno walilohubiriwa halikuchanganyika na imani ndani yao (Ebr 4:2)! Sheria haina Imani ndani yake. Lakini Neno la Imani walipolipokea, “Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu,” Neno hili liliiamsha ile Mbegu ndani yao, “Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”

  Kwa kifupi huo ndio uelewa wangu kuhusu Kanisa na utii wake! Kwamba si jambo la kujibidiisha isipokuwa uwe umehubiriwa Injili na mtumishi aliyewekwa wakfu kwa kazi hiyo ili ile Nguvu iambatanayo na mahubiri hayo, ikufikie nawe upate faida ya Kiungu iliyokusudiwa. Yaani uwe ndani ya Programu. Vinginevyo, iwapo utahubiriwa na mtu wa dini, basi utaishia kuipinga Injili, ukiwa umeandikishwa katika jeshi la Adui, yaani umeunganishwa katika jeshi la Waamaleki! Ni hasara kiasi gani!!

  Kwahiyo mtu yeyote anayejidhania amejazwa RM, basi na ajitazame iwapo njia aliyoipita inalingana na nduguze hao ambao Mungu alituwekea hapo jinsi yao ili kiwe kielelezo kwetu hapo watakapo inuka walimu na manabii wa uongo wakiwafundisha “silly women laden with sins…” madude ya kuzimu na kuwapagaisha na maroho ya dini!

  Basi Siyi ni vizuri ukajikagua wewe mwenyewe, ili uone ulihubiriwa nini kwanza, Torati au Injili? Au uliokota Biblia njiani, ndipo ukajifunza kutoka humo ukianzia huko Mwanzo na sasa ndio umelifikia Agano Jipya?
  FUATA UTARATIBU!!!

 31. Lwembe
  Huenda hii itakusaidia.
  Nilikuuliza swali rahisi sana kaka, kuwa utii unaoendana na injili ukoje? Ona ulivyonichanganyia mambo. Kwa uelewa wako, tunawatii waliotuhubiria injili kwa vile wametuamuru tubatizwe na siyo hiyo injili!!! Ajabu sana!! Kazi yangu ni kukuonesha njia iliyosahihi. Mungu ndiye atakayekutoa huko, siyo mimi!!
  Tangu mwanzo nilikwambia kuwa, ili tuelewane vyema, weka kando udini!! Naona kwenye michango yoote, unagusia udini. Hii ni kuonesha kuwa, kila nikisemacho-ambacho ni cha kibiblia per se, wewe huwa unakihusisha na usabato tu. Hii itakupa kazi sana sana kulielewa NENO. Kuhusu dhambi, hujanijibu vizuri. Maana umesema dhambi ni ile hali ya kutokuamini. Kuna ukweli ndani yake kiasi fulani, maana dhambi huanzia moyoni, sehemu ambayo mtu hunajisika hata kabla ya kitendo chenyewe kukitenda. Hii ni kwa mujibu wa agano jipya. Katika Agano la kale, ilikuwa ni mpaka uonekane kwa macho ukitenda kabisa kile kitendo ndipo uhesabike mdhambi. Yesu alipokuja, kazifanya sheria kuwa za kiroho zaidi. Kazifanya kuwa ngumu zaidi sana kuzitimiza. Hapa ndipo ile nafasi ya NEEMA inapokuwa na muhimu kwako na kwangu.
  Ndiyo maana nakwambia kuwa, wewe una dhambi, mimi nina dhambi, na mwingine yeyote ana dhambi. Why? Ni ukweli usiopingika kuwa, mawazo mabaya humjia kila mtu, chuki anayo kila mtu, hasira anayo kila mtu, tamaa anayo kila mtu nk japo vinaweza visionekane kwa matendo ya mwili wala kwa macho yetu ya nyama. Mbele za Mungu huhesabiwa kama dhambi tayari. Hivyo kwa mujibu wa sheria za Musa, sote tulipaswa kupigwa mawe. Yesu alikuja kuweka vigezo vya mtu kumpiga mawe mdhambi mwenzake- (yaani mtu asiye na dhambi). Ni nani asiye na dhambi sasa achukue jukumu la kupiga mawe wenzake? Jibu ni hakuna!! Maana wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu rumi 3:23. Hakuna aliye msafi wa kumnyoshea kidole mwingine. Kimbilio letu sote ni kwa Kristo, muweka vigezo vya watu kuponda mawe. Hii ndiyo NEEMA inayotuweka huru. Na sote sisi tunahitaji hiyo NEEMA. Tunamuhitaji Yesu kila dakika.

  Ndiyo maana kaka Lwembe, tunapoenda magotini kila saa, huwa tunatubu dhambi mbele za Kristo. Maisha ya muumini ni maisha ya kujiona umepungua kila dakika unapojilinganisha na Kristo. Hushauriwi kwenda kwa mchungaji kutubu dhambi. Yule ni mdhambi mwenziyo tu. Hana lolote. Unashauriwa kwenda kwa Kristo directly (magotini) na kumlilia ili akusamehe. Acheni kudanganyana kwa sala za toba. Watu wana madhambi tofauti tofauti. Mtaungamaje wote kwa sala ileile moja? Halafu na anayewatubisha naye ni mdhambi tu!! Kila aliyezaliwa na mwanamke, ni mdhambi kaka. Ndiyo maana akina Paulo pamoja na kuandika nyaraka nyingi sana katika Biblia, mtume wa Kristo aliyeokoka kikwelikweli, bado alikuwa ni mdhambi…rumi 7:15-20.

  Kuhusu ubatizo kwa jina la Baba, Mwana na RM, wewe umesema kuwa uelewa wa wale mitume ulikuwa juu sana ndiyo maana walimwelewa Bwana wao. Yesu aliposema wakabatize kwa majina hayo matatu, wao walimwelewa kwa jina moja tu. Na wewe umeufuata uelewa huo. Sisi ambao tunafuata nyayo za Kristo, acha tubatize tu kama Yesu alivyosema. Kama ni majina Baba, Mwana, na RM si majina halisi(yaani sifa), acha tu tubatize kwa kutumia hizo sifa maana zinamlenga YEYE huyohuyo. Hakuna tatizo katika hilo. Ni sawa na kumwapisha mtu kwa kutumia jina la Kikwete na badala yake ukatumia sifa zake, kama vile Rais, amiri jeshi mkuu, mkuu wa nchi nk, automatically, utakuwa umemlenga Kikwete huyohuyo. Hivyo haina shida.

  Kuhusu TRINITY, jaribu kupitia kwanza majibu yangu kwa Mabinza kwenye makala niliyokutumia kwa njia ya personal mail. Usipoelewa, niijie tena.

  Kristo ni mwisho wa sheria za kupondwa mawe na siyo amri 10. Tatizo lenu ninyi kwa vile mnataka dini iwafeve kwenye maslahi/matakwa yenu, ndiyo maana huwa mnazikokota hizo sheria zoote kuwa Yesu alizigongomelea msalabani jambo ambalo si kweli. Yesu kama Mungu ana amri zake ambazo mwanadamu alipozivunja kwa mara ya kwanza, hakukuwa na jinsi ya kufanya mbali na kujitoa mwenyewe afe ili kumrejesha tena mwanadamu ktk utawala wake. Kwenye utawala wake humo kuna hizo sheria 10 za Maadili. Sheria hizi ni katiba ya Mungu na tabia ya Mungu. Katika vizazi vyote vya duniani, sheria hizi zimezidi kuwepo milenia hadi milenia. Ndiyo maana, akina Ibrahimu-mababa wa imani, na marafiki wa Mungu, walizijua vizuri na kuzitenda sawasawa. Ninashangaa unaposema kuwa katika sheria hakuna imani!!! Kwani ilikuwaje akina Ibrahimu wakaitwa wazeee wa imani?? Akina Eliya, Henock? Elisha? Vijana watatu wa kiebrania katika daniel 3 nk? Alichokuja kukiondoa Yesu ni sheria za kafara tu peke yake. Acha kubweteka kaka.

  Tatizo jingine ninaloliona kwako, nakuona unachanganya kati ya kuwa rohoni na kuzitunza sheria za Mungu rohoni. Hivi ni vitu viwili tofauti. Kuwa rohoni ni mojawapo ya njia za kunena kwa lugha. Kunena kwa lugha kusikoweza kutamkwa. 1 korinth 14: 2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake. Kwa ufafanuzi zaidi, pitia makala yangu ya LUGHA MPYA. Niliipachika hadi kwenye ukurasa wangu wa facebook. Nenda tu utaikuta huko na iliwabariki wengi sana, maana walinitumia response zao nyingi.

  Kuzishika sheria za Mungu rohoni, ndiko kule kutowaza mabaya kabisa; kutotamani vya watu, kutokasirika, kutochukia watu, kumpenda Mungu nk ambako kwa ujumla wake, utakuja kuishia kwenye zile amri mpya au amri kuu zile mbili ambazo ufafanuzi wake nilikupatia kwenye jana, zoote hizi, zinategemea TORATI na manabii. Hivyo sasa, unapozishika amri za Mungu rohoni, ndiko kumpendeza Mungu. Maana licha ya kutoonekana wazi ukitenda dhambi ktk mwili, hautatenda hizo dhambi tokea rohoni-yaani hautawaza mabaya hayooo. Na hili ndilo fundisho la Biblia. Hakuna mtu anayepambana siku hizi kuzishika sheria za Mungu kimwili. Ni kazi mno. Huwezi wewe!! Kristo mwenyewe alituhakikishia hilo kuwa ni mpaka afanye makazi ndani yetu ndipo tutazaa sana. Yohana 15:4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. RM anapokaa ndani yetu, NENO lake hukaa ndani yetu pia. Neno linapokaa ndani ya mtu, sharti lijidhihirishe ktk mwili-yaani matendo mema. Na hii ndiyo imani iliyo hai. Huwezi kusema kuwa hauzini kimwili ilhali bado unatamani. Bado wewe ni mvunja sheria. Huwezi kusema kuwa wewe unaitunza Sabato kiroho ilhali unaabudu sanamu-mungu-jua. Bado wewe ni mdhambi yuleyule. Sheria inapokuwa rohoni, sharti ionekane ktk matendo ya mwili. Hili ndilo ndilo neno la Mungu.

  Na wajumapili wengi sana wanayachanganya sana haya mambo(kuwa rohoni na kuzishika amri za Mungu rohoni), jambo ambalo si sahihi. Nina imani kuwa una uelewa mzuri na mkubwa tena wa kutosha tu, sijui kwa nini haubaini hilo!!

  Kuhusu sabato, ukweli ni kwamba, umeishiwa hoja kaka. Hivi hadi unahoji kuwa ni wapi imeandikwa kuwa Adamu alipewa Sabato? Ha ha haa!! Ina maana Mungu alipumzika mwenyewe tu akamwacha Adamu akifanya kazi siku ile ya saba? Na kama waisrael hawakujua mambo ya sabato, kwa nini Mungu aliwaambia waikumbuke? Kwani kinachokumbuka ni nini? Ni akili au moyo/roho? Te te teee!! Yaelekea umechoka sasa. Haya aya nyingine hii; Kutoka 31:16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Kama wewe ni kizazi cha Waisrael(wa kimwili ama kiroho), unapaswa kuikumbuka na kuitunza sana hiyo sabato maana ni ya milele. Hakuna ukomo. Acha kung’ang’ana na sabato bandia-jumapili. Torati inapokuwa ya rohoni, hujidhihirisha katika mwili, maana imeandikwa kwa matendo yao mtawatambua….

  Na sidhani kama kweli mimi sielewi kaka ninaposoma rumi 11:26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. Ina maana Yesu atazaliwa tena Israel? Au kuna mtu mwingine anaitwa mwokozi tofauti na Masihi-Kristo? Au na huu nao ni ukituko wa kuwa msabato? Te te tee!! Unachekeshaaaaa japo sometimes unahuzunishaaaa!!

  Kwa Hawa, hapa napo unajitutumua but hauna logic!! Biblia inasema walijitambua wote wawili (katika mmoja) kuwa wa uchi. Sasa wewe unasema Hawa alikuwa ameshakuwa uchi tayari… Mbona alipomwona Adamu kabla hajala hakumwambia kuwa wewe mwanamke, mbona uko uchi? Yaani mara nyingine huwa unauliza ilimradi tu… te te teee!! Anyway, nikushukuru pia kwa vile siku hizi umeleewa kuwa tunda alilokula Hawa halikuwa UZINZI na Nyoka. Hiyo nayo ni hatua nzuri kaka. Nakupongeza sana. Inaonekana safari yako ni ya taratibu sana. Hatari yake ni hiyo ya kuchelewa kufika, ukakuta mlango ulishafungwaaaa, then ukabakia nje. What that a SORROW!! Changamka tafadhari.
  Ubarikiwe na Bwana.

 32. Siyi, kama nilivyokuambia, ninafahamu jinsi ambavyo roho za dini huwang’ang’ania wateja wao, kama Farao! Lakini ngoja nijaribu kuyajibu maswali yako, maana kwa kweli jibu humfaa huyo mwenye kiu ya kujifunza!

  1-4 Kulingana na Injili ya Yesu Kristo, suala la utii kwa kanisa au hao wanaoujia Ukristo, hilo huanzia hapo unapohubiriwa Injili, ndipo kipimo cha utii huja, kikiashiria kuiamini kwako hiyo Injili. Basi aliyekuhubiri Injili hiyo atakuamuru ubatizwe, Mk 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Basi kama ambavyo ulilitii agizo la Kisabato, iwapo unataka kuwa Mkristo utalitii Agizo linalotolewa na Roho Mtakatifu katika Mdo 2:38 likiwa ni utimilifu wa Matt 28:19. Kuanzia hapo sasa unaweza kuyaelewa mafundisho mengine yanayofuata.

  Kuhusu dhambi, hakuna njia ya mkato, asili ya dhambi ni KUTOKUAMINI! Kwahiyo iwapo kuna Neno lolote katika Biblia ambalo unaliona lina makosa, nawe ungependa kulisahihisha kidogo, kama unavyowaona mitume katika ubatizo, si Petro tu, hata Paulo (Mdo19:5 “Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu”), huu ndio mzizi wa dhambi, yanayofuata hapo yanajiendea tu kama boti iliyokata nanga!! Yaani utakuwa mtu wa dini na jirani safi kama Esau. Utayaelewa vizuri sana mafundisho ya dini yenu ambayo umeaminishwa kuwa ndilo Neno la Mungu. Nao ushahidi wa jambo hilo ni pale unapolichukua Neno la Mungu na kulipima katika mafundisho yenu, ambapo huonekana kupwaya!!!

  Pia nimekuambia hivi, Mkristo ni huyo aliyeondolewa dhambi, yaani kutokuamini. Yeye analiamini Neno la Mungu loooote, halitilii shaka hata chembe. Kwake Neno ndiyo Dira ya maisha yake. Yeye hulitazama hilo tu, si mtu anayetembea katika opinions mbili kama mnafiki. Kuzaliwa mara ya pili Siyi sio hadithi, kama unavyoona kuzaliwa kwetu kimwili jinsi ya shughuli yake huko leba, chupa ya maji hupasuka kisha damu humwagika ndipo uhai hupokelewa, nayo sehemu hiyo huchafuka; sasa rudi pale Golgotha, kisha tazama ilikuwaje, ule mkuki ulipozama ubavuni ili kumtoa Hawa, yaani Kanisa, Maji yalimwagika kisha Damu nasi tukazaliwa katika Roho, tukiwaacha makundi yao ya dini wakibaki MWILINI na hawajui hata kilichotokea mpaka leo hii!!!

  Kuhusu Ubatizo kaka, jaribu kuwa mtu wa kiasi, uyasubiri Maandiko yakufunze. Je, iwapo Mungu angekomea kwa Musa, basi ile ahadi ya ujio wa Kristo ungeijulia wapi? Mambo huenda yakijifunua, hatua kwa hatua, unaanza Mwanzo na unamalizia na Ufunuo! Kama mitume waliambiwa wakabatize kwa jina la Baba na la Mwana na la RM, huyo aliyewaambia ndiye aliyeujua uwezo wao wa ufahamu aliowapa ili kuyaelewa maagizo yake, kwahiyo wewe ambaye kupewa kwako ufahamu kutategemea utakavyowapokea hao aliowatuma, unategemea kuwa mjuzi kuliko wao? Hicho kiburi ndio mwanzo wa dhambi!!!

  Kuhusu TRINITY, labda unipe tafsiri yenu ili nami niichunguze katika Maandiko, nipate kuibaini sawa sawa, maana isije kuwa nanyi ndio wale wale wa “miungu mingi lakini Mungu mmoja”!!!

  5: Inaonekana hukunisoma vizuri kuhusu watu wa kale. Nilisema hivi: “…Hawali nguruwe na wanyama wengine walionajisishwa kwa watu wa kale, wanaitunza sabato na zile amri 9 walizopewa watu wa kale” na si kama ulivyoninukuu wewe, “ni mojawapo ya mapokeo YALIYOTOLEWA NA WATU WA KALE?”

  6: Kristo ni mwisho wa sheria kwa sababu kwa kuipokea Injili sasa unaweza kuhesabiwa Haki, lakini kwa Sheria usingeweza kuhesabiwa haki kwa sababu ndani ya Sheria hakuna Imani. Ndipo huyo ALIYEZALIWA MARA YA PILI, HUYO MTU WA ROHONI HATENDI DHAMBI!!! Najua ni ngumu kueleweka, ila ndio hivyo mpaka uwe umejaliwa kuzijua Siri za Ufalme, yaani uwe umejaliwa kuliamini Neno lote ambalo ndilo linalozibeba hizo Siri, vinginevyo utazijua siri za dini yenu tu!

  Kuhusu Upendo ni sawa, bali utaupata wapi Upendo huo ambao umo ndani ya Ufalme nawe ungali uko huko nje kwenye dini? Ni lazima uingie humo ndani ndimo ulimo Upendo huo, vinginevyo unafanya michezo ya kuigiza au uko katika “wishful thinking” tu za huo Upendo which is unrealistic!

  Kuhusu Sabato ya Mungu, iko hivyo hivyo kama Maandiko yanavyosomeka, ila wewe nimegundua kuwa vitu vingi huwa ni marejeo ya mafundisho yenu ambavyo wewe unaamini kuwa unavisoma katika Biblia!! Sijui ni wapi unaposoma kuwa Adamu alipewa sabato? Hivi kati ya hao waliotoka Misri, kuna hata mmoja aliyeyajua mambo ya Sabato? Mimi sioni tatizo hapo Mungu anaposema kuikumbuka Sabato, maana nafahamu kwamba mambo yote huanzia Rohoni na kuishia mwilini, ndipo huko kuikumbuka mimi kwa urahisi kabisa narudi rohoni kulikamata hilo, maana nafahamu pia kuwa Torati ni ya Rohoni, ndio maana inapotimilizwa katika Injili mimi naiona hivyo kwa urahisi!

  Kuhusu Israeli kuwa taifa Teule la Mungu, mimi kwa Maandiko ninajua wao wako hivyo, “Wokovu kwanza kwa Myahudi….” halafu jua kwamba Israeli watapelekewa tena Musa na Eliya, usijichanganye na madude ya Kisabato, hao walichemka zamani sani wewe tu ndio hujui! Rum 11:26 “Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasi yake.” Jaribu kuyaamini Maandiko utakuwa mtu fresh kuliko ambavyo sasa mafundisho ya Kisabato yanavyokufanya kuwa kituko!

  Kuhusu Hawa, Maandiko yako hivyo hivyo unavyoyasoma, hayabadiliki kaka. Tatizo liko katika uelewa wako tu! Mwanzo 3: 6 “Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi ALITWAA KATIKA MATUNDA YAKE AKALA, akampa na mumewe, naye akala. Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo”.
  Jaribu kusoma pole pole huenda utando wa Kisabato ukakuondoka ukayaona Maandiko vizuri. Hawa alipolila lile tunda alikuwa na Nyoka, ndiye aliyemshawishi akalila, baada ya hapo akampelekea na mumewe! Sasa unganisha na mstari wa saba kama unayo Maarifa ya Neno!!

  Agano kuu kuu, kiriba cha zamani hakiwezi kuhifadhi Mvinyo Mpya!!!

  Gbu brother!

 33. Kaka Lwembe,
  Namshukuru sana Mungu kwa kutupa uhai na fursa za kujadili mambo kama haya yahusuyo wokovu kwa watu wake. Aidha, niwashukuru SG na uongozi wake kwa kutupatia uwanja wa kutoa mitazamo/uelewa tofautitofauti juu ya Neno-Biblia. Bwana awabariki sana SG kwa kibarua kizito cha kusoma maoni kiiiiiila siku na kisha kuyaruhusu yawafikie wasomaji. Siyo kazi rahisi. Inahitaji NEEMA ya Bwana na uvumilivu thabiti. Nina imani, Bwana atatenda mambo makuu na waisiyoyajua kwa sasa. Niende kwenye hoja zako kaka sasa;
  Mimi nashukuru kaka kwa kunipongeza kwa msimamo wangu katika NENO na si ukigeugeu unaousema. Bwana akubariki sana na wewe kwa jitihada zako hizo za kujibu maswali ya watu yakiwepo na yangu. Biblia itatuambia kila kitu na tutaielewa vizuri sana endapo tu tutaweka mbali mitizamo na doctrines zetu za kidini!!
  Kuhusu kujazwa RM umejibu vizuri kaka. Ulichoshindwa kuelewa ni ile hali ya kutimilizwa kwa sheria katika injili. Tena ukasema kuwa, injili hiyo sharti iendane na utii…Jambo ambalo ni kweli tupu!! Halafu ukaleta nukuu nzuri kabisa ya 1Yoh 1:8. Na ukasema kuwa, ninanukuu, “KUJITAMBUA KUWA WEWE NI MWENYE DHAMBI NDIO USHUHUDA WA KWANZA KWAMBA NDANI YAKO IMO KWELI, YAANI ILE IMANI IMEUMBIKA! YAANI UKIHUBIRIWA INJILI YA KWELI, NA KAMA NDANI YAKO IMO ILE MBEGU YA MUNGU, ULE UZAO, BASI MOJA KWA MOJA NAWE HUKUPATA HALI KAMA ILIYOWAPATA NDUGUZO PALE WALIPOISIKIA INJILI YA PETRO, NDIPO KATIKA MDO 2:37 WAKIWA CHINI YA MASHTAKA, ”WALIPOYASIKIA HAYA WAKACHOMWA MIOYO YAO, WAKAMWAMBIA PETRO NA MITUME WENGINE, TUTENDEJE, NDUGU ZETU?”INJILI HUKULETA MPAKA HAPO SIYI, IF AT ALL UMEHUBIRIWA!”
  Naomba unijibu haya maswali kaka. Na kwa vile nimesema tuiache Biblia iseme, tafadhari, tumia aya nyingi za maandiko kuliko maneno yako mwenyewe wakati ukijibu maswali haya.
  1. Unaweza kufafanua maana ya injili kuendana na utii baada ya kuonekana kuwa unauelewa uhusiano wa vitu hivi viwili?
  2. Ni kwa namna gani unaweza kuwa kujiona/kujihisi mdhambi ilhali hauko chini ya sheria? Ni kwa nini ujione mkosaji ilhali sheria ulizovunja hazipo?
  3. Ndiyo, ni kweli kuwa wanaochomwa mioyo/kuguswa na ujumbe wakati wa mahubiri ni wenye dhambi ambao kwa mtazamo wako tu ni wale ambao hawajampokea Kristo!! Je, leo mhubiri anapohubiri injili, hakuna watu waumini (au wewe mwenyewe) wanaoguswa na mahubiri ya jinsi hiyo? Je, hao nao ni watenda dhambi? Kama ni ndiyo, dhambi zipi(makosa gani) ilhali hawako chini ya sheria kama walishampokea Kristo tayari?
  4. Kubatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo peke yake, sidhani kama ndiyo iliyokuwa dhana ya Petro akilini mwake. Maana Bwana wao aliwafundisha wawabatize watu kwa jina la Baba, Mwana na RM. Na sina haja ya kukupa hizo aya maana unazifahamu vizuri. Je, Petro alianzisha injili yake au alibadili maelekezo ya Bwana wake ktk kuihubiri injili, akawa anabatiza kwa jina la Yesu tu badala ya vile alivyofundishwa na Bwana wake? Kwa mawazo yangu ya kibnadamu tu, nakuona una uelewa kama wa kaka Mabinza, kuwa there is no TRINITY!! Na kwamba, Yesu ndiye Mungu Baba, RM na Yesu mwana huyohuyo!! Je, ni kweli unaelewa hivyo au ni tofauti?
  5. Ni akina nani wanaomtafuta Mungu bila maarifa kaka Lwembe? Nguruwe alinajisishwa na watu wa kale? Kutunza sabato na zile amri zingine 9, ni mojawapo ya mapokeo YALIYOTOLEWA NA WATU WA KALE? Ni lipi/yepi kati ya haya ni matokeo ya kazi za WATU (na siyo Mungu) wa kale? (kumbuka kujibu kwa aya za maandiko).
  6. Kama “Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki”; Je, leo hii watu waliompokea Kristo bado wana haja ya kuungama dhambi? Dhambi za wapi sasa kama hakuna sheria? Unakumbuka Yesu alikufa lini? So tangu Yesu afe, hadi leo hii watu hawana dhambi? Kwa kupanua mafikara yako kaka, ni yupi aliye na dhambi leo? Mpagani au Mkristo? Au wote?? How still wana dhambi?
  “Amri mpya nawapeni….!” Unaijua amri hii kaka? Hebu twende ukaisome vizuri….Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.Mtt 22:37-40
  Chunguza kwenye zile amri 10. Amri ya 1-4 kwenye ubao wa kwanza, zinasisitiza upendo wetu kwa Mungu. Na hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza kaka Lwembe. Amri ya 5-10 kwenye ubao wa pili, zinasisitiza upendo wetu kwa wanadamu wenzetu. Na ya pili kwa ukuu ndiyo hii. Na kwa hakika, ziliandikwa hivyo. Na kwa vile Yesu alikuja kuzitimiliza, anawaambia kuwa AMRI ZOTE HIZI MBILI HUTEGEMEA TORATI NA MANABII. Kumbe amri mpya, msingi wake uko kwenye TORATI na MANABII. Torati ipi? Amri 10! Torati na manabii ni agano gani??
  Biblia iko wazi sana kaka. Ukiisoma kwa kufuata mtazamo wa kidhehebu/kidoctrine/kidini, utapotea tu maana utataka ikuhalalishie wewe kufanya kile ukipendacho hata kama ni dhambi mbele za Mungu.
  Naomba ninukuu, “Mwa 2:3 “Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.” Hii ndiyo Sabato ya Mungu, ndg yangu Siyi. Fungua uelewa!” Yaani hapa umesema kweli kabisaa. Hii ndiyo Sabato ya Mungu ya siku ya saba. Mimi nilishafungauaga macho tangu zamani sana. Ndiyo maana nakushauri na wewe ufungue macho yako!! Biblia iko wazi sana. Acha kudanganyika na doctrines!!
  Haya, hapa tena kapepo kakakukama shingoni na kukatii kabisa hadi ukaanza kumuita Mungu kuwa ni mwongo na mzushi. Ninanukuu, “Kut 20:1-17 hapo ndipo Israeli wanapopewa sabato, huko jangwani. Kwahiyo hayo mambo yenu ya sabato sijui alianzisha Mungu mwenyewe Edeni, ni uzushi tu wa kawaida ya waongo!” Si wewe uliyekiri hapo juu kwenye mwanzo 2? Hapa imekuwaje tena bro? Kama umekubali kabisa kuwa Adamu alipewa sabato kwa mara ya kwanza na Mungu mwenyewe apumzike siku ya saba ya juma; amri ambayo iliheshimiwa na viazi vyote vya Adamu hadi uzao wa Ibrahimu-Israel, utasemaje tena kuwa Waisrael walipewa sabato? Hivi unajua tofauti ya kupewa sabato na KUIKUMBUKA SABATO? Unasomaje kutoka 20:8-11…? Mungu tena kawa chizi hapa!!! Khaa!! Wewe tabu kweli kaka. Yaani inaonekana hata hujui unachopinga na unachokubaliana nacho!! Te te te teee!! Mungu, msaidie rafiki yangu Lwembe. Najua kuwa unampenda sana, ndiyo maana ulikufa kwa ajili yake pia. Baba, Mwokoe Lwembe na marafiki wengine wote! Kwa jina la Yesu ninawaombea, Amina.
  Ni kweli huko nyuma nilikwishiga kusema kuwa, Israel haitakuwa taifa TEULE tena!! Siyo taifa tu (kwa maana ya nchi) kama ulivyoninukuu wewe. Israel kama nchi hadi leo ipo. Na watu wake wapo japo wengine wamesambaa sana. Wayahudi wana nafasi ya kuokolewa kama mtu mmojammoja tu tena kwa wale watakaolipokea jina la Kristo waliyemkataa. Lakini habari za waisrael kurudishiwa ile heshima ya TAIFA TAKATIFU, TAIFA TEULE mbele za Mungu, haipo tena. Kwa sasa Mungu anadeal na waisrael wa kiroho tu basi(mataifa yote yanayompokea Kristo). Wagalatia 3:29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
  Na kuhusu dhambi, sijui huwa unatumia Biblia ya aina gani!! Maana huwa naona unachanganya mambo kweli kaka. Ninanukuu, “Hivi unadhani ni kwanini Hawa baada ya kulila lile tunda hakujitambua kuwa yu uchi? Umewahi kujiuliza hilo?” Hebu tuiulize Biblia kama kweli baada ya kula tunda, Hawa hakujitambua kama yu uchi!! Mwanzo 3: 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
  Unaona kaka unavyochanganya mambo? Hawa alijijua kuwa yu uchi. Ndiyo maana akakimbia na kutafuta majani. Hivi unaponukuu maandiko tofauti na Biblia, unajijua kuwa unakosea kaka? Ni mpofu kweli au huwa unafanya makusudi tu? Muhuri wa Mungu ni Sabato. RM anapokaa ndani yako, kazi yake huwa ni kukuongoza wewe katika KWELI-(Bibli) yote ambayo ndiyo injili yenye utii wa amri 10 za Mungu. Kazi kubwa ya RM katika maisha ya muumini yeyote, ni kutongoza katika KWELI ya MUNGU huku akituwezesha tusivyoviweza kama binadamu.
  Mwisho, torati(amri 10) ndio skeletoni ya injili aliyoifundisha Yesu na mitume wote. Tafadhari ifuate hiyo injili inayoendana na utii wa sheria za Mungu kama ulivyodokeza kwenye mchango wako hapo juu.
  Ubarikiwe na Bwana.

 34. Siyi, ndugu yangu, unanifurahisha sana kwa ukigeugeu wako! Ila kwa kuwa wewe mwenyewe umetangaza kuwa tuache dini, “tubaki na Biblia tu” hilo ni jema na la msingi sana, nakupongeza brother!

  Unanitaka nikupe Maandiko ambayo yatakuthibitishia kuwa hujajazwa RM, hilo pia ni jema. Sasa unapozungumzia kujazwa RM, tunaporudi katika Biblia, kulingana na Injili waliyopewa mitume, anayejazwa Roho Mtakatifu ni Mkristo tu! Naye Mkristo ni yule aliyehubiriwa Injili, yaani Torati iliyotimilizwa, akaipokea hiyo ikampa kuamini, akaitii kwa kuzitubia dhambi zake, maana ndani ya Injili hiyo kuna mashtaka ya uvunjifu wa sheria ambayo kwayo huyo aujiaye ukristo kutoka katika upagani au Ufarisayo au chaka lolote lile la dini, hukamatwa na hivyo kustahili Hukumu, ambayo ni Jehanamu ya moto! Hebu litazame shitaka hapa: “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu”(1Yoh 1:8). Umeelewa Siyi? Kujitambua kuwa wewe ni mwenye dhambi ndio ushuhuda wa kwanza kwamba ndani yako imo KWELI, yaani ile IMANI imeumbika! Yaani ukihubiriwa Injili ya kweli, na kama ndani yako imo ile mbegu ya Mungu, ule uzao, basi moja kwa moja nawe hukupata hali kama iliyowapata nduguzo pale walipoisikia Injili ya Petro, ndipo katika Mdo 2:37 wakiwa chini ya mashtaka, ”Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?”Injili hukuleta mpaka hapo Siyi, if at all umehubiriwa!

  Haya itazame NEEMA sasa, “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Umeelewa kaka? Maandiko hayapingani, hebu kitazame kifungu hiki, 1Yoh 1:9 ”Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”, umeelewa Siyi? Unaziungama dhambi zako halafu unabatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo, zinaondolewa mpaka mizizi yake, ule udhalimu! Siku ile waliingia watu 3000 katika Ufalme wa Mungu kupitia huo mlango alioufungua Petro, sasa jitazame nawe kama umepitia mlango huo sawa na hao, au wamekuchorea mlango ukutani nawe ungali unagonga kichwa hapo ukijaribu kuingia!

  Kwa wale wabishi, waliokataa kupita katika mlango huo alioufungua Petro, hao hawana cha kutubia, labda kuongozana katika sala za toba wasizo zielewa, yaani hawajui hata kama wana dhambi, bali huendelea katika unafiki, mioyoni mwao wakisema ‘kwamba hatukutenda dhambi, wakimfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwao.’

  Sasa kuhusu ninyi wa jinsi hii mlioikataa Injili na kujibandika ukristo kwa nguvu, angalia tabia zenu hapa, Rum 10:2-3 “Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.” Having a form of godliness …!!! umewaona hao katika bidii yao isiyokuwa na maarifa? Hawali nguruwe na wanyama wengine walionajisishwa kwa watu wa kale, wanaitunza sabato na zile amri 9 walizopewa watu wa kale; yaani kwa kukosa kwao maarifa, kwa mfano ile amri inayokataza kuzini, wao kwa tafsiri yao, kwa vile siku hizi Neema ya Kristo imezuia kuwapiga mawe wazinzi, (sijui ni lini ilizuia), basi wao huwaga wakizini wanakwenda kanisani kuiungamia hiyo dhambi, naye “roho mtakatifu” huwashuhudia msamaha mpaka uzinzi unaofuata!!! Halafu ndani ya makundi yao wanao mashoga na wasagaji wanaowahudumia wakitimiza “upendo”; HAWAIJUI HAKI YA MUNGU, NA WAKITAKA KUITHIBITISHA HAKI YAO WENYEWE! Bali HAKI ya Mungu imeyataka makundi hayo yatolewe katika miji yetu, nao mji wetu ukiwa ni Kanisa!

  Hivi Siyi, kivuli cha saa 3 asubuhi au saa 11 jioni, kinaweza kukupa taswira kamili ya mwenye kivuli? HAKIWEZI, maana kitakuwa ni kirefu kuliko mwenye kivuli, kama unayo maarifa! Ndio maana tunadhihirishiwa kuwa “Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki”; Amri mpya nawapeni….!

  Mambo mengine uliyoyazungumzia Siyi, kimsingi naona ni hayo hayo ya siku zote, na majibu yake uliyopewa yanaweza kujaa hata fuso 10, ila tu nimegundua kuwa huna uhuru wa kufikiri hata kidogo, hiyo ndiyo tabia ya Cults, huzikamata mental faculties za waumini wao in their totality bila hata kuwaachia nafasi ya kupumua. Hebu yaangalie maelezo yako haya uliyoyatiririsha:
  “Sabato ya amri ya nne siyo sabato ya kiyahudi kaka. Ni amri ya Mungu iliyoanzia tena kabla ya anguko la mwanadamu dhambini. Aliianzisha Mungu mwenyewe bustanini Edeni. Wayahudi wanatokea wapi hapo? Acha kuchanganya mambo!! Hata wakati wa amri kudhihirishwa tena pale mlimani Sinai, je waisrael waliokuwa utumwani Misri walikuwa ni Wayahudi? Naomba unisaidie kaka, huenda sielewi, nitafurahi kujifunza kutoka kwako.”

  Mwa 2:3 “Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.” Hii ndiyo Sabato ya Mungu, ndg yangu Siyi. Fungua uelewa! Kut 20:1-17 hapo ndipo Israeli wanapopewa sabato, huko jangwani. Kwahiyo hayo mambo yenu ya sabato sijui alianzisha Mungu mwenyewe Edeni, ni uzushi tu wa kawaida ya waongo!
  Kuhusu Waisraeli waliokuwa utumwani Misri, kwamba ndio hao Wayahudi? Nakumbuka huko nyuma uliwahi kusema kuwa Israeli haitakuwa taifa tena! Lakini ndivyo Cult zilivyo!!! Taifa la Israeli lilizaliwa siku waliyotoka Misri, nao utamaduni unaowafanya waitwe Wayahudi umezaliwa jangwani, ndio hiyo Torati na sabato na rabbinical Talmuds etc, hao wote taifa zima walikuwa katika kiuno cha Ibrahim!

  Pia kuhusu dhambi naona umeshindwa kabisa kuelewa, kwa hiyo huwezi hata kutamani kitu usichokielewa. Naona unao ufahamu mkubwa sana wa dhambi, kiasi kwamba huamini kuwa zinaweza kuondolewa! Na kwa vile hujaondolewa dhambi zako, zingali zinarundikana, basi ninauhakika maungamo unayoyafanya kanisani kwenu yanakusaidia kama zile sadaka za dhambi za kale, nawe hupata unafuu fulani, kitambo kidogo na mzunguko wa mauti hukurudia tena! Lakini kwa waliozaliwa mara ya pili hali zao ni tofauti, hao wamezaliwa kwa Roho wa Mungu, ndio hawa hapa, 1Yoh 3:9-10 “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” Basi mambo ndio yako hivyo ndugu yangu, utazunguka na madude ya uongo mpaka basi! Haya hayaeleweki kwa watu walioikataa kweli na kukubali uongo wa dini. Hivi unadhani ni kwanini Hawa baada ya kulila lile tunda hakujitambua kuwa yu uchi? Umewahi kujiuliza hilo? Asingeweza kujitambua kama ambavyo nawe usivyoweza kuyaona Maandiko yalivyo wazi, kwani upofu unaoandamana na kulikataa Neno la Mungu ni mkubwa sana! Wewe mwenyewe ni shahidi wa upofu huo, Unaoneshwa Muhuri wa Mungu katika Efeso 4:30, lakini huoni, umeng’ang’ana sabato na sijui sifa za mihuri, sijui hata kama unaelewa unachokisema, umepoteza network ya Injili? Hahahahah…..!!!

 35. Shalom kaka Lwembe,
  Nakushukuru kwa kuwa na nia kubwa sana ya kuendelea kujifunza. Tangu mwanzo, nimekuwa nikipiga kelele kuwa, tunapojadili habari za KWELI ya Biblia, ni sharti dini na mitazamo yetu yooote tuiweke mbali sana na tubaki na Biblia tu. Tukifikia hatua hii, tutaielewa vizuri sana Biblia. Tofauti na hapo, mmh!!
  Mimi nitakuomba unipe maandiko yanayothibitisha kuwa mimi sijajazwa na RM na NEEMA iliyotumika kulielewa Agano la kale, kama imeondolewa. Je, uliijua NEEMA hiyo vizuri au umejibu tu kaka? Mwenye kivuli alishakuja, ndiyo maana siku hizi hatuchinji tena mbuzi/kondoo, njiwa nk!! Neema hiyo imekuwa dhahiri sasa. Je, kitu kinapokuwa dhahiri ndiyo hupoteza mwonekano wake? Na kama sivyo, kwa nini tudumu katika dhambi kwa sababu ya NEEMA? Na wapi Mungu ameandika mambo magumu hadi watu wake yawashinde bila ya kuyalazimisha wao wenyewe yakubaliane na mitazamo yao?
  Sabato ya amri ya nne siyo sabato ya kiyahudi kaka. Ni amri ya Mungu iliyoanzia tena kabla ya anguko la mwanadamu dhambini. Aliianzisha Mungu mwenyewe bustanini Edeni. Wayahudi wanatokea wapi hapo? Acha kuchanganya mambo!! Hata wakati wa amri kudhihirishwa tena pale mlimani Sinai, je waisrael waliokuwa utumwani Misri walikuwa ni Wayahudi? Naomba unisaidie kaka, huenda sielewi, nitafurahi kujifunza kutoka kwako.
  Mmh, Yesu hakuja kuondoa dhambi ulimwenguni kaka. Alichokuja kukifanya, ni kitendo cha kumwokoa mwanadamu kutoka dhambini-kutoka mauti ya milele. Asili ya ile dhambi bado tunayo kaka. Ndiyo maana wewe bado ni mwenye dhambi na bado unazaa watoto wenye dhambi!! Na Biblia inakiri hilo kuwa kila aliyezaliwa na mwanamke ni mdhambi… Sasa utakuaje huna dhambi halafu ukazaa chenye dhambi?? Unachekesha kweli wewe!!
  Haya, wewe ni Lwembe rafiki yangu kipenzi tu. Mwangalie Paulo mtume aliyejazwa na RM full time hadi akaandika nyaraka nyingi sana ndani ya Biblia, but anakiri kuwa alikuwa na dhambi licha ya kuwa shosti wa RM wa karibu sana. Soma 7:15-20. Nakushauri uache kudanganyika kwa porojo za abunuasi kaka. Biblia iko wazi sana kwa kila kitu. Shida yako unasikiliza sana Biblia bila kusoma mwenyewe. Usipojishughulisha kujisomea Biblia kaka, utapotea kabisa. Chunga!!!
  Wasabato hatutumii nguvu kutunza amri 10. RM anatuwezesha through what Jesus did on the CROSS. So when we love Jesus, tunajikuta tu automatically-bila nguvu yoyote ya kimwili, tumetii tu amri zake kama ishara za upendo wetu kwake. Maana pendo ndiyo utimilifu wa sheria, rumi 10:13. So sheria zinapokuwa ndani ya mioyo yetu, matokeo yake hujibainisha kwa matendo ya mwili- Ndiyo maana neno linasema kwa matunda yao mtawatambua… Kutunza amri 10 kaka, ni matokeo ya kile kilichoko moyoni mwa muumini-upendo wake kwa Kristo. Mkinipenda mtazishika amri zangu….. Unaelewa sasa?
  Kama hata kujibidisha kusoma sources tunazokupa unaona ni shida, kwa kweli utaendelea kubaki kama ulivyo(kutokuwa na uelewa aka mjinga). Wakatholiki, wanachokifundisha si sawa na hicho walichokiandika kwenye vitabu vyao. Ndiyo maana nikakwambia nenda usome mwenyewe ili uone kama nakudanganya ama la!! Vinginevyo, utakesha kaka na falsafa zako hizo.
  Muhuri wa Mungu ni Sabato. Muhuri huwa una sifa hizi hapa; 1. Jina la mwenye muhuri. 2. Mamlaka yake/ukuu wake/position yake. 3. Eneo la utawala wake. 4. Ishara/alama ya umiliki. Nk. Sasa, cheki mwanzo 2:1-3, kutoka 20:8-11, ufunuo 14:6-7 nk. Soma halafu ujionee kama ni uhuni ama la!!
  Jitahidi kaka kuwa unasoma Biblia.
  Epuka kutumia akili zako kuchambua Biblia kwa kufavour interests zako. Hatari hiyo.
  Barikiwa

 36. Leo, ndg yangu Siyi, nitakupa siri nyingine kuhusu Maandiko, haswa Agano Jipya. Agano hili ndilo lenye ufunguo wa Agano la Kale! Kwa wewe unayeishi katika nyakati za Agano Jipya, ile neema ya kuyaelewa yaliyoandikwa katika Agano la Kale imeondolewa, kwahiyo ni lazima ujazwe RM kwanza huku katika Agano Jipya, ndipo ukirudi huko unaweza kuyajua yanayoelezwa. Jambo jingine linalolifanya jambo lote hilo kuwa gumu zaidi, ni jinsi Mungu alivyoyazungusha maneno yake kwa ustadi mkubwa sana katika Agano Jipya, kiasi kwamba yamewapoteza watu wengi sana wa dini!

  Amewatengeneza hata wanapojitahidi katika kuyatimiza hayo yaliyoandikwa humo, wao huishia katika jitihada za kimwili na hubakia hapo wakifurukuta kuyafikia hayo yasiyofikika! Ndio maana daima wao hupigana kuishinda dhambi, na matokeo yake huishia dhambini humo humo!

  Hebu zitazame kauli zako:
  Kuhusu Neema, unasema:
  “Zamani, NEEMA hii ilikuwepo, lakini ilikuwa ni kivuli cha Kristo” Sasa nikuulize, Je, KIVULI na MWENYE KIVULI chake, hao ni kitu kimoja? Kivuli hukupa shauku ya kumuona huyo mwenye kivuli chake, maana huyo ndiye ukamilifu wa kivuli hicho. Basi ukimuona mtu anag’ang’ana na kivuli, ilhali mwenye kivuli yupo, huyo anahitaji maombi!!!

  Sasa hebu tazama hapa Mungu alivyoyazungusha Maneno yake,
  “Tito 2: 11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.”

  Sasa kwa kuvisoma vifungu hivyo, wako watu wengi sana wa dini hujibidiisha katika hayo. Wamejipangia mambo mengi sana ili kuyafikia hayo. Ndio kama ninyi akina Siyi, milvyojipangia kuishika sabato ya kiyahudi huku mkiendelea katika machukizo mengine kinyume na Maandiko, lakini mkijihesabia Haki katika hiyo sabato, na mkikazana katika “kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa.” Mnajizuia katika hili na lile, leo umeanguka kesho umeinuka kwa maombi! Mnakuwa ni watu wazuri, jirani wazuri, kama Esau!

  Bali Mungu anazungumzia “siri ya utauwa”, hazungumzii bidii zetu! Nako kuzaliwa mara ya pili ni sehemu ya siri hiyo ndio maana kuna jambo la ufunuo ndani yake. Nimewahi kuwaambia huko nyuma kuwa mkristo ni yule ambaye Mungu amemuondolea ule moyo wa jiwe na kumuwekea moyo mpya wa nyama na kisha kumuwekea roho mpya na mwisho Mungu humuwekea ROHO WAKE! Basi hebu wazia jambo hili kwamba labda umchukue mbwa, halafu umfanyie upasuaji kisha umuwekee nature ya paka ndani yake, baada ya hapo mbwa huyo si ni lazima awe na tabia za paka! Umeelewa Siyi? Huyo ndiye Mkristo, huyo aliyebadilishwa nature yake, baada ya kufanyiwa upasuaji huo. Ndiye huyu hapa ambaye “amekombolewa na maasi yote”, ndani yake hakuna uasi tena, ile mbegu ya uasi imetolewa na kutupwa huko nje! Unaona, huyo ndiye Mkristo, amesafishwa, hana taka tena, hatendi tena dhambi, huyo sasa yuko katika milki ya Kristo, siyo milki ya dhehebu fulani, huko ambako dhambi bado inasumbua, kama unavyojishuhudia kwa kuirejea vifungu vya Torati vinavyotushitaki kwa dhambi ili tuikimbilie Neema nayi mkiwa niwale msioelewa mmebaki na mashitaka hayo maisha yenu yote!!!

  “Wale walio na juhudi katika matendo mema.” Watu wa dini hujitahidi sana katika hili. Hata nanyi akina Siyi mwajitahidi saana, hilo ni jambo zuri. Lakini zote ni jitahada zisizo ongozwa kwa ufunuo, ni jitihada za kimwili tu kama ambavyo wewe mwenyewe unavyoshuhudia hapo unaposema, “Matendo mema ni yapi kaka kama siyo yale matendo ya sheria(amri 10) ambayo imani HAI huthibitika?” Kauli kama hizi ndizo zinazothibitisha kwamba uelewa wako wa Maandiko bado uko katika mzunguko wa kimwili, haujavuka kuingia rohoni. Mwema yuko mmoja tu naye ni Mungu! Kwahiyo bila kubadilishwa nature yako na kupewa nature mpya ya Kristo, utaishia kufanya unafiki tu ambao wanafiki wengi hudhania na kuamini kuwa eti wana ‘juhudi katika matendo mema’, kama ambavyo ungewaona makundi ya kikristo wanapokwenda kuwatembela na kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza pamoja na wagonjwa mahospitalini huku wakiongozana na wapiga picha wa magazeti na television, lakini wameambiwa ukitoa na mkona wako wa kushoto hakikisha wa kulia haujui!!!

  Halafu unaposoma michango ya wengine jaribuni kuangalia wanachosema kuepuka kurudia rudia jambo kama sahani ya santuri iliyokwama! Tazama nimeandika hivi:
  “Sasa, kuna makundi yanasema, “Katoliki ya Kirumi ndio walioigeuza siku hiyo kutoka Jumamosi kuja Jumapili.” Nao Katoliki wanadai kulifanya jambo hilo, bali ni uongo mtupu.”
  Halafu wewe unarudi tena unaniambia eti nitafute katekesimu ya Wakatoliki humo ndimo nitaupata ukweli! Hivi unaelewa unachokisema kweli? Tangu lini unaweza kuupata ukweli kwa muongo? Kama ninyi mnautukuza uongo wa Wakatoliki kwa hila ya kuwadanganya maamuma, mnapaswa kujua pia kuwa si watu wote wajinga! Hivi mnafikiri ni mjinga gani asiyeweza kujua kuwa Mdo 20:7 ina maana hiyo hiyo kama ilivyoandikwa? Labda awe ni mjinga wa kupitiliza, huyo ndiye ambaye hawezi hata kujua kuwa katika siku hizo kulitokea mgawanyiko uliopelekea Wakristo kutengwa na hata kuuliwa kutokana na imani yao hiyo mpya ya Yesu Kristo iliyoifunga Torati kwa kuitimiliza kwa wote. Kwamba sasa hivi hata Myahudi asiyempokea Kristo na wapagani wote watahukumiwa kwa Torati iliyotimilizwa ambayo kwa lugha nyepesi inaitwa INJILI!

  Kuhusu Sabato kuwa ni MUHURI wa Mungu unaniambia eti nifananishe na sifa za muhuri wowote! Si nimekufananishia na Muhuri wa Mungu katika Efe 4:30, haulewi kitu, au ndio ule ubishi wa kuyabishia mpaka Maandiko aliokuambia Mabinza? Ninyi kwa mamlaka gani mmeubadilisha Muhuri wa Mungu na kuufanya ni kuitunza sabato? Acheni uhuni huo, au ndio tayari hamjali chochote baada ya kuanguka katika ile Laana mliyowekewa katika Gal 1:8? Ndio maana masikio yote yamekufa, ya kimwili na ya kiroho!!!

 37. Siyi niseme tu ukweli kwamba unakuja kwenye hii mijadala ukiwa umejiaminisha kuwa unachokijua wewe ndo kiko sahihi.
  Kuna ujinga mwingi kichwani mwako ambao umeweka mizizi kwenye mapokeo. ( Neno ujinga si tusi, bali ni sifa ile hali ya kutokujua jambo fulani)

  Tumekuonesha vizuri sana suala la sabato kwenye mjadala wa Yesu kutangua torati, lakini hata hapa bado unaongea vitu vilevile ambavyo tumekujibu kule.

  Kumbuka uliuliza sana kwenye ule mjadala uoneshwe mahali ambapo watu wa Mungu walikusanyika kwa ajili ya kufanya ibada siku ya kwanza ya juma, hpa Lwembe kakuonesha lakini umepinga kuwa hiyo haikuwa ibada kwa hoja dhifu sana.

  Kumbuka na mimi bila shaka nilikuuliza wewe kuwa Roho mtakatifu aliwashukia wale 120 siku gani hukunijibu.

  Ivi wewe unapoisoma hiyo Kutoka 20 inaposema ikumbuke siku ya sabato…,usifanye kazi ilisema kwamba ukusanyike kwa ajili ya Ibada siku nzima?

  Nilikwambia Siyi kuwa mimi kusali J2 siyo kuadhimisha siku, lakini wewe kwa kuwa umekaririshwa mapokea umeng’ang’ana tu kuwa sisi tunazimisha Jumapili. Wewe ni mtu wa namna gani usiyetaka kuelewa Siyi?

  Nikakuuliza tena swali, Je Mungu huwa hafanyi kazi Jumamosi? hukunijibu.

  Unataka tukaangalie maana ya neno sabato kwenye kamusi ili iweje sasa? Kamusi haitakupa majibu sahihi kama tuliyokupa katika blog hii Siyi. Usidhani tuliamua kumwamini Mungu kwa maneno ya mapokea, la hasha bali kwa kuuona udhihirisho wa nguvu zake katika maisha yetu. Hatukuweza kushida dhambi wenyewe ila tulipomwamini tuliweza.

  Na ili ujue kabisa kuwa huwa hatuadhimishi siku, mimi wala Jumapili huwa sishindi kanisani, bali humaliza ibada mapemaa na kuendelea na shughuli zangu zingine.

  Kuna kitu umebeza hapa, nakunukuu ”Aya uliyoinukuu katika matendo 20:7, haina maana ya kuumega mkate kama siku ya ibada. Walikutana kama tunavyokutana siku zingine zingine za kawaida kwa ajili ya maombi, kujifunza neno la Mungu nk…”

  Siyi kumbuka ukisoma mstari wa 6 utagundua kuwa hapo mahali walikaa siku saba,kwa nini hawakukutana siku ya saba wakakutana siku ya kwanza kuumega mkate? Na nataka uniambie kwa maandiko siku ya ibada uliyoisema hapa yenyewe mkate ulikuwa unamegwaje tofauti na hiyo siku ya kwanza walivyoumega kwenye Mdo 20:7?

  Halafu wapi biblia inasema walikuwa wa kwanza kumshuhudia Yesu alipofufuka walikuwa ni wasabato? maana mimi najua hapakuwa na usabato wala ukristo wakati huo.

  Karibu!

 38. KAka Edwini,
  Umesema vyema. Ila hujafafanua vizuri maana ya kuwa chini ya NEEMA. Kumbuka zamani, watenda dhambi wote(wavunja amri 10), badala ya kufa,walipaswa kuchinja kondoo/njiwa/mbuzi/ng’ombe nk kwa ajili kafara ili wasalimike kufa kwa mujibu wa by laws!! Yesu alikuja kuziondoa zile by laws tu na siyo ten commandments. Kwamba, leo wadhambi wote, badala ya kuchinja ng’ombe/kondoo/mbuzi/njiwa nk ambayo kwa kweli ilikuwa ni gharama kubwa kwa watu, Yesu aliiondoa gharama hiyo, hivyo wanapaswa kumwendea Kristo tu na dhambi zzao zitasamehewa mara moja. Yesu mwanakondoo wa Mungu alishachinjwa! Na kifo cha Kristo, hakitupi uhuru wa kuvunja katiba iliyokuwa na hizo by laws zilizoondolewa na Kristo.Kwa maneno mengine, tunapokuwa chini ya NEEMA, ni sharti tuishi kwa kufuata katiba ya Mungu yaani utii wa amri 10 ikiwemo na sabato. Ndiyo maana leo wakristo wote, wanafahamu kuiba ni dhambi, kuzini ni dhambi, kushuhudia uongo ni dhambi, kuvunja sabato ni dhambi nk. Ukiwauliza kwa nini iwe hivyo, wanakwambia Mungu hapendi maana ni dhambi mbele za Mungu. Sasa kama ni dhambi, dhambi tunaijuaje bila bila ya kuwa na sheria(katiba)?
  Kaka Edwini, kuwa chini ya NEEMA ni sawa na kupata msamaha wa Rais kwa wafungwa. Msamaha huo huwa hawaweki huru kwenda kuendelea kuvunja sheria za nchi, bali wanapaswa wakawe raia wema wakiishi kwa kufuata katiba/sheria ya nchi. Na hiki ndicho kilichofanyika msalabani ndg yangu. Tunapokuwa chini ya NEEMA, UTII wa amri 10 ni sharti ufuate!! Tofauti na hapo, tutaitafsiri Biblia tu kwa favour interests zetu jambo ambalo sidhani kama ni zuri.

 39. For English men/women
  Who Are the Children of God?
  Who Are the Children of Satan?

  For those of us who call upon the name of the Lord, we believe that we are the children of God, we believe, with the most sincere of hearts, that we belong to our Heavenly Father. From the very beginning of God’s Word, we can plainly see that there are two different seeds, those whom belong to Yahweh and those whom belong to the devil. But how do we know to whom we belong? If we believe in God, does that mean we belong to Him? Even satan believes in God, but satan will soon face his doom. So how do we know? Whom belongs to whom? Do you belong to God? Do I belong to God? Or do we belong (or give our allegiance to) the enemy???

  Genesis 3:15 “And I will put enmity between thee and the woman, and between thy seed and her seed; it shall bruise thy head, and thou shalt bruise his heel.”

  “Thy seed” is referring to the seed, or spiritual children, of the serpent, the devil, satan. “Her seed” is referring to the spiritual children of the woman, of the church of Yahweh, the children of God. This same spiritual seed that brought forth Jesus Christ, to whom was born of a virgin by this same “spirit”, and in whom no corruption was found.

  Revelation 12:17 And the dragon was wroth with the woman, and went to make war with the remnant of her seed, which keep the commandments of God, and have the testimony of Jesus Christ.

  So you see, this same serpent, the dragon, aka the devil, hates the woman and wages war with the remaining of her seed. This same spiritual seed is found in those who “keep the commandments of God, AND have the testimony of Jesus Christ.”

  May God give us understanding of His word. Let us take a look into this for deeper understanding, for His wisdom and knowledge that all would be led to the truth of God’s perfect Word, praise God!

  So, who’s who? Which is which?

  1 John 3:10 “In this the children of God are manifest, and the children of the devil: whosoever doeth not righteousness is not of God, neither he that loveth not his brother.”

  (here is the NIV translation of the same verse as above 1 John 3:10)

  “This is how we know who the children of God are and who the children of the devil are: Anyone who does not do what is right is not a child of God; nor is anyone who does not love his brother.”

  Doing what is righteous can be summed up in the 10 Commandments, for the Commandments of the Father is righteousness,. Doing “what is right” is walking in obedience to the laws of God. How does one know what love for “his brother” is??? Please revisit the 10 Commandments of the Father in Exodus 20. The first four sum up “loving God” and the last six sum up “loving our neighbors”~ Anything contrary to the commandments of the Father, or the law of God, is of the devil.

  1 John 3:8 “He that committeth sin is of the devil; for the devil sinneth from the beginning. For this purpose the Son of God was manifested, that he might destroy the works of the devil.”

  So what is sin? Sin is transgression from the law of the Royal and eternal 10 Commandments.

  1 John 3:4 “Whosoever committeth sin transgresseth also the law: for sin is the transgression of the law.”

  Christ is the King of this Kingdom and this Royal law is the law of His Kingdom and His Kingdom is now! Sin is of the devil. Christ died, taking upon Himself the penalty for our sin, but there is still a standard. Righteousness comes by faith in Christ, by this faith we are reconciled to God, and in this, having forgiveness for all of our sin, we are NOW obligated to walk in obedience to our Heavenly Father, His way! Becoming His children. Please remember, righteousness is not only achieved by believing in Christ, but by first believing and receiving forgiveness which results in cleansing and then to obedience. Understanding God’s mercy and grace and being led by the Spirit of God will result in obedience to the Father, obedience to the laws of the Father.

  Here’s an example:

  Let’s say that you broke a law that required a penalty of imprisonment, you went in to see the judge. This judge had mercy upon you, he acquitted you of all charges and set you free. What mercy! Now, would you exit the doors of the courthouse to go out and break the same law or laws, which would result in the same penalty???? Absolutely not~ Because of the mercy of this judge, you would now be obligated to walk in obedience to the law or laws of the land. The same law or laws that you once walked in complete disobedience to. Simply because of the mercy that was given to you. This is the same of the Father. In His great love and mercy, He freed us from the penalty of our sin, the penalty of death. He did this through His beloved Son. He paid the penalty and we have now been set free. Our obligation is to go and “sin no more”. Our obligation is to obey the law of His Kingdom, the righteous and eternal 10 Commandments. NOT to continue breaking the same laws for which the penalty was death.

  So we can see from the above verses that those whom continue to sin, or walk in willful disobedience to the Lord, are considered to be “of the devil”~

  1 John 5:18 “We know that whosoever is born of God sinneth not; but he that is begotten of God keepeth himself, and that wicked one toucheth him not.”

  (Remember, sin is the breaking of God’s holy commandments and is of the devil. Sin is contrary to the commandments of the Father.)

  Matthew 5:37 But let your communication be, Yea, yea; Nay, nay: for whatsoever is more than these cometh of evil.”

  (lying is of the devil. Lying is the breaking of God’s holy commandments Exodus 20:16)

  1 John 3:12 “Not as Cain, who was of that wicked one, and slew his brother. And wherefore slew he him? Because his own works were evil, and his brother’s righteous.”

  (murdering is of the devil. Murdering is the breaking of God’s holy commandments Exodus 20:13)

  John 8:44 “Ye are of your father the devil, and the lusts of your father ye will do. He was a murderer from the beginning, and abode not in the truth, because there is no truth in him. When he speaketh a lie, he speaketh of his own: for he is a liar, and the father of it.”

  It is interesting to note that Jesus was speaking to the Sadducee’ and Pharisee’ here. These claimed that the God of Abraham, Isaac, and Jacob was their same God. These claimed that they followed God, Yahweh. But Christ, the King of Kings, saw these men differently, He knew their hearts. Jesus Christ said that these were not of the Father, but of the devil. If they loved God, they would have recognized the Messiah, Jesus~ If God was their Father, they would have not sought to kill Jesus, whom had no sin. Remember the commandment, “thou shalt not kill”. They wanted to slay an innocent man, the very Son of God!

  It is clear to see that those whom belong to the serpent, the devil, satan, are those whom walk in sin, those whom willfully walk in disobedience to the Commandments of the Father.

  So who are the children of God?

  The children of God love their neighbors as themselves, 1 John 3:10 (an example of this is found in the 10 Commandments; Exodus 20 the last 6 Commandments). The children of God keep His Commandments and love one another.

  1 John 5:2 “By this we know that we love the children of God, when we love God, and keep his commandments.”

  Whoever is born of God does not go on sinning (1 John 5:18).

  1 John 3:9 “Whosoever is born of God doth not commit sin; for his seed remaineth in him: and he cannot sin, because he is born of God.”

  1 John 3:6 “Whosoever abideth in him sinneth not: whosoever sinneth hath not seen him, neither known him.”

  1 John 2:4 “He that saith, I know him, and keepeth not his commandments, is a liar, and the truth is not in him.”

  Walking in complete and willful disobedience to the Father’s 10 Commandments is contrary to God. Anything contrary to the Father is of the devil. Are we walking in obedience to the 10 Commandments of the Father? Each and everyone of them? If the answer is no, then we are being tempted, through deception, by the enemy. If we are not walking in obedience to God’s Holy Laws, then we do not know Him. His word says if do not obey His commandments, but say that we know Him, we are a liar. My brothers and sisters, I don’t want the Lord to see me as a liar. I want to be one of His very own and I know that you do as well.

  If we claim to know God, but by our actions we deny Him, we are in big trouble.

  Titus 1:16 “They profess that they know God; but in works they deny him, being abominable, and disobedient, and unto every good work reprobate.”

  Our Father’s 10 Commandments still stand. They are eternal. If we are being taught otherwise, sadly, we are being deceived. Do we want to be known as the children of God? Or do we want to be tricked into a counterfeit worship of the enemy? Belonging to the enemy. Remember, the devil tricked Eve out of having immortality which banned Adam and Eve from the beautiful Garden of Eden. His plan is the same. He wants nothing more than to deceive us. To steal salvation right from underneath us. He wants our fates to be the same as his. He has little time and has devised a plan to do this. What a better way than to deceive God’s people into walking in complete disobedience by creating a “theology” that says that our Father’s 10 Commandments are no longer standing. This is false doctrine at it’s best and the results of not keeping the laws of the Father come with eternal consequences. To know Him is to keep His commandments. To love Him is to obey His commandments. He sent His only Son to take upon Himself the punishment for our sin. That we would be cleansed, receive the Spirit of God, and go and “sin no more”.

  I pray this message finds you well. I pray that you meditate on God’s Word and that He would reveal His truth and love to you.

  Matthew 13:38 The field is the world; the good seed are the children of the kingdom; but the tares are the children of the wicked one;

 40. Yesu hakupingana na Torathi ila aliitimiliza Torathi ,Kolosai 2:14-,Alizikubali hukumu zote torathi ilivyosema.Adhabu zake zote alizikubali na akazilipa kwa kifo pale msalabani(akazilipa).Hivyo torathi ikaishiwa nguvu kwa sababu lolote lililohukumu tayari kifo cha Yesu kilitimiliza(Ndiyo maana Yesu akasema hakuja kuitengua bali kuitimiliza).Na baada ya hapo wayahudu walioongozwa na torathi(sheria) ili kumuona Mungu na Watu wa Mataifa ambao hatukuwa na Mungu Duniani(Wote kwa Imani ya kukubali kwamba yesu amelipa deni letu tunahesabiwa haki bure kwa imani siyo kwa sheria tena),Katika ili haimaniishi kwamba sisi tuwakamilifu bali Yesu tunayempokea na Kumwamini haki yake ndiyo huonekana ndani yetu mbele za Mungu.Rumi 3:23-kwa sababu wote tumetenda dhambi tulistahili hukumu ya Jehanamu kwasababu bado tusingeweza kwenda Msalabani kama Yesu kwasababu sisi tumezaliwa na urithi wa dhambi,Yesu hakurithi dhambi ya asili,Mimba yake ni kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Tunapomwamini yesu tunapata haki bure na hii ndiyo neema.

 41. Ndg Lwembe,
  Binafsi nakushukuru sana kwa jitihada zako za kufuatilia mijadala na kutoa michango mingi yenye tafakari kubwa. Changamoto zako ni nzuri sana. Niende kwenye hoja zako.
  Kwa uelewa wangu kuhusu TORATI na NEEMA, naona kama unavichanganya. Sina haja ya kukueleza maana ya TORATI, ila nitakueleza maana ya NEEMA japo unaifahamu pia. Neema ni upendeleo apewao mtu bila ya kustahili. Zamani, NEEMA hii ilikuwepo, lakini ilikuwa ni kivuli cha Kristo, kwa maana kwamba, badala ya mdhambi kuuwawa kwa mawe, kondoo/njiwa/ng’ombe nk asiye na hatia alichinjwa kumwaga Damu ili kuchukua hatia ya mdhambi. Hii ilikuwa ni Neema ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni fumbo. Neema hiyo ilikuja kufunuliwa dhahiri na Kristo mwenyewe. Tito 2: 11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.

  Matendo mema ni yapi kaka kama siyo yale matendo ya sheria(amri 10) ambayo imani HAI huthibitka? Neema hiyo ambayo ni Kristo mwenyewe yatufundisha kuuacha UOVU/DHAMBI. Warumi 6: 1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
  Kaka Lwembe, uwepo wa NEEMA, tangu zamani, haukuwahalalisha watu kutenda dhambi badala yake, walipaswa kuenenda sawasawa na amri 10 za Mungu-yaani kutotenda dhambi tena. Ndiyo maana Yesu mwenyewe aliye NEEMA, alikuwa akiwapa watu neema na kisha kuwaambia USITENDE DHAMBI tena!! Neema inapokuwepo, hutuondoa kwenye adhabu ya papo hapo na hivyo kutufanya tuishi sawasawa na sheria za Mungu. Kristo aliye NEEMA, anatufundisha kuzishika sheria zake kama ishara za upendo wetu kwake…NEEMA sharti iendane na utii, utii wa nini?-Amri kumi za Mungu.

  Na kuhusu maana ya sabato uliyoitoa, sidhani kama iko sahihi kikamusi na hata kibiblia. Nafikiri iko kimtazamo zaidi. Jaribu kuiangalia kwenye kamusi yoyote ile, au Biblia yenyewe. Mimi nitakupa maana ya sabato. Sabato maana yake ni pumziko. Pumziko la kimwili, kiroho, kiakili nk. Kwa hiyo neno RAHA linaweza kuwepo ndani ya pumziko lakini si kila mwenye RAHA anapumziko!! Isipokuwa, mwenye pumziko, ni sharti awe na RAHA.
  Kipengele kingine, Sabato hawakupewa wayahudi kaka. Amri 10 za Mungu hawakupewa watahudi tu. Walipewa wanadamu wote. Hata sabato, Yesu hakusema kuwa ilikuwa ni ya wayahudi, bali alisema kuwa ni sabato kwa ajili ya wanadamu- kama wewe ni mwanadamu, sabato na amri zingine 9, zilifanyika kwa ajili yako. Marko 2: 27 Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. 28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

  Kuhusu kugeuza jumamosi kupeleka jumapili, Biblia iko bayana/wazi sana kuwa mfumo wa RUMI ndio uliobadili amri za Mungu. Biblia ilitabiri juu ya hilo na ikatoa ONYO KUBWA sana kwa watakaofuata ukengeufu huo wa RUMI. Lakini zaidi ya hayo, RUMI ni watu wasioficha mambo yao sana, maana walichokifanya huwa wanasema wazi wazi. KAMA UNABISHA, TAFUTA KATEKSIMU ile ya kiswahili YA WAUMINI YA SASA, HALAFU ISOME KWENYE SURA YA SIKU YA IBADA NI IPI…Watakwambia live bila chenga kuwa wao ndio waliobadili. Nakupa hiyo homework, nenda katafute. Otherwise, rejea kwenye mjadala wa namna hii ulioanzishwa na ndg Milinga, ndugu yetu Lenda alinukuu kateksimu ya kiingereza hapo akionesha kuwa, RUMI ndiyo waliobadili taratibu za ibada na sheria za Mungu. Wao wenyewe wamekiri hilo. Waweza kupitia huko ama nenda kabisa moja kwa moja kwenye hiyo ya kiswahili ya sasa inasema wazi sana. Aidha, tembelea hata Kuruani nayo itakupa ukweli juu ya kuiheshimu TORATI ya Mwenyezi Mungu ikiwemo Sabato. Aya uliyoinukuu katika matendo 20:7, haina maana ya kuumega mkate kama siku ya ibada. Walikutana kama tunavyokutana siku zingine zingine za kawaida kwa ajili ya maombi, kujifunza neno la Mungu nk na kisha kabla au baada ya hayo, huwa tunaendelea na kazi zetu. Biblia imeiweka bayana kuwa ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma-jumapili, sasa jiulize, ni mtume nani alikutana siku ya kwanza ya juma kama siku ya ibada-yaani pumzikola kimwili, kiroho na kiakili-kutwa nzima? Soma vizuri sura hiyo utaelewa makusudi na malengo ya Paulo kuwambia watu wakutane siku ya jumapili. Aidha, jifunze zaidi siku ya jumapili, Paulo mwenyewe aliiadhimisha kama siku nzima ya ibada? Jawabu ni hapana. Aya lukuki ndani ya Biblia, zinaonesha kuwa, Paulo kama mitume wengine, waliitunza siku ya saba-jumamosi kama siku ya ibada na ndiyo waliyoifundisha kwa kanisa la kwanza. Sasa, jiulize leo kumetokea nini tena? Shetani yuko kazini!! Tena anajua kuwa muda wake ni mchache sana. Afanya haraka kuwapotosha yumkini hata wewe kaka Lwembe mteule wa Mungu. Chunguza vizuri mambo haya!!

  Ndani ya Biblia, hakuna hata aya moja inayoshabikia watu wakutanike siku ya jumapili kama siku nzima ya ibada eti wakiadhimisha kufufka kwa Bwana Yesu. Yesu hakusema siku ya ufufuo wake watu waiadhimishe, hata mitume hawakufanya hayo. Wasabato ndiyo walikuwa watu wa kwanza kutambua Yesu amefufuka na siku ya sabato walipumzika kama ilivyoamriwa. Ukisema kuwa wasabato hawautambui ufufuo wa Yesu, huo nao sidhani kama ni msimamo sahihi kaka. Chunguza vizuri.

  Kuhusu sabato kuwa ni MUHURI wa Mungu, hebu jaribu kuangalia sifa za muhuri wowote, halafu uilinganishe na amri ya nne. Homework nyingine nakupa.

  Kama kweli umeamua kulifuata neno la Mungu, ni dhahiri kuwa huwezi kubweteka kuwa sasa hivi uko huru tu kutenda dhambi kisa Yesu alikufa msalabani. Yesu alipokuja, alizitilia mkazo zile sheria. Yaani badala ya kuonekana kwa mwili ukitenda dhambi, Yesu aliwataka watu wasiwe wanafikiri hata huo uovu ambao matokeo yake, ni hizo dhambi zinazoonekana kwa macho. Kwa maneno mengine, mtu hawezi kutenda jambo lolote ni mpaka lianzie moyoni kwanza. Na moyoni ndimo Mungu huangalia, sisi wanadamu tunaangalia nje tu. Yesu hakutaka kuona uovu wowote anaponiona mie Siyi, ndani ya moyo wangu.

  Tunapovunja amri kumi, siku hizi katika agano jipya, hatupondwi mawe kaka Lwembe wala hatuchinji tena kondoo/mbuzi/njiwa nk, badala yake NEEMA/Yesu Kristo ametuweka huru ktk hilo. Kinachotakiwa, ni kuishi sawasawa na hivyo NEEMA(yaani kutotenda dhambi/kutovunja tena sheria 10 zaMungu), ili ituokoe siku ya mwisho.

  Mwisho, Mungu hakuwapa wayahudi zile amri 10 bali walipewa wanadamu. Mlimani, Sinai, waisrael, walipewa kama kudhihirishiwa tu maana walikuwa utumwani-kwenye kuabudu sanamu za misri. Walimsahau Mungu wa Baba zao akina Adamu, aIbrahim, Isaka nk. Ndiyo maana kwenye ile amri ya nne, Mungu amesema “IKUMBUKE…” maana yake nini? Maana yake ni kwamba, Sabato(na amri zingine zote 9) ilikuwepo tangu mwanzo. Tangu mwanzo, katiba ya Mungu (amri 10), haibadiliki. Yesu hakuibadili na hata mitume wake, hawakuibadili. Sisi wanadamu tuna mamlaka gani ya kulibadili neno la Mungu?? Ni hatari kulibadili neno lake. NEEMA na TORATI, havipingani kaka. TII uishi, ASI ufe…fulstop!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s