Waganga wameshindwa, Yesu Kristo ameweza kuniokoa!!

devine

Mimi naitwa spacio Abubakary (Spacio Devine – {kiuimbaji}, ninatoka katika familia ya kiislamu na nilikuwa muislamu ila baada ya kugundua njia ya Yesu Kristo ndio njia ya kweli yenye uwokovu, nilibadili dini na sasa ni Mkristo na pia nimeamua kueneza Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji. Nimeishi na jini kwa miaka 17, ilikuwa ni mateso na mzigo mzito. Jini liliharibu ujauzito wa mpenzi wangu zaidi ya mara tatu, nilizunguka kwa waganga wa kienyeji zaidi ya 15 lakini sikupata majibu.

Lakini sasa nimebadilishwa kwa damu ya thamani ya Bwana Yesu, ninamuimbia kwa furaha na amani.

Kipindi nilipokuwa katika milki ya jini Maimuna sikuwa una uhuru na mwili wangu, unajua jini anapokufanya kuwa kiti wake (kukumiliki) basi wewe unakuwa umetawaliwa na sheria zake, muda wote nilikuwa ni wa kuumwa, ni kawaida kuugua ugua kwa sababu kuna nguvu inakuwa ndani yako ambayo ni nzito, matatizo kama ya moyo kuuma sana na kubana mara kwa mara ilinitesa sana kiasi kwamba nilikosa raha na hata kunifanya nishindwe kushiriki katika michezo na marafiki zangu kwani maumivu yalikuwa makali sana pindi inapotokea kunibana.Kuna wakati nilihisi sitafika mwaka 2009 kwa kuugua moyo na nilipopima nilikutwa ni mzima sina ugonjwa. 

Hali hiyo ilinifanya kwenda kwa waganga sana, wengi wananishika sikio na kusema maneno ya kumtuliza jini huyo asifanye vurugu katika mwili wangu na anatulia siku kadhaa kisha anaanza tena.Nikajikuta zaidi ya waganga 15 nimepita kila mmoja anasema yake.Lakini baadae nikaja kuambiwa kuwa kumbe kuna vitu alitaka kukabidhiwa ndio atulie, na vitu hivyo mara nyingi waganga wakikupa baadae majini hukubadilikia na kuanza kukulazimisha kufanya kazi ya uganga, kitu ambacho nilikichukia sana. 

Majaribu hayo na taabu nilizopitia zilinichochea sana kuutafuta uzima hadi kuingia katika wokovu. 

Najua ni wengi sana wanasumbuliwa na majini ila wanashindwa na kuelezea, asilimia kubwa ya WATU WALIO NA MATATIZO YA KUTOSHIKA MIMBA HUSABABISHWA NA MAJINI, na napenda kuwaambia kuwa wanaweza kufunguliwa kutoka katika kifungo endapo wataamini kila kitu kinawezekana kwa Mungu na si kwa nguvu za waganga, WAKUBALI WOKOVU HAKIKA WATAPONA NA KURUDI UZIMANI na pia wazidi kufanya maombi kwani hata kama jini akitoka katika mwili wako hatokuwa anacheza mbali na wewe, ukitetereka kiimani basi anaweza kukurudia tena kwa spidi ya juu zaidi. 

Ukiwa na YESU ni raha mustarehe hakuna kitakacho kusumbua iwe majini nk. Ni amani isiyokuwa na expire date. 

Tangu nilipompokea Yesu nimekuwa huru, sisumbuliwi tena na maumivu ya moyo. kiufupi nimepata amani iliyopotea katika maisha yangu. Siishi kwa masharti tena. 

Mungu awabariki,

Spacio .A. Ngalla
Advertisements

7 thoughts on “Waganga wameshindwa, Yesu Kristo ameweza kuniokoa!!

  1. Pole sana Mr. Ngalla kwa mateso makubwa yaliyokupata na nitumie fusa hii pia kukupongeza sana kwa uamuzi mzuri uliochukua wa kumfuata YESU KRISTO ambaye ndiye Bwana na Mwokozi wetu. Endelea kumtumainia na kamwe hatakupungukia. Ubarikiwe.

  2. HAKIKA umechagua JINA jema. jina la YESU KRISTU WA NAZARETI ALIYE HAI DAIMA NA MILELE. DUMU DAIMA KATIKA YESU.
    YOHANA 3:16

  3. MUNGU APEWE SIFA hongera ndugu kwa kufunuliwa kwamba YASU NDIE NJIA YA KWELI NA UZIMA,YASU alisema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa namizigo,nami nitawapumzisha,ndugu YESU amekupumzisho mizigo uliokuwa nayo,kaa miguuni pa YESU na atakutendea mengi zaidi usiyo majua yeye nimwaminifu atatenda kwa nguvu za uwezo wake.AMANI ya BWANA WETU YESU KRISTO IWE NAWE,joseph kiswili nikiwa nairobi.

  4. Wooow! YESU KRISTO ni BWANA wa mabwana! Ooo asante Yesu kwa upendo na huruma zako nyingi kwetu! Heshima na Utukufu ni vyako Unastahili sifa hizi,Mungu akubariki sana ndugu endelea kumtumikia Mungu kwa UAMINIFU utamuona zaidi ktk mambo makubwa zaidi

  5. Yesu ni Bwana , wafilipi 2:9-11. Imetimia , inasema Kwa hiyo tena Mungu alimuhadhimisha mno, akamkilimia jina lile lipitalo kila jina, 10 Hili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe la vitu vya mbinguni ,na vya duniani na vya chini ya nchi , (nimefurahi ukuu wa Mungu wetu kuona hilo jini limepiga magoti mbele ya jina hili kuu la Yesu), 11na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA,kwa utukufu wa Mungu baba. Kaka wewe nafuhai kupita kiasi kwa ajiri yako , umeifahamu kweli ikakuweka huru. endelea kumtafuta Bwana na endelea kupigisha magoti kila kilicho kinyume na mapenzi ya Mungu ktk maisha yako. Imeandikwa ktk Zaburi 107:42 kuwa wanyoofu wa moyo wataona na kufurahi na uovu wa kila namna utajifumba kinywa. kweli uovu wa kila namna umejifumba kinywa ktk maisha yako. na kama alivyosema Isaya 60:20 kuwa siku za kuomboleza kwako zitakoma , naona Mungu wetu amezikomesha siku za kuomboleza kwako.atukuzwe yeye atuchuliaye mzigo siku kwa siku, Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina Yehova Bwana Zaburi 68:19-20. Ubarikiwe sana . Mama K

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s