Je tunaishi katika siku za mwisho?

wakati

* Je ni mambo gani yanayotokea leo yaliyotabiriwa katika Biblia?
* Neno la Mungu linasema watu wangekuwaje katika “siku za mwisho”?
*Biblia inatabiri mambo gani mazuri kuhusu “siku za mwisho”?

VITA MBINGUNI

(Danieli 7:13, 14) Muda mfupi baada ya kupokea mamlaka ya Ufalme, Yesu alichukua hatua. Biblia inasema kwamba “Vita vikatokea ghafula mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka mkubwa [Shetani Ibilisi], naye joka mkubwa na malaika zake wakapigana.”* Shetani na malaika zake waovu, yaani, roho waovu, walishindwa katika vita hivyo na kutupwa duniani kutoka mbinguni. Malaika waaminifu wa Mungu walifurahi kwamba Shetani na roho wake waovu walikuwa wametupwa nje. Hata hivyo, wanadamu hawangepata furaha hiyo. Biblia ilitabiri hivi: “Ole wa dunia…kwa sababu Ibilisi ameshuka kwenu, akiwa na hasira kali, akijua kwamba ana kipindi kifupi cha wakati.”—Ufunuo 12:7, 9, 12.

Tafadhali ona matokeo ya vita hivyo vya mbinguni. Kwa hasira, Shetani angeleta ole au taabu duniani. Kama utakavyoona, sasa tunaishi katika kipindi hicho cha taabu. Lakini hakitakuwa kirefu, ni “kipindi kifupi cha wakati.” Hata Shetani anajua hivyo. Biblia inakiita kipindi hicho “siku za mwisho.” (2 Timotheo 3:1) Tunafurahi sana kujua kwamba karibuni Mungu ataondoa matatizo ambayo Ibilisi husababisha duniani. Hebu tuchunguze mambo fulani yaliyotabiriwa katika Biblia ambayo yanatendeka leo. Mambo hayo yanaonyesha kwamba tunaishi katika siku za mwisho na karibuni Ufalme wa Mungu utawaletea baraka za milele wale wanaompenda Mungu. Kwanza, tuchunguze mambo manne katika ishara ambayo Yesu alisema ingeonyesha kwamba tunaishi katika siku za mwisho.

MATUKIO MAKUBWA YA SIKU ZA MWISHO

VITA,NJAA,MISIBA.
1.“Taifa litasimama kupigana na taifa na ufalme kupigana na ufalme.” (Mathayo 24:7) Mamilioni ya watu wameuawa vitani katika miaka 100 iliyopita. Mwanahistoria mmoja Mwingereza aliandika hivi: “Watu wengi zaidi waliuawa katika karne ya 20 kuliko wakati mwingine wowote… . Katika karne hiyo kulikuwa na mfululizo wa vita, kukiwa na vipindi vifupi vichache vya wakati ambapo hakukuwa na vita mahali fulani ulimwenguni.” Ripoti ya Taasisi ya Worldwatch ilisema hivi: “Idadi ya watu walioathiriwa na vita vya karne [ya 20] ilizidi mara tatu ile ya watu walioathiriwa na vita vyote vilivyopiganwa tangu karne ya kwanza W.K., hadi mwaka wa 1899.” Zaidi ya watu milioni 100 wamekufa kwa sababu ya vita tangu mwaka wa 1914. Hata ikiwa tunahisi maumivu kwa sababu mtu mmoja tunayempenda ameuawa vitani, hatuwezi kuelewa kikamili taabu na maumivu ya mamilioni ya watu wanaofiwa.

2.“KUTAKUWA NA UPUNGUFU WA CHAKULA.” (Mathayo 24:7) Watafiti wanasema kwamba kiasi cha chakula kimeongezeka sana katika miaka 30 iliyopita. Hata hivyo, bado kuna upungufu wa chakula kwa sababu watu wengi hawana pesa za kutosha kununua chakula au mashamba ya kukuza vyakula. Katika nchi zinazoendelea, watu zaidi ya bilioni moja ni maskini hohehahe. Wengi wao hawapati chakula. Shirika la Afya Ulimwenguni linakadiria kwamba watoto zaidi ya milioni tano hufa kila mwaka kutokana na utapiamlo.

3“KUTAKUWA NA MATETEMEKO MAKUBWA YA NCHI.” (Luka 21:11) Kulingana na Uchunguzi wa Kijiolojia wa Marekani, tangu 1990 kumekuwa na wastani wa matetemeko 17 ya nchi kila mwaka ambayo yana nguvu za kutosha kuharibu majengo na kupasua ardhi. Na kwa wastani, kila mwaka kumekuwa na matetemeko yenye nguvu za kutosha kuharibu majengo kabisa. Shirika lingine lilisema: “Matetemeko ya nchi yamesababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu katika miaka 100 ambayo imepita na maendeleo ya kitekinolojia yamepunguza vifo kwa kiwango kidogo tu.”

4.“KUTAKUWA NA TAUNI–MAGONJWA.” (Luka 21:11) Licha ya maendeleo ya kitiba, magonjwa ya zamani na mapya yamewakumba wanadamu. Ripoti moja inasema kwamba magonjwa 20 yanayojulikana sana—kutia ndani kifua kikuu, malaria, na kipindupindu—yameanza tena kuenea katika miaka ya karibuni, na inazidi kuwa vigumu kuponya aina fulani za magonjwa hayo kwa dawa. Angalau magonjwa 30 mapya yamezuka. Baadhi yake ni hatari na hayawezi kutibiwa kwa dawa yoyote.

WATU WA SIKU ZA MWISHO
Wengi hupuuza mwongozo wenye hekima wa Neno la Mungu

Biblia haielezi tu mambo ambayo yangetukia ulimwenguni bali pia ilitabiri kwamba jamii ya wanadamu ingebadilika katika siku za mwisho. Mtume Paulo alieleza jinsi hali ya watu kwa ujumla ingekuwa. Tunasoma hivi katika 2 Timotheo 3:1-5: “Katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.” Kwa sehemu, Paulo alisema kwamba watu wangekuwa

wenye kujipenda wenyewe
wenye kupenda pesa
wasiotii wazazi
wasio washikamanifu
wasio na upendo wa asili
wasiojizuia
wakali
wanaopenda raha badala ya kumpenda Mungu
wenye namna ya ujitoaji-kimungu lakini wakizikana nguvu zake

5. Je, hivyo ndivyo watu walivyo katika eneo lenu? Bila shaka. Watu walio na tabia hizo mbovu wako kila mahali. Hilo linaonyesha kwamba hivi karibuni Mungu atachukua hatua kwa kuwa Biblia inasema: “Wakati waovu wanapochipuka kama majani na wote wanaotenda mambo yenye kuumiza wanapochanuka, ni ili wao wapate kuangamizwa milele.”—Zaburi 92:7.

Kwa maana hiyo yote yanayotokea katika ulimwengu wa sasa wala yasikushangaze kwa maana yalitabiriwa zamani,kelele za shetani zikupe nguvu ya kupambana na kumshinda,silaha kuu ya kumuangamiza shetani sio bunduki,mabomu wala mapanga bali ni BIBLIA TAKATIFU.

HITIMISHO.

Natabasamu ninapoona Matusi ya watu wa imani nyingine wakitukana hapa kwenye kurasa kwa maana wanaonyesha dhahiri shetani anavyoanguka, Hapa ni suala la Muda tu Shetani na wafuasi wake kuumbuka, ila Inasikitisha sana na pia huruma kuu hunijaa pindi ninapoona vijana wadogo na hata watu wazima wakimkana na kumtukana Mungu kwa kupotoshwa tu na imani zao na mahudhui ya shetani waliyopewa,ufunuo wa shetani waliopewa na hata kuabudu Mitume na manabii wa uongo (Hadaa za Shetani), ila atashindwa vita maana Katika siku hizi za mwisho, habari njema ya Ufalme inahubiriwa ulimwenguni pote. —Mathayo 24:14.

MUNGU AKUBARIKI.

– Familia ya Mungu – FB

Advertisements

9 thoughts on “Je tunaishi katika siku za mwisho?

  1. Wapendwa watoto wa Mungu,

    Naamini hamjambo, mimi nami sijambo. Nifaraja sana kuona kuwa watu wanakumbushana kuwa iko siku kutamalizika kitu hiki kinachoitwa utawala wa Kilimwengu, wengi husema mwisho wa Dunia, wengine husema kuja kwa Yesu mara ya pili. Mimi sibishani na Falsafa hizo zote, Kwa mjibu wa Uf. 21:1, nakubali kuwa kweli kuna siku ya mwisho. Ni taabu ya Akili za wanadamu wote, wanadini na wapagani wote kutaka kujua kwamba, hasa mwisho huo utakuwa lini? Inazaniwa na wataalamu wa sayansi za kidunia kwamba, mojawapo ya sababu za watu hushughulika na Dini ni kwa sababu hofu ya mwanadamu juu ya siku hiyo inayoitwa ya Mwiso!

    Falsafa za watu wa Dini, zinakubaliana na falsafa za kidunia Kuwa, Mungu ni utatu, yupo Mungu baba, Mungu mwana na Mungu roho ambao kwa pamoja ni MMOJA. Yesu akiwa Mungu Mwana, hapo hapo wakiliacha bila majibu lile swali kwamba, “IWAPO WATATU HAWA NI MMOJA NA WOTE SAWA, KWA NINI MUNGU BABA PEKEYAKE AIJUE NA KUWA NA MAMLAKA PEKEE JUU YA ILE SIKU YA MWISHO?” Huku hawana uhakika na majibu yao, hubakia tu wakisema kwamba YESU HAKUIJUA SIKU HIYO YA MWISHO kwakuwa yeye ni MWANA tu! Kwangu jibu kama hilo halina maana yeyote; kwa sababu, Thiori kama hizo na zingine za wana Theolojia zimedumisha; Mafundisho hayo ya uongo yanayoendelea kuwepo hadi sasa ninapoandika hapa! KIUKWELI YESU ALIIJUA NA ANAIJUA SIKU HIYO YA MWISHO NA KATIKA SIKU ZETU AMEIWEKA WAZI KUWA NI LINI!

    Mimi ni “MUUMINI” wa Biblia, NAMWAMINI YESU KUWA NDIYE BABA, NDIYE ROHO MTAKATIFU NA NDIYE MWANA, MFALME WA AJABU NA NI MUNGU MWENYE NGUVU. Sasa kama ndivyo, MUNGU KAMWE HAWI MUONGO! Kwa maana hiyo siku hiyo ya mwisho aliijua KABLA YA KUWEKO MISINGI YA DUNIA! Watu huchanganyikiwa wanapomsikia Yesu akisema “BABA” ndiye ajuaye; Hawaelewi kuwa ule mwili wa Yesu ulifanyika kwa Uweza wa Roho mtakatifu, kwa maana hiyo mwili ule ndiyo hasa MWANA, kwa kuwa ndiyo uliozaliwa, kwa mjibu wa Neno la Mungu ambalo linazitaja Sheria za kimaumbile waziwazi kuhusu uzazi kuwa, “CHENYE MWILI HUZALIWA” Gal. 4:4 inasema hivi, “4Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe, ambaye alizaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria”

    Mwenye mbegu ni Baba wakati Mama huwa na Yai. Kwa maana hiyo mtoto ni wa Baba! Baba wa mwili huo lazima awe ndiye Yule Roho mtakatifu, Mt. 1:18 hadi 20 inasema hivi, “18Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu”. Neno linaendelea kusema, “20………… “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu”. Kwa mistari hiyo michache tunaona kuwa “Baba yake Yesu” ndiye Roho mtakatifu, lakini Roho mtakatifu ndiye Mungu (Mungu ni Roho), pia kupitia Yh. 1:1, tunajua kuwa Yesu ni Mungu, lakini katika Uf.19:13 inasema, “..yeye aliitwa NENO la Mungu”; lakini ukisoma ile Yh. 6:63 inasema, Neno ndiye ROHO tena ni uzima.

    Mpaka hapo Napata ujasiri kusema wazi kuwa, Yesu aliijua siku ile ya Mwisho! Maandiko yanaendelea kuthibitsha hili alipoeleza viashiria vya siku yenyewe. Kamwe huwezi kueleza Dalili za Mvua wakati hata mawingu yenyewe huyajui! Labda kilicho cha mhimu hapa ni kujifunza na kujua kwanini hakuitaja ile siku ya mwisho waziwazi kwa jina. Kwa kweli, kujua Dalili za wakati halisi wa tukio fulani ni bora zaidi kuliko kujua jila la wakati husika! Mfano kujua dalili za ugonjwa wa Maralia ni mhimu zaidi kuliko kujua kuwa kuna ugonjwa uitwao Maralia! maana kujisikia kuwa na dalili za Maralia kunamaanisha kuwa tayari Maralia iko ndani yako, tafuta dawa tu! Bwana wetu Yesu Kristo alizitaja Dalili na viashiria vyote vya siku hiyo ya mwisho, ili atakayekuwa na Macho na Masikio ya Kiroho ajue, na akishaona ama kuzisikia hizo dalili zikitokea mahali mahali hapa Duniani AJUE KUWA YUMO NDANI YA SIKU YA MWISHO, kwa hiyo kama YUMO NDANI YA “NYUMBA” ASITOKE NJE TENA KABISA!, Dalili za wakati wa kujihami zimewekwa kwa ajili ya kujihami dhidi ya tukio, vivyo hivyo Dalili za nyakati zipo kwa ajili ya “WAJANJA” wajanja tu peke yao ndiyo wanaoingia katika SAFINA, upo!

    Kama kawaida, SI KAZI YA MWANADAMU KUJUA WAKATI GANI ATAPATWA NA MARALIA, KINACHOFAA KWAKE NI KUJIKINGA DHIDI YA MBU WASABABISHAO MARALIA, KWA WAKATI WOTE, NA AONAPO DALILI ZA UGONJWA HUO AMUONE DAKTARI, TAYARI KWA DAWA! Kwa kutajwa Dalili za “Nyakati” za siku ya mwisho, ni tayari KAITAJA waziwazi siku yenyewe, kuijua siku kama siku kwa tarehe yake haina maana kwake mwanadamu, maana hawezi kufanya marekebisho, maandalizi ama matayarisho yoyote yamfaayo, kwani hana nguvu wala mamlaka hayo! .Yesu aliyasema hayo alipokuwa akiwaaga wanafunzi wake pale mlimani, katika ile Mdo. 1:7 inasema, “7Yesu akawaambia, “Si juu yenu kujua nyakati na majira ambayo Baba ameyaweka katika mamlaka Yake mwenyewe.

    Pamoja na kwamba ndivyo ilivyo, Ni lazima tujulishe na Mtaalamu wa Maralia, kumjua Mbu wa Maralia, madhara yake na namna ya kujikinga, ili tumuonapo tumwangamize au tujikinge naye na pia tuwajurishe na wengine juu ya ugonjwa ule. Ukweli huo upo katika ule mstari wa 8, wa hiyo Mdo. Sura ya kwanza inasema, “8Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu…..”!

    Kwakuwa Sisi ni watoto wa Mungu, ametuwekea Roho wake ndani yetu ili, tuzijue na kuziepuka Nyakati za Hatari kwetu! Ukiisoma ile Gal. 4:6 inasema, “6Kwa sababu ninyi ni watoto wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu,………” Kusudi kuu ni kutujurisha hatari inayoukabili ulimwengu, hivyo kuzijua kwetu zile Nyakati za hatari kunafanya tujue tayari tumo katika siku ya Mwisho, mambo haya, hayajulikani kwa akili ya kawaida, ukiitazama 1kor. 2:10 inasema, “10Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa njia ya Roho Wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu.” Na katika ile 1Kor. 2:14 inasema kwamba, “14Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni. “

    Kwa hiyo wapendwa, ikiwa hujui kama umo katika wakati gani, basi pia hujui lini ni siku ya mwisho. Jiangalie!

    “Maarifa ni chembe ya uhai”

  2. Mwisho ule u karibu sana kuliko wakati wowote ule maana yote twayaona hata tukisoma
    WARUMI 1:24-27

  3. Mpendwa Emmanuel,
    Nimeyapitia maelezo yako nanineona umeeleza kwa kiingeleza kizuri na hakina misamiati, jambo hilo nimelifurahia, hasa mimi nisiyejua kiingeleza kwa kiwango kikubwa. Kwa uelewa wangu, nimeelewa kuwa “Mwanamke” kwa maelezo yako ni “Shetani” kama ulivyosema kama ifuatavyo, nanukuu;

    “……The woman in this context is satan……. and remember that anti Christ is satan in fresh……….all the above mentioned empires were satanic empire that why the women( satan in this case was sitting on them) and all of them were seeking to destroy and persecute God’s people (Jews)…..” Nikisoma kitabu cha Mw.3:15- , ndipo ninapoona Mungu anaainisha uadui kati ya Uzao wa ‘Mwanamke’ na uzao wa ‘Shetani’ hapa Biblia inasema,
    Ge:3:15: “And I will put enmity between thee and the woman, and between thy seed and her seed; it shall bruise thy head, and thou shalt bruise his heel.” Kiswahili chake inasomeka hivi;
    “15nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. ” Kwa uelewa wangu, mustari huu unaniambia kuwa Mwanamke ni mwingine na Nyoka (Shetani) naye ni mwingine! Na nikisoma Rev:12:17: inasema, “And the dragon was wroth with the woman, and went to make war with the remnant of her seed, which keep the commandments of God, and have the testimony of Jesus Christ.” Na kiswahili chake kinasema,katika Uf. 12:17 kuwa, “17Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.” Sasa, unaponiambia kuwa Mwanamke ndiye Shetani kichwa changu ‘kinapata moto!’
    Sasa naomba nikuulize maswali machache kama ifuatavyo:-

    1).Napenda sana kujua iwapo tafsiri hii ya “Mwanamke ni shetani” ni tafsiri ya Biblia au ni tafsiri toka vitabu vingine ama ni yako binafsi? Biblia pia inasema kwamba Bibi Harusi ni Kanisa, nakama nijuavyo mimi ni kwamba, Bibi harusi lazima awe ni ‘mwanamke’ Sasa je.

    2). katika maandiko yafuatayo Bibi Harusi hapa naye ni Shetani? Na hitaji kujua tafadhari. Hebu soma, Katika Uf. 22:17 maandiko yanasema kuwa, 17Na Roho na Bibi-Harusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
    Kwa kiingeleza, Rev:22:17: And the Spirit and the bride say, Come. And let him that heareth say, Come. And let him that is athirst come. And whosoever will, let him take the water of life freely.

    Hebu nisaidie nijue tafadhari.

  4. Definitely we are living in the last days, but we as believers of Jesus we have great hope that God is with us till the end of time… When you read the book of revelation 17:9-11 the bible tells us that the eighth empire is going to be the anti Christ empire and five have fallen and ” one is, “the other has not yet come, and when he comes, he must remain for a little while. The beast that was and is not, is himself an eighth king, yet he belongs to the seven and is going to its destruction.
    Let me break down for you
    Mountains- are empires or kingdoms
    Beast-is the anti Christ
    The woman in this context is satan and remember that anti Christ is satan in fresh
    So let ask ourselves what empires have fallen when apostle John was receiving this revelation,
    “Five have fallen”1-Egyptian empire
    2-Assyrian empire
    3 -Babylonian empire
    4 -Persian empire
    5-Greek empire
    “One is”-let ask ourselves what empire existed during apostle John time or during Jesus time, (“one is” means that empire was present when apostle john was receiving this revelation) the answer is very easy -Roman Empire , so we see here that according to historical facts Roman
    Empire was the sixth empire.
    6-Roman empire
    .. Okay let’s now try to identify the seventh and eight empires which is a empire of anti Christ but remember all the above mentioned empires were satanic empire that why the women( satan in this case was sitting on them) and all of them were seeking to destroy and persecute God’s people (Jews)

    “The other has not yet come, and when he comes, he must remain for a little while- this means next empire which is the seventh empire was yet to come but when it comes, it will not exist for too long, the question is what was this empire? According to history the empire that defeated Roman Empire was Islamic Ottoman Empire which was a caliphate empire ( falme ya muungano wa mataifa ya kiislamu) lead by caliph (khalifa) and his seat was instabul turkey. But did not exist for too long cause the position of caliph was abolished when atuturk mustafa the founder of modern turkey overthrew the caliphate and instituted secular government . So the seventh empire was Islamic Ottoman Empire
    7- Islamic Ottoman Empire

    So wapendwa let’s see what empire is going to be the last one ( the anti Christ empire) before the coming of our lord lion of Judah.
    “The beast that was and is not, is himself an eighth king, yet he belongs to the seven and is going to destruction.—- this means the eighth empire is a resurrected or revived version of the seventh empire…. So here is the news the eighth empire will be revived Islamic Ottoman Empire and not revived Roman Empire because the seventh empire is the same as eighth but roman was the sixth and it can not be the seventh.
    8- revived Islamic Ottoman Empire

    The Muslims savior (Mahdi ) is the anti Christ kwa sababu ndo atakua kiongozi wa hii falme .angalia sana turkey and mataifa mengine ya kiislamu yataunda muungano na kuanzisha caliphate halafu atatokea Mahdi( mpinga kristo) na kuwaongoza to their own destruction.

    Wapendwa Nimejitahidi kupangilia sijui Kama nimeeleweka…. Maswali yanakaribwa

    Mungu awabariki sana sana watakatifu .

  5. Athumani Mlangasa

    Mimi nifahamishe tafadhali, hivi sasa Yesu yupo nasi ama hayupo? Na kama yupo hapa nasi, kumbe tunamsubili arudi kutoka wapi? Na kama hayupo mbona alisema atakuwa nasi hadi ukamilifu wa dahari?!

  6. Shalom,
    Wapendwa mimi nilifikiri tunatakiwa kuwa watu wa shamrashamra tukimsubiri Mwana wa Nazareth Mesiya akirudi mara ya pili kwani alisema aliwenda kututayarishia makazi mapya.Basi tuendelee kusubiri kwa maombi usiku na mchana na msaidizi tunaye ambaye ni Roho Mtakatifu atusaidiae kuomba kwa kuugua kusiko tamkwa.Amen

  7. Wapendwa SG,

    Kwanza nikubali kuwa “TUPO KATIKA SIKU YA MWISHO” Lakini jambo hili linajulikana zaidi kwa Kanisa, kanisa ndilo pekee linajuwa kuwa tupo katika wakati gani, linajua hivyo kwa kuuangalia UNABII. Kweli kama alivyoandika mwandishi kuwa Ishara ndizo hizo zikiwemogofya, na hivyo ndivyo Biblia inavyosema. Lakini, unabii unapaswa kutimia, kama sisi ni kanisa tunapaswa kutambua utimilifu wa wakati. Katika Malaki 4:5-6 insema “5Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. 6Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.

    Je, wangapi wanajua maana ya unabii huo? Na je, Unabii huo unatimia au bado? na kama unatimiia unatimaje?

  8. Naomba kujua kama vita vya mbinguni kati ya mikael na joka ni unabii uliopo sasa au kama ulishapita. Vita mbinguni ni mazuri? Mazuri mbinguni au duniani?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s