Rais Kikwete akutana na viongozi wa madhehebu ya Kikristo Ikulu.

Pichani Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa madhehebu ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam jana.

Wakiwa kwenye mazungumzo 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano) Mhe Steven Wassira.
 

Viongozi wa dini wamewataka waumini kote nchini kulinda amani na  umoja uliopo ili nchi isije ikaingia kwenye mgawanyiko wa kidini na kuleta machafuko hapa Tanzania.

Wito huo umetolewa na viongozi wa dini leo Ikulu ya Dar-Es-Salaam mara baada ya kikao cha pamoja baina ya viongozi wa dini na Rais Jakaya Kikwete. Viongozi hao wa dini wamefika leo wakiongozwa na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Viongozi wengine wametokea Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) Seventh Day Advertist (SDA) na Baraza la Pentekoste Tanzania (PCT). Mkutano huo umeanza kwa Askofu Ngalalekumtwa kusoma tamko lao la pamoja kwa Rais Kikwete ambalo ndilo limetoa muongozo wa mazungumzo hayo ya leo ambayo yamehusu Amani na Usalama wa Taifa na migogoro ya kidini ndani ya jamii.

Mkutano wa viongozi wa dini ya Kikristo Tanzania ni mojawapo ya jitihada za Rais Kikwete kutafuta muafaka na kutafuta utatuzi wa hali ya sintofahamu ambayo inanyemelea nchi yetu katika kipindi hiki.

“Nataka tuzungumze ni namna gani tunaweza kutoka kwenye hali hii na tunakwendaje mbele zaidi na kuhakikisha nchi yetu bado inakua ya  amani na umoja kama ilivyozoeleka”

Rais amesema na kutoa nafasi kwa viongozi wa dini kutoa maoni yao.

Viongozi hao wa dini wamemueleza Rais Kikwete kuwa wanaunga mkono jitihada zake za kutafuta amani na kwa pamoja wamekubaliana uandaliwe mkutano wa pamoja baina ya viongozi wa dini zote ambapo masuala ya amani na umoja wa nchi utajadiliwa kwa kirefu.

Katika kikao cha leo pande zote zimekubaliana kuwa kuna changamoto zilizoko sasa zinahitaji kutatuliwa haraka iwezekanavyo ili kuepusha nchi kutumbukia katika mgogoro mkubwa zaidi, na pia kukubaliana kuwa pande zote, kwa maana ya serikali na taasisi za dini, zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha amani inadumu.

Kabla ya kikao cha leo, Rais amewahi kukutana na viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo mmoja mmoja ambapo alikua akitafuta maoni na ushauri wa pande zote kabla ya pande zote hazijakaa pamoja na kuwa na msimamo wa pamoja.

Kikao cha leo kimehitimisha jitihada hizo na kinachofuata ni mkutano mmoja ambapo Rais Kikwete atakutana na viongozi wa dini zote kwa pamoja hivi karibuni.

…………”MWISHO”……..
Imetolewa na:
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
23
Aprili, 2013
Advertisements

7 thoughts on “Rais Kikwete akutana na viongozi wa madhehebu ya Kikristo Ikulu.

 1. Kanisa linatakiwa kujipanga maana hizi ni nyakati za mwisho, mpinga kristo anachukua nafasi. yaha mateso kwa kanisa ni utangulizi tu picha kamili bado ila i-karibu sana! hawa maaskofu hawatazuia bali wata tuliza tuliza tu kidogo! kanisa kuweni tayari mambo ya mpinga kristo tayari maana ni wakati wa Shetani kuwa kazini!

  Ev.moses mayila
  http://www.mosespk.wordpress.com

 2. MUNGU AWATANGULIE VIONGOZI WETU (WAWAKILISHI) WA TAIFA LA MUNGU NA KUWEKA MANENO YATAKAYOTUUNGANISHA SOTE KAMA TAIFA KUUISHI UMOJA NA AMANI YA KWELI ITOKAYO JUU.

  HOFU YAKE (MUNGU) ITAWALE MIOYO NA MAZUNGUMZO YOTE. AMINA

 3. MUNGU AWABARIKI SANA WATUMISHI KWA KUITAKIA TANZANIA AMANI.MBARIKIWE SANA NA BWANA.AMINA

 4. Uadui unatoka kwa yule mwovu, wanadamu pasipokujuwa wanafanya nini kwa manufaa ya nani wametafsiri vibaya maandiko na kuchukiana wao kwa wao. Biblia inatuambia wapendeni adui zenu watendeeni mema wale wanawachukia na waombeeni wanaowaudhi, wabarikini wanaowalaani na watendeeni wenzenu kama ninyi mnavyopenda kutendewa nao. Kwa bahati mbaya mambo hayo hatuyafanyi ndiyo maana tunafika mahali hapa. Mungu atusaidie sisi wanadamu wenye ufahamu juu ya hayo kuyatenda na kuyahubiri ili tusiingie kwenye madhara ambayo yanatokana na kukosa hekima ya Kimungu.

 5. Ni njia nzuri Mheshimiwa Rais anaitumia kutafuta maoni ya viongozi wa dini nina hakika atafanikiwa katika jitihada za kulinda umoja na amani.Ni wajibu wenu viongozi wa dini wa pande zote mbili wakristo na waislamu kuwaambia ukweli waumini wenu mafundisho yanayochochea uhasama hayafai awe mkristo au muislamu.mnahitajika muwe werevu kwani biblia na kuran vyote vina maandiko ya kuchochea vita kwa adui yako na pia vina maandiko ya kuchochea amani na umoja.Wote Serikali,wanadini na wananchi wa kawaida tujielekeze kwenye kupendena na kuombeana heri.mashiindano ya nani yuko sahihi hayatatusaidia na ikiwezekana Serikali iyapige marafuku kama inavyopiga marufuku ngoma za kanga moja,biashara ya ukahaba,baa mwisho saa 5 usiku,uzururaji,uchafuzi wa mazingira n.k Serikali kuweni makini sana na mambo ya dini,Katiba iliyopo kila mwananchi kapewa uhuru wa kuabudu anachoamini bila ya kuvunja sheria za nchi na katiba imesema serikali haina dini na haifungamani na dini yoyote na sijajua katiba mpya itasemaje kuhusu masuala ya imani na dini.Seikali ikiwapa nafasi mno viongozi wa dini wanaweza kuleta mapendekezo ya kuzipendelea dini zao na watu wake au kuzikandia dini za wenzao na wake huko hatutaki kufika ndiyo yatakuwa kama ya akina Muslim brotherhood huko Misri ambao baada ya kuchukua nchi pia wanaonekana hawafai.Mbarikiwe…Amen

 6. Hiyo huenda itasaidia kwa namna fulani. Tuzidi kuliombea taifa letu wapendwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s