Nimeachwa na mchumba!!

mahusiano

Bwana asifiwe naitwa Ombeni, ninaishi Dar es salaam nimeachwa na mchumba wangu mwezi mmoja kabla ya harusi, nimeumia sana kiasi cha kukata tamaa kabisa na nilijipanga kuoa mwaka huu nimemuomba msamaha kwa yale niliyokosea amegoma kabisa na amesema hawezi kunisamee,wapendwa nashindwa hata kwenda pale kanisani kwa sababu yake. Nishaurini nifanyeje

–Ombeni

Advertisements

16 thoughts on “Nimeachwa na mchumba!!

 1. Songa mbele na BWANA. MPAJI NI YEYE (MUNGU). Yesu KRISTU ALISEMA: Mathayo 7:7, Omba, tafuta, bisha. anza upya. Naamini ukimkimbilia BWANA HUTAPUNGUKIWA. SONGA MBELE. USIHESABU ULIYOMFANYIA, AMINI MWENYE WEMA NI MUNGU MKUU. ATAKUPA WEMA WAKE KUPITIA HITAJI LAKO. ZABR 16;1-2.
  MUNGU NA AKUBARIKI.

 2. Inavyoonekana kuna MAKOSA makubwa uliyomfanyia hadi akaona hakuna sababu ya kuunganishwa muwe mwili mmoja, wakati ambao itakuwa too late kuondoka.
  Kuachwa na mchumba siyo tatizo kubwa. La muhimu jipange, tengeneza maisha na mapito yako. Utapata mke mzuri tu kwa kadri wewe utakavyokuwa mzuri.

 3. Mpendwa Ombeni,

  Kwa sisi wazee, wala hatushangai, maana vitu vya namna hiyo kwa ulimwengu wa sasa ni kawaida tu! “siku za mwisho kutakuwa na kizazi kisicho shika makubaliano!” Biblia inasema. Nikisema hivyo si kwamba nafurahishwa na hali hii, mimi sipendi kuona na kusikia haya yakitokea, ila kwakuwa Biblia inatabiri hayo acha iwe hivyo ili Neno la Mungu lipate kuwa la haki. Tatizo walilonalo vijana wengi wanaoiendea Ndoa, hawafuati kanuni na mpango wa Biblia juu ya jambo hili kubwa. Mungu kama mwanzilishi wa Familia aliweka Mwongozo mahususi juu ya jambo hili ndoa.

  Vijana wengi huzingatia utaalamu wa kisaikolojia zaidi juu ya jambo la Ndoa kuliko kuupata mwongozo kupitia Neno la Mungu. Biblia inasema, Mke mwema hupatikana kwa Bwana na sehemu nyingine katika kitabu cha methali inasema, Mke mwema ni nani atakayemjua? Paulo anasema katika kitabu cha Wakorintho kuwa, Ndoa ni SIRI kubwa! Kwa mantiki ya yote hayo, inathibitisha kuwa ndoa ni ‘Majariwa!’ Muoaji au muolewaji ili afikie Ndoa yenye mafanikio nilazima wamtegemee Mungu ili kutokeza mafanikio yenye tija katika Ndoa tarajiwa. Yapo mambo kadhaa yatakiwayo kuzingatiwa na Mhusika katika Ndoa Yule kijana wa Kiume na Yule wa Kike, baadhi ya mambo haya ni kama yafuatayo:-

  1). Nia ya dhati; lazima mhusika awe na Nia ya dhati katika jambo husika, aweke mipango ili kujua atakavyoanza na atakavyo ishia katika safari nzima ya Ndoa. Katika kuwa na nia lazima aelewe kwanini anataka kuoa ama kuolewa, Mhusika asijiingize katika jambo la Ndoa kwakuzingatia mazingira, kwasababu mazigira hubadilika, pengine mhusika akasukumwa kuingia katika uhusiano wa kindoa na mtu Fulani kwa sababu ya kipato, umaarufu, Elimu, vyeo, Dini nk. Mhusika kama huyu ni wazi hajui afanyalo na hivyo ni rahisi kuishia kunako kinyume cha taraja lake, mtu akioa kwa mzingira kama hayo ama yanayofanana na hayo huwa ameyaoa/yamemuoa ama kuyachumbia/yamemchumbia mazingira hayo, jambo ambalo ni hatari iwapo ikitokea kubadilika kwa mazingira hayo basi na uchumba ama ndoa hiyo inakuwa imekwisha sambamba na kubadilika kwa mazingira!

  2). Jambo jingine ni Kujitambua; mhusika lazima ajitambue kikamilifu kitabia na kiuwezo, ili apate muchumba wa kufanana naye, pia ajijue kama kweli hasukumwi na tamaa ama mihemuko ya ujana, ajue wazi asichokiweza, hataki nini, hapendi nini, anataka mke/mme wa namna gani na kwa nini, ajue pia ni familia ya namna gani anayokusudia kuijenga. Aijue kwa uzuri tabia, imani yake kama ni sawa na imani ya mke/mme anayetaka kuwa mwenza wake, vilevile ajue mienendo ya familia anayoiendea ili kuoa/kuolewa kwayo, ajue japo kwa uchache kuwa ipoje kijamii nk.

  3). Kujikabidhi mbele za Mungu; Mhusika lazima akabidhi mpango wake wote kwa Mungu, hili ndilo tatizo kubwa kwa Wachumba. Wachumba wengi hujidhania wamepata wachumba wao kwa Mungu kumbe siyo! Yapo makosa mawili makubwa katika hili ambayo wachumba hufanya, moja ni kwamba, watu hudhani kuwa Mungu huchagulia mtu mke. Pili, watu hujikabidhi wake/waume wao wenyewe badala ya kukabidhiwa na Mungu! Mungu ni huru, vivyohivyo na watoto wake huwapa uhuru, Mungu anataka uchague Mchumba kutoka popote wa kabila lolote na wa aina yeyote LAKINI TU AWE KATIKA UZAO WA MUNGU. Sasa kutoka katika uchaguzi wako Mungu atakupatia mke/mme wa aina hiyohiyo kama uipendayo, hautajuta katika mahusiano yak ohayo kwakuwa Mungu atakuwa amekupa Mke toka katika familia yake, ambayo haina mawaa yeyote na atakuwa wa kufanana naye kikweli! Kwa Mungu hakuna majuto, tatizo la wengi hawazingatii muda wa kukabidhiwa wenza wao. Watu hawana subira, hawasikilizi sauti ya Mungu na kama ujuavyo ‘Mwenyepupa hudiriki kula damu’ ukifanya haraka lazima bahati uiache nyuma, mungu hufanya maamzi yake kwa wakati unaokubalika kwake, maana Mungu ni wa mipango, kila jambo kwa wakati wake, ndiyo maana Mungu wakati ulipofika wa Adamu apewe mke, Mungu akasema ‘Haifai mtu huyu kuwa peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye!’ Unaona? wa kufanana naye, Mungu anapokukabidhi mke ni lazima awe wa kufanana nawe ili kusiwe na majuto, maana ufalme wake ni pamoja na Amani na Furaha.

  Labda nigusie makosa katika uchaguzi, watu hujidhania ni welevu na kwamba wapo makini vya kutosha, na hivyo kutojiweka mikononi mwa Mungu, hili ndilo kosa kubwa kuliko lolote lile! Kutokana na kosa hili watu hujiaminisha kwa wachumba zao na kujidhania kuwa wamechaguana kwa uangalifu na kwamba wapo makini kiasi kwamba hawajakosea katika uchaguzi wao. Yapo mambo mawili makubwa yanayojitokeza iwapo mtu hatakabidhi mipango yake ya Ndoa kwa Mungu, nayo ni; Moja, Mtu hujiachia kisaikolojia na kuamini kuwa yupo sahihi, humpenda mchumba wake kimapezi yanayosimama kisaikolojia na si katika pendo la ki Mungu. Matokeo ya hali hii hatimaye upande mmoja wa uchumba huumizwa kutokana na upendo huu wa kibinadamu ambao kwakweli ni wa uongo, maana saikolojia ni mwili na katika mwili kuna uongo wa kufisha maana matendo ya mwili ni dhambi, na katika dhambi Mungu hayumo! Kwa hiyo katika mazingira hayo wachuma kuachana ‘Soremba’ ni kawaida, jambo ambalo nazani hata Ndugu yangu Ombeni aliangukia katika kundi hili, aliamini uongo au yeye ndiye muongo, aliamini au alimwaminisha mchumba wake upendo wa kisaikolojia. Yeye au mwenzi wake hakuwa sahihi, hakuwa wa aina ile ya kama Mungu aitakayo na hivyo kutokamilika kama ilivyokusudiwa. Mara zote shetani ni mwongo, angalia, mchumba asiyetokana na Mungu ni lazima asumbue, maana alishafundishwa uongo na Shetani, Biblia inasema, ‘Mwana hafanyi jambo isipokuwa kamuona baba yake akilifanya!’ Kwakuwa shetani ni muongo na mtoto wake ni lazima awe muongo vilevile, kwa sababu hiyo, wachmba hawa hujikuta wakitapeliana na kuongopeana kitabia, na mara baada ya kuzoeana, tabia zao halisi za kila moja hujifunua na kukuta wakitofautiana kwa umbali mkubwa na kupelekea kuumizana kihisia moyo!

  Na jambo la pili ni kwamba, kutojiweka mikononi mwa Mungu, watu hujiingiza katika kujuana kimwili kabla ya Mungu kuwaunganisha kimwili. Wachumba wanapo juana kabla huzarisha upendo wa uongo na hali hiyo ya upendo wa bandia hupelekea wachumba hawa kupuuza na kutojali na kuacha kuzifanyia kazi dosari ndogo ndogo. Kiukweli huwa hawajui ni kwanini upo muda uitwao wakati wa uchumba. Maana upendo au mapenzi kama hayo hutawaliwa na mazingira, na inapotokea mabadiliko yasiyotarajiwa, upande mmoja wa uchumba hujikuta unaumizwa vibaya kihisia moyo. Kwa ujumla yapo mambo mengi sana yapaswayo mtu ajue kabla hajaingia katika mahusiano ya kindoa, upo umhimu wa kujua umri, kujua kiwango cha Imani cha kila mmoja kama kweli ameokoka ama la, kujua ndoa ni nini, Kujua aina ya Familia inayokwenda kujengwa, kujua utayari wa kuilea na nguvu ama uwezo wa kuingia katika majukumu mazito ya ndoa nk. Wengi walioingia katika Ndoa kibinadamu hujikuta wakitaka sana kujiondoa katika mahusiano hayo ya ndoa!

  Mwisho, usinishangae ninaposema kuwa, kuvurugika kwa uchumba ni jambo zuri sana kwakuwa wahusika huwa wametofautiana mapema. Kuongopeana kwa wachumba hawa kwa mapenzi yao ya uongo, huwa tayari umebainika kabla ya ile hatua ya mwisho-ndoa! Unajua Watu wakioana hawawezi kuachana kwa namna yeyote ile, hadi mmoja afe, hayo ni maelekezo ya Mungu mwenyewe, na ikitokea Mume au mke hakuwa chaguo, hili ndilo huwa janga kuu linaloweza kusababisha Dhambi ambayo mshahara wake ni mauti, unaona hasara hiyo? Kumbe kipi kizuri kuachana wakati mtu anapogundua kuwa mchumba aliyenaye hafai, au Aoane tu ili waje watofautiane baadaye hata kama tayari walishapata watoto? Je, huoni kuwa ndugu yangu Ombeni kati yenu kuna Mtoto wa Mungu? Mungu hawezi kuacha mwanaye akakae katika jela ya ndoa na kuishi bila furaha kwa makosa ya mtoto wa Ibilisi, Biblia husema wana wa dunia ni welevu kulikoni wana wa nuru, bila Yesu kupotea kwa wateule ni yakini. Tumtegemee Kristo Yesu wakati wote, yeye ndiye muumbaji wetu anatujua sana kuliko tujijuavyo wenyewe, yeye anasema katkika Yohana kuwa, ‘Bila mimi ninyi hamuwezi Neno lolote’ Mkristo wa kweli anapaswa ajue hili na kulielewa kabisa na kuliweka katika vitendo; Maombi ndiyo kinga na ndiyo njia pekee itakayokupa ukweli wa jambo hili. Maombi ndiyo pekee yatakayokupa huruma ya Mungu na kukupa faraja ya kweli. Mungu hujua kufariji watu wake, jiulize ni wapi ulikoiachia ile kweli yenyewe, maana amini usiamini MAKOSA YA MTU NI MTU MWENYEWE! Jichunguze kwanza mwenyewe kabla kumpa lawama aliyekuwa mchumba wako ama mtu mwingine na kumuona kama sababu ya hiyo ‘Feriya’ mbaya iliyokupata! USHAURI WANGU; Jichunguze, jisamehe, achilia, yahesabu yote ya kale kuwa ni “Mavi” hivyo anza upya na bila ya kujari kuwa aliyevunja uchumba wenu ni Shetani kwa hila zake, ama Mungu mwenyewe ili kumnusuru mwanae, umwamini Mungu maana yote yawezekana kwa kila aaminiye,

  Pole sana, ila muombe mungu akupe faraja, yeye anasema nitawapeni Amani ambayo ulimwengu hauwezi kuwapa, Mungu anajua kufariji watoto wake. Zaidi sana yafaa kuelewa pia kuwa, hakuna ajuaye, pengine hiyo ndiyo njia pekee ili upate Baraka na furaha ya kweli toka kwa Mungu, maana ni tabia ya Mungu kutenganisha watu ili ambariki ampendaye, angali mfano katika maisha ya Ibrahimu na Luthu, Isaka na Ismaeli, Esau na Yakobo, Eliya na Elisha nk.

 4. Pole sana kaka Ombeni nahisi maumivu uliyonayo naona ni jinsi gani uko ktk wakati mgumu,jambo la kwanza TULIA, kisha tafuta kwa bidii kuwa na Amani,nijambo la muhimu sana bila kuwa na amani unaweza kufanya mamuzi yatakayo kupelekea kujuta baadae au maisha yako yote,sijui kama umeokoka au la?!kama umeokoka unaweza kuitafuta amani kwa njia ya kusikiliza muziki wa taratibu za kumwabudu na kumsifu mungu ukiwa umetulia kwa kufanya hivyo utakuwa unavuta uwepo wa mungu na Roho mt atakuasidia either kuomba(na maombi ya aina gani mf ya toba nk)au kusamehe na kumwachilia ili uondokane na roho ya uchungu namengineyo kwani yeye anajua zaidi,omba amani na kataa roho ya uzito(inaweza kukugandamiza na kukufanya usitamani kwenda kanisani na usipende kujichanganya na watu(zaidi fanya kama watumishi walivyokushauri hapo juu)fanya toba ya dhati mbele za mungu kama ulikosa na muombee huyo mdada mungu ampe neema ya kusamehe na kuachilia na roho ya uchungu iondoke!mwisho mshukuru Mungu kwa kila jambo inawezekana mungu anayo makusudi na jambo hilo,kumbuka kwamba “Mungu anatuwazia mema kila siku”Jipe moyo naomba Jehova shaloom”mungu ni amani yetu”akupe amani yake,nakuombea mungu akusaidie”Kama hujaokaoka OKOKA”Yesu anakupenda zaidi ya huyo mdada,ubarikiwe

 5. Barikiwa sana kaka,
  Pole sana kwa yalokukuta lakini shangilia maana mke wako yuko malangoni maana Mungu hatoi kilicho kinyonge bali chenye nguvu, ikiwa ulimshirikisha Mungu bila unafki wala uchafu wowote juu ya kumpata huyo mchumbaako basi jua huyo akuwa wako ulipokea toka kwa ibilisi maana unapomwomba Mungu kama hujajua unaweza kupokea majibu yasiyo ya Mungu lkn yanafanana na ya Mungu, hivyo kaa chini utafakari we ndo unajua ulimwombaje Mungu na alikujibuje, then rudi mbele zake umweleze ili akupe majibu sahihi, lakini usiache kwenda kanisani. Kumbuka shetani naye anafurahi wewe kutoshiriki chakula cha rohoni hivyo tia bidii sana.

 6. SHIKA NENO ULIYEPEWA NEEMA KUBWA! HONGERA KWA USHINDI KAKA OMBENI MAANA KWA KUTOCHUKUA UAMUZI MWINGINE MBAYA BASI HAPO UMESHINDA. NINA NENO MOJA JUU YAKO, KWAMBA, ” MOYO USIOSAMEHE, MOYO WENYE MAKWAZO, MOYO WENYE UCHUNGU, MOYO UNAOONA KUSHINDWA HUO SIO MOYO WA MUNGU HATA KIDOGO. PIA MUNGU HAWEZI KUKAA KWENYE MOYO KAMA HUO. KAMA KWELI UNATAKA MUNGU AINGILIE KATI JAMBO LAKO NA KUKUPA KANISA WAKO (MKE WAKO) NI LAZIMA UKUBALI KUUZIKA MOYO WAKO KWANZA NA UPOKEE MOYO WA MUNGU AMBAO NI UPENDO. KWAKUWA MOYO WA MTU NA MWANADAMU SIKU ZOTE HUWAZA MAMBO MABAYA TU NA KAMWE HAUWEZI KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU WA KWELI. UKISHAUPOKEA MOYO WA MUNGU AMBAO NI UPENDO UKAKAA NDANI YAKO BASI UTAWEZA KUSAMEHE NA KUACHILIA NA MUNGU HAPO ATAPATA NAFASI YA KUFANYA JAMBO JIPYA KWAKO. PIA MOYO WA MUNGU NI MOYO WENYE TOBA YA KWELI, HIVYO UTASIMAMA KAMA KUHANI KUOMBA TOBA KWA AJILI YA HUYO ALIYEKUACHA NA KWA AJILI YAKO. PIA KUMBUKA PIA HUWEZI KUPATA KITU CHOCHOTE KILE UNACHOKIHITAJI KATIKA MAISHA YAKO BILA KULIPIA GHARAMA FULANI. HIVYO TAMBUA KWAMBA UNAPOKUBALI KUZIKA MOYO WAKO NA KUUPOKEA MOYO WA MUNGU NI GHARAMA HIYO UNALIPIA ILI MUNGU AKUPE KILE UNACHOKIHITAJI BASI USIKWEPE KULIPA GHARAMA YA KUSAMEHE KAKA OMBENI ILI UWEZE PATA UNACHOHITAJI. BARIKIWA1 NA BWANA YESU. SHIKA NENO!

 7. Niko sehemu mbili pole, na hongera hii nakupa nafasi ya kuiona pole yangu na hongera kama hukukosea, nauzoefu na moyo wa mwanamke, mdada mpaka kafikia hatua hiyo ni mbaya na wakumhurumia, Mungu amemwumbai mwanamke moyo wa tofauti wa kulibeba jambo Roho ya uvumilivu, nakuomba uwe wazi ndugu yangu, kama kweli unampenda mwombee sana Mungu ampe neema ya pekee.mawazo yangu tuu.

 8. ” BWANA MUNGA akamwambia Adamu nitakufanyia msaidizi wakufanana nae, kaka mbeni Mungu hupanga kila jambo jema huwa baya pindi tu shetani aingiliapo kati inawezekana huyo si msaidizi wa kufanana nae, japokuwa unasema kuwa umemkosea na hukutuambia kuwa umetenda kosa gani kwake.
  Tukumbuke kuwa sisi ni wadhaifu sana juu ya maisha yetu kama Mungu asingekuwa anatoa msamaha je nani angesimama, huyo si chaguo lako ndio maana Mungu akakuonesha mapema na cha ajabu ni kanisa moja huoni hata hofu ya MUngu hana anaingia katika ibada , anatoa sadaka huku akiwa hajatoa msamaha kwa mtu aliyemtegemea kuwa mwili mmoja , muombe Mungu atakupa wakufanana nawe Aimeen

 9. Pooooole sana ndg yangu Ombeni. Je, UMEOKOKA tayari?? Km bado, kabidhi maisha yako sasa, upate amani ya Kristo. Lkn pia, MSHUKURU Bwn kwakuwa, huyo HAKUWA AMEANDALIWA kwa ajili yako. Biblia inasema, “Mke mwema ni nani amjuaye??……….”. Piga moyo konde, anza upya, tafuta mke toka kwa Bwn, utapata tu, na nakushauri, usiffanye sherehe, kafunge ndoa kanisani, hizo fedha walizokuchangia watu ziingize matumizini, waliochanga hawatahuzunika kwani, nao wameumia nawe kwenye hilo, mkiishafunga ndoa mkalale muianze ndoa. Nakushauri, daka yeyote kanisani kwako hapo, na itakuwa nddoa tu, kwani, hakuna au haukuwa hata na wapili yake?? Nong’ona naye. Nasema hy kwakuwa, najua, utakapoanza kuyapa nafasi that gap might be filled with wrong, or unsuitable person, jiangalizie tu yule aliyekuwa akikutamani na kukutaka, sema naye. Bwn yupo kuyasimaia maamuzi magumu, usiohofu. Na najua tuko washauri lukuki, utachambua. Amani ya Bwn iwe nawe. Oguda J.E..

 10. Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.” Ndugu Yangu ombeni, Mke mwema mtu hupewa na Bwana. ni zawadi kutoka kwa Mungu, My question for you is KATI YA ZAWADI NA MTOA ZAWADI KIPI NI CHA MUHIMU KWAKO? manake naona kwenye post yako, umeithamini zaidi ile zawadi ambayo kimsingi hata haikuwa ya kwako KULIKO KUMTHAMINI YULE ANAYEKUANDALIA ZAWADI YA KWAKO. Your relationship with God is more important than your marriage, besides Biblia nisomayo mimi inasema Kichwa cha mwanamume ni Kristo, it means Yesu anapaswa kuchukua nafasi ya Kwanza kwenye maisha yako na si kingine chochote. Ukiona umefika mahali mwanamke amekuwa ni kigezo cha kukufanya uache kwenda kanisani, then tafakari upya wokovu wako na msimamo wako kama mwanamume. Ninachoamini ni kwamba Mungu amefanya mtengane na mwanamke huyo kwa makusudi, kwa kuwa inavyoonesha bado hujajenga stamina ndani yako ya kuelewa Nini ni cha muhimu zaidi, Mke au Mungu. NA HICHO NDICHO CHANZO CHA ANGUKO LA MWANADAMU, KUMSIKILIZA ZAIDI MWANAMKE KULIKO KUTII MAAGIZO YA MUNGU. FOR THAT REASON NAKUAMBIA BADO HUJAWA TAYARI KUOA. MTAFUTE MUNGU, TENGENEZA NA YESU ATAKUPA MKE WA KWAKO UKIWA TAYARI NA STAMINA YA KUISHI NA MWANAMKE NDANI YAKO.

 11. Hilo kosa inaelekea ni zito sana ndo mana mchumba amekasirika,nenda mbele za Mungu kwa toba uombe toba kwa ajili yako na mchumba,na umuombe Mungu ampe roho ya masamaha mchumba wako,amuondolee uchungu kwa makosa uliyomkosea,naamini kama ni ubavu wako atarudi na Mungu atarudisha upendo kati yenu,pia jitahidi njia zako ziwe zinampendeza Mungu na mchumba wako,Mungu akubariki sana.

 12. Pole sana ndugu . sasa mambo kama iyi watumishi wapime kwa ngaliya sana . Juu ya mke kuacha mwezio ama mume kuacha mwezio . ni jambo enye iko mingi sana katika ndoa masiku iyi na apo shetani anaweka mukazo juu ya kupoteza wana wa Mungu

  Watumishi wafanye semina ya maneno iyi ,na tujuwe tamaa ya wanaume ni uu sana koliko ya wa bibi juu ya tendo ya ndoa Mungu atusaidiye

 13. Kaka Ombeni kwanza uwe wazi kosa lako ni lipi? Hili sisi tukupe ushauri wetu na maombi yetu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s