Shai Linne awataja waalimu wa uongo kwenye wimbo!!

shae

Muimbaji wa Gospel Hip-hop Marekani, Shai Linne amewataja Joel Osteen, Creflo Dollar, Benny Hinn, TD Jakes, Joyce Meyer, Paula White, Fred Bei, Kenneth Copeland, Robert Tilton, Eddie Long, Juanita Bynum na Paul Crouch ya kuwa ni waalimu wa uongo katika single yake ya tatu kutoka album yake ya “Lyrical Theology Part 1.”

Shai Linne alipoulizwa kwanini amewataja hao watumishi wa Mungu amesema “”[Injili ya mafanikio ina] imekuwa ya kuvutia,” alisema jinsi gani mafundisho haya yamelivuruga bara la Afrika. “Unaweza kuona mikutano na kampeni hizi zaidi ya watu 100,000 wanasikiliza hawa jamaa wanaongea/kuhubiri kuhusu mafanikio. Watu ambao ni maskini na wanawaamini wakidhani theolojia hii ya uongo itawaondoa kwenye umaskini.

Akiongelea kuhusu nia ya wimbo huo msikilize

Hata hivyo wimbo huo umepelekea mtoto wa Paula White kumuandikia barua ya wazi Shae.

Kwa maelezo zaidi kuona barua hiyo fungua 

–Wade-O Radio

Advertisements

21 thoughts on “Shai Linne awataja waalimu wa uongo kwenye wimbo!!

 1. Mkandya mwana wa Mungu,

  Mtu akifika katika nguvu ya uelewa, jua kwamba Mtu huyo tayari anayo maarifa na Mtu akiwa na Maarifa basi na hekima atakuwa nayo, Biblia inasema, “Hekima ni Chembe ya Uhai”. Kila jibu si jepesi kwa kulinganisha na hoja, Bali huwa jepesi ama zito ukilinganisha na Sheria!

  Sheria yetu ni Neno la Mungu, nimefurahi ulivyoshindwa kuainisha “Wepesi” wa majibu katika hoja nzito. Hoja nzito ni ipi hapo ndugu yangu, kuombewa mafanikio, au? Sikiliza Mtumishi, Neno linasema Mkishaupata ule Ufalme, basi mengine yote mtazidishiwa. Ikiwa kitu kipo kimewekwa tayari kwako, isipokuwa utimize tu sharti Fulani ambalo nalo liko vema katika nguvu uliyonayo, unakwenda kuombewa ili?!

  Umenishangaza kuniambia kuwa, yale Maziwa na Asali ilikuwa Lugha ya Picha tu, na kwamba kama ingekuwa halisi wale waliokwenda kuipeleleza ile Nchi wangekuja wameteka (wamechota) maziwa na Asali! Mimi najua wazi kuwa Maziwa hupatikana katika wanyama na Asali hutengenezwa na Nyuki, nikiendelea kuisoma Biblia inaniambia kuwa Nchi ile ya ahadi ilikuwa imekaliwa na watu wa mataifa nyenye nguvu pia za kiuchumi, mifugo , madini na mali zingine zilikuwemo, na haikuwa si jangwa. Vita vilipigwa humo katika kuitwaa na nyara za kutosha tu zilipatikana humo, wakiwemo, Ng’ombe, kondoo mbuzi nk, na wanyama hao wote hutoa maziwa. Biblia haitaji kuwa nchi hiyo ilikuwa jangwa, kwa hiyo ilikuwa na mistu na katika misitu kuna maua, maji toka katika mito na vijito hivyo nyuki wanaweza kutengeneza Asli ya kutosha, na watoto hao wa Mungu kabisa wasipate kuwaza Maziwa ama Asali ya Misri! Kwa maana hiyo Neno la Mungu lilibaki “Kweli” tupu kuwa Nchi ile ya ahadi ilijaa “Maziwa na Asali”

  Labda nikuweke wazi kuwa, MIMI KABISA SISEMI KUWA MALI NI KIKWAZO CHA MTU KUUPATA UFALME WA MUNGU, bali Matajiri wenye ubinafsi ni ngumu kuuona ufalme wa Mungu. Vilevile Umasikni SI KIGEZO CHA KUUPAATA UFALME WA MUNGU., lakini katika hili la Utajiri na Umasikini ni Vema kujua kuwa Biblia inaposema umasikini hasa ni upi kuwa ni heri zaidi Mtu akiwa nao! Na utajiri ni upi ambao Mtu akiwa nao ni Hasara!

  Kwa kuwa Jambo hili si Mada iliyopo hapa tuache!! Ila, niseme tu kwamba, Mungu alikwisha weka vyote hivi mbele yetu, tatizo ni “Nguvu ya ufahamu” ambayo mtu akiwa nayo nilazima atafikia uelewa. Kama ambavyo si kila mtu anaombewa kuwa MTAWALA, unaona, je Hili halipo katika “Mafanikio” ya kibinadamu? Lakini unaonaje, iwapo kila mwamini atasimama mle kanisani akimtaka Mchungaji amuombee kuwa Mtawala? Ni uelewa tu kaka, mimi naona ni swala la kuelewa tu kuwa kipi ni kpi na haki ni ipi.

  Mafunzo kam ujasilia mali, kufanya kazi kwa Bidii, nidhamu katika Pesa, malengo na Maarifa ya utafutaji mali hivi vyote ni vizuri kwa watu kufundishwa, na kama mtu tayari Roho yake ilishafanikiwa ni rahiisi tu kuwa na ufanisi katika Mali, maana UTAJIRI huanzia Rohoni! Mimi naona kama tunazungumzia kitu kimoja kile kile ila kwa mawazo tofauti.Ki msingi ulisha kubari kuwa kuombewa utajiri kabla ya kufanikiwa kiroho kwanza ni kama kutwanga maji katika kinu!

  Labda ni seme tu kuwa, unajaribu kumchuna tembo kwa kutaka kumgeuza kwanza!

 2. Mabinza ndugu yangu mara nyingi huwa nakuona kama mtu unayejibu suala zito kwa hoja nyepesi!

  Ukisoma vizuri biblia yako utagundua kuwa hapakuwa na maziwa wala asali katik nchi ya ahadi( Canaan). Wapelelezi walipotumwa na Musa hawakuja na magudulia ya maziwa wala asali kama manono ya nchi, bali walikuja na zabibu na komamanga kama manono ya nchi. Kwa mantiki hiyo lazima ujue neno maziwa na asali ni lugha ya picha tu ambayo Mungu aliitumia akimaanisha kitu kingine ambacho wayahudi walikuwa wanakielewa kuliko mswahili Mabinza au Sungura.

  Mtu kama T.D. Jakes huwa anaongea kwa kusanyiko ambalo tayari ni la waamini (waliookoka), ambao tayari wanayo haki ya Mungu na ufalme wake. Ndio maana nilikwambia kuwa sioni shida ya watu hao kuhubiriwa sasa habari za mafanikio maana wokovu tayari wanao.

  Ina maana kuwa tayari roho zao zimeshafanikiwa, kwa hiyo sasa ni zamu ya miili na nafsi zao kufanikiwa, ndio maana wanatakiwa kufundishwa habari za mafanikio.

  Hata mimi sikubaliani na wachungaji wetu wanaowaita watu kuwaombea ili wafanikiwe kiuchumi, bali nakubaliana na wanaowafundisha kufanikiwa kiuchumi.

  Maana ya ufalme wa Mungu kitafsiri ni mfumo wa jinsi Mungu anavyofanya mambo yake (the system of how God operates),ambao huo mfumo kimatokeo huleta haki, amani, na furaha katika Roho mt. Kwa maana zawadi (mafanikio) itokayo kwa Mungu (iliyopatikana kwa mfumo wa ki-mungu) haina majuto ndani yake

  Umasikini utasababisha watu wengi wasimwone Mungu kuliko watu wengi walivyokariri kuwa matajiri ndio wengi watakosa kumwona Mungu siku ya mwisho.

  Mabinza ni rahisi kwa mwenye mali anayemtegemea Mungu kuingia mbinguni, kuliko ilivyo kwa maskini anayemtegemea Mungu kuingia.

  Kuna masikini wakristo wengi sana ambao wanadhani kuwa umasikini wao utawarahisishia kumwona Mungu, maana wamefundishwa kuwa umasikini uko karibu na utaua, kutokana na kutafsiriwa vibaya ile habari ya Lazaro masikini na yule tajiri.

  Kama kuna mtu anafundisha kuwa mali ni za kwanza kabla ya wokovu,huyo anapotosha,bali anayefundisha mali baada ya wokovu yuko sahihi kwa nguvu zote.

  Mabinza kama ulishapitia hali zote mbili, yaani hali ya kuwa nazo na kutokuwa nazo lazima utakuwa unajua kwamba kuwa nazo ni bora zaidi

 3. Mkandya,

  Maziwa na Asali? Aaaaaaaa, Mimi naona hayo yote ni MANONO YA NCHI, hayo SI mafanikio, hayo yalishatangulizwa tayari, mkifika tu kwenye Nchi hiyo ya Ahadi, ni kupitia (kuchukua bila kuomba) “Mstini, kikombe na kijiko” tayari kula! VYAKULA TANGU LINI VIKAITWA NI MAFANIKIO?! Mafanikio ya kimwili kiuchumi ni Pesa, Pesa ni jibu la mabo yote! Paulo anasema, hata katika maana ya mtu kuwa na ufalme wa Mungu, hautambulikani tokana na KULA! Kwani katika Bustani ile ya kule Edeni, mlikuwa na nini cha zaidi ya CHAKULA?

  Ulichosema ni sawa! Lakini Neno la Mungu linasema, “Utafuteni kwanza Ufalme na Haki yake na mengine yote MTAZIDISHIWA!” Ufalme wa Mungu ni nini? Neno linasema, Ufalme ule si Kula na Kunywa bali ni, Amani, Haki na Furaha katika Roho mtakatifu! Sasa iwapo mengine yote tutazidishiwa, kwanini Ahadi hiyo hatuiamini, hadi tukafanyiwe Maombi Maalumu?

  Fikiria una mwanao, umemwahidi kuwa, siku ya Harusi yako nitakupa Nyumba iliyopo Sinza, Unaonaje mtoto huyo akija mbele yako akilia na kugalagala akitaka umpe ile Nyumba, kwa kuwa ulishamwahidi huku hata Mchumba tu hana? Kama ni mimi, kabla sijamtimua kwa fimbo, nitajua tu kuwa Akili zake hazina uwezo wa kuelewa! Mimi najua kuwa Mtoto huyo aoe kwanza, kisha asubiri ile ahadi, na akiona bado haipati pamoja na kusubiri kote kule, aje akukumbushe. Kwakuwa wewe ni Baba yake mwema, utafurahi kwa kukumbushwa, utampa ile Nyumba na Fanicha zinazobidi kuwemo katika nyumba kama vipi!

  Au, unasemaje juu ya wakili ambaye, umemkabithi hati yako ya mirathi kuwa ukifa tu, wanao na Mkeo wagawiwe sawasawa kama ulivyoagiza katika Hati ile; Lakini wewe mwenyewe bado upo hai na mweyewe bado una nguvu zako, si hivyo tu hata kazi ya umma bado hujastaafu, mara Mwanao mmoja na Wakili wako wakasimama mbele yako na Jarada Mkononi, ukiwa unalitazama jarada lile kwa udadisi, unagundua kuwa ni lile lako la Mirathi. Kabla hujauliza Neno, wakili anakujurisha kuwa, ujio ule yeye kama wakili wako Mwaminifu, yupo hapo mbele zako akimuombea mwanao huyo ambaye ambatana naye Urithi! Wewe kama wewe utamjibuje wakili na mwanao huyo? Ujue waombezi ni “MAWAKILI” labda tatizo ni kujua ni mawakili wa nani? iwapo mawakili wa Kristo wanaijua kanuni ya “Mkuu” wao

  Mungu wa mbinguni, kwa Neno lake anasema, “Zitambueni haki zenu mpate kuzidai” lakini Ndugu yangu Mkandya, haipo haki bila kuwepo wajibu. Tunapaswa kujua kuwa kama sisi ni MAWAKILI wa Kristo tuzingatie Maelekezo ya “Mwajiri” wetu ambaye ndiye Kristo. Tusiingie tu Nyumbani mwa Mungu huku tumewatanguliza watoto wake eti tunakwenda kuwaombea “Wapewe” mambo ambayo si ya kuyaomba! Rafiki, kama wewe hujafika katika mikutano ya Maombezi, utashangaa ukifika, ni nguvu nyingi sana zinatumika kwa kuvunja laana, kukemea, na kuamru Mungu atoe! Mafanikio watu hujua ni yale matokeo ya ki ukwasi, hawana habari ya kuwa cha kwanza, kabla ya Kumuombea Mtu mafanikio nilazima kwanza kujua, JE, HUYO UNAYEMUOMBEA MAFANIKIO ROHO YAKE IMEFANIKIWA? Neno linasema, “Ufanikiwe pia kama Roho yako ifanikiwavyo!” Lakini umuonapo mtu kaombewa na kupata mapesa, gari, Watoto, Nyumba nk, huku hayupo “Vizuri” Ki roho, lazima ujiulize kapewa na mungu nani?

  Sikatai watu wasiombe wayatakayo (Mafanikio), ninachosema Watu wasijazwe Vichwani Mwao kuwa “NYONGEZA” ndiyo mhimu kulikoni “HITAJI” lenewe!
  A! baadaye, Rafiki yangu Mkandya!

 4. Mabinza kwamba mtu akitaka kuhubiri mafanikio aanze kuhubiri wokovu kwanza?!!! Akisha hubiri wokovu kwanza si baadae atahubiri mafanikio?

  Yes, kuna makosa mengi kwenye mafundisho mengi tu,yakiwemo hayo ya mafanikio.lakini ukweli uko palepale kuwa tunatakiwa kufanikiwa.

  Jiulize sana kuwa kwa nini Mungu hakukomea tu kuwatoa Israel utumwani Misri, bali aliwaambia atawatoa na kuwapeleka kwenye nchi iliyojaa maziwa na asali.

  Think, what is maziwa na asali!!

 5. Mimi binafsi nimechoshwa na wokovu wenu mnaoongelea kila kukicha, katika dunia hii ya Mungu lakini hakuna dalili za mabadiliko. Dunia sasa hivi inaelekea kubaya zaidi kuliko siku za nyuma ambapo watu walikuwa waenda taratibu katika kulijua neno la Mungu. Sasa hivi hakuna hata utii,kila mtu anajifanya yeye ndo anajua zaidi hata ya Yesu mwenyewe,hapa cha msingi ni kila mtu binafsi aangalie uhusiano wake na Mungu maana wokovu ni siri ya nafsi ya mtu na Mungu wake na wala siyo matangazo. Utawajua kwa matendo yao (waliookoka) wako wapi? sasa hivi karibu asilimia 90 ya watu wote duniani yaani waubiri na wahubiriwa wanaangukia 2Tim 3: 1-9.

 6. Sasa tusemeje basi?
  Je, kwa kuwa Marekani ni Tajiri kuliko Tanzania ina maanisha kuwa Tanzania kuna Uhaba wa Neno? Au ni jambo gani la kiroho linalofanya Marekani kuwa Tajiri kuliko Tanzania?

  Na kwa habari ya mada hii NATAMANI siku moja muimbaji Shai aimbe wimbo ambao ndani yake atawataja WATUMISHI WA KWELI wa Mungu.

 7. Mama K,

  Naungana nawe katika kumshukuru Mungu mkuu huyu aliyekufanikisha na anaye endeleea kukufanikisha, aidha nami nimefurahi sana kusikia ushuhuda wenye mvuto mkubwa kama huo. Mungu hufanya kama atakavyo yeye ili kumlinda mtoto wake atoke katika kila Aibu iletwayo na shetani. Umenibariki sana kwa ushuhuda wako, acha nichukue nafasi hii kukukaribisha Tanzania wewe na Familia yako kwa ujumla, safari yako iwe njema na yenye mafanikio!

  Mpendwa katika Bwana, mimi siko mbali sana nawe, nilichokigundua ni kwamba wote tunakubaliana katika jambo moja kwa upande mmoja lakini hatukubariani katika jambo moja kwa upande wa pili. Na hili ambalo hatukubaliani kwa GHAFURA tumejikuta tumekubaliana, hivyo hakuna tena haja ya kulisema jambo hili kwa mimi na wewe kwasababu limekwisha, labda mwingine alilete kwa sura mpya, Haleluya!

  Tofauti yetu ilikuwa ni katika Ama wapo sawa au ni waongo wahubirio utajirisho! Ubishi umeumaliza wewe ulipo fika katika kusema hivi ifuatavyo, nanukuu, “…..soma Agai 2;8. Kumbuka Mungu wa hapa Marekani ndiye Mungu wa Tanzania , tatizo siyo Mungu yuko wapi tatizo ni neno liko wapi, kama nilivyokueleza mwanzo wewe ukiamua kusikiliza mahubiri ya wale watu , usiishie pale yasikilize lakini usiwe mwisho fanya utafiti mwenyewe , yachambue kwa neno maana neno la Mungu ndilo lenye mamlaka ya mwisho……” Mwisho wa kunukuu.

  Kiukweli KIPIMIO cha mahubiri ya watumishi hawa wa Mungu, ni NENO la Mungu. Nami naongezea tu kuwa ACHA Neno hili la Mungu kwa huyu malaika wa Kanisa lililoko Laodikia, liamue kama tupo katika wakati wa Kanisa hili na ama watendaji wake ndiyo hawa wahubiri wa jinsi hii ama la, wenye masikio nawasikie Neno la Roho kama ambavyo anawaambia MAKANISA, maana NENO la Mungu lipo kwa ajiri ya wanae tu na si vinginevyo!

  Jambo lingine lililonifanya nielewe kuwa tumekubaliana ni hili ulilolisema hivi, nanukuu, “…….imeandikwa rahana isiyo na sababu haimpigi mtu , mithali 26:2. na imeandikwa nitambariki atakayekubariki na nitamurahani atakayekurahani, Mwanzo 12:2-3 kwa hiyo huyu ndugu anavyowaimbia nyimbo za kuwalaani hawa watumishi wa Mungu hata bila yeye kujua anakuwa anajirahani , maana ndivyo ilivyoandikwa. atakayekuraani nitamraani, na ukitaka kujua hii ni kweli tazama tangu alipoanza kuwannenea mabaya si wanazidi kuinuka? na watazidi kuinuka na kusonga mbele kufanya yale ambayo Mungu amewaita wayafanye……. maana kila mmoja ameitwa na Mungu na Mungu anataka kumtumia kila mmoja anavyotaka, na anavyopenda kumtumia…..” mwisho wa kunukuu;

  Mama k, Neno la Mungu halibadiriki, lilikuwa vile vile, lipo vilevile na litabaki vilevile. Neno linasema “mambo yote yatapita lakini NENO kamwe halitapita” Mungu anawatumishi wa aina mbili, aina ya kwanza ni WAVUNAJI WA NGANO wakiikusanyia ghalani, lakini aina ya Pili ni wale WENYEKUYAFUNGA MAGUGU matita matita tiyari kwa Moto, wote hawa Neno linasema ni WATUMISHI WA MUNGU! Na kwamba, haitakiwi kabisa kuwalaani, kuwanenea mabaya au kwa kifupi ‘KUWAUA’ Maana ukilaani au ukimnenea Mtu mabaya unatumia ulimi, Neno linasema katika Ulimi imo nguvu ya Uzima na ya Mauti pia! Mungu ameonya kuwaua watumishi wake hata wale “wakusanyaji Magugu” na si kuwaua tu hata kuwakwamisha wasiifanye ile kazi waliyoitia kama ulivyotangulia kusema, tazama hili katika Mw.4:14-16, inasema “14Tazama, umenifukuza……; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
  16Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.

  Unaona? Kaini yupo hata leo, na Neno hili la Mungu lipo hata leo! Unazani Mungu alimubakiza na kumlinda Kaini asife kwanini? Kwa ajili moja tu Kaini naye ni “Mtumishi wa Mungu” yeye akusanye Magugu, na sasa kaini bado anakusanya magugu tayari kwa moto! Sitaki nikuchoshe wewe ama mtu mwingine kwa maneno mengi, ila tu elewa kuwa Kaini ni uzao wa Yule Mwovu na mwovu ndiye aliyemwahidi Bwana wetu Yesu Kristo ‘Rushwa ya Mali’! Utajirisho? Haya, acha iwe utajirisho, ila tuwe Makini na mambo haya Kama ulivyosema, tuyapime kwa makini na kwa uvumilivu tukimsikiliza Roho wa Mtakatifu kwa kupitia NENO LA MUNGU ambalo kwalo tuyapime mahubiri ya ‘WATUMISHI’ hawa wa Mungu!

  Mama k, Asante na kwa heri ndugu yangu, Bwana wetu Yesu Kristo aendelee kukubariki!

 8. Neno la Mungu ni Nuru yatupasa kutembea katika Nuru,nabii wa kweli ataipenda Nuru na kuwaongoza watu katika hiyo na anaikemea dhambi anapenda utakatifu katika maeneo yote,kinyume cha hapo yupo kibiashara zaidi kupitia jina la Yesu hukumu yake inakuja wala haikawii,watoto wa Mungu tumwangalie Yesu na tusiache kuwaambia ukweli walio pofushwa fikra zao,barikiwa.

 9. Mr Milinga Namushukru sana kwa maelezo yako, maana naona tuko ktk ukurasa mmoja. Mungu akubariki sana tena sana , kwa kuona ninachokiona, kwa yule ambaye hakusoma maelezo ya MR Malinga , anasema hivi huyu Shai amekosa nyimbo za kuimba, na mimi sioni ubaya wa sisi kujipanga na neno la Mungu hili akatubariki tukawa na maziwa na asali hili pia tukawa baraka kwa wengine ,mimi naona ukiokoka ni ishara ya kuwa umetoka misiri na umeingia ktk nchi ya Ahadi hivyo maziwa na asari hupaswi kuvikwepa. Haleluya. Ubarikiwe sana Mr Milinga na 1 Nyakati 29:12 Daudi anasema ,Utajiri na heshima vyatoka kwako wewe (Mungu), nawe unatawala juu ya vyote, mkononi mwako mna uweza na nguvu , tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote. Utajiri siyo tusi , lakini kwa waliokoka wengine ukitaja tu utajiri wa Kimungu, wanakukata jicho jicho kali, wako tayari kuishi wokovu usio na rangi na radha lakini wasijifunze habari za baraka za Mungu zinazopatikana ktk wokovu, , utajiri nilionao unatoka kwa Mungu, na si utajiri wa mali tu bali na utajiri wa upendo , amani, furaha, matunda ya Roho yaliyoolotheshwa ktk wagaratia 5:22. kama hauna hivyo vitu basi kuna upungufu ktk wokovu wako, lakini ujue kuwa na fedha na dhaabu navyo ni sehemu ya wokovu. nasema kama hutaki maziwa na asali kama alivyosema mr Milinga endelea kubanana mbavu na shetani ishi maisha ya wokovu usio na mafanikio. Lakini ukihamua kusimama ktk neno huwezi kukwepa kupokea toka kwa Mungu hili ufanye kazi ya Mungu utapanye na kuwapa masikini , Kumbuka Yesu alisema kuwa masikini hawataisha duniani , hivyo ni wajibu wa sisi tuliokoka kuwasaidia masikini wale ambao Mungu anawaleta maishani mwetu, na huwezi kumpa mtu kitu ambacho hauna . huwezi kutapanya kama huna cha kutapanya na kuwapa masikini. 2 wakolintho 9:8-11. Mkitajirishwa ktk vitu vyote muwe na ukarimu wote umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yenu. Mama K.

 10. BWANA ASIFIWE . mpendwa Mabinza. Yesu alisema ktk Yohana 3:11 kuwa amini amini nakwambia lile tunalolijua tunalinena na tuliloliona tunalishuudia, na mimi mama K ninanena nilichoona ktk wokovu , maana niliwahi kuishi wokovu wa kimasikini , baadae nilijua ukweli kupitia neno nikawa huru kabisa Mungu akakutana na mahitaji yangu na hata mahitaji ya wengine aliowasaidia kupitia mimi na anaendelea kuwasaidia, niliwahi kula mapapai ya kuchemsha, niliwahi kushindia miwa, niliwahi kwenda kulala bila chakula, niliwahi kutembea kwa mguu kilometa 30 na zaidi, niliwahi kuvaa nguo moja , niliwahi kufunga kamba ktk nguo yangu ya ndani maana lastica ilizeeka nguo ile ikatanuka , sikuwa na jinsi bali kufunga kamba, na kipindi kile nilikuwa nikisoma secondari tukianza kupiga mguu pande , roho inaanza kudunda nikifikiria nguo ya ndani kamba ikiachia , itadondoka chini na itakuwa aibu, niliwahi kukosa kalo ya shule , niliwahi kuuza nyanya nabeba ndoo mbili na nusu , natembea tangu saa kumi na mbili hadi saa tano na nusu nafika sokoni kuziuza, niliwahi kuumwa magonjwa ambapo Muhimbili walisema hawakuona tatizo lolote, niliwahi kuuguza ktk familia yangu magonjwa yale ambayo kwa kawaida utasema imekwisha, lakini baada ya kuingia wokovu haswa , nikatembea ktk neno , nilimuona Mungu kwa njia ya ajabu sana , alinifanyia njia jangwani na mito ya maji nyikani, hata ninapoandika haya leo siku mbili zilizopita amenitendea neno la ajabu, kama unajua habari ya matayo 17:27 ni habari ambayo Bwana Yesu alimwambia Petro aende avue samaki na samaki atakayetokea wa kwanza mdomoni mwake mtakuwa na pesa , achuke alipie kodi , na mimi kwangu juzi imetokea vile lakini safari hii Mungu akutokea kupitia samaki kama alivyofanya kwa Petro bali ametokea kupitia Mbwa, Nimekuwa nikimuomba Mungu pesa ya kuja nyumbani Tz , ni pesa nyingi kidogo kwa tickets za watu watatu mimi mme wangu na mwanangu, lakini Mungu acha aitwe Mungu akili zake hazina mpaka sawa na zaburi 147:5. Kuna mtu amenijia juzi akaniambia nimsaidie kumuangalizia mbwa wake kwa muda wa miezi saba, na atanilipa dollar 750 kwa mwezi , hii ni sawa na milioni moja laki moja na tisini na nne elfu na mia saba hamsini. Mabinza kuja kufikia mwezi wa 11 chukua 750 x1593, utapata pesa ya kitanzania nitakayokuwa nayo ndani ya miezi , hiyo saba, Hii sisemi kukusisimua lakini natoa ushuuda huu uone kuwa Mungu anaweza kutumia hata kitu cha ovyo akakutana na hitaji lako, tayari nina pesa ya nauri ya ndege na pia nina pesa ya matumizi madogo nikiwa Tz. hapa uone kuwa unapojipanga na neno la Mungu huwezi kukwepa baraka zake , wokovu unaambatana na baraka za Mungu hii ni pamoja na mali za Mungu , imeandikwa fedha na dhaabu ni mali ya Mungu , hapa ujue kuwa Mungu hana ana fedha na dhaabu lakini hana haja navyo , anachotaka ni watoto wake ambao tumeokoka tukae mkao wa kula hili atubariki , soma Agai 2;8. Kumbuka Mungu wa hapa Marekani ndiye Mungu wa Tanzania , tatizo siyo Mungu yuko wapi tatizo ni neno liko wapi, kama nilivyokueleza mwanzo wewe ukiamua kusikiliza mahubiri ya wale watu , usiishie pale yasikilize lakini usiwe mwisho fanya utafiti mwenyewe , yachambue kwa neno maana neno la Mungu ndilo lenye mamlaka ya mwisho. na mimi niliingia muda wa ziada kusoma neno kwa bidii, tena nakumbuka niliomba maombi haya kuwa Mungubaba najua fedha na dhaabu ni mali zako , lakini sitaki unipe fedha na dhaabu kwanza , bali nataka unifundishe taratibu zako, na ukweli uliomo ktk neno lako, uniongoze ktk njia ya kweli hili hata ukija kunipa pesa yako, nipate kuitumia kwa ajairi ya utukufu wa jina lako. niliomba na kweli kama anavyosema kuwa ombeni nanyi mtapewa Matayo 7;7, niliomba na nikapewa na ninazidi kupewa , ninazidi hata kutapanya kwa masikini , sawa na lile neno nililokupa la 2 wakolintho 9:9.tafuta maandiko yanayohusu mafanikio ya Kimungu Roh mtakatifu akuongoze . akufundishe . hii siyo lazima lakini . maana inategemea unataka kuishi wokovu gani, kama unataka kuishi wokovu wa kwenda kuomba mchicha kwa jirani kila siku , napo fanya hivyo lakini mimi mama K ninasema kuwa Mungu baba unitajirishe ktk vitu vyote hili niwe na ukarimu wote utakaokupatia wewe shukrani kwa kazi zangu. 2 wakolintho 9;11. Mubarikiwe nyote. Kumbuka kwa kadri unavyozidi kuwanenea mabaya watumishi wa Mungu nidvyo Mungu anavyozidi kuwainua, kijicho cha chura hakimuzuii ng’ombe kunywa maji, na imeandikwa rahana isiyo na sababu haimpigi mtu , mithali 26:2. na imeandikwa nitambariki atakayekubariki na nitamurahani atakayekurahani, Mwanzo 12:2-3. kwa hiyo huyu ndugu anavyowaimbia nyimbo za kuwalaani hawa watumishi wa Mungu hata bila yeye kujua anakuwa anajirahani , maana ndivyo ilivyoandikwa. atakayekuraani nitamraani, na ukitaka kujua hii ni kweli tazama tangu alipoanza kuwannenea mabaya si wanazidi kuinuka? na watazidi kuinuka na kusonga mbele kufanya yale ambayo Mungu amewaita wayafanye. . tazama mfano wa Yusufu, ndugu zake walijaribu kumkandamiza na kutaka kuharibu ndoto zake , lakini kadri walivyomkandia ndivyo Mungu alizidi kumuinua , mke wa Potifa akamkandia lakini hata gerezani alipewa cheo awe mkuu wa wafungwa. hadi Mungu akamfanya awe waziri mkuu. naona ingekuwa vema tukafanya yale tuliyoitiwa na Mungu tuyafanye kwa ajiri ya utukufu wake , kuliko kurumbana na kukandiana, maana kila mmoja ameitwa na Mungu na Mungu anataka kumtumia kila mmoja anavyotaka, na anavyopenda kumtumia. Ubarikiwe , sitaandika tena . kwa habari ya Shai na watumishi wa Mungu. hila ni maombi yangu kwa Mungu macho ya mioyo yetu yatiwe nuru tujue kuwa sote tuliokoka ni mwili wa Kristo, tunavyokuwa tunachambana tunakuwa tunajichamba wenyewe. tuombeane. Mama K.

 11. NYUMBANI KWENU KUNA MAZIWA NA ASALI?

  Ishara ya kwamba mtu wa Mungu amebarikiwa siyo kumiliki magari, mashamba, fedha nyingi benki, elimu, majumba, maghala ya chakula na nguo bali ni kama anakula asali na kunywa Maziwa.

  Wana wa Israel walipoondoka Misri waliambiwa kwamba wanaondoka Misri kuelekea Kanaani nchi yenye Maziwa na Asali. Huu ndio utajiri ambao kila mtu aliyeokoka anapaswa kuwa nao.

  Hata kama una mali kiasi gani lakini nikija kwako huwezi kunipa maziwa au asali wewe bado ni maskini hata kama umeokoka. Je, ni wapendwa wangapi wanakula asali na kunywa maziwa?

  Kunywa maziwa na kula asali nyumbani mwako wewe na familia ndiyo ishara pekee ya kwamba UMEBARIKIWA.

  Mwimbaji huyo anayewaponda akina TD Jakes, Benny Hinn na wenzao ni mwimbaji ambaye amekosa korasi za kuimba. Hawa wahubiri hata kama utawaita walimu wa uongo, kusema kweli wamejitahidi sana kufundisha dunia jinsi ya kuvua samaki badala ya kupewa samaki.

  Ukifuata mahubiri ya akina Benny Hinn na akina Joyce Meyer na wengine aliowataja nyumbani kwako utakunywa maziwa na kula asali. Mimi naona kwamba mwimbaji huyo amepotoka tu au amekosa nyimbo za kuimba.

 12. Francis Mbago,

  Mpendwa, taa lazima iwekwe juu ya meza ndipo upate Nuru! Ya Nuru ni ya nuru na ya Giza ni ya giza, wala asiyeona huwezi kumwambia nilelee kitu ile. Lungha uijuayo ndiyo waweza kuijibia swali, bali usiyoijua ni kalele masikioni mwako!

  Ninavyoona mimi nafikiri hujaelewa kinachosemwa hapa anzia mwanzo upate “Konsepti” ya jambo lenyewe kwanza Bro!

 13. Mama K;

  Nakubaliana nawe kabisa bila ubishi kuwa mistari yote uliyoinukuu ndivyo ilivyoandikwa na ndivyo inavyosomeka na kumaanisha kile inachokisema. Na kubali pia kuwa Mistari hiyo ya Biblia ni Neno la Mungu na linafaa kwa mafundisho. Asante sana kwa maelezo mazuri uliyonipa nimefurahi ulivyo mtulivu na mwenye bidii katika kuisoma Biblia.

  Mama k, hukunielewa! Nilisema unionyeshe hata mstari mmoja tu toka katika Biblia Takatifu unaosema, “MALI NI KIGEZO CHA WOKOVU” Kabla ya yote neno KIGEZO nilimaanisha SIFA! Tokana na maelezo yako yote hujaonyesha huo mstari bado! Yesu ansema KIGEZO kimojawapo cha mtu kuwa ameupata WOKOVU ni kuwa MTU HUYO HUSAMEHEWA DHAMBI NA KWAMBA, HUFANYIKA MTOTO WA MUNGU na si kuwa Mtu akishaokoka na kusamehewa dhambi, basi ATAFANYIKA MWENYE MALI!

  Mali kamwe zisitupotezee wakati, mali ni Baraka ya mwisho kabisa katika Baraka zote Mtu anapobarikiwa na Mungu. Selemani amesema mengi sana kuhusiana na jinsi ambavyo Mtu asiweke mawazo yake katika wingi wa mali na kuzitumainia, utayaona hayo katika Methali zake. Selemani alipokuwa akiomba Baraka kwa Mungu, aliomba Hekima na alipojaliwa hilo ndipo Mungu akamuongezea na kitu Mali, na alimpa hivyo kwakuwa tayari alishapewa Hekima, hata hivyo mali alimpa kama Baraka ya mwishoni. Bila Hekima ni mashaka kuitawara Mali. Yesu anasema, “Tajiri ni vigumu kuuona Ufalme wa Mungu”

  LAKINI nikiwa nasema haya mtu asininukuu vibaya Kuwa, nasema mali ni kitu kibaya au hatakiwi Mtu aliyeokoka kuwa nayo hapana, ninachosema ni kuwa, Watumishi WAHUBURI KWANZA NA KWA BIDII SANA WOKOVU UPATIKANAO KWA KRISTO! Wahubiri wengi siku hizi utawasikia, Unanadi Shida na kuwataka watu wenye matatizo waje kwa wingi makanisani mwao badala ya KUWAITA WENYE DHAMBI kwanza! Utawasikia wakitangaza, “Mtu mwenyetatizo la kutopata mimba, kama huna mali, kama unadaiwa sana, kama huna akili Darasani…..njoo katika Kanisa la Mchungaji Mabinza lililoko …..hapo utapata muujiiza wako maana Mungu yupo hapa!

  Lakini kumbuka kuwa Neno linasema, mtakapowasikia wakisema “tazama Kristo yupo hapa ama yuko kule msiwafuate”! Mimi nasema kwamba, wahubiri, wafanye kama Bwana wao alivoagiza. Iwapo kama kweli ni Bwana wao kwani, yeye agiza kuwa “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu…” lakini utakuta na kuwasikia wa Watumishi wengi siku hizi wamekazana kuwatamanisha watu juu ya kupata mali, vitu, mimba na kupona kimwili kama kigezo kuwa ukipata hayo ndiyo utakuwa eti umekubaliwa na Mungu, maana hata mtu akiwa na mali wakati wokovu hana mali itamsaidia nini? Wapagani na wasiomcha Mungu wapo matajiri na masikini pia. Tofauti ni Neno moja tu lisilo la kila mtu nalo ni kule MTU KUPATA HAKI YA KUWA MWANA WA MUNGU!

  Ulipata kuwasikia mitume wakihubiri na kuwaombea watu wapate mali bila kuwafundisha kwanza toba liletalo wokovu? Umesema umebarikiwa tokana na kuelewa kuwa mali ni Baraka, ni sawa, lakini ni kwanini Watu wanaoombewa na kupata mali hutoa tu kanisani kwa waombeaji ile sehemu ya mali hizo na si kuwapa masikini kwanza? kwa nini fundisho la Biblia linasema wenye mali wawape kwanza Masikini? Walioponywa siku za Yesu walipeleka Pesa kanisani na kuwapa wachungaji? Sawa, yote ni yote, wewe unaonaje maisha ya hao waombeaji wa utajiri wanavyoishi ukilinganisha na washirika katika makanisa yao wapi wanaoishi kwa anasa?

  Wote waliookoka wanakuwa Watoto wa Mungu, kama ni hivyo, Je, kanisani kwako wote wana mali? Kama kuna baadhi hawana, inamaana wasiyo na hizo mali hawakuokoka? Mali si kigezo hata kidogo, uwe nazo usiwe nazo si hoja, Mungu yeye anajua kufariji watu wake! Ndiyo maana Yesu alizaliwa kimasikini na hata Eliya alitunzwa na mama masikini nk. SIJAONA PAHALA POPOTE KATIKA BIBLIA PANAPONYESHA KUWA, MALI NI KIGEZO CHA WOKOVU!

 14. Uzushi mtupu, waalimu wa uongo kwa kuwa wanafundisha mafanikio au kuna lingine? Kwani biblia imekaa kimya kuhusu mafanikio? Nani anastahili kufundishwa mafanikio zaidi? Ni aliyefanikiwa na maskini. Kama kuna lingine linalothibitisha uongo wao, tulisikie sasa.

 15. Ndugu Mabinza, umesema nikutajie msitari mmoja unaonyesha kuwa mali ni kigezo kimojawapo cha wokovu, Twende ktk 2 wakolintho 8:9 neno linasema kuwa , maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo jinsi alivyokuwa masikini kwa ajiri yenu , ingawa alikuwa tajiri hili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umasikini wake, ndugu kama hujui ukweli huu umasikini, magonjwa, mikosi, ni sehemu ya Rahana, rahana maana yake ni kutofanikiwa wagalatia 3:13-14 inasema kuwa Kristo alitukomboa ktk rahana ya torati kwa kuwa amefanywa rahana kwa ajiri yetu, ili kwamba baraka ya ibrahimu iwafikirie mataifa ktk Yesu Kristo . Imeandikwa pia kt 2 wakolintho 9:7-12, imeandikwa kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake,si kwa uzuni wala kwa lazima maana Mungu umpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu,(je unaweza kutoa kitu ambacho huna, hii inaonyesha kuwa Mungu anapenda sana kutubariki hili tuwe na cha kutoa kwa walio na mahitaji) ndiyo maana alimwabia baba yetu wa Imani Ibrahimu kuwa nitakubariki hili uwe baraka, mwanzo 12:2-3. mfano kama una mtoto anahitaji kalo ,ukawa na pesa ukamlipia mtoto wako bila shida unaonaje ukiwa na pesa ya ziada ukamsaidia na mtoto wa mzazi ambaye mtoto wake ana akili lakini wazazi wake hawana uwezo wa kumlipia ada mtoto wao?inapendeza maana Mungu anakuwa amemsaidia mtoto yule kupitia wewe. msitari wa 8 anasema kuwa na Mungu aweza kuwajaza kila neema ,kwa wingi , hili ninyi mkiwa na liziki za kila namna siku zote, (liziki hapa anaongelea kiroho na kimwili)mpate kuzidi sana ktk kila tendo jema (nimetoa mfano wa kumsaida mzazi ambaye hawezi kumlipia mtoto wake kalo ya shule ukifanya hivi unakuwa umefanya tendo jema analoongelea Mungu hapa.msitari wa 9 anasema imeandikwa ametapanya amewapa masikini haki yake yadumu milele , unaona unapokuwa umembariki masikini unaingizwa ktk nafasi ya kuitwa mwenye haki nikuulize tena je utatapanyaje kile ambacho hauna hili utapanye uwape masikini?. hili utapanye na kuwapa masikini inabidi uwe na cha kutapanya.Mungu anataka akupe hili uwe muwakilishi wake ktk kutapanya mali zake na kuwapa watu wake , na Mungu tu ndiye atupaye vitu vyote kwa wingi hili tuvitumie kwa furaha. 1 Timothy 6;17 tangu nilipojua ukweli huu nimekuwa nikitia maandiko haya ktk matendo na ninahamini ndiyo maana Mungu amenifikisha hapa nilipo.Kumbuka hawa ndugu wanapohubiri wanawakaribisha watu wampokee Yesu kuwa Bwana na mwokozi wao wanawakaribisha ktk wokovu ,ambapo wakishamjua Yesu wanakuwa na nafasi ya kusimama ktk maandiko na kuchambua wenyewe hili wazidi kujua ukweli wa mambo na ukweli hule uzidi kuwaweka huru, imeandikwa kuwa kwa imani yenu mtasimama. 2 wakolintho 1:24. inabidi wasimame wenyewe wasome maandiko na kuyatia ktk matendo kwa kuwa imani isiyo na matendo imekufa,Kama unajua maana kamili ya wokovu utajua kuwa wokovu maana yake ni kutoka ktk hari mbaya na kuingia hari nzuri, ndiyo maana Yesu alikuja hili atutoe ktk hari mbaya tuliyokuwa nayo na kutuingiza ambayo Mungu alituandalia kabla ya kuumbwa kwa msingi wa ulimwengu,Lakini Adamu kwa kutenda dhambi akatuingiza ktk rahana , atukuzwe Mungu aliyetupa na kurudisha vyote kupitia Bwana Yesu, la kufanya ni kwamba unaposikia mahubiri ya wale watu usiishie pale nenda nyumbani ukae ktk maombi uyachambue mahubiri yale kwa neno, pima kwa neno . na uzuri wa Mungu wetu anasema atakufundisha , na kukuonyesha njia utakayoiendea atakushauri na jicho lake likikutazama zaburi 32:8. Kumbuka ktk kitabu cha mwanzo sura ya Pili Mungu alipokuwa amewaweka Adamu na mke wake ktk busitani ya Edeni , yahani ukisoma unaona walivyokuwa na maisha ya mafanikio ,ktk Mwanzo2:8. inasema Bwana Mungu akapanda busitani upande wa mashariki wa Edeni akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. 9 anasema Bwana Mungu akachipusha ktk aridhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa . 10 anasema ukatoka mto ktk Edeni na kuitilia bustani maji , na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne, 11 jina la wakwanza Pishoni ndiyo unaozunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhaabu, (daka hiyo ya dhaabu)na dhaabu ya nchi ile ni njema (haikuwa dhaabu feki kama iuzwayo siku hizi ktk maduka ya Kariakoo ya ulembo)ilikuwa dhaabu safi. Lakini utaona ktk sura ya 3 Adamu alipotenda dhambi Rahana ikaja sasa Mwanzo 3:17 Mungu anamwambia kabisa Adamu kwa kuwa umemsikiliza mke wako , ukala matunda ya mti ule niliokuagiza usile .aridhi imelaaniwa. na kwa sababu hii Mungu alimtuma mwanaye wa pekee hili aje kutafuta na kuokoa kilichopotea , Luka 19:10, na ndiyo maana alitundikiwa hile taji la miiba kichwani wakati wa mateso soma Yohana 19:2 , miiba ni ishara ya Rahana ilikuwa atuokoe na rahana hile aliyotuletea Adamu. ndiyo wokovu wenyewe huu , tuuone utamu wa Yesu tunapokuwa hapa duniani na ktk wakati ujao uzima wa milele. nimesimama ktk maandiko kutoa maelezo haya. Ubarikiwe . niko ktk wokovu , wokovu haswa uliomfanya Bwana Yesu anifie msalabani . pamoja na baraka zote za Ibrahimu. Lakini kama unataka kuishi maisha ya umasikini hili uonekane wa KiMungu sana na wa KiRoho sana ishi maisha hayo ukabanane mbavu na shetani msubiri Yesu aje kunyakua kanisa .Mama K.

 16. Mungu awasaidie watumishi wake, hali ni mbaya si kwa marekani tu, hata kwetu Tanzania wapo. Tuwaombee Rehema.

 17. Mpendwa Mama k,

  Kuhukumu si kumtaja mtu kuwa hatendi ipasavyo, bali kufanya hivyo ni KUTUHUMU tu! Nionavyo mimi huyu Shai Linne yupo sahii kama mtu huru kutoa maoni yake. Kiukweli, upo upotoshaji mkubwa sana wa Neno la Mungu kupitia Injili hii ya sasa inayo hubiri MAFANIKIO. Utakuta wahubiri wengi katika Afrika na Duniani kote kwa kiasi kikubwa huhubiri sana juu ya Ufanisi wa Kimwili kulikoni kuihubiri TOBA kama ambavyo Yesu mwenyewe alivyoagiza kwa kusema “……Enendeni Duniani kote mkawafanye watu kuwa wanafunzi wangu….” Sasa kama hawa wahubiri wanadai ni Watumishi wa Yesu, lakini lile Yesu alilolisema kama Kazi ya kwanza mbona wanaiacha na kurukia tu Baraka za kimwili?

  Kwani kupona kwa Mtu kumo katika wingi wa Mali? Siamini kabisa kuwa Mtu akiwa na ufanisi wa kifedha inamfanya Mtu huyo japo yungali amefungwa ufamamu wake na Shetani juu ya Elimu ya kutosha ya NENO la Mungu, aweze kuupata wokovu ambao hasa ndiyo mada kuu ya Yesu na kusudi lake kubwa kwamba watu waifikilie Toba ili waokolewe, halafu mtu anakuja na mageuzi yake kuwa “kwakupata mali” umepata Baraka tosha! Huoni kuwa Mtu kama huyo ni Muongo kwasababu anafanya kigezo cha wokovu kuwa ni mali?

  Mwisho niseme tu kuwa, kwa upande wangu mimi, naona kuwa Mtu anapohubiri Injili ya “MALI” ni muongo na anafaa kuitwa NABII WA UONGO! Kwasababu Bwana wetu Yesu Kristo alikutana na Mkasa wa mahubiri kama hayo toka kwa Shetani mwenyewe kuwa, “…..wayaona yote haya? waziona MALI na falme zote hizi za Dunia? UKINIABUDU nitakupa…..!” Sasa tofauti yake ni nini kati ya mahuri ya hao aliowasema Linne? Utakataaje kuwa nao wamepata mahubiri yayohayo toka kwa huyohuyo Shetani? Kama unakataa, nitajie mstari mmoja tu toka katika Biblia takatifu unaosema, MALI ni kigezo kimoja wapo cha WOKOVU! Shetani mara zote ni Muongo, amekuwa muongo tangu mwanzo, alimdanganya Hawa, na hawa alipodanganya akala lile Tunda, hapohapo hakujiona kama yupo UCHI ila hadi mda fulani ulipopita na baada ya kumpa na Mmewe naye alipokula ndipo pale walipojiona wapo uchi. Lakini kumbuka kuwa katika Maongezi yake na Shetani, Shetani kabisa hakumwambia Hawa kuwa ukila tu cha kwanza utakuwa UCHI! Mama K, mali hupofusha macho ya kiroho!

 18. BWANA YESU alisema musihukumu msije mkahukumiwa na nyie,Hawa watu wasiojua neno wamezoea watu wa siomjua Mungu kama wacheza sinema wakifanikiwa sawa, wanafagilia lakini mtumishi wa Mungu akifanikiwa wanaona shida, lakini je si imeandikwa kuwa utajiri wa mataifa utawawasilia Isaya 60:5. Imeandikwa pia Kristo alitukomboa ktk rahana ya Torati , imeandikwa kuwa ameraaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti hili kwamba baraka za Ibrahimu ziwafikie mataifa ktk Yesu Kristo , tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani, Wagaratia 3:13-14, Je baraka za Ibrahimu ni zipi, Twende ktk kitabu cha Mwanzo 24:1. inasema kuwa Ibrahimu alikuwa mzee wa miaka mingi na Bwana alikuwa amembarikia Ibrahimu kwa vitu vyote.Mwanzo 12:2 Mungu anamwambia Ibarahimu kuwa nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa , na kukubariki na kulikuza jina lako nawe uwe baraka. sasa tazama wakati Ibrahimu alipokuwa anakwenda kupigana na jamaa waliokuwa wamemteka Lutu , alikwenda na watu mia tatu kumi na nane , waliozaliwa nyumbani kwake, yahani watumishi wake, angalia mwanzo 14:14.alikuwa na watumishi mia tatu kumi na nane, hii inaonyesha alivyokuwa tajiri, soma tena Mwanzo 13:2 anasema Naye Ibrahimu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo , kwa fedha na kwa dhaabu. neno pia linasema kuwa mtenda kazi anasitahili posho yake. Matayo 10:10. haya aliyasema Bwana Yesu mwenyewe. Mimi hapa ninayekwambia haya kabla sijamjua Mungu huyu nilikuwa napokea mshaara kidogo kwa mwezi lakini baada ya kumjua Mungu nikasimama ktk neno lake sasa hivi nafanyia mara tatu kwa siku pesa hile niliyokuwa ninaifanyia kwa mwezi mzima.hapo kama siyo Mungu ni nani? Pesa ipo kwa Mungu lakini inabidi tuenende ktk taratibu zake, na Mungu hawezi kukupa pesa endapo anaona kuwa hujui kuitumia kwa mambo ya Mungu. kaa tu ktk neno chambua mwenyewe fuata taratibu na mipango ya Mungu , soma maandiko ya mafanikio na yaweke ktk matendo , hakika Mungu ataonekana, kama ameweza kunipa gari mimi, akanipa nyumba , akanipa ndoa nzuri, akanipa mtoto , akanipa amani kila upande, akanipa furaha, , ninaweza kubariki wengine kadri Mungu anavyoniwezeshesha ,kabla sijamjua Mungu kwangu sikuwa na mkokoteni wala baiskeli, nilikuwa nakula mapapai ya kuchemsha wakati mwingine ninashindia miwa , lakini leo hii ninaweza kula chakula aina ninayopenda , kuvaa kiatu ninachotaka, nguo nzuri na kumtukuza BWANA , angalizo ukishapata usimsaau Mungu maana anasema kuwa nawe utamkumbuka BWANA Mungu wako maana ndiye akupate nguvu za kupata utajiri na mali hili alifanye agano lake kuwa imara . kumbukumbu la torati 8:18. , anza kujishughulisha kuwasaidia wengine kwa kidogo ulichonacho , iwe kama mbegu , na Mungu atazidi kukuinua taratibu na mimi ndivyo nilivyoanza. Soma 2 wakolintho 8:9, na 9:6-12. Malaki 3:8-12. Luka 6:38. uone mwenyewe Mungu anasemaje kuhusu utajiri wa kiMungu.

 19. Kuna makubwa zaidi ya haya yatatokea. Yeyote asiyeenenda sawasawa na NEno, ni wa Ibilisi fulstop!!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s